Wednesday, 18 May 2016

Polisi Akamatwa na Noti Bandia Zenye Thamani ya Sh. 870,000

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

ASKARI Polisi Ezekiel Dinoso (32) mkazi wa tarafa ya Mgeta, wilayani Mvomero mkoani Morogoro amekutwa na noti bandia za Sh 10,000 zenye thamani ya Sh 870,000, akijiandaa kuzitumbukiza katika akaunti ya mtandao wa Tigo Pesa katika duka mojawapo eneo la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema jana kuwa tukio hilo ni la Mei 14, mwaka huu saa 1:00 usiku katika eneo la Mawezi , Manispaa ya Morogoro.

Mtuhumiwa alikutwa katika duka la Hadija Hamis (35) mkazi wa Chamwino, wakati alipohitaji kuwekewa fedha hizo, mwenye duka alimtilia shaka hivyo kuarifu Polisi. 
Mtuhumiwa alipokamatwa na askari baada ya kutolewa taarifa Kituo cha Polisi, alikutwa akiwa na noti bandia 87 za Sh 10,000.

Alitaja namba za noti hizo ni BX 7287490 zikiwa noti 22 , BX 728792 zikiwa noti 20, BX 728791 noti 19 na BX7287487 zikiwa noti 15 na kufanya jumla ya thamani ya Sh 870,000 ambazo ni bandia.

Kamanda Matei alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Rashidi Shabani (30) na Michael Lukasa (39), wote wakazi wa Ngerengere wanashikiliwa na Polisi kwa kuwakuta na nyama ya nyati kilo 300 na silaha aina ya gobole iliyotumika kumuulia mnyama huyo.

Kamanda wa Polisi wa Morogoro, Matei, alisema walikamatwa Mei 14, mwaka huu saa 2:00 usiku katika kijiji cha Kinonko, kata ya Gwata, wilaya ya Morogoro. 
Matei alisema, kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jitihada zinazofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kukomesha vitendo vya uhalifu.
Share:

Mtoto wa Chacha Wangwe Abadili Msimamo Mahakamani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii, kuwa Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake.

Mtoto huyo, Bob Chacha Wangwe (24), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alibadili msimamo jana aliposomewa shtaka hilo kwa mara ya pili, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wangwe alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 11, na alisomewa shtaka linalomkabili na alikiri kutenda kosa hilo.

Mshtakiwa anapokiri kosa, kwa kawaida Mahakama inaweza kumtia hatiani na kumpa adhabu kwa mujibu wa sheria, kulingana na kosa siku hiyo hiyo au siku nyingine yoyote.

Baada ya kusomewa shtaka na kukiri, Hakimu Mkazi Mkuu, Waria lwande Lema, aliamuru mshtakiwa huyo apelekwe rumande hadi jana, Mei 17, kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo hakuwapo.

Hata hivyo, jana mshtakiwa huyo alipopandishwa kizimbani na kusomewa shtaka hilo, ili kusomewa maelezo ya awali kabla ya Mahakama kumtia hatiani na kumhukumu, tofauti na siku ya kwanza, alikana kutenda kosa hilo.

Kutoka na mshtakiwa huyo kukana kosa, Wakili wa Serikali, Salim Msemo, aliieleza Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika, hivyo aliiomba ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala aliiomba Mahakama impe dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili linadhaminika, maombi ambayo yalikubaliwa na aliachiwa kwa dhamana na kesi iliahirishwa hadi Juni 15.

Wangwe ambaye baba yake kwa sasa ni marehemu, anadaiwa Machi 15, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Share:

Samia:Sijawahi Kupinga Utumbuaji Majipu, Lakini Nilishauri Wakuu wa Mikoa Wazingatie Sheria Kabla ya Kumfukuza Mtu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma wanapotaka kuwafukuza watumishi wasio waadilifu.

Alisema hajapinga kauli ya Rais John Magufuli ya kutumbua majipu kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, hivi karibuni kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.

Samia aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, wakati akisisitiza zoezi la kuhamisha mifugo iliyopo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Alisema wakuu wa mikoa na wilaya nchini, wanapaswa kuhakikisha wanapotaka kuwawajibisha watumishi wa umma wanafuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Aliongeza kuwa mwenye mamlaka ya kutumbua majipu ni Rais pekee, kwa sababu anateua, anaajiri na kufukuza kwa hiyo viongozi wengine wakiwamo wakuu wa mikoa na wa wilaya wafuate taratibu.

“Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuteua, kutengua na kuajiri lakini sijapinga utumbuaji majipu, bali nasisitiza kila mkuu wa mkoa na DC (mkuu wa wilaya) afuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma,” alisema Samia.

Makamu wa Rais, aliwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha mifugo ya nje ya nchi iliyopo hifadhini inaondolewa ifikapo Juni 30.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela alishukuru Tanapa kwa kuwapa msaada madawati ili kupunguza kero ya wanafunzi kukaa chini.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera alisisitiza kuwa atahakikisha mkoa wake unapunguza migogoro ya ardhi ili hifadhi za Taifa ziweze kulindwa, huku wananchi wakiheshimu na kulinda mipaka ya hifadhi na rasilimali za Taifa.
Share:

Mganga mbaroni akidaiwa kugoma kumhudumia mjamzito

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Polisi mkoani Mara inamshikilia mganga wa zahanati katika Kijiji cha Rwamchanga wilayani Serengeti kwa madai ya kushindwa kumhudumia mjamzito aliyejifungua pacha na kusababisha kifo cha mtoto mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema tukio hilo lilitokea Mei 15.

“Tunamshikilia kwa makosa matatu, likiwamo la uzembe, kufanya makusudi na kushindwa kuwajibika sawa na kiapo cha kazi yake, tunaendelea na mahojiano yatakapokamilika atafikishwa mahakamani,” alisema Ng’anzi.

Akisimulia chanzo cha mwanae kupoteza maisha, Shida Mugesi akiwa katika Hospitali ya Nyerere alisema alifika zahanati saa 12 asubuhi na kumuomba mganga amuhudumie, lakini alikataa.

“Nilikaa kwa muda wa saa mbili bila kupatiwa huduma, ghafla nilihisi uchungu wa kusukuma mtoto tukamuita mganga wa zamu ili anisaidie aligoma na kudai nimsubiri anakwenda kuoga na wakati huo alikuwa anazungumza kwa simu bila kuonyesha ushirikiano. Nilianza kujifungua mwenyewe,” alisema.

Muuguzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema walipopima uzito wa watoto kwa mjamzito huyo walibaini kuwa aliyefariki alikuwa na kilo 2.5 na mwingine 2.3.

Muuguzi wa zahanati hiyo, Frida Kasonga alisema aliposikia taarifa ya kuwapo kwa mgonjwa huyo alilazimika kurudi kituoni kumsaidia lakini alikuta mtoto mmoja ameshafariki dunia.

“Haikuwa zamu yangu ila nililazimika kurudi baada ya kusikia mganga aliyekuwa zamu kagoma kuwasaidia,” alisema Frida.

Ofisa mtendaji kata, Fadhila Nyamburapi na Mwenyekiti wa kitogoji cha Kazi, Samwel Nyakande walilaani kitendo hicho na kutaka sheria ichukue mkondo wake.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAY TAREHE 18.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Tuesday, 17 May 2016

BREAKING NEWS:Shule ya Sekondari Ilala girls islamic school yateketea kwa moto mda huu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

 
Shule ipo maeneo ya ilala bungoni pamoja na msikiti wa TAQWA watoto wako salama ila shule imetetkea takribani yote. 
Fire bado hawajafika kufika.
Share:

Hii hapa orodha ya majina ya Maofisa , Wakaguzi na Askari walioteuliwa kufanya Mtihani ya Local Saat 2016.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Jeshi La Polisi Tanzania

Kitengo cha mahusiano ya kimataifa (IR) makao makuu ya Polisi kimetoa orodha ya majina ya Maofisa , Wakaguzi na Askari walioteuliwa kufanya Mtihani ya Local Saat 2016.



Bofya hapa : Orodha ya majina waliochaguliwa kufanya mtihani wa local saat 2016
Share:

VIDEO MPYA:GIGY MONEY-MAJOJORIJO | DOWNLOAD AND WATCH

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
Share:

Sababu 5 kwanini wanawake wenye akili nyingi hupata tabu ya kupata mapenzi ya kweli

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Akili nyingi ni zawadi na laana. Wanapojiangalia kwenye kioo, wanawake wenye akili nyingi huona picha ya mtu mwenye nguvu mwenye malengo, anayejua anachotaka. Kuwa na akili nyingi ni kitu muhimu kuwa nacho, lakini wakati mwingine kinaweza kuwatisha wengine. Fotolia_92936031_Subscription_Monthly_XL
Pengine ndio maana watu wenye akili nyingi hupata shida ya kupata pendo. Kama unajiuliza kwanini bado upo single, hizi ni sababu tano kwanini unaweza ukawa unapata shida kupendwa.

1. Unakuwa mchambuzi mno

Wasichana wenye akili mara nyingi huchambua sana vitu. Huwa na shaka na kesho yao, njia nzuri za kuimarisha mahaba, na wanataka sana kumpata mtu sahihi. Hiki hata hivyo sio kitu kibaya.

2. Unajua ni bora kuwa peke yako kuliko kuwa na mwenza asiye sahihi

Na hakuna tatizo katika hilo pia. Watu wenye akili wako makini katika kumpata mwenza sahihi ambapo wanaweza kuamua kubaki wenyewe kama asipopatikana.

3. Unajua kuwa mahusiano mara nyingi hufa

Hawa hujua ukweli unaouma kuwa mahusiano mengi hayafiki popote. Matokeo yake, wakati mwingine hufanya mambo pole pole na kuwa na shida katika kuingia miguu miwili. Lakini mwenza sahihi ataelewa hilo.

4. Unaweza kuwa unaogopesha

Sio kwamba watu wenye akili huwatisha mambumbu lakini hata wenye akili pia. Wanaweza wasiwe comfortable na ukweli kuwa unafanya vizuri katika eneo la maisha ambayo hawapo.
5. Unajua kujilinda mwenyewe

Watu wenye akili katika dunia hii wanaelewa sana hatari katika hali yoyote na hiyo inahusisha pia dating. Huwa makini, waangalifu na huweka vikwazo kujilinda wenyewe.
Share:

CALL FOR APPLICATIONS INTO VARIOUS PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2016/2017

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Application Image
A. Graduate Programmes
1. Doctor of philosophy in Education 3 years (Weekend Progamme);September Intake with Specialization in the following areas:-
  1. Curriculum Studies
  2. Educational Administration and Planning
  3. Educational Assessment and Evaluation
Entry requirements:
  • A Masters degree with background in Education from a recognized University/Institution of Higher Learning with average of grade B or above (or upper second class).
  • Must have taken at least three (3) courses in one of the three areas of specialization (Curriculum Studies, Educational Administration and Planning or Educational Assessment and Evaluation).
  • Applicants with lower second class at Master’s level must have a work experience of at least 5 years.
  • Applicants must submit a concept paper of area of research interest in 2 to 3 pages.
2. Master of Education 2 years; (Regular, Evening) September Intake with specialization the following areas:
  1. Curriculum Studies and Instruction
  2. Educational Assessment and Evaluation
  3. Educational Planning and Administration
  4. Professional Practice in Secondary Education
  5. Professional Practice in Higher Education
Entry requirements:
  • Holders of at least a first or an upper second degree or equivalent in non- classified degrees.
  • Holders of lower second class Degree with a minimum of three years of working experience.
  • Holders of postgraduate Diploma in Education or related fields.
3. Master of Business Administration 2 years; (Evening Programme) March and September with specialization in the following areas:
  1. Master of Business Administration in Finance
  2. Master of Business Administration in Accounting
  3. Master of Business Administration in Marketing
  4. Master of Business Administration in Human Resource Management
Entry requirements:
  • Holders of at least first or an upper second degree or equivalent in non- classified degrees.
  • Holders of lower second class or pass degree with a minimum of two and three years of work experience respectively.
  • Holders of postgraduate diploma in business studies or related fields.
  • Applicants with professional qualifications such as (CPA, ACCA, and CSP) plus a year or more of work experience, provided they completed form Six.
4. Post Graduate Diploma in Education (1 year course work and 10 weeks teaching practice)
Entry requirements:
  • Applicant must be a holder of a Bachelors Degree or above, outside of the field of education, from any recognized university, with two teaching subjects at secondary level or other special consideration.
B. Undergraduate Programmes (3 Years)
  1. Bachelor of Education in Science; (Physics, Chemistry, Biology, Mathematics and Computer Science).
  2. Bachelor of Education in Arts; (History, Geography, Kiswahili, English Economics, and Accounting)
  3. Bachelor of Arts in Geography and Environmental Studies
  4. Bachelor of Arts in Sociology and Social Work;
  5. Bachelor of Science in Mathematics and Statistics;
  6. Bachelor of Business Administration and Management;
  7. Bachelor of Philosophy with Ethics.
  8. Bachelor of Science in Computer Science
Entry requirements:
  • Two Principal passes at A’ Level one of which must be relevant to course requirement OR
  • Relevant Diploma from a recognized institution with       a Second Class or a B average
C. Diploma Programmes (2 Years) March 2016 and September
  1. Diploma in Accounting and Finance
  2. Diploma in Business Administration
  3. Diploma in Laws
  4. Diploma in Library, Records and Archives Management
  5. Diploma in Marketing Management
  6. Diploma in Human Resource Management
  7. Diploma in Logistic and Procurement Management
  8. Diploma in Entrepreneurship and Microfinance
  9. Diploma in Computer Science
  10. Diploma in Computer Application and Business Management
  11. Diploma in Information Technology
  12. Diploma in Laboratory Technology
  13. Diploma in Journalism and Media Studies
  14. Diploma of business information technology
  15. Diploma in Social Work
  16. Diploma of Project Planning and Management
Entry requirements:
  • Applicants must hold at least four ‘O’ level D passes in 4 approved subjects which are relevant to course. And
  • Form six certificate holder with one pass or two subsidiaries or
  • Certificate of a related programme with an average of B from a recognized institution.


D. Certificate Programmes; (1Year); March 2016 and September
  1. Certificate in Accounting and Finance
    1. Certificate in Business Administration
    2. Certificate in Laws
    3. Certificate in Library Records and Archives Management
    4. Certificate in Marketing Management
    5. Certificate in Human Resource Management
    6. Certificate in Logistic and Procurement Management
    7. Certificate in Entrepreneurship and Microfinance
    8. Certificate in Computer Science
    9. Certificate in Computer Application and Business Management
    10. Certificate in Information Technology
    11. Certificate in Laboratory Technology
    12. Certificate in Journalism and Media Studies
    13. Certificate of Business Information Technology
    14. Certificate in Social Work
    15. Certificate of Project Planning and Management
    16. Certificate of Cultural Heritage Management
Entry requirement:
  • Applicants must hold at least four ‘O’ level D passes in 4 approved subjects which are relevant to course.
Application Procedures
  • For PhD, Masters, Postgraduate Diploma apply direct to the University by downloading application forms available to MWECAU website;
  • For Undergraduate studies apply through TCU website under Central Admission System CAS
  • For Certificate and Diploma, apply through NACTE Central Admission System
NB:
For inguires call: 0755 154215 au 0758 889984 au 0653 254215 for assistance
Share:

New AUDIO | Mayunga Ft. Akon - Please Dont Go Away | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/feh0fm5tq7eo/Mayunga_Ft._Akon_-_Please_Dont_Go_Away.mp3?d=1
Share:

TAMISEMI YAJIBU SWALI LA MBUNGE WA MASWA KUHUSU MAKAO MAKUU KUPELEKWA BARIADI BADALA YA MASWA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo asubuhi,mbunge wa MASWA MASHARIKI ameuliza swali kwa Tamisemi kwamba je,haioni kwamba maamuzi ya kupeleka makao makuu ya mkoa wa simiyu bariadi haioni kwamba yalifanywa kwa hujuma na kusababisha gharama kubwa kwa serikali ambapo hakukuwa na nyumba za serikali za watumishi na ofisi za kiserikali ukilinganisha na maswa?

Je haioni kwamba aliekuwa mkuu wa moa wa SHINYANGA BALELE alipeleka mkoa bariadi kutona an yeye kuwa anatoka bariadi?

MAJIBU YA TAMISEMI
Mh jaffo kasema kwamba swala la kupeleka mkoa simiyu lilifanywa maamuzi yake na kamati ya ushauri ya mkoa kutoka kwa wananchi wenyewe,hata hivyo pingamizi lililetwa tamisemi na kuonekana kwmba halina mashiko,hivyo mkoa kupelekwa bariadi.
Share:

Serikali Kuajiri Askari Wapya 3700,Askari 7000 na Wakaguzi 1300 Watapandishwa Vyeo

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Serikali  inatarajia kumwaga ajira kwa askari  katika mwaka ujao wa fedha.Taarifa juu ya ajira hizo, zilitolewa jana bungeni  na  waziri  mwenye dhamana.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato ya Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/17 kuhusu ajira za askari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema wataajiriwa askari wapya 3,700 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Waziri Kitwanga alisema mbali ya kuajiri askari hao, pia watawapandisha vyeo askari 7,140, wakaguzi 1,325 na maofisa 991.

Alisema katika mwaka 2015/16, jumla ya askari polisi wapya 3,882 waliajiriwa, na askari wakaguzi na maofisa 4,065 wa vyeo mbalimbali walipandishwa vyeo kwa kufuata utaratibu wa ajira.

“Aidha, serikali imeendelea kuhuisha viwango vya mishahara na posho mbalimbali, ikiwemo posho ya chakula ambayo iliongezwa kutoka Sh 180,000 hadi kufikia Sh 300,000 kwa mwezi,” alieleza Waziri Kitwanga.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha, Jeshi la Polisi litaongeza umakini katika kusimamia nidhamu kwa askari wake kwa kufanya uchambuzi wa kina (vetting) kwa kuchukua vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanaoomba kujiunga na Jeshi la Polisi ili kuwa na askari wenye nidhamu na moyo wa dhati wa kulitumikia Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Jeshi la Magereza, alisema linatarajia kutoa mafunzo kwa maofisa na askari 4,975 katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na yale ya Taaluma ya Urekebishaji.

Alisema ili kukabiliana na changamoto ya uchache wa miundombinu ya makazi kwa askari Polisi, serikali kupitia mkopo kutoka Serikali ya China inakusudia kujenga nyumba 4,136 chini ya usimamizi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi.

Akizungumzia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, alisema jeshi hilo linahitaji vituo 152 Tanzania Bara, lakini kwa sasa lina vituo 57 na kati ya hivyo, 38 vipo katika miji na 19 katika viwanja vya ndege. 
Alisema huo ni upungufu wa vituo 95 hali inayosababisha maeneo mengi kukosa huduma za zimamoto na uokoaji.

Inategemea kujenga kituo kimoja cha zimamoto na uokoaji katika eneo la Kigamboni katika Jiji la Dar es Salaam na kuendelea na ujenzi wa Jengo la Makao Makuu Tazara - Mchicha, Dar es Salaam.

Aidha, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kupambana na makosa yanayovuka mipaka hususani ugaidi, uharamia, biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu, wizi wa vyombo vya moto hususani magari, wizi wa kutumia mitandao ya Tehama, bidhaa bandia, na biashara haramu ya silaha na uchafuzi wa mazingira.
Share:

Bodaboda Wagongana Jijini Mwanza, mmoja afariki

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mwendesha pikipiki ambaye hajafahamika amefariki dunia baada kugongana uso kwa uso na mwenzake, eneo la Mabatini jijini Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema bodaboda mwingine Stanley Maimu (24), alijeruhiwa katika tukio hilo lililotokea Mei 15.

Msangi alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi wa wahusika, hivyo bodaboda wote walishindwa kumudu pikipiki zao na kugongana uso kwa uso.

Katika tukio jingine, Polisi inawashikilia watu wawili; Chacha Mwita (34) na Rashid Mohamed (34) wakazi wa Kata ya Kitangiri wilayani Ilemela kwa kosa la kukutwa na misokoto sita ya bangi kinyume na sheria.

Kamanda msangi alisema Mei 14 saa 14.00 mchana, polisi waliokuwa doria walifanikiwa kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwapo kwa watu hao wanaojihusisha na biashara hiyo haramu ya kuuza dawa za kulevya.

Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wanapobaini vitendo vya uhalifu.
Share:

Mtu Mwingine Auawa Kwa Kukatwa Mapanga Usiku Sengerema Mkoani Mwanza

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Wakati upelelezi wa tukio la watu saba wa familia moja kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ukiendelea, mauaji mengine ya aina hiyo yametokea wilayani Sengerema.

Safari hii, mkazi wa Kijiji cha Bilulumo, Kata ya Kafunzo, James Mgambo (71) aliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Kafunzo, Dotto Bulunda, mke wa Mgambo aliyetajwa kwa jjina la Nyangalo Masisa (65) alijeruhiwa katika tukio hilo na amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Sengerema.

“Chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na polisi wamefika kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Bulunda. 
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bilulumo, Said Makelemo alisema mapanga mawili yanayoaminika kutumika yalikutwa eneo la tukio.

Mmoja wa majirani wa familia hiyo, Lameck Kasabulilo alisema hawakusikia kelele za kuomba msaada.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Hakimu Elisha, mazishi ya Mgambo yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya ukoo yaliyopo kijijni hapo.

Mgaga Mkuu wa Hospitali Teule Wilaya ya Sengerema, Dk Mary Jose alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti, huku hali ya majeruhi ikiendelea vizuri.

Mkuu wa Wilaya Sengerema, Zainab Telack alisema tayari uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo umeanza na kuapa wahusika watasakwa na kutiwa mbaroni.
Share:

Watu 11 Wakamatwa Mkoani Morogoro Kwa Tuhuma za Kumbaka Mwanamke Gesti na Kusambaza Video ya Kujamiiana Mtandaoni

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Watuhumiwa wawili Zuberi Thabiti (30) na Iddy Adamu (32) wanaodaiwa kushirikiana kufanikisha tukio la kumbaka na kumdhalilisha binti wa miaka 21, mkulima (jina limehifadhiwa), mkazi wa Kata ya Dakawa, wilayani Mvomero, mkoani Morogoro, wamekamatwa na kuhojiwa na jeshi la polisi mkoani humo. 





Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo la kinyama usiku wa Mei 4, mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Titii iliyoko Dakawa ambapo Zuberi ambaye ni dereva, mkazi wa Mbarali Mbeya anadaiwa kumbaka binti huyo huku Iddy ambaye ni mkulima, mkazi wa Makambako akirekodi picha za video kwa kutumia simu yake ya mkononi. 




Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, baada ya kurekodi katika simu yake, baadaye Iddy alizituma picha hizo kwa mtu aliyefahamika kwa jina la Rajabu Salehe (26), mkazi wa Dakawa ambaye naye alizisambaza picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa watu mbalimbali. 




Taarifa ya polisi imeeleza kuwa, chanzo cha tukio hilo ni kwamba, binti huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Zuberi ambapo siku hiyo mtuhumiwa alimpigia simu binti huyo na kumwambia aende katika nyumba hiyo ya wageni. 




Taarifa hiyo ya polisi imezidi kueleza kuwa, baada ya kufika katika chumba husika ndipo Iddy alipoingia kisha kumtaka binti huyo afanye atakachomuelekeza huku akimshikia kisu ili asipige kelele na baada ya kutekeleza ukatili huo (ubakaji), walimtaka asitoe siri hiyo vinginevyo atauawa. 




Aidha, baada ya tukio hilo kuripotiwa kituo cha Polisi Dakawa Apliri 5, mwaka huu, polisi walianza uchunguzi mara moja ambapo walifanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 11 wakiwemo Zuberi na Iddy pamoja na walioshiriki kuzisambaza picha hizo za udhalilishaji ambao ni; 




Rajabu Salehe (26), Saidi Athumani (26), Musini Ngai (36), Saidi Mohamedi (24), John Peter (24), Hassani Ramadhani (27), Ramadhani Ally (26), Lulu Peter (38) na Magreth Njonjome (30), wote wakazi wa Dakawa ambapo kwa pamoja wamefunguliwa shitaka la PICHA ZA UTUPU (P.O.N.O.GRAFIA) chini ya kifungu cha 14 (1) (a) cha sheria ya makosa ya mtandao. 




Taarifa hiyo ya polisi pia imeeleza kuwa jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine huku jeshi hilo likitoa onyo kwa wananchi wote kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kutoshiriki makosa ya uhalifu wa kimtandao kwani sheria itachukua mkondo wake. 




Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu leo alikemea suala hilo bungeni na kueleza masikitiko yake makubwa kwa watu hao kutekeleza unyama huo na kusisitiza kuwa watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani haraka.
Share:

Jeshi La Polisi Lanasa Mahausigeli 15 Waliokuwa Wakipelekwa Oman Kufanya Kazi za Ndani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wasichana 15 katika nyumba iliyopo maeneo ya Ukonga, waliokuwa tayari kusafirishwa kwenda Oman kufanya kazi za ndani.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Simon Sirro, alisema wasichana hao walikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa toka kwa msiri kuwa kuna mtu amewaweka wasichana kwa ajili ya kuwasafirisha.


Sirro alisema Polisi walifuatilia na kufika katika eneo hilo na kufanikiwa kuwakuta katika nyumba ya Hadija Mohamed (40) wakiwa wamegawanywa katika vyumba viwili.


Alisema uchunguzi wa awali, umebaini kuwa mwanamke huyo anashirikiana na mwenzake Salma Habibu (43) mkazi wa Temeke kuwatafutia masoko nchini Oman na wao ni mawakala wanaoletewa kutoka mikoani na kuwapokea kwa ajili ya kuwasafirisha.


Aidha alisema watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.


Pia ametoa onyo kwa watu wenye tabia hiyo kuacha, kwani wasichana hao wakifikishwa nje ya nchi hufanyiwa vitendo vya kikatili na unyanyasaji. 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger