Thursday, 19 May 2016

Waliombaka na Kumlawiti Binti wa Miaka 21 Morogoro Wapandishwa Kizimbani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
WATU sita wanaodaiwa kumbaka na kumlawiti msichana kisha kumrekodi na kusambaza video hiyo, leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na Iddi Adamu Mabena (32) Mkazi wa Njombe na Zuberi Thabiti (30) Mkazi wa Mbalali, Mbeya ambapo kesi hiyo inasimamiwa na waendesha mashtaka watatu wa serikali- Grolia Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Kalistus Kapinga.

Akisoma maelezo ya kosa katika shtaka la kwanza la kubaka na kulawiti, Wakili Rwakibalila aliwataja wahusika kuwa ni pamoja na Iddi Adamu na Zuberi Thabiti.

Mwendesha mashataka huyo amedai kuwa, washtakiwa hao kwa pamoja huku wakijua kufanya hivyo ni kosa, walimbaka na kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 21 na kumsababishia maumivu makali.

Wakili huyo alidai kuwa, washtakiwa hao walimbaka na kumuingilia kinyume na maumbile msichana huyo tarehe 27 Aprili, saa 1 usiku katika  nyumba  ya  kulala  wageni ya Titii iliyopo  katika Tarafa  ya  Dakawa  Wilaya  ya  Mvomero.

Hata hivyo, mawakili wote wa serikali walipinga dhamana ya washtakiwa hao kwa madai kuwa, kesi hiyo imegusa hisia za watu wengi hivyo kwa usalama wao pia kuhofia kuharibu ushahidi ni bora waendelee kushikiliwa.

Mbele ya Marry Moyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi washtakiwa hao walikana kuhusika na mashtaka hayo ambapo wamerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Juni Mosi mwaka huu na kwamba, upelelezi haujakamilika.

Katika shtaka la pili washtakiwa hao wakiwa na wenzao wanne walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo wakikabiliwa na shtaka la kusambaza picha chafu za ngono katika mtandao wa kijamii wa whatsapp.
 

Edgar Bantulaki, mwendesha mashataka amedai kuwa, washtakiwa hao wamefanya kosa hilo chini ya kifungu cha sheria namba14 (1) (b) na 2 (b) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Bantulaki amewataja washtakiwa wengine kuwa ni pamoja na mshtakiwa namba 1 na 2 na Rajabu Salehe, (30), Ramadhani Ally (26), Muhsin Ng’ahy (36), John Peter (24) wote wakiwa ni wakazi wa Wami, Dakawa wilayani Mvomero.
 

Mwendesha mashtaka huyo amedai kuwa, washtakiwa wote kwa pamoja walianza kusambaza picha hizo kati tarehe 28 hadi 30 Aprili mwaka huu wilayani Mvomero na mkoa mzima wa Morogoro kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp.
 

Hata hivyo Ignas Kunge, wakili wa mshtakiwa wa nne (Ally) aliiomba mahakama kumpa dhamana mshtakiwa wake jambo lililopingwa na mawakili wa serikali kwasababu suala hilo limegusa jamii zaidi pia kwasababu za kutoingilia na kuharibu upelelezi wa kesi hiyo.
 

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Ivan Msaki, washtakiwa hao walikana kuhusika na shtaka hilo ambapo wamerejeshwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Juni Mosi mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa kwa kujadiliwa suala la dhamana iliyopingwa kwa kiapo na mawakili wa serikali.

Urlich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amesema, washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani kati ya 11 waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na tuhuma hizo kufuatia upelelezi kutokamilika dhidi yao.

Kamanda Matei amesema, katika hatua za awali upelelezi kipolisi ulikamilika kwa watuhumiwa sita wa mwanzo ambao ndio wamefikishwa mahakamani.

Aidha amesema kuwa, vitendo vilivyofanywa na watuhumiwa ni vibaya na ambavyo kamwe haviwezi kuvumiiwa na jamii katika nchi.
 

Hivyo ametoa rai kwa wananchi kuacha kufanya uhalifu kwa kutumia mitandao kwani sheria yake iliyopitishwa na bunge hivi karibuni haitamwacha mtu akiwa salama.
 

Hata hivyo kamanda huyo ameomba polisi wapewe kifaa kama cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili waweze kufanya kazi zao kwa uhuru na kukamilisha mwenendo wa kesi mapema.

Amesema, kwa sasa uhalifu kwa njia ya mitandao unakuwa kwa kasi duniani kote na kwamba, mtu anaweza kutenda makosa mengi yanayosumbua jamii ikiwemo wizi mkubwa na mdogo wa fedha kwenye benki, makosa ya udhalilishaji, lugha za matusi na mengine mengi.


Amesema kuwa, kupatikana na kifaa hicho kutasaidia ushahidi kuwa madhubuti na sio rahisi kumwondoa mtu katika hatia.


Pia amewataka wananchi wote hususan vijana kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao badala ya kutumia muda mwingi katika mitandao
  ya kijamii
Safari ya kuelekea kizimbani ikiwa imeiva.

Zuberi Thabit mtuhumiwa wa ubakaji.
Idd Adamu mtuhumiwa wa kurekodi video za ubakaji.
Share:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MAY TAREHE 19.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Wednesday, 18 May 2016

New AUDIO | Papaa Masai Ft. Yamoto Band - Mtoto Wa Kariakoo | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/yxspo2ucot8g/Papaa_Masai_Ft_Yamoto_Band_-_Mtoto_Wa_Kariakoo.mp3?d=1
Share:

DOWNLOAD NA SOMA HAPA HOTUBA ZA BAJETI WIZARA ZOTE 2016/2017

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

 Image result for SERIKALI




Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ministry of Health and Social Welfare
moh.go.tz/
Wizara ya Ardhi Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Developments Capt. John Z. Chiligati ardhi.go.tz
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Ministry of Education and Vocational Training Hon. Prof. Jumanne A. Maghembe moe.go.tz
Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia Ministry of Higher Education, Science and Technology
*
Wizara ya Fedha na Uchumi Ministry of Finance and Economic Affairs Mhe. Saada Mkuya mof.go.tz
Wizara ya Habari, Utamudini na Michezo Ministry of Information, Culture and Sports
hum.go.tz
Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Ministry of Labour, Employment and Youth Development
*
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Ministry of Agriculture, Food and Cooperatives Mhe. Stephen Masato Wasira (Mb.) kilimo.go.tz
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ministry of Community Development, Gender and Children
mcdgc.go.tz
Wizara ya Maji na Umwagiliaji Ministry of Water and Irrigation Prof. Mark Mwandosya (MP) maji.go.tz
Wizara ya Maliasili na Utalii Ministry of Natural Resources and Tourism
mnrt.go.tz
Wizara ya Mambo ya Ndani Ministry of Home Affairs Hon. Lawrence K. Masha (MP) moha.go.tz
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation Hon. Bernard Kamilius Membe (MP) mfaic.go.tz
Wizara ya Mawasailiano, Sayansi na Teknolojia Ministry of Communication, Science and Technology
*
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Ministry of Livestock Development and Fisheries
*
Wizara ya Miundombinu Ministry of Infrastructure Development Hon. Dr. Shukuru Kawambwa infrastructure.go.tz
Wizara ya Nishati na Madini Ministry of Energy and Minerals Dk. William Ngeleja *
Wizara ya Sheria na Katiba Ministry of Justice and Constitutional Affairs
[1]
Wizara ya Ulinzi na Usalama wa Taifa Ministry of Defence and National Service
*
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Ministry of East African Cooperation Hon.Dr. Diodorus B. Kamala (MP) meac.go.tz
Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko
Share:

Hii ndio siri ya wimbo ‘Yote Maisha’ ya Madee

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 Kajala
“Kuna siku moja nilikuwa nachat naye [Kajala] halafu ngoma inapigwa kwenye TV fulani, nikamwambia angalia TV akakutana na hiyo nyimbo, nikamwambia hiyo nyimbo inakuhusu sana akasema ‘najua,” Madee alisema kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Mimi niliambiwa nifanye na Majani kwahiyo hisia hizo unazoziskia ni hisia za P-Funk.”
www.youtube.com/watch?v=7CBIwv8XgqE
Majani na Kajala wamewahi kuwa na uhusiano maarufu na wa muda muda mrefu uliowabariki mtoto wa kike, Paula. Huyo alikuwa mtoto wa pili wa producer huyo wa Bongo Records na wa kwanza kwa Kajala.
Hivi karibuni Madee aliachia video ya wimbo wake ‘Migulu Pande’ ambamo amemtumia Kajala.
Share:

MPYA:WANAFUNZI WANAOMALIZA VYUO VIKUU KUPATIWA MIKOPO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Image result for serikali
Kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wa vyuo vikuu kila mwaka ambao wamekuwa wakiongezeka mtaani huku kukiwa na tatizo la ukosefu wa ajira.
Tatizo hili sasa limepatiwa ufumbuzi ambapo waziri mwenye dhamana na vijana na ajira amesema leo akiwa bungeni kwamba sasa vijana wanaomaliza elimu ya chuo kikuu wanakopeshwa pesa ambayo itawawezesha kujiajiri wenyewe.
sifa za kupata mkopo amesema kwamba vijana wanatakiwa kujiunga pamoja na kutengeneza group ambalo wataandika proposal na kuipeleka wizarani,wizara itakaa na kupitia hatimae kutoa mkopo kwa vijana hao.
 
Share:

Bavicha Walaani Hotuba ya Godbless Lema Kuzuiwa Bungeni,Wataka Waziri Kitwanga Ajiuzulu na Akigoma Awajibishwe

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Wakati uchunguzi wa kampuni ya Lugumi inayodaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye vituo vya polisi ukiendelea, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga kujiuzulu wadhifa wake kupisha uchunguzi huo.

Limesema haiwezekani waziri anayetajwa kuhusika katika sakata hilo kuendelea na kazi huku Jeshi la Polisi linalodaiwa kutapeliwa na kampuni hiyo likiwa chini ya wizara yake.

Hata hivyo, waziri huyo amewajibu vijana hao wa upinzani kwa kusema hawezi kubishana na watoto na hayo waliyoyatoa ni mawazo yao binafsi wana haki ya kuyasema.

“Nimeshasema mara nyingi, siwezi kuzungumza tena kuhusu haya mambo. Wao kama wamesema waache waseme,” alisema.

Baraza hilo lililoibuka na hoja tatu jana, limesema kama waziri huyo atagoma kujiuzulu kupisha uchunguzi unaofanywa na kamati ndogo ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Rais John Magufuli anapaswa kumwajibisha ingawa suala hilo ni gumu kutokana na uswahiba uliopo kati ya kiongozi huyo mkuu wa nchi na Kitwanga.

Kampuni ya Lugumi ilibainika kutotimiza matakwa ya mkataba wake baada ya kufunga mashine 14 tu kati ya 108 zilizotakiwa kufungwa, licha ya kulipwa zaidi ya asilimia 90 ya fedha kwa mujibu wa mkataba ambazo ni Sh37 bilioni.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14 ndiyo iliyofichua udhaifu huo na baadaye Bunge kuanza uchunguzi baada ya kutoridhishwa na maelezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani na polisi kuhusu mkataba huo.

Kitwanga anahusishwa na Lugumi kupitia kampuni ya Infosys anayodaiwa kuwa ni mmoja wa wanahisa. Infosys ambayo imekanusha kuhusika katika sakata hilo, imedaiwa kuwa iliisaidia kampuni ya Lugumi kupata vifaa kutoka kampuni ya Dell ya Marekani ili viweze kufungwa kwenye vituo vya polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita alisema: “Hotuba ya upinzani inaeleza kuwa Lugumi inamilikiwa na Kitwanga na ana ubia hilo siyo siri. Kilichoelezwa kama kingesomwa bungeni kingemfanya apoteze uhalali wa kuwa waziri na tunajua Magufuli hawezi kumfanya chochote maana ni maswahiba.

“Hotuba ile pia ilimtaja Rais ila cha ajabu upinzani wakaambiwa wafute maneno ‘rais’. Rais Magufuli ameshindwa kuitumbua Lugumi na kwa kilichotokea bungeni suala hilo haliguswi.”

Alisema Rais anapaswa kujibu hoja zilizotolewa na wapinzani kuhusu Lugumi na kubainisha kuwa kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza kampuni hiyo haiwezi kutenda haki wakati Kitwanga akiendelea kuwa waziri.

Katibu mwenezi wa baraza hilo, Edward Sembeye alisema: “Katika ripoti ya CAG ameeleza juu ya ununuzi wa ile feri kuwa ni mbovu na haifanyi kazi hivi hili siyo jipu?

Kuhusu suala la Jaji Mkuu, Mwita alisema kitendo cha kuisifia Sheria ya Mtandao alipokuwa London, Uingereza hivi karibuni si kizuri kwa maelezo kuwa kazi ya majaji ni kutafsiri misingi ya kikatiba: “Tunamtaka afute kauli hii na aseme sheria hiyo imetungwa itumike lakini uzuri na ubaya wake hapaswi kuusema maana ni kama anatoa hukumu kabla watuhumiwa hawajafikishwa mahakamani.”
Share:

Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili,Wenzao Wabaki Vinywa Wazi Kikaoni

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni.

"Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....

"Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.

“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.

Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Magufuli alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana. Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho

Rais Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.

Utendaji wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisadi.
Share:

Mganga Wa Zahanati Aiwa Mbaroni Akidaiwa Kugoma Kumhudumia Mama Mjamzito

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Polisi mkoani Mara inamshikilia mganga wa zahanati katika Kijiji cha Rwamchanga wilayani Serengeti kwa madai ya kushindwa kumhudumia mjamzito aliyejifungua pacha na kusababisha kifo cha mtoto mmoja.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema tukio hilo lilitokea Mei 15.


“Tunamshikilia kwa makosa matatu, likiwamo la uzembe, kufanya makusudi na kushindwa kuwajibika sawa na kiapo cha kazi yake, tunaendelea na mahojiano yatakapokamilika atafikishwa mahakamani,” alisema Ng’anzi.


Akisimulia chanzo cha mwanae kupoteza maisha, Shida Mugesi akiwa katika Hospitali ya Nyerere alisema alifika zahanati saa 12 asubuhi na kumuomba mganga amuhudumie, lakini alikataa.


“Nilikaa kwa muda wa saa mbili bila kupatiwa huduma, ghafla nilihisi uchungu wa kusukuma mtoto tukamuita mganga wa zamu ili anisaidie aligoma na kudai nimsubiri anakwenda kuoga na wakati huo alikuwa anazungumza kwa simu bila kuonyesha ushirikiano. Nilianza kujifungua mwenyewe,” alisema.


Muuguzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema walipopima uzito wa watoto kwa mjamzito huyo walibaini kuwa aliyefariki alikuwa na kilo 2.5 na mwingine 2.3.


Muuguzi wa zahanati hiyo, Frida Kasonga alisema aliposikia taarifa ya kuwapo kwa mgonjwa huyo alilazimika kurudi kituoni kumsaidia lakini alikuta mtoto mmoja ameshafariki dunia.


“Haikuwa zamu yangu ila nililazimika kurudi baada ya kusikia mganga aliyekuwa zamu kagoma kuwasaidia,” alisema Frida.


Ofisa mtendaji kata, Fadhila Nyamburapi na Mwenyekiti wa kitogoji cha Kazi, Samwel Nyakande walilaani kitendo hicho na kutaka sheria ichukue mkondo wake.
Share:

Jinsi ya kujikinga na magonjwa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

brunette sitting down and stretching her legs on white backgroundKuna njia nyingi ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hasa yale ya kuambukiza au kuambukizwa.
Moja ya ugonjwa hatari duniani na ambao huua watu wengi ni malaria.
Ugonjwa huu huenezwa na mbu. Ili kujikinga na ugonjwa huu watu  wanashauriwa wawe wakihakikisha wanaharibu maeneo ambapo mbu huzaliana.
Wanashauri wa kufunika matangi ya maji na beseni za kufulia nguo. Kuharibu vyombo vyote vya kutekea maji ambavyo havina mifuniko.
Watu wanaelekezwa na wasiache maji katika vyombo vya kuwekea maua kwani mbu wanaweza kutaga mayai katika maji ya madimbwi hayo na kuzaliana kisha mbu hao kung’ata watu na kuugua malaria.
Epuka kuwa nje wakati wadudu wengi wanapoanza kutokea, vyandarua na vitumike.
Epuka kuwa karibu na mifugo mara nyingi kwani unaweza kuambukizwa ugonjwa iwapo utaumwa na wadudu waliowauma mifugo hao.
Washiriki wote wa familia wanapaswa kutumia vyandarua hasa vilivyotiwa dawa ya kuwafukuza wadudu, weka nyavu madirishani na uzitengeneze zinapoharibika,  ziba nyufa zilizo pembeni mwa paa la nyumba ambapo wadudu wanaweza kuingia.
Njia hizo za kujikinga zinagharimu kiasi fulani cha fedha, lakini unaweza kupoteza fedha nyingi sana ikiwa utalazimika kumpeleka mtoto hospitalini au mtu anayetegemewa katika familia pale anapougua.
Wazuie wadudu wasijifiche mahali popote nyumbani mwako. Piga lipu ukutani na kwenye dari na uzibe nyufa na mashimo. Ikiwa nyumba imeezekwa kwa nyasi funika dari kwa kitambaa cha kuwazuia wadudu.
Ondoa vitu vilivyorundikana kama vile karatasi, nguo au picha nyingi zilizowekwa ukutani, kwani huko ndiko wadudu hujificha.
Usiwakaribishe kamwe panya na wadudu, tumia dawa za kuwafukuza na za kuwaua, lakini usisahau kufuata maagizo yaliyoonyeshwa.
Tumia mitego ya inzi na vifaa vya kuwaua, uwe mbunifu; mwanamke mmoja alitumia kitambaa kutengeneza mifuko, kisha akajaza mchanga katika mfuko huo na akauweka chini ya mlango ili kuwazuia wadudu wasiingie ndani ya nyumba.

Kuna njia nyingi ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hasa yale ya kuambukiza au kuambukizwa.
Moja ya ugonjwa hatari duniani na ambao huua watu wengi ni malaria.
Ugonjwa huu huenezwa na mbu. Ili kujikinga na ugonjwa huu watu  wanashauriwa wawe wakihakikisha wanaharibu maeneo ambapo mbu huzaliana.
Wanashauri wa kufunika matangi ya maji na beseni za kufulia nguo. Kuharibu vyombo vyote vya kutekea maji ambavyo havina mifuniko.
Watu wanaelekezwa na wasiache maji katika vyombo vya kuwekea maua kwani mbu wanaweza kutaga mayai katika maji ya madimbwi hayo na kuzaliana kisha mbu hao kung’ata watu na kuugua malaria.
Epuka kuwa nje wakati wadudu wengi wanapoanza kutokea, vyandarua na vitumike.
Epuka kuwa karibu na mifugo mara nyingi kwani unaweza kuambukizwa ugonjwa iwapo utaumwa na wadudu waliowauma mifugo hao.
Washiriki wote wa familia wanapaswa kutumia vyandarua hasa vilivyotiwa dawa ya kuwafukuza wadudu, weka nyavu madirishani na uzitengeneze zinapoharibika,  ziba nyufa zilizo pembeni mwa paa la nyumba ambapo wadudu wanaweza kuingia.
Njia hizo za kujikinga zinagharimu kiasi fulani cha fedha, lakini unaweza kupoteza fedha nyingi sana ikiwa utalazimika kumpeleka mtoto hospitalini au mtu anayetegemewa katika familia pale anapougua.
Wazuie wadudu wasijifiche mahali popote nyumbani mwako. Piga lipu ukutani na kwenye dari na uzibe nyufa na mashimo. Ikiwa nyumba imeezekwa kwa nyasi funika dari kwa kitambaa cha kuwazuia wadudu.
Ondoa vitu vilivyorundikana kama vile karatasi, nguo au picha nyingi zilizowekwa ukutani, kwani huko ndiko wadudu hujificha.
Usiwakaribishe kamwe panya na wadudu, tumia dawa za kuwafukuza na za kuwaua, lakini usisahau kufuata maagizo yaliyoonyeshwa.
Tumia mitego ya inzi na vifaa vya kuwaua, uwe mbunifu; mwanamke mmoja alitumia kitambaa kutengeneza mifuko, kisha akajaza mchanga katika mfuko huo na akauweka chini ya mlango ili kuwazuia wadudu wasiingie ndani ya nyumba.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger