Ugumba ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili (au kujamiana) bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12 na kutoweza kushika mimba au kupata ujauzito.
Kuna aina mbili za ugumba;
Ugumba wa asili (Primary infertility) - Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutunguisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiana au kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.
Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) - Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.
Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25-30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini.
Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.
Je mimba hutungwa vipi?
Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya viwanda vyake vya mayai ya kike yaani ovaries, kitendo hiki hujulikana kama ovulation.
Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija ya fallopian.
Mbegu moja ya kiume (sperm) ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye uterus.
Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa kiumbe.
Tatizo la ugumba linaweza likawa ni la nwanaume au mwanamke pekee ingawa wakati mwingine wote wawili wanaweza kuwa na tatizo hili.
Ni sababu zipi zinazoleta tatizo la ugumba (infertility) ?
Kwa wanawake ;
Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa;
- Yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko (uterus) wa uzazi kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto.
- Mayai yaliyo ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining)
- Matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi (uterus).
- Matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai (eggs).
Tatizo la ugumba kwa wanawake husababishwa na;
- Matatizo ya auto immune disorders kama antiphospholipid syndrome (APS)
- Matatizo katika uterus na shingo ya kizazi (cervix) kama uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects
- Matatizo katika mfumo wa kuganda wa damu (clotting disorders).
- Mazoezi kupita kiasi (excessive exercise), afya iliyodhoofika (poor nutrition), matatizo ya kula (eating disoder).
- Baadhi ya madawa au sumu.
- Msongo wa mawazo (emotional stress)
- Tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance)
- Uzito uliopitiliza (obesity)
- Unywaji pombe kupindukia (heavy alcohol intake)
- Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari (diabetes)
- Magonjwa ya kina mama (Pelvic inflammatory infection, PID)
- Ovarian cysts and polycytic ovarian syndrome
- Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted disease, STD) au endometriosis
- Saratani
- Uvutaji sigara, madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk.
- Matatizo ya hedhi - wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai (anovulatory menstrual cycle)
- Kuwepo kwa cervical antigens ambazo huua shahawa za mwanamume na hivyo kusababisha kwa mwanamke kutopata ujauzito.
Tatizo la ugumba - linaweza kutokea kwa mwanamume wakati wa;
- Kupungua idadi ya mbegu za kiume (decrease number of sperm)
- Nguvu za kiume kuzuiwa kutolewa (blockage of sperm)
- Manii ambazo hazifanyi kazi yake vizuri.
Kwa mwanamume, tatizo la ugumba husababishwa na;
- Mazingira yaliyo na kemikali zinazoathiri uwezo wa mwanaume kumbebesha mimba mwanamke (environment pollutants)
- Kukaa sehemu zenye joto kali sana kwa muda mrefu (exposure to high heat)
- Matatizo kwenye mfumo wa viashiria vya asili (genetic abnormalities)
- Unywaji pombe kupindukia, matumizi ya madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk, hupunguza idadi na kiwango (quality) cha shahawa .
- Kuzeeka (older age)
- Kutumia dawa za vichocheo vya mwilini (hormonal supplements) ama kukosekana kwa baadhi ya vichocheo mwilini (hormonal deficiency)
- Kuasiliwa (impotance)
- Magonjwa ya korodani (testicular infections) au kwenye mishipa ya korodani (epididymis)
- Historia ya matumizi ya baadhi ya dawa za saratani
- Magonjwa ya zinaa (STD), ajali (trauma) au upasuaji
- Historia ya mionzi (radiation exposure)
- Retrograde ejaculation (matatizo ya kukojoa au kutoa shahawa)
- Msongo wa mawazo (emotional stress)
- Uvutaji sigara
- Matumizi ya baadhi ya dawa kama cimetidine, spironolactone, nitrofurantoin.
- Varicocele
- Mumps
Viashiria na vipimo vya ugumba (infertility)
Kwa wanaume;
- Semen analysis - Kipimo hiki kinahusisha uchukuaji wa shahawa kutoka kwa mwanamume ambaye amekaa siku 2-3 bila kujamiana na kuzipima kujua wingi, kiwango chake, shepu zake, viscosity of semen, motility and swimming speed.
- Testicular biopsy - Kipimo cha korodani
Kwa wanawake;
- Kipimo cha kiwango cha vichocheo kwenye damu (blood hormone levels)
- Cervical mucus detection - Kipimo cha kuangalia kamasi za kwenye shingo ya kizazi ili kupima jinsi zinavyovutika (stretch), na kama ni za majimaji (wet) wakati wa mzunguko wa hedhi, na kama zina utelezi ambao huusishwa na ovulatory phase
- Kipimo cha kiwango cha joto mwilini (body basal temperature) - Kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa 1 degree kutoka kiwango cha joto cha kawaida cha binadamu (37 C) kinahusishwa na ovulation ambapo mwanamke ana asilimia kubwa ya kushika ujauzito au yai limetolewa na ovaries.
- Postcoital testing - Kupima kamasi za shingo ya kizazi (cervical mucus) zilizochukuliwa masaa 2-8 baada ya wapenzi kujamiana ili kuangalia mwiingiliano wa shahawa na kamasi za shingo ya kizazi.
- Kipimo cha kichocheo aina ya progesterone kwenye damu (serum progesterone testing)
- Kipimo cha ukuta wa uterus (biopsy of uterine lining or endometrium)
- Kupima kichocheo aina ya Luteinizing hormone kwenye mkojo ili kuweza kutabiri lini yai litatolewa na ovaries ili kupangilia siku za kujamiana kwa wapenzi.
- Hysterosalpingography (HSG) - Kipimo cha X-ray kinachotumia dawa maalum (contrast dye) inayoonyesha njia ya shahawa kutoka kwenye shingo ya kizazi kupitia ndani ya mfuko wa kizazi (uterus) na kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes).
- Laparascopy - Direct visualization of pelvic cavity
- Progestin challenge
- Pelvic exam-hufanywa na daktari.
Tiba ya tatizo la ugumba (infertility)
Tiba ni kama ifuatavyo;
1.Ushauri nasaha na kuwaelimisha wapenzi wawili - Matatizo mengi ya ugumba hutokea kutokana na uelewa au ufahamu mdogo wa elimu ya uzazi na ya kujamiana kwa wapenzi au wanandoa.
Kuna wanaume wengi ambao hufika kilele haraka wakati wa kujamiana na hivyo kutoa mbegu mapema (au kukojoa) kabla ya muda muafaka (premature ejaculation), hii husababisha kutopata ujauzito ambapo lawama zote hupelekwa kwa mwanamke pasipo mwanamume kugundua kuwa tatizo ni lake.
Ifahamike kwamba hakuna muda uliotengwa ambao ni muafaka wa kufika kilele au kukojoa kwa mwanamume lakini watafiti wa mambo ya kujamiana wanashauri angalau mwanamume afike au akojoe baada ya dakika 15 na kuendelea. Hivyo ni bora kwa wapenzi kujiandaa kisaikolojia mwanzo na kuchezeana kabla ya kuanza kujamiana ili kurefusha muda kwa mwanamume.
2.Tatizo jengine ni kutofahamu lini hasa ni muda muafaka wa kujamiana ili kushika mimba kwa urahisi. Kuna wanawake ambao hawajui hata mzunguko wao wa hedhi (yaani hawajui wanaanza na kumaliza hedhi lini na wakati wa hedhi wanatumika kwa muda wa siku ngapi).
Ongeza nafasi yako ya kushika ujauzito kwa kujamiana angalau mara 3 kwa wiki kuelekea wakati wa ovulation au kujamiana wakati wa kipindi chote cha ovulation. Ovulation hutokea wiki 2 kabla ya mzunguko wako mwengine wa hedhi, kama una mzunguko wa hedhi wa siku 28 (yaani kila baada ya siku 28 unapata hedhi), ni vizuri kujamiana angalau kwa siku 3 kati ya siku ya 7-18 baada ya kupata hedhi.
3.Kupunguza kunywa pombe kupindukia, kuvuta sigara, kuacha matumizi ya bangi, kokeni nk.
4.Kupunguza kiwango cha mazoezi kwa wanawake.
5.Kupunguza unene uliopitiliza
6.Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu kwani kuwa na wapenzi wengi huongeza athari ya kupata magonjwa ya zinaa.
7.Kuacha tabia ya kuvaa nguo nzito au zenye kuleta joto kali sehemu za siri kwa wanaume kwani joto kali sana hupunguza kiwango na kuathiri utolewaji wa mbegu
8.Kula mlo kamili na wenye virutubisho vyote muhimu kwa afya njema.
9.Dawa za kutibu magonjwa kwenye mfumo wa uzazi, magonjwa ya zinaa nk.
10.Njia za kitaalamu za kupata ujauzito zijulikanazo kama in vitro fertilization na intrauterine fertilization.