Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa
kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha
aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhumiwa faini ya Sh7
milioni au kifungo.
Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha
alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa
facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha
ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.
Diwani wa Kata
ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu
michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh
800,000/- ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.
Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.
"Tumesikia
familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea
kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,”
alisema.
WIzara ya elimu na mafunzo ya ufundi kupitia tume ya vyuo vikuu Tanzania ilifuta udahili wa wanafunzi 628 wa st.joseph arusha na kuwahamishia chuo cha st.joseph kilichopo luguruni kusomea ualimu ngazi ya digrii kwa miaka 5. Wizara ya elimu ikishirikiana na NACTE walifanya uchunguzi na kufuatilia sifa za hawa wanafunzi,na kugundua kwamba wanafunzi 94 ndio wenye sifa za kusomea ualimu ngazi ya cheti. Kutokana na hali hiyo TCU inatangaza kwamba wanafunzi 94 tu ndio wenye sifa za kuendelea kusoma ngazi ya cheti kati ya 628. hivyo wanafunzi 534 hawana sifa za kusoma.
"Ndugu msomaji tunaomba support kwa
kutangaza nasi na kufikia wateja zaidi ya laki moja kwenye blog yetu ili tuendelee kutoa habari zenye uahika
watsup au call 0768260834-kwa matangazo"
Viongozi
na makada wa Chadema waliokuwa wakisafiri kutoka Kahama kuelekea jijini
Mwanza jana wamejikuta wakishindwa kuingia kwenye ofisi za chama hicho
mjini Shinyanga kutia saini kitabu cha wageni baada ya Jeshi la Polisi
kuzuia shughuli yoyote ya chama hicho mjini humo.
Waliokumbwa
na adha hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman
Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji na wabunge Godbless Lema, Ester
Bulaya, John Heche, Halima Mdee na viongozi kadhaa wa kitaifa wa
Chadema.
Magari
manne ya polisi yaliyosheheni askari waliobeba silaha na mabomu ya
kutoa machozi yaliupokea msafara wa Chadema uliokuwa ukielekea Mwanza,
mara tu ulipoingia mjini Shinyanga na kuusindikiza hadi nje ya mji
kuhakikisha hausimami ndani ya mji huo.
Bajeti
ya Serikali iliyotangazwa huenda ikapunguza idadi ya watu wanaopenda
kuonekana tofauti, kwenye usajili wa magari kwa kuandika majina yao
badala ya namba.
Wamiliki
wa magari wanaotaka kusajili namba binafsi kama kuweka majina yao, sasa
watalipa Sh10 milioni badala Sh5 milioni za awali, kwa kipindi cha
miaka mitatu.
Akitoa
mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2016/17 jana,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliomba Bunge liridhie
kufanya marekebisho ya Sheria ya Magari (Kodi na uhamisho wa umiliki)
ili kupandisha usajili wa namba hizo.
Namba
hizo binafsi zilizoanzishwa miaka minne iliyopita, zinaruhusu mtumiaji
kuandika jina au neno lolote kwenye gari lake tofauti na namba za
kawaida zinazotumika nchini.
KINDLY
BE NOTIFIED THAT SIGNING FOR MEALS AND ACCOMMODATION ALLOWANCES 3RD
QUARTER, FOR THE ACADEMIC YEAR 2015/2016, WILL BE ON THURSDAY 9TH JUNE
2016 AT RAILA ODINGA GROUNDS FROM 08:00AM TO 16:00PM.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY The Partnership for Skills in Applied
Sciences, Engineering and Technology (PASET) in collaboration with the
Association of African Universities (AAU) is currently implementing a
Benchmarking Initiative whose goal is to improve monitoring of quality
and relevance of learning, research and knowledge/technology transfer in
Sub-Saharan Africa (SSA) Universities. The exercise, unlike university
ranking, is based on self-assessment and willingness of a university to
participate in the exercise. The main benefits for participation include
collection of data that will be used to enhance students’ experiences
and improve overall university quality. Due to the fact that UDOM strives to
become a centre of excellence, a decision has been made for the
University to take part in this important exercise. Both undergraduate
and postgraduate students are invited to fill in a brief questionnaire
for that matter. Please, spare a few minutes to complete this crucial
exercise. To access the questionnaire, please, log-in using your account in UDOM SR system.
Each student is expected to have completed the exercise in seven (7) days from the date of this announcement.
OFFICE OF THE DEPUTY VICE CHANCELLOR, ACADEMIC, RESEARCH AND CONSULTANCY (DVC – ARC)
Mwanafunzi na mwanachuo wa chuo kikuu cha SUA anaetambulika kwa jina la Magreth amejichoma kisu tumboni na kupata majeraha. Mwanafunzi huyo amejichoma kisu akiwa chumbani kwake maeneo ya hosteli zilizopo barakuda mazimbu. Maswayetu blog imefanikiwa kufanya uchunguzi na kuongea na baadhi ya wanafunzi ambao ni marafiki zake,wamedai kwamba kisa cha kujichoma kisu ni kutokana mapenzi ,lakini wakasisitiza kwa kusema kwamba yawezekana kuna swala jingine,lakini wanahisi ni mapenzi. Hata hivyo jitihada za kumtafuta na kuongea nae yeye mwenyewe ziligonga mwamba kutokana na binti huyo kuwa hospital akiwa aanatibiwa.
Endelea kutembela MASWAYETU BLOG kwa habari mbalimbali za uhakika. kama una taarifa yoyote tutumie watsup kwa namba 0768260834 tutairusha moja kwa moja na itafikiwa na watu zaidi ya laki moja kwa siku.
Wakati naibu spika wa jamhuri ya muungano wa tanzania akihairisha bunge jioni ya leo,amefuta rasmi posho zote za wabunge wa ukawa ambao wa mekuwa wakisusia bunge,baada ya dua ya asubuhi.
Naibu spika ametoa maamuzi kwamba AMEFUTA RASMI POSHO ZOTE ZA WABUNGE WAMBAO WANTOKA BUNGENI BILA RUHUHA.
Habari wakuu,
Leo ni siku muhimu itakayoamua mustakabali wa mambo mengi katika nchi
yetu kwa kipindi cha Julai 2016 mpaka Juni 2017 kutokana na kusomwa kwa
bajeti itakayoamua utekelezaji wa mambo mengi ya msingi ikiwemo kodi na
ugharamiaji wa huduma muhimu. Bajeti hii itaendana na kusomwa kwa bajeti
zote zilizo chini ya jumuiya ya Afrika Mashariki. Tuwe sote pamoja
kujuzana yanayojiri kutoka Dodoma kuhusu bajeti yetu.
YANAYOJIRI MCHANA
Wabunge wameshaingia bungeni na wageni wengi wanaendelea kuwasili
ikiwemo viongozi wa dini, mabalozi, viongozi wastaafu maafisa usalama na
wengine wanaowakilisha marika mbalimbali katika jamii.
Wabunge wa upinzani wametoka nje baada ya naibu spika kuingia bungeni
Waziri wa Fedha, Philip Mpango ameingia bungeni na mkoba uliobeba
nyaraka za bajeti ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mpango anamshukuru
Rais Magufuli kwa kumteua kuwa waziri wa fedha na anawapongeza wengine
waliochaguliwa/kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za serikali.
Dk. Mpango amesema bajeti imezingatia maoni ya wadau mbalimbali ikiwemo
wenye viwanda pia amewashukuru watanzania waliotii Rai ya Rais Magufuli
ya kumuombea na kusema bajeti hio ni ya kwanza ya serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais Magufuli.
Dk. Mpango amesema bajeti amesema bajeti ina sehemu kuu mbili
Kutatua matatizo yanayowakabili wananchi, kufanya mabadiliko makubwa serikalini hususan kuondoa kazi kwa mazoea
Kujenga uchumi wa kiwango cha kati kwa uhalisia na kujenga ajira hasa kwa vijana
Dk. Mpango: Kauli mbiu ya bajeti za Afrika Mashariki ni kuongeza
uzalishaji viwandani ili kuongeza ajira. Bajeti ya maendeleo imeongezwa
mpaka kufikia asilimia 40 kwa mara ya kwanza Tanzania.
Kwa sasa Waziri Mpango anaongolea mapitio ya bajeti ya 2015/16
#Mpango amesema serikali itawasilisha kwa dharula marekebisho ya sheria
ya manunuzi ya umma ili manunuzi yaendane na thamani halisi.
Uzalishaji Viwandani
Kufikia azma ya viwanda serikali itatekeleza mikakati mbalimbali
ikiwemo kulipa fidia kwa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya viwanda,
kuboresha kupitia viwanda vidogo(SIDO)
Serikali itahakikisha viwanda vilivyopo vinafanya kazi ikiwemo
Kuchukua hatua stahiki kwa ajili ya wawekezaji wa viwanda walivyobinafsishiwa na serikali.
Kuimarisha utoaji wa mikopo kwenye sekta ya viwanda
Kuvutia kampuni za nje kuwekeza nchini kwa kuboresha mazingira ya uwekazaji
Utatuzi wa kero za wananchi
Rushwa kwenye utoaji wa huduma: Serikali imetenga shilingi 2.5 kuwezesha uanzishwaji wa mahaka za mafisadi.
Kutenga pesa kwa ajili ya TAKUKURU ili kutekeleza majukumu yake.
Kudhibiti upotevu wa mapato
Wafanyabiashara wanaokaidi kutumia mashine za EFD wanaweza kuzuiwa
kufanya biashara nchini kwa miaka 2. Kuanzia July 1 ni marufuku kwa
taasisi zote za serikali kufanya biashara na wafanyabiashara wasiotumia
mashine za EFD
#Serikali imedhamiria kuondoa kodi kwenye mazao ya kilimo, benki ya kilimo itapanua huduma zake mikoani.
Uchukuzi: Trilioni 2.49 kwa ajili ya upanuzi reli ya kati, ndege
mpya na kununua meli na kufanyia ukarabati za zamani. Kuhakikisha
TANESCO inakuwa na uwezo kifedha ili lijiendeshe lenyewe.
Elimu: Serikali imetenga trilioni 4.77 sawa na asilimia 22 ya
bajeti yote kwa ajili ya elimu ya msingi bila malipo, mikopo elimu ya
juu
Maji: Trilioni 1.02 kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa maji ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya maji.
Kuboresha mazingira ya kufanya biashara ikiwemo kodi na tozo
zinazolalamikiwa, kuboresha huduma za upatikanaji wa mikopo, usambazaji
wa gesi asili, kuondoa urasimu na kupambana na rushwa.
Serikali imetenga bilioni 2.4 kuboresha makazi ya wazee na watoto
Agizo la Rais kupunguza kodi ya mshahara litaanza kutekelezwa Julai mosi
Serikali inavipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa nidhamu,
utaratibu wa kodi kwenye maduka ya vyombo vya ulinzi utabadilishwa.
Marekebisho kwenye sheria ya kodi
Kuondoa kodi kwenye maharage ya soya kwani yalisahauliwa, kuondoa
kodi kwenye mbogamboga zote ili kuwezesha upatikanaji wa lishe bora kwa
gharama nafuu.
Pendekezo la kuondoa kodi kwenye dawa zinazotibu maji.
Bidhaa zinazotengezwa Tanzania Bara na kuuzwa Zanzibar zitatozwa VAT
na kinyume chake kwani kifungu cha sasa hakina kifungu cha marejesho ya
kodi.
Kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye bima ya vyombo vya
usafiri wa anga kukuza sekta ya Anga na mashirika ya kimataifa kutumia
mashirika ya bima ya hapa nchini.
Hatua hizi zinatarajiwa kuongeza mapato kwa serikali.
Kuondoa msamaha wa kodi kwenye kiinua mgongo cha wabunge kinachotolewa kila baada ya miaka mitano.