Tuesday, 11 February 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne February 11






















Share:

Monday, 10 February 2020

Project Officer at IFES-Tanzania

Job Summary The Project Officer will provide program and operations support to the IFES-Tanzania field office. Minimum Qualification: Bachelor Experience Level: Mid level Experience Length: 4 years Job Description Support implementation of activities as directed by the Country Director, based on approved workplan(s), budgeting, and other relevant framework Coordinate and maintain good relations with IFES’ CEPPS partners and other USAID implementing partners, and… Read More »

The post Project Officer at IFES-Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

BREAKING: Sumaye Arejea CCM....Katibu Mkuu Dr Bashiru Ampokea

Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye leo  ametangaza kurudi tena Chama cha Mapinduzi (CCM)

Ametangaza uamuzi huo mchana wa leo tarehe 10/2/2020 katika kikao cha Baraza la Wadhamini, Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba - Dar es salaam.

Sumaye aliwahi kuhudumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo katika serikali ya awamu ya tatu na baadaye alihamia Chadema mwaka 2015.
 

Jumatano Desemba 4, 2019 alitangaza kujiondoa CHADEMA na kusema atakuwa mshauri huru wa masuala ya kisiasa.


Share:

Viongozi wa Afrika walaani pendekezo la mpango wa amani Mashariki ya Kati ulitolewa na Rais Donald Trump

Viongozi wa Afrika wameulaani mpango wa amani ya Mashariki ya Kati uliopendekezwa na Rais Donald Trump wa Marekani wanaosema si halali.

Akizungumza na viongozi wakuu wa mataifa ya Afrika kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika ulioanza leo mjini Addis Ababa, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo, Moussa Faki Mahamat, amesema mpango huo uliotangazwa mwishoni mwa mwezi uliopita unawakilisha uvunjaji usio kipimo wa maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Mahamat, ambaye alitumia hotuba yake hiyo kurejelea mshikamano wa Afrika na lengo la Wapalestina, alisema mpango wa Trump uliandaliwa bila kushauriana na jumuiya ya kimataifa, na kwamba unazikanyaga haki za Wapalestina.

Mpango huo uliopewa jina la makubaliano ya karne, ulikataliwa tangu mwanzoni na Wapalestina wakiungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na mataifa jirani ya Mashariki ya Kati, Ghuba na ulimwengu wa Kiislamu.

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina, ambaye kawaida huhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika kama mgeni mwalikwa, mara hii ameshindwa kuhudhuria, huku maafisa wa serikali yake wakisema anaelekea Umoja wa Mataifa kulishinikiza Baraza la Usalama kuulaani mpango huo wa amani.


Share:

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.



Share:

Breaking : WAZIRI MKUU FREDRICK SUMAYE ATANGAZA KURUDI CCM

Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye ametangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka CHADEMA kupokelewa na Katibu mkuu Wa Chama hicho Dkt.Bashiru Ally leo Jumatatu Februari 10,2020.
Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye n Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa (Waliohama CCM na kuhamia CHADEMA na wamerudi tena CCM)
Share:

Internships Opportunities | Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS) Internship 2020/2021

Application Deadline: 26th September, 2020. The Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS) leads and inspires the world to achieve its shared vision of zero new HIV infections, zero discrimination and zero AIDS-related deaths. UNAIDS unites the efforts of 11 UN organizations-UNHCR, UNICEF, WFP, UNDP, UNFPA, UNODC, UN Women, ILO, UNESCO, WHO and the World Bank-and works closely… Read More »

The post Internships Opportunities | Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS) Internship 2020/2021 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ESRF YAENDESHA KONGAMANO LA KILIMO BIASHARA


 Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi kwa washiriki wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.


 Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Magreth Nzuki akizungumzia malengo ya warsha kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtafiti mshiriki mwandamizi kutoka ESRF, Dr Oswald Mashindano akizungumzia fursa za kilimo kwenye miji na fursa za uwekezaji kama zilivyoainishwa kwenye miongozi ya uwekezaji kwenye mikoa mbalimbali wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Umoja wa Vijana Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS), Bw. Philemon Kiemi akitoa mada kuhusu ufugaji wa kisasa wa nyuki wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu kutoka SUA, Ltn Joseph Lyakurwa akitoa mada kuhusu ufugaji wa Samaki katika matanki kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dr. Hieromin Lamtane akitoa mada kuhusu malisho ya chakula cha samaki kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu kutoka Agriculture Media, Bw. Raphael Majivu akitoa mada kuhusu kilimo cha malisho ya mifugo bila udongo (Hydroponic Fodder) pamoja na kilimo cha Azola (Chakula cha mifugo na mbolea) wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akijadiliana jambo na Meneja wa Data wa ESRF, John Kajiba (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Magreth Nzuki wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakipata maelezo ndani ya kitalu maalum kuhusu kilimo cha mbogamboga bila kutumia udongo wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu kutoka SUA, Ltn Joseph Lyakurwa akitoa maelezo kwa vitendo kwa washiriki kuhusu ufugaji wa Samaki katika matanki wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
***
TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), imeendesha kongamano kubwa la fursa za kilimo biashara kwa lengo kuhimiza matumizi ya teknolojia ili kuboresha tija katika sekta ya kilimo.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ESRF Bi. Margareth Nzuki alisema, Taasisi hiyo ikishirikiana na Serikali kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) limekuwa likifanya tafiti mbalimbali ili kuainisha fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali ya uchumi. 

Ameongeza kuwa kwa ufadhili wa UNDP,  ESRF ikishirikiana na Serikali za Mikoa limefanya  utafiti kuainisha  fursa mbalimbali za uwekezaji katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na mpaka sasa imekwisha kamilisha kutayarisha Miongozo ya Uwekezaji wa Mikoa 15 na inaendelea kumalizia mikoa mingine iliyobaki. Amesema  katika miongozo hiyo fursa nyingi zinatoka katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji.

Bi Nzuki amewaambia washikiri kuwa lengo la Kongamamo hilo ni kushirikishana na kutoa maarifa mapya katika kilimo biashara.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema  kukua kwa teknolojia duniani kumeongeza fursa nyingi na kuwezesha wakulima katika sehemu mbalimbali duniani kutokutegemea mvua.

"Teknolojia imewezesha wakulima kutumia eneo dogo la ardhi kuzalisha kiwango kikubwa cha mavuno ya mazao yaliyo bora; teknolojia pia imewezesha wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo cha kisasa toka kwa wataalamu kwa haraka na muda muafaka, hivyo kusaidia kupata mavuno mengi na bora," alisema Dk. Kida.

Kilimo hicho cha kutegemea teknolojia za kisasa kinachoitwa kwa kiingereza “Smart Farming Agriculture” ambacho hakihitaji maeneo makubwa ya ardhi na kinaweza pia kufanyika katika miji.

Uwingi na ubora wa mazao yanayozalishwa ni kiashiria cha fursa ya kufanya biashara kwa tija, kwa sababu mazao hayo yatamvutia mnunuzi na yanaweza kuuzwa popote duniani kutokana na sifa zake za ubora; mfano kwenye maduka makubwa na mahotelini ambako wateja wengi katika zama hizi wanapenda vyakula vya asili ambavyo havina kemikali ambayo inatumika kukuzia mimea mashambani.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ajili ya wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wengine katika sekta ya Kilimo.
kwa mujibu wa Dk. Kida wakufunzi mbalimbali waliobobea na wanaojihusisha katika fani mbalimbali za Kilimo biashara wametarajiwa kutoa uwelewa kwa kuwajengea uwezo washiriki ili kutafuta utatuzi wa vikwazo mbalimbali ambavyo wakulima na wafugaji mmekuwa mnakabiliana navyo.

Katika kongamano hilo lililofanyika mwishoni mwa juma mada zilizofundishwa naa kujadiliwa Kwa kina ni pamoja na:malisho ya chakula cha samaki,ufugaji wa samaki katika matanki (Recirculating Aquaculture System), kilimo cha mboga mboga bila kutumia udongo (Hydroponic Vegetable),kilimo cha azolla kwa ajili ya malisho ya mifugo na mbolea, ufugaji wa kisasa wa samaki kwa kutumia vizimba, matanki na mabwawa,ufugaji wa kisasa wa nyuki na kubadilishana uzoefu katika kilimo biashara.

Washiriki wengine pamoja na wakulima na wafugaji ni taasisi za fedha nchini za TADB, CRDB, SELF na PASS Trust.
Wadau hao hutumiwa na wadau wengi katika kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya mtu mojammoja, vikundi  na Taifa kwa ujumla.  

Share:

Waliofariki Kwa Virusi Vya Corona Wafika 900

Idadi ya maambikizi mapya ya virusi vya corona imepungua kidogo kutoka siku moja kabla. 

Vifo vingine 97 na maambukizi mapya ya watu 3,062 vimeripotiwa katika muda wa masaa 24 yaliyopita jana Jumapili, ikilinganishwa na maambukizi mapya ya watu 3,399 yaliyorekodiwa siku moja kabla. 

Wakati huo huo, timu ya wataalamu wa kimataifa kutoka shirika la afya ulimwenguni WHO imeondoka kwenda Beijing kufanya uchunguzi wa kuzuka kwa virusi vya corona, shirika hilo la afya la Umoja wa mataifa limetangaza.

 Zaidi ya watu 40,000 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona duniani kote hadi leo Jumatatu asubuhi, ambapo watu 900 wamefariki.

-DW


Share:

Watu 6 wafariki baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuchomwa moto.

Watu sita, wawili wakiwa ni  mama na watoto wao wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuchomwa moto usiku wa manane na kuteketea katika kitongoji cha Uponda kata ya Mjawa wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akizungumza kwa njia ya simu kwa niaba ya kamanda wa mkoa wa kipolisi Rufiji kamishna mwandamizi Onesmo Lyanga mwakilishi wake kamishna msaidizi Richard Ngolle amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa Richard Mathias mkazi wa Buza Dar es Salaam na Masasi mkoani Mtwara anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Rufiji  kwa tuhuma hizo.

Akielezea tukio lilivyotokea bila kuingia kwa undani amesema ni wivu wa mapenzi kati ya Bi.Regina avondo ambaye kwa sasa ni marehemu  na mpenzi wake Bw.Richard Mathias aliyekwenda nyumbani kwa mpenzi wake marehemu Regina Mavondo usiku wa manane tarehe 8/2/2028 na kuchoma nyumba yake ambayo ndani kulikuwa na watu wengine watano wamelala wawili wakiwa ni watoto wa mdogo wake marehemu Regina Mavondo. 

ITV


Share:

Rais Magufuli Aresha Wanyamapori mbalimbali Ikulu Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amerejesha wanyamapori katika bustani za Ikulu Jijini Dar es Salaam hali iliyofanya mandhari ya Ikulu kupendeza na kuvutia.

Wanyama waliopo katika bustani hizo ni pamoja na Pundamilia, Pofu, Swala, Digidigi, Tausi, Mbuni, Tumbili, Kanga, Batamaji na wengine.

Awali wanyamapori hao walifugwa kwa idadi kubwa wakati wa Uongozi wa Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na baadaye walitoweka hadi mwaka 2017 walipoanza kurejeshwa na Mhe. Rais Magufuli.

Katika maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam hivi sasa kuna ongezeko kubwa la ndege aina ya Tausi ambao wanaonekana kulipamba Jiji la Dar es Salaam.


Share:

Ijue Sayansi ya Nguvu za Kiume

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani.

Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?
Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu


Hatua  mbili  Muhimu 
Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  maumbile yake ya kiume yapitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  yaweze  kusimama  barabara  na  kuwa  magumu  kama  msumari.

Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, yaendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION

Endelea na Makala hii kwa <<Kubofya Hapa>.


Share:

Jobs at The Arusha Urban Water Supply and Sanitation Authority

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF WATER ARUSHA URBAN WATER SUPPLY AND SANITATIONAUTHORITY EMPLOYMENT OPPORTUNITIES The Arusha Urban Water Supply and Sanitation Authority (AUWSA) is a legally established entity responsible for the overall operations and management of water supply and sanitation services in Arusha City. It is among of the best Authorities in Tanzania. The core function of… Read More »

The post Jobs at The Arusha Urban Water Supply and Sanitation Authority appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

NACTE yafuta usajili wa vyuo 7

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE imevifutia usajili vyuo saba ambavyo vimethibitika kuendesha mafunzo bila kukidhi vigezo na utaratibu.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya wanahabari, Mkurugenzi wa Opresheni wa NACTE, Dr Geofrey Oleke amesema lengo la kuvifutia vyuo hivyo usajili ni kutaka vikamilishe taratibu ili kutoa elimu yenye manufaa kwa Watanzania kwa kufuata misingi.

Orodha ya vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na ERA Training College - Bukoba (REG/TLF/095), Azania College of Management - Dar es Salaam (REG/BMG/021), Time School of Journalism - Dar es Salaam (REG/PWF/013), Clever College - Dar es Salaam (REG/BTP/205P) na Aces College of Economic Science - Mwanakwerekwe, Zanzibar (REG/BPT/081P).


Share:

LIVE: DPP Aikabidhi Serikali Mali Zilizotaifishwa na Mahakama

LIVE: DPP Aikabidhi Serikali Mali Zilizotaifishwa na Mahakama

-Jumla ya kilo 397.937 za dhahabu zenye thamani ya bilioni 32,274,336,361.73 zimetaifishwa,dhahabu hizi zilikuwa zinatoroshwa na kuikosesha Serikali mapato yake


Share:

Finance & Operations Manager at D-Tree Zanzibar

Finance & Operations Manager Reports to: Program Director Location: Zanzibar, Tanzania Start Date: March 2020 (or as soon as possible) Who we are D-tree International is on a mission to radically improve health by strengthening health systems through innovations in digital technology. D-tree works through partnerships with Ministries of Health and NGOs to bring human-centered design approaches to… Read More »

The post Finance & Operations Manager at D-Tree Zanzibar appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wakulima Wa Mahindi Tabora Waomba Kupatiwa Mbolea Ya Urea

SALVATORY NTANDU
Uhaba wa mbolea aina ya  UREA katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/20 mkoani Tabora  umetajwa kuchangia  wakulima wa zao la mahindi kuzalisha kwa kiwango cha chini na kusababisha baadhi ya wakulima kuiomba kampuni ya usambazaji pembejeo za kilimo ya PETROBENA kuanza kuwakopesha kwa msimu ujao.

Hayo yalibainishwa febuari sita mwaka huu na Wakulima wa zao hilo kwenye mkutano wa mkuu wa 27 wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi (WETCU) ambapo walidai mwaka huu uzalishaji wa mahindi umeshuka kutoka na kukosekana kwa mbolea aina ya UREA.

Juma Madoshi ni mmoja wa wakulima wa zao la mahindi mkoani humo alisema kuwa familia nyingi huenda zikakabiliwa na uhaba wa chakula mwaka huu kutokana na  uhaba wa mbolea hiyo na kuiomba kampuni ya usambazaji Pembejeo za kilimo ya PETROBENA kuwakopesha UREA kwa msimu ujao.

“Sisi wakulima wa zao la mahindi mwaka huu tutapata chakula kidogo,tumezoea kuzalisha kwa wingi,tunaiomba serikali kupita viongozi wetu wa chama chetu (WETCU) kufanya mazungumzo na PETROBENA ili msimu ujao tusipate changamoto hii” alisema Madoshi.

Nae Monika Manwali mkulima wa zao la tumbaku mkoani humo alisema awali walikuwa wanakopeshwa mbelea na kampuni za ununuzi wa zao hilo ambazo walikuwa wanazitumia katika kilimo cha cha mahindi lakini mwaka huu imekuwa tofauti ikilinganishwa mwaka huu ambapo utaratibu umebadilika.

“Tunaomba kukopeshwa mifuko miwili ya UREA ambayo inatosha kuitumia kwenye hekari mbili na itasaidia wakulima kupata mahindi  yakutosha ambayo yatasaidia familia zetu kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha kwa mwaka mzima”alisema Manwali.

Akizungumza kwenye mkutano wa mkuu wa 27 wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi (WETCU) mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanri alizitaka kampuni za usambazaji wa pembejeo za kilimo kuhakikisha wanasambaza mbolea kwa wakati ili kwenda sambamba na msimu wa kilimo wa mwaka huu.

“Msimu wa kilimo umeanza muda mrefu sisi kama serikali hatukubali kuona wakulima wetu wanaendelea kuteseka kwa kukosa mbolea aina ya UREA licha ya kuwa na mashamba ya kutosha na nguvu kazi ipo”alisema Mwanri.

Katika hatua nyingine Mwanri alisema kuwa kwa msimu ujao wakulima watakaobainika mwaka huu hawajapanda miti katika mashamba yao hawataruhusiwa kulima zao la tumbaku hivyo ni budi wakulima wote wakazingatia maelekezo ya serikali.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger