Thursday, 2 June 2016

Kimenuka!! JWTZ Yajitosa Mauaji Ya Watu 8 Tanga,Mkuu wa Majeshi Atangaza Msako usiku na Mchana

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

SERIKALI imetuma kikosi maalumu cha ulinzi, kikiongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuwasaka watu wanaodaiwa kuwa majambazi ambao wanaendesha mauaji ya kinyama mkoani Tanga.


Uamuzi huo umechukuliwa baada ya watu wanane kuuawa kinyama kwa kuchinjwa juzi usiku katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Manispaa ya Tanga.


Habari za uhakika ambazo tulizipata jana, zinasema tayari vikosi hivyo vimeanza operesheni kali katika mapango ya Amboni ambayo yanadaiwa kuwa maficho ya watu hao.


Akitoa salamu za rambirambi wakati wa mazishi ya marehemu wanne kati ya wanane waliozikwa Kibatini jana, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema vyombo vya dola vitahakikisha watu wote waliohusika katika mauaji hayo wanatiwa mbaroni.


“Ndugu zangu nawapeni pole kutokana na kuondokewa na wapendwa wetu… naomba kuwahakikisha sisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola tutahakikisha tunawatia nguvuni watu wote waliohusika na mauaji haya,” alisema Jenerali Mwamunyange.


Alisema tukio la mauaji hayo ni la kusikitisha mno kutokana na Tanzania kusifika kuwa nchi ya amani duniani.


“Tanzania inasifika kuwa na amani duniani kote, lazima hatua za kiusalama zichukuliwe haraka ili kunusuru amani yetu isichezewe.


“Ni tukio la ajabu ambalo limegusa watu wengi wasio na hatia, tutasaidiana na wenzetu kuhakikisha wahalifu hawa wanapatikana,” alisema Jenerali Mwamunyange.


Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Masauni Hamad Masauni, alisema Serikali inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo ili kuwakamata wahusika ndani ya kipindi kifupi.


Aliwahakikisha wananchi kuwa ulinzi unaimarishwa na kwamba matukio hayo hayatajirudia tena.


“Vyombo vya ulinzi vitafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha tunawatia nguvuni haraka watu waliohusika na mauaji hayo,” alisema Masauni.


Aliwaomba ndugu na jamaa ambao wamefiwa na ndugu zao kuwa na subira wakati Serikali inaendelea kuchukua hatua.


Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu alisema wataendelea kuimarisha ulinzi na usalama maeneo yote.


Katika hatua nyingine, wakazi wa mitaa mitatu ya Mleni Kati, Mleni Mashariki na Kibatini katika Kata ya Mzizima, Manispaa ya Tanga, wameanza kukimbia makazi yao kwa kuhofia usalama wao baada ya mauaji hayo.


Mauaji hayo yalitokea juzi usiku ambapo watu wanaoaminika kuwa majambazi walivamia nyumba tatu katika eneo hilo, wakiwa wamelala usiku, kisha kuwateka na kuwapeleka msituni kabla ya kuwachinja.


Wakazi hao wanaounda zaidi ya kaya 30, walisema wameamua kuyakimbia makazi yao kwa kutokuwa na imani ya usalama wao katika eneo hilo, baada ya wale wanaoitwa majamabzi kuvamia makazi yao kwa mara ya pili kwa staili ya kutisha.


Kabla ya tukio hilo la juzi, watu wasiofahamika walivamia makazi yao na kuchinja kuku 40, mbuzi wanne na ng’ombe mmoja na kukimbilia mapango ya Amboni na hawajawahi kukamatwa.


Mwandishi wetu jana alishuhudia wanawake na watoto wakiwa na mizigo mithili ya wakimbizi wakiondoka katika eneo hilo huku wanaume wakibaki kwa ajili ya kuzika ndugu, jamaa na marafiki zao waliouawa katika tukio hilo.


Mmoja wa wananchi hao, Juma Issa, alisema wamelazimika kuwahamisha wanawake na watoto kwa kuhofia wanaweza kuvamiwa tena kwa mara ya pili.


Nae Lucas Muhina alisema kuwa anashindwa kuhama katika eneo hilo kutokana na kuwa na mifugo, hivyo anashindwa kujua mahali salama pa kuihifadhi.


Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibatini, Shabani Mwamini, alithibitisha baadhi ya wananchi wa mitaa mitatu kuhama katika eneo hilo.


“Nyumba nyingi zimebaki na wanaume pekee yake kwani wanawake na watoto wote wamehama kwa sasa,” alisema.


Wakati huohuo, maiti nne kati ya nane zimezikwa jana huku nyingine nne zikisafirishwa nje ya mkoa huo.


Mwamini aliwataja waliozikwa kuwa ni Issa Husein, Mkola Husein, Issa Hamis na Salim Adam.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella alisema kuwa vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.


Simulizi ya Mauaji
Mtoto wa marehemu Mkola Hussein anayeitwa Salimu Mkola (16) alisababisha vilio na simanzi kwa waombolezaji baada ya kusimulia namna watu hao walivyomchukua baba yake na kwenda kumchinja mbele ya nyumba yake.


Akisimulia tukio hilo huku akibubujikwa machozi, mtoto huyo alisema watu hao walifika nyumbani kwao wakagonga mlango saa sita usiku na kumuamrisha baba yao atoke na fedha.


“Nilipoona hivyo nilijaribu kupiga kelele kuomba msaada kwa majirani, lakini mmoja wa wauaji aliingia ndani na kunitoa nje ya nyumba yetu, huku akiniuliza wakati wale vijana saba
wanachukuliwa na polisi mimi nilikuwa wapi.


“Waliendelea kuniuliza kama nina habari ninayoijua, huku wakiwa wameshika mapanga na bunduki, ndipo waliponiambia wapo kwa ajili ya kutetea dini yetu.

“Baadaye waliniruhusu niingie ndani na kulala, lakini niliendelea kusikia vishindo vya kipigo na watu wakikoroma ambayo ilikuwa ni ishara ya kuwa baba yangu alikuwa anakata roho pamoja na watu wengine,” alisema.

Mtoto mkubwa wa marehemu, Abuu Mkola, alisema vijana saba ambao sasa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi awali walionekana katika Kitongoji cha Kibatini wakiwa wanakimbia kusikojulikana.


Alisema baada ya hali hiyo baba yake ambaye ni marehemu, Mkola Hussein akishirikiana na wananchi wa mtaa huo walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambao walikuja na kuwakamata vijana hao lakini mmoja wao alifanikiwa kukimbia.

Abuu alisema kuwa katika tukio la juzi, wauaji hao wakati wanamchukua baba yake walisema wanawahitaji vijana wao saba waliokamatwa na polisi, lakini aliposema hajui ndipo walimuunganisha na watu wengine kwa ajili ya kumchinja.


Bunge Lataka Taarifa
Ofisi ya Bunge imeiagiza Serikali kutoa taarifa rasmi kuhusu mauaji yanayoendelea nchini ili kuwatoa hofu wananchi waliopo katika maeneo mbalimbali.


Akitoa maagizo hayo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alisema Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni anapaswa kuzungumza na Kamati za Ulinzi na Usalama katika maeneo yote ambayo yametokea mauaji ili aweze kutoa taarifa ndani ya Bunge.


“Waziri atuletee taarifa kwa sababu Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) yupo hapa na waziri anayehusika na mambo ya Bunge yupo, naomba watuletee taarifa kwa sababu mauaji yamekuwa yakitokea mara nyingi na tumekuwa tukiwasihi Serikali ituletee taarifa na si mtakuwa mnazitafuta,” alisema Dk. Tulia.


Baada ya maelezo hayo Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) alisimama na kuomba mwongozo chini ya kanuni 68 (7).


“Mheshimiwa Naibu Spika pamoja na haya uliyoyatolea maelezo juu ya mauaji yanayotokea katika nchi yetu, nimelazimika kuomba mwongozo huu kwa sababu matukio yaliyoanza kujitokeza katika maeneo mbalimbali na maeneo mengine mambo haya tuliwahi kuyauliza Serikali na kuahidi watayatolea ufafanuzi.


“Sasa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani amekwenda kuangalia na atazungumzia jambo hilo wakati mambo haya wabunge tulishaiomba Serikali itoe ufafanuzi ni jinsi gani inajipanga kukabiliana nayo,” alisema Lugola.


Alisema kitendo cha Serikali kusema Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amekwenda kushughulikia jambo hilo wakati huo huo mambo ambayo yametokea Mwanza na maeneo mengine yalishaombewa ufafanuzi lakini hakuna majibu si kizuri.



Share:

MPYA:RAIS MAGUFULI ATOA HATMA YA WANAFUNZI 7000 WA SPECIAL DIPLOMA UDOM WALIORUDISHWA NYUMBANI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Amezungumzia  wanafunzi walioenda chuo kikuu cha Dodoma waliofukuzwa ambao hawakuwa na vigezo vya kujiunga chuo na kushangazwa wanasiasa wanaowatetea.
 

Ameongezea kusema wanafunzi walioondoka wamefukuzwa na hata wanafunzi wote wangefukuzwa kama wangegoma. \

VIDEO

Share:

New AUDIO | Abdu Kiba - BAYOYO | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DOWNLOAD
https://mkito.com/song/11812?referrer=154e1d3df2f4565bce82116a79366f13618ab1ec
Share:

Video | Stan Bakora - Natafuta Kiki ya Raymond A.K.A Rayvanny | Watch/Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

https://youtu.be/8TlbVJ1qHvU
Share:

VIDEO::HOTUBA YA RAIS MAGUFULI CHUO KIKUU CHA UDSM HII HAPA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
IVE UPDATES UDSM




Yanayojiri ziara ya Magufuli chuo kikuu Dar es Salaam

Wanafungua mkutano kwa kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania na na wimbo wa Taifa wa China
Wengine waliohudhuria ni ya ni waziri wa elimu Joyce Ndalichako, rais msataafu Jakaya Kikwete, balozi wa china nchini Tanzania, makamo wa rais mstaafu Gharibu Bilali, waziri mkuu mstaafu Joseph Warioba na mkuu wa wilaya ya Kinondon Ally Hapi.


Hotuba ya makamu mkuu wa chuo Rwekaza Mukandara
Anamuelezea rais changamoto zinazoikabili chuo ikiwemo miundombinu bora ya kufundishia mabweni ya wanafunzi ambayo ni machache na yamechakaa ndio changamoto kuu.
Ametaja changamoto nyingine ni kusomesha wanafunzi wa Uzamivu na uhaba wa wakufunzi kwenye mafunzo ya kiufundi kuboresha maslahi ya wafanyakazi na wanafunzi.

Ameongezea mradi wa maktaba kwamba ukikamilika utakidhi mahitaji ya sasa kutokana na wanafunzi kuwa wengi ambayo ni maktaba kubwa zaidi ukanda wa afrika mashariki na kati na kuishukuru serikali ya China kwa ufadhili wao.

Mwakilishi wa kampuni ya ujenzi wa China amelezea maktaba hiyo itakavyokuwa na uwezo mkubwa na teknolojia ya juu.

Hotuba ya Balozi wa China Tanzania
Balozi wa China nchini Tanzania , amezungumzia historia ya ushirikiano kati ya China na Tanzania kukikisifia chuo hicho kwa kutoa viongozi mashuhuri Afrika pamoja na kutoa wataalamu wa fani mbalimbali.
Amesifia uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya China na Tanzania na misaada mbalimbali ambayo China imeipa Tanzania na itakayozidi kuisaidia Tanzania.

Ameongezea maktaba hiyo itagharimu dola milioni 40 na ni maktaba kubwa zaidi kujengwa na China barani Afrika.

Hotuba ya waziri wa elimu Joyce Ndalichako
Amesema mradi huu umekuja kwa wakati muafaka kwa kua kipaumbele kikubwa cha serikali ya awamu ya 5 ni elimu na wizara ya elimu itafuatiia mradi hu kwa makini kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Hotuba ya Mwenyekiti wa chuo Jakaya Kikwete.
Rais aliyepita Jakaya Kikwete amezungumzia miundombinu ya chuo kama barabara na miundombinu ya chuo inavyohitaji kurekebishwa, maabara zilivyo na teknolojia ya zamani na ambazo hazitoshi.
Amesema ili akamilishe kazi yake vizuri kama mwenyekiti wa chuo ni vizuri rais Mghufuli akashughulikia changamoto hizo.

Hotuba ya rais Magufuli
Rais amemshukuru Kikwete kwa kuleta mradi huo na kuwashukuru China kwa misaada yao isiyo na masimango na masharti tangia enzi za uhuru na mpaka sasa hivi.

Amezungumzia ongezeko la wanafunzi wanaopata mikopo na changamoto ya wanafunzi 'hewa' wanaopata mikopo na kumtaka waziri wa elimu aendelee kupambana na tatizo hilo.
Amezungumzia pia wanafunzi walioenda chuo kikuu cha Dodoma waliofukuzwa ambao hawakuwa na vigezo vya kujiunga chuo na kushangazwa wanasiasa wanaowatetea.

Ameongezea kusema wanafunzi walioondoka wamefukuzwa na hata wanafunzi wote wangefukuzwa kama wangegoma.
Ameongezea kuwa chuo kikuu cha Dar es Salaam ndio alichosoma atakuwa anakisaidia na atatoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kujenga majengo na chuo watenge eneo kwa ajili ya ujenzi huo.
Pia ameomba hifadhi za jamii kusaidia kujenga ujenzi wa majengo ya chuo badala ya kujenga majengo sehemu nyingine ambazo hakuna watu wa kuyatumia.

Amesema pia changamoto zilizotajwa na makamo mkuu wa chuo na mwenyekiti atazibeba na kuzifanyia kazi.
Amemshukuru Makamo mkuu wa chuo kwa ulezi mzuri wa chuo na kuwaasa wanafunzi wasikubali kutumiwa na wanaiasa.

Ameongezea mikopo ilichelewa kutolewa kwa kuwa walikuwa wanahakiki majina ya wapokeaji wa mikopo yao na hata UDOM bado hawajapata lakini hawajagoma.
Amemsifu profesa Mgaya kwa kusimamia ukweli na akasema japokuwa ametolewa kwenye bodi ya TCU atampa kazi nyingine.
Amemaliza kwa kuishukuru nchi ya China kwa ushirikiano wao na kuahidi kuendeleza uhusiano kati ya Tanzania na China




==========

Juni 02, 2016

UONGOZI wa chuo kikuu cha Dar es salaam umetangaza kufuta ratiba zote za masomo chuoni hapo katika siku ya leo ambapo Rais Magufuli anatarajiwa kufika chuoni hapo kwa lengo la kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa maktaba ya kisasa.

Sambamba na hilo pia ratiba ya ziara hiyo ya rais Magufuli imebadilishwa sasa na baada ya kumaliza uwekaji wa jiwe la msingi katika maenwo ya Yombo ataelekea katika uwanja wa mpira wa Chuo hicho ili kuweza kuwahutubia wanafunzi hao na taifa kiujumla.

[​IMG]

Taarifa za chinichini toka chuoni hapo zinasema kuwa huenda rais Magufuli akapokelewa na mabango yenye jumbe mbalimbali kutoka kwa wanafunzi hao huku suala la uhaba wa mabweni chuoni kufikia hata wanafunzi 10 kulala chumba kimoja kilichotengenezwa kwaajili ya wnafunzi wanne tu kulala.

Aidha, suala la kurudishwa nyumbani kwa wanafunzi wa UDOM, kusitishwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya bunge pamoja na kuchelewa kwa fedha za mikopo ya wanafunzi na kupelekea migomo yakitarajiwa kujitokeza katika mabango.
Share:

NECTA: ADVERTISEMENT OF TENDER

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

Serikali Yazidiwa Mzigo wa Vijana Wanaotakiwa Kujiunga JKT,Waziri Asema ni Vigumu Kuwachukua Vijana Wote Kutokana na Uhaba wa Fedha

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

VIJANA wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa mujibu wa sheria wamekuwa wengi kiasi cha kuifanya Serikali kushindwa kuwachukua wote, Bunge limeelezwa.

Hivyo, kutokana na sababu hiyo, Serikali imeamua kuongeza idadi ya kambi za mafunzo ili wachukuliwe wote. Hayo yalisemwa bungeni jana mjini hapa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Munira Mustafa Khatib (CCM) aliyetaka kufahamu ni kwa nini Serikali isianzishe mpango maalumu wa kuwapeleka JKT vijana wanaomaliza kidato cha nne.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwinyi alisema, “Uwezo wa JKT kwa sasa kuchukua vijana wa kujitolea ni kati ya vijana 5,000 hadi 7,000 kwa mwaka kutokana na bajeti inayotolewa. 
Alisema, utaratibu wa sasa wa vijana kujiunga na JKT ni ule wa kujitolea kwa vijana wenye elimu ya kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu na ule wa mujibu wa sheria unaowahusu waliomaliza kidato cha sita.

“Kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kama anavyoshauri mbunge hautowezekana kutokana na uwezo mdogo kifedha,” alisema. 
Hata hivyo, alisema ushauri huo ni mzuri na serikali itafanya maandalizi ya kambi nyingi zaidi na kutenga bajeti kubwa zaidi kwa ajili ya uendeshaji kwa kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.
Share:

Dr. Shein Aahidi Kutumbua Majipu ndani ya CCM

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wanaCCM kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha chama na kuahidi kuyatumbua majipu hadi katika chama.

Dk Shein alisema kwa upande wa serikali kazi ya kuunda serikali inaendelea na kuwataka watendaji walioteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali kufanya kazi kwa maslahi ya taifa na wananchi wake.

Alisema mtendaji atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake katika sehemu za kazi ni bora akajiondoa kabisa hata kabla ya kusubiri kuondolewa. 
Kwa upande wa CCM, aliwataka watendaji kusimamia majukumu yao bila ya kusubiri kusimamiwa kwa ajili ya kuimarisha chama, kwani kazi hiyo ni ya kujitolea na waliopewa dhamana hizo wanatakiwa kulifahamu hilo na kujituma kwa kujenga chama imara.

“Wapo watendaji katika chama hawatekelezi na kusimamia majukumu yao vizuri na kama ndiyo majipu yenyewe basi tutayaondoa,” alisema.
Share:

Jambazi auawa Mwanza akirushiana risasi na polisi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
POLISI mkoani Mwanza imemuua jambazi baada ya mtu huyo akiwa na wenzake wawili kurushiana risasi na polisi waliokuwa doria baada ya kushindwa kutii amri ya kusimama walipotakiwa kufanya hivyo na polisi.

Akizungumza ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema mauaji hayo yalitokea Mei 31, mwaka huu saa 4.10 usiku katika Mtaa wa Ilemela katikati ya barabara inayopita kati ya eneo zilipo ofisini za Radio Free Afrika (RFA) na Kiwanda cha Samaki cha Mwanza.

Alisema polisi waliokuwa doria katika eneo hilo waliwatilia mashaka watu watatu waliokutana nao usiku huo wakiwa wamebeba sanduku na walipoamriwa kusimama, hawakutii.
“Hawakutii, badala yake watu wale waliongeza mwendo, huku mmoja wao akitoa mfuko uliokuwa na kitu, kumbe ilikuwa ni bunduki na kuanza kurushiana risasi na polisi,” alieleza Kamanda Msangi.

Alisema mtu huyo alifyatua risasi kati ya tatu hadi nne kwa polisi, lakini hazikuleta madhara kwa walinzi hao wa usalama wa raia waliomuua kujibu mapigo kwa kumpiga risasi na kumuua papo hapo huku wenzake wawili wakikimbia na kuelekea kusikojulikana.

Alisema baada ya tukio hilo, polisi walimkuta jambazi huyo akiwa na silaha aina ya SMG iliyochakaa na namba zake zikiwa zimefutika ikiwa na magazini yenye risasi 16. Alisema upelelezi kwa ajili ya tukio hilo unaendelea.

Kamanda Msangi alisema silaha iliyokamatwa hutumika kwenye majeshi na kuwa mwananchi wa kawaida haruhusiwi kutumia silaha ya aina hiyo. 
“Tutapeleka silaha hii kwa wataalamu kwa ajili ya kuitambua maana bunduki ya aina hii hatuna kwenye majeshi yetu,” alisema na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya utambuzi.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 2

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Wednesday, 1 June 2016

Audio | Jay Moe - Pesa Madafu | Mp3 Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Audio | Jay Moe - Pesa Madafu | Mp3 Download

Share:

Walioandaa mgomo UDSM kukiona

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Wanafunzi walioandaa mgomo wa jana Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu kwa kosa la kukikuka sheria ndogo ya Chuo kwa kuandaa mkusanyiko pasipo kibali cha Menejimenti.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo taaluma Florens Luoga amesema kuwa hadi  sasa mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinendelea na uchunguzi kubaini nani alihusika na ni kwa namna gani na baada ya hapo hatua za kinidhmu zitafuata.
“Taratibu na sheria ndogo za chuo haziruhusua mtu kuandaa mkusanyiko ambao haujaidhinishwa na menejimenti na kimsingi taratibu hizo lazima ziheshimiwe ili kuzifanya kuendelea kuwa imara hivyo tunasubiri ripoti ya walio husika endapo itaonesha  kuwa wanamakosa basi watachukuliwa hatua za kinmidhamu,” amesema Luoga.
Share:

TCU:Mgogoro baina ya Uongozi na wanafunzi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Francis (SFUCHAS), Ifakara

Share:

WIZARA YA ELIMU:SHINDANO LA PICHA LA AFRIKA "MY AFRICA PHOTOGRAPH COMPETITION

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
SHINDANO LA PICHA LA AFRIKA "MY AFRICA PHOTOGRAPH COMPETITION" icon SHINDANO LA PICHA LA AFRIKA (280.36 kB)
Share:

TANZIA:MWANAFUNZI WA SUA NDG.NYAVA RICHARD J AFARIKI DUNIA (R I P BROTHER)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Image result for suanet

Kwa masikitiko makubwa MASWAYETU BLOG TEAM imepokea msiba kutoka serikali ya wanafunzi SUA kwamba mwanafunzi wa mwaka wa pili jina tajwa hapo juu kozi ya HUMAN NUTRITION amefariki dunia leo asubuhi tar 1.6.2016.

MASWAYETU BLOG inatoa pole kwa familia na jumuiya nzima ya wanafunzi.

Bwana alitwaa jina lake lihidimiwe.
Share:

NAFASI ZA KAZI CHUO KIKUU UDOM JUNE 2016

Share:

Magufuli: Serikali Itakomesha Watumishi na Wanafunzi Hewa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


RAIS John Magufuli (pichani) amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kumaliza makosa yote yaliyojitokeza huko nyuma ikiwemo tatizo la watumishi na wanafunzi hewa lililoibuka hivi karibuni.

Amewataka Watanzania kuacha kuingiza siasa kwenye makosa yanapojitokeza, hasa yale yanayogusa sehemu nyeti kama elimu, kwani yakiachwa kuna uwezekano wa kutengeneza taifa la watu wa ajabu.

Alisema tangu aingie madarakani amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwemo matatizo ya rushwa, ukwepaji kodi, watumishi hewa na sasa amekumbana na tatizo la wanafunzi hewa.

“Nchi yetu ina changamoto na mambo mengi sana hata mimi nimekumbana na changamoto naziona mwenyewe, nikigeuka hivi watumishi hewa ambao hadi sasa wamefikia 10,500, nikigeuka hivi kuna wanafunzi hewa,” alisisitiza.

Alisema ni Tanzania pekee ambayo mtu anaweza kupata daraja la nne kidato cha nne katika elimu ya sekondari, halafu akapata fursa ya kujiunga na chuo kikuu na kupatiwa mkopo wa serikali, wakati mhitimu aliyefaulu kidato cha sita akikosa fursa hiyo.

Alisema endapo kulifanyika makosa lazima yarekebishwe, kwani inafahamika fika mtu akimaliza kidato cha nne akifeli ataanzia ngazi ya Astashahada, Stashahada ndio apate nafasi ya kujiunga chuo kikuu.

“Sasa hapa kwetu ni tofauti ukifeli kidato cha nne unajiunga chuo kikuu,” alihoji na kuwataka watu waache siasa kwenye makosa kwani mambo kama hayo yakiachwa kuna hatari ya nchi kutengeneza taifa la ajabu.

Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako aliivunja Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na kuwasimamisha kazi viongozi wanne waandamizi kwa tuhuma za kudahili wanafunzi wasio na sifa.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya TCU, Awadh Mawenya naye alisimamishwa kazi kwa kosa la kushindwa kuwachukulia hatua watumishi waliodahili wanafunzi hao wasio na sifa. 
Profesa Ndalichako alichukua hatua hizo baada ya TCU kudahili wanafunzi 489 waliopata daraja la 4.32 katika mitihani yao ya kidato cha nne lakini walijiunga na chuo kikuu na kupatiwa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 784.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger