Thursday 1 October 2020

MAASKOFU NA WACHUNGAJI WAZINDUA KITABU CHA UONGOZI ULIOTUKUKA WA RAIS JOHN MAGUFULI


Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naioth Gospel Assemblies of God ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Dkt. David Mwasota.(kushot) akiwaongoza Maaskofu na Wachungaji kwenye maombi ya kukiombea Kitabu cha Uongozi Uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki.
Maombi ya kukiombea kitabu hicho yakiendelea kufanyika.
Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naioth Gospel Assemblies of God ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Dkt. David Mwasota., akizungumza na Maaskofu na Wachungaji kwenye maombi ya kukiombea Kitabu cha Uongozi Uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki.
Muonekano wa kitabu hicho.
Askofu Sedrick Ndonde wa Kanisa la Restroration Bible ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo walioandika kitabu hicho.
Uzinduzi wa kitabu hicho ukifanyika.

Na Dotto Mwaibale

MUUNGANO wa Maaskofu zaidi ya 15 na Wachungaji 100 mwanzoni mwa juma walizindua kitabu kinachoelezea uongozi uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Kitabu hicho kimeandikwa na Mtendakazi katika shamba la Bwana, Restoration Bible Church Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa kitabu hicho kiitwacho Uongozi Uliotukuka, JPM ni Kiongozi wa Kisiasa na Kiroho, uliofanyika jijini Dar es Salaam uliongozwa na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naioth Gospel Assemblies of God ambaye pia ni katibu Mkuu mstaafu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Dkt. David Mwasota.

Mwasota alisema lengo la kuandikwa kitabu hicho ni kutazama uongozi wa Rais Magufuli kwa pande za kisiasa na kiroho.

Askofu huyo alisema katika utendaji kazi wake, Magufuli anamtegemea Mungu hivyo kumfanya aonekane anaiongoza nchi kwa upande wa kiroho.

“Imani ya Mheshimiwa Magufuli katika kushughulikia janga la Corona kiroho limefanya kuinua imani ya watu wengi kwa kulisaidia kanisa ambalo ndiyo kazi yake kubwa kuwajenga watu kiimani,” alisema askofu huyo.

Mwasota aliwaomba maaskofu, wachungaji na waumini wote kuendelea kumuombea Rais Magufuli kwani ndiyo yalikuwa maombi yao kwa miaka mingi kwa Mungu atuletee kiongozi kama yeye.

“Tunamshukuru Mungu aliyejibu maombi yetu kwa kutuletea kiongozi tuliyemuomba miaka mingi ambaye ni Magufuli anayeliongoza taifa letu kisiasa na kiroho,” alisema Mwasota.

Askofu huyo aliongeza kuwa katika nchi yetu hatukuwahi kumpata kiongozi wa juu anayemtaja Mungu wakati wote na kuwaagiza watendaji wake kila anapowaapisha wamtangulize na kumtegemea Mungu.

Naye Bishop Sedrick Ndonde wa Kanisa la Restroration Bible ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo walioandika kitabu hicho, alisema lengo la kitabu hicho ni kuelezea ukweli kuhusu Rais Dkt. John Magufuli ili kufahamu zaidi nini alichobeba mbali ya wadhifa wa urais alionao na kulikumbusha kanisa na watumishi wa Mungu kuutafakari uongozi wake.

“Umuhimu wa kitabu hiki ni kuwakumbusha watumishi wa Mungu kuwa na muda wa kutafakari uongozi wa JPM kwa yote aliyoyafanya kwa upande wa kiroho,” alisema Askofu Ndonde.

Aliongeza kwa kumtegemea Mungu amefanya mambo makubwa kama kujenga miundombinu ya barabara, umeme, maji, shule, hospitali na kuwawezesha watanzania kunufaika na madini, mbuga za wanyama ambapo awali waliokuwa wakinufaika walikuwa watu kutoka nje.

 “Magufuli ni mfalme anayekiri ufalme wa Mungu kutawala taifa letu,” alisema Ndonde.

Ndonde aliongeza kuwa kuna umuhimu wa kukisambaza kitabu hicho kwa waumini wao na wananchi wengine kwa ujumla  bila kujali dini wala madhehebu wanayotoka ili waweze kuwa na mtazamo chanya. 




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi October 1
















Share:

Wednesday 30 September 2020

Individual National consultancy at UNICEF

The aim is to assess whether the Parenting Education Programme has been implemented effectively and whether it has brought about positive change in the knowledge and behaviour of parents and caregivers in how to protect their children from violence. UNICEF works in some of the world’s toughest places, to reach the world’s most disadvantaged in […]

The post Individual National consultancy at UNICEF appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HESLB Yatoa Siku Tano (05) Kwa Wahitimu Mafunzo Jkt Kuomba Mikopo


Na Mwandishi Wetu, HESLB
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa muda wa siku 5 kuanzia Oktoba mosi hadi 5 mwaka huu ili kuwawezesha wanafunzi waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hivi karibuni kuingia katika mfumo wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao na kukamilisha maombi yao.

Katika taarifa yake aliyotoa kwa vyombo vya habari leo Jumatano (Septemba 30, 2020) Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru alisema uamuzi huo unatokana na maombi ya wanafunzi, wazazi na walezi ambao hawakuweza kuomba au kukamilisha maombi yao kutokana na sababu ya kujiunga na mafunzo hayo.

Kwa mujibu wa Badru alisema katika muda huo wa siku tano, mfumo pia utakuwa wazi ili kuwawezesha waombaji ambao maombi yao yana upungufu kurekebisha kwa kuweka nyaraka sahihi ili kuiwezesha HESLB kuendelea na hatua nyingine.

“Kwa wanaorekebisha taarifa, wanapaswa kuingia katika akaunti zao walizofungua kuombea mkopo na watapata ujumbe kuhusu maeneo ya kurekebisha. Tunawasihi watumie muda huu wa siku tano kurekebisha na kukamilisha maombi yao’’ alisema Badru.

Katika mwaka wa masomo 2020/2021, Serikali imetenga TZS Bilioni 464 zitakazowanufaisha jumla ya wanafunzi 145,000. Kati yao, wanafunzi 54,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na wengine 91,000 ni wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo. Mwaka 2019/2020 jumla ya TZS 450 bilioni zilitengwa na zimewanufaisha jumla ya wanafunzi 132,119.

MWISHO


Share:

Barabara za juu kutoka Mwenge kwenda Buguruni katika makutano za barabara ya morogoro,Nelson Mandela na Sam Nujoma zaanza kutumika rasmi leo

Barabara za juu kutoka Mwenge kwenda Buguruni katika makutano za barabara ya morogoro,Nelson Mandela na Sam Nujoma zaanza kutumika rasmi leo( Picha- MAELEZO)


 


Share:

PICHA: Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Dr Magufuli ahutubia wananchi wa Mbeya mjini

PICHA: Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Dr Magufuli ahutubia wananchi wa Mbeya mjini





 


Share:

Vijana Kagera Watakiwa Kutosubiri Ajira kutoka Serikalini.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Vijana katika halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera wameaswa kutosubiri ajira kutoka  serikalini bali wajikite katika kujiajili haswa katika kilimo,uvuvi na ufugaji ili kuweza kujikwamua na umasikini.


Hayo yamesemwa na bwana Agape Ishabakaki wakati akizungumza na mpekuzi blog ambaye pia ni mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la FUAP TANZANIA linalojiusisha na masuala ya kusaidia wakulima na wafugaji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya watu haswa vijana ili kujenga utamaduni wa kujiajili uku wakiwa wamesubiri ajira kutoka serikalini. 


Bwana Agape amesema kuwa shirika hilo kwa sasa limetua mkoani Kagera hususani katika wilaya ya Missenyi na litazungukia kata mbalimbali ili kutoa elimu kwa vijana juu ya faida za kujiajili na kutoa elimu kwa vijana hao kujikita katika kilimo kwa manufaa yao ya badae . 


Katika hatua nyingne bwana Agape amesema kuwa  zaidi ya miti elfu kumi ya matunda itazalishwa na shirika hilo na zoezi hilo litaanza tarehe mbili mwezi wa kumi katika kata ya Bugorola ili kuwapa fursa vijana pamoja na wananchi wa Missenyi kuwa na elimu juu ya utunzaji mazingira pamoja na kuwa na utamaduni wa kupanada miti  katika maeneo yaliyowazunguka.


Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo bwana  Josephat Joseph John amesema  kuwa kwa sasa hivi shirika ilo lina mradi unaoitwa AGRI EXPERIENCE  ambapo mradi huo utawawezesha  vijana wengi kujifunza na  kujua namna ya kufuga kuku wa kisasa pamoja na kufahamu ujuzi mbalimbali wa biashara ya mayai ya kisasa, ufugaji wa nyuki nk.

Bwana Josephat amesema  kuwa vijana watumie shirika hilo vizuri kwa  kuwa elimu itatolewa bila malipo yoyote na ku ongeza kuwa kabla yakuondoka mkoani hapa vijana wawe wameisha pata maarifa na ujuzi wa kujiajili wenyewe kupitia kilimo na ufugaji wa kisasa uku akitaja kauli mbiu yao kuwa ni “Kijana wa kagera kulima kwa tija kwa maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla 2020-2025”.





Share:

Serikali Kusimamisha Mishahara Ya Maafisa Utumishi Watakaosababisha Watumishi Kutolipwa Mishahara

 Na. James Mwanamyoto-Dodoma
Maafisa Utumishi watakaozembea na kusababisha Watumishi wa Umma nchini kutolipwa mishahara yao kwa wakati, watasimamishiwa mishahara na Serikali mpaka watakapohakikisha watumishi hao wamelipwa mishahara yao.

Hayo yamesemwa jana na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya Mfumo Mpya wa Kitanzania wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara kwa kundi la pili la Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala 140 kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Kigoma na Tabora yanayofanyika jijini Dodoma katika Ukumbi wa VETA.

DKt. Michael amesema, kuna tatizo katika baadhi ya Taasisi za Umma kwani wapo Maafisa Utumishi wanajifanya miungu watu wakati wajibu wao ni kumtengenezea mazingira mazuri ya kikazi mtumishi ili ajisikie yuko sehemu salama na aweze kutekeleza ipasavyo jukumu la kuwahudumia wananchi.

“Msiwafanye watumishi mnaowasimamia kuona sehemu ya kazi kama jehanamu, hivyo mbadilike kwani Serikali haitomvumilia yeyote atakaye kinzana na azma yake ya kuboresha huduma kwa wananchi”, Dkt. Michael alisisitiza.
Ameongeza kuwa, ni lazima Maafisa Utumishi wabadilike kwa kuwajengea mazingira Watumishi wa Umma kuipenda Serikali yao kwasababu inawajali na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya taifa.

Dkt. Michael amefafanua kuwa, Serikali inamhakikishia mtumishi usalama wa ajira yake tofauti na sekta binafsi, hivyo hakuna Afisa Utumishi atakayevumiliwa pindi akisababisha Serikali kulaumiwa na Watumishi wa Umma au Wananchi.

Naye, Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi, Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw. Boniface B. Chatila kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, ameahidi kuwa, wakirejea katika maeneo yao ya kazi watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuondoa kero ya Watumishi wa Umma kufuata huduma Ofisi ya Rais Utumishi Dodoma, huduma ambazo wanastahili kupewa katika maeneo yao ya kazi.

Aidha, Bw. Chatila amemhakikishia Dkt. Michael kuwa, ujuzi watakaoupata kupitia mafunzo ya Mfumo Mpya wa Kitanzania wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara watautumia ipasavyo kuongeza ufanisi kiutendaji ili kuboresha utoaji huduma kwa umma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, ACP Ibrahim Mahumi amesema, suala la mtumishi kukosa mshahara hivi sasa linachukuliwa kama ni kosa kubwa hivyo Afisa Utumishi atakayebainika atasimamishiwa mshahara ikiwa ni hatua ya awali na atachukuliwa hatua za kinidhamu ikizingatiwa kuwa, mfumo mpya utaonesha uzembe wa afisa huyo.

Mfumo Mpya wa Kitanzania wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara utaanza kutumika rasmi Mwezi Novemba, 2020 mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya makundi yote ya Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala ambao ndio wenye jukumu la kuutumia mfumo huo kiutendaji.


Share:

Sumaye aishukia CHADEMA, asema hawawezi kuongoza nchi


Na John Walter-Hydom, Mbulu
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema vyama vya Upinzani nchini haviwezi kuongoza nchi kwa sababu hawana sera.

Ameyasema hayo Leo septemba 30,2020 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini katika mkutano wa Mgombea Mwenza Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia  Suluhu Hassan kunadi Sera za  Chama cha Mapinduzi katika viwanja Vya Haydom.

Sumaye amesema Chama alichotoka  CHADEMA,  ni Chama cha Uwana harakati na hakina sera  zozote za kuwasaidia wananchi.

'CHADEMA wanafikiri kuwa nchi ya Tanzania bado ipo  mikononi mwa  Wakoloni, wanapiga kelele utafikiri bado tunatawaliwa' alisema Sumaye

'Nilienda kule  lakini baada ya kugundua hawana chochote nikaamua kurejea nyumbani' alisisitiza Sumaye

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Simon Lulu amesema Chama hicho kinajiandaa kwa ushindi wa kishindo kwa sababu kimefanya maendeleo kwa wananchi.

Amemweleza Mgombea Mwenza kiti  cha Urais Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28 mwaka huu, Upinzani mkoani hapo hawataambulia hata kiti  cha Udiwani.


Share:

Wahamiaji Haramu 32 Wakamatwa Wilayani Pangani

 ASKARI wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani Pangani wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 32 waliokutwa wakiwa karibu na hifadhi hiyo wakisafirishwa kupelekwa nchi za kusini mwa Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa wahamiaji hao Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora alisema kwamba wahamiaji hao walikamatwa Septemba 27 mwaka huu usiku.

Alisema ukamatwa huo waliofanya baada ya kupata taarifa kutoka wananchi wa Kijiji cha Buyuni kupitia Mwenyekiti wa Kijiji hicho Diwani Akida ambaye aliwaeleza uwepo wa mazingira yasiyoridhisha kwenye eneo lake hasa eneo la bahari baada ya boti moja kukwama.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo wao kama wahifadhi wana jukumu la kulinda maliasili na kuangalia usalama kwenye miji yote inayowazunguka waliandaa kikosi kazi cha kwanza waliokwenda eneo la tukio na walipofika waliwakuta wahamiaji hao eneo la bahari karibu na hifadhi hiyo katika kijiji cha Buyuni.

Alisema baadae hapo waliamua kutuma kikosi cha pili na ndipo walipofika na kufanikiwa kukaweka chini ya ulinzi wahamiaji 28 ambao ni raia wa Ethiopia lakini alfarji  wakapata taarifa nyingine ya uwepo wa wahamiaji wengine wanne ambao ni raia wa Somalia na wakatuma kikosi na kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi.

“Kati yao wapo wahamiaji 32 raia wa Ethiopia 28 na raia wa Somalia wanne akiwemo mwanamke mmoja kwa hiyo baada ya kufanikisha tukio hilo tumewafikisha na kuwakabidhi kwenye mamlaka ya Polisi kwa ajili ya hatua zaidi”Alisema

Awali akizungumza kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda aliwapongeza askari wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa kazi nzuri kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Polisi wilaya ya Pangani.

Hata hivyo amesema kwamba hivi sasa wametangaza vita mpya kwa mawakala wanaojishuhulisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu mkoani Tanga kwamba hawatasalimika watasakwa popote iwe ni nchi kavu, majini na kisha kufikishwa mahakamani.


 


Share:

Tundu Lissu adai bado hajapokea wito wa malalamiko

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kuwa hadi sasa bado hajapokea wito wala malalamiko yoyote kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kama taarifa ya tume hiyo ilivyoeleza hapo jana.

Lissu ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 30, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, na na kusisitiza kuwa kwa sababu hana wito wowote yeye ataendelea na ratiba zake za kampeni kama ilivyo kwenye ratiba.

Jana Septemba 29, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Wilson Mahera alitoa taarifa ya kuthibitisha kumuandikia barua ya wito Tundu Lissu, kufuatia tuhuma mbalimbali anazodaiwa kuzitoa kati ya Septemba 25 na 26 mjini Musoma



Share:

Armenia yakataa upatanishi wa Urusi katika mzozo na Azerbaijan Huku Mapigano Yakizidi Kupamba Moto

Armenia Jumatano imekataa pendekezo la Urusi la kutaka kuwa mpatanishi katika mazungumzo ya amani na hasimu wake mkubwa Azerbaijan, huku mapigano yakiwa yanaendelea kupamba moto kwa siku ya nne katika jimbo linalotaka kujitenga la Nagorno Karabakh.

Waziri mkuu  wa  Armenia Nikol Pashinyan amesema haitakuwa sahihi kufanya mazungumzo ya  amani  na Azerbaijan chini ya upatanishi wa  Urusi, wakati mapigano ya kuwania udhibiti wa jimbo yakiwa yanaendelea.

"Sio sahihi kabisa kuzungumzia kuhusu mkutano kati ya  Armenia, Azerbaijan na Urusi  katika wakati wa uhasama mkubwa," amesema Pashinyan wakati akizungumza na shirika la habari la Urusi Interfax.

Ameongeza kuwa hali endelevu na mazingira yanahitajika kwa ajili ya mazungumzo hayo.

Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti Jumatano kuwa waziri mkuu Pashinya amesema Armenia  haifikirii kuweka walinzi wa amani katika jimbo la Nagorno-Karabakh.

Kwa miaka kadgaa, vikosi vya Armenia na Azabajani vimekuwa vikizozania jimbo hilo la Karabakh, ambalo liliamua kutaka kujitenga na Azabajani baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieeti katika miaka ya 1990.

Mzozo huo wa muda mrefu uliibuka tena Jumapili huku pande hizo mbili zikirushiana silaha nzito za moto na kulaumiana kwa kuzuka kwa vurugu.

Karibu watu 100 wamethibitishwa kufa katika mapigano hayo ya hivi karibuni na pande zote mbili zinadai kuwa zimesababisha hasara kubwa kwa vikosi vya wapinzani.

 

DW



Share:

Benki ya Maendeleo ya Afrika yaipa Tanzania bilioni 15


Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imetoa zaidi ya shilingi bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya kutoa huduma kwa jamii katika Wilaya ya Buhigwe, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini na Kibondo mkoani Kigoma.
Hayo yamesemwa na na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya mtandao wa barabara ya Afrika Mashariki (EARNP) inayojenga mkoani humo.

Choma amesema kuwa AfDB imetoa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 256.2 kwa ajili ya kujenga barabara ya kujenga barabara ya kutoka Kabingo-Kasulu hadi Manyovu yenye urefu wa 260km. Ujenzi wa barabara hiyo ni moja ya utekelezaji wa miradi ya EARNP ambao unaiunganisha Tanzana na Burundi.

Kutokana na fedha zilizotolewa na benki hiyo miradi mbalimbali itatekelezwa katika wilaya hizo ikiwa ni pamoja na vituo vya mabasi, shule za msingi na sekondari, ujenzi wa masoko na ukarabati wa mabomba ya kusambaza maji, ujenzi wa vituo ya afya na hospitali za wilaya pamoja na barabara za mtaa.

 



Share:

Hospitali Ya Wilaya Karagwe Yakamilika Kwa 98%

SERIKALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imetumia sh. bilioni 1.8 kujenga majengo mbalimbali ya hospitali ya wilaya ya Karagwe ambayo yamekamilika kwa asilimia 98.

Hayo yamesemwa jana (Jumanne, Septemba 29, 2020) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kayanga, katika mikutano uliofanyika kwenye uwanja wa Changarawe, wilayani Karagwe, mkoani Kagera wakati .

Akielezea ujenzi wa vituo vya afya kwenye wilaya hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. milioni 900 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya vituo cha afya ambapo kati ya hizo, sh. milioni 500 zimetumika wa majengo ya kituo cha afya cha Kayanga ambapo kituo hicho kimekamilika na kinatoa huduma.

“Shilingi milioni 400 zimetumika kwa ujenzi wa majengo ya kituo cha afya cha Nyakayanja na ujenzi umekamilika. Pia shilingi bilioni 2.5 zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi huku fedha za dawa kwa mwezi zilikuwa ni wastani wa shilingi milioni 53,” alisema.

Akielezea uboreshaji wa miundombinu kwenye wilaya hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alisema uk. 74-76 wa Ilani ya uchaguzi ya CCM, unaelezea mpango wa Serikali kuanza ujenzi mpya (km 6,006.04) na ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Mugakorongo - Kigarama - Murongo yenye urefu wa km 105.

“Ilani yetu imeenda mbele zaidi na kuelezea mpango wa kukamilisha/kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina (km 7,542.75) barabara za mikoa kadhaa ikiwemo barabara ya Murushaka – Murongo yenye km 125.”

Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe, Bw. Innocent Bashungwa, mgombea udiwani wa kata ya Kayanga, na wagombea wa CCM wa kata za wilaya hiyo.

Alisema sh. bilioni 1.4 zimetolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya kufungua barabara mpya, matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi, muda maalum na makalvati. Alisema kati ya hizo, sh. milioni 585 zimetolewa kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofi na baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa kazi ni ukarabati katika barabara ya Nyakagoyagoye-Karongo ambao uligharimu sh. milioni 31.

Akielezea ukarabati uliofanywa, alisema sh. milioni 19 zimetumika katika barabara ya Kanyabuleza-Runyaga; sh. milioni 14 zimetumika na katika barabara ya Mato-Karehe; sh. milioni 23 zimetumika katika barabara ya Kihanga - Rwabitembe – Mshabaiguru, sh. milioni 16 zimetumika katika barabara ya Nyakahanga – Kamahungu, sh.  milioni 16 zimetumika katika barabara ya Kishoju – Bujuruga na sh. milioni 23 zimetumika katika barabara ya Igurwa-Kibona-Nyakahita.

Alizitaja barabara nyingine zilizofanyiwa ukarabati kuwa ni Katoju-Ihembe – Bisheshe iliyogharimu sh. milioni 98, barabara ya Kanyabuleza Jct-Makabulini iliyotumia sh. milioni 69, barabara ya KDVTC FADECO iliyotumia sh. milioni 73, barabara ya AMRI – CLASIC iliyogharimu sh. milioni 38 na barabara ya Rukore – Chanika iliyotumia sh. milioni 115.

Alisema TARURA ilifanya matengenezo ya madaraja na makalvati katika barabara za Katoju- Rugu - Ruhita (sh. milioni 17), Igurwa-Nyakashozi-Rwentuhe (sh. milioni13), Rukore - Chanika (sh. milioni 12), Rubale - Kibogoizi (sh. milioni 6) na barabara ya Kasheshe - Rubare (sh. milioni 7).

“Shilingi milioni 124 zimetumika kwa ajili ya matengenezo maalum katika barabara za Kajunguti - Rubare - Misha (km. 9), Nyabiyonza-Kafunjo (km. 6), Kibaoni Nyabiyonza Sec - Kakuraijo (km. 3.15), Nyakakika - Kandegesho (km.5), Lukole - Kigarama, Lukoyoyo – Kantabire -Nyakasimbi na Ahamulama – Busecha,” alisema.  

 


Share:

Vijiji 73 Kati Ya 77 Misenyi Vyapatiwa Umeme

 
VIJIJI 77 kati ya vijiji 73 vya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera vimepelekewa huduma ya umeme na vijiji 4 bado havina umeme.

Hayo yamesemwa jana (Jumanne, Septemba 29, 2020) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kassambya, katika mikutano uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, wilayani Missenyi, mkoani Kagera.

Amevitaja vijiji ambavyo havina umeme na vipo kwenye mpango wa kupelekewa umeme kuwa ni vijiji vya Buchurago, Katano, Kakunyu na Bugango.

Akizungmzia sekta ya mifugo ambayo imetajwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 hadi 2025 kuanzia ukurasa 47-52, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeisimamia vizuri sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wanapata manufaa.


“Shilingi milioni 23 zimetumika kukarabati machinjio ya Bunazi hapa Misenyi, pia tumerahisisha uuzaji wa mazao ya mifugo kwa kufuta tozo kero 114 katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na kuimarisha masoko ya mazao ya mifugo kwa kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo,” alisema.

Alisema Serikali imepanga kuanzisha vituo vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika mikoa 18 ambayo haina vituo, kuimarisha huduma za tiba za mifugo kwa kuhakikisha kila wilaya ina maabara, kliniki na daktari wa mifugo.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Nkenge, Dkt. Florent Kyombo na wagombea udiwani 13 wa CCM wa kata za wilaya hiyo. Mgombea udiwani wa kata ya Kassambya, Bw. Yusuph Jumbe na wenzake sita, wamepita bila kupingwa.

Kuhusu barabara, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 3.57 zilitolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara za wilaya hiyo zikiwemo barabara za Bukwali-Kashenye-Bushango, Ngorogoro-Kyabugombe, Mabuye –Itara na Ruzinga - Mugongo.

Alizitaja barabara nyingine kuwa ni za Gera – Ishozi – Ishunju, Nyankele – Kilimilire, Mabale–Mwemage-Kyaka, Nyankele-Nyamilembe–Kenyana na Kituntu–Bwengabo. Alisema mwaka 2020/2021, sh. milioni 711.6 zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara kwa muda maalum.

(mwisho)



Share:

GGML, RAFIKI SURGICAL MISSION WATOA GARI LA WAGONJWA KWA ZAHANATI BUKOLI – GEITA


Makamu Rais wa GGML, Simon Shayo (kulia) akimkabidhi kadi ya gari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Ali Kidakwa (kushoto.) 
Makamu Rais wa GGML, Simon Shayo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Afya Bukoli- Geita katika hafla ya kukabidhi gari la kubeba wagonjwa. 
****
NA MWANDISHI WETU, GEITA 
Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission kutoka Australia wametoa msaada wa gari la wagonjwa lenye gharama ya Sh milioni 32 kuhudumia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Bukoli na maeneo jirani wilayani Geita. 

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari hilo katika Kituo cha Bukoli Wilayani Geita, Makamu Rais anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo endelevu, Simon Shayo amesema msaada wa gari hilo umetolewa kwa wakati na utasaidia kutatua changamoto za usafiri kwa wagonjwa mahututi katika kata hiyo ya Bukoli na maeneo ya jirani. 

“Halmashauri ya Wilaya ya Geita iliomba msaada wa gari la wagonjwa kutoka GGML ili kuwasaidia wagonjwa katika jamii ya watu wa Bukoli ambao waliokuwa na changamoto kubwa kila ilipobidi kusafirisha wagonjwa kwa ajili matibabu makubwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Geita ambayo ipo wastani wa kilomita 35 kutoka kijiji cha Bukoli. 

" Ushirikiano kati yetu na Rafiki Surgical Mission ni mwitiko wa maombi hayo na umekuja muda mwafaka kwa kuwa wamekuwa pia na dhamira ya kusaidia huduma za afya mkoani Geita kwa miaka kadhaa sasa,” alisema Bw Shayo. 

Kwa karibu miaka 20 sasa, mbali na kutoa msaada wa vifaa tiba, Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission wameongeza wigo wa matibabu kwa watoto na watu wazima mkoani Geita ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya midomo sungura na migongo wazi kwa kuwapatia matibabu ya upasuaji bure. 

Bw Shayo amefafanua kuwa GGML pia walitoa msaada katika kituo cha afya cha Bukoli mwaka 2004 kwa kujenga jengo la Wagonjwa wa Nje (Outpatient Department) na nyumba ya watoa huduma wa afya. GGML pia imefadhili miradi mbalimbali ya afya wilayani Geita ikiwemo ukarabati wa Hospitali ya Rufaa mkoani Geita na ujenzi wa vituo vipya vya afya katika vijiji vya Nyamalembo, Nyakahongola, Kasota na Kakubiro ambapo miradi yote hiyo kwa pamoja iligharimu Shilingi bilioni moja na milioni mia nane (1.8bn) za Kitanzania. 

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka kwa niaba ya Serikali ametambua mchango wa GGML katika kutatua changamoto ya huduma za afya katika halmashauri ya wilaya na kwengineko mkoani Geita na kuwaomba washirika wengine waliopo katika Wilaya ya Geita kushirikiana na Serikali kwa lengo hilo hilo. Aidha mwaka 2019, GGML ilichangia pia vifaa tiba vyenye gharama ya Shilingi za kitanzania milioni 142 katika vituo vya afya vya Katoro na Bukoli. 

Share:

Wellness & Customer Service Manager at CVPeople Tanzania

CVPeople Tanzania | Full time Wellness & Customer Service Manager Dar es Salaam , Tanzania Job Description Our client is looking for Wellness & Customer Service Manager, the ideal candidate will supervise day-to-day operations in the customer service medical department Responsibilities: Respond to customer service issues in a timely manner. Create effective customer service procedures, […]

The post Wellness & Customer Service Manager at CVPeople Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger