Dereva wa Basi la Isamilo lenye namba za usajili T609 CQB Scania linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Mbeya Sebastian Mathias (43) mkazi wa Mwanza amefariki dunia wakati akiendelea na safari kutoka Mbeya kwenda Mwanza.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Machi 20,2020 saa nne asubuhi.
Kamanda Magiligimba amesema Sebastian wakati akitoka Mbeya kwenda Mwanza alikuwa akijisikia vibaya walipofika Singida ndipo hali yake ilibadilika wakawa wamebadilishana na dereva mwenzake.
"Sebastian alitoka Mwanza kwenda Mbeya akiwa anajisikia vibaya. Huwa wapo madereva wawili,wameenda hadi Mbeya,wakati wanatoka Mbeya kwenda Mwanza Sebastian alikuwa anaendelea kujisikia vibaya, walipofika Singida akawa anajisikia vibaya zaidi ndipo akabadilishana na yule dereva mwenzake",amesema Kamanda Magiligimba.
"Wamefika Tinde leo saa nne asubuhi akawa amezidiwa sana, wakambeba kwenda kwenye Kituo cha Afya Tinde,baada ya kumfikisha,Daktari akabaini kuwa tayari Sebastian Mathias alikuwa amefariki dunia",ameeleza Kamanda Magiligimba

Amesema kwa kuwa gari lina madereva wawili, dereva mwingine ameendelea na safari kwenda Mwanza na maiti imehifadhiwa katika kituo cha afya cha Tinde.