Sunday, 12 May 2019

Kutana na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff  Mwenye UWEZO wakufanya dua mbali mbali  Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Adam shariff Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO   Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? . Adam shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN  . Anatafsiri Ndoto. , KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na Biashara.


Mawasiliano: (+255 )715971688 au (+255  )756914036



Share:

Juhudi Za Serikali Kupiga Marufuku Mifuko Ya Plastiki Ziungwe Mkono Na Wadau Wote

Na Ismail Ngayonga
KATIKA kipindi cha miaka Hamsini iliyopita, dunia imeshuhudia ongezeko kubwa la uzalishaji wa bidhaa za plastiki, ambapo kwa katika mwaka 2013, jumla ya tani Milioni 299 Milioni za plastiki zimezalishwa duniani ikiwa ni ongezeka la asilimia 4% ikilinganishwa na uzalishaji wa mwaka 2012.


Kwa mujibu wa Shirika la Uhifadhi Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) matumizi ya plastiki yameongezeka duniani kutoka tani  Milioni 5.5 katika miaka ya 50 hadi tani Milioni 110 Milioni mwaka 2009.

Licha ya kuongezeka kwa uzalishaji wa plastiki kwa kiwango kikubwa, kiwango cha taka za plastiki zinazovurugwa kwa matumizi mengine ni madogo ukilinganisha na uzalishaji, kwani matumizi ya bidhaa za plastiki yamekuwa yakiongozeka kwa kasi na kuchukua nafasi ya bidhaa za chuma na vigae zilizokuwa zikitumika kabla.

Uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki huathiri na kuharibu mazingira ya miji, ardhini, mito, maziwa, mashambani na hata bahari na pia kutokana na kuenea kwa taka hizo, viumbe kadhaa wa baharini huathiriwa na kemilaki zitokanazo na taka hizo au kwa kula mabaki ya plastiki.

Katika kuunga mkono juhudi za Jumuiya ya Kimataifa za kupinga matumizi ya bidhaa za plastiki ikiwemo mifuko, Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu (Muungano na Mazingira), imetangaza kuwa ifikapo Juni mosi mwaka huu, itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake yatakoma ifikapo Mei 31, 2019.

Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari Jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Balozi Joseph Sokoine anasema Serikali imekuwa ilitoa taarifa mbalimbali ili kuwaelimisha wananchi kuhusu katazo hilo kupitia magazeti, televisheni, redio, mitandao ya kijamii, pamoja wadau na mikusanyiko ya watu ikiwa ni pamoja na taarifa kusomwa katika nyumba za ibada.

Balozi Sokoine anasema Serikali imeandaa kanuni za utekelezaji wa katazo hilo zitakazoanza kutumika tarehe 1 Juni 2019, ambapo kanuni zitatoa maelekezo mbalimbali kwa ajili ya kupiga marufuku kuzalisha, kuingiza, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki iliyotajwa katika Katazo hilo,  ambapo kiwanda, Kikundi cha Watu au Mtu Binafsi atakayebainika kukiuka matakwa ya Kanuni hizi atakuwa ametenda kosa la jinai na hivyo sheria itachukua mkondo wake.

Anoongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais tayari imetoa maelekezo mahsusi kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa katazo hilo ambapo baadhi yao wameanza kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya uhifadhi wa shehena ya mifuko itakayosalimishwa.

“Kwa kushirikiana na Makampuni ya Simu ya Vodacom, Tigo, Airtel na Halotel tumefanikiwa kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwa watumiaji wa mitandao hiyo ambapo watumiaji milioni 11 wa Tigo, Milioni 15.5 wa Vodacom wameshapata ujumbe huu, hii itakuwa endelevu kila wiki” anasema Balozi Sokoine.

Akifafanua zaidi, Balozi Sokoine anasema Serikali imeendelea kufanya juhudi mbalimbali katika kutoa matangazo kwa kutumia vipaza sauti katika ngazi ya Kata, Mitaa na Vijiji pamoja na kufanya vipindi maalum katika vyombo vya habari ikiwemo kutumia redio za kijamii na redio za mikoani katika kutoa matangazo juu ya katazo hili. 

Aidha Balozi Sokoine alisema jitihada zote hizi zinapaswa kuungwa mkono na si kubezwa kwa kuwa ifikapo tarehe 1 Juni 2019, Serikali itaendesha operesheni kabambe nchi nzima ya kusaka mifuko hii na operesheni hiyo itahusisha Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Kwa mujibu wa Balozi Sokoine kikosi kazi hicho pia kitaongozwa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP), pamoja na Mamlaka za Viwanja vya Ndege (TAA), Bandari, Forodha, Uhamiaji, na Usafiri wa Nchi Kavu.

Kuhusu maeneo yatayotumika kwa ajili ya kusalimisha mifuko ya plastiki, Balozi Sokoine anasema Serikali itatoa utaratibu wa mahali rasmi wanapotakiwa kusalimisha   shehena ya mifuko watakayokuwa nayo kwa wale ambao watakuwa tayari kusalimisha kwa hiari.

“Kwa taarifa zaidi kuhusu utekelezaji wa katazo hili Wananchi kwa ujumla mnashauriwa kutembelea Ofisi za Kanda za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) zilizopo Dar es Salaam, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Kigoma na Arusha na pia wanaweza pia kuwasiliana na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa Miji na Wilaya.

ili kutimiza azma ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ni wajibu wa wadau wote wa mazingira wakiwemo wajasiriamali na wawekezaji na ili kupata maoni kuhusu namna ya kujenga mazingira wezeshi kwa wadau kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa mifuko mbadala.


MWISHO


Share:

Amri ya Kim Jong-un ya kuimarishwa uwezo wa jeshi la Korea Kaskazini

Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini ametoa amri ya kuimarishwa uwezo wa jeshi la nchi hiyo kwa ajili ya kukabiliana na adui.

Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini (KCNA) limetangaza kwamba Kim Jong-un ametoa amri hiyo kufuatia hatua ya Marekani kutwaa meli ya kubeba mizigo ya serikali ya Pyongyang kwa kisingizio kuwa imekiuka vikwazo vilivyowekwa.

Kufuatia hatua hiyo kiongozi huyo amesisitiza udharura wa kuongezwa uwezo wa vikosi vya ulinzi vilivyo katika mstari wa mbele na ngome ya Magharibi kwa lengo la kuwa tayari kutelekeza operesheni za kiulinzi ili kukabiliana na hali yoyote ile hatari. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ya Korea Kaskazini imeainisha ajenda yenye kipaumbele muhimu kwa ajili ya kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi. 

Kadhalika Kim Jong-un amebainisha kwamba amani na usalama wa kweli utadhaminiwa kupitia vikosi vya askari wenye uwezo ambao wanaweza kutetea haki ya kujitawala nchi hiyo.

Ikumbukwe kuwa, meli iliyokuwa na mzigo wa tani elfu 17 ya Korea Kaskazini iliyosimamishwa mwaka jana nchini Indonesia kwa tuhuma za kubeba makaa ya mawe, ilitwaliwa na Marekani Ijumaa usiku kwa kisingizio cha kukiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa, hatua ambayo imelaaniwa vikali na serikali ya Pyongyang.

Amri mpya ya Kiongozi wa Korea Kaskazini ya kuimarishwa uwezo wa kiulinzi wa jeshi la nchi hiyo ni sehemu nyingine ya misimamo ya serikali ya Pyongyang juu ya kuendelea mienendo ya uhasama ya Marekani, ukiwemo wa kuvunja mazungumzo ya pande mbili yaliyokusudiwa kutatua mzozo wa nyuklia katika Rasi ya Korea. 

Katika wiki za hivi karibuni na baada ya kufeli duru ya pili ya mazungumzo kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong-un huko mjini Hanoi, Vietnam, Korea Kaskazini ilianzisha tena majaribio yake ya makombora.

Katika duru ya kwanza ya mazungumzo ya pande mbili nchini Singapore, Pyongyang iliahidi kusitisha majaribio yake ya makombora na silaha za nyuklia, hata hivyo White House ikakiuka ahadi zake kuhusu kusimamishwa vikwazo dhidi ya nchi hiyo ya Asia ambapo ilirefusha kwa kipindi cha mwaka mmoja mwingine vikwazo vyake dhidi ya Korea Kaskazini.



Share:

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka ni mtu aliye jaliwa KUBULI SHUFAA pia anatoa DUAH   za RUHIA. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho, Kama una Majini wa Kichawi pia yanaondoka UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary  ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA WALIVYOSAIDIWA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 6 tu)
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu na ANATIBU KWA KUTUMIA QUR AN. Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!?
 
Hupati kazi kwa mda mrefu na vyeti unavyo
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa
Unataka nyota ing'ae ukiongea usikilizwe Ipo TARASIMU kwa Ajili yako...
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa. Kama umezulumiwa Mali irudi ikiwa haija pita Mwezi .
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu ni mtu mkarimu mpenda watu,Anahudumia  MASKINI  na TAJIRI, NJOO ATAKUSAIDIA.. Sheikh Omary 0673531992 WhatsApp/Call


Share:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kupokea Watalii 343 Leo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo jioni Jumapili Mei 12  anatarajiwa kuwapokea watalii 343 kutoka China wanaokuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii kwa siku tano.

Mara baada ya watalii hao kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) itafanyika hafla fupi ya kuwakaribisha na kesho wataanza safari ya kutembelea vivutio  huku baadhi yao wakishiriki kongamano la uwekezaji sekta ya utalii litakalofanyika kesho.

Ujio wa watalii hao unatokana  Bodi ya Utalii (TTB) kuingia makubaliano na kampuni ya Touchroad International Holdings Groups ya China Novemba mwaka jana wakati wa ziara ya kutangaza utalii katika miji ya Beijing, Shanghai, Chengdu, Guangzhou na Hong Kongna nchini China.

Wanaowasili leo ni wafanyabiashara na watu maarufu, wawekezaji kutoka kampuni 27, waandishi wa habari 40, maofisa wa Serikali ya China na mawakala wa kampuni za utalii.


Share:

Serikali Yashauriwa kutowapuuza wawekezaji wanaotoka China

Serikali  imeshauriwa kutowapuuza wawekezaji wanaotoka China na kuja kuwekeza badala yake wawatumie kama daraja la kuweza kufikia malengo ya kuwa nchi yenye uchumi mkubwa duniani.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda,   alipokuwa katika ghafla ya uzinduzi wa  pombe kali aina ya Moutai ambayo kiwanda chake kipo China.

Alisema pamoja na uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na China, lakini bado wameamua kutafuta kila mbinu ili kuweza kushirikiana katika masuala ya kiuchumi.

“Ushirikiano uliopo baina yetu na China ni jambo kubwa, tuendelee kuukuza, wao kama nchi wameamua kutafuta kila mbinu ya kushirikiana na nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania, hivyo tunapaswa kutumia nafasi hii ambayo wawekezaji hawa wameamua kutupa kama daraja kufikia malengo tunayoyataka kama nchi,” alisema.

 Pinda alisema China ni taifa la pili kwa ukuaji wa uchumi duniani, hivyo hawapaswi kupuuzwa wanapokuja na mawazo yao ya kuanzisha biashara.

Alisema wawekezaji wa China wameamua   kutangaza biashara zao kubwa nchini, ikiwamo pombe hiyo ambayo ni maarufu  China na nchi za Afrika Magharibi.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi na Naibu Katibu wa Bodi ya Moutai, Wang Yan, alisema miaka 40 iliyopita China ilikuwa miongoni mwa mataifa masikini duniani kuliko umasikini uliopo katika baadhi ya nchi za Afrika.

Alisema kwa sasa kampuni zilizoanzishwa nchini humo zimefanikiwa kubadili mfumo wa maisha ya Wachina na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara na kuchangia kuleta maendeleo kwa haraka.

“Sisi kama Moutai, tumechagua Afrika kutokana na kuwa na ushirikiano mzuri katika kipindi kizuri kilichopita na ushirikiano huu unaonekana utazidi kuimarika katika siku zijazo na kuongeza mafanikio,” alisema.

Alisema mwaka jana mapato ya kampuni zilizopo chini ya kampuni mama ya Moutai Group yalikuwa ni Dola za Marekani bilioni 12.6, faida halisi ilifikia dola bilioni 5.8 na mapato ya kodi yalikuwa ni dola bilioni 5.6 na iliweza kumiliki mali zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 30.


Share:

DCEA waeleza walivyomnasa Shamim Mwasha na mumewe akiwa darini kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya

Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema mfanyabiashara Abdul Nsembo maarufu kama Abdukandida ni papa (kinara) katika mtandao wa biashara ya dawa hizo na anajulikana katika nchi mbalimbali zikiwamo Brazil na Marekani.

Nsembo alikamatwa na DCEA Mei Mosi mwaka huu, usiku wa manane akiwa amejificha juu ya dari nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam, mpaka sasa anaendelea kushikiliwa na mke wake Shamim Mwasha kwa kudaiwa kukutwa na gramu kati ya 560 hadi 700 za heroin zilizopatikana baada ya kupekuliwa nyumbani kwao kwa muda wa saa sita kuanzia saa nane usiku hadi saa moja asubuhi.

Akizungumzia sakata hilo, Kamishina wa Operesheni wa DCEA, Luteni Kanali Fredrick Milanzi, amedai Nsembo ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliokuwa wakiwachunguza na kuwatafuta kwa muda mrefu.

“Nyinyi mnamuona Nsembo ni mtu mdogo, Nsembo si mdogo katika mtandao wa dawa, ana network (mtandao) kubwa, ukiwauliza wenyewe watakwambia ni mjanja na amekuwa akifanya biashara hii kwa muda sasa, na huyu kijana pia tuliomkamata juzi sio mdogo ni mkubwa, yeye ndio anatumiwa na wakubwa, hawa watu kuwakuta na kilo mbili tatu si kitu cha ajabu, ingekuwa tunawakuta na gramu tatu mbili ndiyo tungesema wadogo,” amesema Luteni Kanali Milanzi.

Chanzo: Gazeti la Mtanzania.


Share:

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0759208637 au 0620510598


Share:

Wimbo Mpya: Beka Flavour Ft. Pierre - LAMBA LOLO

Wimbo Mpya: Beka Flavour Ft. Pierre - LAMBA LOLO


Share:

Marekani yafanya maangamizi dhidi ya Magaidi wa IS nchini Somalia

Marekani imefanya mashambulizi ya Anga ya  siku tatu dhidi ya magaidi wa IS  nchini Somalia.

Kwa mujibu wa habari,magaidi 17 wa kundi hilo wameangamizwa katika operesheni hiyo.

Taarifa kutoka kwa Amri ya Umoja wa Mataifa ya Afrika (AFRICOM) ilielezea kwamba kiwanja cha ndege kiliandaliwa dhidi ya wapiganaji wa IS ambao walianzisha makambi katika Mlima Golis.

Mashambulizi ya anga yalianzishwa mnamo 8 Mei ambapo magaidi 13 waliangamizwa na 9 Mei ambapo magaidi wanne wameangamizwa.

Hakuna raia yoyote aliyejeruhiwa katika operesheni hiyo iliyofanywa kwa pamoja na serikali ya Somalia.

Marekani imekuwa ikiwashambulia magaidi wa Al Shabaab pia nchini Somalia.


Share:

LIVE: Ibada Ya Kumsimika Askofu Mkuu Wa Jimbo Kuu Katoliki La Mwanza

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika Ibada ya Kumsimika Askofu mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Mwanza Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande katika eneo la Kawekamo Jimbo kuu Katoliki la Mwanza .Mei 12,2019.


Share:

Inbar Yaitaka Tanzania Kuwekeza Mkazo Biashara Ya Mianzi

Na Grace Semfuko, MAELEZO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Kimataifa la Kuendeleza na Kusimamia Biashara ya Mianzi (INBAR) limesema ipo haja kwa Serikali ya Tanzania kutunga Sera zitakazoweza kuhamasisha wakulima hapa nchini kulima zao hilo ambalo pamoja na kuhifadhi Mazingira pia lina tija kiuchumi.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam jana Jumamosi (Mei 11, 2019) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Balozi Ali Mchumo alisema ni muhimu kwa nchi ya Tanzania kuzalisha zao hilo ili kuongeza uchumi kutokana na kuwa na soko la uhakika hasa kwa nchi zilizoendelea.
 
“Soko la zao la Mianzi ni kubwa sana Duniani, nawasihi wakulima wazalishe kwa wingi kwani kwenye mataifa mengine wanatumia mpaka kuendeshea mitambo ya viwanda,ndege, kuhifadhi mazingira pamoja na ujenzi, zao hili lina faida kubwa tusilidharau” alisema Balozi Mchumo.
 
Alisema kuna aina zaidi ya 1,600 za mianzi Duniani na zote hizo zikiwa na ubora wa hali ya juu hivyo uzalishaji wa zao hilo kwa Tanzania hautakosa soko na kwamba Shirika lake limejikita katika kuhamasisha na kutafuta masoko.
 
Balozi Mchumo aliwatoa wasiwasi wakulima wa Tanzania kuhusiana na kuzalisha zao hilo kwa kusema kuwa ni rahisi, halina gharama kubwa katika utunzaji wake na lina faida kubwa kwenye soko la Dunia kwani nchi nyingi hasa zenye matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara hutumia mianzi katika kujengea nyumba zao.
 
Aliongeza kuwa kwenye fukwe za Bahari zao hilo limekuwa likihifadhi mmomonyoko wa ardhi kutokana na mizizi yake kushikamana na hivyo kuondoa kabisa athari za kimazingira.
 
Aidha Balozi Mchumo alizitaja sifa za mmea huo kuwa ni pamoja na kustawi kwa haraka kwa kipindi cha  miezi nane hadi tisa mpaka kufikia matumizi yake, ni mgumu kuvunjika au kuoza na ni mwepesi kuubeba, unahifadhi mazingira na kwamba  unafaa kwa ujenzi, na pia unatumika kutengeneza sakafu za majumbani na sehemu nyinginezo inatumika kutengenezea samani za majumbani na maofisini.
 
Akifafanua zaidi Balozi Mchumo alisema Shirika hilo lina nchi wanachama zaidi ya 45 katika Bara la Asia na Afrika ambapo wameuona umuhimu wa kuendeleza na kusimamia biashara ya mianzi Duniani inayotajwa kuwa na tija kiuchumi na kimazingira na hivyo kuwahamasisha mataifa ya nchi wanachama kuzalisha kwa wingi zao hilo. 
 
Inakadiriwa kuwa Duniani kote eneo ambalo linalooteshwa mianzi ni zaidi ya hekta Bilioni 30 huku Barani Asia pekee zao hilo linaliingizia zaidi ya dola Bilioni 60 kwa mwaka kutokana na matumizi mbalimbali ya zao hilo.
MWISHO.




Share:

Mazungumzo kati ya Marekani na China yaambulia patupu

Mvutano wa kibiashara umeendelea kati ya Marekani na China huku nchi hizo zikitoa kauli zinazokinzana wakati ambapo Rais Trump ameamua kuongeza ushuru maradufu kwa bishaa za China.

China na Marekani zinatoa taarifa zinazotofautiana juu ya mazungumzo ya biashara. China imesema bado ina matumaini kuhusu kuutatua mvutano wa kibiashara, wakati Marekani imesema imeongeza ushuru mara mbili kwa bidhaa kutoka China. Hata hivyo mjumbe wa China katika mazungumzo na Marekani Liu He ameonya kwamba kuna viwango ambavyo nchi yake haitakuwa tayari kuvivuka.

Makamu wa waziri mkuu wa China Liu He amesema mazungumzo kati ya nchi yake na Marekani hayajavunjika licha ya kuwepo vikwazo vidogo ambavyo ni vya kawaida na kwamba China itaendela kuwa na mtazamo chanya juu ya mazungumzo ya biashara na Marekani, licha ya Rais Trump kuamua kuziongezea ushuru bidhaa za China.
 
Maoni ya Liu yanakinzana na ya waziri wa fedha wa Marekani Steve Mnuchin, ambaye aliwaambia waandishi wa habari wa CNBC kwamba hakuna mazungumzo yoyote ya biashara yaliyopangwa kufanyika kati ya nchi hizo mbili kwa sasa.

Rais wa Marekani Donald Trump amejisifu kwa kuandika kwenye Twitter kwamba ameikomoa China kwa kiasi ambacho labda nchi hiyo haitotaka kurudi kwenye meza ya majadiliano kabla ya uchaguzi wa 2020.

Marekani imechochea vita vya biashara kwa kuongezaushuru kwa thamani ya dola bilioni 200 kwa bidhaa za China zinazoingia nchini humo. Wachambuzi wa China wamesema huenda Marekani haina utayarifu kwa kile inachoweza kuhimili.Gazeti la kizalendo la Global Times limeandika kwenye tahariri yake kwamba Marekani haijatambua maslahi ya pande zote mbili, na wala haizingatii kwa kiasi kikubwa uvumilivu wa China.

Mnamo siku ya Ijumaa, Rais Donald Trump aliweka vikwazo vipya dhidi ya bidhaa zinazoingia Marekani kutoka China. 

Hatua hiyo iliongeza ushuru kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwenye bidhaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na simu za mkononi, kompyuta na vitu vya kuchezea watoto. Wizara ya Biashara ya China imesema imehuzunishwa mno na uamuzi wa Marekani.


Share:

UCHAGUZI MKUU AFRIKA KUSINI 2019 MASELE AMPONGEZA MALEMA KWA KUONGEZA VITI BUNGENI.



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele amempongeza kupitia ukurasa wake wa tweeter kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) Julius Malema kwa kupata viti vingi vya ubunge kwenye uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini uliofanyika Mei 8 2019.


Ukilinganisha na ushindi waliopata miaka mitano iliyopita. EFF ndio chama pekee kilichoongeza viti vingi ukilinganisha  na vyama vikongwe kama ANC iliyopoteza viti 19 na Chama Cha DA Pia kimepoteza viti 6. 

Malema “the Son of the Soil", kama anavyotambulika na wafuasi wa chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF), ameweza kuongeza viti 18 bungeni  nakufikisha viti 44 ikilinganisha na viti 26 vya kipindi kilichopita.

Masele ambaye ni Mbunge wa jimbo la shinyanga Mjini na Malema ni marafiki wa karibu na wa muda mrefu tangu wakiwa viongozi wa vijana wa vyama vya CCM na ANC. Pia ni wabunge wa Bunge la Afrika ambalo Makao  Makuu yako nchini Afrika kusini.

Viongozi hao vijana wameonekana jijini Johannesburg  wakiwa pamoja wakipongezana. Masele ambaye yuko nchini Afrika kusini kikazi katika Bunge la Afrika. 

Mheshimiwa Masele pia amempongeza  kiongozi wa  chama tawala ANC Rais Cyril Ramaphosa kwa ushindi wa chama chake. Rais Ramaphosa anatarajiwa kuchaguliwa na Bunge la Afrika kusini kuwa Rais wa nchi hiyo. 

Uchaguzi mkuu wa mwaka huu umekuwa  chini uangalizi wa taasisi mbalimbali za kimataifa ambapo timu ya  Umoja wa Afrika ilikuwa ikiongozwa na Rais mstaafu wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete. 

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, shughuli za kuhesabu kura katika uchaguzi huo zimekamilika kwa asilimia 100 na chama tawala nchini Afrika ya Kusini African National Congress (ANC) kimepata asilimia asilimia 57.5 ikiwa ni ushindi mdogo zaidi kwa chama hicho ambacho kimeitawala Afrika ya Kusini tangu kukomeshwa kwa utawala wa ubaguzi wa rangi miaka 25 iliyopita. 

Idadi ya watu waliopiga kura nchini humo imeshuka baada ya asilimia 65 pekee ya raia kujitokeza katika uchaguzi huo.

 Chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) kimejipatia asilimia 20.7 ya kura huku chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Julius Malema kikijipatia asilimia 10.7 ikiwa ni mafanikio ikilinganishwa na asilimia 6.3 ya kura ilizopata chama hicho miaka mitano iliyopita.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akikumbatiana na Kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Julius Malema Mei 11,2019

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiteta jambo na Kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Julius Malema Mei 11,2019

Share:

Agizo la Rais Magufuli Njombe latekelezwa,stendi kuu mpya yaanza kazi

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkoa wa Njombe umeanza rasmi kutumia kituo kipya cha mabasi mjini Njombe ikiwa ni baada ya agizo la rais alilotoa april 10 akiwa mkoani humo kuwa kituo hicho kianze kazi baada ya siku 30

Ujenzi wa kituo hiki unaofadhiliwa na benki ya dunia ulioanza 2013 umekuwa ukisuasua kwa kipindi kirefu licha ya uwepo wa fedha jambo ambalo lilimkasirisha Rais Magufuli na kuamua kutoa siku therathini kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe kukamilisha ujenzi huo.

Emmanuel George ambaye ni katibu tawala wilaya ya Njombe Yenye Halmashauri tatu ikiwemo mji Njombe,akizungumza mara baada ya kuanza Kutumika Kwa  kituo hicho mapema alfajiri amesema serikali imefanya jitihada za lazima kukamilisha mradi huo ambao umeanza kutumika licha ya kuwepo kwa baadhi ya maeneo machache ambayo hayaja kamilika huku akitaja faida zake kiuchumi.

"Licha kuanza kwake kuna changamoto ndogo ndogo ambazo tunaendelea nazo na leo ndio imeanza kufanya kazi, ni stendi kubwa na ya kisasa na itakuwa ni chachu ya kwenye mapato ya halmashauri,vitu ambavyo havijakamilika ni vichache kwasababu ya mvua"alisema katibu tawala

Baadhi ya madereva na abiria Akiwemo Michael Msilu na Amosy Kusalula wakizungumzia kituo hicho wamepongeza hatua zilizochukuliwa na serikali huku wakidai bado kuna changamoto ya miundombinu muhimu ikiwemo jengo la abiria na eneo la mama Lishe ambayo bado yanaendelea kujengwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Iluminatha Mwenda Amesema Ujenzi wa Kituo Hicho Kipya Umefikia Asilimia 95 na Kwamba Zoezi la Ukamilishaji Linaendelea.

"Sasa hivi stendi yetu imekwishakamilika kwa asilimia 95 kama mnavyoona magari yamekwishaanza kuingia na hizi asilimia tano ndani ya wiki mbili tutakuwa tumekwisha kamilisha,na kama unavyo jua Njombe ni mvua sana tunaendelea kuomba ile sala ambayo tunasali kila siku ya toba basi iendelee kutusaidia ili mvua isiendelee kunyesha"alisema Iluminatha Mwenda

Ujenzi wa kituo hicho Kipya Cha Mabasi Mjini Njombe umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 9 za kitanzania Ikiwa Kila Mtu Anayeingia Ndani ya Kituo Hicho Anapaswa Kulipa Ushuru wa Shilingi 200 na Baada ya Mabasi Kutoka Ndani ya Stendi Hiyo Kituo Cha Kwanza Kwa Barabara ya Kwenda Makambako Kitakuwa Kibena Huku Wanaokwenda Songea Kikiwa Nundu .


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 12




Share:

Saturday, 11 May 2019

WAANGALIZI WASEMA UCHAGUZI WA AFRIKA KUSINI ULIKUWA HURU NA HAKI


Waangalizi wa Kimataifa ambao wamekuwa wakifuatilia Uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini, katika ripoti yao ya awali, wanasema Uchaguzi huo ulikuwa huru, haki na wa amani.

Ripoti hii imekuja siku mbili baada ya raia wa nchi hiyo kupiga kura tarehe nane ,na matokeo ya awali yanaonesha kuwa chama tawala ANC kinaongoza na kinaelekea kupata ushindi.

Mwenyekiti wa waangalizi wa Umoja wa Afrika, rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete, amesema kuwa zoezi la upigaji kura liliendelea kwa amani na utulivu katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Aidha, ameongeza kuwa waangalizi wa Umoja wa Afrika wanasema Tume ya Uchaguzi ilijiandaa vema, kufanikisha Uchaguzi huu, huku maafisa wa usalama wakitoa ushirikiano wa kuhakikisha kuwa usalama unakuwepo kipindi chote cha upigaji kura.

Hata hivyo, Kikwete amesema vijana wengi hawakuonekana wakipiga kura licha ya kuwa ndio wengi nchini humo, suala ambalo Umoja wa Afrika unataka wadau kuliangazia.

“Licha ya mambo mengine, kwenda vizuri, tuliona kuwa vijana wengi hawakujitokeza kupiga, hili ni suala ambalo linastahili kupewa ufumbuzi wa haraka,” alisema Kikwete.

Waangalizi wa Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC pia walitoa ripoti yao ambayo pia imeeleza kuwa Uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.

Wachambuzi wa siasa barani Afrika, wamekuwa wakisema miaka ya hivi karibuni, waangalizi wa Uchaguzi wamekuwa wakitumia mbinu za kidiplomasia, kutuliza joto la kisiasa katika mataifa mbalimbali ya Afrika.

Chama cha ANC ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1994, kinatarajiwa kushinda Uchaguzi huo kwa kati ya asilimia 55-59 huku kile cha EFF kikitarajiwa kumaliza katika nafasi ya tatu.

Tume ya Uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokea ya mwisho, mwishoni mwa wiki hii.
Chanzo - RFI 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger