Friday 2 May 2014

CHID BENZ NA USTAA PORI

NI bwana mdogo, lakini ana mwili mkakamavu wenye kumuonyesha kama kijana mwenye ubavu. Ana sauti nzuri ya kukwaruza akiwa nyuma ya Mic, ambayo kwa mashabiki wa Hip Hop za Kimarekani, wanaweza kumlinganisha na rapa Ja Rule!
Namzungumzia Rashid Makwiro, maarufu kama Chid Benz, mtoto wa Ilala Maflet, aliyeingia katika anga la Bongo Fleva miaka michache iliyopita na kuteka mashabiki wengi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kurap.
Uwezo wake unadhihirishwa na jinsi alivyoweza kushirikishwa na wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya katika nyimbo zao. Unapowataja wasanii waliofanya kolabo nyingi, ni jambo gumu kumtupa nje ya Top Ten Chid Benz.
Anajua kuitumia sauti yake au kama wenyewe watu wa muziki wanavyosema, ‘ananata na beat’. Msikilize kwa mfano katika wimbo wa Mwasiti uitwao Hao au sikia kibao cha Tunda Man kiitwacho Neira. Kuonyesha anajua, amepiga hadi taarabu akiwa na Mzee Yussuf katika wimbo wa Mashalaah Raha za Dunia na Nampenda sana aliofanya na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa.
Licha ya hizo za kushirikishwa, dogo pia amekamua mwenyewe katika nyimbo za kutosha kama Nakaza Roho, Kila Nnapokuona, Nipokee aliomshirikisha Ben Paul, Get Down (Nonini), Viini vya Macho (Solo Thang), Nimerudi (Dully), Dar Stand Up, Niaje na nyinginezo kibao.
Kifupi, Chid Benzi ni mmoja kati ya vijana wenye vipaji ambao taifa limewahi kuwapata. Katika nchi ambayo wasanii wangepata stahiki zao kiasi wanavyostahili, bila kuibiwa na wajanja wachache wanaolegezewa na serikali, huyu angekuwa mmoja wa mamilionea wakubwa kwa sasa.
Lakini nyuma ya sifa hizi, Chid ana tabia ya utukutu, tena ule wa kizamani, wa kupenda kupiganapigana ovyo na wenzake. Nilianza kumsikia mapema tu alipojiingiza katika Bongo Fleva akiwa bado hana jina kubwa, zilipotapakaa habari kwamba alimpiga Prof Jay.
Zilikuwa ni shutuma za kushtusha mno, ingawa siku moja nilipokutana nao wote wawili kwenye tukio moja la kisanaa pale JB Belmont jijini Dar, Chid alikataa kumpiga Jay na hata Jay alikataa kuwahi kupigana naye.
Najua walikwaruzana, lakini Prof alitumia utu uzima na busara kutolikuza jambo hilo.
Baada ya pale, mchizi ameendelea kuwa na matukio mengi yanayomhusisha na kupigana hadi mtu unapatwa na mshangao, kama kijana wa kisasa, aliyezaliwa, kukulia na kusomea Dar es Salaam, anaweza kuwa na mambo ya kizamani kama haya ya kupigana ngumi.
Juzikati aliripotiwa kupigana Maisha Club kama ilivyotokea siku kadhaa nyuma, alipodaiwa kutaka kupigana na msanii mwenzake Club Billicanas.
Lakini mbaya zaidi ni tukio lake la hivi karibuni, analodaiwa kumpiga na kumjeruhi vibaya msichana anayedaiwa kuwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.
Kwanza, kijana wa kiume, mwenye umbo kakamavu kama la Chid, ni kujidhalilisha kumpiga msichana. Halafu, staa wa levo zake, ni vipi umdunde mwanamke hadharani kama wafanyavyo watemi wanaovuta bangi?
Nimshauri tu mdogo wangu Chid, naona kama umaarufu unamlevya. Katika dunia ya sasa, kupigana ngumi nje ya ulingo ni ushamba.
Watu hawapigani vibao usoni, wanapigana kujikomboa kimaisha, ili kesho maisha yawe rahisi kuliko jana.
Kuna wasanii wamekuwa maarufu tangu yeye anasoma, lakini hawajawahi kuripotiwa kuwa na upuuzi kama huu na bado hawafikii kimuziki wala kimaisha.
Enzi za ubabe wa kupandisha bega juu na kudunda kwa mikogo zilishapotea na haziwezi kurudi tena.
Share:

MSANII HUYU KUTOKA KENYA AAMUA KUACHIA PICHA AKIWA UCHI, ICHEKI PICHA HIYO HAPA


Victoria-Kimani

Mwimbaji wa Kenya Victoria Kimani ameamua kuweka picha yake ya uchi akiwa  ufukweni akiogelea.picha hipo hapo chini

Kuangalia picha shariti uwe na umri +18 





Share:

FOOD SCIENCE AND TECHNOLOGY SCHORALSHIP 2014/2015

: International financial aid and grants are offered for those students who are pursuing career in food science. Food science is the applied ...ANGALIA ZAIDI HAPA
Share:

MAURITIUS - AFRICA SCHOLARSHIPS 2014



The Government of the Republic of Mauritius is offering scholarships for undergraduate studies in public tertiary education institutions in Mauritius.

Applications are invited from qualified Tanzanians to apply for undergraduate programs tenable in the Republic of Mauritius for 2014/2015 academic year in the following areas of specializations:-
  • Medicine,
  • Engineering,
  • Science and Technology,
  • Oil and Gas,
  • Agriculture,
  • Telecommunications  and,
  • Geology.
1. Financial conditions of the scholarship
1.1. The scholarship will cover:-
a)  A monthly living allowances of Rs 8,300 (USD 266 approx.)
b)  Tuition fees up to Rs 100,000 (USD 3205 approx.) yearly, and
c)  Airfare (economy class) by the most economical route to and from Mauritius at the start and the end of the studies.

1.2.  
The duration of the scholarship will be for a maximum of four (4) years depending on the course duration.

2.  Eligibility
2.1  Students must have:-
(a)  Passed 3 principals at Advanced Certificate of Secondary Education or at an equivalent level acceptable to the scholarship panel;

(b)  Secured an Admission letter from  a fully accredited and on campus undergraduate programme on a full- time basis from one of the following public institutions in Mauritius:-

Institution                                                           Website

(i)  University of Mauritius                                 www.uom.ac.mu
(ii) University of Technology, Mauritius               www.utm.ac.mu
(iii) Universities des Mascareignes                      www.udm.ac.mu
(iv) Open university                                          www.open.ac.mu
(v) Fashion and Design Institute                         www.fdi.mu
(vi) Mauritius Institute of education                    www.mie.ac.mu
(vii) Mahatma Gandhi Institute                           wwww.mgirti.ac.mu
(viii)Rabindranath Tagore Institute                     www.mgirti.ac.mu

2.2 Candidates should be resident citizens of the United Republic of Tanzania.

2.3 Scholarships shall not be awarded for:

(a) Top –up degree programmes;

(b) Foundation programmes; and

(c) Mixed modes (distance and non-campus undergraduate programme on a full time basis at a Public Tertiary education institution).

2.4 Age Limit
    Candidates should not be more than 25 years of age at the date of application.

3. Procedures for Submitting Applications
3.1  Candidate should submit their  application forms and a copy of the following documents;-
(a)   Birth certificate
(b)   Certified  copies of certificates, of Secondary  School results (“O” and  “A” level;
(c)     Mark sheets relating to their qualifications;
(d)  Letter of conditional offer/admission by a public tertiary education institution in Mauritius.

Note: Non- submission of one of these documents will result in the elimination from the award of the scholarship

3.2  Candidate should indicate in their application the name of the institution, the title and the course code of the programme to which they have been admitted.

3.3 All applications should include a medical report and an AIDS-free certificate before the scholarship is approved.

4. Other conditions

4.1  Self-financing candidates already studying in Mauritius in an  undergraduate programme before  July  2014  will not  be converted into  studentship.

4.2 The scholarship holders would be required to sign an undertaking to return to their home country as soon as the studentship comes to an end.

4.3  The candidate, once selected, should:-

(a) Be available to commence their   academic studies in Mauritius by the start of the academic  year of the respective institution where they have been admitted;
(b) Be attending full time and on-campus (not distance learning) programme;
(c) Not   be in receipt of a full fee studentship from any other source; and
(d) Be able to pay any outstanding costs not covered by the scholarship.

5.   Important  Information
5.1  Candidates must submit their application through the Ministry of Education and Vocational Training after securing admission in a Public Tertiary Education Institution in Mauritius at the following address.

Permanent Secretary, 
Ministry of Education and Vocational Training,
P.O.BOX 9121,
DAR ES SALAAM

5.2   Deadline for submission is 14th June 2014.
Share:

Thursday 1 May 2014

TUCTA "KIMA CHA CHINI CHA MFANYAKAZI KIWE 750,000"

Wakati Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kuhutubia wafanyakazi katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), limeitaka Serikali kupandisha kima cha chini hadi kufikia Sh750,000.

Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya alisema jana kuwa wanahitaji kuona wafanyakazi wakipata kiwango cha mshahara kinachokidhi mahitaji.

Alisema kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi na mfumuko mkubwa wa bei uliopo kwa sasa, kiwango hicho angalau kinaweza kukidhi mahitaji muhimu ya wafanyakazi wa kima cha chini, ikiwamo malazi, mavazi, chakula na mahitaji ya afya.

“Katika hali halisi, tunaona namna bei za vitu muhimu ikiwamo umeme, maji, mafuta, gharama za vifaa vya ujenzi, nyumba vyakula na gharama nyingine za maisha zimekuwa zikipanda maradufu katika miaka ya karibuni, lakini hakuna namna inayofanyika kuleta unafuu kwa wafanyakazi.

Kimsingi kima cha chini lazima kiongezwe ili kikidhi mahitaji ya maisha ya wakati huu,” alisema.
Share:

WAKUBWA TU!!. VIDEO YA KINA MAMA WACHEZA UCHI KAMA WALIVYO ZALIWA BAADA YA KUVURUGWA NA POMBEEE


tazama video hapa chini
Share:

RAYUU "NATAFUTA MWANAUME WA KUNIOA NA KUNIWEKA NDANI"

Staa katika tasnia ya filamu Alice Bagenzi "Rayuu" amefunguka na kusema amechoka maisha ya kuishi kiupweke hivyo anatafuta mwanaume wa kumuoa ili naye awe katika ndoa na aachane na maisha ya ukapera maana kwa sasa yanamuelemea na kila aonapo watu walio olewa jinsi wanavyoishi na wanaume zao basi na yeye anatamani sana maisha hayo.

Akifunguka Rayuu alisema "natafuta mwanaume wa kuniweka ndani ambaye atakuwa mkweli atanipenda kwani nimechoka maisha ya kisela nataka niwe mke halali wa mtu tena mwanaume atakayekuja kwangu nitampenda sana"
Pia aliongezea kwa kusema "mimi ni binti mzuri tena bado mdogo hivyo maisha ya kurukaruka nimechoka"
Share:

BREAKING NEWS:Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi YATANGAZA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015,SASA WENYE DIVISION FOUR YA 32 HADI 34 RUKSA KUAPPLY



Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatangaza nafazi za Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Cheti kwa Mwaka wa Masomo 2014/2015.

Kuzidownload bofya link hizo hapo chini, ya kwanza ngazi ya cheti (Certificate Grade A) na ya pili ni stashahada (Diploma).











TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 UTANGULIZI



Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa, wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni wale wenye ufaulu mzuri katika mtihani ya kidato cha NNE. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa alama 26 au 27 (mwaka 2004 hadi 2012) na alama 32 hadi 34 (mwaka 2013) watadahiliwa katika programu ya mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.


Aidha, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya ualimu na kufaulu mafunzo yao watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za Serikali.



VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/2015.

1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’: MUDA MIAKA 2
  1. Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, Kitangali, Mandaka , Murutunguru , Ndala , na Tarime
  2. Cheti Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya Kabanga, Kinampanda, Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
  3. Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala na Mtwara (U)
Mwombaji awe:
Mhitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye ufaulu wa kiwango kisichopungua Daraja la III katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.

2: MAFUNZO KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI:- MUDA MWAKA 1
Mafunzo katika vyuo vya ualimu Bustani, Kinampanda, Mhonda, Mpuguso, Mtwara (U), Nachingwea, Singachini, Tandala, Katoke na Sumbawanga
Mwombaji awe:
  1. Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na awe amefaulu kwa kiwango kisichopungua Daraja la IV kwa alama 26 au 27 (kwa mtihani wa mwaka 2004 hadi 2012) na alama 32 hadi 34 (mtihani wa mwaka 2013) kwa mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
  2. Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Watakaofaulu mtihani wa mafunzo kabilishi wataendelea na mwaka wa pili wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti Daraja A

3: ELIMU MAALUM: MIAKA 2 katika chuo cha ualimu Patandi:-
Mwombaji awe:
  1. Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  2. Mwenye ufaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi:Walimu wanaofundisha Elimu Maalum hata kama hawana mafunzo maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho uambatishwe).

MAELEZO MUHIMU
  1. Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
  2. Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
  3. Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ kwenye ‘Selforms’ wakati wanamaliza Elimu ya Sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;
  4. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
  5. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz);
  6. Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
  7. Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya ualimu watume maombi yao kwa njia ya Barua ikionyesha anuani kamili ya mwombaji pamoja na viambatisho vifuatavyo:
  • Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV;
  • Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti (kwa waombaji walioajiriwa); na
  • Barua zilizopitishwa na waajiri (kwa waombaji walioajiriwa).
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30 MEI 2014.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)




TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI
Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa, wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni wale wenye ufaulu mzuri katika mitihani ya kidato cha NNE na SITA. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu tu.



Aidha, kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati wa takribani walimu 26,000, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuziba pengo hili. Nia ya Serikali ni kuwavutia wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi na Hisabati. Kuanzia mwaka huu wa masomo 2014/2015, wanafunzi watakaojiunga na fani ya Ualimu kwa masomo ya Sayansi na Hisabati watagharimiwa na Serikali kupitia mfumo wa ruzuku na mkopo. Wanafunzi watakaokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza watapatiwa Ruzuku na wale wenye Daraja la Pili na la Tatu watapewa mkopo ili kuwasaidia katika masomo yao. Watakaofaulu mafunzo ya ualimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za serikali.

VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/2015.
1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MASOMO YA SAYANSI, HISABATI NA UFUNDI: MUDA MIAKA 2



  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Klerruu na MonduliMwombaji awe amehitimu: Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa ‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi na Hisabati.
  2. Ualimu wa ufundi katika chuo cha ualimu Klerruu. Mwombaji awe amehitimu:



a.Mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2004 na 2010 kutoka Vyuo vya Ufundi, Au
b. Mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA Level 6 au sifa linganishi (equivalent qualification) kati ya mwaka 2007 na 2013 kutoka chuo chochote cha Ufundi kinachotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
(iii) Ualimu wa Kilimo katika chuo cha ualimu Monduli
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu ‘Principal Pass’ mbili katika somo la ‘Agricultural Science’ na ‘Biology’, ‘Chemistry’ au ‘Food and Nutrition’.

2: MAFUNZO MAALUM YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA KWA KIDATO CHA NNE MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA ENGLISH: MUDA MIAKA 3
Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati na English katika vyuo vya Butimba, Morogoro, Korogwe, Songea na Mpwapwa
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu, na Credit mbili (yaani A, B+, B au C) katika masomo ya Sayansi, Hisabati na English.

3: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MUDA MIAKA 2
  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango cha ‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi Jamii.
  2. Biashara katika vyuo vya Shinyanga na Kasulu. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Biashara.
  3. Sanaa za Ufundi, Sanaa za Maonyesho, Muziki na Michezo katika chuo cha Butimba. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja



Tanbihi: Masomo ya ‘Economics’, Basic Applied Mathematics’, ‘General Studies’, ‘Divinity’ na ‘Islamic Knowledge’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji.

4: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 3
Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
Tanbihi: Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya ‘Mathematics’, ‘Biology’, ‘Physics’, ‘Chemistry’, ‘Agriculture’, ‘Food and Nutrition’, ‘English’ na Kiswahili na wahitimu wenye mahitaji maalumu.

5. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA (SEKONDARI): MUDA MIAKA 2
  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Klerruu na Monduli.Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi na Hisabati; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  2. Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa, Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu. Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi Jamii; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  3. Ualimu wa masomo ya Biashara katika vyuo vya Shinyanga, Kasulu. Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass” moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Biashara; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  4. Ualimu wa masomo ya Elimu Maalumu katika chuo cha Patandi. Mwombaji awe: Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi ya ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili, Au Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.



Tanbihi: Walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum kama wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili, n.k. ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).

6: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 2:

Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.

MAELEZO MUHIMU
  1. Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
  2. Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
  3. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
  4. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)
  5. Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
  6. Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu;



VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya ualimu watume maombi yao kwa njia ya Barua ikionyesha anuani kamili ya mwombaji pamoja na viambatisho vifuatavyo:



  • Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV, VI na Ufundi;
  • Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada (kwa waombaji walioajiriwa); na
  • Barua zilizopitishwa na waajiri (kwa waombaji walioajiriwa).



MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30 MEI 2014.

Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
Share:

KIKWETE ALIVYOSHEREHEKEA MEI DEI JIJINI DAR

Rais Jakaya Kikwete akihutubia wafanyakazi katika Uwanja wa Uhuru, Dar leo wakati wa kilele cha Siku kuu ya Wafanyakazi Duniani, Mei Dei iliyofanyika kitaifa.
Brass Bend ikipita mbele ya Rais Kikwete wakati wa maandamano ya wafanyakazi.
…wafanyakazi wa mali asili wakipita mbele ya Rais Kikwete.
… wafanyakazi wakipitia mbele ya Rais Kikwete na vitendea kazi vyao.
Rais Kikwete akiwa ameshikana mikono na viongozi wa wafanyakazi kuonesha mshikamano.
…hapa anatoa zawadi kwa mmoja wa wafanyakazi bora.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadiki akihutubia kabla hajamkaribisha Rais Kikwete.
Wachezaji wa Azam FC wakipita mbele ya Rais Kikwete na kombe lao la ubingwa walionyakua mwaka kuu katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Msichana huyu alikuwa kivutio kwa danadana zake alizocheza uwanjani hapo mbele ya Rais Kikwete.
Baadhi ya umati uliohudhuria sherehe hizo Uwanja wa  Uhuru wakifuatilia sherehe hizo.
Share:

HUYU NDIYE SNURA MAMA WA MAJANGA , JIONEE PICHA ZAKE ZA UTATA AKIWA JUKWAANI..!!NI SHIDAAA

 Naamini kwapicha hizi uwezi kosa show yake jumapili hi EW MAISHA CLUB atazindua video yake ya majanga kuwa mjanja kuwa wa kwanza kuiona, atasindikizwa na WEMA SEPETU atakata utepe wa video ya majanga,MIRROR,SAMIR,ALI NIPISHE,TIMBULO,BAUCHA,MENINAH, na MADEE kiingilio 10,000 tu hii show sio yakukosa kabisa.
 


Share:

HUYU NDIYE MREMBO WA OMMY DIMPOZ...TAZAMA PICHA YAKE HAPA


ommy dimpozMastaa wa muziki wa Marekani wanafahamika kwa desturi yao kuwatambulisha wapenzi wao hadharani na kwenda nao kwenye matukio mbalimbali. Tanzania ni tofauti hata hivyo. Ni mastaa wachache wenye ujasiri wa kuwaweka hadharani wapenzi wao, mfano mzuri akiwa Diamond Platnumz. Mastaa wengine akiwemo Ommy Dimpoz hawajawahi kuwatambulisha wapenzi wao hadharani labda kama ni tetesi tu. Ommy Dimpoz ameshare picha kwenye Instagram akiwa na mrembo ambaye hata hivyo hajafafanua kama ni mpenzi wake ama rafiki tu.
Share:

Wednesday 30 April 2014

MAJINA AJIRA WIZARA YA KILIMO NA MIFUGO 2014

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
KUITWA KAZINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 04 hadi 30 Machi, 2014 kuwa walioorodheshwa katika tangazo hili wamefaulu usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri kama ilivyoonyeshwa katika tangazo hili. Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vipya vya kazi katika muda ambao umeainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
Barua za kuwapangia vituo vya kazi
zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
Kufungua majina yote BOFYA HAPA
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger