Tuesday, 21 May 2019

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0757996194 au 0717339771


Share:

SUA : Revised Undergraduate-programmes Admission and examination Requirements 2019

Sua application 2019, sua admission 2019, sua login, sua net, sua admission, sua prospectus, suasis almanac, sua library, sua almanac, sua online application

SUA : Revised Undergraduate-programmes Admission and examination Requirements 2019

ADMISSION REQUIREMENTS, EXAMINATION REGULATIONS AND GUIDELINES FOR UNDERGRADUATE AND NON-DEGREE PROGRAMMES,2019

new regulations

SUA : Revised Undergraduate-programmes Admission and examination Requirements 2019

DOWNLOAD HERE: ADMISSION REQUIREMENTS, EXAMINATION REGULATIONS AND GUIDELINES FOR UNDERGRADUATE AND NON-DEGREE PROGRAMMES 2019 (PDF)

The post SUA : Revised Undergraduate-programmes Admission and examination Requirements 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUIBA BIBLIA

Jamaa watatu waliopatikana na kosa la kuiba Biblia 500 kutoka kituo cha utafsiri wa vitabu cha Bible Translation and Literacy wamepigwa faini ya Ksh 500,000 kila mmoja nchini Kenya.

 Jamaa hao ambao ni Reuben Rogoi Maina, John Mapesa Andulu na Josephat Gatheru wamefikishwa mahakamani na kupigwa faini ya KSh 1.5 milioni kwa kosa hilo na wamekanusha mashtaka ya wizi huo na kuachiliwa kwa dhamana. 

 Kulingana na Gazeti la Taifa Leo, watatu hao wanakisiwa kuiba Biblia hizo kutoka kwa kituo cha utafsiri wa Bibilia (Bible Translation and Literacy (EA) mtaani Upperhill, Nairobi. 

Mahakama iliarifiwa kuwa watatu hao walikuwa wamelaghai kituo hicho kwa kuandika hundi bandia ya kulipia bei ya vitabu hivyo huku wakijifanya ilikuwa halali.

 Baada ya kugundua ukora wa waili hao, kituo hicho kilitoa taarifa kwa polisi na kukamatwa kwa watatu hao. Kesi hiyo itatajwa baada ya wiki mbili. 
Share:

TUNU NG'ONDYA : JPM AMEIPATIA HESHIMA KUBWA TANZANIA KUWA NA PASPOTI YENYE UBORA WA KIMATAIFA


Afisa wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Iringa Tunu Ng'ondya akionyesha hati mbali mbali za kusafiria nje ya Tanzania jana wakati alipozungumza na wanahabari kuhusu kujaza fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote(picha na Francis Godwin)
Na Francis Godwin ,Iringa 


Ofisa Uhamiaji mkoa wa Iringa Tunu Ng'ondya amepongeza jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.  John Magufuli katika kuboresha idara hiyo na kupelekea kuliletea Taifa heshima kubwa katika dunia kwa kuwa na hati ya kusafiria nje ya Tanzania yenye ubora wa kimataifa .
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kuhusu kujaza fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote,   Ng'ondya alisema kabla ya jitihada za serikali ya awamu ya tano kufanyika pass hiyo ya kusafiria ilikuwa katika hali ya ubora wa chini ila baada ya kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha idara ya uhamiaji hivi sasa kati ya hati bora za kusafiria duniani hati ya Tanzania ni miongoni na hivyo imeweza kuingia katika ubora wa ulimwengu .

Hata hivyo aliwataka wananchi kufika katika ofisi za uhamiaji kukata pass za kusafiri ili kuweza kuchangamkia fursa mbali mbali za kibiashara nje ya Tanzania kwa kwenda kufuata bidhaa na kuja kuuza nchini ama kupeleka bidhaa zinazozalishwa na watanzania kuuza nje ya Tanzania.

Alisema serikali imeweka utaratibu mzuri wa kila mwenye sifa ya kuwa na hati ya kusafiria kuweza kumiliki pasipo usumbufu wowote na kuwa suala la maombi na malipo ya gharama za kupata pass hiyo yanafanyika kwa njia ya mtandao na kuwa ofisi yake haipokei fedha yoyote taslim kutoka kwa mwombaji isipo kuwa mwombaji anapaswa kufika ofisini akiwa na viambatanishi vya vinavyohitaji baada ya kufanya maombi kupitia mtandao .

" Kama kuna mtu ataombwa fedha taslimu na ofisa yeyote atakapofika ofisini kwangu naomba achukue jina la mhusika na kuniletea ili achukuliwe hatua kali za kinidhamu kwani hatupokei fedha yoyote ile "

Alisema hakuna usumbufu wowote wa kupata hati hiyo kwani ndani ya wiki tatu pekee kwa waombaji wa mikoani wanaweza kupata pass zao baada ya kukamilisha taratibu zote na wale wanaohitaji hati ya haraka wanaweza kupewa ndani ya muda mfupi zaidi .

Ng'ondya alisema mwombaji anayehitaji kupata hati hiyo hatua ya kwanza anapaswa kuingia katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz na kisha kwenda katika kitufe cha e-Services.

Wakati hatua ya pili mwombaji atapaswa kuchagua fomu ya maombi ya hati tatu, kuchagua ombi jipya, nne, atatakiwa kutiki kiboksi kukubaliana na maelekezo na tano anaanza kujaza taarifa zake kwa ukamilifu ukifuata maelekezo na mpangilio katika kila kipengele.

Baada ya mwombaji kukamilisha kujaza taarifa zake, atafahamishwa ya kwamba usajili umekamilika na kupatiwa namba ya ombi, ambayo ni muhimu aiandike pembeni na kuihifadhi kwa kumbukumbu za baadae.

Kuwa mwombaji atapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na kutakiwa kwenda kulipia malipo ya awali Sh20,000.

Hata hivyo alisema baada ya mwombaji kumaliza hatua hiyo, ukurasa huo, ataingia katika menu ya M-Pesa/Tigopesa (*150*00#/*150*01#).

Amesema baada ya hapo atatakiwa kubonyeza namba 4 (lipa kwa M-Pesa) au kubonyeza namba 4 (kulipia bili)-Tigo na baada ya kuchagua mtandao wa malipo, atatakiwa kuingiza namba ya kampuni 888999 na mwombaji atatakiwa kuingiza kumbukumbu namba (Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….), kisha kiasi (kama ilivyo elekezwa mfano: 20,000), atapata maelezo kuwa unalipa pesa NMB, baada ya hapo ataingiza namba ya siri, atahakiki na kupata ujumbe mfupi wa maneno kutoka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika.

Kuwa baada ya hatua hiyo mwombaji atapata ujumbe kutoka kwenye mfumo namba 15200 kama muamala umekubalika, kisha kurudi katika ombi linaloendelea na mwisho ataingiza namba ya ombi au simu na namba ya risiti na hapo atapakua fomu yake ya maombi na baada ya kuwa amepata fomu atatakiwa kuiwasilisha katika ofisi ya Uhamiaji wilaya ya Mufindi ,Ilula kwa wilaya ya Kilolo ama makao makuu ya mkoa mjini Iringa .
Share:

Kauli ya Masele baada ya Kuhojiwa...."Sijawahi kukurupuka, nasimamia haki na najitambua"

Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemhoji mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele kuhusu tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu.

Masele alihojiwa na kamati hiyo inayoongozwa na  Emmanuel Mwakasaka  jana Jumatatu Mei 20, 2019.

Mara baada ya kutoka katika mahojiano Masele alizungumza na wanahabari, “Mimi ninaheshimu  sana viongozi wangu, nimelelewa vizuri na wazazi, nimelelewa vizuri na chama changu, nimetokea umoja wa vijana kuanzia ngazi ya chini kabisa mpaka ngazi ya kitaifa na kuwa mjumbe wa baraza kuu Taifa, nimekuwa mbunge hii awamu ya pili.

“Nimekuwa naibu waziri  natambua miiko ya uongozi, sijawahi kukurupuka, fuatilia rekodi zangu chochote ninachokisema ninasimamia haki, ukweli na ninaheshimu viongozi wenzangu.

“Ni matarajio yangu haki itatendeka na mimi sijafanya jambo lolote kinyume na taratibu, kwenye kazi zangu ndani ya Bunge na pia Bunge la Afrika kama makamu wa rais.”

Kuhusu utovu wa nidhamu amesema, “Nawahakikishia Watanzania, nilichokuwa nasimamia ni misingi ya haki za binadamu na kufanya hivyo nisitafsiriwe kwamba ni utovu wa nidhamu.”


Share:

Makonda atoa Sadaka zaidi ya misikiti 1,000

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Mhe. Paul Makonda leo amewakabidhi shehena ya viungo vya kutengeneza futari kwa maimamu, mashehe na viongozi wa Dini ya Kislamu kutoka Misikiti zaidi ya 1,000 kama sehemu ya sadaka na shukrani ya Amani na Utulivu ndani ya mkoa huo.

Miongoni mwa vitu alivyokabidhi RC Makonda ni Mchele, Sukari, Unga, Maharage, Mafuta na vitu mbalimbali kwaajili ya kuwawezesha viongozi hao kufurahia futari majumbani mwao.

RC Makonda amewashukuru viongozi wa dini kwa kuwa wasimamizi wazuri wa Amani na mshikamano ndani ya mkoa huo jambo linalofanya mkoa huo kuendelea kuwa kisima cha Amani.

Hata hivyo RC Makonda amewaeleza Viongozi wa Dini kuwa namna bora ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli na kumuombea ni kuhakikisha waumini wao wanajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wachague viongozi wa serikali za mitaa wanaochukia Rushwa.

Aidha RC Makonda amemshukuru Balozi wa Falme za Kiarabu kwa kumkabidhi misaada hiyo huku akiwasihi waislamu kutumia mfungo huu Kuliombea taifa na viongozi pamoja na kuwahimiza wazazi kuwalea watoto katika malezi bora.

Kwa upande wake Balozi mdogo wa Falme za Kiarabu amesema wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwakuwa wanamuamini akipokea kitu kinawafikia walengwa na amekuwa mtu wa kuwasaidia watu wasiojiweza bila kujali dini wala kabila.


Share:

Video ya Dayna Nyange – Dua

Video ya  Dayna Nyange – Dua

Share:

MITAMBO YA KUTENGENEZEA SILAHA YAKAMATWA SINGIDA


Kikosi Kazi Cha Jeshi la Polisi Makao Makuu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Singida kimefanikiwa kukamata silaha aina ya gobore lililotengenezwa kienyeji pamoja na mitambo mbalimbali ya kutengenezea silaha.

Akiongea na waandishi wa Habari jana katika maeneo ya ofisi ya RPC Singida, Mkuu wa Oparesheni maalumu za Jeshi la Polisi Tanzania Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) Mihayo K. Msikhela ameeleza kuwa mafanikio hayo yalipatikana siku ya tarehe 19.05.2019 Majira ya saa 3:30 usiku huko katika Kijiji cha nguvumali, Kata na Tarafa ya Ndago Wilayani Iramba ambapo zilipatikana taarifa za kiintelijensia zilizopelekea kukamatwa mtuhumiwa Hamisi Mohammed, (52), Mkazi wa Mtaa wa Nkulusi - Ndago ambaye alikutwa na silaha aina ya gobore na mitambo ya kutengenezea silaha.

Mihayo ameeleza kuwa msako ulieendelea na kukamatwa watuhumiwa wengine 6 ambao ni Mohammed

Hassan, (89) Mhunzi na mkazi wa Kijiji cha Nkingi - Misigiri , Kassim Mohamed, (34) mkazi wa Nkulusi - Ndago , Mkapa Msengi (47), mkazi wa Nguvumali - Ndago.

Amewataja wengine kuwa ni Hassan Hamis (28) , mkazi wa Nkulusi - Ndago, Idd Mohammed, (45), Mkulima na mkazi wa Ndago na Swaleh Ally , (49), mkazi wa Nkulusi Ndago.

Mkuu wa Oparesheni huyo amesema kuwa watuhumiwa wote 7 wanshikiliwa kwa mahojiano zaidi na baada ya mahojiano kukamilika watafikishwa Mahakani ambapo ametoa wito kwa wananchi wote hasa wenye mapenzi mema kuendelea kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini wahalifu na viashiria vya uhalifu ili kuendelea kuifanya nchi iendelee kuwa salama.
Share:

Video Mpya: Lava Lava ft. Salha - Hatuachani

Msanii wa muziki nchini, Lava Lava anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la Hatuachani. Itazame hapa.


Share:

Iran yasema Marekani haiwezi kuiangamiza

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammed Javad Zarif amesema kile alichokiita ''kejeli za maangamizi'' za rais wa Marekani Donald Trump haziwezi kuimaliza Iran. 

Kupitia mtandao wa Twitter, Zarif amesema Iran imesimama imara kwa maelfu ya miaka, wakati maadui wake wote wakiwa wametoweka. 

Haya Zarif anayasema wakati mvutano ukizidi kushamiri baina ya nchi yake na Marekani, na onyo la Trump kwamba ikiwa Iran haitaacha kuitishia Marekani, basi mwisho rasmi wa Iran utakuwa umewadia. 

Mahusiano baina ya nchi hizo mbili yalizidi kuzorota mwaka jana baada ya Rais Trump kuiondoa Marekani katika makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, yaliyosainiwa mwaka 2015 kati ya taifa hilo la Kiislamu na nchi zenye nguvu duniani. 

Mvutano huo ulichukuwa sura mpya mwezi huu pale Marekani ilipopeleka katika eneo la Ghuba manowari na ndege za kivita chapa B-52 kujibu ilichokitaja kuwa kitisho kutoka Iran ambacho haikukifafanua.


Share:

COSTECH YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI KURIPOTI TAARIFA ZA MATOKEO YA UTAFITI

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuripoti taarifa za matokeo ya tafiti zinaofanywa na taasisi mbalimbali ili wananchi waweze kupata taarifa.

Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Bakari Msangi kwenye Mafunzo yaliyohusisha wana habari,Watafiti na wawakilishi kutoka SIDO na VETA yanayofanyika katika ukumbi wa VETA Mtwara.

Dkt. Msangi ameongeza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza zaidi habari za Michezo,Burudani na Siasa kuliko Habari za Utafiti ambazo zingesaidia wananchi kupata Elimu kuhusu mambo mbalimbali yatokanayo na tafiti ikiwemo kilimo

Amefafanua kuwa ni vema kuripoti matukio na matokeo ya Tafiti kwa lugha rahisi na zinazoeleweka kwa wananchi kutokana na mahitaji husika ya habari

Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameanza jana yameandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) lenye jukumu la kuhamasisha, kuratibu, kuhifadhi, kusambaza na kuendeleza tafiti chini.
Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Bakari Msangi akifungua mafunzo hayo.
Share:

MTANDAO WA REDIO ZA JAMII TANZANIA (TADIO) WATOA MAFUNZO KWA WARATIBU WA VIPINDI


Mtandao wa redio za jamii Tanzania- TADIO,kwa kufadhiliwa na Best Dialogue wametoa mafunzo ya siku mbili kwa waratibu wa vipindi juu ya namna ya kubuni, kuandaa na kutangaza vipindi vyenye ubora. 

Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa ofisi za radio Dodoma fm jijini Dodoma.

Akifungua rasmi mafunzo hayo Mwenyekiti wa TADIO nchini Prosper Laurent Kwigize amesema redio za kijamii zimefanya vizuri katika tafiti zilizotolewa hivi karibu Katika uandaaji wa vipindi vinavyolenga mahitaji ya wasikilizaji lakini bado zinakabiliwa na mapungufu mbalimbali. 

Amesema TADIO kwa kufadhiliwa na Best Dialogue wameamua kutoa mafunzo hayo kwa waratibu wa vipindi ili wakafanye mabadiliko katika redio zao na kuongeza kuwa ikiwezekana katika tuzo za EJAT mwaka kesho redio hizo zitoe washindi.

Kwigize amesema pamoja na umuhimu wa waratibu wa vipindi Katika redio lakini walisahaulika badala yake mafunzo mengi yalielekezwa kwa wahariri wa vituo na kusahau kuwa waratibu ndiyo "Moyo" wa kituo cha redio. 

Naye mkufunzi wa mafunzo hayo Dotto Bulendu ambae pia ni mkufunzi chuo kikuu cha ST AUGUSTINE jijini Mwanza amewataka waratibu wa vipindi kubuni na Kuandaa vipindi vinavyoendana na Maeneo yao na yanayoweza kuwafanya wakazi wa Maeneo hayo kujimudu kiuchumi.

Mafunzo hayo yamehusisha waratibu wa vipindi wapatao 18 kutoka redio mbalimbali za Tanzania bara na visiwani na yanafanyika ikiwa radio nyingi za kijamii zinakabiliwa na chamgamoto kubwa ya ukata wa kifedha jambo ambalo linaelezwa kuwa linaweza kumalizika kwa maandalizi bora ya vipindi.

Share:

Basi la Arusha Express lateketea kwa moto

Basi la kampuni ya Arusha Express linalofanya safari zake kati ya Bukoba na Arusha limeungua moto asubuhi ya leo katika maeneo ya Kibeta, Manispaa ya Bukoba. 

Hakuna madhara kwa binadamu yaliyoripotiwa wala chanzo cha moto huo hakijajulikana.


Share:

MASELE : SIJAWAHI KUKURUPUKA

Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM) Stephen Masele, amesema, hajawahi kukurupuka katika kusimamia jambo lolote. 

Alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutoka kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge jijini Dodoma kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu. 

“Fuatilia rekodi zangu huko nyuma, chochote ninachokisema ninasimamia haki, ukweli na ninaheshimu viongozi wenzangu,” amesema Masele.

Masele amefika mbele ya kamati hiyo baada ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kudai kwamba, mbunge huyo amekuwa akitoa maneno ya hovyo hovyo na hata kugonganisha mihimili miwili ya dola.

Masele ambaye ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), alifika mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Emmanuel Mwakasaka, Jumatatu ya tarehe 20 Mei 2019 kama alivyoelekezwa na Spika Ndugai.

Mbele ya wanahabari Masele alisema, anatambua miiko ya uongozi kwa kuwa, ameshika nafasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na unaibu waziri akisisitiza kuwa, hajawahi kukurupuka katika kufanya uamuzi ama kwenye misimamo yake.

“…ninasimamia haki, ukweli na ninaheshimu viongozi wenzangu , amesema Masele na kuongeza “nimekuwa naibu waziri, natambua miiko ya uongozi.

“Nawahakikishie Watanzania kwamba, kile nilichokuwa nasimamia ni misingi ya haki za binadamu na kufanya hivyo nisitafsiriwe kwamba, ni utovu wa nidhamu.”

Amesema kuwa, amelelewa kwenye familia yenye maadili mema na pia amepitia kwenye umoja wa viajana hivyo hana tabia ya kudharau viongozi wake

“Ninaheshimu sana viongozi wangu, nimelelewa vizuri na wazazi wangu, na chama change pia. Nimetokea umoja wa vijana kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya kitaifa na kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa,” amesema.

Masele hakueleza namna ya mjadala ulivyokuwa mbele ya Kamati ya Maadili, ila ameeleza kuwa na matumaini ya kutendewa haki.

Hata hivyo, Spika Nduga alisema kuwa, baada ya Masele kuhojiwa na kamati hiyo, atahojiwa pia na Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Chanzo- Mwanahalisionline
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 21




Share:

Monday, 20 May 2019

Breaking : ILUNGA ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU MPYA

Share:

RIDHIWANI KIKWETE AANZISHA UJENZI WA SHULE YA MSINGI



Na Shushu Joel, Chalinze. 
Mbunge wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amekuwa wa kwanza kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya uanzishwaji wa ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha choza,Kata Ubena Zomozi ili kusaidia watoto wa maeneo hayo.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa kata,vijiji na vitongoji wa kata hiyo alisema kuwa amefanya  maamuzi hayo ya kuanzisha ujenzi wa shule hiyo kutokana na changamoto zinazowakabili wazazi/walezi na wanafunzi kwa kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata elimu ya shule ya msingi huku wazazi kwa ajili ya masuala ya kimaendeleo.

Alisema kuongezeka kwa watu katika hilo eneo la Choza kimepelekea kuhitajika kwa haraka kwa huduma za kijamii ili kuendana na mahitaji ya wakazi wa eneo hilo.

"Saruji niliyotoa ni uanzilishaji wa ujenzi wa shule hiyo lakini si kwamba ndio mwisho wa utoaji wangu wa mahitaji katika ujenzi huo bali ni kama kiongozi wa mfano ili hata wananchi wanapoambiwa wachangie  wasisite" ,alisema Ridhiwani Kikwete 

Aidha aliongeza kuwa wananchi ndiyo nguzo ya maendeleo hivyo wanapoamua jambo lolote lile la kimaendeleo ni lazima lifanyike kutokana na umoja, nguvu na mshikamano wao katika ufanikishaji wa maendeleo katika eneo husika.

Pia mara baada ya kutoa mifuko hiyo ya saruji Ridhiwani aliwataka viongozi wa eneo hilo kutafuta eneo jingine  kubwa lenye kufaa ujenzi wa zahanati ili pia Choza pajengwe zahanati.

Pia amewataka wananchi wa Choza kujitokeza kwa wingi  katika kuhamasishana  juu ya maendeleo kwani serikali inatambua  makusudi yao.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Ubena  Zomozi Nicholaus  Muyuwa amempongeza Mbunge huyo kwa uanzilishi wake wa kutoa saruji kwa lengo la ujenzi wa shule katika eneo hilo ili kuwaondolea changamoto watoto wa maeneo hayo.

Aidha amemhakikishia Ridhiwani kuwa saruji hiyo itatumika kama ilivyokusudiwa kufanyika kwani hata wao walikuwa wakilifikiria tu lakini Mbunge huyo kafanya kweli. 

Naye Cosmos Alphonce ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kaloleni ameshukuru kwa mchango uliotolewa na mbunge na kumtaka aendelee na moyo huo wa kujitolea kwa wananchi wake.

Aliongeza kuwa kujengwa kwa shule katika eneo hilo kutaondoa changamoto ya watoto wa eneo hilo kutembea kilometa  nyingi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger