Sunday, 2 June 2019

EDWIN SOKO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA


Mwenyekiti mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko (katikati) akitoa salamu zake za shukrani baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika jana Juni 01, 2019 katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza kumchangua kushika nafasi hiyo hadi hapo mwakani 2020 uchaguzi mkuu utakapofanyika.
 *****
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club -MPC) uliofanyika jana jumamosi Juni 01, 2019, wamewaondoa viongozi waliokuwa madarakani na kuwachagua viongozi wapya watakaokaa madarakani hadi mwakani 2020 utakapofanyika Uchaguzi/ Mkutano Mkuu.

Hatua hiyo ilijiri huku tayari tayari baadhi ya nafasi kama vile Mwenyekiti na Katibu Mkuu zikiwa wazi baada ya kujiuzulu mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu 2019 kufuatia mashinikizo kutoka kwa wanachama waliokuwa wakiwalalamikia kutotimiza vyema majukumu yao.

Katika uchaguzi huo, Edwin Soko alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Albert Gsengo, Katibu Mkuu Magreth Kusekwa (akipanda kutoka Katibu Mkuu Msaidizi), Katibu Mkuu Msaidizi Projestus Binamungu, Mweka Hazina Paulina David (akitetea nafasi yake). Aidha mkutano huo pia uliwachagua wajumbe watano wa Kamati Tendaji MPC ambao ni George Binagi, Gloria Kiwia, Nashon Kennedy, Sitta Tuma pamoja na Philmon Malili (akitetea nafasi yake).

Itakumbukwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, viongozi wa MPC waliochaguliwa walikuwa ni Mwenyekiti Osoro Nyawana (alijiuzulu), Makamu Mwenyekiti Neema Emmanuel, Katibu Mkuu Calvin Jilala (alijiuzulu), Katibu Mkuu Msaidi Magreth Kusekwa, Mweka Hazina Paulina David huku wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa ni Philmon Malili, Martha Lume, Antony Gervas, Shagatta Suleiman (amehamia mkoani Simiyu kikazi) na Neema Mwita (ametangulia mbele za haki).

Viongozi hao walipaswa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu lakini baadae UTPC ambayo ni taasisi inayolea klabu za waandishi wa habari Tanzania ilibadili Katiba na hivyo kufanya kupindi cha uongozi kwa klabu zote nchini kuwa miaka mitano badala ya mitatu.

Tazama picha na kisha video kujua zaidi yaliyojiri kwenye Mkutano Mkuu Maalum MPC
Makamu Mwenyekiti wa MPC, Albert George Sengo akisisitiza umoja na mshikamano baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Katibu Mkuu MPC, Magreth Kusekwa akitoa shukrani zake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ambapo aliahidi ushirikiano ili kuhakikisha MPC inasonga mbele kimaendeleo.
Katibu Mkuu Msaidizi MPC, Projestus Binamungu akitoa salamu za shukrani ambapo alisisitiza uvumilivu miongozi mwa viongozi na wanachama kwa maslahi mapana ya chama.
Mweka Hazina MPC, Paulina David akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumuamini na kumchagua kuitumikia tena nafasi hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Tendaji MPC yenye wajumbe wa watano akitoa salamu za shukrani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Nashin Kennedy akitoa salamu zake za shukrani.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Philmon Malili akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumuamini na kumchagua tena kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Sitta Tuma akitoa salamu zake za shukrani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Gloria Kiwia akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumchagua kushika nafasi hiyo.
Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo kwa kushirikiana na Hilda Kileo (hayupo pichani), akitoa ujumbe wako kwa wanachama na viongozi wapya MPC.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan (katikati) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum MPC wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia mijadala kwa umakini.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti MPC, Deus Bugaywa (katikati) wakifuatilia mawasilisho mbalimbali kwenye mkutano huo.
Viongozi wapya waliochagua kuiongoza MPC hadi hapo mwakani uchaguzi mkuu utakapofanyika kwa mujibu wa Katiba.
Wanachama wa MPC na viongozi wa UTPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya MPC.
Wanachama wa MPC na viongozi wa UTPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya MPC.
Baadhi ya viongozi wapya MPC wakipongezana baada ya uchaguzi.
Maakuli pia yalikuwepo.
Tazama Video hapa chini


Share:

WAJASIRIAMALI 3400 WANUFAIKA NA MIKOPO YA BENKI YA POSTA (TPB) TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la Benki ya Posta kwenye maonyesho ya saba ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kulia ni Meneja wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) Tanga Jumanne Wagana
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Edward Bukombe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la TPB Benki kushoto ni Meneja wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana 
Meneja wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana aliyevaa koti jeusi akizungumza na wageni mbalimbali waliotembelea banda lao kwenye maonyesho hayo
Meneja wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana kulia akisalimiana na kiongozi wa TCCIA Mkoani Tanga wakati wa maonyesho hayo
Maafisa wa Benki ya Posta Tawi la Tanga (TPB) kulia wakimsikiliza mmoja wa wakazi wa Jiji la Tanga aliyetembelea banda lao
Meneja wa Tawi la Benki ya TPB la Tanga Jumanne Wagana kushoto akimkabidhi zawadi kiongozi wa TCCIA ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo

WAJASIRIAMALI wadogo na wakubwa wapatao 3400 mkoani Tanga wamenufaika na mikopo kutoka Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya Bilioni 9.1 ambao umewawezesha kujikwamua kiuchumi. 

Hayo yamesemwa na Meneja wa Benki ya Posta (TPB) tawi la Tanga Jumanne Wagana wakati wa maonyesho ya Biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini hapa. 

Alisema kwamba mikopo hiyo ilitolewa pia kwenye vikundi mbalimbali, watumishi wa umma na wazee waastaafu kwa mkoa mzima wa Tanga. 

Aidha alisema wakati wanaanza kutoa mikopo hiyo mwaka jana waliweza kuitoa kwa wateja 3000 ambao ulikuwa na thamani ya sh.bilioni 8 huku wakiweka lengo la kuwafikia wateja wengi zaidi. 

Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo ni baadhi ya wateja kushindwa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati huku wengine wakiwa na mikopo zaidi ya mmoja. 

Hata hivyo aliwataka wateja wao kuendelea kutumia huduma zao mara kwa mara kwa sababu mikopo yao wanatoa kwa riba nafuu na huduma nzuri zinazowajali wateja wao.
Share:

BINTI HUYU NI MGONJWA ANAHITAJI MSAADA WAKO... HANA PESA ZA MATIBABU


Happiness Stephen Makala,mkazi wa mtaa wa Busulwa kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga anaomba msaada wa matibabu kwa mtoto wake aitwaye Rogathe Cyprian Makala mwenye umri wa miaka 18, ambaye anayesumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa ngozi kwa muda wa miaka 16 sasa.


Anasema amehanghaika katika hospitali mbalimbali hapa nchini, lakini siku moja alikutana na Daktari Bingwa kutoka Apolo India katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ndipo akampima na kumgundua kuwa homoni zake ziko kwenye njia ya mkojo, hivyo anatakiwa apatiwe matibabu ndani ya miezi tisa kwa kupatiwa dawa kutoka India, ambapo kila mwezi inatakiwa shilingi 504,000 ambapo kwa miezi hiyo tisa ni sawa na shilingi milioni 4.5 (4,536,000/-).

Kwa mujibu wa Daktari huyo,binti  huyo akifikisha umri wa miaka 20 ugonjwa huo wa ngozi utaweza kugeuka na kuwa kansa, na ataweza pia kuwa anazaa watoto wenye kisukari, na kichwa kikubwa na hata kuambukiza watu wengine kwa njia ya kuchangia choo.

Daktari huyo huwa anakuja kila baada ya mwezi hapa mkoani Shinyanga ambapo dozi ya dawa hiyo anatakiwa aanze Juni 2 mwaka huu ambapo itakuja na daktari huyo.

Mama wa binti huyo anasema yeye hana uwezo wa kumtibu binti yake, mume wake alishafariki kwenye ajali mwaka (2007) ambaye alikuwa Mhasibu wa shirika la umeme TANESCO mkoani Shinyanga.

Mama wa mtoto anasema mwanae huwa halali usiku kucha anashinda anajikuna tu na hata wakati wa jua kali huku vipele vikimtoka mwili mzima, na anatarajia kujiunga na kidato cha tano kwani amefaulu kidato cha nne.

Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo:

Vodacom : 0764206669 ukitaka kutuma kwa m-pesa jina litasoma Happines Makala

Halotel: 0626845953 jina litasoma Eliud Makala
Happines Stephen Makala (kushoto) akiwa na mtoto wake Rogathe Cyprian Makala (18) ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi na kuomba msaada wa matibabu.
Msichana Rogathe Cyprian Makala akionyesha namna ugonjwa huo wa ngozi unavyomsumbua na kutoka vipele mwili mzima na hawezi kulala usiku akishinda ana jikuna na kuomba msaada wa fedha za matibabu shilingi milioni 4.5
Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo: 

Vodacom : 0764206669 ukitaka kutuma kwa m-pesa jina litasoma Happines Makala

Halotel: 0626845953 jina litasoma Eliud Makala
Share:

KIJANA SALUM RAMADHAN SALUM ABICHI AMEPOTEA...TUNAMTAFUTA

Habari za Leo,

Pole na majukumu ya siku nzima. 

Napenda kukujulisha kuwa ndugu Salum Ramadhan Salumu (18) ,BADO hajapatikana wala hatujapata taarifa zake.

Tafadhali naomba msaada wako wa kila njia (Instagram,Facebook,Twitter,Radio,TV,Blog,Makundi ya WhatsApp,Website Nakadhalika) kusambaza taarifa ya Kupotea kwa kijana Salum Ramadhan Salum (18) ambaye hakurejea nyumbani tangu tarehe 12th May 2019.

 Mara ya mwisho ameonekana stendi ya Ukonga madafu akipanda gari ya kutoka Gongo la Mboto likielekea buguruni ikiwa ni safari yake ya kurejea nyumbani majira ya saa 2 usiku. 

Alikuwa amevaa shati jeupe na Suruali ya kijivu na saa rangi ya dhahabu na sendoz za wazi. Tafadhali toa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu na wewe au naomba unijulishe kwa kupiga ama kuandika sms kwenda nda namba 0713/0766-202748. 

Ni kijana mpole na mwenyeji wa Kiwalani BomBom kwa DSM na Mwanza ndio alipozaliwa. 

Naomba Ushirikiano wenu kwenye changamoto hii.

Asante
Share:

TAKWIMU ZA MIMBA ZAMSHITUA KAMANDA WA POLISI MWANZA "HATUWEZI KUKUBALI"


Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, ACP. Jumanne Muliro akifungua kikao kazi cha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali za Mitaa, Ustawi wa Jamii, Dawati la Jinsia, Jeshi la Polisi na wataalamu wa afya mkoani Mwanza.

Kikao hicho kiliandaliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto (KIVULINI) la jijini Mwanza ili kuweka
mikakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma rafiki za afya kwa vijana na wahanga wa ukatili ikiwemo ubakaji na kutokomeza mimba katika umri mdogo.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezajiwa mradi wa “sauti yangu, haki yangu katika kupunguza mimba za umri mdogo
Manispaa ya Ilemela” unaosimamiwa na shirika la KIVULINI.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wanahabari wakinasa matukio kwenye warsha hiyo ya kikazi.
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Mwakilishi kutoka jeshi la polisi mkoani Mwanza akiongoza wajumbe wa kikao kazi hicho kuweka mikakati ya upatikanaji wa huduma rafiki kwa wahanga wa ukatili.
Mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho akichangia mada.

Tazama video  hapa chini



Share:

KAMPUNI YA GREENWASTEPRO YAHAMASISHA WANANCHI KUTUMIA MIFUKO MBADALA


Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakionyesha aina mifuko (vibebeo) ambayo haipaswi kutumika kuanzia leo Juni 01, 2019 baada ya kuanza kwa katazo la Serikali la uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko hiyo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kampuni ya huduma ya usafi ya "GreenWastePro Ltd" imewahimiza wananchi na wafanyabiashara wote nchini kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ni adui wa mazingira na badala yake kujikita kwenye matumizi na biashara ya mifuko mbadala isiyohatarisha mazingira.

Meneja wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa, Salim Madafa ametoa rai hiyo leo jijini Mwanza baada ya zoezi la kuhamasisha katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na uzinduzi rasmi wa matumizi ya mifuko mbadala. Kampuni ya GreenWestPro ni miongoni mwa wadau wa mazingira walioshiriki kwenye zoezi hilo.

"Mifuko ya plastiki imekuwa na athari kubwa katika uchafuzi wa mazingira, mitaro kujaa maji kutokana na mifuko hiyo kuziba hatua ambayo hukwamisha kazi yetu ya uzoaji taka hivyo nitumie fursa hii kuwahimiza wananchi kutumia mifuko mbadala na kuachana na mifuko ya plastiki" amesisitiza Madafa.

Baadhi ya wafanyabiashara wadogo waliokuwa wakisalimisha mifuko ya plastiki katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza, wameomba Serikali kusaidia uzalishaji wa mifuko mbadala kwa wingi na kusambazwa katika maeneo yote huku ikiuzwa kwa bei nafuu hadi shilingi hamsini (Tsh. 50) kama ilivyokuwa mifuko ya plastiki, tofauti na hivi sasa ambapo inauzwa kuanzia shilingi mia mia tatu (Tsh.300).
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakionyesha aina ya mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku kutumika ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala na kuachana na matumizi ya plastiki ambayo ni hatari kwa mazingira.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (kushoto) akikusanya mifuko ya plastiki iliyozuiliwa matumizi yake kutoka kwa baadhi ya akina mama wajasiriamali katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (kushoto) amesema mifuko ya plastiki ilikuwa ikisababisha uchafunzi wa mazingira hivyo wananchi wahamasike kutumia mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Mmoja wa wafanyabiashara wadogo katika eneo la "Market Street" jijini Mwanza akiendelea na uuzaji wa mifuko mbadala.
Gari la kisasa la kampuni ya usafi ya GreenWastePro linalotoa huduma ya ukusanyaji uchafu katika Mitaa mbalimbali jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wadogo waliojitokeza kupata elimu kuhusu matumizi ya mifuko mbadala kwenye zoezi la kuhamasisha katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wadogo jijini Mwanza wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki na badala yake wajikite kwenye matumizi ya mifuko mbadala.
Wananchi na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakiwa kwenye zoezi hilo.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo pamoja na viongozi wa dini jijini Mwanza wakifuatilia wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWestPro Kanda ya Ziwa wakiwapungia mikono wananchi baada ya kutambulishwa kwenye zoezi la kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala ambapo kampuni hiyo ni miongoni mwa wadau muhimu wa usafi na utunzaji wa mazingira.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza (kushoto), akimuonyesha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) aina ya mifuko mbadala ambayo tayari ameanza kuiuza sokoni hapo.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza (kushoto) akieleza kuhusu upatikanaji wa mifuko mbadala na hivyo kuwatoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa mifuko hiyo jijini Mwanza.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (wa pili kulia) akiteta jambo na wadau wa mazingira jijini Mwanza wakati wa zoezi la kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala na kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki.
Ujumbe muhimu unaohamasisha matumizi ya mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira kutoka kampuni ya GreenWestPro inayohusika na usafi na utunzaji wa mazingira kwa sasa ikifanya shughuli zake katika mikoa ya Mwanza, Dodoma na Dar es salaam.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger