Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Maganga Masunga (42)mkazi wa Kitongoji cha Luhumbo, kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga amekutwa amefariki dunia katika eneo la daraja la barabara itokayo Shinyanga Mjini kuelekea kijiji cha Galamba.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao mwanaume huyo alikutwa amefariki dunia Julai 8,2019 majira ya saa moja usiku
Ameeleza kuwa "kwa mara ya mwisho marehemu aliondoka nyumbani kwake kuelekea kijiji cha Nobora kata ya Ukenyenge wilaya ya Kishapu kwa madhumuni ya kuangalia michezo ya ngoma za kienyeji iliyokuwa inafanyika kijijini hapo Julai 3,2019 saa mbili asubuhi".
Kamanda Abwao amesema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog