Mbunge wa arusha mjini Godbless lema amesema leo bungeni swala la
Zanzibar si la kichama,Ni swala la nchi na lisipotafutiwa ufumbuzi lina
athari kwa kila mtu,
Lema ameenda mbali zaidi na kuwaambia Wabunge Wa CCM hii nchi
ikiharibika hata watoto wao wataharibikiwa na hawawezi kukaa madarakani
kwa maisha yao yote.
Lema amemtolea mafano mbunge Marry nagu na kumwambia akumbuke serakali
iliyopita alikuwa waziri,Lakini leo naye anauliza maswali ya nyongeza.
Lema alienda mbali zaidi na kumwambia Mwenyekiti wa bunge Chenge asijione ni mdogo wake mungu kwa kukalia kiti cha spika.
Serikali
katika mwaka wa fedha 2016/2017 imepanga kuongeza ajira kwa vijana ili
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa
kitanzania kwa kuongeza ajira na kuwezesha wengine kujiajiri kupitia
mifuko ya uwezeshaji toka Halmashauri za Wilaya nchini.
Akijibu
swali la Mhe.Mgumba Tebweta Omary Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM) lenye
sehemu a na b lililouliza Serikali itaanza lini kuwawezesha vijana wa
Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki kifedha ili waweze kujiajiri na
kuondokana na tatizo la ajira na umaskini ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe Suleiman Jafo
amesema vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kusini Mashariki
wamekuwa wakiwezeshwa kiuchumi kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana ambapo kila Halmashauri hupaswa kutenga asilimia 5 ya mapato yake
ya ndani kila mwaka kwa ajili ya vijana.
Mhe
Suleiman Jafo ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka
2014/2015,Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilifanikiwa kutoa Shillingi
Millioni 10.3 kwa vikundi vya vijana 19 kwa ajili ya kutekeleza shughuli
mbalimbali za kiuchumi na katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016
vikundi vya vijana vilitengewa Shilllingi Millioni 87.5 ili kuviwezesha
kiuchumi kwa kujiajiri.
“Katika
kutatua changamoto zilizopo kwa vijana tunawawezesha kifedha ili
kujiajiri ili kumekuwa na tatizo la fedha kuchelewa kufika kwa walengwa
ila Serikali kupitia Wizara yangu tunalifanyia kazi ili fedha zifike kwa
wakati na tumetenga Shillingi Millioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya
kuwezesha vijana walioko katika vikundi mbalimbali mfano SACCOS ili
waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi kwa kujiondoa katika hali ya
umaskini”
“Napenda
kuwaomba wabunge tusaidiane sababu wao wanahusika katika kamati za
fedha za Halmashauri za Wilaya, waende wakasimamie hizo fedha kwa ajili
ya kuwezesha vijana zitoke na ziwasaidie walengwa” Alisema Mhe Jafo.
Aidha
Mhe Suleiman Jafo amesema kuwa Serikali imetenga Shillingi Billioni
233 kwa ajiri ya kuajiri vijana wapya takribani 71,408 kati ya hao
watumishi wapya wa Afya wanatarajiwa kuwa takribani 10,871 na Waalimu
40,000 kwa nchi nzima ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana
wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini.
Serikali
kupitia Halmashauri za Wilaya imejipanga katika kuwawezesha vijana
katika maeneo yao kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri na kwa mwaka wa
fedha 2016/2017 Serikali itaboresha zaidi mifuko ya kuwezesha vijana
katika Halmashauri za Wilaya kwa kununua vifaa zaidi vya kujifunza stadi
mbalimbali za kazi zitakazowezesha vijana wengi zaidi kuwa na ujuzi
utakaowasaidia kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.
1.0 UTANGULIZI Imebainika kwamba bado malalamiko ya baadhi ya wanafunzi
hayashughulikiwi ipasavyo katika muda mfupi na kupelekea wanafunzi
kwenda kulalamika ofisi za juu hata kwa masuala ambayo yako wazi na
ambayo maelezo yake wangepaswa kuyapata katika ngazi za vyuo au katika
Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Aidha, itakumbukwa kuwa, ili kuboresha ufanisi wa utoaji mikopo,
mwezi Agosti mwaka 2011, Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi ilivielekeza vyuo vyote za elimu ya juu kuanzisha
madawati yatakayoratibu na kusimamia masuala ya mikopo na ruzuku kwa
wanafunzi wa vyuo husika. Agizo hili limetekelezwa vizuri kiasi na hivi
sasa kila chuo cha elimu ya juu kina Afisa anayesimamia masuala ya
mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wao wanaokopesheka. Hivyo, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda
kuwakumbusha wadau wake wote, wakiwemo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya
juu, kuhusu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko au maswali yanayohusu
mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa elimu ya juu kama ifuatavyo hapa
chini. 2.0 UTARATIBU WA KUWASILISHA MALALAMIKO i. KWANZA, mwanafunzi yeyote anayefadhiliwa na Serikali kupitia
Bodi ya Mikopo mwenye swali au malalamiko anatakiwa kuwasilisha suala
lake kwa Afisa mhusika anayesimamia Dawati la Mikopo/Ruzuku (Loan
Officer) aliyepo chuoni kwake. Hao ‘Loan Officers’ hivi sasa wana uzoefu
wa masuala ya mikopo na ruzuku zitolewazo na Bodi; ii. PILI, baada ya swali au malalamiko kupokelewa, ‘Loan Officer’
huyo anapaswa kuyapokea na kuyatafutia suluhisho malalamiko hayo na
kumjibu mwanafunzi ndani ya siku mbili (02), kama siyo siku hiyo hiyo,
tangu apokee swali au malalamiko hayo; iii. TATU, ikiwa siku mbili (02) zitapita bila mwanafunzi kupata
jibu, mwanafunzi awasilishe malalamiko yake kwa mamlaka ya juu ya huyo
‘Loan Officer’ ambaye naye anapaswa kutoa majibu au kuchukua hatua
ndani ya siku mbili (02), kama siyo siku hiyo hiyo; iv. NNE, ikiwa kiongozi wa chuo husika cha elimu ya juu atakuwa
hana jibu la swali au malalamiko yaliyowasilishwa kwake, anapaswa
kuwasilisha suala hilo Ofisi ya Bodi ya Mikopo ya Kanda iliyo karibu na
chuo chake. Ofisi ya Kanda itawajibika kutoa jibu siku hiyo hiyo ya
kupokea maswali au malalamiko hayo au kuwasilisha suala hilo Makao Makuu
ya Bodi ya Mikopo kama hana maelezo yake; v. TANO, kwa vyuo vya elimu ya juu ambavyo havipo karibu na ofisi
za Kanda za Bodi ya Mikopo, uongozi wa chuo husika unapaswa kuwasiliana
na makao Makuu ya Bodi ya Mikopo moja kwa moja kwa njia ya barua pepe
ifuatayo: malalamiko@heslb.go.tz ; vi. SITA, baada ya kupokea malalamiko hayo, Bodi ya Mikopo Makao
Makuu itatoa majibu kwa malalamiko/maswali yaliyowasilishwa siku hiyo
hiyo au ndani ya siku mbili (02) tangu kupokelewa kwa malalamiko au
maswali hayo; na vii. SABA, mara tu baada ya kupokea majibu ya swali au malalamiko
yaliyowasilishwa kutoka Bodi ya Mikopo, uongozi wa chuo cha elimu ya juu
utayafikisha majibu hayo kwa mwanafunzi husika siku hiyo hiyo kupitia
kwa ‘Loan Officer’ wa chuo husika.
3.0 HITIMISHO Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inasisitiza kuwa ni
muhimu kwa wanafunzi na wadau wote kuzingatia utaratibu huu ili kuongeza
ufanisi katika kushughulikia malalamiko ya wanafunzi.
IMETOLEWA NA: MKURUGENZI MTENDAJI, BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Wabunge
wa upinzani, wakiwamo wanaootoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), wamepata pigo la aina yake baada ya jukumu mojawapo
muhimu la kamati wanayopaswa kuiongoza kuondolewa kwao, imefahamika.
Kamati
hiyo ni ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) ambayo
imehamishiwa kwenye kamati mpya inayoongozwa na wabunge wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Majukumu hayo muhimu yaliyohamishwa PAC ni yale yanayohusiana na hesabu za mashirika ya umma.
Majukumu
hayo sasa yamehamishiwa kwenye kamati mpya ya Bunge ya Uwekezaji na
Mitaji ya Umma (PIC), chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Jimbo la Sumve
(CCM), Richard Ndasa, huku makamu mwenyekiti akiwa Lolesia Bukwimba
(Busanda-CCM).
Naibu
Katibu wa Bunge anayeshughulikia masuala ya Bunge, John Joel,
amethibitisha juu ya kuwapo kwa mabadiliko hayo, akisema kwamba ni
kweli PIC imepewa jukumu la kusimamia hesabu za mashirika ya umma
kutokana na kanuni za Bunge, toleo la Januari 2016.
Alisema uamuzi wa kupeleka jukumu hilo PIC, umetokana na pendekezo la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kutokana na PAC iliyopita kushindwa kutimiza majukumu yake iliyopewa.
Katika
mabunge yaliyotangulia, hesabu za mashirika ya umma zilikuwa
zikisimamiwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyokuwa ikiongozwa
na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia (Chadema), Zitto Kabwe. Hivi
sasa, Zitto ni Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo.
Kamati hiyo pia iliwahi kuongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo.
Kumbukumbu
zinaonyesha kuwa mara zote PAC ndiyo iliyokuwa mstari wa mbele katika
kuibua ‘madudu’ mbalimbali yanayohusiana na rushwa na ufisadi bungeni na
kuilazimu serikali kubadili mawaziri wake mara kadhaa.
Baadhi
ya mambo yaliyowahi kuibuliwa na PAC ni pamoja na kashfa ya Akaunti ya
Tegeta Escrow ambayo ripoti yake ilisababisha mawaziri wawili wa
serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete na maofisa wengine
kadhaa wa juu kuachia ngazi.
Taarifa ya PAC kuhusiana na ripoti ya CAG mwaka 2012 pia ilisababisha vigogo kadhaa, wakiwamo mawaziri, kung’olewa.
Zitto Atoa ufafanuzi
Aliyekuwa Mwenyekiti wa PAC kwenye Bunge la 10, Zitto, amesema si kweli kwamba kuna jukumu walilopewa na kushindwa kulitimiza.
“Kwa
kweli tulitimiza majukumu yetu yote. Na ili tufanye kazi yetu kwa
ufanisi, tuliigawa kamati, eneo moja likawa chini ya Makamu Mwenyekiti
(Deo Filikunjombe) na moja chini yangu. Deo mashirika na mimi serikali.
"Hata
hivyo, kazi ilikuwa kubwa na muhimu kugawa PAC kuwa na PIAC na PAC.
Isipokuwa, PIC ya sasa haina mamlaka ya kushughulikia hesabu za
mashirika ya umma kwa mujibu wa kanuni. Kamati za mahesabu ni mbili tu,
PAC na LAAC,” alisema Zitto.
Aliongeza
kuwa iwapo Bunge linataka PIC ishughulike na hesabu za mashirika ya
umma, itabidi iitwe Public Investments Account Committee (PIAC) na
itabidi iongozwe na mbunge wa upinzani na siyo wa CCM.
“Kanuni
za Bunge za sasa hazielekezi PIC kushughulikia taarifa ya CAG kuhusu
mahesabu ya mashirika ya umma. Pia kanuni haziipi PAC mamlaka hayo pia.
Kikanuni, hivi sasa mahesabu ya mashirika ya umma hayana kamati,” alisema Zitto.
Stori: Mayasa Mariwata, Wikienda
Dar es Salaam: Inauma sana! Baada ya kuwepo kwa madai kuwa mwanadada
Rehema Chalamila ‘Ray C’ amerudia matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’,
Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kiliingia
mzigoni kujua kama anaendelea na dozi ya kuacha ishu hiyo na kujua
anakopatia ulevi huo kwa sasa.
Katika kusaka majibu ya mambo hayo mawili, yalipatikana madai kuwa
kwa sasa ameacha kwenda kuchukua dozi ya kupona ya Methadone kwenye
Hospitali ya Mwanayamala, Dar kama alivyokuwa akifanya awali.
Habari zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vyetu zilieleza kwamba,
msanii huyo ambaye tangu alipoanza kupatiwa matibabu ya kuacha unga
alikuwa akihudhuria hospitalini hapo kuchukua lakini sasa haendi.
Ili kung’amua ukweli wa madai hayo, OFM ilizama kwenye Hospitali ya
Mwananyamala na kuongea na Mganga Mkuu, Dk. Delila Moshi aliyethibitisha
Ray C kutofika tena hospitali hapo kwa ajili ya kupatiwa dozi.
“Ray C haji tena hapa siku hizi labda amehamia Muhimbili,” alisema Dk. Delila.
OFM ilifika Muhimbili ili kujua maendeleo ya mwanadada huyo ambapo Afisa
Habari aliyejitambulisha kwa jina moja la John alidai kuwa Ray C si
miongoni mwa watu waliohamishiwa hapo.
“Kuna wagonjwa wamehamishiwa hapa lakini Ray C hayupo,” alijibu kwa
kifupi na hata alipobananishwa kuwa mwanadada huyo amehamishiwa hapo na
huenda ameamua kuacha dozi aliishia kucheka.
Katika fukunyuafukunyua, OFM ilipokea madai kwamba, baada ya kuacha
dozi kwa sasa ana machimbo yake ambayo huwa anakwenda kununua unga.
Katika hilo, yalitajwa maeneo mawili, Magomeni na Mwananyamala nyuma ya hospitali hiyo.
OFM ilifika maeneo hayo yote na kushuhudia pilika za watu
wasioeleweka huku wakijishtukia na kumshangaa Kamanda wa OFM,
wakiambizana kuwa kulikuwa na sura ngeni katika maeneo yao hivyo
wachukue tahadhari.
Kwenye eneo hilo la Mwananyamala, OFM ilibaini nyumba moja iliyodaiwa kuwa ndilo chimbo la ‘mambo hayo meupe’.
Katika kujiridhisha na mzani wa habari hiyo, OFM ilimtafuta Ray C ili
kueleza juu ya madai ya kuacha tiba hiyo huku akitajiwa maeneo
anayokwenda kuchukua unga ambapo aliwaka akidai kwamba hajaacha kwenda
kuchukua dozi Mwananyamala.
Hii ni orodha kamili ya washindi Best Audio Producer
Dr Fizol Best Video Producer
Savy Films – Sasha Vybz Best Songwriter
Moses Radio Best Hip Hop Song
Kigozi (Iko Hivi) by Navio Best RnB Song
Linda by Rema and Chris Evans Best Ragga Dancehall Song
Friendly Match by Ziza Bafana & Zanie Brown Best Reggae Song
Go Mama by Bebe Cool Best Religious Song
Saum Kareem by Swahaba Kasumba Best Band Song
Nkuze by Maureen Nantume Best Folk/Kadongo Kamu Song
Akalulu by Saava Karim Best Zouk Song
Memories by A Pass & Lillian Mbabazi Best Afrobeat Song
Mpulunguse by Diana Nalubega Best Afropop Song
Tusasanya by Prof. Big Eye Best Regional Song
Go On – Pine Avenue 5 All Stars and Barbi Jay (North) Best DJ
DJ Shiru East Africa Best Video
Nana by Diamond Platnumz Ft Mr Flavour (Tanzania) East Africa Super Hit
Nana by Diamond Platnumz (Tanzania) Most Active Fans Group
Gagamel Phamily Artist of the Year
David Lutalo Best Male Artist
David Lutalo Best Female Artist
Sheebah Karungi Best Music Group
Radio and Weasel Best Breakthrough Artist
Winnie Nwagi Album of the Year
Go Mama by Bebe Cool Video of the Year
Siri Zari by Sheebah Song of the Year
Juicy by Radio and Weasel
Winner of Convertible Peugeot 207
Igama Benedict. Life Time Achievement Award.
Paul Saka. Video Trailblazer Award.
Triplets (Ghetto kids).