INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tuesday, 27 October 2015
Lowassa na Magufuli Waendelea Kuchuana kwa Karibu...Mpaka sasa Magufuli Anakura 1,689,003 Huku Lowassa Akiwa na 1,239,105
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ushindani ni mkubwa sana kati ya Lowassa na Magufuli. Wote wanakabana kwa karibu sana katika majimbo yote yaliyotangazwa na tume.
Ushindani ni mkubwa sana kati ya Lowassa na Magufuli. Wote wanakabana kwa karibu sana katika majimbo yote yaliyotangazwa na tume.
Hadi sasa ni ngumu sana kutabiri ni nani ataibuka kidedea. Tume imeshatangaza majimbo 87 hadi sasa na imeahidi kuendelea kutangaza majimbo mengine ifikapo saa mbili usiku huu.
Katika majimbo hayo 87, Magufuli ana kura 1,689,003 huku Lowassa akiwa na 1,239,105
Bila shaka unaweza kuona......wanachuana kwa karibu sana.
Mpekuzi tutakuletea majimbo mengine yatakayo tangazwa Muda huu.
CREDIT:YUVINUSM
HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA SCHORALSHIP NCHINI ALGERIA & EGYPT 2015/2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Habari yako,
Yafuatayo ni majina ya wanafunzi waliochaguliwa katika schoraship zmilizotangazwa na wizara ya elimu mapema mwaka huu,
KUANGALIA MAJINA HAYO BONYEZA HAPO CHINI,
Names of Candidates Selected for Undergraduate Scholarships Tenable in the Egypt and Algeria for the
Academic Year 2015/2016

WILFRED LWAKATARE (CHADEMA) ATANGAZWA KUWA MBUNGE WA BUKOBA MJINI
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Hatimaye Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare ameibuka kidedea na kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yalitangazwa usiku na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa matokeo usiku wa jana majira ya saa 2:30 usiku mara baada ya kumalizika kuhesabu kura zilizopigwa jimboni hapo na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Aron T. Kagurumjuli (Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgembea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki jana usiku.
LICHA ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika jana jumatatu asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo mapema baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia jana kuwa Chadema imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana katika maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu ambacho hakikufanyika na kupelekea kuleta ghasia jimboni hapo. Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya wafuasi wa chama cha Chadema ambao mpaka usiku wa jana walikuwa wamejaa katika eneo la ofisi za Halmashauri ya Bukoba Mjini waishinikiza matokeo kutangazwa. Wafuasi wa chama cha Chadema walisababisha vurugu zikiwemo kurusha mawe na ndipo ndipo jeshi la polisi mjini hapo walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri. Hali hiyo ilitulia baada ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo yakatangazwa.
Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa kutosha.
Kura zilizokubalika ni 54,211 sawa na asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni 805 sawa asilimia 1.46, Matokeo ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis Sued Kagasheki wa CCM amepata kura 25,565 sawa na asilimia 47.2, Wilfred Muganyizi Lwakatare wa Chadema amepata kura 28,112 sawa na asilimia 51.9Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge.
Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba wakisubilia matokeo kutangazwa.
Diwani wa Kata ya Kahororo Chif Kalumuna(kulia) akiwa amembeba mshindi wa ubunge jimbo la Bukoba Mjini bw. Wilfred Lwakatare mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo mkubwa.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii.
Hali ilivyokuwa hapo jana jioni maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri.
Hapa ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya Kashai kupitia chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.
- See more at: http://www.tangayetu.com/2015/10/wilfred-lwakatare-chadema-atangazwa.html#sthash.in2efhP9.dpuf
Updates Za Matokeo Malimbali Ya Ubunge na Udiwani Zinapatikana Hapa
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Updates:Wiliiam Lukuvi ametangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge toka tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ismani, mkoani Iringa kwa kuwa na jumla ya kura 26,119 na mpinzani wake Patrick Sosopi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 15,534
Updates: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215
Updates: Jimbo la Same Mashariki:Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539
Updates:Jimbo la Ilemela jijini Mwanza Angelina Mabula wa chama cha Mapinduzi CCM ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Hainess Kiwia kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshindwa kukitetea kiti chake
Updates:Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966.
Updates:Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyengo Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894
Upadate: Jumanne Kishimba (CCM) ameshinda Jimbo la Kahama Mjini, Steven Masele ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini.
Update: Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini
Jimbo la Serengeti
Jimbo la Chalinze
Jimbo la Moshi Mjini
Japhary Michael wa Chadema ameshinda kwa kura-51647, huku mpinzani wake Davies Mosha wa CCM akipata kura-26920
Jimbo La Arumeru Mashariki
Jimbo la Shinyanga
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi
Jimbo la Tandahimba
Ubunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, Ndugu Julius Kalangaametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.
Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemtangaza Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo
Jimbo la Lindi Mjini
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi - See more at: http://www.tangayetu.com/2015/10/updates-za-matokeo-malimbali-ya-ubunge.html#sthash.Mvl83BZx.dpuf
Updates:Jimbo la Sumbawanga Mjini: Aeshi Hilaly wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41763, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ikuwo Malila wa Chadema, aliyepata kura 36183.
Updates: Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata kura 13665
Updates:Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa Chadema, aliyepata kura 13480
Updates:Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM, aliyepata kura 18614.
Updates: Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema, aliyepata kura 16702
Updates:Jimbo la Mtama: Nape Nnauye wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 28110, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa Chadema, aliyepata kura 13918
Updates: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215
Updates:Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa Chadema, aliyepata kura 15347
Updates: Jimbo la Same Mashariki:Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539
Updates:Jimbo la Mbogwe: Augustino Manyanda wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 32921, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Maganga Nicodemas Henry wa Chadema, aliyepata kura 13975
Updates:Jimbo la Ilemela jijini Mwanza Angelina Mabula wa chama cha Mapinduzi CCM ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Hainess Kiwia kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshindwa kukitetea kiti chake
Updates:Mtwara mjini Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshindwa kukitetea kiti chake
Updates:Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966.
Updates:Jimbo la Ngara: Alex Gashaza wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 53387, dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Dkt.Peter Bujari wa Chadema aliyepata kura 35254
Updates:Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyengo Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894
Updates:Jimbo la Kigoma Mjini: Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 31546, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Amani Kaburou wa CCM, aliyepata kura 16344
Updates:Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 54660, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa Chadema aliyepata kura 12580
Updates:Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 14578
Updates:Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas Kalinde, aliyepata kura 18649
Update: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini.
Update: Edwin Sanda (CCM) ametangazwa mshindi Jimbo la Kondoa Mjini na Dotto Biteko (CCM) ameshinda ubunge Jimbo la Bukombe.
Update: Edwin Sanda (CCM) ametangazwa mshindi Jimbo la Kondoa Mjini na Dotto Biteko (CCM) ameshinda ubunge Jimbo la Bukombe.
Update: Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini
Jimbo la Serengeti
Marwa Ryoba (Chadema) amengazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kupitia tiketi ya Chadema katika jimbo la Serengeti.Jimbo hilo lilikuwa chini ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe
Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete wa CCM, aibuka mshindi katika Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani kwa jumla ya kura 52695, dhidi ya Mang’unda Torongei wa Chadema aliyepata kura 23470
Jimbo la Moshi Mjini
Japhary Michael wa Chadema ameshinda kwa kura-51647, huku mpinzani wake Davies Mosha wa CCM akipata kura-26920
Jimbo la Bunda
Wassira aangushwa!
Ni baada ya Esther Bulaya wa Chadema kuchukua Jimbo la Bunda KWA KURA 26207, huku Wassira kupata kura 17573.
Jimbo la Peramiho
Wassira aangushwa!
Ni baada ya Esther Bulaya wa Chadema kuchukua Jimbo la Bunda KWA KURA 26207, huku Wassira kupata kura 17573.
Steven Wassira |
Jimbo la Peramiho
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peremiho kwa tiketi ya CCM , Jenister Mhagama ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo
Jimbo La Arumeru Mashariki
Mgombea Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema , Joshua Nassari ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo
Nassari ameshinda kwa kura 86694, na mpinzani wake wa karibu John Pallangyo wa CCM amepata kura-31847
Nassari ameshinda kwa kura 86694, na mpinzani wake wa karibu John Pallangyo wa CCM amepata kura-31847
Jimbo la Shinyanga
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi
Jimbo la Tandahimba
Katika jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Katani Ahmed Katani wa CUF ameshinda kiti cha ubunge kwa kura-55156, huku mpinzani wake mkubwa wa CCM, Shaibu Salimu Likumbo akipata kura-41088
Jimbo la Mkinga
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mkinga Dustan Kitandula ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Mbinga Mjini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Mjini Sixtus Mapunda ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Musoma Mjini
Ubunge: Vicent Nyerere(Chadema) 25,549 na Vedastus Mathayo(CCM) 32,836.
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Musoma Mjini Vedastus Mathayo ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Mbinga Vijijini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Vijijini Martin Msuha ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la MonduliUbunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, Ndugu Julius Kalangaametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.
Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).
Jimbo la TundumaUbunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.
Jimbo Buyungu
Ubunge: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934
Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041.
Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo
Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041.
Christopher Chiza |
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo
Jimbo la Tarime Mjini
Ubunge: Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356.
Jimbo la Lindi Mjini
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi - See more at: http://www.tangayetu.com/2015/10/updates-za-matokeo-malimbali-ya-ubunge.html#sthash.Mvl83BZx.dpuf
CCM Waongea na Vyombo vya Habari.....Wamesema Hadi sasa Wameshinda Majimbo 176 kati ya 264
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wanachama, wapenzi na washabiki wake na kwa umma Watanzania.
CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wanachama, wapenzi na washabiki wake na kwa umma Watanzania.
Tathmini ya Upigaji Kura
Kama tulivyoeleza jana, tumeridhishwa na amani na utulivu uliotawala katika sehemu kubwa ya nchi yetu wakati wa zoezi la upigaji kura. Licha ya changamoto zilizojitokeza, ambazo baadhi zimeshughulikiwa, kwa jinsi zoezi la kupiga na kuhesabu kura lilivyoendeshwa kwa uwazi, matokeo ya uchaguzi huu yatakuwa ni kielelezo cha utashi halisi wa Watanzania na kutakuwa hakuna sababu ya mtu yoyote kukataa matokeo.
Kupokea na Kutangaza Matokeo
Kipindi cha kupokea na kutangazwa matokeo ni muhimu kama ilivyo kipindi cha kampeni na siku ya kupiga kura. CCM inahimiza utulivu kwa wafuasi wake na wananchi kwa ujumla na kuziachia mamlaka husika zifanye kazi yake. Katika kipindi hiki, kazi za vyama ni kupokea matokeo na na kazi ya Tume ni kutangaza matokeo.
Tunasikitishwa na propaganda zinazoendeshwa na wapinzani wetu kuhusu matokeo ya uchaguzi. Tunaona matokeo yanayotangazwa na wafuasi wa vyama vya upinzani, hasa mitandaoni. Bahati nzuri, propaganda hizi zinakosa maarifa kiasi cha kutoa hata matokeo ya Ubunge katika majimbo ambayo uchaguzi wa Wabunge haukufanyika, mfano Handeni na Masasi.
Tunawataka wana-CCM wapuuze matokeo yanayotembezwa kwenye mitandao ya kijamii. Matokeo rasmi yatatolewa na Tume. Bahati mbaya sana, wenzetu wanatoa matokeo ya uongo mapema ili Tume ikitoa matokeo rasmi waseme wameibiwa kura na kutafuta kisingizio cha kuingia mitaani na kufanya vurugu.
Pia tunabaini jitihada na nguvu kubwa za wapinzani wetu kupeleka kilio chao kwa waandishi wa habari wa nje ya nchi pamoja na mataifa ya nje kwa ujumla. Wameajiri magwiji wa propaganda kutoka nje ya nchi kwa fedha nyingi kujenga taswira kwenye Jumuiya ya Kimataifa kwamba Tanzania ni kama nchi nyingine yoyote ya Kiafrika ambapo hakuna ustaarabu wala utaratibu wa kidemokrasia na Serikali hukandamiza watu wake.
Mkakati wao ni kuitaka Jumuiya ya Kimataifa itumie nguvu yake ya misaada kwa nchi yetu kulazimisha matokeo ambayo hayatokani na utashi wa Watanzania. CCM haitalikubali jambo hili.

Matokeo ya CCM
Kwa kuwa matokeo kwenye vituo vya kupigia kura matokeo yamebandikwa hadharani na Wasimamizi wa Vituo, na nakala kupewa mawakala wetu, kwa mujibu wa matokeo yaliyobandikwa vituoni , CCM hadi sasa imekwishapata majimbo 176 kati ya majimbo 264 katika mikoa kadhaa ambayo tumefanikiwa kujumlisha hadi sasa. Pia, hadi sasa, tumeweza kukomboa majimbo 11 ambayo yalikuwa upinzani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Tunawaomba wana-CCM watulie, wasiwe na hofu, wawe na subira hadi Tume imalize kazi yake. Matokeo ya Urais, ambayo yanaendelea kutangazwa na Tume, hayana tofauti na mwenendo tunaouona katika kura za Ubunge.
Imetolewa:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
26.10.2015
Matokeo Ya Urais: Dk Magufuli anaongoza Majimbo 17, Lowassa Majimbo 10
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Majimbo hayo ni kama ifuatavyo:
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Usiku huu imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 27 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza kwa majimbo 17 wakati Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa anaongoza majimbo 10.
Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa awamu tatu, ambapo asubuhi mwenyekiti huyo alitangaza majimbo matatu ambayo ni Paje, Makunduchi na Lulindi ambayo yote Dk Magufuli ameongoza.
Majira ya alasiri , Jaji Lubuva alitangaza majimbo mengine 10 ambapo kati ya hayo majimbo sita yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo manne yakionyesha Lowassa anaongoza.
Usiku huu majira ya saa mbili , Jaji Lubuva ametangaza majimbo mengine 14 ambapo kati ya hayo majimbo 8 yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo 6 yakionyesha Lowassa anaongoza.
Matokeo ya Urais Singida Mjini
Kura: 56,558
Magufuli (CCM): 36,035
Edward Lowassa (Chadema): 19,007
Matokeo ya Urais Jimbo la Lindi Mjini
Kura: 38,992
Magufuli (CCM): 21,088
Edward Lowassa(Chadema): 17,607
Matokeo ya Urais Jimbo la Njombe Mjini
Kura: 55,772
Magufuli (CCM): 33,626
Edward Lowassa(Chadema):20,368
Matokeo ya Urais Jimbo la Peramiho
Kura:45,374
Magufuli (CCM): 32,505
Edward Lowassa (Chadema): 11,291
Matokeo ya Urais Jimbo la Mkinga
Kura: 39,788
Magufuli (CCM): 23,798
Edward Lowassa (Chadema): 15,142
Matokeo ya Urais Jimbo la Moshi Mjini
Kura:79,814
Magufuli (CCM): 28,909
Edward Lowassa (Chadema): 49,379
Matokeo ya Urais Jimbo la Nanyamba
Kura: 44,437
Magufuli (CCM): 24,904
Edward Lowassa (Chadema): 16,992
Matokeo ya Urais Jimbo la Mbinga Mjini
Kura: 42,717
Magufuli (CCM): 29,295
Edward Lowassa (Chadema):11,695
Matokeo ya Urais Jimbo la Kisarawe
Kura: 38,012
Magufuli (CCM): 24,086
Edward Lowassa (Chadema): 13,093
Matokeo ya Urais Jimbo la Mgogoni
Kura: 7,539
Magufuli(CCM):710
Edward Lowassa (Chadema): 6,506
Matokeo ya Urais Jimbo la Mtambwe
Kura: 7,620
Magufuli (CCM): 428
Edward Lowassa (Chadema): 6,937
Kura: 38,992
Magufuli (CCM): 21,088
Edward Lowassa(Chadema): 17,607
Matokeo ya Urais Jimbo la Njombe Mjini
Kura: 55,772
Magufuli (CCM): 33,626
Edward Lowassa(Chadema):20,368
Matokeo ya Urais Jimbo la Peramiho
Kura:45,374
Magufuli (CCM): 32,505
Edward Lowassa (Chadema): 11,291
Matokeo ya Urais Jimbo la Mkinga
Kura: 39,788
Magufuli (CCM): 23,798
Edward Lowassa (Chadema): 15,142
Matokeo ya Urais Jimbo la Moshi Mjini
Kura:79,814
Magufuli (CCM): 28,909
Edward Lowassa (Chadema): 49,379
Matokeo ya Urais Jimbo la Nanyamba
Kura: 44,437
Magufuli (CCM): 24,904
Edward Lowassa (Chadema): 16,992
Matokeo ya Urais Jimbo la Mbinga Mjini
Kura: 42,717
Magufuli (CCM): 29,295
Edward Lowassa (Chadema):11,695
Matokeo ya Urais Jimbo la Kisarawe
Kura: 38,012
Magufuli (CCM): 24,086
Edward Lowassa (Chadema): 13,093
Matokeo ya Urais Jimbo la Mgogoni
Kura: 7,539
Magufuli(CCM):710
Edward Lowassa (Chadema): 6,506
Matokeo ya Urais Jimbo la Mtambwe
Kura: 7,620
Magufuli (CCM): 428
Edward Lowassa (Chadema): 6,937
Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo ya majimbo mengine ambayo yatakuwa tayari yatatolewa kesho saa tatu asubuhi.
Matokeo Yaliyotangazwa mchana Yako Hapo Chini. Bonyeza Picha Kuyaona Vizuri