Wednesday, 2 September 2020

LIVE: Mgombea Urais CCM Dr. Magufuli Akiomba Kura - Nzega


LIVE: Mgombea Urais CCM  Dr. Magufuli   Akiomba Kura - Nzega


Share:

SITAWAJIBU WANAONITUKANA KWENYE MAJUKWAA –UMMY MWALIMU

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu (CCM)ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza wakati akifungua ya Mafunzo ya uongozi kwa wagombea wanawake Ubunge na Udiwani ambayo itasaidia kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi semina hiyo imeandaliwa na Shirika la Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) ikiratibiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira kushoto na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo Rehema Maro


Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira akizungumza wakati wa semina hiyo
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation Rehema Maro akizungumza wakati wa semina hiyo
KATIBU wa UWT Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa semina hiyo Sophia Nkupe
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Husna Sekiboko
Sehemu ya washiriki mbalimbali kwenye semina hiyo
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema kwamba kamwe hatawajibu wanaomtukana kwenye majukwaa badala yake ataeleza namna nitakavyoweza kuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wakati akipewa ridhaa ya kuwaongoza.

 

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo leo wakati  semina hiyo itasaidia kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi semina hiyo imeandaliwa na Shirika la Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) ikiratibiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation .

 

Alisema kwamba atakachokifanya wakati akiendesha kampeni zake za kuwania Ubunge Jimbo hilo atajikita kwenye kueleza namna atakavyosaidia wananchi kuweza kujikwamua kimaendeleo kwa kuona namna ya kushirikiana nao katika kufikia mafanikio.

 

“Niseme tu kwamba nitakapokuwa kwenye kampeni sitatumia jukwaa kuwajibu ambao wananitukana badala yake nitajikita kwenye kutangaza maendeleo makubwa na mipango ambayo nitawafanyia wananchi wa Jimbo la Tanga lakini pia niwashukuru wajumbe wa UWT kwa sapoti kubwa kwangu”Alisema

 

Hata hivyo aliwaomba wanawake wanaowania uongozi kwenye nafasi mbalimbali wasiwe mawakala wa kuwatukana watu ikiwemo kuwadhalilisha wanawake wenzao na ukisikia neno limesemwa mwananke unakuwa wa kwanza kulishikia bango hiyo sio sawa hakikisheni mnabadilika.

 

Ummy aliwataka pia kuhakikisha hawawi mawakala wa kusambaza mambo ya ovyo yanayodhalilisha utu na haki ya wanawake kwa sababu wao ndio walezi wa familia na ndio watapambanaji ambao wanalea familia hivyo watambue wana umuhimu mkubwa kwenye jamii

 

“Ndugu zangu tusifanye kampeni za matusi za kudhalilisha wanawake wenzetu kwenye majukwa lakini niwaambie kwamba wakati wa kampeni zangu hawatanisikia nikiwajibu ambao wananitukana badala yake nitajikita kwenye kutangaza namna nitakavyoleta maendeleo”Alisema Ummy Mwalimu.

 

Hata hivyo aliwataka wanawake kuhakikisha wanasaidiana, kuacha kuoneana wivu na choyo badala yake washirikiane katika kujiletea maendeleo ambayo yatawasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii ambazo zinawazunguka.

 

Ummy aliwaomba wakati mwengine kuipeleka semina hiyo katika mikoa mingine wanawake kuwa mstari wa mbele kupigania vipaumbele vya wanawake katika afya ya mama na mtoto, elimu kwa watoto wa kike kwa lengo la kuweza kuwakomboa

 

Awali akizungumza wakati wa semina hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira amesema wamejikita kutoa elimu kwenye masuala ya lishe na kuhamamisha kilimo lishe.

 

Alisema kwamba mwaka juzi walianza mchakato maalumu wa kisera kuhakikisha agenda hiyo inaingia kikamilifu kwenye ilani ya uchaguzi mafanikio ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2025 agenda ya lishe imeingia kikamilifu kwani imekuwa kati ya vipaumbele vikubwa ya CCM.

 

Neema alisema kwa sababu watoto wanapokuwa na lishe duni hiyo ndio nguvu kazi ya kesho ili Taifa lolote likuwa lazima kuwepo na nguvu kazi thabiti ya kiuchumi

 

Hata hivyo alisema aganeda ya lishe imepata nafasi yake maalumu kwenye ilani ya CCM ya Mwaka 2020/2025 kati ya malengo ni kushuha hali ya udumuvu hadi kufikia kiwango cha asilimia 24 ndani ya miaka mitano.

 

 

Share:

Majaliwa Avunja Makundi Ccm Babati


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa  na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul (katikati) na   Esther Mahawe (kushoto) wakati alipowaasa  wanaCCM wote waliotia nia ya kugombea ubunge wa Jimbo hilo  waondoe tofauti zao  na wamuunge mkono mgombea aliyeteuliwa na CCM . Alikuwa akizindua Kampeni za CCM katika Mkoa wa Manyara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati


Share:

SHINYANGA SUPER QUEENS YATEMBEZA KICHAPO CHA MBWA MWIZI KWA VIVA QUEENS

Timu ya Shinyanga Super Queens

Timu ya Shinyanga Super Queens imeendelea kuonyesha makali kwenye michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwa Soka la Wanawake, baada ya kucheza michezo mitatu mfululizo bila kufungwa.

Leo mapema asubuhi ya Septemba 2, 2020, Shinyanga Super Queens imetoa kipigo cha mbwa mwizi kwa wapinzani wao wa Viva Queens baada ya kuishushia mvua ya mabao kwa kuikung'uta magoli 16-0 na kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Katika michuano hiyo inayofanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya Puma na Fountain Gate, Shinyanga Super Queens ambayo inasaka nafasi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao ilianza kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mkwawa Queens.

Katika mchezo wa Pili kwenye kundi lao la C uliochezwa jana dhidi ya Mt. Hanang ya Manyara, Vijana wa Shinyanga walilazimishwa sare ya mabao 3-3.

CHANZO : Shinyanga Press Club Blog

Share:

Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Magufuli aahidi neema zaidi Singida


Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli amesema shilingi bilioni 470.4 zimetumika katika miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Singida katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Akizungumza wakati wa kampeni za kuomba ridhaa ya wakazi wa Singida kumchagua tena katika nafasi ya Urais, Dkt. Magufuli ameainisha miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa vituo vya afya 15, hospitali za wilaya tatu, na wakina mama 730 wamefanyiwa upasuaji kupitia hospitali hizo.

Dkt. Magufuli amesema shilingi bilioni 52.6 zimetumika katika ujenzi wa shule, madarasa, mabweni na ukarabati wa shule kongwe za Mwenge na Tumaini

Ameongeza kuwa vijiji 232 vimepata umeme katika mkoa wa Singida na ameahidi kufikisha umeme katika vijiji vyote vilivyosalia katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu.

Mgombea huyo amefanya kampeni katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Manyoni, Ikungi na Singida katika mkoani Singida.


 



Share:

Mambo itakayofanya CHADEMA siku 100 za kwanza ikishinda Urais

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeainisha mambo 16 kitakachofanya siku 100 za kwanza iwapo kitachaguliwa na kupewa ridhaa ya kushika dola katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Katika Ilani yake yenye kurasa 104, chama hicho kimetaja mambo 16 ya kipaumbele ambayo yatatekelezwa siku 100 za kwanza, ambayo pamoja na mambo mengine itapeleka bungeni muswada wa sheria mbalimbali ikiwamo ya maridhiano.

Pia, ilani hiyo imeainisha vipaumbele 20 katika kujenga nchi yenye demokrasia, utawala bora na haki za binadamu.

Ilani hiyo imebainisha kuwa serikali ya CHADEMA itapeleka bungeni muswada wa sheria ya maridhiano ambayo pamoja na mambo mengine, itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza taifa.

Pia imejinasibu kuwa ndani ya siku hizo itapeleka bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ili kurekebisha kikokotoo cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wastaafu ili kiendane na mahitaji ya wastaafu.

“Serikali ya CHADEMA itaruhusu wafanyakazi na watumishi waliochangia katika mifuko ya jamii kuchukua mafao yao wakati wowote (Fao la kujitoa),” ilisema.

Ilani hiyo imebainisha kuwa itapeleka muswada wa sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi juu ya utoaji wa elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi sekondari.

Aidha, imesema itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia asilimia tatu ya mshahara wa mnufaika na kutanua wigo wa muda wa marejesho hadi kufikia miaka 25 tangu mnufaika apate ajira.

Kadhalika, imesema itafuta riba na tozo zote zitokanazo na adhabu ya kuchelewesha marejesho ya mkopo wa elimu ya juu.

“Serikali ya CHADEMA itashirikiana na sekta binafsi kuweka utaratibu wa kutoa huduma za afya ya msingi kwa wananchi bila malipo,” ilisema sehemu ya ilani hiyo.

Kwa mujibu wa ilani hiyo, serikali hiyo itarejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia iliyoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba.

Aidha, Serikali ya CHADEMA itatekeleza matakwa ya Katiba kuhusu Tume ya Pamoja ya Fedha ya Muungano ili kila nchi mshirika wa Muungano ipate mgawo wake wa fedha kwa mujibu wa Katiba na sheria.

Pia CHADEMA imejinasibu kuwa itarejesha uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuruhusu kurushwa moja kwa moja vikao vya kamati za Bunge, mikutano ya Bunge na mwenendo wa uendeshaji wa mashauri mahakamani.

Kwa mujibu wa Ilani hiyo, CHADEMA imesema itaanzisha utaratibu wa mazungumzo kati ya serikali ya Jamuhuri na Zanzibar kwa lengo la kufikia muafaka juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi wa bahari kuu na usajili wa meli.

“Serikali ya CHADEMA itaandaa mazingira rafiki na wezeshi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, kukosa ada, mimba kurejea kwenye mfumo rasmi wa elimu na kuamlizia masomo yao,” ilisema sehemu ya ilani hiyo.

Aidha, ilani hiyo ilibainisha kuwa itapeleka bajeti ya nyongeza bungeni katika mwaka wa fedha 2020/21 kwa ajili ya kuongeza mishahara ya watumishi wote wa umma, kulipa malimbikizo, sambamba na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa na kulipa mishahara inayoendana na madaraja yao.

Pia imesema itaanzisha bima maalum ya afya kwa watumishi wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wawapo kazini na baada ya kustaafu vikiwamo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.

CHADEMA imesema itarejesha maduka yasiyotozwa kodi katika vyombo vya ulinzi na usalama vikiwamo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.



Share:

ENGINEER II (WATER) at TANESCO

POST ENGINEER II (WATER) – 1 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) APPLICATION TIMELINE: 2020-09-01 2020-09-14   JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.Responsible for setting criteria and methodologies for hydrological data collection, compilation and analysis. ii.Undertake cost effective hydrological data analysis work at pre-feasibility, feasibility and other […]

The post ENGINEER II (WATER) at TANESCO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TECHNICIAN II (SURVEY) at TANESCO

POST TECHNICIAN II (SURVEY) – 1 POST POST CATEGORY(S) LAND MANAGEMENT WATER, MINING AND NATURAL RESOURCES EMPLOYER TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) APPLICATION TIMELINE: 2020-09-01 2020-09-14   JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.Assist to prepare drawings, plans, and topographic maps; ii.Prepare Survey instruments such as total stations, differential GPS and level machine prior […]

The post TECHNICIAN II (SURVEY) at TANESCO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ARTISAN – MECHANICS – 7 POST at TANESCO

POST ARTISAN – MECHANICS – 7 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) APPLICATION TIMELINE: 2020-09-01 2020-09-14 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.Servicing and repairing power generation machines under the directives from the supervisor. ii.Continuous checking of operating machines for preventive maintenance. iii.Assist mechanical technician sindisassembling machines during […]

The post ARTISAN – MECHANICS – 7 POST at TANESCO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Market Risk Manager at Absa Bank

Bring your possibility to life! Define your career with us Truly African We are a diversified standalone African financial services group, delivering an integrated set of products and services across personal and business banking, corporate and investment banking, wealth, investment management and insurance. Absa Group Limited is listed on the JSE and is one of […]

The post Market Risk Manager at Absa Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

16 Kortini Kwa Mauaji ya Kada wa CCM Songwe

Watu 16 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Songwe juzi, wakikabiliwa na shtaka la mauaji ya anayedaiwa kuwa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Briton Mollel.

Mauaji hayo yalitokea baada ya kuzuka vurugu kati ya watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusababisha watu wengine wawili kujeruhiwa.

Waliofikishwa mahakamani ni Peter Charahani, Ijumeleghe Mwanjila, Elia Sichone, Charles Simkonda, Daudi Mwajunga, Wiliam Simkoko, Oscar Philip, Yohana Mkumbwa, Feston Kitta, Tonny Siwale na Ayubu Mwakasege.

Wengine ni James Simkoko, Julius Wilson, Emmanuel Msinjili, Hidaya Mwangoka na Jenifer Mwasenga.

Wakili wa Serikali, Renatus Mkude, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kassim Mkwawa, kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo Agosti 25, mwaka huu katika eneo la kata ya Mwakakati Mji wa Tunduma wilayani Momba, mkoani Songwe.

Akiwasomea shtaka hilo katika kesi hiyo ya jinai , Wakili Mkude alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo la kuua kinyume cha kanuni ya adhabu Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania.

Hakumu Mkwawa aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 14, mwaka huu, ambapo watuhumiwa walirudishwa mahabusu kwa sababu kesi hiyo haina dhamana.


Share:

Shamimu Mwasha na Mumewe Wakutwa na Kesi ya Kujibu

Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mafisadi imesema kwamba mfanyabiashara Abdu Nsembo (45) na mke wake Shamimu Mwasha (41), wana kesi ya kujibu.

Kadhalika, mahakama hiyo imesema wanafamilia hao wataanza kujitetea kesho (Septemba 3).

Uamuzi huo umetolewa jana na mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Elinaza Luvanda baada ya kusikiliza mashahidi wanane na vielelezo sita vya Jamhuri.

Hata hivyo, washtakiwa waliieleza mahakama kwamba wanatarajia kuita shahidi mmoja pamoja na wenyewe, utetezi utakuwa na mashahidi watatu.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Veronica Matikila na Wakili wa Serikali Constantine Kakula.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei Mosi, mwaka huu, wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.




Share:

Technical Specialist – Water, Sanitation, Finance and Governance at Catholic Relief Services (CRS)

In Tanzania, CRS has served vulnerable communities for over 50 years and implements its programs through partnerships with the Government of Tanzania, International and local organizations and community entities for maximum impact and sustainability. CRS will be working in consortium with other international and national NGOs, and private sector partners, with the aim of expanding […]

The post Technical Specialist – Water, Sanitation, Finance and Governance at Catholic Relief Services (CRS) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Technical Specialist – WASH and Water Resource Management at Catholic Relief Services (CRS)

About CRS Catholic Relief Services is the official international humanitarian agency of the Catholic community in the United States. CRS works to save, protect, and transform lives in need in more than 100 countries, without regard to race, religion or nationality. CRS’ relief and development work is accomplished through programs of emergency response, HIV, health, […]

The post Technical Specialist – WASH and Water Resource Management at Catholic Relief Services (CRS) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 2,2020






















Share:

Tuesday, 1 September 2020

Monitoring & Evaluation Officer at Nelson Mandela African – AIST

Job Description Nelson Mandela African Institution of Science and Technology (NM-AIST) invites applications from suitably skilled, competent, and experienced Tanzanians for the post of the Monitoring &Evaluation officer at its Centre of excellence Water Infrastructure and Sustainable Energy – Futures (WISE- Futures).The Centre is funded by the World Bank under its eastern and southern Africa […]

The post Monitoring & Evaluation Officer at Nelson Mandela African – AIST appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tutors/Teachers at Andigo Tanzania

Science Tutor/Teacher (Physics, Chemistry, Biology) (Part Time) Job Summary We are seeking a passionate Sciences tutor capable of teaching Physics, Biology and Chemistry at primary and secondary school level Responsibilities Documenting and reporting on student’s progress Attending meetings with parents and staff whenever necessary Grading assignments in a timely manner Preparing and distributing learning materials Delivering […]

The post Tutors/Teachers at Andigo Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger