Saturday, 17 May 2014

MWILI WA KUAMBIANA WAHIFADHIWA MUHIMBILI, VILIO VYATAWALA!


Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa leo mchana.
Rais wa Bongo Movies, Steve Nyerere akiwa analia nje ya chumba cha maiti Muhimbuli.
Wasanii wakilia kwa uchungu nje ya chumba cha maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mchana wa leo.
Share:

MAJANGA: WAZAZI WASUSA MAITI YA MTOTO WAO


Haijakaa sawa! Tofauti na desturi ya Kitanzania watu kuwa pamoja katika kipindi cha matatizo, wazazi wa marehemu, Leonard Jorome Mwakanyamale, wanadaiwa kususa kuzika maiti ya mtoto wao kisa ugomvi kati ya marehemu na nduguze. 
Kijana Leonard Jorome Mwakanyamale,enzi za uhai wake
Leonard ambaye alikuwa akiishi Buguruni jijini Dar, alifariki dunia Mei 10, mwaka huu kwa Ugonjwa wa Malaria.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa jirani mmoja ambaye hakutaka jina lichorwe , Leonard alikuwa na ugomvi na familia yake na aliapa kutokanyaga kwao mkoani Mbeya tangu alipokwenda kumzika bibi yake, zaidi ya miaka mitano iliyopita.
“Tangu nijuane na Leonard zaidi ya mwaka wa tano, hajakanyaga kwao.
“Nilisikia mara ya mwisho kwenda kwao ilikuwa msiba wa bibi yake.
“Tunasikia wakati anatoka Mbeya kuna maneno yaliwakera wazazi wake, inawezekana ndiyo yamewachefua na kushindwa kumsamehe kwani nasikia alidai hatarudi tena Mbeya kwa kuwa watu aliokuwa akiwapenda walishamalizika, yaani bibi yake.
Mwili wa Leonard Jorome Mwakanyamale,ukiwa makabulini tayali kwa mazishi
“Sijui kwa nini alisema maneno hayo japokuwa uwezo wa kumsafirisha ulikuwepo kabisa lakini wazazi walikataa asipelekwe kwa kuwa alipasusa kwao hivyo azikwe Dar es Salaam na siyo mkoani Mbeya,” alisema jirani huyo.
Jitihada za kuwatafuta ndugu wa marehemu ziligonga mwamba kwani simu zao hazikuwa hewani, kupitia habari hii wakiisoma, wanaweza kutoa ufafanuzi.
Naye mke wa marehemu, Letisia Mbilite hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa haamini kilichotokea na alikuwa na majonzi mazito.
Baada ya wazazi kutokubali kushiriki mazishi ya mtoto wao, marafiki waliungana, wakauhifadhi mwili katika Hospitali ya Amana, Dar kisha kusomewa misa na Mwenyekiti wa Kanisa la Parokia ya Stephano, Shahidi Anton Makala na kuzikwa katika Makaburi ya Wailes yaliyopo Chang’ombe, 
Share:

TANGAZO MAALUMU KUTOKA BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WOTE WA VYUO VIKUU KUHUSU KU UPDATE MKOPO

                          
Continuing students who are loan beneficiaries
All other continuing students’ loan beneficiaries shall continue to receive their loans as per their previous Means Test grades. However all continuing students who are loan beneficiaries need not to reapply for loans except those who are no longer in need should notify the Board through the Online Loan Application System (OLAS).
Share:

TANGAZO MUHIMU KWA VIJANA KIDATO CHA SITA 2014 MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA KWANZA NA AWAMU YA PILI


                                              
ORODHA YA VIJANA KIDATO CHA SITA WANAOKWENDA JKT MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA KWANZA IMEFANYIWA MAREKEBISHO KAMA IFUATAVYO:-
  • VIJANA 1200 WAMEONDOLEWA KUTOKA KIKOSI CHA RUVU NA KUPELEKWA VIKOSI VYA MAKUTUPORA, MAFINGA NA WACHACHE VIKOSI VINGINE.

  • MAREKEBISHO MACHACHE PIA YAMEFANYIKA KATIKA VIKOSI MBALIMBALI.

  • KUTOKANA NA MAREKEBISHO HAYO VIJANA WANASISITIZWA KUHAKIKI TENA MAJINA YAO KATIKA ORODHA MPYA ILIYOPO KWENYE TOVUTI HII.

VIJANA WOTE AMBAO HAWAJAPANGWA AWAMU YA KWANZA, WAMEPANGIWA AWAMU YA PILI NA ORODHA YAO ITAWEKWA KWENYE TOVUTI HII MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.
Share:

MAREKEBISHO YA MAJINA VIJANA MUJIBU WA SHERIA KWENDA VIKOSI MBALIMBALI

Share:

Friday, 16 May 2014

BREAKING NEWS:BARCELONA ANNOUNCE MESSI AGREEMENTS

Barcelona announce Messi agreement 
The Camp Nou side have confirmed that the Argentine attacker is set to sign a new and improved deal in the upcoming days

Bet

Barcelona have announced that they have reached an agreement with Lionel Messi over a new and improved contract.

The Catalan club had been in talks with the Argentina international over a renewal for a number of weeks and the forward has now agreed to a new deal worth around €20 million net per season which will make him the highest-paid player in the world.

"FC Barcelona has reached an agreement to adjust the terms in the contract binding Leo Messi to the club as a professional first team player," a short statement said on Friday.

"The revised and updated contract will be signed over the next few days."

The new deal marks a happy ending to a difficult season for Messi, who has missed large chunks of the current campaign through injury and also faced a court case for tax evasion late last year.

The Argentine, who has hit 354 goals in 424 appearances since making his debut for Barca at the age of 17 in 2004, signed improved terms in February last year to earn around €12.5m annually but later saw that deal eclipsed by Cristiano Ronaldo's new contract at Real Madrid.

"It should give peace of mind to him and especially to the club, who can continue to count on the best player in the world," coach Gerardo Martino said on Friday."

Martino is set to leave the Catalan club this summer and will be replaced by Luis Enrique, who is keen to make Messi the cornerstone of his new sporting project at Camp Nou next season.
Share:

HOTUBA YA BAJETI YA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA DKT ASHA-ROSE MIGIRO KWA MWAKA 2014/2015



images_3b1a7.jpg
HOTUBA YA WAZIRI WA KATIBA
NA SHERIA MHESHIMIWA ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO
NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA
MWAKA 2014/2015

A.    UTANGULIZI

1.    Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo ndani ya Bunge lako tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2014/2015.
Read more...
Share:

WEREMA ALIKOROGA, alinywa: Atoa kauli ya kuwabagua Wazanzibari


weremapx_89c87.jpg
Dodoma. Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema 'amelikoroga na kulinywa mwenyewe', baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka.
Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama bungeni na kuwaangukia akiwaomba radhi waliokerwa na kauli yake na pia kuliomba radhi Bunge, Spika wake, Anne Makinda na wananchi.
Kuondoka kwa wabunge hao kulitokana na mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mbarouk Mohamed kutokana na majibu Jaji Werema kwa mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa aliyekuwa ameomba ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya kupitisha vifungu vya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2014/15.
Mnyaa alisema Wizara ya Katiba na Sheria ni muhimu lakini imekuwa ndiyo ya kwanza kuvunja sheria na haki za binadamu na akataka ufafanuzi.
Hata hivyo, aliposimama kujibu swali hilo, Jaji Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na siyo katika Bunge la Jamhuri kwa kuwa si kila kitu kitaulizwa ndani ya Bunge hilo.
"Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu," alisema Werema.
Mara baada ya Bunge kurejea, Mbarouk aliomba mwongozo wa Spika akitaka ufafanuzi wa kauli hiyo kwamba ilikuwa ya kibaguzi.
"Mheshimiwa Spika, huu ni ubaguzi na haupaswi kufanywa na mtu msomi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali," alisema Mbarouk.
Alisema ubaguzi huo umewabagua wabunge ambao wamekula kiapo cha kulitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano na unaonyesha namna ambavyo Wazanzibari wanabaguliwa.
"Mheshimiwa Spika, yanapofanyika mambo kama hayo na wewe mwenyewe uko hapa unaona ni sawa na kubariki jambo hilo, huu ni ubaguzi unaoufanya wewe kwa kuwa lilifanyika ukiona bila hata ya kukemea," alisema Mbarouk.
Hata hivyo, Spika alipinga na kusema: "Hakuna mwongozo wowote kwa kuwa hata wewe umevunja sheria kwani hata nilipokuambia kaa chini umeendelea kuzungumza, tunaendelea.... Katibu (akimtaka Katibu wa Bunge kutoa mwelekeo wa shughuli iliyokuwa inafuata ambayo ilikuwa Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)."
Baada ya kauli ya Spika, wabunge wa Zanzibar walihamasishana na kuamua kutoka nje kwa wakati mmoja na huku wenzao wa upinzani wakiendelea kutafakari cha kufanya. Wakati huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alikuwa akisoma hotuba yake.
Muda mfupi baadaye, wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi nao walitoka na katika viti vya upinzani, alibaki John Cheyo wa UDP peke yake.
Baada ya kutoka
Akizungumza nje ya Viwanja vya Bunge, Mbarouk alisema wametoka kwa sababu Spika na Jaji Werema wamewadharau. "Hatutarejea ndani ya Bunge hadi hapo watakapotuomba radhi, wasipotuomba radhi hatutarejea bungeni," alisema Mbarouk.
Hata hivyo, wakiwa nje ya Ukumbi wa Bunge, mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed aliwafuata na kuwaeleza kuwa amezungumza na Werema na amekubali kuomba radhi kwa wabunge na Watanzania.
"Ndugu zangu nimeongea na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amekubali kuomba radhi," alisema Hamad Rashid jambo ambalo liliungwa mkono na wabunge wa CUF waliokuwa wamekaa katika makundi katika Viwanja vya Bunge.
Hata hivyo, wabunge hao baada ya muda wa dakika 15, walikwenda katika kikao cha dharura kwenye Ukumbi wa Kambi ya Upinzani ambako pamoja na mambo mengine, walijadiliana kusudio la kumuona Spika Makinda kumweleza mambo yasiyowaridhisha.
Werema aomba radhi
Muda mfupi kabla ya Bunge kuahirishwa, Jaji Werema alisimama na kusema: "Kwa imani yangu, ninaamini kila binadamu ana nyongo, isipokuwa watu wawili... Yesu Kristo na Mtume Muhammad (SAW), ndiyo pekee ambao hawakuwa na nyongo. Naomba maneno yangu yafutwe katika kumbukumbu za Bunge hili.
"Mimi ni Jaji kwa taaluma na kwa nafasi yangu nimekosea kwa kutoa maneno hayo. Nimetambua kosa langu na naomba radhi... kwanza kwako Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rajab Mbarouk, Mheshimiwa Injinia Habib Mnyaa, Bunge hili na Watanzania kwa jumla."
KULIKOROGA
"Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu."
KULINYWA
"Mimi ni Jaji kwa taaluma na kwa nafasi yangu nimekosea kwa kutoa maneno hayo. Nimetambua kosa langu na naomba radhi... kwanza kwako Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rajab Mbarouk, Mheshimiwa Injinia Habib Mnyaa, Bunge hili na Watanzania kwa jumla.(E.L)
Share:

NECTA YABADILISHA MFUMO WA VIWANGO VYA UFAULU FORM 6,DIV 1 3-7


NECTA imetoa mwongozo wa matumizi ya viwango vya Ufaulu (Aprili 2014) ambao umesambwazwa katika shule zote ze sekondari kupitia kwa Maafisa Elimu wa Mikoa. Kwa mujibu wa mwongozo huo Madaraja ya ufaulu kwa Kidato cha Sita 2014 yatapangwa kwa kutumia mfumo uliooneshwa kwenye ukurasa wa 8 wa mwongozo huo ambao ni:
Div I pointi 3-7
Div II pointi 8-9
Div III Pointi 10-13
Div IV awe na D mbili au C moja
Div 0 aliyepata chini ya D mbili.

Kwa mujibu wa mwongozo huo masomo yatakayohesabika kwenye kupanga pointi ni yale tu yaliyoko kwenye tahasusi yaani combination. Kwa maneno mengine suala la kupata cheti kwa mgongo wa Bible Knowledge au Islamic Knowledge litakuwa halipo tena.

Kuanzia Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Tano Sita 2015 mfumo wa GPA utatumia. Kwa maelezo Zaidi soma kurasa wa 8 na 9 na pia unaweza kukipata kijitabu hicho toka shule yoyote ya sekondari au kwenye ofisi za elimu za mkoa na wilaya.
Share:

Leo ni birthday ya mwigizaji Vicenti Kigosi ray, Johari ampa salamu tata, isome hapa


Leo mwigizaji maarufu nchini Vicent kigosi - Ray anasherehehea siku yake ya kuzaliwa huku akipata salamu mbalimbali za pongezi toka kwa mastaa mbalimbali nchini.
Moja ya watu wa kwanza kwanza kumpa salamu hiyo ni swahiba na rafiki yake mkubwa, JB akifuatiwa na mpenzi wake wa zamani Johari ambaye salamu yake inadaiwa na wachunguzi wa mambo kuwa ni kwa namna flani inamponda mpenzi wa sasa wa Ray , Chuchu hans, kutokana na maneno yaliyotumika ya salamu hiyo ambayo Johari anadaiwa kuwahi kuyatumia kumponda Chuchu siku za nyuma.
JB ameandika
''Happy birth day mdogo wangu ray.mungu akupe haja ya moyo wako.''
Na huku Johari akiandika 
''Happy birthday director wa rj na swaiba wangu mungu akuongoze akupe maisha marefu na akuepushe na ‘’mabarazuri’’
Hongera sana kaka kigosi. Mungu akupe maisha marefu
Share:

VIDEO:ANGALIA VIGODORO"MAMBO YA PWANI"


Share:

SOMA HATUA SITA ZA KUMFANYA MTOTO WAKO AWE INTELLIGENT AKIWA TUMBONI



                                                      
                                 



Wazazi wengi siku zote  wanataka mtoto wao kukua na na kuwa ubora akiwa mkubwa;hii ni fahari kwa wazazi wengi kuona mtoto wao ni mwenye akili darasani na maishani.
Kumfanya mtoto wako awe mwenye akili nyingi huanza tumboni mwako.
hatua ya 1Hakikisha unakula matunda na mboga za majani mara nyingi hii imethibitika kitaalamu kwamba hu,jenga mtoto aliepo tumboni kuwa na uwezo mkubwa kufikiri.


hatua ya 2Mara zote mama mwenye ujauzito huwa na hasira na msongo wa mawazo sana,hakikisha unapunguza vyote hivi.


hatua ya 3

Hakikisha unasikiliza muziki classical. nunua earphones maalum kwa mahali ya tumbo yako. Kucheza muziki kama wewe kwenda juu ya shughuli za kila siku inaweza kusaidia kujenga madaraja neural katika ubongo wa mtoto wako , kwa mujibu wa BBC.

hatua ya 4Hakikisha unatumia mafuta ya samaki ambayo yana virutubisha vya omega 3-fatty acid ambayo husaidia kimarisha ubongo wa mtoto wako awapo tumboni. 

hatua ya 5
                                      Kuepuka madawa ya kulevya, pombe na uchafu mwingine,hii imethibitika kuharibu ubongo wa mtoto. 
hatua ya 6
                                                    
Kubeba mtoto wako full mrefu. Sayansi Daily ripoti kwamba watoto waliozaliwa mapema hawana ngazi moja ya maendeleo ya ubongo kama watoto waliozaliwa full mrefu. Ingawa mtoto kinaendelea kuja wakati yeye ni tayari , unaweza kuchukua huduma ili kuepuka hali ambayo inaweza kuweka wewe katika kazi mapema .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger