Wednesday, 5 February 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano February 5











Share:

Tuesday, 4 February 2020

Wimbo Mpya : NTEMI 'NG'WANA KANG'WA' - UKIMWI


Msanii wa nyimbo za asili Ntemi 'Ng'wana Kang'wa' kutoka Kahama mkoani Shinyanga ametualika kusikiliza wimbo wake mpya,ameupa jina la UKIMWI...Usikilize hapa mtu wangu


Share:

T-MARC TANZANIA YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE ZA FLOWLESS, SEKONDARI YA MUGABE DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Bidhaa za Kijamii wa T-MARC Tanzania, Flavian Ngole, akiongea na wanafunzi wa kike wa sekondari ya Mugabe wakati wa hafla ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa shule hiyo.
 Mkurugenzi wa Bidhaa za Kijamii wa T-MARC Tanzania,Flavian Ngole (kushoto) akikabidhi taulo za kike kwa Mwalimu mlezi wa shule ya sekondari ya Mugabe iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, Theresia Paulo, wakati wa hafla ya hafla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike zilizozinduliwa na taasisi hiyo nchini zinazojulikana kama Flowless, wa pili kushoto ni balozi wa bidhaa hiyo, Dinnah Marrios.

Mkurugenzi wa Bidhaa za Kijamii wa T-MARC Tanzania, Flavian Ngole, (kushoto) akikabidhi taulo za kike kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mugabe iliyopo wilayani Kinondoni,Judith Michael, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike zilizozinduliwa na taasisi hiyo nchini zinazojulikana kama Flowless, kwa wanafunzi wa shule hiyo ,wa pili kushoto ni balozi wa bidhaa hiyo, Dinnah Marrios.
Share:

Mahakama yatoa hati ya kukamatwa Jacob Zuma

Mahakama ya juu ya Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma baada ya kushindwa kufika mahakamani kukabiliana na mashtaka kuhusu rushwa dhidi yake.

Hati hiyo itafanya kazi ikiwa atashindwa kuhudhuria kesi yake itakayoanza mwezi Mei. Bwana Zuma anakabiliwa na makosa 16 ya kughushi, rushwa , ulaghai na utakatishaji fedha ukihusisha biashara ya silaha ya thamani ya mabilioni ya dola iliyofanywa tangu miaka ya 1990.

Rais huyo wa zamani amefanikiwa kukwepa shutuma za rushwa dhidi yake kwa zaidi ya miaka 10. Lakini leo, sheria haikuwa upande wake.

Hati ya kukamatwa kwake imetolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake. Jopo la wanasheria wake waliwasilisha nyaraka wakisema kuwa mteja wao alikuwa mgonjwa na amekuwa akipatiwa matibabu nje ya Afrika Kusini tangu mwezi uliopita.

Jaji Dhaya Pillay alihoji maelezo yaliyo kwenye nyaraka za matibabu za Zuma zilizowasilishwa na mawakili wake mahakamani. Lakini rais huyo wa zamani atakamatwa ikiwa atashindwa kufika mahakamani tarehe 6 mwezi Mei kesi yake itakapoanza rasmi.

Bwana Zuma anakabiliwa na mashtaka kadha wa kadha ya rushwa ikihusisha malipo 783 yenye utata anayodaiwa kupokea kutoka kwa aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya fedha Schabir Shaik.

Madai hayo pia yamerejelea mkataba wa silaha uliofanyika miaka ya 1990 na kampuni moja ya masuala ya ulinzi ya nchini Ufaransa.


Share:

Serikali Yawataka Waajiri Wa Makocha Kutoka Nje Kutoa Taarifa Zao TRA Ili Walipe Kodi

Na. Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imezitaka timu zote za mpira zinazoajiri makocha na wachezaji kutoka nje ya nchi kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya waajiriwa walionao wanaotakiwa kulipa kodi.

Hayo yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Selemani Nkamia, aliyetaka kujua Serikali inatambuaje Kocha au Mchezaji wa Nje aliyelipa na asiyelipa kodi kwa kuwa malipo yao hufanywa kiholela kwa kuwa hakuna mfumo rasmi.

Dkt. Kijaji alisema kuwa Kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na kipato chake.

“Kila mgeni akifikisha miezi 6 anahesabika ni mkazi (local resident) na anapaswa kulipa kodi, ni jukumu la mwajiri kutoa taarifa ya nani analipwa nini ili kodi zote stahili ziweze kulipwa kwa mujibu wa sheria”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa ulipaji wa kodi ya ajira ni kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 na ni jukumu la mwajiri kwenda kutoa taarifa kwenye Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ya waajiriwa walionao wanaotakiwa kulipa kodi hiyo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya Sh. milioni 1,733.6 zilikusanywa kama malipo ya kodi ya ajira kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini.

Mwisho.


Share:

Waziri Mhagama Awafunda Watumishi Wa Ofisi Yake

Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewaasa watumishi wa Ofisi yake kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma katika utendaji kazi wao ili kuendelea kuitumikia nchi kwa weledi na ufanisi na kufikia malengo kwa wakati unaostahili.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha kwanza cha mwaka cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo kilichofanyika Februari 3, 2020 Jijini Dodoma.

Waziri Mhagama aliwataka watendaji wote kuona umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa weledi huku wakizingatia sheria za utumishi wa umma ikiwemo nidhamu kazini, kauli nzuri kwa wateja, kuzingatia mavazi ya staha na kuwahi kazini.

Waziri aliongezea kuwa, ni lazima mtumishi wa umma afanane na kanuni na sheria za kiutimishi kwa kuwa na maadili mazuri awapo kazini na nje ya kazi ili kujipatia sifa njema kuanzia muonekano hadi tabia kwa ujumla.

“Hatutegemei mtumishi wa umma tena wa ofisi hii anakuwa ndiye mlevi wa kupindukia yaani ndiye namba moja Dodoma hii , wala kuvaa mavazi yasiyoendana na hadhi ya utumishi wa umma, hiyo kwetu hatutoivumilia lazima tuikatae na kuhakikisha tunakuwa mfano wa kuingwa,”Alisistiza

Waziri aliwakumbusha watendaji wa ofisi hiyo kuzingatia nafasi zao za kiutendaji wawapo kazini kwa kuzingatia jukumu la ofisi yake ni Kuratibu Shughuli zote za Serikali hivyo lazima iwe ofisi ya mfano.

“Ofisi yetu inaratibu shughuli zote za Serikali , muone ni kwa namna gani sisi ni viungo kwa Serikali hii hivyo mtumie fursa ya baraza hili kukumbushana wajibu wetu kwa kuhakikisha mnatekeleza majukumu kwa nidhamu ya hali ya juu sana,”alisema Waziri Mhagama

Aliutaka uongozi pia kuendelea kuwa na umoja na kufanya kazi kwa kuzingatia dhana ya ushirikishwaji ili kujenga tija kwa kupitia vikao ambavyo vitaibua changamoto zinazowakabili pamoja na kuishauri vyema Serikali kuhusu usimamizi wa kazi na rasilimali watu tunayoisimamia kila siku.

“Ni muhimu kuwa na vikao ili kuendelea kusimamia ustawi sehemu zetu za kazi, na uwepo wa mabaraza haya utaleta tija kwa kuzingatia mchango wake kwa Serikali nzima na hakikisheni mnayatumia kwa kuzingatia dhana ya ushirikishaji,”alieleza Waziri

Aidha aliongezea kuwa ni muhimu viongozi wote kuanzia ngazi ya Vitengo, Idara na Taasisi zote kuendelea kusimamia utekeleaji wa majukumu kwa kufuata sheria, miongozo na kanununi za utumishi wa umma huku wakiwa na upendo kati yao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Tixon Nzunda aliahidi na kumhakikishia Waziri kuwa, watatekeleza maagizo na maelekezo aliyoyatoa ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili mazuri na kuahidi kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo juu ya utoaji wa huduma bora inayozingatia viwango vya hali ya juu.

“Tunakushukuru Waziri na nikuhakikishie kuwa unatimu imara, tulivu na chapakazi na tutatekeleza maagizo yote kwa kasi ya mabadiliko ya hali ya juu,”alisema Bw.Tixon

Naye mmoja wa wajumbe wa baraza hilo Bi. Numpe Mwambeja alieleza furaha yake kwa kumshukuru Waziri kwa maelekezo yake yenye nia njema ya kuendelea kuona ofisi yake inakuwa ya mfano katika utendaji kazi wa kila siku na kuahidi kuzingatia maagizo aliyoyatoa.

“Kwa niaba ya wajumbe wenzangu wa kikao cha baraza nimefarijika sana na maagizo yaliyotolewa na waziri ikiwemo kuzingatia suala la uadilifu, kuwahi kazini, kuvaa mavazi ya staha, kuacha uvivu na kuwa na kauli nzuri katika hudumia wateja wa ndani na nje ya ofisi ili kufanya kazi zetu kwa ufanisi unaotakiwa,”alisema, Numpe.


Share:

MAZISHI YA MOI HUENDA KENYATTA AKASUBIRIWA BAADA YA KUKUTANA NA TRUMP


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kulia ni Rais Mstaafu Daniel Moi wakati wa uhai wake.

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Pili wa Jamhuri ya Kenya, Daniel Arap Moi, tayari umekwishapelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kinachoitwa Cha Lee, kilichopo jijini Nairobi nchini Kenya.

Rais Mstaafu wa Taifa hilo amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Februari 4, 2020, akiwa na umri wa miaka 95, katika hospitali Jijini Nairobi alikokuwa akipatiwa matibabu na kifo chake kimetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta, akiwa safarini kuelekea nchini Marekani katika mkutano wake na Rais Donald Trump.

Kufuatia kifo hicho Rais Kenyatta ametangaza kuwa bendera nchini Kenya na katika Ubalozi wa Kenya, kupeperushwa nusu mlingoti hadi atakapozikwa, ambapo hadi sasa taarifa za mazishi bado hazijatangazwa na huenda Rais Kenyatta akasubiriwa, kwani atarejea nchini siku ya Alhamisi ya Februari 6, 2020.

Daniel Moi aliingia madarakani mwaka 1978, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza Hayati Jomo Kenyatta, na kuapishwa kama Rais wa Pili wa Jamhuri ya Kenya na kuhudumu kwa miaka 24, ambapo mkewe Lena Moi, alifariki mwaka 2004.

Moi ameacha watoto Saba ambao ni Gideon (Seneta Baringo), Raymond (Mbunge wa Rongai ), Jeniffer Moi, June Moi, Philip Moi, John-Mark and Doris Moi. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Daniel Arap Moi, mahala pema peponi Ameen.
Share:

SERIKALI YAWATAKA WAAJIRI WA MAKOCHA KUTOKA NJE KUTOA TAARIFA ZAO TRA ILI WALIPE KODI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma.


Na. Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imezitaka timu zote za mpira zinazoajiri makocha na wachezaji kutoka nje ya nchi kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya waajiriwa walionao wanaotakiwa kulipa kodi.
Hayo yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Selemani Nkamia, aliyetaka kujua Serikali inatambuaje Kocha au Mchezaji wa Nje aliyelipa na asiyelipa kodi kwa kuwa malipo yao hufanywa kiholela kwa kuwa hakuna mfumo rasmi.

“Kila mgeni akifikisha miezi 6 anahesabika ni mkazi (local resident) na anapaswa kulipa kodi, ni jukumu la mwajiri kutoa taarifa ya nani analipwa nini ili kodi zote stahili ziweze kulipwa kwa mujibu wa sheria”, alieleza Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa ulipaji wa kodi ya ajira ni kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 na ni jukumu la mwajiri kwenda kutoa taarifa kwenye Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ya waajiriwa walionao wanaotakiwa kulipa kodi hiyo.
Dkt. Kijaji alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya Sh. milioni 1,733.6 zilikusanywa kama malipo ya kodi ya ajira kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini.

Share:

MAHAKAMA YATOA HATI YA KUKAMATWA KWA JACOB ZUMA


Mahakama ya juu ya Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma baada ya kushindwa kufika mahakamani kukabiliana na mashtaka kuhusu rushwa dhidi yake.


Hati hiyo itafanya kazi ikiwa atashindwa kuhudhuria kesi yake itakayoanza mwezi Mei. Bwana Zuma anakabiliwa na makosa 16 ya kughushi, rushwa , ulaghai na utakatishaji fedha ukihusisha biashara ya silaha ya thamani ya mabilioni ya dola iliyofanywa tangu miaka ya 1990.

Rais huyo wa zamani amefanikiwa kukwepa shutuma za rushwa dhidi yake kwa zaidi ya miaka 10. Lakini leo, sheria haikuwa upande wake.

Hati ya kukamatwa kwake imetolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake. Jopo la wanasheria wake waliwasilisha nyaraka wakisema kuwa mteja wao alikuwa mgonjwa na amekuwa akipatiwa matibabu nje ya Afrika Kusini tangu mwezi uliopita.

Jaji Dhaya Pillay alihoji maelezo yaliyo kwenye nyaraka za matibabu za Zuma zilizowasilishwa na mawakili wake mahakamani. Lakini rais huyo wa zamani atakamatwa ikiwa atashindwa kufika mahakamani tarehe 6 mwezi Mei kesi yake itakapoanza rasmi.
Chanzo- BBC
Share:

WAKAZI WA PEMBEZONI MWA FUKWE ZA BAHARI YA HINDI WAELIMISHWA ATHARI ZA MAGENDO

Na Veronica Kazimoto

Wakazi na wafanyabiashara waishio pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi katika kata za Somangila, Kimbiji na Pemba Mnazi zilizopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wameelimishwa kuhusu athari za magendo yanayopitishwa kinyume na sheria katika maeneo hayo.

Elimu hiyo imetolewa wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo inafanyika maeneo mbalimbali katika mikoa ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi.

Akizungumza na wakazi hao katika maeneo ya Buyuni na Kimbiji wilayani Kigamboni, Afisa Kodi Mkuu Rose Mahendeka kutoka mamlaka hiyo, amewaambia wakazi hao kuhakikisha wanatoa taarifa pindi wanapoona bidhaa za magendo ikiwa ni pamoja na kuepuka kutumia bidhaa hizo kwani zinaweza kuwa na madhara kwa afya zao.

“Ndugu zangu athari za magendo siyo tu kukwepa kodi ya serikali, lakini pia bidhaa hizo zinazopita katika njia zisizo rasmi, zinakuwa hazijathibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na hivyo zinaweza kuwaletea madhara kiafya,” alisema Mahendeka.

Naye, Afisa Forodha kutoka TRA Ernest Mngube, amewaasa wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara za magendo kuacha tabia hiyo mara moja kwani wakibainika licha ya kuchukuliwa hatua za kisheria, watataifishiwa bidhaa zao ikiwa ni pamoja na vifaa vilivyotumika kubeba au kuhifadhi bidhaa hizo.

“Ni muhimu wafanyabiashara mtambue kwamba kupitisha bidhaa katika njia zisizo rasmi ni kinyume na sheria na mkibainika siyo tu mtachuliwa hatua kwa mujibu wa sheria bali bidhaa zenu zitataifishwa pamoja na vifaa kama gari, pikipiki, mashua zinazotumika bidhaa hizo na hata majengo yatakayokutwa yamehifadhi magendo hayo,” aliwaasa Mngube.

Mgumbe amezitaja namba ambazo wananchi wanaweza kutoa taarifa kila wanapoona biashara za magengo katika maeneo yao ambazo ni 0746 23 24 91, 0800 75 00 75, 0800 78 00 78 au kutuma ujumbe wa whatsapp kwenda namba 0744 23 33 33 au kutuma barua pepe kwenda huduma@tra.go.tz. 

Kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11 Februari, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi ikiwa na lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla madhara mbalimbali yatokanayo magendo hayo.

Mwisho.


Share:

WANAWAKE USHETU WAKERWA NA TATIZO LA KUJIFUNGULIA NJIANI

Na Salvatory Ntandu - Kahama
Tatizo la kufuata  huduma za matibabu umbali mrefu kwa wakazi wa kata ya kinamapula katika halmashauri ya Ushetu limetajwa kuchangia akinamama wajawazito kujifungulia njiani hali ambayo huhatarisha usalama wao na watoto wao.

Kauli hiyo imetolewa na Magdalena  bundala mkazi wa kijiji butibu mbele ya  kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya kahama mkoani shinyanga ambayo imefika katika kijiji hicho kwa lengo la kukagua ujenzi wa zahanati  mpya ya kijiji hicho uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 174.

“Akinamama wengi hujifungulia njiani kutokana na kutembea  umbali mrefu wa kilomita 12 kwenda zahanati kijiji cha  kisuke kupata matibabu na wakati mwingine hulazimika kukodi pikipiki kwa shilingi elfu 10000 kwa nyakati za usiku na kwa kipindi cha mvua za masika bei hupanda zaidi alisema”alisema bundala.

Alisema kuwa Kukamilika kwa zahanati hiyo kutasaidia kuondoa adha hizo walizokuwa wanazipata pindi wanapokuwa wanahitadi huduma za matibabu hususani kwa akinamama na watoto ambao ndio mara nyingi hukumbwa na magojwa mbalimbali.

Nae Elizabeth Maziku mkazi wa kijiji cha Butibu alisema kuwa kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wamekuwa wakipata shida kwenda kufuata dawa kutokana na umbali mrefu na wakati mwingine hulazimika kuacha dozi kama wanavyoelekezwa na wataalam.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kusikiliza kilio chetu cha muda mrefu cha kupata zahanati tunaimani tutapata huduma zote za kitabibu hapa ikiwemo dawa za watu wanaishi na virusi vya ukimwi ambazo tulikuwa tunalazimika kuzifuata katika zahanati ya kisuke ambayo ni mbali”alisema Maziku.

Kwa upande wake Kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya Ushetu Dk Nikodemas Senguo alisema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo umegharimu shilingi milioni 174 na unatarajiwa kukamili mwezi wa tatu mwaka huu fedha ambazo zimetolewa na serikali ya watu wa Japan.

“Niwatoe hofu wananchi wa kijiji hiki pindi ujenzi huu utakapo kamilika tuanza kutoa huduma za matibabu mara mmoja ili kuwasogezea huduma karibu wananchi “alisema Dk Senguo.

Nae katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya kahama Emanuel Mbamange alimtaka mkandarasi anayejenga zahanati hiyo kuhakikisha anajenga kwa kuzingatia ubora ili majengo hayo yaweze kudumu kwa muda mrefu na huduma kwa wananchi zianze kutolewa.

“Serikali ya awamu ya Tano chini ya Dk John Pombe Magufuli imelenga kusogeza huduma karibu na wananchi ndio maana sisi wasimamizi wa Ilani ya CCM tuko hapa kuangalia utekelezaji wake katika miradi mbalimbali ya maendeleoa katika halmashauri hii”alisema Mbamange.

Aliongeza kuwa Mwaka huu CCM inadhimisha  miaka 43 ya kuzaliwa kwake kwa kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yote iliyoainishwa kwenye Ilani yake katika maeneo mbalimbali ili kuona utekelezaji wake.

Maadhimisho ya miaka 43 ya CCM yanakwenda na kauli mbiu isemayo “tumeahidi,tumetekeleza na tunaahidi tena kuchapa kazi kwa juhudi,ubunifu na maarifa zaidi”.

Mwisho.


Share:

Mbunge Ataka Wabakaji Wahasiwe....Serikali Yagoma Yasema Adhabu Zilizopo Ni Kali Na Zinatosha.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imesema haiwezi kuongeza adhabu kali kwa wabakaji  zikiwemo adhabu za kuhasiwa  kwani zilizopo ni kali na zinatosha.

Hayo yamesemwa leo Feb.4.2020  jijini Dodoma na Waziri wa katiba na sheria  Balozi.Dkt.Augustne Mahiga wakati akijibu swali la  nyongeza la mbunge wa viti Maalum [CCM]Mhe.Zainab Katimba aliyehoji kutokana na vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike hususan ubakaji kuendelea kuripotiwa mara kwa mara ,je,serikali haioni namna ya kuongeza adhabu kali dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivyo.

Akijibu  swali hilo,Waziri wa Katiba na Sheria ,Balozi.Dkt.Augustine Mahiga amesema adhabu zilizopo kwa sasa ni kali kwani mtu aliyefanya kosa la ubakaji ni miaka 30 mpaka wengine wanafia magerezani.

Akilitolea ufafanuzi zaidi   juu ya suala hilo,Mwanasheria  mkuu wa Serikali Dkt.Adelardus  Kilangi amesema pendekezo la kuhasiwa litapekekea kuvunja katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika ibara  ya 13,ibara ndogo ya 6 ambapo inaeleza ni marufuku kwa mtu kuteswa,kuadhibiwa kwa kinyama au kupewa adhabu  zinazomtesa au kumdhalilisha .

Naye Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ,Mhe.Ummy Mwalimu amesema sheria peke yake hazitoshi na kinachotakiwa ni wazazi na walezi kutimiza wajibu katika ulinzi na malezi kwa watoto.


Share:

Rais Magufuli: Tusizuie Shughuli za Kidini na badala yake yashughulikiwe mapungufu yaliyojitokeza.

Rais  Magufuli amesema shughuli za kidini ama kiimani, hazipaswi kufungwa kutokana na maafa ya vifo vya watu 20 mkoani Kilimanjaro, yaliyosababishwa na watu kukanyagana, wakiwahi kukanyaga mafuta ya upako, badala yake yashughulikiwe mapungufu yaliyojitokeza.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ametoa ujumbe huo wa Rais Magufuli jana wakati wa mazishi ya kitaifa ya watu 19, kati ya 20, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa mjini Moshi. Watu hao walikufa baada ya kukanyagana walipokuwa wakifuata mafuta ya upako ya Mtume Boniface Mwamposa.

“Asubuhi wakati nazungumza na Rais kuhusu tukio hili, alisisitiza tushughulikie mapungufu yaliyojitokeza, badala ya kufunga shughuli za kiimani…mimi nasema tuzingatie vibali vyetu ili kuepusha maafa kama haya,” amesema Mghwira.

Alisema tayari Jeshi la Polisi, linafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo, ambapo pia viongozi waandamizi wa Mtume Mwamposa, wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Mghwira alisema pia baadhi ya watu, wanaodhaniwa ni vibaka, walikuwa miongoni mwa vyanzo vya watu kupata maafa hayo, kutokana na kitendo cha kujaribu kuwaibia waumini waliokuwa wakitoka mlangoni.

“Ninyi vibaka ambao ni sehemu ya maafa haya, lazima mjue damu ya watu iliyopotea na iliyomwagika, itakuwa juu yenu na malipo yenu yanakuja,” alisema mkuu wa mkoa.

Alisema tukio hilo limegusa pia wananchi wa mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro. Kwa upande wao, viongozi wa madhehebu ya dini, walisema wanapinga mfumo wa maombezi ya kidini, unaofanywa sasa kwa kasi, kwa kigezo cha kuleta uponyaji kwa waumini wao.

Aidha, viongozi hao waliomba serikali kutazama baadhi ya madhehebu, yanayotumia mgongo wa dini na ufahamu mdogo wa waumini katika kuwarubuni na kuwasababishia maafa.


Share:

Wanafunzi 14 wafariki kwa kukanyagana Kenya

Wanafunzi 14 wamefariki dunia huku wengine 39 wakijeruhiwa katika Shule ya Msingi Kakamega nchini Kenya kutokana na kukanyagwa na wenzao na kuanguka wakati wakikimbia.

Ajali hiyo imetokea Jumatatu Februari 3 majira ya saa 11 joni wakati watoto hao wakitoka madarasani kurejea makwao, ambapo tayari wanafunzi 20 waliojeruhiwa wameruhusiwa kutoka hospitali.

“Kumpoteza mtoto ni tukio linalouma sana. Natoa salamu za pole kwa wazazi wote waliofiwa na watoto wao,” Waziri wa Elimu, George Magoha amesema.

Kamanda wa Polisi wa Kakamega, David Kabena amesema chanzo cha tukio hilo hakijafahamika lakini amebainisha kuwa tayari uchunguzi umeanza.


Share:

Marekani yamaliza mafuzo ya kijeshi na kukabidhi vifaa kwa JWTZ

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson amekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 18 (Tsh bilioni 41.6) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama sehemu ya Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Afrika (African Peacekeeping Rapid Reaction Program – APRRP).

Ubia wa Majeshi ya Kulinda Amani ya Afrika (APRRP), ni ubia kati ya Marekani na nchi sita za Afrika ambazo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Senegal na Ghana wenye lengo la kujenga uwezo na utayari wa kutoa msaada wa kiuongozi na vifaa kwa oparesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU).

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, wakufunzi wa Kimarekani wamekuwa wakifanya kazi na kikosi cha JWTZ ambacho ni sehemu ya Kikosi cha Kimataifa cha Kulinda Amani ili kukijengea uwezo wa kushiriki katika operesheni za kulinda amani, utoaji misaada ya kibinadamu na huduma wakati wa majanga iwe nchini Tanzania na barani kote.

“Marekani itaendelea kuwa mbia imara wa JWTZ,” amesema Patterson katika hafla ya makabidhiano, na kuongeza kuwa “tutaendelea kuisaidia APRRP pamoja na mafunzo ya awali ya askari walinda amani wa Kitanzania.”


Share:

Wabunge Wataka Serikali Iruhusu Kilimo cha Bangi.....Ndugai Apigilia Msumari, Waziri Kairuki Asema Ofisi Yake Inasaka Wawekezaji

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Anjela Kairuki, amesema ofisi yake imepata wawekezaji wakubwa wawili ambao wameonyesha nia ya kuwekeza katika kilimo ikiwamo kuchakata mafuta ya bangi kwa ajili ya matibabu.


Kairuki alikuwa akimpa taarifa mchangiaji aliyekuwa akichangia mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba, aliyetaka serikali ipitishe jambo hilo mapema kabla bei ya bangi haijaporomoka.

Kishimba wakati anachangia mjadala huo alisema bei ya bangi duniani imepanda maradufu na nchi zote alizozizunguka wamesharuhusu kilimo cha zao hilo, hivyo anamwomba Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, atoe ufafanuzi kwamba watu wanaotaka kulima wamuone nani.

“Waliopiga marufuku bangi ni Wazungu miaka ya 40, lakini Wazungu walewale waligundua ndani ya bangi kuna dawa, na sisi wenyewe tunaenda kwenye viwanda vya dawa. Je, sisi tuki- import dawa zenye material ya bangi (tukiagiza dawa zenye malighafi itokanayo na bangi) tutakuwa tumeagiza kutoka wapi na tuta declare (kutangaza maslahi) namna gani. Kwa kuwa bei ya masoko duniani ni bei ya ushindani… ni vizuri serikali ifanye uamuzi huo mapema zaidi.

Kishimba aliongeza: “Tanzania kwa Afrika ni nchi ya tatu kwa kulima bangi kwa magendo na kama wataruhusu na sheria kama ilivyo inaweza sana ikatusaidia kutupeleka mahali. Lakini kwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (George Simbachawene) yuko hapa anaweza akatoa msamaha hata kwa bangi iliyokamatwa kwa muda wa miezi sita, kama msamaha anavyoutoa wa silaha.”

Kwa mujibu wa Kishimba, msamaha huo kama utatolewa na wananchi wakawasilisha bangi hizo Polisi, watu wakauziana bangi hiyo Polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watapata mapato na wanunuzi wakaja kununua hapa, linaweza kusaidia wenzetu wakapata pesa na kwa hali hiyo, lazima tuende haraka sana.

“Uganda wamepewa na Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU), zaidi ya Dola milioni 500 kwa ajili ya kilimo cha bangi, na kwamba kwa kuwa tulianza kulima bangi muda mrefu, lakini basi namuomba waziri wakati wowote kama watapitisha iwe mapema kabla bei haijaporomoka,” alisema.

Wakati Kishimba anachangia mjadala huo, Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma alisimama na kumpa taarifa akisema:

“Kikawaida Bunge linapotunga sheria kinachofuata ni kanuni tu, sasa nilikuwa nafikiria Mheshimiwa Waziri angetuambia kanuni ziko tayari ili tuanze kulima kwa sababu bangi itaporomoka bei.”

Baada ya michango hiyo ya wabunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema: “Niwa assue this is not a joke (niwahakikishie kwamba hili sio jambo la utani), anachochangia (Kishimba)… nilikuwa Canada majuzi hapa kwenye mkutano wa ma Spika wa Common Wealth (Jumuiya ya Madola) duniani. Ni big business in Canada (Ni biashara kubwa). Kwa hiyo anazungumza kitu cha msingi sana wala sio utani.

“Tena linaweza kuwa ni zao kubwa la biashara linaoweza kundoka kuliko mazao mengi tu kabisa, likafanya mapinduzi makubwa sana ya kipato. Kwa hiyo anachokizungumza Mheshimiwa Kishimba hazungumzi bangi itumike vile ambavyo tunavyofahamu inatumika hapa nchini.

“Tunazungumzia habari ya kilimo, moderated, monitored na taratibu zote halafu wanapelekewa wote wanaohitaji kwa ajili ya kutengeneza dawa za wanyama na binadamu.”
 


Share:

DKT NCHIMBI AJA NA MJALI MTOTO WA KIKE KWA MAENDELEO YA TAIFA,RAS DKT LUTAMBI APIGILIA MSUMARI




Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi  (mwenye nguo za kijani ) akiwapatia wanafunzi  wa Shule ya Sekondari Ikungi boksi la  taulo za kike. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi(mwenye suti nyeusi) Edward Mpogolo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi


 Wanafunzi wa shule ya Sekondari  ya Ikungi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi  mara baada ya kupokea maboksi ya taulo za kike kutoka kwa wadau mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye skafu) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi wakijadiliana  mara baada ya kutoka kwenye mkutano wa mafanikio  ya miaka 4 ya Rais Magufuli ambapo Waziri wa TAMISEMI Suleimani Jaffo alipongeza jitihada za Mkoa wa Singida kwenye utoaji wa huduma za afya.


Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi (mwenye suti ya Bluu)  akiwa  pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa Singida, Victorina Ludovick (mwenye sketi nyeusi)na Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Singida(mwenye suruali nyeusi), Mwalimu Eva Simon Mosha wakicheza kuhamasisha uchangiaji wa taulo za kike.

Na John Mapepele

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi  ametoa onyo kali kwa wawekezaji na wafanyabiasha wa kutengeneza na kuuza taulo za watoto wa kike  kuacha  mara moja tabia ya kutengeneza taulo zisizo  na ubora kwa kuwa Mkoa wake umeanzisha msako wa kiintelijensia na kistratejia wa kuzisaka taulo zisizo na ubora  ambapo  atakayebainika sheria itachukua mkondo wake mara moja.

Dkt Nchimbi ameyasema haya leo wilayani Ikungi wakati wa zoezi maalum la uzinduzi wa uchangishaji wa taulo za mtoto wa kike katika Mkoa wa Singida lililopewa jina la “Mjali mtoto wa kike kwa maendeleo yake na Taifa lake” ambapo ametoa rai kwa wadau wote kushiriki kikamilifu katika kuwabaini na kutoa taarifa za wafanyabiashara watakaojaribu kuuza taulo zisizo na ubora ili kuwalinda watoto wa kike

Alisema kutokana na mageuzi makubwa ya kiuchumi yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli nchi yetu imekuwa kwenye mashindano ya kiuchumi duniani hivyo mikakati madhubuti ya kudhibiti ubora unahitajika katika kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote.

Dkt Nchimbi alisema vyombo vya dola, viongozi wa dini na wazazi wana mchango mkubwa katika kumlinda mtoto wa kike kwa ustawi wa taifa letu.
“Ndiyo maana tunasema na tunamaanisha kuwa tunataka kujua mipango ya udhibiti wa ubora kwa watengenezaji hawa kwa kuwa majuto ni mjukuu, tusisubiri kufika huko “ alisisitiza Dkt .Nchimbi

Aliongeza kuwa ubora wa taulo za kike ni ubora wa maisha yao hivyo ni muhimu  kuchukua hatua za kuangalia na kudhibiti mnyororo mzima wa uzalishaji na usambazaji wa taulo sizizo kuwa na ubora.

Aidha alitoa wito wa wajasiliamali kuja na andiko zuri la utengenezaji wa taulo bora za kisasa zitakazotengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nchini ambapo alisema mshindi atakayepatikana atamzawadia tuzo  ya shilingi milioni moja.

Aliwataka watoto wa kike kote nchini kujiamini kwa  kuumbwa wanawake na kwamba hedhi ni kitu cha thamani kwa kuwa hedhi ni uhai ambapo alisisitiza  elimu ya jinsia na mtoto wa kike kutambua mabadiliko ya miili yao iendelea kutolewa ili kuwajenga watoto wa kike kujua thamani ambayo mungu amewajalia kwa kuwaumba wakamilifu.

Aliwataka wadau wote kuendelea kuchangia kwa kutambua thamani ya mtoto wa kike ambapo katika  uzinduzi wa huu lengo lilikuwa ni kuchangia paketi 8000 za taulo za kike lakini zilipatikana jumla ya paketi 9089 kulingana na fedha zilizotolewa.

Lengo la jumla kwa mwaka 2020 katika Wilaya ya Ikungi ni kuchangia taulo 192,000 kwa watoto wote wa kike kwenye shule 36 za Sekondari,  na shule  131 za Msingi  zenye jumla ya  watoto wa kike 16,000

Naye KatibuTawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina  Lutambi amesema Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao.

Dkt. Lutambi amesema Serikali inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake kwani afya bora ni raslimali muhimu kwa maendeleo. Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa wananchi wana afya bora, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.

“Serikali haitamfumbia macho mdau yoyote wa utoaji wa huduma ya afya ambaye atafanya kazi   kwa mazoea bila kuzingatia  sheria na taratibu za utoaji huduma na kwamba kuanzia sasa Serikali itakaa na kupanga  kwa pamoja ili kuwapatia wananchi huduma  bora wakati wote kwa wananchi wa Mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla” amesisitiza Dkt. Lutambi

Aidha, Waziri wa Nchi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo, amepongeza juhudi zinazofanywa  na Serikali ya Mkoa wa Singida kwenye  utoaji wa huduma za afya  wakati akiwasilisha  mafanikio ya TAMISEMI kwa kipindi cha miaka mine ya Rais Magufuli
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa wazo la kutaka Halmashauri zote katika Mkoa wa Singida kutoa elimu ya jinsia mashuleni na kuwachangia wa watoto wa kike taulo hizo kwa kuwa jambo lenye manufaa kwa taifa kwa kuwa ukimuelimisha mtoto  wa kike umeelimisha taifa zima.

Alizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike kuwa ni pamoja na mimba za utotoni,kubakwa,kuozeshwa katika umri mdogo na kufanyishwa kazi  nyingi nyumbani.

Mratibu wa program hii ya  uchangiaji wa taulo za mtoto wa kike ambaye pia ni Afisa Maendeleo wa jamii wilaya ya Ikungi Haika Massawe alipendekeza wazazi wahusishwe kikamilifu katika  program hii.

Alisema vyombo vya Serikali  kama polisi na mahakama  vitende  haki katika kushughulikia haki za mtoto wa kike aidha  wazazi wa wanafunzi wa kike mashuleni  waelekezwe kutoa fedha  maalum kwa ajili ya kununua taulo za watoto wao.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger