Wednesday, 8 June 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNE TAREHE 8.6.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

Tuesday, 7 June 2016

New AUDIO | MR BLUE Ft. ALIKIBA - MBOGA SABA | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

https://my.notjustok.com/track/download/id/99012/by/PSDOElRiG6
Share:

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) 

Tarehe 3 Juni 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya udahili wa kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya juu na Shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja unaoratibiwa na NACTE.

Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilisha mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki tatu hadi nne kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.

Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopenda kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.

Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa wazi na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.

Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya juu na Shahada ya kwanza kati ya wiki ya mwisho ya mwezi wa sita, 2016  na wiki ya kwanza ya mwezi wa saba , 2016.

Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 7 Juni, 2016

Share:

MWENYEKITI CHADEMA ADAIWA KUTEKWA, KUTESWA NA AFISA USALAMA WA TAIFA.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY



Mwenyekiti wa Chadema kata ya Sola Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu anayedaiwa kutekwa na Afisa usalama wa Taifa Wilayani humo.


AFISA Usalama wa Taifa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu,Peter Tewele anadaiwa kumteka, Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Sola wilayani humo Natalis Mataba(62) kisha kumpiga, kumtesa na kumtelekeza porini katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Tukio hilo linadaiwa kutokea juzi majira ya saa 2:30 asubuhi katika ofisi za
Usalama wa Taifa wilayani humo zilizoko katika kata hiyo, ambapo chanzo kinaelezwa kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akiwatukana.



Akizungumza na Waandishi wa habari akiwa hospitali ya wilaya akipatiwa matibabu, Mataba alisema kuwa Afisa huyo alifika nyumbani kwake majira ya saa 2:30 asubuhi akiwa ameambatana na mlinzi wa ofisi hiyo na kumtaka waongozane naye ofisini.




“Nilipofika ndani ya Ofisi hiyo Ofisa Usalama huyo wa wilaya alinieleza ya kuwa hii ni ofisi ya Usalama na siyo ya CHADEMA na kisha wakanipeleka kwenye moja ya vyumba vilivyoko ndani ya ofisi hiyo ambacho kina giza  na kisha kuniamuru nilale kifudifundi na ndipo walipoanza kunipiga ngumi na mateke”alisema.





Alisema kuwa baada ya kipigo hicho walimfunga kamba miguu na mikono
huku kichwani wakimvalisha mfuko wa sandalusi ambapo walimtoa nje na  kumuingiza katika gari dogo na kuondoka naye kwa kasi huku kukiwa na vijana wawili ndani ya gari hilo wakiwa wamemkandamiza kichwa chini.
 
“…walinipiga sana huku nikiwa nimefungwa kamba mikono hadi nikapoteza fahamu na baada ya kuona nimepoteza fahamu walinivua mfuko wa plastiki waliokuwa wamevalisha usoni kisha kunitupa katika moja ya pori ambalo sikulitambua na baadaye waliondoka” Alisema Mataba

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Rosemary Kirigini alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo alikiri
kupokea taarifa za Kiongozi huyo kutekwa na mfanyakazi wa serikali.
Kirigini alieleza kuwa hatua mbalimbali zikiwemo za uchunguzi zinaendelea, huku akibainisha kuwa ameshangazwa kusikia Afisa huyo akifanya jambo hilo wakati anafahamu taratibu za kisheria kwa mtu aliyekosea.
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Juni, 2016 amemteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Juni, 2016 amemteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi.
Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaaban Ally Lila aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mkoani Tanga.
Uteuzi huu unaanza mara moja.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Juni, 2016
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5 2016-ZANZBAR

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Title Image

WANAFUNZI WALIOTEULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANAO KATIKA

 SKULI MBALI MBALI ZA SERIKALI MWAKA 2016


KIDATO CHA TANO SANAA MWAKA 2016


JANG'OMBE FARAJA HAMAMNI


ZANZIBAR COMMERCIAL KIPONDA MWANAKWEREKWE "C"








KIDATO CHA TANO SAYANSI MWAKA 2016




BENBELLA KIEMBESAMAKI LUMUMBA


MPENDAE SUZA TUMEKUJA














KIDATO CHA TANO PEMBA MWAKA 2016




CCK CHASASA FIDEL CASTRO


MADUNGU SHAMIANI UWELENI


UTAANI

Share:

BODI YA MIKOPO YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KUPITIA MITANDAO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na mara mchakato utakapokamilika, wadau wote watatangaziwa.
Mwisho.
IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016
Share:

TANGAZO MAALUM KWA WANAFUNZI WA ST.JOSEPH WALIOKUWA WANACHUKUA DEGREE YA UALIMU 5 YEARS

Share:

BREAKING NEWS:TANGAZO KUTOKA BODI YA MIKOPO KUHUSU MAOMBI YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU 2016/2017

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 HESLB LOGO

Kutokana na kutapakaa kwa habari za uzushi mitandaoni bodi ya mikopo imesema kwamba;



"Hatujaanza Kupokea maombi ya mkopo kwa njia ya mtandao kwa mwaka 2016/2017. Tutaujulisha umma tukianza kupokea.
Tafadhali Subiri !"
source:heslb.go.tz
tafadhali endelea kutembela BLOG YETU YA MASWAYETU BLOG KWA MORE UPDATES 
Share:

magazeti ya leo jumanne june tarehe 7.6.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY



Share:

Mikopo ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Yafutwa......Waliokuwa chini ya Programu ya Miaka Mitano ya Ualimu Watakiwa Kurudi Diploma

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Kampasi ya Arusha (kilichofutiwa usajili), waliokuwa chini ya programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi, wametakiwa kusoma ngazi ya cheti au stashahada. 

Kama watataka kusoma ngazi ya juu, watapaswa kuomba upya udahili.

Aidha, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imesema wanafunzi waliokuwa wakipata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), mikopo yao pia imesimamishwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila alitoa agizo hilo jana kupitia taaarifa kwa vyombo vya habari. 

Profesa Msanjila alisema hatua hiyo, inatokana na kubainika kwamba wanafunzi hao hawastahili kusoma shahada na pia hawakustahili kupewa mkopo.

“Tunawafahamisha wanafunzi wa SJUIT waliokuwa kwenye programu ya miaka mitano kwamba watatakiwa kuishia daraja la cheti na stashahada... Kama wanafunzi hao watataka kuendelea na masomo ya juu, watatakiwa kuomba upya,” ilisema taarifa hiyo.

Februari 25, mwaka huu, Wizara kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) baada ya kujiridhisha kuwa Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Joseph Tanzania imepoteza sifa na vigezo vya kuendelea kutoa elimu ya chuo kikuu, ilifuta kibali cha kuanzishwa kwake.

Iliidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote, waliokuwa wanasoma katika Kampasi hiyo ya Arusha kwa gharama za Chuo Kikuu cha SJUIT. 

Aidha, ilifuta udahili wa wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi.

Ilielekeza wanafunzi waliokuwa wakiendelea na masomo katika programu hiyo, wahamishiwe katika Kampasi ya Luguruni, Dar es Salaam. 

TCU ilielekeza kwamba wanafunzi watalazimika kwanza kuhitimu katika ngazi ya Stashada, kama ilivyokuwa imeidhinishwa na Tume hapo awali. 

Wanafunzi waliohamishiwa kwenye vyuo mbalimbali, waendelee na masomo.

Taarifa hiyo ilisema wakati wa mchakato wa uhamisho, wanafunzi wote walihakikiwa kubaini kama wanakidhi vigezo vya kusoma kwenye ngazi hiyo. 

Wanafunzi wote waliokuwa wakisoma programu hiyo ya miaka mitano, walihamishiwa kwenye Kampasi ya Luguruni, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kutokana na mchakato wa uhakiki, baadhi ya wanafunzi walikutwa hawana sifa za kujiunga na mafunzo hayo ya ualimu. 

Wale waliobainika kuwa na sifa, walitaarifiwa kuendelea na masomo kwenye kampasi hiyo ya Luguruni.Wanafunzi katika kundi hili waliobainika kuwa na vigezo, walitaarifiwa kuendelea na masomo katika Kampasi ya Luguruni. 

"Maana ya kuwa na vigezo vya ufaulu tunavyovizungumzia hapa ni kwamba wanafunzi husika wamefaulu katika masomo lengwa yanayowawezesha kusoma Cheti cha Ualimu Daraja “A” ambacho ni kigezo cha kwanza kwa mujibu wa mtaala wa programu hiyo."
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger