Thursday, 27 February 2020

Picha : RC TELACK AFUNGUA MKUTANO WA TATHMINI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI,LISHE NA CHF ILIYOBORESHWA...ATAKA JITIHADA ZAIDI KUTOKOMEZA VIFO VYA UZAZI NA WATOTO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi, Lishe na CHF iliyoboreshwa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameziagiza halmashauri zote za wilaya mkoa wa Shinyanga na wadau wa afya kuongeza jitihada,mikakati na raslimali ili kutokomeza vifo vya uzazi na vifo vya watoto wachanga.

Telack ametoa agizo hilo leo Alhamis Februari 27,2020 wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi, Lishe na CHF iliyoboreshwa uliokutanisha wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Mkuu huyo wa mkoa alisema Takwimu zinaonesha kuwa kimkoa vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua na kufikia vifo 50 kutoka vifo 56 mwaka 2018 na vifo 73 mwaka 2017 hivyo kuzipongeza Halmashauri,hospitali na vituo vya vinavyotoa huduma za dharura za upasuaji kwa kuchangia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Alisema pamoja na takwimu za vifo vitokanavyo na uzazi kuonesha kupungua,bado kuna changamoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambayo vifo viliongezeka kutoka vifo 5 mwaka 2018 hadi vifo 14 mwaka 2019.

“Hali hii inasikitisha,mara kwa mara nimekuwa naagiza kwamba viongozi na watendaji msimamie masuala ya uzazi. Katika mkoa huu sitaki kuona mama au mtoto mchanga anafariki wakati wa uzazi. Nawaagiza Halmashauri na na kuwaomba wadau wa afya tuongeze jitihada,mikakati na rasilimali ili kutokomeza vifo vya uzazi na watoto wachanga”,alisema Telack.

Katika hatua nyingine Telack alisema mkoa wa Shinyanga bado unakabiliwa na tatizo la lishe kwa watoto walio chini ya miaka mitano na akina mama walio kwenye umri wa kuzaa na kusisitiza kuwa kila mmoja anatakiwa kuwajibika kukabiliana na changamoto hiyo.

“Tatizo la upungufu wa damu kwa akina mama wenye umri wa kuzaa limepungua kutoka asilimia 59.4 mwaka 2015/2016 hadi asilimia 30.4 mwaka 2019. Kwa watoto walio chini ya miaka mitano udumavu umeongezeka kutoka asilimia 30% hadi asilimia 32.1%,ukondefu kutoka asilimia 2.4% hadi 4.3% wakati uzito pungufu kwa watoto umepungua kutoka 22% hadi 15%”,alieleza Telack.

Aidha alisema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikichukua hatua za kukabiliana na utapiamlo mkoani Shinyanga ikiwemo kusaini mkataba wa utendaji wa masuala ya lishe kati ya mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri,watendaji wa kata na vijiji ili kufuatilia viashiria vya lishe.

“Hatua hii imesaidia kuinua baadhi ya viashiria vilivyomo kwenye mkataba kwa mfano,akina mama wenye watoto wenye umri wa miezi 0 hadi miezi 23 wanapata elimu ya unasihi,watoto wanaendelea kupata matone ya Vitamin A, na matibabu ya utapiamlo yanaendelea kutolewa wenye vituo vya afya”,aliongeza Telack.

“Natoa wito kwa wadau wote wa afya ndani ya mkoa wetu kuendelea kushirikiana na serikali kutekeleza mipango mbalimbali iliyopo ili kuinua viashiria vyote vya lishe. Narudia tena kuziagiza halmashauri zote katika kipindi hiki cha maandalizi ya Mipango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 zitenge shilingi 1,000 kwa kila mtoto aliye chini ya miaka mitano kwenye mapato ya ndani”,alisema.

Telack aliziagiza halmashauri kuweka mikakati ya kuongeza kiwango cha uandikishaji wa kaya katika Mfuko wa Afya ya Jamii ‘CHF iliyoboreshwa’ ili wananchi wafurahie huduma za kiafya kupitia CHF.

“Nawashukuru wadau wote kwa michango na misaada yenu mnayotoa katika kuboresha huduma za afya na lishe. Naomba muendelee kushirikiana na mkoa wetu ili tuweze kukabiliana na changamoto zinazotukabili katika utekelezaji wa afua za afya. Kila mmoja wetu ana wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na lishe”,alisema Telack.

Mkutano uliolenga kutathmini huduma za afya ya uzazi na mtoto,afua za lishe na uandikishaji wa kaya katika Mfumo wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa (CHF iliyoboreshwa) umeenda sanjari na utoaji wa ngao na vyeti kwa halmashauri, hospitali na wadau waliochangia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi,kutekeleza mkataba wa lishe na kuinua kiwango cha kaya zilizoandikishwa kwenye CHF iliyoboreshwa.

Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Nuru Mpuya alizitaja halmashauri zilizopata ngao za Ushindi kutokana na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kuwa ni Kahama Mji,Kishapu na Ushetu.

“Halmashauri zilizopata ngao ya ushindi kutokana na kutekeleza vizuri mkataba wa lishe ni Ushetu,Kishapu na halmashauri ya Shinyanga. Kwa upande wa halmashauri zilizopata vyeti kwa ajili ya kutambua mchango wao katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ni Kahama Mji,Kishapu,Msalala,Shinyanga na Ushetu”,alifafanua Dkt. Mpuya.

“Halmashauri zilizopata vyeti kwa ajili ya kutambua mchango wao katika kuinua kiwango cha kaya kujiunga na CHF iliyoboreshwa ni Kahama Mji,Manispaa ya Shinyanga na Kishapu. Hospitali zilizopata vyeti kwa ajili ya kutambua mchango wao katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ni Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga,Hospitali ya wilaya ya Kahama,Hospitali ya Jakaya Kikwete Kishapu,Hospitali ya Mwadui na Kolandoto”,alisema.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi, Lishe na CHF iliyoboreshwa uliokutanisha wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga leo Alhamis Februari 27,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi, Lishe na CHF iliyoboreshwa uliokutanisha wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi, Lishe na CHF iliyoboreshwa uliokutanisha wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga.
Wadau wa afya wakiwa ukumbini.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi, Lishe na CHF iliyoboreshwa uliokutanisha wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga.
Afisa Lishe Mkoa wa Shinyanga, Dennis Madeleke akiwasilisha mada kuhusu hali ya Lishe mkoani Shinyanga.
Afisa Lishe Mkoa wa Shinyanga, Dennis Madeleke akiwasilisha mada kuhusu hali ya Lishe mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Deborah Magiligimba akichangia hoja kwenye Mkutano wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi, Lishe na CHF iliyoboreshwa.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama, Julius Chagama akichangia hoja ukumbini. Chagama alilalamikia kitendo cha wauza maziwa kuchanganya maji kwenye maziwa hali inayohatarisha afya za watumiaji.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Wadau wa afya wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wa pili kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Nuru Mpuya akizungumza wakati wa zoezi la utoaji wa ngao na vyeti kwa halmashauri, hospitali na wadau waliochangia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi,kutekeleza mkataba wa lishe na kuinua kiwango cha kaya zilizoandikishwa kwenye CHF iliyoboreshwa.
Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali wakati wa zoezi la kukabidhi ngao na vyeti kwa waliofanya vizuri na vinyago kwa waliofanya vibaya.
Zoezi la kukabidhi vyeti likiendelea


Share:

Mkurugenzi Wa Kampuni Inayojenga Reli Ya Kisasa Ahukumiwa Kulipa Faini Ya Dola Milioni 100 Ama Kifungo Cha Miaka Mitatu

Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet ((54) raia wa Uturuki amehukumiwa kulipa faini ya USD milioni 100 ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kukiri shtaka la kushindwa kutoa tamko la fedha USD 84,850 alizokutwa akizisafirisha.

Aidha mahakama imeamuru kutaifishwa kwa fedha hizo zote kuwa mali ya serikali.

Mehmet ambaye nchini Tanzania anaishi Ilala jijini Dar es salaam amesomewa hukumu yake na Hakimu Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kufikishwa mahakamani leo Februari 27 ma kusomewa shtaka moja la kushindwa kuzitolea taarifa fedha alizokutwa kusafiri nazo.

Mapema akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mkuu Shadrack Kimaro amedai kuwa Februari 13, mwaka huu huko katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere terminal III jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa anaondoka nchini kwenda Instabul Uturuki alikutwa na USD 84,850 ambazo hakuwa amezitolea taarifa kwa Idara ya Forodha.

Mapema akisoma maelezo ya awali kabla ya kusomewa adhabu wakili Kimaro alidai mshtakiwa Mehmet ni raia wa Uturuki na ameajiliwa na kampuni ya Yapi Merkezi  ambayo inashughulika na ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge hapa nchini Tanzania.

Imedaiwa siku hiyo alikuwa akisafiri kuelekea Instabul Uturuki kwa kutumia ndege ya Turkish namba TK 0604 huku akiwa amebeba mabegi. Akiwa amefuata taratibu zote za uwanja wa ndege akiwa anaelekea kupanda ndege alikutwa na Ofisa wa usalama akiwa na kiasi hicho cha fedha ambazo hakuwa amezitolea taarifa.

Aidha imedaiwa fedha hizo zimehifadhiwa NMB banki kwenye kitendo cha intelejensia.

Mahakama pia imeamuru mshtakiwa kurudishiwa pasi yake ya kusafiria na tiketi yake ya ndege.


Share:

Wafanyabiashara 1,950 Wapatiwa Elimu Ya Kodi Mkoani Iringa

Na Veronica Kazimoto-Iringa
Jumla ya wafanyabiashara 1,950 wa Mkoa wa Iringa wamefikiwa na kupatiwa elimu ya kodi wakati wakampeni ya elimu kwa mlipakodi iliyofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 27 Februari,2020.

Kampeni hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kuwafikia na kuwaelimisha baadhi ya wafanyabiashara wa Wilaya za Kilolo, Manispaa ya Iringa na Mufindi.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha kampeni hiyo mkoani humo, Afisa Msimamizi wa Kodi Mwandamizi wa TRA Bi. Catherine Mwakilagala amesema kuwa, zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kuwaelimisha jumla ya walipakodi 1,950.

“Mamlaka ya Mapato Tanzania tumehitimisha kampeni ya elimu kwa mlipakodi katika mkoa huu wa Iringa na zoezi hili limekuwa na mafanikio makubwa kwa sababu tumeweza kuwafikia jumla ya walipakodi 1,950 ambao wote tumewapatia elimu ya kodi na wamepata nafasi ya kutoa maoni na changamoto zao ambazo tumezipokea na nyingine tumezipatia ufumbuzi,” alisema Bi. Mwakilagala.

Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoani humo Bw. Lamson Tulyanje ametoa wito kwa wafanyabiashara wote waliotembelewa na maafisa wa TRA kwenye maduka yao na wale waliopata elimu kupitia semina wakati wa kampeni hiyo, kutumia elimu walioipata kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati na hiari.

“Elimu ambayo wameipata wafanyabishara mbalimbali kwenye kampeni hii ya elimu kwa mlipakodi, ni vizuri waitumie katika kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati ili Serikali iweze kutimiza majukumu yake ya kuwapatia huduma mbalimbali wananchi,” alieleza Bw. Tulyanje.

Bw. Richard Kilawa ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi kutoka Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoani humo ambaye ameishukuru TRA kwa kumfikishia elimu ya kodi dukani kwake na ameahidi kuendelea kulipa kodi kwa hiari.

“Ninashukuru sana TRA kunitembelea dukani kwangu na elimu yao imenifundisha kulipa kodi kwa hiari. Hivyo, nitawashawishi wafanyabiashara wenzangu walipe kodi kwa hiari ili tujenge nchi yetu,” alisema Bw. Kilawa. 

Naye, mfanyabiashara wa mbao wa Halmashauri hiyo, Bi. Maura Ng’umbi amesema kuwa, kupitia elimu iliyotolewa na maafisa wa TRA wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi, imewasaidia kujua umuhimu wa kulipa kodi stahiki kwa manufaa ya Taifa.

Kampeni ya elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mkoani Iringa ni mwendelezo wa kampeni zilizofanyika katika Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam kwa lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara kuhusu masuala mbalimbali ya kikodi, kupokea maoni na mapendekezo yao pamoja na kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.

MWISHO.


Share:

VIFO VYA BARABARA VYAPUNGUA TANGA


Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga Solomon Mwangamilo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa usalama barabara kwa shule za msingi na sekondari Jijini Tanga        
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MWAKILISHI wa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahaman Shiloo ambaye ni Diwani wa Kata ya Mzingani na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Mazingira akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mkurugenzi wa Asasi inayojishughulisha na Usalama Barabara ya Amend Tom Bishop akizungumza wakati wa halfa hiyo


 MWAKILISHI wa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahaman Shiloo ambaye ni Diwani wa Kata ya Mzingani na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Mazingira wa pili kutoka kushoto akikata utepe wakati wa uzinduzi huo


 MWAKILISHI wa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahaman Shiloo ambaye ni Diwani wa Kata ya Mzingani na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Mazingira wa pili kutoka kushoto akikata utepe wakati wa uzinduzi huo

 MEZA Kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi huo
 SEHEMU ya wanafunzi wa shule za Msingi Chuma, Masiwani,Kana na Shule ya Sekondari Maawal
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji  kushoto akiwa na Mwakilishi wa Meya wa Jiji la Tanga Abdurahaman Shiloo akiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga Solomon Mwangamilo wakati wa uzinduzi wa mradi wa usalama barabara kwa shule za msingi na sekondari Jijini Tanga.
 Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo

Udhibiti wa makosa ya usalama barabara mkoani Tanga umesaidia kupunguza matukio ya ajali zilizohusisha watoto kutoka 41mwaka 2018 hadi kufikia ajali 9mwaka 2019.

Takwimu hizo zimetokewa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga Solomon Mwangamilo wakati wa uzinduzi wa mradi wa usalama barabara kwa shule za msingi na sekondari Jijini Tanga.

Alisema kuwa ukaguzi wa Mara kwamara ya vyombo vya moto pamoja na elimu ya usalama barabara ndio imeweza kusaidia kupunguza ajali hizo.

"Changamoto pekee iliyobaki kwa  Sasa ni watoto chini ya miaka 9  kupakiwa kwenye usafiri wa bodaboda zaidi ya watatu kwa ajili ya kupelekwa shule Jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao "alisema RTOMwangamilo.

Aidha alisema kuwa kupitia mradi huo anaamini utaweza kuja na suluhisho la kumaliza ajali za barabara kwa wanafunzi hususani katika shule ambazo zipo karibu na maeneo yabarabara kuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa asasi inayojishughulisha na usalama barabara  Amend Tom Bishop alisema kuwa mradi huo utasaidia kujenga vivuko katika maeneo ya shule pamoja na kutoa elimu ya matumizi ya barabara kwa wanafunzi.

"Tunajua kwamba maendeleo ya miji mikubwa duniani inakuja na changamoto ya ongezeko la ajali hivyo kupitia mradi huu tumekuja kusaidiana na serikali katika kuhakikisha ndoto ya mtoto wa kitanzania inatimia"alisema Bishop

Nae Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kuwa mradi kupunguza ajali ambazo walikuwa wanapata wakati wanapokwwnda shule na wanaporudi nyumbani.

"Sasa Kuna njia maalum ya kupitia waenda kwa miguu kwani awali vyombo vya moto na watembea kwa miguu walikuwa wanatumia kwa pamoja na hivyo kuweka hatari ya uwepo wa ajali"alisema Mayeji
Share:

Nzige Wavamia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC

Kundi la nzige wa jangwani limeingia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa wadudu hao hatari kuonekana katika taifa la Afrika ya Kati tangu mwaka 1944.

Shirika hilo la chakula FAO aidha limeonya juu ya kitisho kikubwa cha njaa katika mataifa ya Afrika Mashariki baada ya kuvamiwa na nzige hao.

Kenya, Somalia na Uganda zimekuwa zikipambana na wadudu hao, katika mripuko mbaya kabisa wa nzige ambao maeneo kadhaa ya ukanda huo yalishuhudia miaka 70 iliyopita. 

Umoja wa Mataifa umesema nzige hao wa jangwani pia wameonekana Djibout, Eritrea na katika siku za karibuni wamefika Sudan Kusini, taifa ambalo kwa takribani nusu ya idadi ya watu wake tayari wanakabiliwa na njaa baada ya miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa jana jioni na mkurugenzi mkuu wa FAO Qu Dongyu, mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Mark Lowcock na mkurugenzi mtendaji wa mpango wa chakula duniani, WFP, David Beasley, imefananisha kundi hilo la nzige kama janga la kiwango kilichozungumziwa katika bibilia na linalokumbushia hatari inayoukabili ukanda huo.

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric, akiwa mjini New York hapo jana amezungumza mwito wa ufadhili uliotolewa na FAO  wa dola milioni 76 wa kupambana na wadudu hao, ambao hata hivyo unatekelezwa kwa kasi ndogo.

"Maafisa wameomba msaada huo wakati nzige walipoendelea kuvamia kote mashariki mwa Afrika. Gharama za kukabiliana nao zimeongezeka mara mbili hadi dola milioni 138. Mpango wa chakula umeonya gharama za kupambana na athari za nzige kwenye usalama wa chakula tu, zinaweza kuwa mara 15 zaidi ya gharama ya kuwazuia kusambaa. Hadi sasa ni dola milioni 33 tu zimetolewa au kuahidiwa."amesema Dujarric.

FAO imesema nzige waliozeeka , wanaoletwa kwa sehemu na upepo, waliwasili katika pwani magharibi mwa ziwa Albert,  karibu na mji wa Bunia mashariki mwa Congo siku ya Ijumaa. Taifa hilo halijawahi kushuhudia nzige kwa miaka 75.


Share:

Program Director at Care

Vacancy title: Program Director Jobs at: CARE International – Tanzania Deadline of this Job: 05th March, 2020 Overview OB SUMMARY The Program Director (PD) is senior leadership position responsible for ensuring that CARE’s programs in Tanzania contribute to CARE’s vision, CARE Tanzania’s Wezesha strategy and Multiplying Impact Framework. The PD is expected to provide strategic leadership in the… Read More »

The post Program Director at Care appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mahakama yaruhusu Rugemarila kuleta hoja za kutaka aachiwe huru

Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imekubali kupokea hoja za maombi ya mfanyabiashara James Rugemalira anayetaka kuondolewa kwenye kesi ya utakatishaji fedha wa Sh. Bil 309.4.

Hatua hiyo inakuja wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili wa utetezi, John Chuma amedai kuwa mteja wake ameshawasilisha hoja za pingamizi la awali lakini hajapata majibu yoyote kutoka upande wa Jamuhuri.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai baadhi ya nyaraka amezipata leo mahakamani hapo na kuwa upande wa Jamhuri upo tayari kusikiliza hoja hizo kwa njia ya mdomo kama nyaraka hizo zimeshaingizwa kwenye kumbukumbu ya mahakama hata kwa wakati huo kama ratiba ingeruhusu.

Wankyo amedai mshtakiwa wa pili amekua anajiwasilisha mwenyewe huku akiwa na uwakilishi wa mawakili hivyo anapaswa kusema kama amewaacha ama wanaendelea.

Akijibu suala hilo, Rugemarila amedai kuwa amekua na wawakilishi hata zaidi ya thelasini lakini kuna hoja lazima aziwasilishe mwenyewe na kuwa hilo jambo walitakiwa kulalamika mawakili wake na sio yeye kwani sheria inamruhusu kujiwakilisha.

Baada ya hoja hizo, Hakimu Shaidi Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Machi 12, 2020 litakapokuja kwa ajili ya  kutajwa na upande wa jamuhuri kuwasilisha majibu.

Mbali na Rugemalira, washitakiwa wengine ni Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power (IPTL) na Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege.


Share:

Regional HIV Testing Services MDH

JOB ANNOUNCEMENT Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH); Nutrition; Non-Communicable Diseases of public health… Read More »

The post Regional HIV Testing Services MDH appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Saudi Arabia yazuia wageni kutembelea miji ya Makka, Madina Kwa Hofu Ya Virusi Vya Corona

Serikali ya Saudi Arabia imezuia wageni wote wanaoingia nchini humo kwa safari za kidini, ikiwemo wanaotembelea miji mitakatifu katika dini ya Kiislamu - Makka na Madina.

Mamilioni ya watu huingia Saudia mwaka mzima kufanya ibada ya Umra, na wengi zaidi huingia kwa pamoja kufanya ibada ya Hija.

Tofauti na Hija, Umra hufanyika katika kipindi chochote cha mwaka, na kwa sasa marufuku hiyo inawalenga mahujaji raia wa nchi za nje wanaoenda kuitekeleza.

Bado haijulikani kama ibada ya Hija, ambayo inategemewa kuanza mwishoni mwa mwezi Julai kama itaathirika na zuio hilo pamoja na kusambaa kwa virusi vya corona duniani.

Saudia pia imewapiga marufuku watu kutoka nchi zilizokumbwa na virusi hivyo kuingia nchini humo.

Mpaka sasa Saudia bado haina mtu ambaye amethibitika kuambukizwa virusi hivyo.

Makka, ndio mji ambao Mtume Muhammad alipozaliwa, na kuna msikiti mtakatifu zaidi. Madina ndipo alipofariki na kuzikwa.

Soma Hii: Nafasi za Kazi 92 TANESCO...Mwisho wa Kutuma Maombi ni March 1, 2020 
Wizara ya mambo ya nje ya Saudia inasema marufuku hiyo ni ya muda - lakini wizara hiyo haijataja lini marufuku hiyo itaondolewa.

Watalii ambao si wa kidini ambao wanatoka katika nchi ambazo virusi vya corona vimethibitisha kuingia pia watakataliwa kuingia Saudia.


Share:

Job vacancies at SUN FLAG (T) LTD,

SUN FLAG (T) LTD is versatile vertical integrated textile manufacturer and exporter with its facility located in Njiro, Arusha – Tanzania. It started its operations in 1965 without fail or close down and employing thousands of working force from all walks of life of working forces. 30 JOBS VACANCIES AT SUN FLAG (T) LTD  We are looking… Read More »

The post Job vacancies at SUN FLAG (T) LTD, appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jobs Vacancies at Right To Play

Right To Play is recruiting exciting positions below to support implementation of education program in Kibondo Kigoma:Position – Project Officer Closing Date: – March 7th 2020 Work location: – Kibondo- Kigoma Authorized to Work in – Tanzania (for Tanzanian national only) Employment Start Date: – Immediately Contract Duration: – 1 year with possibility of Extension based on funding… Read More »

The post Jobs Vacancies at Right To Play appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Procurement Specialist/Buyer Coca-Cola Kwanza

PROCUREMENT SPECIALIST/BUYER Reference Number CCB200226-16 Job Title Procurement Specialist/Buyer Function Procurement Company Coca-Cola Kwanza (Tanzania) Job Type Permanent Location – Country Tanzania Location – Province Not Applicable Location – Town / City Dar es Salaam Job Description Coca-Cola Kwanza Ltd has an exciting opportunity in Procurement Department. We are looking for a talented individual with relevant skills and… Read More »

The post Procurement Specialist/Buyer Coca-Cola Kwanza appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sugu Afunguka Baada Ya Madiwani Wake 11 Wa CHADEMA Jijini Mbeya Kutimkia CCM

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amemtumia salamu katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally akibainisha kuwa madiwani 11 wa Chadema katika Jiji la Mbeya kuhamia chama tawala hakuwezi kubadili mapenzi ya wananchi wa Mbeya kwa Chadema.

Jumatatu, Dk. Bashiru akiwa jijini Dodoma, aliwapokea madiwani hao 11 kutoka Chadema walioongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi, huku sababu kuu ya kutimkia kwao CCM ikidaiwa kuwa kuvutiwa na utendaji wa Rais John Magufuli.

Madiwani hao  na kata zao kwenye mabano ni Mwashilindi (Nzovwa), naibu Meya, Fanuel Kyanula (Sinde); Fabian Sanga (Ghana); Anyandwile Mwalwiba (Isanga);  Dickson Makilasa (Ilomba); Constantine Mwakyoma (Kalobe); Furaha Mwandalima (Ilomi); Anderson Ngao (Mwasanga); Ibrahim Mwampwani (Isyesye); Henry Mwangambaku (Forest) na Kigenda Kasebwa (Viti Maalumu).

Baada ya kuwapokea, Dk. Bashiru alisema mitambo aliyoweka ya majaribio kwenye mikoa jirani, imemfikia Mbunge wa Mbeya Mjini (Sugu), akifafanua zaidi kuwa:

Akizungumza jana kwenye mkutano wa viongozi waandamizi wa Chadema Kanda ya Nyasa uliofanyika jijini Mbeya jana, Sugu alidai kupigiwa simu na Dk. Bashiru baada ya madiwani hao kujiuzulu uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.

Sugu alidai madiwani wote walioondoka Chadema, walikuwa wamekata tamaa ya maisha ya siasa.

“Juzi alinipigia simu Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali, akitaka kujua hali yangu na nilichomjibu nilimwambia 'wewe ni rafiki na mtani wangu, lakini kwa sasa umekuwa ndugu kwa sababu umeniimarisha kisiasa kuliko wakati wowote,’ nilimwambia hivyo kwa sababu ametuondolea mizigo,” alisema.

Sugu alisema kuhama kwa madiwani hao 11 akiwamo Meya, Mwashilindi na Naibu Meya, Fanuel Kyanula, hakujakidhoofisha chama hicho, bali kumekiimarisha zaidi.

Alisema awali baada ya kupata taarifa ya madiwani hao kutimka, alipata wasiwasi kwamba chama hicho kitakuwa kimepoteza mwelekeo, lakini alipofanya utafiti mdogo kwenye baadhi ya maeneo, alibaini bado kinakubalika kwa wananchi.

Alisema hofu yake ilikuwa huenda madiwani hao walihama pamoja na wanachama, lakini utafiti wake ulibaini wameondoka peke yao na familia zao na sio wanachama wa Chadema ambao ndiyo wapigakura wake.

“Suala la ubunge na kura za urais Mbeya tulikwisha kulimaliza tangu mwaka 2010, wakiwa hawaamini basi wasubiri wataona,” Alisema.

Alidai Meya wa Jiji la Mbeya, Mch. Mwashilindi, alikuwa hashiriki kwenye shughuli za chama hicho kwa muda mrefu, akieleza kuwa hata mkutano mkuu wa Chadema uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana jijini Dar es Salaam hakuhudhuria.

Mbunge huyo alidai Chadema ina mtaji wa wapigakura zaidi ya 250,000 ndani ya jiji hilo, akibainisha kuwa 200,000 ni wanachama wa chama hicho na wengine zaidi ya 50,000 ni wanachama wa CCM na vyama vingine.

Alisema kupitia kampeni yao ya Chadema ni Msingi, chama hicho kimeandikisha wanachama zaidi ya 60,000 na kwamba mpaka kufikia Juni mwaka huu, kitakuwa kimeandikisha wengine 100,000 na mpaka kufikia tarehe ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu, kitakuwa na uhakika wa wanachama 200,000.

Kuhusu picha ambayo imekuwa ikizunguka mitandaoni ikimwonyesha yeye na baadhi ya vijana wa CCM, Sugu alisema ni ya mwaka 2017 wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ambayo vijana hao walimwomba apige nao picha.

“Wale vijana baada ya kuniona mimi mbunge wao, waliniomba tupige picha, mimi nisingeweza kukataa kwa sababu najua wale ni wanachama wa CCM mashati, lakini mioyoni mwao ni wapigakura wangu japokuwa ile picha imeanza kutumika vibaya,” alisema.


Share:

Senior Specialist; Card Governance & Compliance at NMB

Senior Specialist; Card Governance & Compliance Job Purpose To provide the overall Card governance, controls, fraud prevention and compliance process; Derive as much value from Card Business by preventing Fraud and creating frictionless payment experiences. Main Responsibilities • Provide leadership in collaboration with other senior managers and business partners to develop and implement strategies that effectively manage financial… Read More »

The post Senior Specialist; Card Governance & Compliance at NMB appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

IGP Sirro azungumzia kuhusu Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Pamoja na Kutengwa Eneo Kwa Ajili Ya Mazoezi

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini, Simon Sirro amemuagiza Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Kamishna Msaidizi wa Polisi, Paul Sanga ahakikishe anatenga eneo maalum jijini Dodoma litakalotumiwa na askari wa kikosi hicho kwa ajili ya mafunzo.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la polisi ambalo sasa linatumika kama Makao Makuu ya FFU.

Kwa upande wake Kamanda Sanga amemuhakikishia IGP Sirro kuwa watatekeleza maelekezo aliyowapatia.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger