Wednesday, 7 December 2016
Tuesday, 6 December 2016
Mbunge wa Ukonga apinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mbunge
wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) amepinga amri iliyotolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya wafanyabiashara kufunga maduka
yao kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa nne ili
wafanye usafi.
Amesema
amri hiyo ni batili na haitekelezeki kwa sababu inarudisha nyuma uchumi
wa wananchi hususani wafanyabiashara ndogondogo ambao wanategemea
kipato chao cha siku kuendesha maisha yao.
Akizungumza
na wananchi wa Mtaa wa Kivule mwishoni mwa wiki, Waitara alisema yeye
hapingani na watu kufanya usafi katika maeneo yao, lakini amri ya
kufunga maduka kila Jumamosi inaathiri uchumi wa wananchi hivyo ni
batili na haipaswi kuendelea kuwapo.
Siku
chache baada ya kuteuliwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda
alipiga marufuku kufungua maduka na biashara zingine kabla ya saa nne
asubuhi ili muda huo utumike kufanya usafi na anayekaidi agizo hilo
hutozwa faini isiyopungua Sh 50,000.
Mbunge
huyo wa Ukonga alisema uchumi wa watu masikini hususani wa mjini
unategemea kile wanachokizalisha kila siku, hivyo amri ya kufunga
biashara kila wiki ni kurudisha nyuma juhudi za wananchi kujiletea
maendeleo yao.
Katika
mkutano huo aliwaambia wananchi hao kujiwekea utaratibu kuhakikisha
maeneo yao yanakuwa safi wakati wote na kila Jumamosi wafungue biashara
zao asubuhi kama kawaida na wasibughudhiwe na mtu yeyote.
“Mimi
naunga mkono utaratibu wa kufanya usafi kila mwezi uliotangazwa na Rais
Dk. John Magufuli ambao upo kwa mujibu wa taratibu, lakini huu wa kila
Jumamosi mimi sina mwongozo nao na hizo faini za kila wiki sizitambui na
ni batili.
“Ninachotaka
kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, hizi faini zinatozwa bila
utaratibu hata kama eneo la mtu ni safi sitaki kuzisikia, wananchi hawa
si wanyama, waelimishwe waachwe wajiwekee utaraibu wao.
“Hivi
mama, baba ntilie anayepika maandazi, vitumbua, chapati afunge
biashara tangu asubuhi mpaka saa nne halafu hiyo chai itanywewa na nani,
huyu mtu unamwambia afunge biashara ili akaibe mtaani?” alihoji mbunge
huyo na kuongeza:
“Watendaji
lazima muwasikilize watu, nasikia kinachofanyika ni mwendo wa
kuviziana, waacheni watu wafanye kazi, hapa ni kazi tu sio faini tu”
alisema Waitara.
Katika
hatua nyingine, Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Kivule alivunja kikundi cha ulinzi kilichokuwa katika ofisi hiyo kwa
tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kuwanyanaysa
wananchi.
Badala
yake, alisema uitishwe mkutano wa hadhara watu wote wanaohitaji kazi
hiyo walete maombi katika ofisi hiyo na baadaye wajadiliwe na wananchi
katika mkutano wa hadhara ili kuepuka kuwapa kazi watu wasiokuwa
waaminifu katika jamii.
Monday, 5 December 2016
Waziri Mkuu Majaliwa Aitembelea Familia Ya Marehemu Sokoine Monduli Juu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Napono Sokoine (wapili kulia) na
Nekiteto Sokoine (kulia) ambao ni wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu,
Marehemu Edward Sokoine wakati aipokwenda nyumbani kwa marehemu, Monduli
Juu kuisalimia familia akiwa katika ziara ya wilaya ya Monduli
Desemba 4, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliekuwa
Waziri Mkuu, Edward Sokoine wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu,
Monduli Juu akiwa katika ziara ya wilaya ya Monduli
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa
aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia
akiwa aktika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 20, 16. Kushoto
kwake wajane wa marehemu, Napono Sokoine (wpili kulia) na kulia ni
Nekiteto Sokoine . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa
aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia
akiwa aktika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 20, 16. Kushoto
kwake wajane wa marehemu, Napono Sokoine (wpili kulia) na kulia ni
Nekiteto Sokoine . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo.(Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)