Sunday, 7 June 2020

Yanga Yapigwa Bao 3- 0 Na KMC

Dakika 90 za mechi ya kirafiki kati ya Yanga na KMC Uwanja wa Uhuru  zimekamilika kwa Yanga kukubali kichapo cha mabao 3-0.

KMC ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Sadala Lipangile dakika ya 31 kwa pasi ya Charlse Ilanfya na bao la pili likapachikwa na Ilanfya kwa pasi ya Emmanuel Mvuyekule 

Bao la tatu lilifungwa na Hassan Kabunda dakika ya 65 kwa mpira wa adhabu.


Share:

Wagonjwa wa Corona Nchini Kenya Wafika 2767 baada ya Wengine 167 Kuongezeka Leo

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 2,767 baada ya wagonjwa wengine 167 kupatikana na virusi hivyo kutoka sampuli 2,833 zilizofanyiwa vipimo.

Akitoa taarifa za kila siku kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba wagonjwa hao wapya wanaume 125 na wanawake 42.

Bwana Kagwe amesema hatahivyo wagonjwa wengine 46 wamepona, hatua inayoongeza idadi ya wagonjwa waliopona kufikia 752.

Amesema kwamba mgonjwa mwingine mmoja amefariki kwa ugonjwa huo na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 84.


Share:

Waziri Mhagama Apongeza Mafanikio Yaliyofikiwa Katika Ujenzi Kiwanda Cha Bidhaa Za Ngozi Cha Karanga

Na; Mwandishi Wetu, Moshi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametoa pongenzi kwa Jeshi la Magereza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa hatua waliyofika katika ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za Ngozi cha Karanga.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo wa ujenzi wa kiwanda hicho uliopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro ambapo hatua za ujenzi umefikia asilimia 97 Waziri Mhagama alieleza kuwa mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuendeleza uchumi wa Taifa kupitia Viwanda.

“Mradi huu wa ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha bidhaa za Ngozi hapa Karanga ni mmoja ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ambayo inatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano na utakuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengine utakapoanza uzalishaji wa bidhaa za Ngozi ambazo zitakuwa zinazalishwa hapa nchini,” alieleza Mhagama

“Nimeridhika na kasi ya ujenzi wa mradi huu, na nitoe pongezi zangu kwa Jeshi la Magereza linalosimamia ujenzi wa mradi huu kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF) hatua mliyofikia kwa kweli ni nzuri,” Alisema Mhagama

Alifafanua kuwa, Kiwanda hicho kitakavyo kamilika mapema kitakuwa na manufaa makubwa kwa taifa ikiwemo kutoa fursa za ajira kwa Watanzania pamoja na kuongeza mapato ya Serikali kupitia bidhaa zitakazokuwa zinazalishwa na kiwanda hicho kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Aliongeza kuwa kukamilika kwa majengo manne ya msingi katika kiwanda hicho ina ashiria kuwa hatua iliyobaki sasa ni kusimikwa mitambo ya uchakataji wa ngozi ili kiwanda hicho kiweze kuanza kazi ya uzalishaji haraka.

Aidha, Waziri Mhagama ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma kuhakikisha anasimamia kwa karibu matumizi ya fedha ya mradi huo.

“Ujenzi wa mradi huu umefikia asilimia 97 na matumizi ya fedha yanaridhisha ikionesha kwenye kumbukumbu zenu kuwa kuwa hadi sasa asilimia 63 ya malipo yamekishafanyika, hivyo suala la ‘Value for Money’ limeweza kutekelezwa katika mradi huu,” alisema Mhagama.

Pia Mheshimiwa Mhagama alielezea namna alivyofurahishwa na utekelezaji wa mafunzo ya vitendo sehemu za kazi ambayo yamekuwa ni chachu ya kuwawezesha vijana kukuza ujuzi walionao.

“Katika mradi wa ujenzi wa kiwanda hiki nimefurahi kuona vijana ambao wanataaluma ya uhandisi wameweza kushiriki na kutoa mchango wao katika mradi huu wa muhimu kwa taifa ambao umewawezesha kupata ujuzi na wameonyesha namna walivyojitoa katika kujenga nchi yao,” alisema Mhagama

Kwa Upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, RPO Dkt. Miraji Katumbily alieleza kuwa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 97 na hatua iliyobaki sasa ni pamoja na kusimikwa kwa mashine ya uchakataji, kuweka miundombinu ya umeme, vifaa vya TEHAMA na kukamilisha ofisi ili uzalishaji katika kiwanda hicho uanze rasmi.

Naye Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba alimuhakikishia Waziri huyo kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza nchini kuwa watatekeleza maagizo yote yaliyotolewa ili kuhakikisha mradi huo unakamilika bila kuwa na kasoro zozote.

Wakati huo huo, Kijana mmoja wapo anayejitolea kwa mafunzo ya vitendo katika mradi huo Mhandisi Edward Chalamila alimshukuru Waziri kwa Ofisi yake kuweza kutambua umuhimu wa Programu hiyo ambayo imekuwa na manufaa kwa vijana katika kukuza ujuzi wa fani walizozisomea.


Share:

WAKULIMA WA MPUNGA KAHAMA WASHAURIWA KUUNDA AMCOS

 Kaimu Mrajis wa mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace katikati akiwa juu ya mpunga ulio katika ghara la nje nyumbani kwa mkurugenzi wa Nyanhembe Agricultural Farm Bw. Khamis Mgeja, wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kahama KACU, Emmanuel Charahani, na kulia ni  mkulima wa mpunga  Bw.Khamis Mgeja ambaye ni mkurugenzi wa Nyanhembe Agriculture Farm.

 *****
Wakulima wa zao la mpunga Wilayani Kahama,mkoani Shinyanga wameshauriwa kujiunga pamoja na kuanzisha AMCOS zinazonunua mazao ya mpunga kitakachopelekea kuanzishwa kuundwa kwa Chama Cha Ushirika wa Zao la Mpunga ili kuwawezesha kuuza mazao yao kwa bei yenye tija kwani umoja ni nguvu.

Akizungumza juzi na wakulima wa zao hilo Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Shinyanga, Hilda Boniphace mara baada ya kuwatembelea wakulima wa zao la mpunga katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya kilago wilayani Kahama, aliwataka kuanzisha AMCOS itakayoshilikiana na Chama Kikuu cha Ushirika KACU ili ijishughulishe na ununuzi wa zao la mpunga.

“Niseme tu hawa walanguzi wameanza kupita siku nyingi kwa wakulima mashambani na kwamba mbali na zao la mpunga pia tumesikia walanguzi hao wanalangua mazao mbalimbali hivyo serikali haitawavumili, niwaombe tu wakulima msikubali kulanguliwa kiholela na uzuri wa mpunga unatunzika na ndiyo maana uwekewe utaratibu wa mfumo wa stakabadhi gharani,” alisema Mrajis msaidizi.

Aidha Hilda alibainisha kuwa kumekuwa na taarifa za wakulima kunyanyaswa na walanguzi wa zao hilo ambapo wanadaiwa kwenda moja kwa moja mashambani wakiwa na ndoo kubwa za jina maarufu muzambiki lililopanuliwa kwa kuchemshwa kwa mafuta na maji ya moto ili litanuke zaidi badala ya kutumia kipimo cha mizani halali lengo ni kuwapunja wakulima wa mpunga na kupelekea kutonufaika na kilimo chao.

Kabla ya kufanya ziara fupi mashambani ili kuonana na wakulima wa mpunga, Kaimu Mlajis alitoa maagizo na ushauri alipokutana na jopo la wazee la Wilayani Kahama (UWAKA) likiongozwa na Mwenyekiti Nathan Omgani na katibu wa umoja huo Paul Ntelya na baadhi ya wakulima wakiongozwa na Khamis Mgeja katika kikao cha mashauriano kilichofanyika katika kiwanda cha kuchambulia pamba cha Kacu Ukumbi wa Charahani Hall eneo la Mhongolo wilayani Kahama.

Katika kikao hicho cha ndani cha mashauriano kilikuwa pia na wajumbe wa bodi ya chama cha ushirika wilayani Kahama Kacu menejmenti, maafisa Ushirika wa Halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo Mrajisi huyo aliwaeleza wazee na wakulima hao kuwa serikali kwa upande wake ipo pamoja na wakulima inahakikisha wakulima siku zote wananufaika na kilimo chao ndiyo maana inaelekeza mpango wa stakabadhi gharani.

Baada ya kikao cha mashauriano, mrajis huyo pamoja na bodi ya Kacu alishauri wote waongozane kwenda kijijini kuona maendeleo ya mashamba ya mpunga ikiwa ni pamoja na kusikiliza changamoto zainazowakabili wakulima huko huko mashambani.

Akizungumza wakati wakiwa mashambani katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya kilago wilayani Kahama naye Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kacu Emmanuel Charahani aliyeongozana na bodi nzima, alisema kuwa chama chake kimejipanga kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya mpunga na kuandaa kibali kutoka kwa Mrajis na bajeti ya kununua hilo.

Hata hivyo baadhi ya wakulima wa zao hilo akiongea kwa niaba ya wakulima hao Khamis Mgeja ambaye ni mkurugenzi wa Nyanhembe Agriculture Farm akizungumzia suala la mateso wanayokabiliana nayo ni pamoja na wakulima kutonufaika na zao hilo kutokana na wimbi la walanguzi uchwala wanaokuja na ndoo za mozambiki jambo ambalo ni kuwapunja wakulima na ni unyonyaji mkubwa.

Mgeja pia kwa niaba ya wakulima walimpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kusikiliza kilio cha wanyonge wakulima wa zao la mpunga mkoani Shinyanga na kutoa maagizo ya ushauri wasiwakubalie walanguzi kuwanunulia m,ashambani badala yake aliwataka watunze mazao yao ili baadaye wauze kwa bei nzuri.

“Ushauri huo wa Mheshimiwa Rais sisi wakulima wa zao la mpunga tumeupokea kwa mikono miwili na kuanza kuuzingatia kwani Mheshimiwa Rais siku zote anania njema na wakulima wote wa Tanzania kwani yeye siku zote ni mtetezi wa wanyonge,”alisema Khamis Mgeja.

Kutokana na hali hiyo pia Mgeja aliwapongeza bodi ya Kacu na menejiment yake pamoja na Kaimu Mrajis Hilda Boniphace kuondokana na umangimeza wa kukaa maofisini tu kwa kuwatembelea wakulima mashambani na kuona maendeleo na changamoto za wakulima na kuahidi kuendelea kuzingatia maagizo, Ushauri na maelekezo yanayotolewa na serikali kwa wakulima.
 Kaimu Mrajis Hilda Boniphace akizungumza na baadhi ya wakulima alipotembelea kwenye mashamba yao ya mpunga katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya kilago wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
kushoto kaimu Mlajis Hilda Boniphace na mwenyekiti wa KACU Emmanuel Charahani wakipepeta mpunga baada ya kufika nyumbani kwa mkulima Khamis Mgeja katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya Kilago Wilayani Kahama Mkoani shinyanga.
Baadhi ya wakulima wa mpunga katika kijiji cha Nyanhembe kata ya Kilago wialayani Kahama mkoani shinyanga wakiwa katika mashamba yao ya Mpunga huku wakifurahia kutembelewa na kaimu Mlajis Bi. Hilda Boniphace pamoja na uongozi mzima wa bodi ya KACU ukiongozwa na Mwenyekiti wake Emmanuel Charahani.
Share:

KAMPENI SITETEREKI TULONGE AFYA YASHIKA KASI


Mmoja wa wanamuziki nyota nchini kwa jina la kisanii aitwaye Lady Jay Dee akitumbuiza kwenye moja ya tamasha hilo hivi karibuni jijini Dar es salaam.

****
Kampeni ya SITETEREKI Tulonge Afya ambayo ilizinduliwa hivi karibuni ikiwa ni mahususi kwa ajili ya vijana wa Kitanzania imeendelea kushika kasi. SITETEREKI ni jukwaa maalum la mawasiliano ya kubadilisha tabia linalowalenga vijana huku lengo ikiwa ni kuwa kimbilio kwa vijana, kuwa sehemu ambayo vijana wataungana, wakiiamini na kuitegemea, inayowapa hamasa na taarifa zitakazowawezesha kujiboresha, na kuboresha maisha yao. 

SITETEREKI itasaidia kuunganisha na kuboresha shughuli za mawasiliano ya mabadiliko ya tabia kwa vijana nchiniTanzania ili kuwahamasisha kuwa na tabia za kiafya ambazo zitaboresha hali zao na afya zao kwa ujumla.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mkazi wa shirika la USAID Tanzania Andy Karas alisema kuwa SITETEREKI ni mahususi kwa ajili ya vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24. Hata hivyo jukwaa hili litatoa taarifa za kiafya ambazo zitawanufaisha vijana wote na kuhamasisha tabia ambazo zitakuwa zinamlenga kila kijana wa Kitanzania bila kujali umri wake, jinsia au hali yake ya kiuchumi.

Karas aliongeza, ‘SITETEREKI imeundwa kuwapatia vijana taarifa sahihi, kuwapa hamasa na kuwajengea ujuzi unaokidhi mahitaji yao ya sasa. Jukwaa hili litawafikishia vijana taarifa za afya kupitia vyanzo mbalimbali vya mawasiliano, kwa kutumia vyombo vya habari kama vile redio, mbinu mbali mbali za kijamii, mawasiliano ya ana kwa ana, pamoja na mbinu za kidijitali na mitandao ya kijamii, ili kuwahamasisha kuwa na tabia za kiafya na kujijengea maisha chanya.’

Alisema kuwa Jukwaa la SITETEREKI lipo chini ya uangalizi wa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, likiwezeshwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ndani ya mradi wa miaka mitano wa USAID Tulonge Afya (2017 – 2022) unaotekelezwa na FHI360. 

‘SITETEREKI inalenga maeneo yatakayoonesha mafanikio makubwa katika kuboresha maisha, afya na ustawi wa vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya VVU na mimba zisizotarajiwa huchangia kwa kiasi kikubwa vijana kuwa na afya duni, na vifo vya vijana. Hata hivyo, wigo wa jukwaa hili unaweza kutanuka ili kufikia maeneo mengine ya kiafya na makundi mengine ya vijana,’ Karas aliongeza.

Mkurugenzi wa Miradi Tulonge Afya Waziri Nyoni alisema kuwa SITETEREKI inawezesha ufikiwaji wa malengo makuu ya kudhibiti maambukizi ya UKIMWI kwa vijana na katika afya ya uzazi, kwa kuhamasisha tabia kwa vijana wasiooa/olewa wenye kati ya miaka kama matumizi za afya ya uzazi, matumizi ya kondomu kwa usahihi na kila mara, kupima VVU na kuanza matumizi ya ARV mapema kama una maambukizi, kuzingatia matibu kama unaishi na VVU na kufanya tohara kwa hiari kwa wanaume.

Nyoni aliongeza kuwa SITETEREKI imebuniwa kama jukwaa la mawasiliano lenye utayari. Kwa sasa, SITETEREKI inalenga maeneo yatakayoonesha mafanikio makubwa katika kuboresha maisha, afya na ustawi wa vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya VVU na mimba zisizotarajiwa huchangia kwa kiasi kikubwa vijana kuwa na afya duni, na vifo vya vijana.

‘Uhamasishaji wa SITETEREKI utafanyika katika ngazi ya jamii kupitia majadiliano katika vikundi vidogo yatakayoendeshwa na waelimishaji vijana, programu za redio za kijamii zilizoandaliwa kwa kushirikiana na vijana, pamoja na maigizo-jamii yaliyoandaliwa na vijana. 

Hata hivyo, shughuli hizi zitahusisha vijana kwenye majadiliano ya vikundi kuhusu vipaumbele muhimu vya tabia zinazohamasishwa, mabadiliko ya tamaduni, majadiliano juu ya vikwazo na fursa, zikioanishwa kupitia vyombo vya habari ili kusisitiza jumbe muhimu kwa vijana. Yote haya yatawafanya vijana wajione kitu kimoja, na kuwajengea uwezo na ujasiri wa kuwa na tabia chanya za kiafya’ Nyoni alisema.
Share:

Serikali Haitopanga Bei Ya Zao La Pamba Msimu 2020 - Waziri Hasunga

Serikali imesema  haitopanga bei ya zao la pamba ya wakulima katika msimu wa mwaka 2020 unaotarajia kuanza mwezi huu  ili kuwezesha soko kuamua na mkulima kupata soko la uhakika.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Kilimo  Japhet Hasunga  wakati akifungua kikao cha wadau wa zao la  pamba kilichofanyika jijini Mwanza leo (07.06.2020) na kuwashirikisha wakuu wa mikoa 17 inayolima pamba nchini.

Waziri Hasunga amesema kuwa serikali  itakuwa msimamizi mkuu kuhakikisha maslahi ya wakulima wa pamba yanalindwa muda wote.

“Kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi ya biashara ya zao la pamba kufanyika kama ilivyo kwa mazao mengine.Hivyo leo hapa hatutapanga bei badala yake tunaachia soko liamue” alisema Waziri Hasunga

Hasunga aliongeza kusema dhamira ya serikali ya awamu Tano ni kufanya Kilimo kuwa cha kibiashara na si cha kujikimu kwa wakulima kuondolewa vikwazo zaidi.

Aidha,amesema ni lengo la serikali kuhakikisha pamba yote ya wakulima inaongezwa thamani hapa nchini kwa kutumia viwanda vya ndani na kuwataka wafanyabiashara wengi kujitokeza kununua pamba yote ya wakulima.

Akihitimisha hotuba yake Waziri Hasunga alisisitiza kuwa serikali itahakikisha pamba ya wakulima inapata soko la uhakika kwa kuzingatia ushindani ili wakulima wapate faida.

" Nitashangaa kuona mzalendo wa Tanzania akinunua pamba kwa bei ndogo na kuwanyonya wakulima" alisema Hasunga

Kuhusu kiwango cha uzalishaji kushuka Hasunga alisema kumetokana na uwepo wa mvua nyingi msimu huu na pia upungufu wa madawa na viuatilifu kwa baadhi ya wakulima.

" Tathmini ya awali imeonesha msimu huu uzalishaji pamba utashuka hadi tani 150,000 toka tani 348,000 msimu wa 2019 kutokana na mvua kuwa nyingi na kuathiri uzalishaji nchini" alisema Hasunga

Hasunga aliwafahamisha wadau kuwa katika msimu uliopita  wakulima nchini walipata zaidi ya shilingi bilioni 419 zilizotokana na mauzo ya pamba takribani tani 348,000 iliyozalishwa nchini mwaka 2019.

Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Kilimo alitangaza rasmi kuanza kwa msimu wa ununuzi wa pamba kuwa tarehe 15 Juni 2020  na kusema Bodi ya pamba ikamilishe taratibu zote za kuanza msimu ili wakulima wauze na kupata fedha zao kwa wakati.

Kwa upande wake Naibu Waziri Kilimo Hussein Bashe alisema ili kuhakikisha wakulima wanapata fedha zao kwa uhakika tayari akaunti 128,000 za benki zimefunguliwa na wakulima kwa ajili ya kutumika kulipa fedha zao.

Bashe amezipongeza taasisi za fedha kwa kufungua akaunti hizo za wakulima bure na kuwataka waendelee kufungua nyingi zaidi ili asiwepo hata mkulima mmoja asiye na akaunti.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ameipongeza serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano uliowezesha pamba ya wakulima msimu wa 2019 kupata mafanikio na wakulima kuweza kuuza pamba yote.

Naye mwakilishi wa wanunuzi wa zao la pamba Christopher Gachuma alisema wamejipanga tayari kuanza ununuzi wa pamba yote ya wakulima kwa kuzingatia bei ya soko.

Gachuma ameshukuru serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania kwa kuwahakikishia wanunuzi kuwa fedha zipo kwa ajili ya taasisi za fedha kukopa ili kununua pamba ya wakulima nchini.

Mwisho.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Kilimo
MWANZA
07.06.202



Share:

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Uchaguzi Wa Viongozi Chama Cha Wafugaji Tanzania ( CCWT)




Share:

Taarifa Kwa Umma Toka Kurugenzi Ya Mawasiliano Ya Rais IKULU

Rais Dkt.Magufuli amewashukuru Viongozi wa Dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba mwenyezi Mungu aepushe Corona.

Ametoa shukrani hizo katika Misa takatifu kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imaculata Chamwino Dodoma

Akiwa Kanisani hapo, Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia upanuzi wa Kanisa hilo na kufanikiwa kuchangisha zaidi ya Tsh. Mil 17 ikiwemo Tsh. Mil 10 aliyochangia yeye mwenyewe na mifuko 76 ya saruji, ametaka upanuzi wa kanisa uanze kesho.


Share:

Kaliua Yatoa Mikopo Ya Milioni 332 Kwa Vikundi

NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imetoa mikopo ya shilingi milioni 332 kwa vikundi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.

Mikopo hiyo imekabidhiwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mikopo hiyo , Mkurugenzi Mtendaji Dkt. John Pima alisema kati ya fedha shilingi milioni 215 kwa vikundi 38.

Alisema wametoa pikipiki 10 zenye thamani ya milioni 25 kwa Kikundi cha Umoja wa Bodaboda Stendi na kukabidhi vifaa vya viwanda kwa vikundi 7 vyenye thamani ya milioni 92.

Dkt. Pima alisema tangu wa fedha ulipoanza hadi hivi sasa wametoa mikipo ya jumla ya shilingi milioni 584 kwa vikundi 99 ambapo vikundi 44 vya wanawake wamepokea milioni 251, vijana vikundi 36 vimepokea milioni 281 na walemavu vikundi 16 vimepokea milioni 51.5.

Kwa upande wa Waziri Jaffo amezitaka Halmashauri nyingine mfano wa Kaliua katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya vijana , walemavu na Wanawake.

Alisema Kaliua imeweza kutoa mikopo ambayo itayasaidia makundi hayo kujipatia kipato na kujiletea maendeleo yao na Taifa.

MWISHO


Share:

Waziri Biteko ataka mchango sekta ya madini kutazamwa vinginevyo

Na Nuru Mwasampeta, WM
WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amewataka Watanzania kuutazama mchango wa sekta ya madini kwa namna unavyosaidia kuinua sekta nyingine za uchumi, kwani tayari kwa upande wa kuongezeka kwa ukusanyaji wa maduhuli sekta hiyo imeonesha mafanikio makubwa.

“Niliwaambia wenzangu wizarani, lazima tuhame sasa kwenye mfumo wa kufurahia kuona mapato yameongezeka kutokana na ukusanyaji wa maduhuli twende kwenye mfumo wa kujiuliza je? Sekta ya madini imechangiaje ukuaji wa sekta nyingine?.

"Anayelima mchele awe na uhakika wa wanunuzi kwa sababu wachimbaji wapo, anayefuga ng’ombe awe na uhakika wa soko kwa sababu wanunuzi wapo, anayelima nyanya na shughuli nyingine hivyo hivyo, na huo ndio tunaita ufungamanishaji wa uchumi wa madini na sekta nyingine;

Waziri Biteko aliyabainisha hayo hivi karibuni mkoani Geita alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayofanywa kwa fedha za huduma za jamii (CSR) zinazotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) ambapo alikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya unaoendelea katika soko kuu la dhahabu Geita pamoja na soko la Katundu litakalohusisha biashara za kawaida lililojengwa katika Halmashauri ya Mji wa Geita.

Pamoja na kukagua miradi ya maendeleo inayowezeshwa na GGML, Waziri Biteko alizungumza na wafanyabiashara wa madini mkoani humo na kueleza kuwa kutokana na changamoto ya Covid-19, wizara imetoa kipindi cha miezi mitatu kwa wafanyabiashara wa madini kununua madini mahali popote nchini na kuwataka kuzingatia uwepo wa vibali vyote muhimu vinavyoonesha mahali madini hayo yamenunuliwa na yanakopelekwa mara baada ya kuyanunua.

Akitoa taarifa ya sekta,  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema mwenendo wa biashara ya madini ya dhahabu katika mkoa wake tangu soko la dhahbu kufunguliwa mwezi Machi 2019 hadi Mei 2020 kipindi cha miezi 14 jumla ya kilo 5,320.99 zenye thamani shilingi Bilioni 522.44 zimeuzwa na kuchangia mapato ya serikali kupitia  mrabaha na ada ya ukaguzi kwa jumla ya shilingi bilioni 36.57.

Amesema, ongezeko hilo linaonesha namna sekta ya madini ilivyokuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na usimamizi makini na uongozi bora wa wizara, lakini pia utii na utekelezaji wa ushauri na maelekezo yanayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliongeza kuwa, fedha inayopatikana kutokana na makusanyo kwenye sekta ya madini ndiyo inayokwenda kulipa elimu bure, kujenga vituo vya afya, inatumika katika kujenga hospitali za wilaya na mambo mengine mengi yanayotekelezwa na serikali yetu.

Amebainisha kuwa, mkoani Geita kuna ongezeko kubwa la viwanda vya kuchenjua dhahabu  (Illusion Plant) kutoka viwanda 20 vilivyokuwepo awali na kufikia viwanda 39 na kubainisha kuwa hayo ni mageuzi makubwa katika sekta ya madini kwa kuwezesha uwepo wa viwanda vidogovidogo mkoani humo.

Ameendelea kusema, kwa mwaka 2018  halmashauri zilizoko katika Mkoa wa Geita zilinufaika kutokana na utekelezaji wa takwa la kisheria la utekelezaji wa mpango wa kuchangia huduma za kijamii ambapo Mgodi wa Geita (GGML) uliotoa kiasi cha shilingi bilioni 9.2 kama mchango wa mgodi kwenye masuala ya kijamii na kupelekea maendeleo ya mkoa huo kwenda kwa kasi.

 Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Mjiolojia Daniel Mapunda amesema, Mkoa wa Geita una leseni kubwa za utafiti wa madini 283, leseni za uchimbaji mkubwa wa madini 2, leseni 17 za uchimbaji wa kati, leseni 1487 za uchimbaji mdogo wa madini na leseni 384 za uchenjuaji wa madini (illusion plant na vat-reaching plant).

Kwa upande wa leseni za biashara ya madini, Mapunda amesema kuna jumla ya leseni kubwa za biashara ya madini 33 kwenye soko kuu la dhahabu Geita na leseni ndogo za biashara ya madini 69 zilizopo katika vituo vidogovidogo vya ununuzi wa madini zilizotolewa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.

Akizungumzia mwenendo wa ukusanyaji wa maduhuli ya serikali, Mapunda ameeleza kuwa lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 lilikuwa ni kukusanya shilingi bilioni 156.34 ambapo kufikia Juni 2, 2020 kiasi cha shilingi bilioni 191.52 sawa na asilimia 122.5 ya lengo la makusanyo kimekusanywa.

Amesema, makusanyo hayo ni ongezeko la kiasi cha shilingi bilioni 62.54 ukilinganisha na kiasi kilichokusanywa kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Amebainisha kuwa, kati ya hizo jumla ya shilingi bilioni 34.2 zimetokana na shughuli za uchimbaji mdogo wa madini sawa na ongezeko la asilimia 310 ya mapato yaliyopatikana kutokana na uchimbaji mdogo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo kiasi kilichokusanywa ni shilingi bilioni 11 pekee.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Makamu wa Rais anayeshughulikia Miradi Endelevu (GGML), Simon Shayo, amesema, kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 9 kilitolewa kwa mwaka 2018 ili kuzinufaisha jamii zinazozunguka mgodi huo na kuongeza kuwa mgodi unafurahi kuona wananchi wa kawaida wakiboresha maisha yao kutokana na mgodi kuwepo katika jamii yao.

Katika ziara hiyo, Waziri wa Madini alikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya litakalohusisha wafanyabiashara wengine wa dhahabu katika soko la dhahabu Geita, ujenzi wa soko la Katundu, kukagua kituo cha uwekezaji Bombambili, pia alikagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata madini kinachojengwa na mwekezaji binafsi mkoani humo.

MWISHO


Share:

Waziri Simbachawene Asema Mitambo Mipya Nida Kuanza Kufanya Kazi Hivi Karibuni

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema mitambo mipya ya uzalishaji wa vitambulisho vya taifa itaanza kufanya kazi hivi karibuni baada ya wataalamu kuwasili nchini.

Mitambo hiyo ya kisasa ambayo inauwezo wa kuzalisha vitambulisho 144,000 kwa siku, ilishafungwa muda mrefu ofisini za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), na ilipaswa iwe imenza kufanya kazi tangu mwezi Aprili, mwaka huu lakini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ilichelewa kuanza kufanya kazi kutokana na watalaamu wa mitambo hiyo kutoka Ujerumani kushindwa kuja nchini.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya na Ipela, jimboni kwake Kibakwe, Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, leo, baada ya kupokelewa kwa shangwe kwa kumpongeza kwa kuchaguliwa kuiongoza Wizara hiyo, Simbachawene amesema Watanzania waondoe shaka kwani kupatikana kwa mitambo hiyo ambayo sasa itafanya kazi muda wowote kuanzia sasa baada ya wataalamu kutoka nchini Ujerumani kuwasha mitambo hiyo.

“Naomba nitumie mkutano huu hapa Kijijini kuwatangazia Watanzania wote sasa tatizo la kukosa vitambulisho limeisha, hakuna atakayekosa kitambulisho, kila Mtanzania mwenye sifa atapewa, tulichelewa kuwasha mitambo kwasababu ya ugonjwa wa corona uliofanya wataalam washindwe kuja nchini,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, “mitambo hiyo ni ya kisasa, na inauwezo wa kuzalisha vitambulisho 144,000 kwa siku, hivyo kwa idadi hiyo ndani ya miezi michache wale wote waliosajiliwa watapewa vitambulisho vyao.”

Aidha, Waziri Simbachawene alisema kutonakana na utendaji kazi wa Rais Dkt. John Magufuli, upinzani umekufa wenyewe hivyo uchaguzi ujao chama tawala kimejingea uwezo mkubwa wa ushindi wa kishindo.

“Rais wetu na Serikali ya Chama chetu Cha Mapinduzi kimefanya kazi iliyotukuka, na upinzani unakufa wenyewe, sasa hivi hakuna upinzani, mnasikia wanavyokatika wanarudi CCM kwasababu ya kishindo cha kazi kilichofanywa na Serikali ya Awamo ya Tano,” alisema Simbachawene.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejenga na inaendelea kujenga miradi mikubwa ambayo inaifanya Tanzania kuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi ndani na nje ya nchi.

“Tumenza ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati ya nchi ambayo itakua michipa mikubwa ya kiuchumi, ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma, na itakamilika, na pia amenunua ndege leo hii tunajivunia, na mradi wa umeme mkubwa ambao utawezesha kutumia umeme ndani na kuuza nje ya nchi,” alisema Simbachawene.

Pia alisema kwa upande wa ujenzi wa vituo vya afya, rais Magufuli amejenga vituo zaidi ya 450 nchini, hivyo kutokana na vituo hivyo watanzania watapata matibabu katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kikao hicho, Emmanuel Kagali, alimpongeza Waziri huyo kwa utendaji wake wa kazi ndani ya Jimbo la Kibakwe, kutokana na uwepo wa umeme katika vijiji vyote, ujenzi wa zanahani na barabara.

Pia alimuomba waziri huyo kuwasaidia kupata vitambulisho vya taifa, kwani idadi kubwa ya wananchi wa Kata ya Malolo hawajapata vitambulisho.

“Mheshimiwa Waziri nimefurahi sana kupata nafasi hii ya kukupongeza na pia kukupa moyo uendele kufanya kazi, na pia tumefurahi sana kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi, hivyo hatutakuangusha, nawe ni tegemeo letu katika maendelo ya jimbo letu,” alisema Kagali.

Naye Mkazi wa Kata ya Ipela jimboni humo, Jeremia Kibwingu alimuomba Waziri huyo kufikisha maombi ya wananchi wa Kibakwe, ya kuongezewa muda wa kuiongoza nchi Rais Magufuli kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuanzisha miradi mikubwa nchini.

“Naomba utufikishie ujumbe huu kwa Rais Magufuli, tutaka aongoze mpaka mwisho wa maisha yake, Rais huyu si wakawaida, Watanzania naomba muelewe, huyu anapaswa aiongoze nchi hii milele,” alisema Kibwingu.

Waziri Simbachawene anaendelea na ziara yake jimboni humo kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa chama pamoja na kukagua miradi ya maendeleo jimboni humo.


Share:

Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADO 'MALIGANYA' - GUMBA



Msanii wa Nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' anakualika kutazama video yake mpya inaitwa Gumba...
Itazame hapa chini


Share:

Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADO 'MALIGANYAA' - MASHABIKI



Ninayo hapa ngoma nyingine mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado ' Maliganya kutoka Kahama mkoani Shinyanga inaitwa Salamu kwa mashabiki zangu...
Itazame hapa chini

Share:

Chama cha Wananchi - CUF Chatoa Tamko Kuhusu Mchakato wa Kura za Maoni za Uteuzi wa Watakaogombea Kupitia Chama Hicho

Chama cha Wananchi - CUF kimesema ratiba yao ya kura za maoni na uteuzi wa  nafasi za  udiwani, uwakilishi, ubunge na urais imeanza tangu mwezi Mei ambapo  inatarajiwa kuhitimishwa tarehe Julai 27, ambapo agombea wa urais  kwa tiketi ya chama hicho Bara na Zanzibar watataeuliwa.

Hayo yamesemwa jana tarehe 6 Juni 2020, na Juma Killghai, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, alipokuwa akitoa ratiba ya kuwapigia kura za maoni na uteuzi watia nia wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu 2020. 

Alisema chama hicho kimejidhatiti kusimamisha wagombea wa nafasi zote nchi nzima na kuwataka wanachama wote wenye sifa kujitokeza kugombea.

“Tunatarajia kuweka wagombea nchi nzima katika ngazi za udiwani, uwakilishi na ubunge.

“Aidha, tunatarajia kusimamisha wagombea Urais wawili, mmoja akisimama kwa ajili ya Urais wa Zanzibar na mwingine akisimama kwa ajili ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.


Aidha Killghai alisema chama hicho kitashirikiana na chama chochote chenye dhamira ya dhati ya kuiondoa CCM madarakani.

“Chama chetu kipo tayari kushirikiana na chama chochote chenye dhamira ya kweli ya kuiondoa CCM na kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi, isiwe kinaingia madarakani kinafanya yaleyale yaliyokuwa yakifanya na CCM,” alisema

Alisema, mchakato wa kugawana majimbo ama kata utafanyika kwa utaratibu watakaokubaliana baina yao na chama ambacho kitaafikiana nacho.


Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ILI TUWE TUNAKUMIA HABARI ZOTE KWENYE SIMU YAKO BURE

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.


Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.



⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50


⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4


⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.



Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama



Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

HASHIM RUNGWE ATANGAZA CHAUMMA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2020


Chama cha Upinzani cha CHAUMMA,  kimetangaza rasmi kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


Mwenyekiti wake, Hashim Rungwe Spunda amesema wanavikaribisha vyama vingine kuungana nao  wakati ambao CHAUMMA inaelekekea kuchukua dola.

Rungwe amesema, hivi karibuni Chaumma itatoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu za wanachama wake watakaohitaji kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

Wakati huo huo, Rungwe amesema Chaumma imekamilisha kuandaa ilani yake ya uchaguzi na kwamba kiko katika mchakato wa kuiwasilisha katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Aidha, Rungwe ameomba wananchi wenye mapenzi mema na chama hicho, kuchangia fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kampeni.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger