Thursday, 5 March 2020

Head of Retail Banking at Maendeleo Bank

Maendeleo Bank PLc commenced operations in September 2013 as a Regional Bank with its Headquarters at Luther House, Sokoine Drive – Dar es Salaam. It is the first bank in Tanzania to be registered in Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) from its inception through Enterprise Growth Market (EGM) window.The bank has been awarded as ‘the best listed… Read More »

The post Head of Retail Banking at Maendeleo Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Circulation Field Officer at Guardian Limited

CIRCULATION FIELD OFFICER  The Guardian Limited publisher of leading Tanzania newspapers, The Guardian and Nipashe, is looking for motivated and experienced people to fill the position of: CIRCULATION FIELD OFFICER – DAR ES SALAAM Job Purpose: To boost copy sales and develop relationships with agents and vendors in the sales channel in the assigned area to meet your set… Read More »

The post Circulation Field Officer at Guardian Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Branch Managers at CRDB Bank (37 Posts)

Branch Managers (37 Positions) CRDB Bank Plc is an African bank and a leading Financial Services Provider in Tanzania with a current presence in Tanzania and Burundi, East Africa. The Bank was established in 1996 and was listed on the Dar Es Salaam Stock exchange (DSE) in June 2009. Over the years, CRDB Bank PLC has grown to become… Read More »

The post Branch Managers at CRDB Bank (37 Posts) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Bank Officers (Several Positions) at NMB Bank

Bank Officers (Several Positions) Location:  Central Zone, Dar Zone, Eastern Zone, Highland Zone, Lake Zone, Northern Zone, Southern Zone, Western Zone. Job Purpose To provide outstanding customer experience to NMB customers and prospective customers. To ensure customer satisfaction is met at all times through giving professional advice on NMB’s products and services To provide quick and friendly service in… Read More »

The post Bank Officers (Several Positions) at NMB Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jinsi Ya Kuandika CV Nzuri Ambayo Itamvutia Mwajiri na Kukufanya Upate KAZI Kirahisi

WATU wengi nchini wamekosa ajira  kwa sababu ya makosa wanayoyafanya wakati wa kuandika CV zao.


Kumbuka,  makampuni  karibia yote yanayotangaza nafasi za kazi hupokea wastani wa maombi 200-500 ya kazi kwa tangazo moja la kazi. 

Hivyo, CV yako lazima ikae vizuri ili kumshawishi mwajiri. Utaratibu wa kuomba kazi unaweza ukawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote yatahitaji uwatumie CV.

CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa kiundani ya historia yako ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye maombi ya kazi ya nafasi za kati, za juu na za utafiti.

Mambo yafuatayo yatasaidia kuifanya CV yako iwe bora na hivyo, kukusaidia kupata interview za kazi.

👉Soma na kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri anatafuta mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza hiyo kazi au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na kufanya maombi yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.

Kwa mfano, kama kazi inaweka umuhimu kwenye ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii kwa matangazo, hakikisha CV yako ina kazi zote zilizohitaji matumizi ya mitandao ya kijamii.

👉Andika maneno muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi, uyatumie kwenye CV
Usichukue sentensi nzima kutoka kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia lugha na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.

👉Fanya utafiti juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo ya kazi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au wapo kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi wanayohusika nayo. 

Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa kampuni hiyo. Hii itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii itakusaidia kuweka maombi yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.

👉Orodhesha ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote ulizozifanya maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo kusaidia kufanya kazi unayoomba.

==>Format/Staili inayotumika zaidi kwenye kuandika CV:
   1. Lengo la CV na ujuzi wako
    2.Ujuzi wako wa kazi
   3. Mafanikio maalum
   4. Elimu
   5. Ujuzi muhimu binafsi

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Angalizo:
  1.  Tumia maandishi ya kawaida ya Times New Roman
  2.  Tumia size 9 – 12 ya herufi
  3.   Hakikisha unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
  4.   CV isiwe zaidi ya ukursasa 2
  5.   Usitumie sentensi ndefu
  6.  Hakikisha CV yako inasomeka kiurahisi na inawasilisha   mafanikio yako kwa uwazi.
  7.  Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya hivi karibuni alafu rudi nyuma.
   ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 
   ==>.Hakikisha Yafuatayo:
1.Ukiwa unaandika jina la kampuni uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. 
2.Eleza kwa ufupi kampuni yao inahusika na nini. 
3.Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na mwaka).  
4.Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu yako kwenye hiyo kampuni.
5.Usidanganye

👉Maandalizi ya Mwisho

1.Pitia kila kitu kwa mara ya mwisho
 -Print CV yako alafu ipitie. Hii huwa inasaidia kuona makosa yako.

2.Mpe Rafiki  yako apitie CV
-Muombe rafiki yako apitie CV yako. Macho manne ni bora zaidi ya mawili!

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Hatua ya kwanza kwenye kupata kazi unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba maelezo yaliyoelezwa humu yatakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kuandika CV nzuri, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini.

AU 



Share:

MKUNGA AKATA KICHWA CHA MTOTO MCHANGA MAMA MJAMZITO AKIJIFUNGUA

Mkunga akimbeba mtoto mchanga nchini Zimbabwe

Maafisa wa polisi nchini Uganda wanachunguza kisa kimoja ambapo mkunga mmoja aliripotiwa kumuhudumia visivyo mama mjamzito aliyekuwa katika uchungu wa kujifungua ambapo kichwa cha mwanawe kilikatika.

Inadaiwa kwamba muuguzi huyo alimvuta mtoto huyo kwa kutumia nguvu nyingi mtoto huyo ambaye tayari alikuwa amefariki na kuishia akibeba kiwiliwili chake wakati mama huyo alipokuwa akijifungua.

Wakati mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 21 alipoingia katika chumba cha kujifungua , familia yake inasema kwamba alisubiri kwa muda mrefu kabla ya kuhudumiwa.

Kwa siku nne mfululizo alikuwa amelazwa katika Kituo cha Afya cha Bulumbi 111 akisubiri wakati mwafaka wa kujifungua mwanawe.

Kulingana na gazeti la Daily Monitor , wakati mmoja familia yake iliwasilisha ombi la kuitaka hospitali hiyo kumhamisha hadi katika kituo cha msalaba mwekundu iwapo hospitali hiyo ilikuwa imeshindwa kumsaidia ajifungue.

Kulingana na gazeti hilo babake mtoto huyo alisema: Tulienda hospitalini siku ya Alhamisi, iwapo walikuwa wameona tatizo lolote wangekuwa wangetuhamishia kwenye kituo cha msalaba mwekundu , lakini wakalazimika kutumia nguvu.

Wakati mkunga huyo alipokuwa akimhudumia muda wa saa sita mchana , miguu ya mtoto ilikuwa ya kwanza kutoka lakini mtoto akakwama kuanzia mabegani kwenda juu.

Inasemekana kwamba Mkunga aliyekuwa anamsaidia mama huyo kujifungua alimvuta mtoto huyo na baadaye kwenda kuketi chini. Baadaye alirudi akamvuta mtoto na kuanza kumgeuza geuza. Muuguzi huyo hatahivyo anadaiwa kuomba usaidizi kutoka kwa muuguzi mwenzake.

Muuguzi huyo alimvuta mtoto huyo huku akimgeuzageuza na baadaye mtoto akatoka lakini bila kichwa.

Babake mtoto huyo alisema: Wakati mtoto alipotoka , muuguzi aliendelea kumvuta mtoto na kumrudisha ndani . Mtoto alikufa kifo kibaya .Serikali inahitaji kuwafunza hawa watu.

Bi Musazi anasema kwamba mwanawe alikuwa mzima kutokana na ushahidi wa miguu yake iliokuwa ikicheza.

Kisa hicho kimezua hisia kali nchini Uganda huku wakaazi wakitoa wito kwa serikali kuwafunza wakunga jinsi ya kusaidia katika kujifungua.

Bwana Ibrahim Okelo ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho alisema: Tunaitaka serikali kuwabadilisha wakunga hao na msimamizi wa hospitali,

Mwili wa mtoto huyo ulipelekwa kituo cha Afya cha Busia kwa uchunguzi kabla ya kupelekwa nyumbani kwa mazishi.

Maafisa wa polisi wamesema kwamba wanachunguza kesi hiyo wanayodai kuwa kisa cha uzembe dhidi ya mkunga huyo.

Wakaazi wanadai kwamba katika kipindi cha miezi mitatau , wanawake wawili na watoto wawili wamefariki wakati wa kujifungua katika kituo hicho.

Maafisa wa polisi wanadaiwa kuwa walipelekwa ili kuweka usalama katika kituo hicho cha Afya baada ya wakaazi kujaribu kukivamia kutokana na masuala hayohayo.

Jaribio la gazeti la Daily Monitor kuzungumza na msimamizi wa kituo hicho cha Bulumbi 111 pamoja na afisa wa afya wilayani hazikufua dafu kwa kuwa hawakushika simu zao.

Wale walioshika simu walisema kwamba hawajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.
CHANZO- BBC
Share:

MABINGWA WA KOMBE LA STANDARD CHARTERED, TIMU YA DAR ES SALAAM CORRIDOR, KUISHUHUDIA LIVERPOOL 'LIVE'

Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani(kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shindano la Kombe la Standard Chartered lililofanyika mwaka jana pamoja na kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered. Katikati ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke(kulia) akizungumza na waandhi wa habari kuhsu wanavyoshirikiana na Benki ya Standard Chartered hasa kwenye masuala ya mpira ili kudumisha urafiki uliopo kati ya nchi mbili ambazo ni Tanzania na Uingereza wakati wa kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered. wa tatu kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu TFF inavyoshirikiana bega kwa bega na Benki ya Standard Chartered ili kuinua vipaji vya wachezaji wachanga ili kuweza kufikia malengo yao wakati wa hafla ya kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani na kushoto ni Mwakilishi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, George Msonde.


Mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars)  Ally Mayai Tembele akitoa hamasa kwa Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor wanaosafiri leo kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani na katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani(kulia) akimkabidhi pasipoti na tiketi ya ndege mchezaji wa timu ya Dar es Salaam Corridor wakati wa hafla ya kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke(kulia) akimkabidhi pasipoti na tiketi ya ndege Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba(kushoto) wakati wa hafla ya kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia(kulia) akimkabidhi pasipoti na tiketi ya ndege Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Majuto Omary (kushoto) kwa ajili ya kuripoti mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) kati ya Liverpool na Bournemouth itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor wanaokwenda kuishuhudia  mtanange wa Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) itakayochezwa Ijumaa hii chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.

Na Mwandishi wetu Globu ya Jamii.
BENKI ya Standard Chartered wadhamini Mabingwa
wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwaajili
ya kwenda katika uwanja wa Anfiel uliopo nchini Uingereza kwaajili ya
kwenda kuangalia mchezo katika Uwanja huo.

akizungumza  na waandishi wa habari jiji ni Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa  Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani  amesema kuwa wachezaji hao wataenda kujifunza mamo mbalimbali.

Amesema
mbali na fursa mbalimbali watakazopata, Watanzania hao watashuhudia
laivu moja ya mechi za Ligi Kuu ya England kati ya Liverpool na FC
Bournemouth katika Uwanja wa Anfield nchini Uingereza.

"Mechi itachezwa Jumamosi kwenye uwanja wa Anfield," amesema na kuongeza.

"Pia
watapata fursa ya kukutana na nyota wa zamani na sasa wa klabu ya
Liverpool, bahati nzuri uwepo wa Samatta (Mbwana) kwenye ligi ya kule
imeifanya Tanzania kujulikana, hivyo mkatumie nafasi hii kutangaza na
vivutio vya Tanzania," amesema Rughani.

Kwa
Upande wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia
amewaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam
Corridor wanaoondoka jioni ya leo kwenda Uingereza kwa ziara ya siku
tatu kwenye klabu ya Liverpool.

Msafara
wa timu hiyo wenye watu tisa unaondoka nchini kwenda kuishuhudia
Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England
(EPL) chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.

Akizungumza
wakati wa hafla ya kuwaaga asubuhi hii, Karia amewataka Watanzania hao
kutumia vizuri fursa hiyo na kuwa mabalozi wa soka watakaporejea nchini.

"Nimeambiwa
katika ziara hiyo watajifunza mambo mbalimbali kuhusu klabu ya
Liverpool, uzoefu watakaoupata huko wakiutumia vema itakuwa chachu
katika soka letu watakaporejea nchini.

"Naamini
watajifunza miiko ya uwanja Anfield, mazingira ya klabu na nambo
mbalimbali ambayo yanaihusu klabu ya Liverpool na mashabiki wake na
watakaporejea itakuwa ni chachu kwao kuwapa elimu Watanzania wengine
kuhusu klabu hiyo kongwe," amesema Karia.




Share:

MAREKANI YAENDESHA MASHAMBULIZI YA ANGA DHIDI YA TALIBAN

Marekani imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa Taliban Jumatano  Machi 4, katika jimbo la Helmand, Kusini mwa Afghanistan, msemaji wa vikosi vya Marekani ametangaza.


Ni mashambulizi ya kwanza ya Marekani tangu Washington na Taliban kutia saini makubaliano ya kuondoka kwa vikosi vya nchi hiyo nchini Afhganistan siku ya Jumamosi wiki iliyopita.

Kanali Sonny Leggett, msemaji wa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan, amethibitisha mashamulizi hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter. 

Amesema wapiganaji wa Taliban "walishambulia kwa nguvu kizuizi cha barabara [cha vikosi vya usalama vya Afghanistan]. Mashambulizi tuliyotekeleza ni ya kujihami ili kukomesha shambulio hilo la taliban. "

Mkataba uliotiwa saini Jumamosi huko Doha, unaitaka Marekani kuondoa vikosi vyake ndani ya kipindi cha miezi 14 na serikali ya Kabul na Taliban kuanza mazungumzo.

Mashambulizi hayo ya kujihami ya Marekani yanajibu mashambulizi ya Taliban yaliyotokea usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano. Karibu askari 20 wa Afghanistan na polisi waliuawa.

-RFI


Share:

Tanzania Haina Upungufu Wa Dawa Za ARV

Na Englibert Kayombo WAMJW – Arusha
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema kuwa Tanzania haina upungufu wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV)

Dkt. Subi amesema kauli hiyo jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya walipofanya ziara ya pamoja kutembelea Gereza la Arusha (Kisongo)

“Hatuna upungufu wa dawa za ARV Tanzania na hatujawahi kuwa na upungufu wa dawa hizo zaidi miaka kumi iliyopita” amesema Dkt. Subi

Amesema kuwa upatikanaji wa dawa za ARV umekuwa ni wa uhakika na wagonjwa wote wanapata dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi.

“Ni kweli kuna baadhi ya dawa hasa za magonjwa nyemelezi, kuna muda kulikuwa na upungufu lakini hivi sasa tuna dawa za kutosha” amesema Dkt. Subi

Dkt. Subi ametolea mfano katika Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD), dawa ya “Ceptrin” kwa nchi nzima viko vidonge zaidi ya Milioni 62, ambapo kwa kanda ya Kaskazini wakiwa na vidonge Milioni 8.6 huku dawa za watoto zikiwa ni 786,000.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Suleiman Mzee amesema kuwa Jeshi la magereza ni moja ya wahanga wa ugonjwa wa VVU/Ukimwi, na hawapo nyuma katika kupambana na ugonjwa huo kwa wafungwa, mahabusu, watumishi na familia zao.

Kamishna Mzee amesema kuwa Jeshi la magereza linatoa huduma za uchunguzi wa afya, tiba, ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi pamoja na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

“Jeshi la Magereza lina jukumu la kuhakikisha wafungwa na mahabusu wanapata huduma bora za afya kama ilivyo kwenye jamii nyingine” amesema Kamishna Suleiman Mzee.


Share:

Rais Magufuli Ateua Katibu Mkuu Mpya Wizara ya Kilimo




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi March 5



















Share:

Wednesday, 4 March 2020

Breaking news : NYUMBA ZAIDI YA 20 ZAEZULIWA NA UPEPO MKALI KIMARA GOLANI


Na Andrew Chale, Dar es salaam

UPEPO mkali na mvua iliyoandamana na radi imesababisha nyumba zaidi ya 20 kuezuliwa mapaa huku Kaya 50 zikikosa makazi.


Tukio hilo la aina yake limetokea masaa mawili yaliyopita ambapo katika eneo la Kimara Golani kwa 'Bibi Rosta'  mwandishi wa habari hizi ameshuhudia nyumba 19 zikiwa zimezuliwa paa za nyumba huku nyumba moja ikiwa imebomoka ukuta.

Katika tukio hilo nyumba mmoja iliyobomoka imeweza kujeruji mtu mmoja aliyekuwa ndani.

Mashuhuda:

"Tunashukuru mvua wakati inanyesha nyumba nyingi hazikuwa na watu ndani.

Athari ni kubwa hatuelewi tunaomba Serikali kama itaweza ije ifanye tathimini hata msaada kidogo." Alisema Saphia mkazi wa Golani.

Eneo lililoathirika kwa wingi ni eneo la kwa Bi. Rosta  kwa Mama Mzungu nyumba 7 huku upande wa Bi Rosta michungwani nyumba 8 na nyumba zingine eneo la Golab Kanisani pamoja na mapaa ya shule ya Msingi Saranga.

Hali ya muda bado ni ya mvua huku radi zikipiga na upepo watu wengi wakiwa watoweka barabarani kuwahi nyumba zao.
Share:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka wenyeviti wa vijiji kuacha biashara ya ardhi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameonya tabia ya baadhi ya wenyeviti wa vijiji wanaofanya biashara ya ardhi waache na badala yake amewataka wajihusishe katika kutekeleza majukumu yao ya msingi.

Ameyasema leo(Jumatano, Machi 4, 2020) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Bokwa wilayani Kilindi akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.

Waziri Mkuu amesema tabia ya baadhi ya wenyeviti wa vijiji kujihusisha na biashara ya uuzaji wa ardhi inachangia kuwepo kwa migogoro, hivyo amewataka wasijihusishe na masuala hayo.

“…Wanaouza ardhi za vijiji bila ya kuwa na vibali vya halmashauri wachukuliwe hatua kwa sababu ndio wanaosababisha migogoro ya ardhi. Viongozi acheni tabia ya kuwaingiza wananchi kwenye migogoro.”

Pia, Waziri Mkuu ameonya tabia ya wafugaji kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.“Haikubaliki na haiingii akilini katika hali ya kawaida mtu amelima shamba lale la chakula alafu mwingine anaenda kuingiza mifugo haikubaliki.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “kama unadhani mahindi ndio chakula bora cha ng’ombe wako lima ulishe mifugo. Hakuna Mtanzania aliyeko juu ya sheria kama kuna mtu ameua kwa kulinda ng’ombe wake, Mkuu wa Wilaya fanya uchunguzi wa jambo hilo na hatua zichukuliwe.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliodai kuwa kuna mkulima ameuawa na mfugaji kutokana na mgogoro uliotokea wakati mfugaji alipoingiza mifugo kwenye shamba la mkulima.

Akizungumzia kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya Kilindi (Tanga) na Kiteto (Manyara) amesema suala hilo iachiwe Serikali kwani tayari imeshaanza kulishughulikia.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema wilaya ya Kilindi itajengewa hospitali ya wilaya ili kuwapunguzia wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Pia, Waziri Mkuu aliwataka wananchi waendelee kuiamini Serikali yao na kwamba changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za upatikanaji wa huduma za maji, umeme na miundombinu ya barabara zitafanyiwa kazi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezindua mradi wa maji wa Bokwa na amesema kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo na wilaya ya Kilindi.

Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao. 

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mswelo kilichopo kwenye kata ya Kwediboma, ambapo amesema awali Serikali ilitoa sh. milioni 300 kwa ajili ya ujenzi huo na itaongeza sh. milioni 200 ili kituo hicho kikamilike.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Tumia Mwika Kujitibu Busha, Nguvu za Kiume

Mwika ni dawa  ya asili ya nguvu za kiume yenye kutibu matatizo kwa wakati mmoja ;

(1)Nguvu za kiume
(2) Kunenepesha Maumbile
(3)Kuchelewe kufika kileleni

Yajuwe matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

(1) Ngiri ya kupanda na kushuka
2.Korondani moja kuvimba
3.Tumbo kuunguruma kujaa gesi
4.Kisukari
5.Presha
6.Kiuno kuuma
7.Kutopata choo vizuri 

Pia tunatibu kisukari siku (14) vidonda vya tumbo siku (30), Miguu kufa ngazi, kuwaka moto .

Pia tunayo dawa ya mvuto wa mpenzi hata yupo mbali amekuacha atarudi na kutimiza ahadi zote mvuto wa biashara.

Wasiliana nasi kwa namba 0747100745 (Whatsap/ Kupiga kawaida)


Share:

Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu Atoa Masaa 5 Kwa Halmashauri Zote Kutenga Sehemu Maalumu Za Kuweka Washukiwa Wa Virus Vya Corona

Waziri Ummy Mwalimu ametoa masaa 5 kwa kila Halmashauri kutenga sehemu maalum kwaajili ya kumuweka mshukiwa wa ugonjwa wa Corona na kufanya utaratibu wa uchunguzi na kutoa taarifa haraka Wizara ya Afya.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo kwa viongozi wa dini nchini jinsi ya kuepuka maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinazidi kusambaa katika nchi mbalimbali duniani. 

“Ninatoa muda mpaka saa 10 jioni vituo vyote vya afya vya umma nchini viwe vimetenga sehemu maalum ya kuweka mshukiwa wa Virusi vya Corona na kuripoti haraka iwezekanavyo katika Wizara ya Afya kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki”. Amesema Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema mpaka sasa nchi yetu ni salama, hakuna mshukiwa wa COVID19 lakini Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini ikiwa ni pamoja na kushirikisha taasisi mbalimbali za dini. 

“Tunawaomba viongozi wa dini muende mkatoe elimu kwa waumini wenu kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni za usafi na pia kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua ambaye ana historia ya kusafiri nje ya nchi”. Mhe. Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa taasisi za dini, taasisi za umma, maofisi na mashule ya Serikali na binafsi kuweka sehemu maalum ya kunawa mikono kwa maji yenye dawa ya kuua bakteria (hand sanitizers) ili kuepuka maambukizi yatokanayo na bakteria.


Share:

TFF Yapiga Marufuku Timu Kusalimiana Kwa Kushikana Mikono ili Kukabiliana na Tishio la Virusi Vya CORONA



Share:

WATU 7 WAFARIKI DUNIA BAADA YA LORI LA DANGOTE KUGONGANA NA NOAH


Watu saba wamefariki dunia papo hapo baada ya gari dogo aina ya Toyota Noah kugongana uso kwa uso na Lori la kampuni ya Dangote katika kijiji cha Mavuji, wilayani Kilwa mkoani Lindi.



Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Foka Dinya, amesema hadi sasa ni miili miwili ndiyo imeweza kutambuliwa kwa majina, kutokana na vitambulisho vilivyokutwa kwenye mifuko yao.



"Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa gari ndogo, na walikuwa ni wafanyabiashara wana mradi wao wa kutengeneza Furniture Luangwa, miili yote saba imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wawili vitambulisho vyao vilikutwa kwenye mifuko yao ya suruali ndio wameweza kufahamika, watano bado hawajafahamika" amesema Kamanda Dinya.

Ajali hiyo ilitokea jana Machi 3, 2020, majira ya 12:00 Alfajiri, katika Kijiji cha Mavuji, Wilaya ya Kilwa, ambapo gari ndogo aina ya Hiace iligongana uso kwa uso na Lori la Kampuni ya Dangote, baada ya dereva wa gari ndogo kushindwa kuimudu vizuri gari yake wakati anakwepa shimo.

Waliotambulika ni dereva Jerome Goefrey Kileo pamoja na Christopher Kitigo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger