Tuesday, 1 September 2020

NJOO TUTETEME PAMOJA KWA LADHA SAFI YA DIAMOND ROCK NA HANSON'S CHOICE


Njoo tuteteme pamoja kwa ladha saaafi!!

Hanson's Choice!!

Diamond Rock!!

Share:

Hatua za Msingi za Kuzingatia Katika Usajili wa Ndege Zisizo na Rubani ( Drones)





Share:

picha: Mwenyekiti Wa CCM Rais Magufuli Ahutubia Wananchi Wa Bahi

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na mamia ya wananchi wakati akiwasili  wilayani Bahi mkoa wa Dodoma kwa mkutano wa kampeni wa hadhara leo Jumanne Septemba 1, 2020, ikiwa ni kituo chake cha kwanza toka azindue rasmi kampeni zake za kugombea Urais



Share:

Wizara Ya Kilimo Yagawa Vifaa Vya Tehama Vya Kujifunzia Vyenye Thamani Ya Tsh.milioni 248.69 Kwa Vyuo 14 Vya Kilimo Nchini.

Na.Faustine Galafoni,Dodoma.
Katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vitabu vya kujifunzia katika vyuo vya kilimo hapa nchini,Wizara ya kilimo imeamua kugawa vifaa vya kielektroniki  katika vyuo 14  vya kilimo   nchini vyenye thamani ya Tsh.Milioni 248.69.

Akizungumza na waandishi wa Habari Agosti,31,2020 jijini Dodoma katika hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo vya TEHAMA , Katibu mkuu Wizara ya Kilimo  Gerald Msabila Kusaya  amebainisha kuwa  tangu ateuliwe kuwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo tarehe 5,Machi mwaka huu amebahatika kufanya ziara katika vyuo mbalimbali vya elimu ya kilimo  hapa nchini na kubaini changamoto ya uhaba wa vitabu hivyo na kuamua kununua vifaa vya kielekroniki kwa ajili ya kujifunzia .

“Baada ya kuona changamoto hiyo tulijadili na wadau tukaona namna nzuri ya kusoma  kwa njia ya kielekrtoniki  hivyo tumeamua kununua kununua vifaa mbalimbali hali itakayosaidia wanafunzi wetu ambao ni wataalam wa baadae wa kilimo kujifunza kwa njia ya mtandao na vifaa hivyo vikigharimu Tsh.Milioni 248.69 “amesema.

Aidha,Katibu mkuu huyo wa Wizara ya kilimo ametoa wito kwa wakuu wa vyuo vya kilimo kuhakikisha wanasimamia vinatumika vizuri na mara kwa mara ili kuwandaa  wataam wa kilimo wanaoendana na wakati.

Wakitoa neno la shukrani baada ya kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya Wakuu wa vyuo 14 vya serikali,mkuu wa chuo cha Kilimo Mlingani Samson Cheyo pamoja na kaimu mkuu wa chuo cha Sukari [National Sugar Institute-NSI] Kilichopo Kilombero Mkoani Morogoro  Aloyce Kasmir wamesema vifaa hivyo vya TEHAMA vitarahisisha katika ufanisi wa kujifunza.

Baadhi ya vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa ni pamoja na Rooter Machine,Kompyuta mpakato[laptop],Desk top,TV vikiwa na thamani ya Tsh.Milioni 248.69.


Share:

CCM Yafanya Uteuzi wa Wagombea Uwakilishi katika Baraza la Wawakilish Zanizbar

Kamati  Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya uteuzi wa wagombea Uwakilishi katika Baraza la Wawakilish  Zanizbar katika majimbo 50 kwa kuzingatia uwezo, umahiri na utendaji wao.
Kikao cha kamati kuu kimefanyika jana Jumatatu tarehe 31 Aagosti 2020 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole alitangaza majina ya walioteuliwa.

Polepole aliwataja waliopitishwa na majimbo kwenye mabano kuwa ni Zawadi Aamour Nasoro (Konde), Shamata Shahama Khamisi (Micheweni), Saidi Sale Salim (Tumbe), Tunu Mwalimu Masoud (Wingwi), Maliam Dhani Juma (Gando), Makame Said Juma (Kojani) na Othman Ali Khamis (Mtambwe).

Wengine ni Khamis Dadi Khamis (Pandani), Harus Said Suleiman (Wete), Shaibu Hassan Kaduara (Chake) Suleiman Masoud Makame (Chonga) Masoud Ali Mohammed (Ole), Bakari Hamad Bakari (Wawi), Suleiman Makame Ali (Ziwani), na Bahati Khamis (Chambani).

Mussa Kombo Mussa (Kiwani), Abdul Hussein Kombo (Mkoani), Mohammed Mgaza Jecha (Mtambile), Nadir Yussuf (Chaani), Juma Mkungu Juma (Kijini) na Mkwajuni ni Sulubu Kidongo Amour.

Pia wamo Abdul Abbas Wadi (Nungwi), Haji Omar Kheri (Tumbatu), Mtumwa Peya Yussuf (Bumbwini), Khalid Salum Mohammed (Donge), Asha Abdallah mussa (Mahonda), -Issa Haji Gavu (Chwaka), Haroun Ali Suleiman (Makunduchi), Paje- Dk. Soud Nahoda Hassan (Paje) na Mwanaasha Khamis Juma (Dimani).

Wengine ni Yussuf Hassan Iddi (Fuoni), Suleiman Haroub Suleiman (Kiembe Samaki), Ameir Abdallah Ameir (Mwanakerekwe), Ali Suleiman Ameir (Pangawe), Mudrik Ramadhan Soraga (Bububu), Machano Othman Said (Mfenesini), Hussein Ibrahim Makungu (Mtoni), Mihayo Juma Nhunga (Mwera), Hassan Khamis Hafidh (Welezo) na Rukia Omar Mapuri (Amani).

Miraji Khamis Mussa (Chumbuni), Jamaal Kassim Ali (Magomeni), Shaaban Ali Othman (Mpendae), Hamza Hassan Juma (Shaurimoyo), Ali Gullam Hussein (Jang’ombe), Nassor Salum Ali (Kikwajuni), Yahya Rashid Abdallah (Kwahani) na Malindi ni Mohammed Ahmada Salum


Polepole alisema Kamati Kuu imepitisha majina ya wawakilishi kundi la wanawake kwa Mkoa wa Kaskazini Pemba ambao ni Bihindi Hamadi Khamis, Chumu Kombo Khamis, na Farida Hamad Juma na Kaskazini Unguja ni Panya Ali Abdalah, Mwanajuma Kasim Makame na Fatma Hamza Mohamed.

Mkoa wa Kusini Pemba waliopitishwa ni Shadia Mohamed Suleimani, Zuhura Mgeni Othman na Zainab Omar Amir wakati Mkoa wa Kusini Unguja ni Salma Juma Bilal, Rahma Kasim Ally na Arafa Ali Yusuph.

Katika mkoa wa Magharibi Unguja, waliopitishwa ni Fatma Ramadhani Mandoba, Mwanaidi Kassim Mussa na Fatma Ali Akhmed na Mkoa wa Mjini Magharibi ni Saada Ramadhani Mwendwa, Mgeni Hassan Juma na Salma Abdi Ibada.

Kadhalika, Polepole alisema Kamati Kuu imewapitisha wawakilishi wanawake kwenye kundi la wenye ulemavu, ambao ni Mwantatu Mbaraka Khamis na Zainab Abdallah Salum na kundi la wasomi ni Riziki Pembe Juma,

Kwenye kundi la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) waliopitishwa ni Salha Mohamed Mwinjuma na Rahma Mbaraka Tahir na kwa upande wa wazazi ni Sabiha Filfili na Aza Januari Joseph.


Share:

CCM Wamuonya Maalim Seif...."Aache Kuchafua Viongozi Wetu"

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  amemtaka Maalim Seif Sharif Hamad kuacha kuchafua viongozi wa chama hicho, vinginevyo atashughulika naye.

Bila ya kumtaja jina, Polepole amesema ‘Mzee Yule’ amekuwa na tabia ya kuchafua viongozi wa chama hicho.

Polepole ametoa kauli hiyo jana  Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020, wakati akitaja orodha ya wagombea uwakilishi visiwani humo.

"Lakini nataka kutoa rai mzee yule (ambaye hakumtaja jina) aache kutaja majina ya viongozi wetu, aache na leo nimetoa heshima kubwa , nimeambatana hapa na wajumbe wenzangu wa Halmashauri Kuu Taifa Bara na Zanzibar ili haya ambayo ninawaeleza ifahamike ndio msimamo wa Chama chetu,"alisema Polepole.

Alisisitiza ni vema akaacha na anajua Chama Cha Mapinduzi wamepiga hatua na itakuwa ngumu kwa vyama vingine kupiga siasa ya kueleweka ,wajipange sio kutengeneza hoja ya kubumba bumba zisizo na mashiko.

",Nimehuzunika sana mzee yule kwasababu anasema uongo kabisa tena hadharani na sina hakika huenda anatafuta namna tumshitaki ili apate kiki kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, hakuna kitu kingine anachotaka zaidi ya kuvuta hisia za watu.

"Anataka kutengeneza kitu hivi, kutengeneza umaarufu sisi hatutafanya hivyo lakini tunamuonya afanye siasa yake,mambo ya CCM atuachie  , ziko kauli ambazo Chama Cha Mapinduzi hatuna tatizo nazo zilishakwisha atuache,ni vizuri ajifakari afanye kazi ambazo zitakuwa na tija .

"Wapiga kura wengi ni vijana zaidi na wazee ni wachache ,tunasema kwa mkiki huu tunaokwenda nao miaka mitano ya kutekeleza ilani tunakwenda mara tatu zaidi  ya miaka mitano iliyopita.Basi ni vizuri tukamaanisha watu, tumekwenda kule Pemba eneo la Mtambwe Taya ambako ndiko anatoka hajawahi kufanya kitu chochote hata kujenga mnara wa mita moja hajawahi.

"Pale Mtwambwe Taya kimejengwa chuo cha ufundi stadi na pale wanafunzi watasoma ,kuna shule ya bweni , ziko bweni za kutosha watoto karibu 200 watakaa pale watadundishwa ufundi wa aina mbalimbali.Na mambo hayo yote yamefanyika pale lakini huyu mzee hakufanya chochote, huyu ameshika nafasi ya uandamizi katika serikali hakufanya chochote.

"Sasa anatupotezea muda anamsema mgombea wetu , tunasema acha, hii ni mara ya mwisho,tutashulika na wewe katika namna ambayo inaweza kuleta habari nyingine, fanya kampeni za kistaarabu na sisi tumezindua kampeni juzi nzuri kabisa hatutaki kusema watu, tunasema hoja, tunajenga sababu kwa watanzania,tumepewa heshima kubwa sana katika miaka mitano tumefanya kazi kubwa, kazi imefanyika kule Zanzibar."  Alisema Polepole


Share:

Maofisa Benki, BRELA Kizimbani Kwa Kughushi Dola 300,000

Raia wawili wa kigeni, wafanyakazi wawili wa benki ya Equity na Msajili Msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 13 likiwemo la kughushi na kutakatisha  USD 300,000.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa jana mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon imewataja washtakiwa hao kuwa ni,  Mohammed Nur (48) raia wa Afrika Kusini, Umulkher Mohammed (34) raia wa Somalia, wote wafanyabiashara na Noel Shani (44) mfanyakazi Brela.

Wengine ni wafanyakazi wa Benki, Alex Ndondole (33) na Emma Chikaonda ambaye hakuwepo mahakamani.

 Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu imedaiwa kati ya Machi 2011 na Mei 30, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wote walikula njama kufanya kosa la kujipatia fedha kwa udanganyifu.

Katika shtaka la pili, mshtakiwa Nur na Mohamedi, wanadaiwa kughushi maamuzi ya bodi ya Kampuni ya Alliance Cargo Handling ltd ya February 8,2014 kuonyesha kuwa Kampuni hiyo imekubaliana kufungua akaunti katika Benki ya Equity tawi la Prestige wakati si kweli.

Wakili Wankyo amedai katika shtaka la tatu kuwa, Aprili 12, 2015 washtakiwa Nur na Mohamedi, walighushi maamuzi ya bodi ya Aprili 12, 2015 wakionyesha kwamba bodi imekubali kufungua akaunti Benki ya Amana tawi la Nyerere Road huku wakijua kuwa siyo kweli.

Pia inadaiwa, Aprili 18 mwaka 2011 washtakiwa hao walighushi barua kuonesha kuwa imetolewa na Brela kwa kuonesha kwamba Mohammed ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance huku akijua si kweli.

Aidha katika shtaka la tano mshtakiwa hao hao, Nur na Mohamed, wanadaiwa kughushi maamuzi ya bodi ya Machi 5, 2016 wakionesha Kampuni ya Alliance inabadili jina kutoka Alliance Cargo kwenda Africa Flight Service Tanzania wakati si kweli.

 Februari 8, 2014 mshtakiwa Nur aliwasilisha nyaraka ya uongo ya maamuzi ya bodi kuonesha kwamba wamekubali kufungua akaunti Equity benki huku katika shtaka la saba mshtakiwa huyo aliwasilisha nyaraka  Amana benki kuonesha kuwa kampuni imekubaliana kufungua akaunti.

Aidha mshtakiwa Nur anadaiwa kuwasilisha Brela  nyaraka kuonesha wamekubaliana kubadilisha jina la kampuni huku wakijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la tisa, inadaiwa Februari 10,2014 maeneo ya Equity Benki , mshtakiwa Nur na Mohamed  kwa nia ya kufanya udanganyifu katika akaunti ya Kampuni ya Cargo iliyopo Equity , kwa udanganyifu walichukua mkopo wa USD 300,000.

Wankyo alidai shtaka la 11, mshtakiwa tatu akiwa Msajili Msaidizi Brela anadaiwa kushindwa kuzuia uhalifu huku katika shtaka la 12 na 13 washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha  USD. 300,000.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Pia wakili Wankyo aliomba washtakiwa hao warudishiwe polisi kwa kuwa bado hawajapimwa Corona, ombi ambalo mahakama iliridhia kwa ajili ya vipimo na kesi itatajwa Septemba 7 mwaka huu.


Share:

Mgombea Urais wa CCM Dr Magufuli Kutua Singida Leo

Maandalizi ya kumpokea mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida Dkt John Pombe Magufuli yamekamilika.

Akizungumza jana  na waandishi wa habari juu ya maandalizi hayo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu alisema maandalizi yamekamilika ambapo leo  wanatarajia kumpokea Mgombea huyo mkoani hapo.
 
Alisema pamoja na maandalizi yote mgombea huyo atahutubia wanachama na wananchi pamoja na kunadi ilani ya chama hicho ya mwaka 2020-2025 ambayo alisema imejaa shehena ya vitu vizuri,pia atapata fursa ya kuwatambulisha na kuwanadi wagombea nafasi ya ubunge katika majimbo nane ya mkoa huo.


Share:

Watu Wanne Mbaroni Kwa Tuhuma Za Makosa Ya Kupanga Tukio La Mauaji Ya Mtu Mmoja Jijini Mwanza

Jeshi  La  Polisi  Mkoa  Wa  Mwanza  Linawashikilia  Watu  4  Kwa  Tuhuma  Za  Makosa    Ya Kupanga Tukio  La  Mauaji  Ya  Mtu  Mmoja Wilayani  Ukerewe.

Tarehe 25.08.2020 Majira Ya 02:00hrs Usiku Eneo La Mission, Kata Ya Nyamanga, Kisiwa Cha Ukara, Wilaya Ya Ukerewe, Mkoa Wa Mwanza, Andrew Magai, Miaka 48, Mkara, Mkristo, Mkulima Wa Kijiji Cha Chibasi, Aliuawa Kwa Kupigwa Sehemu Mbalimbali Za Mwili Na Kukatwa Na Vitu Vinavyodaiwa Kuwa Na Ncha Kali Kwa Madai Kuwa Marehemu Kabla Ya Kifo Chake Aliwasafirisha Watu Ambao Hawakutambulika Kwenda Kuvunja Nyumba Ya Magesa Simon @ Wile.

Uchunguzi Wa Awali Umebaini Kuwa Tukio La Kuvunja Nyumbani Kwa Magesa Simon @ Wile Lilikua Ni La Kutengenezwa Ili Kuhalalisha Mauaji Yaliyotokea Eneo Hilo. 

Uchunguzi Wa Kina Unaendelea Ukihusisha Wataalamu Mbalimbali. Mwili Wa Marehemu Ulifanyiwa Uchunguzi Na Daktari Katika Kituo Cha Afya Bwisya Na Kukabidhiwa Kwa Ndugu Kwa Mazishi.

Waliofikishwa Mahakamani Leo 31/08/2020 Ni:-

1.Magesa Simon @ Wile, Miaka 50, Mkala, Mkulima, Mkazi Wa Nyamanga.

2.Makanje Mgeta, Miaka 28, Mkara, Mkazi Wa Kijiji Cha Chibasi.

3.Mkapa Magesa@simon, Miaka 24, Mkara, Mkulima, Nyamanga.

4.Selestini Datusi, Miaka 22, Mkerewe, Mkristo, Mkulima, Nyamanga.

Watuhumiwa Wote Wamefikishwa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kujibu Tuhuma Zinazowakabili.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawataka Wananchi, Wanasiasa Wa Vyama  Vyote  Kutojiingiza Katika Mambo Ambayo Yanaweza Kuhamasisha Uvunjaji Wa Sheria Na Kuvuruga Amani Na Utulivu Wa Nchi, Limeapa Kuendelea Kuchukua Hatua Kali Kwa Kila Atakayekiuka Sheria.

Imetolewa Na:-
Muliro Jumanne Muliro – Acp
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
31 August, 2020


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne September 1


















Share:

Monday, 31 August 2020

Picha : KEMBAKI AZINDUA RASMI KAMPENI UBUNGE TARIME MJINI …AAHIDI MAKUBWA AKICHAGULIWA, MAKADA WATIA NENO



Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia chama cha Mapinduzi CCM Michael Kembaki akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni zake.
**
Na Dinna Maningo - Tarime
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) Michael Kembaki amezinduka Kampeni ya kugombea ubunge huku  akiahidi kufanya maendeleo makuwa ikiwemo upatikanaji wa huduma ya maji safi ,miundombinu ya barabara na ujenzi wa Soko kuu.

Katika uzinduzi huo walihudhuria Viongozi na wanachama wa CCM, Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara,kada maarufu wa CCM na mmiliki wa Mabasi,Peter Zakaria ,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa mkoa wa Mara Christopher Gachuma,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Samwel Kiboye (Namba Tatu) na wananchi.

Kembaki alisema kuwa Tarime haina maji safi na salama  na kwamba hata chanzo cha maji mto Nyanduruma hakitoshekezi mahitaji na wakati wa kiangazi chanzo hicho hukauka.

"Nashukuru chama changu kuniamini na kuniteua,kura mlizonipa 2015 wakati nagombea Ubunge zilinipa imani nikaamua kurudi ,ndugu zangu muungwana ni yule anayeshukuru hata kwa kidogo,najua kuna wananchi waliniamini walinipigia kura",alisema Kembaki.

Aliongeza "Nakumbuka ahadi nilizozitoa niliona kero mbalimbali nikajinyima na baadhi nikazitatua hii kero ya maji imekuwa ni kilio, chanzo cha maji kipo Kenyamanyori lakini hata wananchi wa hapo hawapati maji na ni machafu ukifua nguo nyeupe ina badilika rangi naomba mnichague nitatue kero ya maji na soko kuu lililotelekezwa kwa muda mrefu bila kujengwa nitahakikisha linajengwa".

Akizungumzia ubovu wa miundombinu ya barabara Kembaki alisema kuwa wilaya ya Tarime ina rasilimali nyingi ambapo barabara za mjini zote zilitakiwa kuwa za lami na si za vumbi.

"Akina mama wanauza matunda kwenye vumbi huwa nikipita na kuwaona roho inauma, mkinichagua ntahakikisha naboresha mazingira rafiki ya biashara ,waendesha pikipiki wanapata tabu pikipiki zinawahi kuharibika kwa sababu ya ubovu wa barabara", alisema Kembaki.

"Nimezunguka kata 8 nimechangia maendeleo mwenzangu Esther Matiko wa CHADEMA wakati wa kugombea 2015 aliahidi kujenga ghorofa shule ya msingi Sabasaba ahadi ambayo mpaka leo hajaitekeleza ila mimi nilisema sina uwezo ntajenga darasa la kawaida nanyi ni mashahidi mnaona wanafunzi wanasoma niliyoyaahidi nimetekeleza kwa asilimia 80 ",alisema Kembaki.

Mke wa mgombea huyo Magreth Rhobi aliwaomba wananchi kumpa kura mmewe ili afanye maendeleo.

Katika uzinduzi huo  baadhi ya makada wa CCM waliokuwa wakitia nia kugombea ubunge kupitia chama hicho akiwemo Jackson Kangoye aliyekuwa mshindi namba moja ambaye hata hivyo jina lake halikurudi na badala yake vikao vya chama Taifa  vilimteua Michael Kembaki wamehudhuria uzinduzi huo wa Kampeni .

Kangoye aliwashukia watu wanaoeneza maneno kupitia mitandao ya kijamii kuwa yeye hamuungi mkono Kembaki na kusema habari hizo ni za uongo.

"Nimesikia maneno mengi kuwa mimi simuungi mkono Kembaki ni uongo mimi nitashiriki na Kembaki katika kampeni zake tumsaidie aweze kushinda,aligombea 2015 kura hazikutosha saizi kajipanga na ninaamini tutashinda na ikiwezekana aongoze miaka 10",alisema Kangoye.

Manchare Suguta ambaye ni ndugu wa mgombea ubunge jimbo la Tarime vijiini John Heche aliwaomba wananchi kumpigia kura Kembaki na Mwita Waitara anayegombea jimbo la vijijini.

"Hatuna muda wa kupoteza hapa ni kazi tu kwahiyo ndugu zanngu tumpe kembaki ni mtu wa kazi msidanganyike hapa ni kazi tu",alisema Susy Chambili.

Veronica Nyahende alisema "Wana Tarime tumepata nafasi tusiicheze tuwape kura CCM kwa maendeleo ya Tarime,akina mama tumechoka kubeba maji kichwani.

Wakili wa kujitegemea Onyango Otieno alisema"tuna matatizo mengi maji yetu ni shida UTI,Typhoid ni nyingi tunamtuma Kembaki atuletee maji,bararaba ni shida kama ya Kenyamanyorii".

"Mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Vijana wa mkoani, nafahamu mambo mengi ambayo jimbo la Tarime mjini imeyakosa,huwezi kupata maendeleo kwa chama kisicho na Ilani  niwaombeni kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ndiyo kosa mpigieni Kembaki",alisema Ditu Manko.

Hezbon Mwera alisema "Tarime mjini tunataka sasa tumtume Kembaki atuletee maendeo tunachohitaji sisi ni maendeleo tunataka mipango na miradi inayoonekana.

Mgombea ubunge viti maalum Mara Amina Makilagi aliwaomba wananchi" naomba mpigie CCM nina uzoefu ndani ya bunge sisi wabunge wa ccm tukikutana tunajadiliana kwanza kwenye vikao tupeni Kembaki atakayekwenda kusemea maendeleo, katika bajeti iliyopita tumepata mradi wa maji na Tarime imo,jiulize tangu tumepitisha fedha mbona hazijaja tupeni Kembaki maji yaje".

Roselina mgombea viti maalumu kundi la walemavu alisema "nashukuru kwa kunichagua hadi ngazi ya Taifa sisi watu wenye ulemavu tunapata shida hatuna mtu wa kutusemea nilitembelea shule moja hakuna vifaaa, walemavu wanahangaika mazingira si salama huku mgombea ubunge viti maalumu kundi la vijana akiwaomba vijana kumchagua Kembaki.

Wazee wa mila kutoka koo 12 za jamii ya Wakurya nao hawakuwa nyuma kumnadi Kembaki na Waitara, Nchagwa Mtongori mzee wa mila kutoka koo ya Wanchari alisema kuwa ili wananchi wapate maendeleo ni vema wachague CCM kwakuwa wao ni watekelezaji.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa Charles Mniko aliwataka wazee wa mila kuungana pamoja kuiwezesha CCM kushinda.

Kada wa CCM ambaye pia ni mmiliki wa mabasi ya Zakaria yanayofanya safari zake Sirari-Mwanza Peter Zakaria alisema"nimejitahidi kuchangia maendeleo hospitali ilikuwa imeoza hatukutumia pesa za Serikali hata sh.100 najua nilipopata matatizo mlilia sana sasa naomba msiniangushe niko salama mpeni kura Kembaki"alisema Zakaria.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tarime Daud Ngicho  alisema kuwa Rais Magufuli ametatua kero nyingi ikiwemo ya uanzishwaji wa masoko ya dhahabu ambayo yamewawezesha wafanyabiashara kuuza dhahabu huku akiwalalamikia waliokuwa wabunge wa Tarime kutoka CHADEMA kuingilia kesi zisizowahusu na kushindwa kushughulikia kero za watu wa Tarime  hili hali hawakuwa na kesi kwenye majimbo yao wanayotoka.

Mjumbe wa Halmashauri ya Taifa mkoa wa Mara Christopher Gachuma alisema uzinduzi ulikuwa wa kuwatambulisha wagombea nakwamba anaimani CCM itashinda kwa kishindo.

Mwenyekiti wa chama CCM mkoa wa Mara Samwel Kiboye (Namba tatu) alisema kuwa baadhi ya wanaCCM ni vigeugeu.

"Safari hii hatutawakubali wasaliti ndani ya chama,Kembaki Unapoenda kuomba kura mtangulize mungu ukimtanguliza shetani hakusogelei na mungu hasemi uongo mungu mambo yake yamenyooka safari hii lazima tukomboe majimbo.

"Tunataka kampeni ya Kiungwana sisi ndiyo tuna Serikali lakini tunaomba kampeni za heshima,tutangulize mungu mbele kwa kila jambo,tumeshavunja makundi ,mimi saizi Waitara namuunga hatuna utofauti lengo letu tunataka CCM ishinde tofauti zetu tumeziondoa,wanaccm msilizike tafuteni kura."alisema Keboye

Naye mgombea Ubunge jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara alisema "wagombea wote wa upinzani nawafahamu,kama tunataka kero zitatuliwe nakuomba pigia CCM ,kama mnataka tuachane na maji ya tope pigia Kembaki,mimi niiliona nijipendekeze ili nipate miradi nikaingia CCM ,Ukija spidi nitakutuliza ,ukija taratibu nitatulia vijana tumejipanga hii ngoma mtoto hatumwi sokoni",alisema Waitara.
Umati wa watu wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia CCM Michael Kembaki
Katibu wa CCM wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka wakicheza na wana CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini
Wafuasi wa mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni
Wafuasi wa mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni
Wafuasi wa mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Makada wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni .Kulia ni mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki,wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Samwel Keboye,wa kwanza kushoto ni mmiliki wa mabasi Peter Zakaria,wa pili kushoto ni Mjumbe wa NEC Christopher Gachuma
Wananchi wakicheza ngoma ya Ritungu wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Wasanii wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge Michael Kembaki


Wasanii wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge Michael Kembaki
Share:

ACT WAZALENDO YAZINDUA ILANI YAKE YA UCHAGUZI MKUU 2020 IKIWA NA VIPAUMBELE 10


Chama cha ACT-Wazalendo leo Agosti 31, 2020 kimezindua Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu 2020 ikiwa na vipaumbele 10 vyenye majibu ya changamoto mbalimbali za Watanzania.


Chama hicho kimezindua ilani hiyo itakayowawezesha wagombea urais, ubunge na udiwani kuinadi katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Mbali na uzinduzi huo, pia Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe alimkabidhi Ilani hiyo, mgombea urais wa chama hicho, Bernard Membe na mgombea mwenza Omar Fakih Hamad ili waitumie kusaka kura kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa Ilani hiyo, chama hicho kimejinasibu kutekeleza na kuvisimamia vipaumbele hivyo ambavyo ni pamoja na:- Ujenzi wa Demokrasia na utoaji Haki za watu, Ufanisi na ubora wa Huduma za jamii, -Uchumi wa watu, Uhuru kwa kila mtu na Elimu bora itakayotolewa bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu.

Vipaumbele vingine ni Kilimo cha kimapinduzi na mazingira wezeshi ya biashara, Usawa na Ustawi wa Wanawake na Vijana, Hifadhi ya Jamii kwa kila mtu/Afya bora kwa wote, Ushirika wa kisasa kwa maendeleo jumuishi, Haki za watu wenye ulemavu, Maji safi, Salama na gharama nafuu na ajira mpya milioni 10.


Share:

Watumishi Wanne Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mikononi Mwa TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwafikisha mahakamani watu watano wakiwemo wanne watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa makosa ya rushwa, uhujumu uchumi na ukwepaji kodi wa Sh.153.5 milioni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 na Doreen Kapwani, Afisa Uhusiano wa Takukuru kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo imesema, watumishi hao walikwisha fukuzwa kazi watafikishwa mahakamni leo.

Doreen imetangaza kutafutwa kwa Madaraka Robert Madaraka, aliyekuwa mhasibu wa Bandari ya Kigoma anayetuhumiwa kuhusika katika tuhuma hizo ili aweze kuunganishwa na wenzake.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger