Wednesday, 5 June 2019

BENKI YA AKIBA YAKABIDHI VIFAA VYA USAFI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA 2019

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Juni 05, 2019, benki ya Akiba (Akiba Commercial Bank) imekabidhi vifaa vya usafi kwa uongozi wa Soko Kuu jijini Mwanza ili kuimarisha huduma ya usafi sokoni hapo.


Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo imeambatana na zoezi la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Soko Kuu jijini Mwanza ambapo wafanyakazi wa benki ya Akiba wamejumuika pamoja na wafanyabiashara sokoni hapo kufanya usafi huo.

Meneja wa benki ya Akiba tawi la Mwanza, Herieth Bujiku amesema lengo ni kuhakikisha kunakuwa na zoezi endelevu la kufanya usafi katika soko hilo na kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kuzuia magonjwa ya milipuko huku akitoa pongezi kwa Serikali kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba aliyepokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella na kuvikabidhi kwa uongozi wa Soko Kuu jijini Mwanza, amesema vifaa hivyo vina umuhimu mkubwa wa kuimarisha usafi na hivyo wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira safi na salama kiafya.

Naye Mwenyekiti wa Soko Kuu jijini Mwanza, Hamad Nchola ameishukru benki ya Akiba kwa kutoa vifaa hivyo na kuomba liwe zoezi endelevu huku akitoa rai kwa wafanyabiashara sokoni hapo kuvitumia vyema kuimarisha usafi kama ilivyo desturi yao ya kufanya usafi kila jumamosi.
Meneja wa benki ya Akiba (Akiba Commercial Bank) tawi la Mwanza, Herieth Bujiku (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba (wa pili kushoto) vifaa vya usafi vilivyotolewa na benki hiyo ili kuimarisha hali ya usafi eneo la Soko Kuu jijini Mwanza. Zoezi hilo limeambatana na shughuli ya usafi sokoni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2019.
Meneja wa benki ya Akiba (Akiba Commercial Bank) tawi la Mwanza, Herieth Bujiku (kulia) akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi ili kusaidia huduma ya usafi katika Soko Kuu jijini Mwanza. Hafla hiyo imeambatana na zoezi la usafi sokoni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2019.
Vifaa vilivyokabidhiwa na benki ya Akiba ni pamoja na mifagio, mapipa ya kutunzia taka, koleo, reki, buti za usafi, glovusi, toroli na maski.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa Soko Kuu jijini Mwanza, Hamad Nchola (kushoto) vifaa vya usafi vilivyotolewa na benki ya Akiba. Kulia ni Meneja wa Benki ya Akiba tawi la Mwanza, Herieth Bujiku.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba (wa tatu kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Soko Kuu jijini Mwanza, Hamad Nchola (wa pili kushoto) vifaa vya usafi vilivyotolewa na benki ya Akiba.
Meneja wa benki ya Akiba tawi la Mwanza, Herieth Bujiku akisoma taarifa fupi kuhusu vifaa vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2019.
Meneja wa benki ya Akiba tawi la Mwanza, Herieth Bujiku akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba amehimiza vifaa vya usafi vilivyotolewa na benki ya Akiba kutumika vyema kuimarisha usafi katika Soko Kuu jijini Mwanza ambalo amesema miezi michache ijayo litaanza kujengwa upya kuwa la kisasa zaidi.
Mwenyekiti wa Soko Kuu jijini Mwanza, Hamas Nchola akitoa salamu za shukrani kwa benki ya Akiba baada ya kupokea vifaa vya usafi.
Afisa Mazingira (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza), Mangabe Mnilago akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Akiba jijini Mwanza wakijumuika na wafanyabiashara Soko Kuu jijini Mwanza kufanya usafi katika maeneo ya soko hilo. 
Wafanyakazi wa benki ya Akiba wakifanya usafi katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani 2019.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Akiba wakiwa kwenye usasi katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Akiba jijini Mwanza wakijumuika na wafanyabiashara Soko Kuu jijini Mwanza kufanya usafi katika maeneo ya soko hilo. 
Wafanyakazi wa benki ya Akiba wamejumuika na wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza kufanya usafi sokoni hapo ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani, Juni 05, 2019.
Wafanyakazi wa benki ya Akiba wakiendelea na usafi eneo la Soko Kuu jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa benki ya Akiba (Akiba Commercial Bank) wakiondoa uchafu katika eneo la kukusanyia uchafu lililopo Soko Kuu jijini Mwanza.
HOTUBA YA FUPI YA MENEJA WA TAWI LA MWANZA BI: HERIETH BUJIKU ILIYOSOMWA KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI VIFAA VYA USAFI KWA UONGOZI WA SOKO KUU LA MWANZA KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI.



Mheshimiwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza

Uongozi wa Soko la Kuu Mwanza

Ndugu Wanahabari

Wafanya biashara kutoka soko kuu Mwanza

Mabibi na Mabwana

Itifaki ikizingatiwa



Ndugu Mgeni Rasmi

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa ajili ya siku njema ya leo. Nasema ni siku njema kwani sisi kama Benki ya Akiba tumefarijika sana kupata fursa hii ya kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi katika soko kuu la Jiji la Mwanza.


Soko hili ni kati ya masoko makubwa sana hapa Mwanza na linapokea bidhaa nyingi kutoka sehemu mbali mbali za kanda ya ziwa. Kwa hiyo ni soko ambalo linasaidia kuinua maisha ya wakulima pamoja na kutoa ajira kwa watu mbali mbali. Sisi kama Benki ya Akiba tunao wateja wengi tu tunaowahudumia kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo mikopo ambayo inasaidia kukuza mitaji na kuendeleza biashara za wafanyabiashara mbali mbali katika soko hili.



Ndugu Mgeni Rasmi

Benki ya Akiba inatambua na inathamini mazingira na ni mdau mkubwa katika harakati za kutunza mazingira. Najivunia kusema hilo kwani sera ya Akiba ya huduma za kijamii yaani Corporate Social Responsibility imeweka kipengele cha mazingira kama sehemu mojawapo ambayo Benki itakuwa inashughulikia katika kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii inayoihudumia.



Kwa kudhihirisha hili napenda kusema kuwa Benki inafanya jitihada nyingi katika eneo hili mathalan Benki imechukua jukumu la kuendeleza na kutunza Viunga vya bustani ya Indepence Square vilivyopo jijini Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi yetu. Viunga vipo katika mandhari nzuri kabisa ya kuvutia na vinapendezesha sana muonekano wa jiji la Dodoma. Jitihada hizi zilianza kuanzia mwaka 2013 na napenda kusema kuwa zoezi hili kwetu litakuwa la kudumu na endelevu.



Pia napenda kusema kuwa jitihada zetu za kufanya usafi pamoja na kuhakikisha kuwepo kwa zoezi endelevu la usafi limedhihirika sehemu mbali mbali kama Soko la Tandale,Buguruni Jiji la Mbeya n.k. Maeneo haya yameweza kufaidika na huduma hii pamoja na kukabidhiwa vifaa vya usafi kwa ajili ya kuhakikisha kuwepo kwa usafi endelevu. Vivyo vivyo kwa leo hapa Soko Kuu Mwanza zoezi hili linahitimishwa kwa kukabidhi vifaa vya usafi kwa uongozi wa soko kwa ajili ya matumizi ya baadaye.



Ndugu Mgeni Rasmi

Benki ya Akiba ni Benki ya Kibiashara ambayo imejikita kuhudumia wananchi wa hali ya chini na wa kati kwa lengo la kuboresha maisha yao na kuinua jamii kiujumla. Benki hii inatoa huduma zote za kibenki kama nilivyoainisha hapo mwanzo yaani mikopo, amana mbali mbali, kutuma na kupokea fedha nje na ndani ya nchi. Huduma nyinginezo kama za mawakala wa kuuza na kupokea float zinapatikana na Mawakala wa kuuza float yaani M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Halo Pesa n.k wanahudumiwa kwa haraka bila kusimama foleni na wengi wao wameweza kukuza mitaji yao kupitia mikopo tuliyowapa.


Huduma nyingine za kurahisisha upatikanaji wa huduma za Kibenki kupitia simu za mikononi yaani Akiba Mobile inaptika masaa 24 na imeleta faraja na unafuu kwa wateja wetu kwani inarahisisha na kuokoa muda. Wateja wengi wanatumia huduma hii kuweka fedha kwenye akaunti zao, kufanya marejesho ya mikopo pamoja na mahitaji mengi kama kulipia ving’amuzi, LUKU, bili za maji n.k.



Aidha, huduma za kuuza na kununua fedha za Kigeni zinapatikana katika matawi yetu na tunawakaribisha mtutembelee kwa ajili ya mahitaji yenu yote ya kuuza na kununua fedha kigeni. Pia huduma ya E-statement inapatikana; huduma hii inaleta wepesi wa mteja kupata taariza za akaunti yake kwa urahisi pasipo kwenda Benki kupitia simu ya mkononi, kompyuta n.k. Mteja anatakiwa tu aende kwenye tawi lake kuhakiki taarifa zake pamoja na kutoa anuani ya barua pepe au E-mail address.



Manufaa ya huduma ya E-statement hayaishii kwa mteja kwani yanasaidia pia katika utunzaji wa mzingira kwa sababu inapunguza na kuondoa matumizi ya karatasi. Hii pia ni jitihada za Benki za kutunza mazingira inaonyesha jinsi ambavyo Benki ya Akiba ni Rafiki Bora wa mazingira.



Ndugu Wanahabari

Kwa kuhitimsha naomba niwashukuru wote kwa kutuunga mkono katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani amabayo kauli mbiu ya mwaka huu ni "Kupinga Uchafuzi wa Hewa- yaani Air Pollution", sisi kama benki tunauunga na dunia katika hilo kwani tunatambua umuhimu wa kuwa na hewa safi. Takwimu zinasema kwamba 92% ya watu duniani hawavuti hewa safi hili ni tatizo kubwa sana na zinahitajika juhudi za makusudi kwa ajili ya kupambana na tatizo hili kwani linahatarisha afya za watu pamoja na viumbe hai wengine na mazingira kwa ujumla.



Ndugu Mgeni Rasmi

Kwa niaba ya Benki ya Akiba naomba pia nitoe pongezi kubwa kwa Serikali ya awamu ya tano kufuatia juhudi za makusudi za kupiga marufuku matumzi ya mifuko ya Plastiki ambayo kwa kwa kweli inaleta uharibifu mkubwa kwa mazingira. Sisi kama taasisi pia tupo mstari wa mbele katika kutekeleza agizo hili na tunatoa rai kwa wananchi wote hususan wakazi wa Mwanza kuachana na matumizi ya vitu hivi kwa ajili ya kutunza mazingira yetu ili kuhakikisha urithi bora wa vizazi vijavyo.


Mwisho kabisa, naomba nichukue fursa kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi vikiwemo fagio, mapipa ya kutunzia taka, koleo, rake, buti za usafi, gloves, toroli, masks na vingine kwa uongozi wa soko kwa matumizi ya badae. Lengo ni kuhakikisha kuweko kwa zoezi endelevu la usafi katika soko hili kwa ajili ya kutunza mazingira na kuzuia magonjwa ya milipuko. Hili eneo ni muhimu sana kwa jamii kwani mahitaji ya chakula yanapatikana sana katika soko hilo. Kwa umuhimu huo basi naomba uongozi wa soko undelee kutilia mkazo wa usafi katika eneo hili kwani eneo lenye mahitaji muhimu kama haya linahitaji kutunzwa kwa umakini mkubwa.



Asanteni sana kunisikiliza

Herieth Bujiku – Meneja wa Tawi la Mwanza

Akiba Commercial Bank.

Tazama video hapa chini

Share:

Picha : WATANZANIA WAISHIO DENMARK,ICS,CIS WASHEREHEKEA SIKUKUU YA EID -EL-FITR NA WATOTO WENYE UALBINO SHINYANGA


Shirika lisilo la kiserikali la Investing in Childrean and Societies (ICS Africa) kwa kushirikiana na Watanzania Waishio Denmark,shirika la CIS na familia ya Robert Mugaya iliyopo Marekani wamesherekea Sikukuu ya Eid El-Fitr pamoja na Watoto wenye mahitaji maalumu (wenye ualbino,wasiosikia na wasioona) waliopo katika bweni la Shule ya Msingi Buhangija 'Kituo cha Buhangija' Mjini Shinyanga.


Wadau hao wa watoto wameungana na watoto hao leo Juni 5,2019 kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa kucheza,kunywa,kula pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali  ikiwemo sabuni,pipi na biskuti.

Akizungumza wakati wa sherehe hizo,Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania linalohusika na masuala mbalimbali ikiwemo malezi na makuzi bora ya watoto,ulinzi na usalama kwa watoto, Kudely Sokoine Joram amesema wanapenda watoto hivyo furaha yao ni kuona watoto hao wanafurahi kama watoto wengine katika jamii.

“Tumefanikisha jambo hili kwa kushirikiana na Watanzania wenzetu waishio Denmark,shirika la CIS la Denmark na familia ya Robert Mugaya iliyopo Marekani .Tumekuja hapa kusherehekea na watoto sikukuu ya Eid El Fitr lengo ni kuwafanya watoto hawa wajione wanathaminiwa,wanapendwa na tunawajali waone kuwa wao ni sehemu ya jamii”,ameeleza Sokoine.

“Watoto hawa wengi wakiwa ni wenye ualbino wanaishi pamoja hapa Buhangija,tumeona ni vyema kusherehekea nao pamoja tofauti na watoto waliopo majumbani ili kuwapa furaha.Tunaushuru serikali na uongozi wa shule kwa kuturuhusu kujumuika nao. Kwa kweli watoto wamefurahia sana”,amesema Sokoine.

Sokoine ameongeza kuwa wataendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha wanapata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili shule ya Buhangija ‘Kituo cha Buhangija

“Sisi ICS Africa kwa kushirikiana na marafiki zetu tutashirikiana na serikali kutatua changamoto zilizopo hapa,Tukio la leo ni hatua za mwanzo za kutengeneza mahusiano lakini Mwenyezi Mungu akitujalia tuna kazi kubwa ya kufanya hapa shuleni siku zijazo”,amesema.

Aidha amewataka watoto hao kuwa watiifu,kufuata maelekezo wanayopewa na walimu na kusoma kwa bidii,kushirikiana na kuwapenda wenzao ili waweze kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wao,watoto hao wameeleza kufurahia ujio wa wadau hao huku wakizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni ukosefu wa fensi na taa kwenye mabweni mapya yaliyojengwa hivyo kuomba wadau kujitokeza kuwasaidia.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI
Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akizungumza na watoto wenye ualbino,wasioona na wasiosikia katika bweni la Shule ya Msingi Buhangija wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Eid - El-Fitr leo Juni 5,2019. Sherehe hiyo imeandaliwa na shirika la ICS kwa Kushirikiana na Watanzania waishio Denmark na Marekani - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akizungumza na watoto wanaoishi katika bweni la Buhangija.
Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram na watoto wakizungumza live kwa njia ya simu 'Video Call' na Watanzania waishio Denmark ambao hawajafanikiwa kufika Buhangija kusherehekea Sikukuu ya Eid El-Fitr pamoja na watoto.
Kulia ni Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akikabidhi zawadi ya sabuni za kufulia maboksi nane kwa ajili ya watoto hao.
Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akishikana mkono na mtoto wakati wa kukabidhi zawadi ya sabuni kwa niaba ya Watanzania waishio Denmark,shirika la CIS na familia ya Robert Mugeta iliyopo USA.
Watoto wakishindana kucheza muziki.
Watoto wakiimba na kucheza.
Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akicheza wimbo wa Diamond Platnmuz 'Tetema' na Watoto.
Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akitoa zawadi ya pipi kwa watoto waliocheza muziki.
Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya Mambo ya Ndani, Monica Dawa akigawa juisi kwa watoto.
Kila mtoto akipata zawadi ya biskuti.
Zoezi la kugawa zawadi likiendelea.
Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akitoa maelekezo wakati wa ugawaji zawadi kwa watoto huku akiwa ameshikilia mifuko ya pipi za vijiti.
Zoezi la ugawaji zawadi likiendelea.Katikati mwenye tisheti ni Afisa Miradi wa shirika la ICS, Sophia Singu akigawa juisi. 
Watoto wakicheza wimbo wa msanii wa nyimbo za asili Bhudagala 'Kundi wa Ng'wamoto'.
Watoto wakicheza ngoma za asili 'Wimbo wa msanii Ng'wana Ishudu'
Watoto wakisakata ngoma.
Watoto wakilishukuru shirika la ICS na Watanzania waishio Denmark,shirika la CIS na familia ya Robert Mugeta iliyopo USA kwa kusherehekea nao pamoja sikukuu ya Eid na kueleza changamoto ya ukosefu wa fensi na taa kwenye mabweni mapya.
Mwakilishi wa mkuu wa shule ya msingi Buhangija akitoa neno la shukrani kwa shirika la ICS na Watanzania waishio Denmark,shirika la CIS na familia ya Robert Mugeta iliyopo USA.
MC wakati wa sherehe hizo,Mwalimu Jackson Leonard akizungumza.
Mwalimu mlezi wa watoto hao,Flora Gelard akizungumza na kueleza changamoto walizonazo kuwa ni kukosa ajira hivyo wanafanya kazi kwa kujitolea zaidi.
Muda wa msosi ukawadia : Watoto wakichukua chakula.
Ugawaji chakula kwa watoto ukiendelea. Nyama ya kuku,nyama ya ng'ombe,pilau,chips,matunda,maji,soda kama kawaida.
Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya Mambo ya Ndani, Monica Dawa akiwafungulia soda watoto huku wakiendelea kula chakula.
Huku Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akigawa soda upande mwingine Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya Mambo ya Ndani, Monica Dawa akifungua soda.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija.
Picha ya pamoja baada ya sherehe : Kikosi kilichofanikisha maandalizi ya sherehe za sikukuu ya Eid El Fitr kwa watoto wenye ualbino,wasioona na Wasiosikia katika bweni la Buhangija mjini Shinyanga,
.
Picha zote na Kadama Malunde -  Malunde1 blog
Share:

KAKA WAWILI WAMUUA MPENZI WA MAMA YAO BAADA YA KUMFUMANIA NDANI

Kaka wawili kutoka kijiji cha Kilungu kaunti ya Makueni nchini Kenya wamekamatwa baada ya kumshambulia na kumuua jamaa aitwaye Onesmus Kivuna aliyedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama yao.

 Wawili hao wanasemekana kumvamia jamaa huyo akiwa kwenye nyumba ya mama yao majira ya saa nne usiku Jumanne Juni 4,2019 na kumkatakata Onesmus Kivuna kwa panga hadi akafariki dunia. 

 Maafisa wa polisi waliupata mwili wa marehemu kwenye kichaka kilichoko mita 300 kutoka kijiji chake cha Mbukuni kata ndogo ya Kilome. 

Kulingana na taarifa ya polisi, marehemu alikuwa na majeraha mabaya kwenye shingo na kichwani, ishara kwamba alikatwa kwa panga. 

Naibu kamishna wa kaunti ya Makueni Rebecca Ndirangu alithibitisha kisa hicho na kusema mama huyo pamoja na washukiwa wanazuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.

 Jirani wa mama huyo ambaye pia ni mjane, Muthini Kilonzo anasema kwamba marehemu alikuwa ameonywa mara kadhaa na vijana hao dhidi ya kumtongoza mama yao ila hakutilia maanani onyo hilo.

 " Nilikuwa mwendo wa saa nne usiku ambapo tulisikia mtu akipiga yowe akiomba usaidizi, tulipofika kwa jirani yetu, tulimpata jamaa huyo akiwa sakafuni akivuja damu nyingi, alikuwa na majeraha mabaya kwenye shingo na kichwani, "Kilonzo alisema.

 Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha hospitali ya Kilungu. 
Chanzo- Tuko
Share:

MAKALA: Mbinu Za Kupanga Jinsia Ya Mtoto Wakuzaa ( Mvulana Au Msichana ) Kabla Mkeo Hajashika Mimba

Mpendwa  msomaji  wetu, Maada  yetu  nyingine  ya  leo  ni  mbinu za kupanga  jinsia  ya  mtoto  wa  kuzaa  kabla  mkeo  hajashika  mimba....

Siku  hizi  ulimwengu  umeendelea  sana, matatizo  mengi  yanatibika  kwa  msaada  wa  wataalamu...Hakuna   tena  haja  ya  kupigana  na  kupeana  talaka  kisa  jinsia  ya  mtoto...

Somo letu   la  leo  litajikita  zaidi  katika  mbinu  za  kuzaa  mtoto  wa  kike. 


Ni vipi jinsia ya mtoto huainishwa?
Kinyume na wengi wanavyofikiria kwamba mwanamke au mwili wa mwanamke ndio wenye jukumu la kuainisha jinsia ya mtoto kwa kuwa yeye ndiye anayebeba mimba, uhakika wa mambo ni kuwa mwanamume ndie mwenye uwezo wa kuainisha jinsia.
 
Kila yai la mwanamke lina chromozomu mbili za X. Iwapo manii ya mwanamume au spemu(ambayo ina chromozomu X na Y) itakuwa na X na kurutubisha yai la mwanamke lenye X tupu, basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanamke.
 
Vilevile iwapo spemu ya mwanaume itakuwa na Y na kurutubisha yai la mwanamke lenye X, basi mtoto atakayezaliwaatakuwa mwanamume.
 
Hivyo kwa kufahamu suala hilo, ni matumaini yetu kuwa vile visa vya kinamama kuachwa eti kwa kuwa hawakuzaa watoto wa kiume au wa kike vitapungua katika jamii zetu. Mke wako asipozaa mtoto wa jinsia uitakayo, usifikiri kuwa yeye ndiomwenye makosa.
 
Wakati mwanamume anapomwaga mbegu, spemu kati ya milioni 200 hadi 400 humwagwa katika uke wa mwanamke. Baadhi ya spemu hizo huwa zina chromozomu X na baadhi zina chromozomu Y.
 
Hata hivyo, ni spemu moja tu ambayo hutakiwa kwa ajili ya kurutubisha yai la mwanamke nakuunda mimba.
 
Nadharia mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kuchagua ni jinsia gani unaitaka awe nayo mwanao, zinategemea suala la kuandaa mazingira katika uke na mwili wa mwanamume na mwanamke,yatakayosaidia spemu ya baba yenye chromozomu inayotakiwa irutubishe yai la mama, na hivyo kutungwa mimba ya jinsia inayotakiwa.
 
Njia ya Dr. Shettles ya kuzaa mtoto wa kike
Njia hii imekuwa ikitumiwa na watu wengi kwa miaka mingi sana na imewasaidia kuweza kuzaa mtoto wa kike.
 
Wengi wanasema kuwa uwezekano wa kufanikiwa njia hii ni asilimia 90. Njia ya Dr. Shettles inategemea msingi kwamba, chromozomu Y (yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kiume) ni ndogo na yenye kwenda kwa kasi zaidi ikilinganishwa na chromozomu X(yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kike) ambayo ni kubwa na huenda polepole.
 
Pia kwa kutegemea kuwa chromozomu X inaishi muda mrefu zaidi kuliko ile ya Y.Hivyo Dr. Shettles anashauri kuwa iwapo unataka kuzaa mtoto wakike uhakikishe kuwa:
 
1.Unajamiiana siku 2 au 3 kabla ya Ovulation. Kinadharia spemu za kiume zitakuwa zimeshakufa hadi kufikia siku hasa ya Ovulation na kuziacha spemu za kike zikiwa hai tayari kurutubisha yai na kuunda mtotowa kike.
 
2.Anashauri pia wanawake wajizuie kufikia kileleni (orgasm) kwani hali hiyo itaufanya uke uwe na hali ya asidi ambayo ni kwa faida ya spemu ya kike yenye chromozomu X.
 
3.Pia anawashauri wazazi wanapojamiina wawe katika haliya mwanamke kulala chini na mwanamume juu au missionary position. Kwani anasema kuwa mtindo huo huziwezesha spemu zenye chromozamu X zimwagike karibu na mlango wa uke na kuwa na uwezekano mkubwa wa kuingia ukeni na kutungwa mimba.
 
Njia ya O+12
Njia hii inamaanisha Ovulation jumlisha siku 12 na ilivumbuliwa na mama mmoja wa Australia aliyekuwa akihangaika kupata mtoto wa kike baada ya kuzaa watoto 6 wa kiume.
 
Mama huyo anawahusia wale wanaotaka kubeba mimba ya mtoto wa kike wajamiiane masaa 12 baada ya Ovulation.
 
Mama huyo alifuata njia ya Dr. Shettles bila mafanikio katika mimba zake za nyuma. Lakini baada ya kugundua njia yake hii mwenyewe mwishowe alibeba mimba na kujifungua mtoto wa kike.
 
Kuna wengine wanaamini kwamba baadhi ya lishe na vyakula vya aina mbalimbali husaidia kutunga mimba ya mtoto wa kike.
 
Kwa mfano kuna wanaoamini kuwa kula baadhi ya vyakula huufanya uke uwe na hali ya asidi ambayo husaidia Chromozomu Y ife katika uke.
 
Nadharia nyingineyo inayotumiwa katika kuchagua jinsia ya mtoto inasema kwamba,mwanamke anayetaka kubeba mimba ya mtoto wa kike ale vidonge vya virutubisho (supplements) vya Calcium na Magnessium mwezi mmoja kablaya kubebea mimba.
 
Iwapo unataka kutumia vidonge vya virutubisho ili uweze beba mimba ya mtoto wa kike, ni bora ushauriane na daktari wako kwanza.
 
Hii ni kwa sababu dawa hizo huweza kuingiliana na dawa nyinginezo za magonjwa mbalimbali.
 
Baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa vinasaidia katika kutunga mimba ya mtoto wa kike ni.
 
-->>>Mahindi, nyama, maharagwe, samaki, tunda damu, mayai na maini.
 
Vyakula hivyo ni vya asidi hivyo huifanya PH ya mwili wako hupungua na kuwa ya acidi. Hali hiyo husaidia kuua spemu za Y na hivyo kusaidia kuzifanya spemu za X ziwe na uwezekano mkubwa wa kurutubisha yai.
 
Hivyo mwanamke anayependelea kubebea mimba ya mtoto wa kike anashauriwa kutokula vyakula vyenye alikali ambavyo ni kama, ndizi, chokleti, juisi ya machungwa, viazi, tikiti maji na vinginevyo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger