Monday, 9 March 2020

46 Job Vacancies at Tanzania Posts Corporation – POSTAL OFFICER II

POST POSTAL OFFICER II – 46 POST POST CATEGORY(S) HR & ADMINISTRATION TAXATION AND SOCIAL PROTECTION EMPLOYER TANZANIA POSTS CORPORATION TPC APPLICATION TIMELINE: 2020-03-07 2020-03-21 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES To check counter’s imprest for stamps, cash and other saleable items; To attend Public inquiries at Postal counter; To perform shipping duties including ticking and verification of… Read More »

The post 46 Job Vacancies at Tanzania Posts Corporation – POSTAL OFFICER II appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Head of Customer Network and Business Development at National Bank of Commerce (NBC)

Position: Head of Customer Network and Business Development Location: Head Office NBC NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description​ Reporting to Head of Retail banking, Head of Customer network & Business Development has responsibilities:… Read More »

The post Head of Customer Network and Business Development at National Bank of Commerce (NBC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Ukuaji wa uchumi unavyotegemea sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi

Takwimu zinaonyesha kwamba Tanzania imepitia kipindi kizuri cha ukuaji wa kiuchumi katika muongo mmoja uliopita na kuifanya hivi sasa kuwa moja ya chumi zinazokua vizuri katika eneo la Afrika Mashariki. 
 
Ripoti ya UK ThinkTank inaongeza kuwa mafanikio ya ukuaji wa kiuchumi Tanzania yamewezeshwa na juhudi za serikali kukuza sekta ya viwanda na kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji katika sekta mbalimbali. Matokeo ya juhudu hizo yameifanya Tanzania kuwa mmoja ya wauzaji wakubwa nje wa dhahabu na pia kuwa moja ya nchi inayopata watalii wengi zaidi barani Afrika.
 
Wakati huo huo serikali ya Tanzania imeendelea kujiweka imara katika kuwekeza kwenye miundombinu muhimu kama miradi ya Standard Gauge Railway (SGR), kupanua zaidi bandari na kuunganisha maeneo ya vijiji na nishati ya umeme. 
 
Ripoti hiyo ya UK ThinkTank inaeleza kuwa maendeleo ya Tanzania yamechangiwa sana na ubunifu katika teknolojia na uwepo wa huduma nzuri ya mawasiliano ya simu na data. Maendeleo haya katika teknolojia ni matokeo ya uwekezaji wa muda mrefu kwenye sekta ya mawasiliano ya simu ambayo taarifa zinaonyesha kuwa mpaka sasa ni uwekezaji unaozidi shilingi za Kitanzania trilioni 6.  
 
Uwekezaji huu katika sekta ya mawasiliani ya simu za mkononi umekuza sana mabadiliko ya kidijitali Tanzania mfano huduma ya kasi ya 4G na mtandao wa intaneti kupitia simu za mkononi. Ubunifu katika sekta hii pia umeleta huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambapo zaidi ya watu milioni 25 Tanzania sasa wanatumia simu zao kutuma, kupokea, kulipia huduma na hata kutunza fedha. 

Wafanyabishara wadogo na wa kati nao wanafurahia maendeleo ya sekta ya mawasiliano ya simu ambayo inawasaidia kuendesha biashara zao kwa namna mbalimbali kama kuwapa intaneti, kupokea malipo, kulipia huduma mbalimbali, kutangaza bidhaa mitandaoni na hivyo kupunguza gharama za kuendesha biashara, miaka si mingi nyuma ilikuwa lazima ukapange foleni benki kufanya huduma nyingi ambazo leo unazifanya kupitia simu yako.  
 
Uimara wa sekta hii ya mawasiliano ya simu ni jambo muhimu na ili uendelee ni budi kuendelea kujenga mazingira bora ya sekta hii kukua. Kujenga mazingira ya sekta binafsi kuwekeza mtaji zaidi huku serikali ikiendelea kuweka sera bora za kuratibu sekta hii ni mambo muhimu kuwezesha sekta kukua zaidi ili Tanzania na Watanzania wote wazidi kunufaika zaidi.


Share:

Manager: Transactional Services at National Bank of Commerce (NBC)

Position: Manager: Transactional services Location: Head Office NBC NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description​ Accountability The design, development and delivery of the Transactional services operational plan Formulate and own overall operational plan across… Read More »

The post Manager: Transactional Services at National Bank of Commerce (NBC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Vacancies at the President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat

On behalf of the Vocational Education and Training Authority (VETA), The University of Dodoma (UDOM), Tanzania Posts Corporation (TPC), Tanzania Institute of Education (TIE), Architects and Quantity Surveyors Registration Board (AQRB) and the Institute of Judicial Administration Lushoto, President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat invites qualified Tanzanians to fill 152 vacant posts as mentioned below:

The post Job Vacancies at the President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Angalia Picha : MAANDALIZI YA KUFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA SHINYANGA

Maandalizi ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga yamekamilika.

Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala amesema mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 4,2019 yatafungwa kesho Jumanne Machi 10,2020 katika Viwanja vya Sabasaba Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

“Maandalizi yamekamilika,Jumla ya wanafunzi 141 kati yao wanaume 101 na wanawake 40 watahitimu mafunzo yao kesho.Tunawakaribisha wananchi kuja kua kushuhudia ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Akiba”,amesema Kamala.

Malunde 1 blog leo Jumatatu Machi 9,2020 imeshuhudia wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wakifanya mazoezi ya maandalizi ya kufunga mafunzo hayo katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Kambarage Mjini Shinyanga.
Mapema leo Jumatatu Machi 9,2020 ,Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala (mwenye tisheti nyeupe) na  Mkufunzi wa mafunzo ya Jeshi la Akiba Isaya Mbise wakikagua Gwaride la Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga Machi 10,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye Gwaride la Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga.
Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye Gwaride la Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala akiangalia  Bendi ya Wahitimu wa Jeshi la Akiba wakiwa kwenye Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga Machi 10,2020. 
Kulia ni Mkufunzi wa mafunzo ya Jeshi la Akiba Isaya Mbise akiangalia  Gwaride la Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga Machi 10,2020. 
Kulia ni Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala akiangalia  Gwaride la Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga Machi 10,2020. 


Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye Gwaride la Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga
Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye Gwaride la Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga
Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye Gwaride la Maandalizi ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

WAZIRI MKUU WA SUDAN ANUSURIKA KIFO BAADA YA MSAFARA WAKE KUSHAMBULIWA

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok amenusurika kifo baada ya msafara wake kushambuliwa na Watu wasiojulikana.

 Mlipuko mkubwa umetokea eneo la tukio katika Mji mkuu wa Nchi hiyo wa Khartoum na tayari Waziri Mkuu huyo amekimbizwa katika eneo salama.

Hamdok aliteuliwa Kuwa Waziri Mkuu Agosti mwaka jana baada ya maandamano makubwa yaliyomng'oa Rais Omary Al-Bashir


Share:

Business Official/Program Administrator at PATH

PATH is currently seeking a qualified Business Official/Program Administrator for an upcoming CDC-funded program, “Health Information System Development, Project Management and Coordinated Deployment for National HIV and Health Sector Systems in the Republic of Tanzania under the Global Health Security Agenda and under PEPFAR”. The project’s goal is to increase the ability of information systems to support high… Read More »

The post Business Official/Program Administrator at PATH appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Laini zote ambazo hazijasajiliwa kuzimwa Jumamosi

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kazi ya kuzima laini zote za simu, ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa (NIDA), itakamilika Jumamosi ijayo. Itakamilika ili kutoa fursa kwa wananchi kuendelea na mambo mengine ya kitaifa, ukiwemo Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Uzimaji huo wa laini ulianza mwishoni mwa Januari mwaka huu, baada ya Rais John Magufuli kuongeza siku 20, ili kutoa fursa kwa wananchi, ambao walikuwa hawajasajili laini zao, wakamilishe usajili huo kwa alama za vidole.

Mbali na kuzima laini hizo, TCRA pia imesema kuanzia Juni 30, mwaka huu, kila mmiliki wa laini atatakiwa kumiliki laini moja tu ya simu kwa kila mtandao.

Kama kuna mtu anamiliki laini zaidi ya moja katika mtandao mmoja, atalazimika kuchagua laini moja anayoihitaji ili zilizobaki zizimwe.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa TCRA, Frederick Ntobi, amelieleza HabariLeo kuwa ifikapo Machi 14, mwaka huu watoa huduma ambao ni kampuni za simu za mkononi, watatakiwa kuzizima laini zote, ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha NIDA.

“Kutakuwa na awamu mbili za uzimaji wa laini zilizokuwa zimesajiliwa awali kwa kutumia Kitambulisho cha Mpiga Kura na Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, ambapo laini za simu 8,722,527 zilizobakia hadi tarehe 02/03/2020 zitafikia ukomo wake rasmi tarehe 14/03/2020,” alisema Ntobi.

Katika hilo, alifafanua kuwa laini milioni tatu zilizimwa jana Machi 8 ; na awamu ya pili ambayo ni ya mwisho, laini milioni tano zilizobaki, zitazimwa Jumamosi ya wiki hii.

Alisema awamu hizo mbili, zitakuwa zimefanya kazi ya kuzima laini zilizosajiliwa kwa kutumia Kitambulisho cha Mpiga Kura na Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi kufikia tamati, ambapo jumla ya laini za simu 8,722,527 zitakuwa zimezimwa.

Ntobi alisema watoa huduma, wanatakiwa kuwasimamia vizuri na kwa weledi mawakala wao wa usajili wa laini za simu ili wafuate sheria na utaratibu katika usajili kwa kutumia alama za vidole. Alisema mpaka sasa laini 35,044,629 zimeshasajiliwa kwa alama za vidole, sawa na asilimia 80.1.

Hadi kufikia Machi 2, mwaka huu, jumla ya laini zote za simu zilizounganishwa mitandaoni ni 43,767,156. Laini moja kwa mtandao mmoja.

Kwa mujibu wa Ntobi, Kanuni ya 18 na 19 ya Sheria za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta (Usajili wa Laini) ya mwaka 2020, kila mtu atatakiwa kumiliki laini moja kwa mtandao mmoja wa simu kuanzia Juni 30, mwaka huu.

Endapo mtu anamiliki laini zaidi ya moja kwenye mtandao mmoja, atalazimika kuchagua laini anayoihitaji kati ya hizo. Zilizobaki zitazimwa.

Wanaotumia CCTV
Sambamba na hilo, watu wanaotumia mawasiliano ya mashine kwa mashine, kama vile kamera za CCTV watatakiwa kumiliki laini nne tu na laini hizo hazipaswi kuhamishwa kwenda kwenye matumizi mengine, isipokuwa kwa yale tu yaliyoainishwa wakati wa uombaji na usajili.

Vivyo hivyo, kwa watu waliosajili laini kwa ajili ya matumizi ya ‘moderm’ nao hawapaswi kuzitumia kwa matumizi mengine yoyote.

Suala la akina ‘Tuma Pesa’
Kutokana na matapeli kuendelea kuwatumia watu ujumbe usemao ‘Tuma Pesa Kwenye Namba Hii’ au wengine kuwapigia watu simu, wakijifanya ni wafanyakazi wa kampuni za simu au wengine namba zao kutumika katika uhalifu mwingine wowote, TCRA ilisema atakayebainika, namba yake ya NIDA itafungwa na hataweza kupata huduma katika kampuni yoyote ya simu nchini.

Ntobi alisema wananchi wanaopokea jumbe hizo za kitapeli, au kupigiwa simu na matapeli, wanapaswa kutoa taarifa za namba hizo kwenye kampuni ya simu husika, ili namba ya NIDA ya tapeli huyo ifungwe moja kwa moja.

Waliowasajilia laini wengine, wageni Kuhusu watu waliowasajilia watu wengine, alisema wajiandae kukabiliana na taratibu za sheria, pale laini hizo zitakapobainika kuhusika kwenye matatizo.

Na wale ambao wamewasajilia wageni kutoka nje ya nchi kinyume cha utaratibu, wajue kuwa ni kosa la jinai, nao namba zao za NIDA zitafungwa moja kwa moja.

Chanzo: Habari Leo


Share:

Mgonjwa Wa Kwanza Wa Corona Misri Afariki Dunia

Misri imeripoti kifo cha kwanza kilichosababishwa na virusi vya corona ambapo Waziri wa Afya nchini humo amesema Mtalii kutokea Ujerumani (60 yrs) aliingia Misri siku saba zilizopita na kukimbizwa Hospitali baada ya kubainika ana virusi hivyo.

Katika taarifa yake ya hivi karibuni, Wizara ya Afya ya Misri imeeleza kuwa idadi ya watu wanaogua homa ya corona nchini humo imefikia 55.


Share:

Daraja la Mto Simuyu lililoko katika barabara kuu ya Mwanza-Musoma Lafungwa Kwa Siku 10

Daraja la Mto Simuyu lililoko wilayani Magu katika barabara kuu ya Mwanza-Musoma limeharibika, hivyo Serikali kulifunga kwa siku 10 ili kupisha matengenezo makubwa.

Daraja hilo limeharibika kutokana na uchakavu uliosababisha vyuma kukatika.

Akiwasilisha taarifa ya ufungwaji wa daraja hilo Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Rubirya, alisema ameifunga barabara hiyo kuanzia jana hadi Machi 8, mwaka huu ili kupisha matengenezo makubwa ya daraja.

Mhandisi Rubirya aliongeza kuwa wameamua kufanya matengenezo ya haraka ili kujiepusha na athari zitakazoweza kujitokeza kwa sababu kuchelewa kwa ujenzi huo unaweza kuwasababishia athari watumiaji wa barabara hiyo.

Alisema kuwa barabara hiyo imefungwa ili kupisha matengenezo kuanzia saa tatu usiku hadi saa 11 asubuhi, huku akiomba ushirikiano wa Jeshi la Polisi katika kutekeleza kazi hiyo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa daraja hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alisema kutokana na changamoto hiyo njia zitafungwa kwa muda uliopangwa kwa siku kumi ili kupisha matengenezo hayo.

Alisema serikali ina mpango wa kujenga daraja jipya, hivyo hatua zinazofanyika sasa ni za muda mfupi, na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu ili waboreshewe njia itakayowanufaisha na kuendeleza ujenzi wa taifa.

 
-Nipshe


Share:

Uganda Yawataka Raia 22 wa kigeni wanaotoka kwenye Nchi zenye maambukizi makubwa ya Corona Warudi Kwao

Wizara ya afya nchini Uganda imesema raia wa kigeni 22 waliokuwa wamewasili nchini humo kutoka katika mataifa yaliyoathiriwa na maambukizi ya Corona na kuombwa kutengwa kwa siku 14 watarudishwa katika nchi zao baada ya kukataa utaratibu huo wa serikali.

Wageni hao walikuwa wamewasili nchini humo kuhudhuria mkutano wa kibiashara kati ya Uganda na bara Ulaya ambao unaanza leo na kumalizika kesho.

Waziri wa Afya wa Uganda Ruth Aceng, pia ametangaza mataifa ambayo raia wake hawataruhusiwa nchini humo kwa sasa.

Mapema mwezi Februari wasafiri zaidi ya 100 waliwekwa karantini baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Kampala nchini Uganda wakitokea nchini China. Raia 44 wa China ni miongoni mwa wasafiri hao waliotengwa.


Share:

Korea Kaskazini yarusha makombora matatu katika Bahari ya Mashariki

Korea Kaskazini imerusha makombora matatu yasiyojulikana kwenye bahari ya mashariki, wiki moja baada ya kurusha makombora mawili ya masafa mafupi katika bahari hiyo. 

Baraza la wanadhimu wakuu la jeshi la Korea Kusini limetoa taarifa fupi ikisema, makombora yalirushwa upande wa kaskazini mashariki kutoka maeneo yaliyoko karibu wilaya ya Sondok mkoani Hamgyong Kusini.


Share:

Kaliua Yatoa Mkopo Wa Milioni 345 Kwa Vikundi 57 Katika Kusherekea Siku Ya Wanawake Duniani

NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imekabidhi mkopo wa shilingi milioni 345 kwa vikundi 57 ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani katika mwaka wa fedha unaoendelea.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kimkoa yalifanyika jana Wilayani humo.

Alisema kati ya fedha hizo vikundi 28 vya wanawake vimepokea milioni 184, vikundi 19 vya vijana vimekopeshwa 133.5 na vikundi 10 vya walemavu vimekpeshwa milioni 27.

Alisema fedha hizo ni sehemu ya utekelezaji ilani yaChama cha Mapinduzi iliyoagiza kutenga asilimia 10 kutokana na mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa vikundi hivyo.

Dkt Pima alisema tangu nwaka 2015 hadi desemba 2019 , Kaliua ilikuwa imeshatoa jumla ya mikopo ya shilingi milioni 839.7 kwa vikundi 209.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema hadi hivi jumla ya shilingi milioni 591.9 bado haijarejeshwa kitendo ambacho kimewafanya waandikie notisi ya 90 ili warejeshe.

Dkt. Pima alisema baada ya hapo wadaiwa sugu wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Akikabidhi hundi kwa vikundi , Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amevitaka vikundi ambavyo bado havijaresha mikopo waliopatiwa kurejesha ili iweze kuwasadia wengine.

Aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na kuzitaka Halmashauri nyingine za Mkoa wa Tabora kuhakikisha wanatenga asilimia 10 za mapato yake ya ndani kwa ajili ya kupeleka katika vikundi kama ilivyoelekezwa.

Mwanri alisema kuwa ni vema Halmashauri zikahakikisha zinatoa fedha ambazo zitavisaidia vikundi kupata matokeo mazuri na kuwapatia maendeleo.


Share:

Wizara ya Kilimo Yajivunia kwa kuongeza eneo la uzalishaji wa mbegu, miche bora pamoja usajili wa Wakulima na watoa huduma za kilimo

Na Issa Sabuni, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema Watendaji wa Wizara ya Kilimo anayoiongoza wanapaswa kujivunia kwa mafanikio mengi waliyoyapata chini ya uongozi wake.

Ameyasema hayo mapema jana tarehe 8 Machi 2020 wakati akifunga mkutano wa kikazi, mkutano uliowajumuisha Wenyeviti, Wakuu wa Bodi za Mazao, Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo pamoja na Idara na Vitengo vya Wizara ya Kilimo, Jijini Dodoma.

Waziri Hasunga amesema Wizara ilifanikiwa kusajili Wakulima wa mazao ya kimkakati na yanasimamiwa na Bodi za Mazao; mazao hayo ni pamoja na chai, kahawa, korosho, sukari, pamba, mkonge, tumbaku na pareto.

“Najivunia kuanzisha mfumo wa usajili wa Wakulima wa mazao nane ili kuwa na kanzidata ya Wakulima wa mazao hayo yenye kusimamiwa kupitia Bodi za Mazao na baada ya zoezi hili kukamilika; tutaanza kuwasijili Wakulima wa mazao mengine, na sambamba na hili tumeanza kuwasajili Wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa kilimo.” Amekaririwa Waziri Hasunga.

“Kwa ujumla tumefanya vizuri kwa kuvuka lengo la usajili wa Wakulima kwani tumesajili Wakulima 1,279,884 kati ya Wakulima 1,377,069 na tunataraji kuanza kuwapa vitambulisho ili na wao watambulike kama Watumishi wengine katika kada mbalimbali wanavyotambuliwa.” Amesisitiza Waziri Hasunga

Waziri ametaja mafanikio mengine ni pamoja na Wizara kuanza kutoa vibali mbalimbali vya mazao ya kilimo kwa mfumo wa Kielektroniki (ATIMS), mafanikio mengine ni pamoja na kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa mbegu bora, kutoka hekta 10,887 mwaka 2015/2016 hadi 94,368 2018/2019 ambapo uzalishaji umetoka tani 10,000 hadi tani 71,207

Waziri Hasunga ameongeza kuwa uzalishaji wa miche na vipando bora vya mazao ya kilimo umeongezeka kutoka miche milioni 5 mwaka 2015/2016 hadi miche na vipando milioni 22,707,000

Waziri Hasunga amesisitiza kuwa Watendaji wa Wizara wanapaswa kuongeza juhudu katika masuala ya mikakati, programu na usimamizi kwa Maafisa Ugani ili uzalishaji uongezeke kwenye mazao ya kimkakati kama pamba, kahawa, tumbaku na chai.

Katika kulitekeleza hilo Waziri Hasunga amemuagiza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kuhakikisha anaanda malengo ya kuongeza uzalishaji kwa mazao yote kwa mwaka ujao wa 2020/2021.


Share:

Rais Magufuli Alivyoshuhudia Yanga Ikiichapa 1-0 Simba Sc Uwanja Wa Taifa Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Vijana, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ali Karume pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wakiwapungia mkono wa salamu kwa Wapenzi nan a Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo wa Ligi kuu wa Watani wa jadi kati ya Yanga na Simba Uliochezwa katika Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam. Machi 08, 2020. Mchezo uliomalizika kwa Ushindi wa goli moja kwa Yanga na Simba sifuri.



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu March 9
















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger