Friday, 3 April 2020
Thursday, 2 April 2020
Picha : MWILI WA MTANGAZAJI WA TBC MARIN HASSAN MARIN WAZIKWA ZANZIBAR
WANANCHI wakibeba Jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Marin Hassan Marin, wakitoka nyumbani kwa marehemu na kuelekea katika Msikiti wa Kibweni KMKM kwa ajili ya kuombea dua kwa ajili ya maziko yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar leo Aprili 2,2020.(Picha na Othman Maulid )
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakiuombea dua mwili wa Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) baada ya kumalizika Sala ya Maiti iliofanyika katika Msikiti wa KMKM Kibweni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Habaro Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Mahmoud Thabot Kombo akizungumza na kutowa shukrani kwa niaba ya Wizara yake wakati wa hafla ya maziko ya Mwandishi wa Habari Muandamizi Tanzania Marehemu Marin Hassan Marin, yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar.(Picha na Othman Maulid)
MAWAZIRI wa Habari wa SMT na SMZ. Kushoto Waziri Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, wakiwasili katika viwanja vya Msikiti wa Kibweni KMKM kuhudhuria maziko ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Marin Hassan Marin, yaliofanyika leo 2/4/2020 na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.(Picha na Othman Maulid)
WANAICHI na Waumini wa Kiislam wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Marin Hassan Marin Mwandishi wa Habari Muandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) yaliofanytika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 2/4/2020.(Picha na Othman Maulid)
MFANYAKAZI WA MAHAKAMA MBARONI KWA TUHUMA YA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 10 MAHAKAMANI SHINYANGA
Na Salvatory Ntandu - Shinyanga
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Joseph Masanja (58) mlinzi wa Mahakama ya Hakimu mkazi Wilaya ya Shinyanga kwa tuhuma ya kumbaka Mwanafunzi mwenye umri wa Miaka 10 wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi.
Tukio hilo lilitokea tarehe 21 Machi mwaka huu ambapo inaelezwa kuwa mtuhumiwa alimdanganya binti huyo aliyekuwa na mwanzake mwenye umri wa miaka saba kwenda katika eneo lake la kazi kwa madai ya kuwapatia fedha za kununua ndala.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo Alhamis Aprili 2,2020 Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema mtuhumiwa alikamatwa baada ya binti hiyo kutoka katika eneo la kazi majira ya saa kumi na moja jioni.
“Ilikuwa saa nane mchana siku ya Jumamosi,mabinti hao walifika mahakamani, Joseph aliagiza binti wa miaka saba kubakia getini na kisha yeye kuingia ndani binti huyu na kumbaka katika moja ya chumba cha ofisi katika eneo la Mahakama”,alisema Magiligimba.
Magiligimba alifafanua kuwa baada ya Joseph kutekeleza tukio hilo alimwamuru binti huyo kuondoka eneo la tukio kwa kupitia geti jingine ambapo mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi aliyefahamika kwa jina moja la Leticia alipomkamata binti huyo na alimhoji kuwa ametokea wapi ndipo alipokiri alikuwa akifanya mapenzi na mlinzi huyo.
“Pia kuna Afisa wa polisi alimwona binti wa miaka saba aliyekaa getini muda mrefu,alipomhoji kwanini amekaa kwa muda mrefu katika eneo hilo alijibiwa kuwa anamsubiri mwenzake tangu majira ya saa 8 mchana alipoingia ndani na Mlinzi huyo hajatoka”,aliongeza Magiligimba.
"Askari huyo alimchukua binti huyo na kuingia naye ndani ya eneo la mahakama na kukutana na mwalimu aliyemkamata binti wa miaka 10 wakati akipitishwa geti la pili na Joseph,ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa wazazi wa mabinti hao",alieleza Magiligimba.
Aidha alisema kuwa baada ya mabinti hao kufikishwa polisi wazazi wao walifika na kupewa kibali cha kwenda hospitali kwa ajili ya vipimo na vipimo vilibaini kuwa binti wa miaka 10 ameingiliwa (amebakwa)
Hata hivyo Magiligimba alisema,baada ya Joseph kutekeleza tukio ,alikimbia kusikojulikana hadi alipokuja kukamatwa na jeshi la polisi na Alipohojiwa alikiri kumbaka mwanafunzi huyo,na upepelezi wa tukio utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Wimbo Mpya : MAN NKELEBE - AGNESS
Msanii Man Nkelebe anakualika kusikiliza wimbo wake mpya uniatwa Agness ..Usikilize hapa chini
Wizara ya afya yatoa ufafanuzi maswali ya Wananchi kuhusu Virusi Vya Corona
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema amekuwa akipokea maoni, maswali na ushauri kutoka kwa wananchi wakitaka kujua jitihada mbalimbali za Serikali za kukabiliana na homa kali ya mapafu na amewaagiza wataalamu wake kuanza kujibu maswali.
Waziri Ummy amesema maswali, maoni na ushauri huo unatoka kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na kituo cha wizara cha kupokea simu kuhusu ugonjwa wa homa ya Corona.
“Moja ya swali linaloulizwa kutoka kwa wananchi ni suala la kupima ugonjwa wa Corona (covid-19), hivyo katika kutoa ufafanuzi ni vema Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dkt. Nyambura Muremi, aeleze Watanzania nani anakidhi vigezo vya kupima ugonjwa wa Covid-19 na taratibu za kupima ugonjwa huu zikoje,” amesema Ummy Mwalimu.
Katika hatua nyingine, Waziri Ummy Mwalimu amesisitiza wananchi kwamba wanapaswa kukaa umbali wa mita mbili kati ya mtu mmoja na mtu mwingine ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Akizungumzia kuhusu maswali ya wananchi, Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dkt. Nyambura Muremi amesema kuwa anayepaswa kupimwa ugonjwa wa corona ni yule alitimiza vigezo kama vile mtu kuwa na dalili ya ugonjwa wa covid-19.
“Kama mtu amepata kirusi, ataanza kuonyesha dalili kama vile kupata homa, hapa ndio tutanza kuchukua kipimo na huu ndio uthibitisho wa kisayansi,” amesema Dkt. Muremi.
Akizungumzia taratibu za kupima ugonjwa wa corona, Dkt. Muremi amesema katika ngazi ya mkoa wapo wataalamu wanashughulika kupima sampuli na kwamba wao ndio wamekuwa wakiratibu shughuli zote za kimaabara kila mkoa.
“Baada ya kupima huko mikoani wanaleta Maabara Taifa ya Afya ya Jamii ambayo ina vigezo vitatu vinavyotambulika kimataifa,” amefafanua Dkt. Muremi.
Dkt. Muremi ametaja vigezo vya Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii ni kwamba ina usalama wa kibailojia ngazi ya tatu (BSL-3), wataalamu waliothibitishwa kupima magonjwa hatarishi na mashine stahiki ambayo imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Kutokana na maswali mengi ya Wananchi kuanzia sasa Wizara ya Afya itaendelea kujibu maswali yao.
KAMPUNI YA TIGO WAUNGA JUHUDI KUPAMBANA NA CORONA WATOA WITO KWA JAMII
Kampuni ya Tigo Waunga juhudi kupambana na Corona watoa wito kwa jamii, tazama video hapo chini
Picha : DC MBONEKO AONGOZA KAMPENI YA KUHAMASISHA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI WANAODAIWA SHINYANGA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ameongoza Kampeni ya Kuhamasisha Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wamiliki wa viwanja vya biashara na makazi katika manispaa ya Shinyanga inayoendeshwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kutoa elimu ya ulipaji kodi na kufuatilia wadaiwa wenye madeni makubwa na malimbikizo ya muda mrefu.
Kampeni hiyo imefanyika leo Alhamis Aprili 2,2020 ambapo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami,Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Shinyanga,Hezekiel Kitilya na Maafisa wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Shinyanga amekutana na wafanyabiashara na wananchi wanaodaiwa Kodi ya Pango la Ardhi.
Miongoni mwa wafanyabiashara waliotembelewa leo ni Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah kinachomilikiwa na Wawekezaji kutoka China kinachodaiwa shilingi Milioni 66,Kampuni ya Gaki Investment Ltd (Milioni 120), Phantom Oil Tanzania Ltd (Milioni 105) na Mwananchi Garage (Milioni 9.3).
Akizungumza, Mboneko alisema ni wajibu wa kila mmiliki wa ardhi kuhakikisha analipia kodi ya pango la ardhi hata kama hana hati ya ardhi akibainisha kuwa kutolipa kodi ya pango la ardhi ni kuiibia serikali hivyo kuchangia kudhorotesha maendeleo ya nchi.
“Msiidanganye serikali kwa sababu serikali ina macho makubwa, ina macho marefu itawafuata popote mlipo ili mlipe kodi.Ni lazima deni lilipwe.Tutahakikisha tunawafuatilia wale wote wanaodaiwa kwani kodi zinazokusanywa ndiyo zinatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini”,alisema Mboneko.
“Niwashukuru na kuwapongeza wafanyabiashara na wananchi tuliowafikia leo mmeonesha kutambua umuhimu wa kulipa kodi ya pango la ardhi na mmesema mpo tayari kulipa madeni yenu.Hakikisheni mnalipa madeni yenu kabla ya mwaka wa fedha haujaisha Juni,2020.Tutaendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili kuhakikisha kila mmoja analipa kodi ya ardhi anayodaiwa”,aliongeza Mboneko.
Kwa upande wao wafanyabiashara na wananchi wanaodaiwa kodi ya pango la ardhi wameishukuru serikali kuwatembelea na kuwakumbusha wajibu wao kulipa kodi huku wakibainisha kuwa wapo tayari kulipa madeni yao.
“Mimi sikujua kuwa ukiwa na kiwanja tu bila hati ya ardhi unatakiwa ulipie kodi ya pango la ardhi.Nilijua nikipata hati ndiyo naanza kulipia.Nimejipanga kuanza kulipa deni ninalodaiwa ambapo hadi mwisho mwezi huu wa Aprili nitakuwa nimemaliza kulipa deni”,alisema Polycarp Kimario ambaye ni Mkurugenzi wa Mwananchi Garage.
Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda cha Fang’ Wah, Alice Mingyang Yan alisema wapo tayari kulipa deni lao wanalodaiwa kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2020 muda ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao badala ya kudaiwa kuanzia mwaka 2013 kipindi ambacho kulikuwa na wawekezaji wengine waliouza kiwanja.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo alisema anatambua umuhimu wa kulipa kodi na tayari alishaanza kulipa deni analodaiwa akibainisha kuwa awali alikuwa anadaiwa shilingi Milioni 30 lakini deni lake limekuwa likiongezeka kutokana na mgogoro wa ardhi uliokuwepo katika kiwanja chake kilichopo eneo la Matanda.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami alisema lengo la Kampeni ya Kuhamasisha Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wamiliki wa viwanja vya Biashara na makazi inayoendeshwa katika mikoa mbalimbali ni kutoa elimu ya ulipaji kodi ya pango la ardhi na kufuatilia wadaiwa wenye madeni makubwa na malimbikizo ya muda mrefu.
“Kampeni hii pia inalenga kutatua changamoto zinazowakabili walipa kodi na kuchukua hatua za kisheria kwa kusambaza hati za madai ili kuwafikisha mahakamani watakaokaidi tutawakamata mali na kuuza ili kufidia deni husika”,alisema Masami.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akitoa elimu ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Phantom Oil Tanzania Ltd John Maguru (kushoto) inayodaiwa shilingi milioni 105 za pango la ardhi tangu mwaka 2007 leo Alhamis Aprili 2,2020 wakati akiongoza Kampeni ya Kuhamasisha Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wamiliki wa viwanja vya Biashara na makazi katika manispaa ya Shinyanga. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Mji Manispaa ya Shinyanga,Salu Ndongo akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Phantom Oil Tanzania Ltd John Maguru akimuahidi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kuwa Kampuni yao ipo tayari kuanza kulipa kodi ya pango la ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiendelea kutoa elimu ya ulipaji wa kodi ya pango la ardhi. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Shinyanga,Hezekiel Kitilya.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami (katikati) akielezea hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa wafanyabiashara na wananchi wasiolipa kodi ya pango la ardhi kuwa ni pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa kusambaza hati za madai ili kuwafikisha mahakamani watakaokaidi tutawakamata mali na kuuza ili kufidia deni husika.
Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Mji Manispaa ya Shinyanga,Salu Ndongo (wa pili kushoto) akitoa elimu ya ulipaji kodi ya pango la ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipokelewa na Meneja wa Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah, Alice Mingyang Yan (kulia) alipotembelea kiwanda kicho kwa ajili ya kuhamasisha Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wamiliki kiwanda hicho kilichopo Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikagua nyaraka mbalimbali katika Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah na kubaini kuwa Kiwanda hicho kinadaiwa shilingi milioni 66 za pango la ardhi tangu mwaka 2013 na kuwataka walipe deni hilo.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah wakijitetea mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kuwa wao walinunua kiwanda hicho mwaka 2018 kutoka kwa Mwekezaji Mwingine hivyo wapo tayari kuanza kulipa deni la kuanzia mwaka 2018 hadi 2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiwataka wamiliki wa kiwanda cha Fang’ Wah kulipa kodi ya pango la ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na waandishi wa habari katika Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah na kuhamasisha ulipaji wa kodi ya pango la ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na waandishi wa habari katika Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah na kuhamasisha ulipaji wa kodi ya pango la ardhi.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami akizungumza na waandishi wa habari katika Kiwanda cha Machinjio ya Punda cha Fang’ Wah na kuhamasisha ulipaji wa kodi ya pango la ardhi.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami akitoa elimu ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo (wa pili kulia) ambaye pia anadaiwa deni la shilingi milioni 120 kwa ajili ya pango la ardhi katika kiwanja chake kilichopo katika eneo la Matanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimhamasisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo kumalizia kulipa kodi ya pango la ardhi anayodaiwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo akielezea hatua alizochukua baada ya mgogoro wa ardhi kuisha katika viwanja vyake katika eneo la Matanda ambapo kwa kutambua umuhimu wa kulipa kodi tayari alishaanza kulipa deni analodaiwa.
Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Shinyanga,Hezekiel Kitilya akimueleza jambo Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gasper Kileo akimweleza jambo Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Shinyanga,Hezekiel Kitilya.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akitoa elimu ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa Mkurugenzi wa Mwananchi Garage Polycarp Kimario (kulia) ambaye anadaiwa kodi ya shilingi milioni 9.3 katika kiwanja chake ambacho anakitumia kufuga samaki.
Kulia ni Mkurugenzi wa Mwananchi Garage Polycarp Kimario akimuahidi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kuwa atalipa kodi ya pango la ardhi mwezi huu Aprili 2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwahamasisha wamiliki wa ardhi kuhakikisha wanalipa kodi ya pango la ardhi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 110...Wawili Zaidi Wafariki Dunia
Idadi ya visa vya ugonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imefikia 110 baada ya visa vingine 29 kuthibitishwa.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari jijini Nairobi waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba watu wengine wawili wamepoteza maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi hivyo.
Amesema kwamba idadi hiyo inaongeza idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia 3. Kagwe ameongezea kwamba wagonjwa waliofariki wanatoka miji ya Nairobi na Mombasa.
Waziri huyo pia amepiga marufuku usafiri wa Wakenya kuelekea katika maeneo ya mashambani akionya kwamba huenda wakapeleka maambukizi ya virusi hivyo katika maeneo hayo.
Amesema kwamba serikali imewapima watu 662 katika kipindi cha saa 24 ambapo takriban watu 29 wamepatikana na virusi hivyo.
Kagwe amesema kwamba wagonjwa 28 kati ya wale waliopatikana na virusi hivyo ni raia wa Kenya huku mmoja akiwa raia wa DR Congo.
Waziri huyo pia amepiga marufuku usafiri wa Wakenya kuelekea katika maeneo ya mashambani akionya kwamba huenda wakapeleka maambukizi ya virusi hivyo katika maeneo hayo.
Amesema kwamba serikali imewapima watu 662 katika kipindi cha saa 24 ambapo takriban watu 29 wamepatikana na virusi hivyo.
Kagwe amesema kwamba wagonjwa 28 kati ya wale waliopatikana na virusi hivyo ni raia wa Kenya huku mmoja akiwa raia wa DR Congo.
Mkuu Wa Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji Afanya Mabadiliko Ya Makamnda
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) John W. Masunga, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa.
Makamanda walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto na Uokoaji (SACF) ABDALLAH MAUNDU anakwenda kuwa (RFO) Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, kabla ya nafasi hii
alikuwa Makao Makuu Dodoma.
Aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) SALUM M. OMARI, anayekwenda kuwa (RFO) Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, kuchukua nafasi ya Mrakibu Msaidizi wa
Zimamoto na Uokoaji (ASF) JENIFER V. SHIRIMA anayehamia Makao Makuu kuwa Mkuu wa dawati la Mambo ya Nje.
Aidha nafasi ya (RFO) Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ASF) AUGUSTINE B. MAGERE.
Pia aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) ELIA P. KAKWEMBE, anayekwenda kuwa (CFO) Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi (ACF) BAKARI K. MRISHO anayekwenda kuwa (RFO) Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Temeke.
Aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Mrakibu wa Zimamoto na Uokoaji (SF) OMARI H. SIMBA anayekwenda kuwa (RFO) Kamanda wa Mkoa wa Simiyu na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu wa
Zimamoto na Uokoaji (SF) GEORGE G. MRUTU anayetoka Makao Makuu.
Mabadiliko haya ni ya kawaida kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
RC Tabora Awaagiza Kusakwa Na Kukamatwa Kwa Walimu Wanaofundisha Tuisheni Kipindi Hiki Cha Mapambano Dhidi Ya Corona
Na Daudi Tiganya
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameagiza kuwasakwa kwa walimu ambao wamekuwa wakiwakusanya wanafunzi kwa ajili ya kufundisha tuisheni kwa kuwa wanapingana na kampeni ya kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa Covid -19.
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameagiza kuwasakwa kwa walimu ambao wamekuwa wakiwakusanya wanafunzi kwa ajili ya kufundisha tuisheni kwa kuwa wanapingana na kampeni ya kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa Covid -19.
Hatua hiyo inalenga kuzuia vitendo hatarishi vinavyoweza kuwepo na mazingira kupata virusi vya Corona.
Mwanri alitoa kauli hiyo wilayani Nzega wakati ziara yake ya kukagua Vituo na Zahanati zilizoandaliwa kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa wa covid -19 kama itatokea bahati wakaonekana wakaonekana Mkoani humo.
Alisema ni marufuku kwa walimu kutumia janga la ugonjwa wa Covid -19 kujipatia maslahi kwa kufanya hivyo ni kuvunja Sheria kwa kisingizio kuwa wanawafundisha watoto masomo ya ziada.
Mwanri aliongeza kuwa baadhi ya Wamiliki wa Shule binafsi ndio wanasababisha walimu kujiingiza kwenye ufundishaji wa tuisheni baada ya kusema kuwa kuambiwa kuwa hatawalipa mshahara kwa sababu hawakufundisha katika kipindi ambao shule zimefungwa kutokana na Covid -19.
Alisema hilo halikubaliki na ndio linalowafanya baadhi yao kujiingiza katika ufundishaji wa tuisheni kinyume cha maagizo ya serikali katika kukabiliana na Covid 19.
Mwanri alisema ni lazima walimu wote walipwe mshahara wao ili kutowaweka katika vishawishi vya kujiingiza katika kuvunja maagizo ya Serikali ya kuzuia mikusanyiko kwa wanafunzi.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honaratha Rutatinisibwa aliwataka wazazi kutowaruhusu watoto wao kuzuzura ovyo mitaani kwa kuwa vitendo vinaweza kuwasababisha kupata maambukizi ya virusi vya Corona.
Alisema kuna baadhi ya maeneo kunaonekana makundi ya watoto wakiwa wamekusanyika pamoja jambo ambalo ni hatari kwao na kwa jamii zinazowazunguka.
Dkt. Rutatinisibwa alisema ni vema wanafunzi wakasisitizwa kubaki majumbani katika kipindi hiki ambacho mapambano dhidi ya Corona yakiendelea.
RC Tabora Asimamisha Likizo Za Waganga Na Wauuguzi Ili Kutoa Elimu Ya Kupamabana Na Corona
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesimamisha kwa muda likizo za watumishi wakiwemo wa Idara za Afya ili waendelee kuunganisha nguvu katika kusaidia jamii kwenye kampeni za mapambano ya ugonjwa wa Covid -19.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwakuwepo na wataalamu wa kutosha katika maeneo yote ambao wataendelea kutoa elimu ya kujikinga na kudhibiti ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi aina ya Corona usiingie Mkoani Tabora.
Mwanri alitoa kauli hiyo wilayani Uyui na Nzega wakati ziara yake ya kukagua Vituo na Zahanati zilizoandaliwa kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa wa covid -19 kama itatokea bahati wakaonekana wakaonekana Mkoani humo.
Alisema kipaumbele hivi sasa ni kuhakikisha tahadhari zote zinachukuliwa ili wakazi wa Mkoa wa Tabora waendelee kuwa salama kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu na viongozi wa Kitaifa.
Aidha Mwanri alizitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kutumia redio zilizopo na magari ya matangazo kupeleka elimu katika maeneo mbalimbali ya wananchi juu ya kujikinga na kulinda dhidi ya Covid -19.
“Tumieni magari yenye vipaza sauti kupitia katika mitaa mbalimbali kutoa elimu ya kujikinga wakati wote…na pia wataalamu nendeni katika Redio zote zilizopo mkoani Tabora kupeleka ujumbe ambao utawasaidia wananchi kuepuka kupata maambukizi ya Corona” alisema.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha magari yote ya abiria yanayosafirisha abiria ndani na nje Mkoa wa Tabora yanapuliziwa dawa kabla ya safari ili kuwakinga abiria ya uwezekano wa kupata corona.
Alisema ni lazima gari linapofika Stendi lipuliziwe dawa na taarifa zake zijazwe kwenye fomu ili kuonyesha kuwa limetekeleza agizo hilo ndio liruhusiwe kupakia abiria na kuendelea na safari zake.
MWISHO