Saturday, 15 February 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi February 15


















Share:

Friday, 14 February 2020

Regional Finance and Grants Officer at FHI 360

Regional Finance and Grants Officer  Dodoma FHI 360 is a nonprofit human development organization dedicated to improving lives in lasting ways by advancing integrated, locally driven solutions. Our staff include experts in Health, Education, Nutrition, Environment, Economic Development, Civil Society, Gender, Youth, Research and Technology; creating a unique mix of capabilities to address today’s interrelated development challenges. FHI… Read More »

The post Regional Finance and Grants Officer at FHI 360 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Finance and Grants Officer at FHI 360

Finance and Grants Officer Shinyanga FHI 360 is a nonprofit human development organization dedicated to improving lives in lasting ways by advancing integrated, locally driven solutions. Our staff include experts in Health, Education, Nutrition, Environment, Economic Development, Civil Society, Gender, Youth, Research and Technology; creating a unique mix of capabilities to address today’s interrelated development challenges. FHI 360… Read More »

The post Finance and Grants Officer at FHI 360 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Picha : WANAFUNZI 700 WA SHULE YA SEKONDARI SHINYANGA 'SHY BUSH' WAANDAMANA ZAIDI YA MASAA MANNE KWENDA KWA MKUU WA MKOA

Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Wanafunzi zaidi ya 700 wa shule ya Sekondari Shinyanga maarufu 'ShyBush'  wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wameandamana hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, umbali wa zaidi ya kilomita 30 kufikisha kilio chao wakidai kunyanyaswa na mkuu wao wa shule na mwalimu wa nidhamu.

Wanafunzi hao wameanza kuandamana leo Ijumaa Februari 14,2020 kuanzia majira ya 11 alfajiri hadi saa nne tatu asubuhi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack huku wakiamini kuwa yeye ndiye anayeweza kutatua tatizo lao kutokana na kuvumilia kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi wa kusikilizwa.

Kaka mkuu wa shule hiyo Mwendesha Manyangu akizungumza kwa niaba ya wanafunzi amesema malalamiko mengi ya wanafunzi ya kudai kutotendewa haki na mkuu wao wa shule Malambi Malelemba pamoja na baadhi ya walimu akiwemo wa nidhamu yameshindwa kupatiwa ufumbuzi ndiyo maana wameamuwa kwenda kwa mkuu wa mkoa ili kupata ufumbuzi.

Kiongozi huyo wa wanafunzi alisema wanafunzi wanashindwa kujua simu wanazokamatwa nazo zinakwenda wapi kwani hawazioni zikichomwa moto licha ya kujua kuwa hairuhusiwi kuwa na simu pamoja na kupewa adhabu kwa makosa ambayo wangeweza kuonywa na baada ya kubaini hayo walikubaliana kwenda kwa mkuu wa mkoa kufikisha kilio chao.

“ Tunaamini mkuu wa mkoa atatusikiliza  na kutatua matatizo yaliyopo na hapa tatizo ni mkuu wetu wa shule tunapomueleza matatizo yaliyopo hayapatii ufumbuzi hata idara ya nidhamu nao hawachukui hatua sasa mwanafunzi anaambiwa anyowe kipara wakati haitakiwi anapewa adhabu”,alisema Manyangu.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amewasihi wanafunzi hao kuacha kujiingiza kwenye migomo isiyo ya maana ambayo inawapotezea muda wa masomo yao,huku akiwataka kuzingatia maadili na kujiepusha na vitendo ambavyo vitarudisha nyuma maendeleo ya taaluma yao na kushindwa kufikia ndoto zao.

Aliwataka wanafunzi kuwa watulivu kwani suala lao analifanyia kazi ili kuhakikisha changamoto zilizopo zinatatuliwa,huku akiiagiza idara ya elimu halmashauri ya Kishapu kuhakikisha wanafika shuleni hapo na kutatua changamoto za wanafunzi ikiwa ni pamoja kufuatilia maendeleo yao .


Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Joseph Paul aliwataka wanafunzi kuachana na makundi ambayo hayawajengi kuanzisha migomo isiyo na maana na kuwaeleza kuwa anawashukuru kwa kuwa hawakufanya fujo na kuharibu mali za shule.
Maandamano ya Wanafunzi wakiingia kwenye geti la kuingia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo



Wanafunzi wakiwa wamekaa chini wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
Wanafunzi wakipanda kwenye gari la polisi kwa ajili ya kurudishwa shuleni kwao.
Wanafunzi wakipanda kwenye gari la polisi kwa ajili ya kurudishwa shuleni kwao.
Wanafunzi wakiwa katika eneo la Ibadakuli barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Wanafunzi wakiwa katika eneo la Ibadakuli barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Wanafunzi wakiwa katika  barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga


Wanafunzi wakiwa katika  barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Share:

Mganga wa Kienyeji Aliyesababisha Wanawake 29 Wabakwe na Kuuawa Atiwa Mbaroni

Mganga wa kienyeji anayedaiwa kusababisha wanawake 29 kubakwa na kisha kuuawa baada ya kutoa masharti ya dawa kwa mtu aliyekua akitaka utajiri, amekamatwa na Polisi waliofanya oparesheni ya siku 11 maeneo ya Kanda ya Ziwa.

Mbali na mganga huyo, pia Polisi wanaishikilia fimbo ya mganga mmoja wa kienyeji iliyotumika kuwaaminisha wakata mapanga walioua askari wawili wa kituo cha polisi Nguruka mkoa wa Kigoma, askari mmoja wa Suma JKT na mgambo wa Mkoa wa Tabora, kisha kutolewa sehemu zao za siri kwa ajili ya dawa.

Akizungumza na waandishi wa habari  wakati akitoa tathmini ya opareshini maalumu ya kudhibiti matukio ya mauaji ya kupiga ramli chonganishi na makosa mengine kwa mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga, Mkuu wa operesheni maalumu wa jeshi la Polisi, Mihayo Nsekela leo Ijumaa Februari 14, 2020,  amesema inadaiwa fimbo hiyo ilitumika kuwakinga wakata mapanga na nguvu ya sheria pindi wanapokwenda kwenye matukio ya kihalifu ili wasikamatwe.

Katika operesheni , wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa mauaji hayo ambao wapo wakata mapanga 44, watuhumiwa wa ramli chonganishi 75, kufanya uganga bila kibali, unyang’anyi wa kutumia silaha, kupatikana na nyara za Serikali, wizi wa mifugo na watuhumiwa wa makosa mengine.


Share:

Makonda Agoma kuzungumzia kuzuiwa kuingia nchini Marekani

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amegoma  kuzungumzia kuzuiwa kuingia nchini Marekani kwa maelezo kuwa kuna siku atalizungumzia suala hilo.

Makonda ametoa majibu hayo leo Ijumaa Februari 14, 2020 wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds
 
Katika kipindi hicho ambacho Makonda alikuwa anazungumzia mambo mbalimbali  ya mkoa wa Dar es Salaam, aliulizwa kama tayari ameshapokea barua kutoka Marekani ya kumpiga marufuku kuingia nchini humo.

Akijibu sali hilo, Makonda amesema kuwa leo alifika katika kipindi hicho kuzungumzia masuala ya kiserikali si binafsi.

“Hapa nimekuja kama mkuu wa mkoa, subiri nikija binafsi tutajadiliana, nimekuja kama Serikali,” amesema

Tarehe 1, February  2020 Marekani ilieleza kumzuia Makonda kuingia Marekani pamoja na mkewe, Mary na kwamba sababu ni tuhuma za kushiriki kukandamiza haki za binadamu.


Share:

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aagiza Mkurugenzi Mwanga asilipwe mshahara kwa kushindwa kujibu swali

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Zefrin Lubuva asilipwe mshahara wa Februari hadi atakapojirekebisha.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mghwira kukasirishwa na kitendo cha mkurugenzi huyo kushindwa kujibu maswali aliyomuuliza .


"Mkurugenzi naomba kupata taarifa ya makusanyo yenu na kiasi mlichotoa kwa vikundi vya kina mama, vijana na watu wenye ulemavu, mmetoa kwa asilimia ngapi na kwa nini hamjafikia malengo kama Serikali ilivyoelekeza, “alihoji RC Mghwira.

Baada ya swali hilo, mkurugenzi alipewa kipaza sauti ili kujibu lakini alitaka ajibu mtaalamu mwingine jambo ambalo Mghwira alilipinga na kutaka ajibu mwenyewe.

Licha ya kutakiwa kujibu Lubuva alishindwa na kunyamaza kimya na kumfanya mkuu huyo wa Mkoa kumtaka mwenyekiti wa halmashauri hiyo kujibu.

Mwenyekiti wa Halmashauri,  Theresia Msuya amesema kutofikia malengo kumetokana na uzembe wa watendaji.

Baada ya maelezo hayo,  Mghwira  alimtaka tena Lubuva kusimama na kutoa majibu  kwa nini hawajafikia lengo la kutoa asilimia 10 kama Serikali inavyoelekeza lakini kwa mara ya pili alishindwa kujibu.

"Mkuu naomba radhi tugange yajayo" alijibu   Lubuva na kisha kuketi.

"Sasa wanaokulipa mshahara wasikulipe mwezi huu, tugange yajayo mpaka huo mwezi Machi,” amesema mkuu huyo wa Mkoa.

Sakata hilo limetokea leo Ijumaa Februari 14, katika kikao maalumu cha kamati ya ushauri ya mkoa cha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika leo.


Share:

Waziri Mkuu: Tusitumie Corona Kujipatia Umaarufu Wa Kisiasa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaasa wanasiasa nchini kutotumia mlipuko wa virusi vya corona uliotokea China na kuua watu zaidi ya 1,400 kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Hivyo, Waziri Mkuu amewataka Watanzania waendelee kuitegemea Serikali katika kupata taarifa za mara kwa mara kuhusu masuala mbalimbali zikiwemo na za mlipuko wa virusi hivyo. “Tusiupoteshe umma.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 14, 2020) mara baada ya kushiriki swala ya Ijumaa katika msikiti wa Gaddafi, jijini Dodoma. Amesisitiza umuhimu wa wananchi kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aliepushe na maafa mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema kazi inayofanywa na Serikali kwa sasa nchini ni kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama, ambapo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi waendelee kumuomba Mwenyezi Mungu aliepushe Taifa na maafa mbalimbali ikiwemo mlipuko wa corona, baa la nzige na mafuriko

Amesema katika mji wa Wuhan ambako virusi hivyo vilianzia, wapo vijana 497 wa Kitanzania huko na wote wapo salama na Serikali inaendelea kuwasiliana nao kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na ofisi za ubalozi.

“Taifa hili ni muhimu sana kwetu na ni msingi wa maisha yetu, hivyo watu wasiwe wanapotosha umma na kuwatia hofu Watanzania, vijana wetu wapo salama. Pia tumejipanga kukabiliana na majanga hayo ikiwa ni pamoja na nzige. Tumuombe sana Mwenyezi Mungu atuepushe”

Kadhalika,Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi wawasikilize viongozi wa dini na waendelee kumuomba Mwenyezi Mungu awape uvumilivu na waliombee Taifa lidumishe amani.

“Viongozi wa dini muendelee kuhamasisha uwepo wa amani nchini. Taifa linaendelea kuwa na amani kutokana na mawaidha yanayotolewa na viongozi mbalimbali wa dini.”

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Wanzania waendelee kushikamana na wafuate maelekezo yanayotolewa na viongozi wa dini ili waweze kujenga msingi imara kwa vijana.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

RAIS SHEIN AIMWAGIA SIFA BENKI YA CRDB...ATAKA WANANCHI WOTE WAFAIDIKE NA MATUNDA YA BENKI HIYO


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza haja kwa Benki ya CRDB kuendelea kutoa huduma zake kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wananchi wote wafaidike na matunda ya benki hiyo. 

Dk. Shein aliyasema hayo leo, Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB Abdulmajid Mussa Nsekela aliyefika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha akiwa amefuatana na uongozi wa Benkihiyo ulioongozwa na Mwenyekitiwa Bodi ya Wakurugenzi Ally Hussein Laay. 
Katika maelezo yake Rais Dk. Shein aliipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kutoa huduma zake hapa Zanzibar sambamba na mikakati na malengo yake iliyoyaweka katika kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Rais Dk. Shein alisisitiza haja kwa Benki hiyo kuongeza matawi yake hapa Zanzibar pamoja na kuipongeza azma yake ya kushirikiana na Serikali katika kuendeleza na kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo. 

Pia, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Benki hiyo kwa mipango waliyoipanga ya kuhakikisha Benki hiyo inaleta tija kwa nchi na wananchi wake huku akieleza matarajio yake makubwa katika uongozi wa Mkurugenzi huyo mpya wa Benki hiyo ya CRDB. 

Alisisitiza kuwa iwapo Benki hiyo itaendelea kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi Benki nyengine hapa nchini zitaweza kupanua wigo kutoka Benki hiyo hatua ambayo itapelekea kufuatwa ile dhana ya uzalendo kwani wananchi, Makampuni na hata Serikali wataitumia benki hiyo ikiwemo kukopa fedha badala ya kwenda kukopa kwenye benki za nje ya nchi. 

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza kuwa Benki ni taasisi ya kiuchumi hivyo, kuongezeka kwa benki hapa Zanzibar ambapo hivi sasa zipo Benki 13 kutaendelea kuongeza ushindani wa kibiashara sambamba na kukuza uchumi wa Zanzibar ambao umekuwa ukiimarika kila uchao. 

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alieleza uzoefu alionao wa Benki hiyo kutokana na shughuli zake inazozifanya kwa muda mrefu hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuunga mkono sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo kilimo, afya, viwanda, biashara, miundombinu ya barabara, wajasiriamali na mambo mengineyo. 

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein aliuhakikishia uongozi wa Benki hiyo ya CRDB kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Benki hiyo. 

Nae Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB Abdulmajid Mussa Nsekela alimueleza Rais Dk. Shein kuwa atahakikisha anatekeleza vyema majukumu yake ili benki hiyo iendelee kupata mafanikio zaidi. 

Alieleza jinsi Benki hiyo inavyofanya kazi zake hapa Zanzibar pamoja na Tanzania Bara na kueleza azma ya Benki ya CRDB ya kuunga mkono miradi mbali mbali ya maendeleo hapa Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Aliongeza kuwa Benki hiyo inayomilikiwa na Serikali imekwua ikipata mafanikio makubwa katika utoaji wake wa huduma hali ambayo ilitokana na hatua iliyochukuliwa ya kwenda kwa wananchi. 

Alieleza kuwa kwa upande wa Zanzibar Benki hiyo ina matawi mawili hapa Zanzibar ambapo tawi moja liko Unguja na jengine liko Pemba na ina wafanyakazi 42 hapa Zanzibar na wateja wapatao 30,062 ikiwa na Mawakala kwa ujumla 145 (128 kwa Unguja na 17 Pemba) sambamba na kutoa huduma za kifedha katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume. 

Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo alieleza azma ya Benki hiyo ya kufungua tawi lake jipya hapa Zanzibar huku akionesha maeneo ambayo Benki yake imedhamiria kushirikiana na Zanzibar yakiwemo miundombinu, kilimo, utalii na ukusanyaji mapato. 

Mkurugenzi huyo pia, alitumia fursa hiyo kumueleza Rais Dk. Shein jinsi Benki ya CRDB ilivyodhamiria kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi ya kimkakati kwa lengo la kuendelea kuimarisha uchumi wa Zanzibar. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Ally Hussein Laay kwa upande wake alisema kuwa Benki hiyo inayofuata misingi ya Utawala Bora imekuwa na mikakati na Sera madhubuti katika kuhakikisha inabadilishana madaraka huku akieleza namna Benki hiyo inavyochangia uchumi wa Tanzania. 

Aidha, alieleza mafanikio makubwa yaliopatikana tokea kuanza kazi kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya Abdulmajib Mussa Nsekela ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Charles Kimei ambaye amestaafu. 

Mapema Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akiutambulisha uongozi huo kwa Rais Dk. Shein alieleza jinsi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inavyoshirikiana na Benki hiyo ya CRDB katika mambo mbali mbali. 

Pamoja na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi, Benki ya CRDB imeendelea kutumia mfumo wake imara wa kibiashara ili kutekeleza mkakati wa kuimarisha biashara na uendeshaji wa shughuli zake za kibenki. 

Hivi karibuni Benki hiyo imepata tuzo ya Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira ambapo ikidhihirisha utekelezaji wa falsafa yake, imekuwa ikiendelea na dhamira ya kutoa huduma bora zaidi kwa wateja pamoja na bidhaa za kifedha za kisasa kwa wateja binafsi na wakubwa kwa kutumia mifumo imara ya tehama na mtandao wake mpana wa huduma. 

Azma na dira ya benki hiyo wakati wote imelenga katika kukidhi mahitaji ya wateja huku ikitumia uwezo wa teknolojia kutoa pato zuri kwa wanahisa pamoja na kujali jamii na jumuiya inayowazunguka ikiwa na kauli mbiu yake isemayo “Benki inayomsikiliza mteja”. 

Benki ya CRDB ni taasisi ya kibenki nchini Tanzania iliyo na thamani kubwa ya rasilimali, mikopo na amana za wateja ikiwa na lengo la kujipanua katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo mnamo Julai 29, mwaka 2017 Benki hiyo ilizindua Tawi lake jipya kisiwani Pemba. 

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar 

Share:

IMF Kushirikiana Na Serikali Kuimarisha Sera Za Kiuchumi

Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali ya Tanzania inatarijia kukutana na Timu ya wataalamu kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa ajili ya kujadili Programu mpya ya Ushauri wa Kisera (PSI) yenye dhima ya kusimamia sera za kiuchumi kwa lengo la kutatua changamoto zitakazoonekana pamoja na namna ya kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini.

Haya yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi mpya wa IMF nchini, Bw. Jens Renke, aliyekuja kujitambulisha rasmi kwa Waziri huyo jijini Dodoma baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hapa nchini.

Dkt. Mpango alisema kuwa pamoja na kufanya majadiliano na wataalamu hao, Serikali inatarajia kuwa wataafikiana nao ili kuanzisha programu hiyo ya Serikali ambayo Shirika hilo limekuwa likishauri.

“Tumekuwa tukishirikiana na IMF kwa muda mrefu na imekuwa ikitushauri mambo mbalimbali ya kusimamia Sera za Kiuchumi katika kuondoa changamato ya umasikini na kuwa na maendeleo endelevu kwa usimamizi wa Sera za Uchumi “, alieleza Dkt. Mpango.

Aidha Dkt. Mpango alimueleza Mwakilishi huyo kuwa vipaumbele vya Serikali na juhudi mbali mbali zilizofanyika katika kukabiliana na tatizo la umaskini ni pamoja na kujenga uchumi jumuishi, kusimamia fedha za umma vizuri, kuhakikisha kwamba nchi inaendelea kuwekeza katika kilimo pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kisasa.

Waziri Mpango alibainisha kuwa vipaumbele vingine ni pamoja na kuziba mianya ya rushwa na kukusanya mapato ya ndani ipasavyo ili kuweza kutumia rasilimali zote za nchi vizuri na kuboresha huduma muhimu za wananchi kama elimu na afya.

Aidha, alimueleza mgeni huyo kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana nae katika kuleta maendeleo nchini.

Naye Mwakilishi Mkazi mpya wa IMF nchini, Bw. Jens Renke, aliahidi kuwa balozi mzuri wa Tanzania katika Shirika hilo na kuiomba Serikali ushirikiano katika kazi zake.

Aliiomba Serikali imtumie katika kutatua matatizo mbalimbali na yuko tayari kutoa ushauri wa kisera na kichumi, na kubainisha kuwa atafanya kazi kama sehemu ya Serikali katika kutatua matatizo na kuleta maendeleo nchini.

Bw. Renke alisema anapenda kujifunza mengi nchini na atatembelea katika mikoa, Serikali za Mitaa pamoja na vyuo mbalimbali ili kuona mambo ambayo Serikali imeyafanya katika kujikwamua kiuchumi.

Mwisho.


Share:

Picha : TGNP YAENDESHA MAFUNZO YA JINSIA, DEMOKRASIA NA UONGOZI…WADAU WAWEKA MIKAKATI KUSHIKA MKONO WANAWAKE


Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakiwemo viongozi wa Taasisi za Kijamii, Mashirika yasiyo ya kiserikali,waendesha bodaboda,watu wenye ulemavu na viongozi wa dini na kimila wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wakipeana mrejesho wa mambo waliyojifunza kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na kufanya maamuzi kwa nia ya kubadili mtazamo wa jamii kuhusu ushiriki wa wanawake leo Ijumaa Februari 14,2020 katika ukumbi wa BM Maganzo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mzee wa Mila Juma Kidaha Makwaiya kutoka kata ya Ukenyenge akitoa mrejesho wa alichojifunza katika mafunzo hayo. Aliitaka jamii kuachana na mila zilizopitwa na wakati na kuhakikisha inawaamini wanawake kuwa viongozi ili kuwa na ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nhobola kijiji cha Bulimba kata ya Ukenyenge,Anjelina Mahona akiwataka wanawake kujitambua na kujiamini na kutopenda kuitwa wapiga debe wa wagombea wanaume bali wao wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi.
Mwenyekiti wa Chama cha waendesha bodaboda kata ya Ukenyenge,Zephania Charles akiwashauri wanawake kujikubali na kujiamini kuwa wanaweza kuwa viongozi na kuacha kubezana wao kwa wao na wanaume kuwashika mkono wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mayanji kata ya Ukenyenge, Sheikh Othman Ndamo ambaye ni Sheikh wa kata ya Kishapu akizungumza wakati wa mafunzo hayo. Alisema wanawake wanatakiwa kupewa nafasi za uongozi kwani kinachohitajika katika uongozi ni akili,busara na hekima  na hivyo vyote mwanamke anavyo.
Mratibu wa miradi wa Shirika la AGAPE ACP linalojihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto,Peter Amani akishauri wadau kutowaacha nyuma wanaume katika kupigania haki za wanawake na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Mhudumu wa afya ngazi ya jamii,Costantine Dasse akizungumza wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi.
Katibu wa Chama cha Watu Wenye Ualbino wilaya ya Kishapu, Seif Rashid akizungumza wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi. Alisema Watu wenye ualbino wanatamani kuona wanawake wanakuwa viongozi kwani asilimia 99 ya watu wenye ualbino wamelelewa na akina mama baada ya akina baba kutelekeza familia zao. 
Mzee wa Mila Isanzule Nkinga kutoka kijiji cha Mwaweja kata ya Mwaweja akizungumza wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi . Alisema : “Wanawake wakihamasishwa watajitokeza kugombea nafasi za uongoze tuendelee kuwatia moyo na kuwapa elimu wanaume wanaohisi kudharauliwa kama wanawake watakuwa viongozi,tuwaambie kuwa suala la uongozi ni la kila mtu katika dunia ya leo”.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi  wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakitengeneza mpango kazi wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakitengeneza mpango kazi wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakitengeneza mpango kazi wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi.
Mchungaji wa Kanisa la KKKT kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge, Godlisten Mzula akiwasilisha mpango kazi wa kundi lake wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi.
Mwezeshaji Jamii, Genes Tarimo akiwasilisha mpango kazi wa kundi lake wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi.
Mwenyekiti wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilaya ya Kishapu, Rahel Madundo akiwasilisha mpango kazi wa kundi lake wakati wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo hayo.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) umeendesha mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Uongozi kwa viongozi wa Taasisi za Kijamii, Mashirika yasiyo ya kiserikali,waendesha bodaboda,watu wenye ulemavu na viongozi wa dini na kimila wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika masuala ya uongozi.

Mafunzo hayo ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Wanawake na Uongozi unaosimamiwa na TGNP Mtandao kwa ufadhili wa UN Women yamefanyika Februari 12,2020 hadi Februari 14,2020 katika Ukumbi wa BM katika kata ya Maganzo yakishirikisha wadau zaidi ya 40.

Lengo mafunzo hayo ni kuwawezesha wadau hao kupeleka elimu kuhusu masuala ya jinsia,demokrasia na uongozi kwa makundi wanayoyaongoza ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na kufanya maamuzi kwa nia ya kubadili mtazamo wa jamii kuhusu ushiriki wa wanawake.

Washiriki wa mafunzo hayo wamesema mila potofu na wanawake kutojiamini bado ni changamoto kubwa inayochangia wanawake wengi kuwa na hofu ya kugombea nafasi za uongozi hivyo wamekubaliana kuendelea kutoa elimu kuhusu faida za wanawake kuwa viongozi

Aidha wameshauri elimu ya wanawake kujiamini ianze kutolewa katika ngazi ya shule ya msingi ili vijana wakue wakiwa na uelewa na jamii ipewe elimu ya haki za binadamu na usawa na kijinsia.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mayanji kata ya Ukenyenge, Sheikh Othman Ndamo ambaye ni Sheikh wa kata ya Kishapu
alisema wanawake wanatakiwa kupewa nafasi za uongozi kwani kinachohitajika katika uongozi ni akili,busara na hekima  na hivyo vyote mwanamke anavyo kwa hiyo ana sifa ya kuwa kiongozi huku akiwashauri wanaume wawape uhuru wa kuamua,kushiriki maamuzi na kumiliki rasilimali.

"Mwanamke ni chuo cha familia na mwanamke ndiyo mwenye kujenga familia hivyo akiwa kiongozi, ndani ya uongozi wa uongozi kunakuwemo huruma,upendo na uadilifu",aliongeza Sheikh Ndamo.

Kwa upande wake, Mzee wa Mila Juma Kidaha Makwaiya kutoka kata ya Ukenyenge aliitaka jamii kuachana na mila zilizopitwa na wakati na kuhakikisha inawaamini wanawake kuwa viongozi ili kuwa na ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi.

“Mwanamke na mwanaume wakiwa pamoja katika ngazi za maamuzi,wakawa na maamuzi shirikishi wanaleta maendeleo chanya.Tusiwachulie wanawake kuwa hawawezi bali tushirikiane nao kwa faida yetu sote”,alisema Makwaiya.

“Zamani wanawake waliothubutu kugombea nafasi za uongozi walionekana kuwa ni wahuni na Malaya na wasio na maadili. Malezi waliyolelewa wakielezwa kuwa wanawake hawawezi kuongoza ndiyo yaliwafanya wawe waoga na wakimya kumbe walikuwa wanajiumiza wenyewe na kujikuta wanakosa haki zao”,alisema Mzee Makwaiya.

Mzee wa Mila Isanzule Nkinga kutoka kijiji cha Mwaweja kata ya Mwaweja alisema : “Wanawake wakihamasishwa watajitokeza kugombea nafasi za uongoze tuendelee kuwatia moyo na kuwapa elimu wanaume wanaohisi kudharauliwa kama wanawake watakuwa viongozi,tuwaambie kuwa suala la uongozi ni la kila mtu katika dunia ya leo”.

Hata hivyo, Mchungaji wa Kanisa la KKKT kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge, Godlisten Mzula alisema ukosefu wa elimu ya uongozi ndiyo changamoto kubwa inayowafanya wanawake washindwe kujiamini hivyo panahitajika jitihada ziendelee kufanyika kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya wanawake.

Mchungaji wa Kanisa la FPCT kata ya Ukenyenge,Silvery Shartieli alishauri jamii ipewe elimu ya kwamba mwanamke ana uhuru wa kugombea na anaweza kuongoza jamii.

“Viongozi wa dini tunakutana na wananchi kila wiki,tuendelee kutoa elimu hii kwani inasikitisha kuona baadhi ya watu kuwabeza wanaume wanaotetea haki za wanawake na kuonekana pengine wana maslahi kwa wanawake hao",alisema.

Mratibu wa miradi wa Shirika la AGAPE ACP linalojihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto,Peter Amani aliwashauri wadau kutowaacha nyuma wanaume katika kupigania haki za wanawake na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi.

“Wakati tunahamasisha wanawake,ni lazima tuzungumze pia na wanaume waone umuhimu wa kutoa nafasi kwa wake zao,watoto washiriki kwenye chaguzi mbalimbali”,alisema Amani.

Mwenyekiti wa Chama cha waendesha bodaboda kata ya Ukenyenge,Zephania Charles aliwashauri wanawake kujikubali na kujiamini kuwa wanaweza kuwa viongozi na kuacha kubezana wao kwa wao na wanaume kuwashika mkono wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi.

Mkurugenzi wa asasi ya Access Facility Tanzania yenye makao makuu yake kata ya Ukenyenge,David Isange alisema baadhi ya wanawake wenye sifa za kuwa viongozi hawana elimu na kipato cha kutosha hivyo kusababisha kutojiamini na kujinyanyapaa kwa hofu ya kuogopa kupambana na wanaume katika masuala ya uongozi.

Katibu wa Kikundi cha VICOBA kata ya Maganzo, Happiness Sang’udi na Katibu wa Kikundi cha VICOBA kata ya Mondo,Martha Abel waliwataka wanawake kuacha kubezana wao kwa wao kutokana chuki binafsi na badala yake washikamane na kujiamini kusimama mbele ya umma.

Katibu wa Chama cha Watu Wenye Ualbino wilaya ya Kishapu, Seif Rashid alisema Watu wenye ualbino wanatamani kuona wanawake wanakuwa viongozi kwani asilimia 99 ya watu wenye ualbino wamelelewa na akina mama baada ya akina baba kutelekeza familia zao. 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nhobola kijiji cha Bulimba kata ya Ukenyenge,Anjelina Mahona aliwataka wanawake kujitambua na kujiamini na kutopenda kuitwa wapiga debe wa wagombea wanaume bali wao wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi huku akiwashauri wanawake kuwashirikisha waume zao wanapotaka uongozi.

Mwenyekiti wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilaya ya Kishapu, Rahel Madundo alisema hivi sasa wanawake wengi wameanza kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ambapo sasa baadhi ya wanawake wamefanikiwa kuwa viongozi wa serikali za mitaa na udiwani.

Mila na desturi kandamizi mkoani Shinyanga bado zinatajwa kuwajengea nidhamu ya uoga wanawake na kuwa na hofu ya kugombea nafasi za uongozi kwani jamii inamchukulia mwanamke kuwa hawezi kuongoza.

Mbali na changamoto za kiuchumi,ukosefu wa elimu,pia kazi nyingi za nyumbani zinawafanya wanawake kukosa muda wa kushiriki katika masuala ya uongozi.

Share:

Infinix Kuipamba Valentine Kwa Uzinduzi Duka La Pili La Kisasa-Infinix Smart Hub.

Katika Kusheherekea sikukuu ya wapendanao, kampuni ya simu, Infinix Mobile Tanzania imezindua rasmi duka Jipya, maarufu kama Infinix Smart Hub, lililopo China Plaza Kariakoo. Hili ni duka la pili la kuzinduliwa na kampuni hiyo huku lengo kuu ni kuwafikia wateja wake kwa urahisi zaidi.

Katika uzinduzi huo afisa wa mahusiano wa kampuni ya simu ya Infinix, Aisha Karupa alivieleza vyombo vya habari kuwa, “Infinix imejipanga vizuri katika kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu wa maeneo mbalimbali pasipo kuwa na hofu ya kutufikia kwa uharaka zaidi na katika kuhakikisha tunafanikiwa katika hilo Infinix Smart Hub itakuwa ikitoa huduma kwa siku saba za kila wiki yani jumatatu hadi jumapili kuanzia saa 9:00 asubuhi hadi saa 11:30 jion”.
 
Aisha aliwashukuru watanzania kwa kuzipokea bidhaa za Infinix na kuwa wateja wazuri kwao, kusema “kwa mapenzi yenu tutaendelea kutanua wigo ili kuhakikisha mnapata huduma stahiki kama vile simu na bidhaa nyingine za Infinix zenye ubora zaidi zikiwa chini ya warranty ya mwaka mmoja na mwezi moja pamoja na elimu ya bure kuhusiana na utunzaji na utumiaji wa simu za Infinix kwa muda mrefu pasipo kuwaletea shida ya aina yoyote”. 
 
Vile vile Meneja wa Masoko Bwana Saiphone Asajile alieleza machache kuhusiana na mauzo ya Infinix tangu kuingia kwake rasmi Tanzania mwaka 2018 na ni nini watanzania wategemee kutoka Infinix hasa kwa kipindi hiki cha valentine,
“Watanzania wameonyesha upendo wa hali ya juu sana kwetu na hadi kufikia hatua ya kuzindua duka la pili la kisasa sio hatua ndogo, kwani kuna kampuni nyingi za simu tumezikuta lakini hawajafanikiwa kufanya hili tunalolifanya Infinix, hiki ni kiashirio tosha Infinix imeliteka soko la simu kwa asilimia kubwa lakini vile vile katika kuendeleza upendo kama ilivyo kawaida yetu katika Msimu huu wa Valentine Infinix inakupa ofa ya 10%, Infinix gift package na chakula cha usiku kwa wewe na umpendaye katika restaurant ya kisasa”.
 
Uzinduzi huo ulishamirishwa na michezo mbalimbali pamoja na muziki wa live band na kuufanye uwe wa kipekee.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger