Thursday, 2 May 2019

MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI 2019 YAANZA DODOMA


Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 yameanza hii leo jijini Dodoma ambapo yanafanyika kitaifa kwa awamu ya pili mwaka huu. Kilele cha maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Mei 03 ambapo wadau wa habari hukutana pamoja kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari/ wanahabari katika gurudumu la maendeleo.Picha na KD Mula, Funguka Live Blog
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akiwasilisha mada kwa niaba ya makundi ya washiriki kwenye maadhimisho hayo.
Lilian Kallaghe kutoka taasisi ya SIKIKA akiwasilisha mrejesho wa majadiliano kwa niaba ya washiriki wengine. 
Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu (UNESCO) nchini Tanzania, Nancy Kaizirege akitoa salamu za shirika hilo kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho hayo walisimama kwa muda kama ishara ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na pia mmiliki wa makampuni ya IPP, Mzee Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia leo akiwa nchini Dubai akiwa na miaka 75.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (katikati) akimsikiliza kwa umakini Mweka Hazina wa taasisi hiyo, Michael Gwimile kwenye maadhimisho hayo (kulia).
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari wakifuatilia mada kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye maadhimisho hayo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo akiwemo Mkurugenzi wa kampuni ya Uhuru Media Group, Ernest Sungura wakifurahia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji mada kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho hayo akiwemo Joyce Shebe kutoka Clouds Media Group (kushhoto) wakifuatilia mada kwa umakini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 yameanza hii leo jijini Dodoma, yakilenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari.

Msisitizo mkubwa umetolewa kwa wadau wa habari kujadili viashiria vya kushuka kwa uhuru vya habari nchini Tanzania na namna ya kuviepuka hususani baadhi ya waandishi wa habari kupotea, kukamatwa na kushikiliwa kwa muda na mamlaka nchini.

Aidha wanahabari pamoja na wahariri wamepewa changamoto ya kuhosi sababu za Tanzania kushuka kwa nafasi 25 kutoka nafasi ya 93 mwaka jana hadi nafasi ya 118 mwaka huu kwenye orodha ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.

“Tunapaswa kuhoji kwa nini tumeshuka kwenye nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, mwaka jana tulishuka kwa nafasi 10 kutoka nafasi ya 73 hadi nafasi ya 93 na mwaka huu tumeshuka kutoka nafasi ya 93 hadi nafasi ya 118”, wamehoji washiriki kwenye maadhimisho hayo.

Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa amesisitiza waandishi wa Habari Tanzania kuongeza kiwango chao cha elimu ili kuendana na matakwa ya sheria hatua itakayosaidia kufanya shughuli zao kwa mujibu wa taaluma bila vikwazo kutoka kwa mamlaka za kisheria.

Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu (UNESCO) nchini Tanzania, Nancy Kaizirege amesema waandishi wa habari wanapaswa kushikamana pamoja ili kulinda usalama wao.

“Waandishi 99 waliuawa mwaka jana wakiwa kazini na tangu mwaka 1994 hadi 2018 jumla ya waandishi 1,377 wameuawa kutokana na majukumu hayo”, amebainisha Kaizirege akieleza jinsi usalama wa waandishi wa habari ulivyo mashakani.

Taasisi mbalimbali zimeshiriki kwenye maandalizi ya maadhimisho hayo ikiwemo MISA Tanzania, Internews, IMS, UTPC, TMF, TEF, UK Aid, TAMWA, MCT, UN Tanzania, FES, Unesco na Serikali ya Tanzania, kauli mbiu ikiwa ni “Vyombo vya Habari kwa Demokrasia, Tasnia ya Habari na Uchaguzi nyakati za upotoshwaji wa taarifa” ambapo kilele cha maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Mei 03.

Share:

RC MONGELLA AGOMA KUFUNGUA MRADI, RUNGU LAMUANGUKIA MHANDISI


Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa pamoja na viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya anaendelea na ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Mwanza. Hapa Mongella akiwasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Lumnve iliyopo Kata ya Bujora wilayani Magu.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kwenye ukaguzi wa kisima kirefu cha maji Isangijo ikiwa ni moja ya visima 16 vinavyochimbwa wilayani Magu ili kuondoa adha ya maji kwa wananchi.
Ukaguzi wa shamba la miti la Bahati Kwangu ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Busekwa, Kata ya Bujashi wilayani Magu lenye miti zaidi ya elfu 10 likiwa na ukubwa wa Hekali saba, lengo likiwa ni kuhifadhi mazingira pamoja na kitega uchumi kwa baadae.
Ukaguzi wa Zahanati ya Isangijo wilayani Magu.
Ukaguzi wa mradi wa maji wa kisima kirefu katika Kijiji cha Matela, Kata ya Isangijo wilayani Magu.
Ukaguzi wa mradi wa uzalishaji mali wa kikundi cha ESM Kangara ambapo kinajihusisha na ufugaji wa kuku, bata, njiwa, mbwa na paka.
Ukaguzi wa Zahanati ya Bundilya wilayani Magu.
Jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha kwanza kujengwa wilayani Magu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kwenye ukaguzi wa Kituo cha Afya Nyerere kilichopo Kata ya Kangara wilayani Magu.
Ukaguzi wa shughuli za kikundi cha wazalishaji mali cha "Meremeta Leather Group" wilayani Magu kinachojihusisha na utengenezaji wa bidhaa za ngozi ikiwemo viatu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alitembelea Shule ya Musabi wilayani Magu ambapo kuna klabu ya TAKUKURU kwa wanafunzi wa shule ya msingi.
Wanafunzi wakafurahi kukutana na viongozi wao.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akaweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari Maligisu wilayani Kwimba.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alipotembelea Shule ya Sekondari Maligisu wilayani Kwimba.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aligoma kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Kadashi wilayani Kwimba ambao ulianza mwaka 2013 ambapo aliagiza mradi huo ukamilike na kutoa maji katika magati yote 21 ifikapo Juni Mosi 2019.

Tazama BMG Online TV hapa chini

Share:

SIKU YA WAFANYAKAZI(MEI MOSI) MKOA WA ARUSHA YAPENDEZA


Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha(Auwsa) wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya Mei Mosi jijini Arusha. 
Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya mkoa wa Arusha wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya Mei Mosi jijini Arusha 
Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya Mei Mosi jijini Arusha. 
Wafanyakazi wa kampuni ya Lodhia wakiwa na furaha wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi 2019. 
Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Idd Kimanta akimkabidhi kombe la ushindi katika michezo ya Mei Mosi 2019,Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shanna. 
Wafanyakazi wa kiwanda cha A to Z wakifurahia ushindi wa kwanza 
Viongozi jukwaa kuu wakiimba wimbo wa mshikamano. 

Share:

WANANCHI WA BUSI, MAUNO AMBAO HAWAJAJENGA MAENEO YAO KUPATA UMEME


Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akizungumza na baraza la madiwani wa Kondoa kabla ya kuanza ziara ya kuwasha umeme katika kijiji cha Mauno pamoja kituo cha Afya cha Busi mkoani Dodoma.
Sehemu ya madiwani wakimsikiliza Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika kikao hicho

Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akizungumza na wananchi wa Kinyasi alipfanya ziara ya kuwasha umeme kijiji cha Mauno pamoja na Kituo cha Afya cha Busi wilayani Kondoa
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akiwaonyseha wananchi kifaa cha kuunganishia umeme
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani akiwakabidhi wananchi kifaa cha kuunganishiwa umeme katika kitongoji cha Kinyasi.
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akimueleza jambo mbunge wa Kondoa ambaye pia ni Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kabla ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Busi
Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani,akisisitiza jambo kwa wananchi wa kijiji cha Busi kabla ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya
Baadhi ya wananchi wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani alipokuwa anazungumza nao kabla ya kuwawashia umeme katika kituo cha Afya cha Busi.
Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani,akiwasha umeme katika kituo cha Afya cha Busi wilaya ya Kondoa.

Picha Zote na Alex Sonna-Fullshangwe blog
***
WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani amewataka wakazi wa vijiji vya Mauno na Busi wilayani Kondoa ambao bado hawajajenga kwenye maeneo yao kuweke miti ili wasogezewe huduma ya umeme kwa haraka.

Pamoja na hayo, amemwagiza Meneja wa shirika la umeme (Tanesco) pamoja na mkandarasi kuhakikisha wanamaliza kusambaza huduma ya umeme katika vijiji vyote vilivyosalia wilayani Kondoa ndani ya wiki moja.

Waziri Kalemani ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Mauno pamoja na kituo cha Afya cha Busi huku akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Kondoa ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji. 

Waziri Kalemani amewataka wananchi hao kuwa, kuanzia sasa uunganishwaji wa umeme ni sh. 27,000 tu, uwe wa Tanesco au Rea huku akiahidi kupiga mnada wa kuku wa mkazi ambaye atashindwa kulipia kiasi hicho kwa ajili ya kuunganishiwa huduma hiyo.

Kalemani amefafanua kuwa Tanesco kupitia mkandarasi hawana sababu ya kusuasua kuwasha umeme katika maeneo hayo kwa kuwa nguzo na nyaya wanazo za kutosha.

Aidha Waziri Kalemani ameahidi kurejea kwenye kata hiyo mwezi ujao kufuatilia agizo lake.

Mbunge wa Kondoa,Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,aliwataka wananchi kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali za kuwapelekea huduma ya umeme kwa kutumia fursa hiyo kuingiza umeme katika nyumba zao.

Pia ameishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa jitihada kubwa inazozifanya kupeleka maendeleo kwa wananchi na kujali wananchi wanyonge na wenye hali ya chini.

Mmoja wa wakazi kijijini cha Busi Bw.Nuru Bi Mdanga akizungumza baada ya kuwashiwa umeme ameelezea furaha yake ya kupunguzwa kwa gharama ya uunganishwaji wa huduma hiyo pasipokujali unatokea Rea au Tanesco.

Share:

MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA AMLILIA DR. REGINALD MENGI


Mhe. Stephen Masele
Makamu wa rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kilichotokea huko Dubai Falme za Kiarabu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter,Mheshimiwa Masele ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) ameandika :


"Nimepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha mzee wetu Reginald Abraham Mengi. Mzee Mengi atakumbukwa daima kwa mchango wake wa maendeleo kwa taifa letu. Naungana na watanzania wenzangu kumuombea na kuwapa pole ndugu na marafiki wote.Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani.Amen"- Stephen Masele.


R.I.P Dr. Reginald Mengi.
Share:

Mbunge Adai Ukosefu wa Maji Unahatarisha Ndoa

Mbunge wa Handeni Vijijini, Mboni Mhita (CCM), amesema ndoa za wanawake wa jimbo hilo zimetetereka kwa sababu wanaamka alfajiri kwenda kuchota maji.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji bungeni leo Mei 2, Mboni amesema badala ya wanawake kuhudumia ndoa zao muda huo hutoka kwenda kusaka maji na hivyo kuhatarisha ndoa zao.

“Ndoa nyingi za wanawake wa Handeni Vijijini ziko hatarini wanaamka alfajiri na kushindwa uaminifu, wengine ndoa zao wamezikosa kwa sababu ya kudamka muda huo kwenda kusaka maji na wakati mwingine hurudi bila maji,” amesema Mbunge huyo.


Share:

Wizara ya Maji Yaomba kutengewa Sh634.19 bilioni katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2019/2020.

Waziri wa wizara ya maji, Profesa Makame Mbarawa amewasilisha mapendekezo ya  kutengewa Sh634.19 bilioni katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2019/2020.

Ametoa mapendekezo hayo leo   Alhamisi  Mei 2 bungeni jijini Dodoma akitaka Bunge kuridhia mapendekezo hayo ili kuiwezesha kutekeleza malengo na miradi ya kipaumbele.

Katika fedha hizo, waziri huyo amesema Sh23.72 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh610.46 bilioni zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Katika fedha za miradi, amesema asilimia 57 zitatokana na vyanzo vya ndani na asilimia 43 zitatoka nje.

“Katika fedha za matumizi, Sh17.45 bilioni zitatumika kulipa mishahara ya watumishi wa wizara na chuo cha maji na Sh6.26 bilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo,” amesema Profesa Mbarawa.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019  ya Sh697.57 bilioni, amesema hadi Aprili 2019 wizara ilikuwa imepokea Sh16.65 bilioni sawa na asilimia 68 ya Sh24.36 bilioni zilizotengwa kwa matumizi ya kawaida na Sh343.48 bilioni sawa na asilimia 51 ya Sh673.21 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.


Share:

Maandalizi Ya Maadhimisho Ya 26 Ya Siku Ya Uhuru Wa Vyombo vya Habari Duniani Yapamba Moto Jijini Dodoma.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ikiwa kila ifikapo Mei 3,kwa kila mwaka Tanzania huungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya vyombo vya habari Duniani,Maandalizi ya maadhimisho hayo yamepamba moto jijini Dodoma ambapo kitaifa yanafanyika hapa mkoani Dodoma.
 
Akizungumza     jijini Dodoma katika maandalizi hayo  Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi  Nevili Meena amesema Wameshirikisha wadau mbalimbali wa habari wakiwamo waandishi wa habari,wahariri ,wamiliki vya vyombo vya habari, maofisa wa Serikali pamoja na mashirika mbalimbali ya Kijamii na Kimataifa  hapa nchini.
 
Sanjari na hayo ,Meena amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na mada mbalimbali zinazohusu changamoto zinazoikabili tasnia ya habari hapa nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha habari shirika la Elimu ,Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) ,Nancy Kaizilege amesema Jumla  ya waandishi wa habari 1,307 waliuawa kati ya mwaka 1994 na 2018 wakati wakitekeleza majukumu yao ya kikazi katika nchi mbalimbali Duniani
 
“Tishio hili linafanya tuwe macho wakati wote, lazima tusimame pamoja, tushikamane ili kulinda uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari”alisema.
 
Alisema kuwa ripoti  hiyo iliyotolewa na UNESCO, inadai kuwa waandishi wa habari 99 waliuawa katika kipindi cha  mwaka 2018 wakitekeleza majukumu yao maeneo mbalimbali.
 
Amesema  kuwa mwaka huu maadhimisho ya mkutano wa kimataifa yameandaliwa  kwa pamoja na Serikali ya Ethiopia na Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, kuanzia 2 hadi 3 Mei 2019.
 
Aidha ameongeza kuwa,mada ya Mwaka huu ya  maadhimisho ya  26  uhuru wa vyombo vya habari ni “Vyombo vya Habari kwa Demokrasia: Tasnia ya Habari na Uchaguzi katika Nyakati za Upotoshaji wa Taarifa”



Share:

Taarifa Kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu

Jeshi la  Polisi limesema kuwa halijatangaza nafasi za ajira katika chombo chochote cha habari, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na kuzipuuza taarifa hizo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger