Saturday, 4 June 2016
Friday, 3 June 2016
USHAURI MUHIMU KWA WANAFUNZI WA SPECIAL DIPLOMA WALIOFUKUZWA UDOM 2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Habari zenu,
Wiki iliyopita Serikali kupitia chuo kikuu cha udom,ilitangaza kwamba Wanafunzi wote wanaosoma diploma ya ualimu "special diploma" chuo kikuu cha Udom wanatakiwa warudi nyumbani kutokana na mgomo wa walimu wao kutokuwafundisha tangu tarehe 6.5.2016.
Kutokana na hali hiyo ni kwamba wanafunzi hao waliharibika kiakili na kisaikolojia,na hawajui nini cha kufanya,lakini siku ya jana Mkuu wa nchi JPM alitangaza kwamba,wanafunzi wamerudishwa nyumbani kutokana na kwamba hawana sifa za kujiunga chuoni hapo.
MASWAYETU BLOG tumeona si vyema mkabaki mkiwa nyumbani hamna cha kufanya ,tumeamua kuleta ushauri ambao utawasaidia watu wote walirudishwa nyumbani.
Kutokana na kauli ya JPM ni kwamba wanafunzi hawa hawatarudi chuoni hivyo wakatafute vyuo vya level yao.
nini ufanye?
Naamini una matokeo mazuri ambayo ulifaulu vizuri ya kidato cha nne ,div 1,2,au 3.
Fanya application za vyuo vya AFYA,KILIMO NA MIFUGO,UALIMU na kozi mbalimbali ktk vyuo vyetu vilivyopo hapa Tanzania.
DEADLINE YA KUFANYA APPLICATION NI TAR 3/6/2016,fanya upesi kufanya application NAKUHAKIKISHIA UTAPATA CHUO na UTASOMA.
HII ITAKUEPUSHA KUKAA NYUMBANI MWAKA MZIMA NA KUENDELEA KUPOTEZA MUDA.
CHUKUA HATUA SASA.

Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Sammata amteua Prof. Kusiluka kuwa makamu mkuu Mzumbe.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Hii ni kukufahamisha kwamba, Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Mh. Barnabas A. Sammata (Jaji Mkuu Mstaafu), kwa Mamlaka aliyokabidhiwa na sehemu ya Pili, Kifungu Na. 5(1) cha Hati Ridhia ya Chuo Kikuu Mzumbe, 2007 amemteua PROFESA LUGHANO J. KUSILUKA kuwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe kwa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia tarehe 3 Juni, 2016 badi tarehe 2 Juni, 2021.
Wanajumuiya wote mnaombwa kumpa ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kufikia misheni ya Chuo kikuu Mzumbe.
PROFESA LUGHANO J. KUSILUKA ATEULIWA KUWA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU MZUMBE
Hii ni kukufahamisha kwamba, Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Mh. Barnabas A. Sammata (Jaji Mkuu Mstaafu), kwa Mamlaka aliyokabidhiwa na sehemu ya Pili, Kifungu Na. 5(1) cha Hati Ridhia ya Chuo Kikuu Mzumbe, 2007 amemteua PROFESA LUGHANO J. KUSILUKA kuwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe kwa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia tarehe 3 Juni, 2016 badi tarehe 2 Juni, 2021.
Wanajumuiya wote mnaombwa kumpa ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kufikia misheni ya Chuo kikuu Mzumbe.
TCU imeanza kufanya uhakiki wa taarifa za wanafunzi Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU) itapitia taarifa za wanafunzi wa chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TECU) hasa vigezo vilivyotumika kudahiliwa chuoni. Wanafunzi wote wametakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya shule ya sekondari kwa vidato vya nne na sita na vyeti vya stashahada kabla ya Juni 04, 2016.
Kushindwa kufanya hivyo kutapelekea wanafunzi hao kuondolewa vyuoni.

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA IKULU,ISOME TAFADHALI
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake ya awamu ya tano itahakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanapatiwa mikopo, lakini haitakubali kulekeza mikopo hiyo kwa wanafunzi wasiokuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 02 Juni, 2016 wakati akizungumza na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chuo hicho inayojengwa katika kampasi ya Mlimani upande wa mashariki mwa chuo.
Akiwahutubia maelfu ya wanajumuiya hiyo wanaojumuisha wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi wa chuo, Dkt. Magufuli amesema serikali yake imedharia kutoa elimu bora kwa watanzania na imejipanga kuhakikisha inakabiliana na changamoto mbalimbali zinazovikabili vyuo, lakini ameelezea kusikitishwa kwake na uwepo wa wanafunzi waliodahiliwa na baadhi ya vyuo hapa nchini pasipo kuwa na sifa zinazomwezesha mwanafunzi kujiunga na chuo kikuu.
"Wapo wanaokopeshwa mikopo hii ya elimu ya juu lakini hawana sifa, Mheshimiwa Profesa Ndalichako (Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi) nakushukuru kwa hatua unazozichukua katika kusafisha wizara yako na hili nalisema kwa uwazi, na ukweli lazima usemwe hata kama ni mbele ya wanachuo.
"Una D,D unasajiliwa kuchukua digrii chuo kikuu na unapata mkopo wa serikali, ni aibu ya ajabu, haiwezekani, haiwezekani, haiwezekani. Lakini wakati tunawalipia wanafunzi 489 waliomaliza kidato cha nne na kupata D,D manaake wengine ni divisheni 4, kuchukua digrii, wapo wanafunzi wengine wa kidato cha sita wamekosa mikopo, wapo wanafunzi wengine walio na diploma wamekosa mikopo" Amesema Rais Magufuli.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia amewataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini kuacha kujihusisha na masuala ya siasa na badala yake wazingatie jukumu kuu lililowapeleka vyuoni ambalo ni kusoma, huku akibainisha kuwa serikali yake haitavumilia vitendo vya vurugu vyuoni.
"Ifike mahali watanzania tukubali ukweli, tuache siasa kwenye masuala ya msingi, ukimpeleka mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye ufaulu wa divisheni 4, anachukua digrii, akishatoka pale, hata kama atafanikiwa kupata digrii itakuwa ni ajabu.
"Lakini niwaombe wanafunzi mahali kote, msitumiwe na wanasiasa, mmekuja kusoma, someni, siasa mtazikuta mkiondoka, nawambia mmekuja kusoma someni, na ndio maana hata katika kutoa mikopo hatubagui, sijui huyu CCM, sijui huyu CHADEMA, sijui huyu nini, nyie wote ni watanzania, ndio lengo letu. Amesisitiza Dkt. Magufuli.
Amewaahidi kuwa serikali yake itahakikisha inatoa mahitaji ya wanafunzi ikiwemo mikopo na kuboresha miundombinu ya vyuo, lakini amewataka wanavyuo nao kuwa wavumilivu na wazalendo pale ambapo mahitaji hayo yatachelewa kutokana na mchakato wa kuyapata kuhitaji muda.
Kabla ya kuwahutubia wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mkuu wa chuo hicho ambaye ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemuomba Rais Magufuli asaidie kuboresha miundombinu ya chuo hicho ikiwemo ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ambao kwa takribani asilimia 70 wanaishi nje ya chuo, ambapo Rais Magufuli ameahidi kutoa shilingi bilioni 10 na ameuagiza uongozi wa chuo hicho kuainisha eneo ndani ya chuo ili ujenzi wa mabweni uanze mara moja.
Uzinduzi wa ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa umehudhuriwa na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing ambaye nchi yake ndio imetoa msaada wa dola za Marekani zaidi ya Milioni 41 kwa ajili ya ujenzi wa Maktaba hiyo.
Maktaba hiyo ya kisasa itakapokamilika itakuwa ndio maktaba bora kuliko zote barani Afrika, ikiwa na ukubwa wa eneo la meta za mraba 20,000 na itakuwa na uwezo wa kuwa na vitabu 800,000 na kuchukua wanafunzi 2,600 kwa mpigo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Wananchi Waanza Kuhama Wakiogopa Kuchinjwa Tanga
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ukatili uliofanywa na watu wasiojulikana wa kuwachinja watu wanane wa
kitongoji cha Kibatini mkoani Tanga, umesababisha wakazi wa kitongoji
hicho kuanza kuyahama makazi yao.
Watu hao walichinjwa usiku wa
Mei 31 nje ya nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho kwa madai kuwa
walisababisha “vijana” wao kukamatwa na polisi baada ya kutoa taarifa
zao wakati wakizurura kwenye eneo lao.
Waliouawa katika tukio
hilo ni mwenyekiti huyo, Issa Hussein, kaka yake, Mkola Hussein, Hamis
Issa, Issa Ramadhani na wengine wawili waliotambulika kwa jina moja la
Kadir, Mikidadi na Salum.
Jana baada ya mazishi ya watu hao,
mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbarouk alipeleka lori aina ya Mitsubishi
Fusso kwa ajili ya kuwahamisha wanakijiji hao.
Wakazi wayahama makazi
Diwani wa kata ya Mzizima, Fredrick Chiluba alisema wakazi wa Kibatini
wameamua kuhamia kitongoji cha Kona-Z kilichopo kijiji jirani Kiomoni.
Mwandishi alishuhudia wakazi takriban 60 wa Kibatini wakitoa vyombo, huku wengine
wakiezua mabati kwenye nyumba zao wakati wakisubiri gari ambalo baadaye
liliwasili na kuwachukua.
“Wameingiwa na hofu ya kibinadamu na
jambo hili lipo moyoni mwa mtu, hivyo huwezi kumng’ang’aniza kukaa hapo
wakati anahisi hayupo salama,” alisema Chiluba.
Hadija Hussein
alisema wameamua kuhama kwa sababu mara baada ya kukamilishwa kwa
shughuli za mazishi ya ndugu zao wanne, ilipofika saa 6:00 usiku, askari
waliokuwepo kwenye viwanja vya nyumba ya marehemu Mkola Hussein kulinda
usalama hawakuonekana.
“Tulipatwa
na wasiwasi mkubwa tulipoona askari na magari yao wameondoka, tukajua
sasa na sisi tunakuja kuchinjwa.Hatukupata usingizi kwa hofu, ndipo
asubuhi tukaamua kuondoa vyombo,” alisema.
Alisema mbunge alipokwenda kuwahani, walimuomba gari la kuhamisha vyombo vyao ili waondoke kabla jioni haijafika.
Mbunge
Mbarouk alisema alipowasili eneo hilo na kukuta hakuna ulinzi,
alimpigia simu mkuu wa polisi wa Wilaya ya Tanga ambaye alipeleka
askari.
“Nilipowauliza viongozi wa Jeshi la Polisi waliniambia
askari wapo wanafanya kazi ya kuzungukia maeneo, lakini haikuwa haki
kuwaondoa askari mara tu baada ya kufanyika mazishi,” alisema Mbarouk.
Mbunge
huyo alisema ameushauri uongozi wa polisi kupeleka ulinzi hata
wanakohamia kwa sababu wauaji lazima watapata taarifa ya waliko na
wanaweza kuwatendea chochote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Leonard Paulo alisema askari hawakuwa wameondoka kijijini hapo bali
walikuwa wamefanya mbinu za kufanya doria maeneo yanayozunguka kitongoji
hicho.
“Usiku huo kwenye kitongoji kulikuwa na kikosi maalumu
cha FFU ambacho mimi mwenyewe nilikuwa nakiongoza usiku kucha. Tulikuwa
tukifuatilia maficho ya wahalifu, kitaalamu tunaita undercover,”
alisema.
Kamanda huyo alisema wakati polisi ikiendelea na operesheni, si
vyema kuwatisha wananchi kwa kuwa tangu yalipofanyika mauaji hayo,
askari hawajaondoka.
RC: Mauaji ya Tanga si ugaidi
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Martine Shigela amesema mauaji yanayotokea katika mitaa ya jijini
Tanga na Amboni si vitendo vya kigaidi, bali yanatendwa na kundi la
watu wanaotaka kuvuruga amani.
Amesema hii ni vita ya kiuchumi
inahusiana na ujio wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanga na
kwamba Serikali itahakikisha inawakamata waliohusika.
Alisema
hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Serikali, Halmashauri ya
Wilaya ya Muheza pamoja na vyama vya siasa vya wa wilayani humo.
Shigela,
ambaye alikuwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza kupokea taarifa
ya maendeleo ya kabla ya kuanza ziara wilayani humo, alisema Serikali
haiwezi kukubali kuona kundi la watu wachache wanaharibu amani iliyopo.
Watoto Mkoani Iringa Wapigwa Marufuku Kutembea Saa 12 jioni na Kuendelea
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Aliwataka wananchi kupinga imani za kishirikina zinazowahamasisha kufanya ukatili kwa watoto kwa madai ya kutajirika
Serikali wilayani Iringa imetoa waraka unaozuia watoto wenye umri wa
kuanzia miaka 14 kushuka chini, kutotembea usiku kutokana na kukithiri
kwa vitendo vya ulawiti na ubakaji.
Wiki moja iliyopita wananchi
walimpiga hadi kumuua kijana aliyefahamika kwa jina moja la Emmanuel
(25-30), baada ya kukutwa akimbaka mtoto mwenye umri wa miaka kumi,
katika eneo la Mtwivila, Manispaa ya Iringa.
Pia, katika kipindi
cha miezi mitatu iliyopita matukio 36 ya ubakaji yameripotiwa kutokea
manispaa hiyo huku watuhumiwa 17, wakitiwa mbaroni.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alisema hali ni mbaya hivyo kila mzazi na mlezi anapaswa kumlinda mtoto wake.
Kasesela
alisema waraka huo unawataka wazazi na walezi kutowatuma watoto kuanzia
saa 12.00 jioni.
“Ni marufuku mtoto kutumwa kuanzia saa 12, wazazi na walezi wanatakiwa kuwalinda na kuwatunza watoto wao kwa kuwahakikishia usalama,” alisema.
“Ni marufuku mtoto kutumwa kuanzia saa 12, wazazi na walezi wanatakiwa kuwalinda na kuwatunza watoto wao kwa kuwahakikishia usalama,” alisema.
Waraka huo pia umezuia watoto kuzurura hovyo
mitaani kwa kuwa wabakaji wamekuwa wakitumia mbinu nyingi ikiwamo
kuwalaghai kwa pipi au kuwatuma.
“Ni marufuku watoto kuonekana baa au vilabu vya pombe za kienyeji, ikibainika wamiliki watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema.
“Ni marufuku watoto kuonekana baa au vilabu vya pombe za kienyeji, ikibainika wamiliki watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema.
Alisema matatizo ya ubakaji na
kuwalawiti watoto yamekuwa sugu na kwamba unahitaji ushirikiano baina ya
polisi, wananchi na viongozi kupambana nayo.
“Nimeagiza polisi kuongeza doria na watuhumiwa wanaokamatwa kwa ubakaji, sheria ichukue mkondo wake ili kukomesha hali hii,” alisema.
Aliwaomba
viongozi wa dini kusaidia kutoa elimu kwa waumini wao juu ya kuwalinda
watoto na kukemea ukatili huo ambao ni hatari ikiwa utaachwa kuendelea.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Lyata alisema imani za kishirikina
zimechangia ubakaji na ulawiti kwa watoto kukithiri.
Alisema
katika uchunguzi wao walibaini vikaratasi vilivyokuwa vikisambazwa
mitaani vikishauri wanaume wanaotaka kufanikiwa kimaisha, wabake na
kulawiti watoto wadogo kisha wajiunge na dini yao ya ‘freemason’.
“Mtaa
wa Semtema ndiyo ulikuwa tishio na huko tuliokota vikaratasi
vilivyokuwa vimeandikwa ukitaka kutajirika, jiunge na freemason pia
ubake au kulawiti mtoto chini ya miaka 14,” alisema.
Lyata alisema sababu nyingine ni ulevi wa kupindukia na utumiaji wa dawa za kulevya kama bangi.
Alisema
kukithiri kwa vitendo hivyo kumeifanya manispaa hiyo kutangaza jambo
hilo kuwa ni janga ambalo lazima wapambane nalo kwa kuwasaka wabakaji.
Naibu meya aliwataka polisi kudhibiti vitendo hivyo vinginevyo watoto wataendelea kuteseka.
Alisema
wapo watoto wanaofanyiwa ukatili huo majumbani na wengine mitaani.
Alisema wameanza kuwatambua watoto wa mitaani na kuwarudisha makwao ili
kuwanusuru kubakwa.
Watoto wasimulia
Baadhi ya watoto walisema wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo na vijana waliopo mtaani, hasa nyakati za jioni.
“Siku hiyo nilitumwa na mama dukani, wakati narudi kuna mtu akanipa hela nimnunulie mafuta ya taa nimpelekee kwake, nilipompelekea akanifanyia hivi,” alisema mtoto huyo.

Alisema mbakaji huyo
alimtishia endapo atasema angemfanyia tena ukatili huo bila huruma.
“Nilimpa mama mafuta, nikaenda kulala nikilia sana niliogopa kumwambia, bahati aligundua kwa sababu sikuwa naweza kutembea na aliponikagua akakuta nimeumizwa,” alisema.
“Nilimpa mama mafuta, nikaenda kulala nikilia sana niliogopa kumwambia, bahati aligundua kwa sababu sikuwa naweza kutembea na aliponikagua akakuta nimeumizwa,” alisema.
Mama wa mtoto huyo alisema mbali na kuumizwa mwanaye aliambukizwa magonjwa ya zinaa. Aliiomba Serikali kutowanyamazia wanaume wenye tabia ya kuwabaka watoto.
Mtoto
mwingine wa kiume alisema kijana asiyemjua alimpatia pipi akijifanya
rafiki yake, hali iliyomfanya waongozane hadi mlima wa Semtema, ambako
alimlawiti.
Wananchi walia
Kukithiri kwa vitendo hivyo kuliwafanya wananchi waandamane hadi kwa mkuu wa wilaya kuomba msaada. Wananchi hao walieleza kuwa kinachowatesa ni watuhumiwa kuachiwa huru na polisi na kurejea mtaani.

“Ndiyo maana tumeamua tutakayemkuta tunammaliza kwa sababu akienda polisi atarudi tu,” alisema Gerald Matibabu.
Wazazi hao walidai vitendo hivyo vimewachosha, na kwamba wapo watoto walioambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwamo Ukimwi.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Semtema wenye wakazi 3,800, Reminus Ndale alisema mpaka sasa
idadi ya watoto waliofanyiwa unyama huo kwenye mtaa wake ni wanne.
Alisema
kwa kushirikiana na wananchi wameamua kuhakikisha watoto wao wanalindwa
na kuwachukulia hatua kali watakaobainika kuwabaka.
Polisi
wazungumza
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, John Kauga alikiri kuwapo kwa vitendo vya ulawiti na ubakaji na kuwataka wananchi kutoa taarifa haraka vinapotokea.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, John Kauga alikiri kuwapo kwa vitendo vya ulawiti na ubakaji na kuwataka wananchi kutoa taarifa haraka vinapotokea.
“Kuna matukio mengi pia majumbani, wazazi wasifiche, watoe taarifa kwa polisi ili hatua kali za kisheria zichukuliwe,” alisema.
The Deadline to apply for Admission into Further and Higher Education for academic year 2016/2017 through NACTE is Today
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
- - Admission into Certificate/Diploma and Higher Diploma
- Administration, Business, Law, Planning, Social Work, Community Development, Tourism and related Programmes :- Deadline 03/06/2016
- Agriculture, Livestock, Engineering, ICT and other related Sciences :- Deadline 03/06/2016
- Health and Allied Sciences (Including Community Health, Health Records etc) :- Deadline 03/06/2016
- Teacher Education :- Deadline 03/06/2016
- - Admission into Bachelor Degree Programmes :- Deadline 03/06/2016
Thursday, 2 June 2016
Rich Mavoko - Ibaki Story (Official Video) | Download Mp4
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Rich Mavoko - Ibaki Story (Official Video) | Download Mp4
Rich Mavoko - Ibaki Story (Official Video) | Download Mp4
- See more at: http://www.johventuretz.com/2016/06/video-rich-mavoko-ibaki-story.html#sthash.fLnYXfSU.dpuf
Rich Mavoko - Ibaki Story (Official Video) | Download Mp4
BREAKING NEWS:CHUO KIKUU NIT WAGOMA ,KISA BOOM WANAFUNZI WAANGUKA HOVYO,NJAA IMETAWALA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Nit kimenuka,wanafunzi wanaandamana kudai hela zao za quarter 3 na 4, pia ubovu wa ratiba ya mwaka wa masomo ya chuoni.
TAARIFA KAMILI INAKUJA
TAARIFA KAMILI INAKUJA