Thursday, 12 March 2020

Specialist; Enterprise Applications Support at NMB Bank Plc

Position: Specialist; Enterprise Applications Support Job Purpose To ensure implementation, continuous availability and security of Enterprise Applications Main Responsibilities Fully responsible with the implementation, maintenance and administration of the Enterprise Application Systems including but not limited to entire Active Directory (AD) System, Email Systems, HR Management System, ERP, E-learning Systems and internal developed systems. Serve as an escalation point… Read More »

The post Specialist; Enterprise Applications Support at NMB Bank Plc appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga Asema Atamchukulia Hatua Kali Godbless Lema

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema watamchukulia hatua Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa kitendo chake cha kusambaza taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Lema anadaiwa kutoa taarifa hizo hilo Februari 2020 wakati akizungumza katika mazishi ya katibu wa Chadema jimbo la Singida Mashariki, Alex Joas ambaye mwili wake ulikutwa kando ya barabara ukiwa na majeraha kichwani.

Akizungumza leo Machi 12, 2020, DPP Mganga amesema kuwa taarifa alizozitoa Lema zimeleta taharuki kwa Watanzania na kuwafanya wasiishi kwa amani na kwa jambo hilo lazima atalichukulia hatua na kwamba alichokisema Mbunge Lema ni kauli za kisiasa, kwani matukio hayo yote yalikwishachukuliwa hatua stahiki.

"Na kama yeye aliona hawa wamechinjwa na anawajua waliowachinja kwa mujibu wa sheria yeye anawajibika kutoa taarifa Polisi, Lema naomba ajitokeze aje kuniambia ni lini alienda kutoa taarifa kwamba kuna watu wanachinjwa na hatua hazikuchukuliwa" amesema DPP Biswalo Mganga.

Aidha DPP Mganga ameongeza kuwa "Tunapochukua hatua mnielewe, hatuwezi kuendelea kuwa Taifa la watu wenye uzushi, kwa hili nitachukua hatua, hatuwezi kuendelea kuwa na upotoshaji wa namna hii, halafu watu wanasema wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaonewa wakati wanafanya upuuzi".


Share:

Director at DCB Commercial Bank Plc Tanzania

Position: Independent Non Executive Director and Non Executive Director DCB Commercial Bank Plc is one of the leading commercial banks in Tanzania. Established in 2002. The Board of Directors of DCB Commercial Bank Plc would like to invite applications from suitable candidates for the position of Independent Non Executive Director and Non Executive Director. Duties and Responsibilities The… Read More »

The post Director at DCB Commercial Bank Plc Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Cargo Sales & Services Executive at Qatar Airways –

Senior Cargo Sales & Services Executive  Qatar Airways Welcome to a world where ambitions fly high. From experienced pilots to dynamic professionals embarking on new careers, Qatar Airways is searching for talented individuals to join our award-winning team. We take pride in our people—a dynamic and culturally diverse workforce is essential to why we are one of the… Read More »

The post Senior Cargo Sales & Services Executive at Qatar Airways – appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wabunge wa CHADEMA , Halima Mdee, Esther Matiko na Ester Bulaya Watoka Gerezani

Wabunge wa Chadema, Halima Mdee, Esther Matiko na Ester Bulaya wametoka gereza la Segerea leo baada ya kulipa faini ya Sh110 milioni.

Mkurugenzi wa itikadi, uenezi, mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema ameendelea kuwashukuru wananchi walio ndani na hata nje ya nchi kwa kujitoa kwao kwa michango mbalimbali iliyosaidia wabunge hao kulipiwa faini zao na hatimaye kutoka gerezani.

Viongozi hawa wa Chadema pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji juzi Jumanne Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa faini ya Sh350 milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili.


Share:

Chief Nutrition,(P-4),Dar es salaam,Tanzania

Job no: 530550 Position type: Fixed Term Appointment Location: Tanzania,Uni.Re Division/Equivalent: Nairobi Regn’l(ESARO) School/Unit: United Republic of Tanzania Department/Office: Dar Es Salaam, United Rep. of Tanzania Categories: Health, Nutrition, Planning, Communication / External Relations, P-4, Innovation, Programme Management UNICEF works in some of the world’s toughest places, to reach the world’s most disadvantaged children. To save their lives. To defend their rights. To help them… Read More »

The post Chief Nutrition,(P-4),Dar es salaam,Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Career Opportunities: Communications Intern (118742) at The United Nations World Food Programme

ABOUT WFP The United Nations World Food Programme is the world’s largest humanitarian agency fighting hunger worldwide.  The mission of WFP is to help the world achieve Zero Hunger in our lifetimes.  Every day, WFP works worldwide to ensure that no child goes to bed hungry and that the poorest and most vulnerable, particularly women and children, can access the… Read More »

The post Career Opportunities: Communications Intern (118742) at The United Nations World Food Programme appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Kambi Ya Jeshi la Marekani Nchini Iraq Yashambuliwa kwa Makombora, Watatu Wafariki

Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa askari wake wawili wameuawa katika shambulizi la maroketi dhidi ya kituo chake nchini Iraq. 

Askari hao wawili wa Marekani na mhudumu mwingine kutoka Uingereza wameuawa katika shambulizi hilo dhidi ya kambi ya Taji, kaskazini mwa Iraq, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. 

Kambi hiyo inayotumiwa na muungano wa nchi kadhaa za Magharibi zikiongozwa na Marekani  imeshambuliwa kwa makombora 18


Share:

Consultancy to Develop Immunization Policy Guideline in Tanzania at UNICEF

Job no: 530569 Position type: Consultancy Location: Tanzania,Uni.Re Division/Equivalent: Nairobi Regn’l(ESARO) School/Unit: United Republic of Tanzania Department/Office: Dar Es Salaam, United Rep. of Tanzania Categories: Gender Equality, Health, Nutrition, Planning, Consultancy, Programme Management UNICEF works in some of the world’s toughest places, to reach the world’s most disadvantaged children. To save their lives. To defend their rights. To help them fulfill their potential. Across 190… Read More »

The post Consultancy to Develop Immunization Policy Guideline in Tanzania at UNICEF appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Trump azuia safari za kutoka Ulaya Kwenda Marekani Ili Kukabiliana na Virusi Vya Corona

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitishwa kwa safari za ndege kutoka nchini humo hadi barani Ulaya kama mbinu ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Trump amesema, marufuku hayo yatatekelezwa kwa muda wa siku 30 zijazo kuazia siku ya Ijumaa lakini hatua hii haitaithiri Ireland na Uingereza, ambayo ina maambukizi 460.

"Ili kuzuia visa vipya maambukizi ya Covid-19 kuingia katika nchi yetu, nitazuia safari zote kutoka Ulaya hadi Marekani kwa siku 30 zijazo," amesema rais Donlad Trump katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni siku ya Jumatano.

Donald Tump amenyooshea kidole cha lawama Umoja wa Ulaya akisema ''umeshindwa kuchukua hatua za tahadhari kama hizo'' zilizoanzishwa na Marekani.

Hata hivyo rais wa Marekani ametangaza kutoa mkopo wa mabilioni ya dola kwa wafanyabiashara wadogo, na kutaka bunge la Congress kupitisha nafuu ya kodi ili kukabiliana na athari za mlipuko wa corona kiuchumi.

Marekani ina maambukizi 1135 na tayari watu 38 wamepoteza maisha.

-RFI


Share:

Serikali Yapanga Kutumia Trilioni 34.88 katika Bajeti ya 2020/21

Na Mwandishi wetu
Serikali imepanga kutumia kiasi cha shilingi trilioni 34.88 katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo ikiwa ni ongezeko la shilingi trilioni 1.76 kulinganisha na bajeti ya mwaka 2019/2020 ya shilingi trilioni 33.11.

Hayo yamesemwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akitoa Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa mwaka 2019/20 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka
2020/21.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 21.98 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 12.90 ni za matumizi ya maendeleo, ambazo ni sawa na asilimia 37 ya bajeti yote.

“Bajeti ya maendeleo inajumuisha shilingi trilioni 10.16 fedha za ndani, sawa na asilimia 78.8 ya bajeti ya maendeleo na shilingi trilioni 2.74 fedha za nje, matumizi haya yanajumuisha gharama za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2020”

Waziri Mpango, aliongeza kuwa mpango na bajeti kwa mwaka 2020/21 unazingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha ustawi wa jamii.

Aidha, alisema kuwa bajeti hii itaendelea na utekelezaji wa maeneo makuu manne ambayo ni kuondoa umasikini, kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana, kuendeleza vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali za umma, pamoja na kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.

Ili kufikia malengo hayo, Serikali itaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, kugharamia shughuli za Serikali ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati na uboreshaji wa huduma za kijamii kwa lengo la kuleta maendeleo kwa haraka.

Mwisho


Share:

Vijiji 8,641 vyafikiwa na umeme wa REA

Na Mwandishi Wetu
Jumla ya vijiji 8,641 kati ya vijiji 12,268 vya Tanzania Bara vimeunganishwa  na umeme kupitia Mradi ya Usambazaji Umeme Vijijini (REA) sawa na asilimia 70.4.

Hayo yamesemwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akitoa Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa mwaka 2019/20 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2020/21.

“Katika kipindi cha Julai 2015 hadi Januari 2020, jumla ya shilingi trilioni 1.53 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huu ikijumuisha shilingi bilioni 207.2 zilizotolewa katika kipindi cha Julai 2019 hadi Januari 2020.” Alisema Dkt. Mpango.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mpango alisema kuwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu nyingine kubwa duniani imeendelea kuwa tulivu kwa kipindi chote cha mwaka 2019.

Ameeleza kuwa utulivu wa sarafu ya Tanzania dhidi ya sarafu kubwa duniani umetokana na utekelezaji mzuri wa sera ya fedha na ya kibajeti, pamoja na kupungua kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje.

Kwa upande wa afya, Waziri Mpango ameeleza kuwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kugharamia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya vituo 540 vituo vya afya 361, hospitali za halmashauri za wilaya 71, hospitali za zamani tisa na zahanati 99 ambapo watumishi  477 wameajiriwa na kupangwa kwenye vituo hivyo.

Dkt. Mpango  alifafanua kuwa katika kipindi cha Julai 2015 hadi Januari 2020 jumla ya shilingi trilioni 3.01 zimetumika kugharamia huduma za afya ikijumuisha shilingi bilioni 14.5 zilizotumika kununua mashine ya Positron Emmission Tomography (PET scan) kwa ajili ya hospitali ya Ocean Road.

Akiongelea kuhusu mkakati wa uwezeshaji wa kaya maskini kiuchumi, amesema kuwa kwa sasa Serikali inatekeleza Awamu ya III ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III), ambapo jumla ya kaya 1,067,041 zenye wanakaya 5,130,001 zimetambuliwa na kuandikishwa katika vijiji na mitaa 9,627 kwenye Halmashauri 159 Tanzania Bara na kaya 32,248 zenye wanakaya 169,999 katika shehia 204 za Zanzibar na ruzuku ya fedha shilingi bilioni 968.73 imehawilishwa katika kaya hizo.

Amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 935.94 ni kwa ajili ya kuhudumia Kaya zilizopo Tanzania Bara na shilingi bilioni 32.79 ni kwa ajili ya Kaya zilizopo Zanzibar.

Aidha, katika kipindi cha Julai 2019 hadi Januari 2020, ufanisi wa kukusanya mapato ya kodi umeimarika na kufikia asilimia 96.9 ya lengo ikilinganishwa na ufanisi wa asilimia 88.6 katika kipindi cha Julai 2018 hadi Januari 2019, sawa na ukuaji wa asilimia 16.6.

Mwisho


Share:

Wadau Wa Uvuvi Mdogo Wakiwemo Wanawake Kuanza Kunufaika

Na. Edward Kondela
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema ana matumaini makubwa na mradi wa Mwongozo wa Masuala ya Uvuvi Mdogo (Small Scale Fisheries Guidelines) kwa kuwa mbali na kushughulika na wavuvi wadogo unalenga pia katika kuhakikisha wanawake wanahusishwa kikamilifu katika mnyororo wa uzalishaji kuanzia ngazi za awali.

Akizungumza jana majira ya jioni (11.03.2020) katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za wizara hiyo katika jengo la NBC jijini Dodoma, kilichohusisha baadhi ya wajumbe wa timu ya kitaifa inayoratibu utekelezaji wa mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), Naibu Waziri Ulega amesema serikali imekuwa ikitaka kuona namna wavuvi wadogo wanavyonufaika kupitia sekta ya uvuvi wakiwemo wanawake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah amesema wafadhili wa mradi huo wako tayari na wanaichukulia Tanzania kama mfano utakaotumika katika nchi nyingine katika bara la Afrika.

Ili kutimiza malengo hayo, timu hii ya kitaifa (National Task Team) inalenga kukusanya maoni ya wadau wote ikianzia na watunga sera, viongozi wakuu katika sekta ya uvuvi, mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na wavuvi.

Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti Alhaj Yahya Mgawe wameeleza kuwa ili uvuvi mdogo ambao unahusisha zaidi ya asilimia 90 ya uvuvi wote duniani uweze kuwa na tija ni lazima wavuvi wawezeshwe kwa kutumia mkakati uliokubaliwa na mataifa yote duniani.

Malengo ya mkakati huo ni kuondoa umasikini, matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi na kuhakikisha usalama wa chakula.

Timu ya kitaifa inayoratibu utekelezaji wa mradi wa Mwongozo wa Masuala ya Uvuvi Mdogo (Small Scale Fisheries Guidelines) unaofadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), iko katika hatua ya kukusanya maoni ya kuandaa mpango mkakati wa kitaifa ili kufikia malengo hayo.

Maoni na michango ya mawazo yataisaidia nchi kuandaa mpango wa utekelezaji na kuhakikisha maisha ya wavuvi wadogo yanaboreshwa na sekta ya uvuvi inachangia kukua kwa uchumi wa nchi.


Share:

Taasisi Wizara Ya Kilimo Zatakiwa Kutekeleza Majukumu Yake Kwa Weledi

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Taasisi zilizopo Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi za Mazao zimetakiwa kufanya kazi kwa Bidii na utashi mkubwa ili kutekeleza matakwa na taswira ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya ameyasema hayo jana Tarehe 11 Machi 2020 wakati akizungumza na Uongozi na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma.

Kusaya amesisitiza kuwa wataalamu hao wanapaswa kufanya Utafiti na kuonyesha matokeo chanya ya utafiti huo, Ameongeza kuwa utafiti haupaswi kuishia kwenye makaratasi pekee bali matokeo chanya kwa wakulima.

Amesema kuwa Wizara ya Kilimo inashika nafasi ya pili kwa kuwa na wasomi wengi kwa ngazi za PHD na Maprofesa hivyo taaluma hiyo inapaswa kuwa na matokeo chanya kwani kutokuwa na matokeo hayo ni kazi bure kwa wananchi na uwepo wa taasisi hiyo.

Kuhusu Changamoto ya fedha kwa ajili ya utafiti wa Mazao iliyobainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt Geoffrey Mkamilo, Katibu Mkuu huyo amesema kuwa hakuna mafanikio ya kilimo bila kuimarisha utafiti hivyo lazima kutafuta njia ya kupata fedha kwa haraka ili kuendeleza utafiti.

Kusaya ametoa mwito kwa wafanyakazi wa TARI kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiendeleza kielimu. "Taasisi ya utafiti ni muhimu sana kwa watu kujielimisha zaidi, Hata kama una miaka 60 sisi tutakupeleka shule, hakuna kada ambayo tutaiacha zote tutazipeleka shule ili tuweze kwenda na wakati" Alikaririwa Katibu Mkuu Ndg Kusaya

Hii ni ziara ya kwanza ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya tangu alipokabidhiwa kijiti kuiongoza wizara hiyo kama mtendaji Mkuu Machi 6, 2020.


Share:

Serikali Kuanzisha Mfuko Maalum Wa Kilimo

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema wizara ya kilimo inakusudia kuanzisha mfuko maalum kwa ajili kusimamia maendeleo ya mazao ya pamba,tumbaku na korosho.

Ametoa kauli hiyo jana mjini Chato alipokuwa akizunguzma kwenye kongamano la kilimo kwa vijana wa mikoa ya Geita,Shinyanga na Kagera na kuutaja mfuko huo utakaojulikana kama “Seed Fund For AAgriculture”

Bashe amewaeleza vijana hao kuwa mfuko huo utakaochangiwa na wakulima ili kuondoa chanagamaoto za upatikanaji pembejeo,viuatilifu na masoko nchini

Amesema wizara inatarajia wakulima wa pamba wachangie sh .20 kwa kilo,korosho sh.20 na tumbaku sh.200 kwa kilo hivyo kuwezesha serikali kupata fedha za kutosha kusimamia changamoto za mazao haya ya kimkakati.

“Ukichukua takwimu za uzalishaji za msimu uliopita 2019 tunatarajia kukushanya fedha shilingi Bilioni 24 ambazo tutzaifungulia akaunti maalum Benki Kuu wa Tanzania kutunza fedha hizo,alisema Bashe

Aliongeza kusema taasisi za fedha kama mabenki yatapewa fursa ya kwenda kukopa kawa riba itakayokubaliwa na serikali ili waweze kudhamaini wakulima kupitia AMCOS au Ushirika kwa ajili ya pembejeo na mahitaji mengine ya shambani.

Ili kufanikisha hilo Bashe amesema kila mkulima nchini atasajiliwa na kuwa na kitabu chake kitakachoonyesha mahitaji ya shamba,kiasi cha eneo alilozalisha na mavuno yake na kiasi atakachopeshwa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo wa Kilimo amezipongeza Benki za NMB,CRDB na Azania kwa kuwashiriki katika kukwamua ununuzi wa zao la pamba msimu wa 2019 kwa kudhamini mikopo ya wanaunuzi wa pamba kwa asilimi 13 jambo ambalo lililotoa manufaa kwa wakulima


Share:

Serikali Yaridhishwa Na Utendaji Kazi Mfuko Wa Mawasiliano Kwa Wote.....Yasema hakuna atakayeachwa bila kupata mawasiliano

Na Prisca Ulomi, WUUM, Songwe
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeridhishwa na utendaji kazi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kwa kujenga minara ya mawasiliano maeneo ya vijijini na yasiyo na mvuto wa kibiashara ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za mawasiliano

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye alipokuwa katika ziara ya kuzindua minara ya mawasiliano iliyojengwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) mkoani Songwe kwenye kijiji cha Maleza, Kata ya Mbangala baada ya kupatiwa ruzuku na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

Nditiye amesema kuwa ni haki ya kikatiba kwa kila mwananchi kuwasiliana na UCSAF imetambua hilo kwa kuzipatia kampuni za simu za mkononi ruzuku ili zijenge minara kwenye vijiji mbali mbali nchini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa kuwa kampuni hizo huwa zinawekeza kwenye maeneo yenye wateja ili wafanye biashara na kupata faida

Akizungumza mbele ya wananchi wa kijiji hicho, Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba amesema kuwa watahakikisha hakuna mwananchi atakayeachwa bila kupata huduma ya mawasiliano kwa kuwa wanatambua majukumu waliyokasimiwa na Serikali ya kufikisha huduma za mawasiliano kwa kujenga minara ya mawasiliano, kuzipatia shule vifaa ya TEHAMA ikiwemo kompyuta zilizounganishwa na mtandao wa intaneti kwa ajili ya waalimu na wanafunzi kufundishia na kujifunzia na kuendesha mafunzo ya TEHAMA kwa waalimu nchini

“Hadi sasa tumetangaza zabuni za ujenzi wa minara ya mawasiliano kwenye kata 956 zilizopo maeneo mbali mbali nchini na tayari ujenzi umekamilika kwenye kata 652, minara hiyo imewashwa na wananchi wanapata huduma za mawasiliano na hadi kufikia mwaka 2020 asilimia 94 ya wananchi wanapata huduma za mawasiliano ukilinganisha na asilimia 46 katika kipindi cha mwaka 2009” amefafanua Mashiba

Akizungumza kuwakilisha wananchi wake, Mbunge wa jimbo la Songwe, Phillip Mulugo amesema wanaishukuru na kuipongeza UCSAF na TTCL kwa kujenga minara ya mawasiliano bila kujali umbali wa mahali eneo lililopo ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kuwasiliana

“Nataka nitoe ofa kwa mabalozi wote wa Kijiji cha Maleza na Mbangala na Kata ya Mbangala nataka niwanunulie simu 100 za TTCL ila masharti waweke laini za simu za TTCL,” amesema Mulugo baada ya kufurahishwa na uwepo wa mawasiliano.

Meneja wa TTCL Mkoa wa Songwe, Martha Joachim akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kabla ya Nditiye kuzindua mnara huo alisema kuwa wataendelea kujenga minara nchi nzima kwa kushirikiana na UCSAF ili watanzania wapate huduma kutoka kwenye Shirika lao kwa gharama nafuu na za uhakika

Vile vile Nditiye alifika kwenye kijiji cha Udinde kilichopo kwenye kata ya Udinde mkoani humo kukagua mnara wa mawasiliano wa TTCL baada ya kupewa taarifa na Mulugo kuwa mnara huo haujawashwa kwa kuwa vifaa vyake vipo bandarini Dar es Salaam ambapo ameipa TTCL siku 36 tu kuhakikisha kuwa vifaa husika vinafika kijijini hapo na
kufungwa kwenye mnara huo ili uwashwe kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano


Share:

Waziri Mhagama Ataka Mafunzo Ya Kilimo Cha Kisasa Kwa Kutumia Teknolojia Ya Kitalu Nyumba Kuimarishwa Usimamizi Na Uendeshaji

Na: Mwandishi Wetu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka waratibu na wadau wa Programu wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba “Greenhouse” ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Kilimo, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na wakandarasi ambao walijenga vitalu nyumba kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa mafunzo hayo ili yawe na ubora zaidi.

Waziri Mhagama ameyasema hayo jana Machi 11, 2020 wakati wa kikao kilichowakutanisha Waratibu hao pamoja vijana kwa lengo la kujadili namna bora ya kuimarisha mafunzo ya Kilimo hicho kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba.

Alieleza kuwa kuimarishwa usimamizi na uendeshaji wa programu ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba “Greenhouse” kutachangia kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya kilimo.

“Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ndio yenye dhamana na masuala ya vijana iliamua kupitia ilani ya uchaguzi ibara ya 6 kifungu (a) inayosema kuhamasisha kilimo kupitia kauli mbiu ya Kilimo Kwanza kwa kuwawezesha wakulima kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa, pembejeo, zana za kisasa na wataalamu wa ugani pamoja na mbinu za kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao, ambao ulipelekea kutambua umuhimu wa mchango wa vijana hasa waliopo vijijini ndipo mradi huu wa Kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba ulianzishwa kwa lengo la kuwezesha vijana,” alisema Mhagama.

Aliongeza kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ina nia ya dhati ya kuwawezesha vijana kupitia programu mbalimbali inazoazisha kwa lengo la kuwasaidia vijana kuondokana na changamoto ya ajira.

“Serikali ina lengo la kufikisha ujuzi huo wa kilimo cha kisasa katika halmashauri zote za Tanzania bara kwa kuwa asilimia 63 ya fursa za ajira zinapatikana kwenye kilimo na tena maeneo ya vijijini,” alisema Mhagama 

“Mataifa makubwa mengi yaliyoendelea wamekuwa wakitumia kilimo cha aina hiyo kwa lengo la kulima kisasa, kuongeza thamani ya mazao, kupata masoko endelevu na la uhakika na kulima kwa tija, hivyo tukiwawezesha vijana wetu watanufaika na kilimo hicho na sekta hiyo italeta tija katika kukuza uchumi wa nchi,” alieleza Mhagama.

Sambamba na hayo Mheshimiwa Mhagama alitoa maagizo yafuatayo (i) Kufanyika maamuzi ya haraka yatakayowezesha vijana katika halmashauri ambazo bado mradi huo haujafika wanafikiwa (ii) Fedha zote zilizokusanywa na vijana katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo zikaguliwe na vijana washirikishwe ili waweze kutoa taarifa ya idadi ya mazao waliyozalisha na kiwango walichoweza kuuza (iii) kuanzishwa mfumo wa ufuatiliaji ambao utakuwa na taarifa ya utekelezaji wa majukumu (iv) Kuwezesha upatikanaji wa mikopo ambayo itawasaidia vijana hao kuanzisha vitalu nyumba vyao (v) kutengeneza mfumo wa ukusanyaji mapato na matumizi (vi) Wakandarasi waliojenga vitalu nyumba katika halmashauri 84 awamu ya kwanza kufanyia marekebisho vitalu nyumba ambavyo vimekuwa na matatizo.

Aidha Waziri Mhagama amewataka vijana kutumia ujuzi waliopata katika mafunzo hayo ili waweze kusimamia mradi huo vizuri na wajenge moyo wa kuthubutu katika kuwasaidia vijana wenzao kupata ujuzi wa mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe alikiri kupokea maagizo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili programu hiyo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa iweze kuwa endelevu.

“Ofisi ya Waziri Mkuu iliona umuhimu wa kushirikiana na , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Kilimo, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, wakandarasi pamoja na Vijana ili kutathmini utekelezaji wa mradi huo na kuona namna ya kukabili changamoto ambazo zilijitokeza, mafanikio yaliyopatikana ili kuona namna bora ya kuimarisha mafunzo hayo,” alisema Massawe.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Msaki alielezea maazimio waliyofikia pamoja na wadau katika kuimaarisha usimamizi na uendeshaji wa mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kuangalia namna bora ya kuendesha mafunzo hayo, uwepo wa utaratibu maalum wa makusanyo, utunzaji na matumizi ya fedha, kuwezesha vijana kuwa na ujuzi wa kuongeza thamani ya mazao, kuelezea wananchi mafanikio yaliyopatikana kupitia mradi huo wa kilimo cha Kitalu nyumba,kuwezesha vijana kufanya kilimo biashara na uwepo wa muendelezo wa kutoa mafunzo na kuongeza vitalu nyumba katika kila halmashauri.

Naye Mmoja wa wanufaika wa Programu hiyo Bw. Festo Masiba ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamewajengea ujuzi mkubwa wa kuweza kulima kwa tija.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutuamini sisi vijana na kutuwezesha kupata mafunzo ya Kilimo bora kwa kutumia eneo dogo na upatikanaji wa mazao ni mwingi, tumeweza kukua kiuchumi na tunaujuzi wa kuwajengea wadau wengine vitalu nyumba,” alisema Masiba 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger