Monday, 25 April 2016
Sunday, 24 April 2016
download Mafikizolo & Diamond Ft. Dj Maphorisa - Colors Of Africa | Mp3 Download [New Song]-VIDEO &MP3
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
wimbo mpya wa diamond platnumz -Mafikizolo & Diamond Ft. Dj Maphorisa - Colors Of Africa | Mp3 Download [New Song]
Saturday, 23 April 2016
Friday, 22 April 2016
MPYA:WAMILIKI WA SHULE ZIFUATAZO WANAARIFIWA KUCHUKUA VYETI VYAO VYA USAJILI WA SHULE
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
WAMILIKI WA SHULE ZIFUATAZO WANAARIFIWA KUCHUKUA VYETI VYAO VYA USAJILI WA SHULE
Property | Value |
Name: | WAMILIKI WA SHULE ZIFUATAZO WANAARIFIWA KUCHUKUA VYETI VYAO VYA USAJILI WA SHULE |
Description: | Registered Schools |
Filename: | VYETI VYA USAJILI AWALI MSINGI NA SEKONDARI.pdf |
Filesize: | 114.33 kB |
Filetype: | pdf (Mime Type: application/pdf) |
Creator: | lukweme |
Created On: | 04/22/2016 19:41 |
Viewers: | Everybody |
Maintained by: | Editor |
Hits: | 6 Hits |
Last updated on: | 04/22/2016 19:49 |
Homepage: |
Hatima ya Mkataba Tata wa Lugumi Mikononi mwa Spika Job Nduagai
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Hatima ya mkataba tata wa kampuni ya Lugumi Enterprises ipo mikononi
mwa Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya jana, Kamati ya Bunge ya Hesabu
za Serikali (PAC) kuwasilisha muhtasari wa ilichokibaini baada ya
kupitia maelezo ya utekelezaji wake.
Moja kati ya mambo yaliyomo
katika muhtasari huo ni kulitaka Bunge kutoa ruhusa kwa kamati ndogo
iliyoundwa na PAC juzi kuchunguza kwa kina mkataba huo wa kufunga mtambo
wa utambuzi wa vidole (AFIS), ikiwa ni pamoja na kutembelea vituo
vinavyodaiwa kufungwa mashine hizo.
Kamati ya PAC ilinusa
ufisadi kwenye mkataba huo wa AFIS ulioitaka Lugumi kufunga mitambo
kwenye vituo vya polisi 108 kwa gharama ya Sh37 bilioni lakini
ilibainika kwamba kampuni hiyo ililipwa kiasi cha Sh34 bilioni zaidi ya
asilimia 90 ya fedha zote ilhali imefunga mashine 14 tu mkoani Dar es
Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly alisema jana muda
mfupi baada ya kukutana na Spika kuwa wamepeleka mapendekezo hayo na
wanachokisubiri ni kauli ya ofisi yake.
Muhtasari huo umekuja
siku moja baada ya PAC kuwaweka kitimoto Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,
Abdulrahman Kaniki kuhusu mkataba huo.
Bunge liliagiza maelezo ya kina
kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo baada ya kubaini kuwa una
maswali mengi kuliko majibu na liliwaita viongozi hao ili kupata
ufafanuzi wa kina.
Katika maelezo yake jana, Aeshi alisema kesho
watakuwa wameshapata majibu kutoka Ofisi ya Spika na wataweka wazi
mambo yote waliyokuwa wakiyajadili kuhusu Lugumi.
“Hili ni jambo
zito ambalo linahusu usalama kwa hiyo ni lazima twende nalo taratibu
ili kujua ukweli na kuja na majibu ya kueleweka... kila kitu tutawaeleza
Jumamosi,” alisema.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA LINDI ASIMAMISHWA KAZI
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Alitoa ushauri kujenga banio dogo. Zambi alisema kwa jumla ushauri wao haukuwa mzuri na kusababisha hasara kwa mamlaka husika
Serikali
ya Mkoa wa Lindi imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Lindi, Oliver Vavunge na kumwomba Waziri Mkuu amsimamishe
kazi Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Kilimo cha Umwagiliaji Maji Taifa
kutokana na hasara ya Sh milioni 500 katika mradi wa umwagiliaji maji wa
Kiwalala Narunyu, Lindi.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliyasema hayo jana wakati
alipozungumza na wananchi kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Kiwalala
wilayani humo juzi.
Zambi
alisema kati ya fedha zilizowekwa kwa ajili ya kutekeleza mradi wa
umwagiliaji maji ni Sh milioni 700, kati ya hizo Sh milioni 500
zilishatumika na kubakia Sh milioni 200.
Alisema
mradi huo ulioanza mwaka 2011 mpaka mwaka huu haujakamilika na fedha
zilishachukuliwa, na kufafanua kuwa mkurugenzi anaingia hatiani kutokana
kutokuwa makini juu ya mradi huo katika usimamizi.
Alitoa
fedha kwa nyakati tofauti kumlipa mkandarasi wa kwanza na kuvunja
mkataba naye Sh milioni 121, wa pili alivunja na alitoa Sh milioni 226
na Sh milioni 116, mwaka jana.
Zambi
alisema fedha hizo zilikuwa zinachukuliwa baada ya makandarasi wakidai
kwa kazi walizokuwa wakizifanya kwa kuweka miundombinu ya shamba hilo.
Alisema
Tume ya Umwagiliaji Maji nayo wataalamu wake hawakuwajibika ipasavyo
juu ya usimamizi wa mradi huo kwani wao ndiyo waliotia hasara kwa
mamlaka kutokana na barua zao walizokuwa wanaziandika juu ya mradi huo.
Barua
ya kutoka Ofisi ya Kanda ya Kusini Tume ya Umwagiliaji Maji
iliyoandikwa Septemba mwaka jana ilieleza kuwa mradi huo unatekelezeka
kwa kiwango hicho cha fedha, na Novemba 27, mwaka jana, Kaimu Mkurugenzi
wa Umwagiliaji Maji alifika na kuandika barua kuwa mradi huo hauwezi
kutekelezeka, kinachotakiwa ni kufanya tathmini upya.