Friday, 19 February 2016

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 19 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Thursday, 18 February 2016

Mwanamke kakutwa Hostel za wanachuo Dar akiwa kang’olewa meno, jamaa wakataka kumbaka…(Hekaheka+Audio)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kwenye Hekaheka ya Clouds Fm Feb 18 2016 inamuhusu Mwanamke  mjamzito na watoto wake wawili kukutwa katika hostel za Wanafunzi Dar, kaamua kuondoka nyumbani baada ya kuwa akipokea kipigo mara kwa mara kutoka kwa mume wake kwa madai kuwa kamsababishia maambukizi ya UKIMWI.
Geah Habib alipata time ya kuhoji imekuwaje hadi akawa hapo? ‘Ugomvi wetu ni wa muda mrefu, baada ya kupata mwanamke mwingine mume wangu akaanza kuninyanyasa hadi tumefikishana kwa mabalozi
Madai yake eti mimi nimeuleta UKIMWI ndani ya nyumba, mimi nikaamua kuondoka hadi muda huu nipo hapa kwasababu pia amekuwa akininyanyasa
Full stori nimekurekodia kwenye hii sauti hapa chini…
http://cdn12.hulkshare.com/dev12/0/009/752/0009752381.fid/hekaheka_february_18.mp3?key=59f5ac62e592ef7ac71e7450fe8c7f6c&dl=1
Share:

Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kwa watainiwa zaidi ya 40 Matokeo Kidato cha nne 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


 









 
 
1. Pande ya mkoani Lindi,
2. Igawa ya Morogoro, 
3.Korona ya Arusha, 
4. Sofi ya Morogoro,
 5. Kurui ya mkoani Pwani
 6. Patema ya Tanga
7. Saviak ya Dar es salaam, 
8. Gubali ya Dodoma, 
9. Kichangani ya Morogoro
10. Malinyi ya Morogoro.
 KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CSEE 2015

KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE QT 2015
<<<<  BONYEZA HAPA>>>>>>
Share:

HIZI NDIZO SHULE ZILIZOONGOZA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

1.Kazirege –Kagera 
2.Alliance Girls-Mwanza
3. St Francis Girls-Mbeya 
4. Alliance Boys-Mwanza 
5. Canossa-DSM
6. Marian Boys-Pwani 
7. Alliance Army Rock-Mwanza
 8. Feza Girls-DSM 
9. Feza Boys-DSM 
10. Uru Seminary-Kilimanjaro

KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CSEE 2015

KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE QT 2015
<<<<  BONYEZA HAPA>>>>>>
Share:

AUDIO:Alichokiandika Wema Sepetu baada ya mimba yake kuharibika

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Moja ya stori kubwa zilizokamata kwenye mitandao ya kijamii feb 17 2016 ilikuwa ni post ya mrembo wa bongo, Wema Sepetu. Wema aliandika maelezo kuhusu kuharikika kwa mimba yake.
Full stori nimekuwekea pia kwenye hii sauti ikiwa ni pamoja na interview niliyowahi kufanya na Idris Sultan…
Share:

NECTA:UFAULU ,MATOKEO KIDATO CHA NNE 2015 WASHUKA WANAFUNZI 113,489 WAPATA ZERO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mpekuzi blog

Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
 
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
 
Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
 
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
 
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
 
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
 
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
 
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
 
Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
 
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.


==>>  Bofya  <<Hapa  Kuona  Matokeo >>
 AU
Share:

Kasi Ya Rais Magufuli Yawagonganisha Waziri Wa Afya na Mkuu wa Wilaya Temeke

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Siku mbili baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema Wilaya ya Temeke inaongoza mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na wagonjwa sita wa kipindupindu, Mkuu wa wilaya hiyo (DC), Sophia Mjema amesema hadi jana hakukuwa na mgonjwa hata mmoja.

Baada ya DC huyo kukanusha, jana wizara hiyo ilitoa taarifa ikisisitiza kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na ugonjwa huo.

Kipindupindu ni moja ya vigezo vinne vilivyowekwa na Rais John Magufuli kupima utendaji kazi wa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kabla ya kufanya uteuzi mpya.

Jumatatu iliyopita akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Waziri Ummy alitoa takwimu za ugonjwa huo na kuitaja Temeke kuwa kinara lakini juzi, Mjema alisema kulikuwa na wagonjwa ambao hawakuwa wamethibitika kama wanaugua kipindupindu.

Jana, Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema juzi kulikuwa na mgonjwa mmoja wa kipindupindu lakini aliruhusiwa baada ya kupona.

“Kwa hiyo leo (jana) Manispaa ya Temeke haina hata mgonjwa mmoja na kambi ni nyeupe haina mtu,” alisema.

Alisema manispaa hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kanuni za afya ili kujikinga na ugonjwa huo baada ya kufanikiwa kuutokomeza.

“Hatutapumzika tutaendelea kuwakumbusha wananchi kutunza mazingira yao kuwa safi kwa sababu kipindupindu ni hatari,” alisema.

Wakati ofisa hiyo akisema hayo, Waziri Ummy alitoa taarifa akisema Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku 10 zilizopita kuanzia Februari 7 hadi 16 kulikuwa na wagonjwa 16; Temeke 12 na Ilala wanne.

Alisema wizara yake ndiyo yenye dhamana ya kusimamia huduma za afya kwa jamii, hivyo wagonjwa hao walikidhi vigezo vya ainisho sanifu na kupata matibabu katika kambi ya kipindupindu kwa wagonjwa wa Temeke na Hospitali ya Amana kwa wagonjwa wa Ilala hivyo kulazimu kutolewa taarifa kwa mujibu wa mwongozo.
Share:

Afukuzwa CCM Kwa Kumfanyia Kampeni Edward Lowassa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Halmashauri ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu, Peter Mwininga baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM).

Licha ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao.

Akizungumza baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani hapa, Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kupokea malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya ujumbe huo kutokana na kupungukiwa na sifa.

Kalidushi alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama chao na kumfanyia kampeni mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, huku akijua wazi kuwa ni kosa.

Katibu wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kitendo cha Mwininga kuvuliwa nafasi aliyokuwa nayo kinatokana na usaliti na huo ni mwanzo wa chama hicho kuwafukuza wasaliti.
Share:

Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Februari 18

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Share:

Wednesday, 17 February 2016

Walimu Watatu Wakatwakatwa Mapanga Huko Musoma, Mara

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Walimu watatu wa shule ya Secondary Mara iliyopo katika manispaa ya mji wa Musoma Mkoani Mara,Vedastus Rwechungula ,Juma Amos Na Maccelo Ndege, Wamekatwa Mapanga sehemu mbali mbali ya miili yao walipokuwa wakirejea shuleni hapo Usiku wa Saa Nne toka matembezini.

Wakizungumza wakiwa wamelazwa katika hospital ya Rufaa ya Musoma,Walimu hao wamesema kuwa Vitendo vya Uhalifu jirani na Shule hiyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara kutokana na vibaka waliopo katika eneo hilo kuwakata watu kwa mapanga.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger