Sunday, 10 November 2024

ZAHA SOAP !! MABINGWA WA SABUNI BORA ASILIA




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 10, 2024













Share:

Saturday, 9 November 2024

VITA YA MADARAKA INAVYOSAMBARATISHA CHADEMA

 


Mgogoro wa uongozi unaoendelea kati ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, na Makamu wake Tundu Lissu, umeleta mtikisiko mkubwa ndani ya chama hicho, ukidhihirisha kushindwa kwao kuonesha umoja au dira ya wazi kwa taifa. Wakati CCM ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya kazi kwa bidii katika kusukuma maendeleo ya nchi, uongozi wa CHADEMA umejikita kwenye malumbano madogo na vita vya ndani, jambo linaloonesha wazi kuwa upinzani huo hauko tayari kuiongoza Tanzania.

Upinzani Usio na Umoja

Kwa miezi kadhaa, mpasuko kati ya Mbowe na Lissu umekuwa ukiongezeka, huku Lissu akimtuhumu Mbowe kwa kumzuia kufanya mikutano ya hadhara na vikao vya ndani vya chama. Mgogoro huu ndani ya CHADEMA unaonesha wazi ukosefu wa umoja ambao ni muhimu kwa chama chochote kinachotamani kuongoza taifa. Badala ya kushirikiana na kuonesha sera ambazo zingeweza kuwafaidisha wananchi, viongozi wa CHADEMA wamejikita kwenye mvutano wa nguvu na ushawishi, bila kujali maslahi ya umma.

Mbowe anadai kuwa hatua zake ni kwa ajili ya kudumisha nidhamu ndani ya CHADEMA, lakini Watanzania wanabaki na maswali ikiwa CHADEMA ina uwezo wa kujiongoza yenyewe, sembuse kuongoza nchi. Mgawanyiko huu wa ndani unadhihirisha ukosefu wa dira ya pamoja na unazidi kudhoofisha uaminifu wa chama hicho mbele ya wananchi, ambao wanaona kwamba kipaumbele cha CHADEMA ni mivutano ya madaraka badala ya kuwahudumia wananchi.

Uongozi Usio na Mwelekeo

Tundu Lissu ameikosoa waziwazi uongozi wa Mbowe, akisema kuwa CHADEMA haina mwelekeo chini ya uongozi wake, na kwamba hatua zake za kuepuka fursa za kuungana na wananchi na kushiriki mijadala ya maana zinadhoofisha chama. Wakati serikali ya Rais Samia imejikita katika kukuza uchumi, maendeleo ya kijamii, na kuimarisha umoja wa kitaifa, uongozi wa CHADEMA umenaswa kwenye malumbano ya ndani, bila kutoa mwelekeo wowote kwa wananchi.

Kadri Lissu na Mbowe wanavyoendelea kuvutana, ukimya wa upinzani unaonesha kwa nini uongozi thabiti na wenye malengo kama wa Rais Samia ndio unaobaki kuwa chaguo sahihi kwa Watanzania. Tofauti na CHADEMA, ambayo viongozi wake wamepotea katika malumbano ya kibinafsi, CCM imeendelea kuzingatia masuala ya msingi ya kitaifa na kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

Chama Kilichoparaganyika

Wakati CCM ikizidi kuimarisha demokrasia na kudumisha utulivu, mgogoro wa ndani wa CHADEMA unaonesha wazi kushindwa kwao kuonesha mbadala wa kweli. Kitendo cha Mbowe kumzuia Lissu kuhutubia umma kinaonesha vipaumbele vya upinzani. Watanzania wanastahili serikali inayothamini maendeleo kuliko vita vya madaraka, serikali inayohudumia badala ya kugawanya.

Hatua za Mbowe za kumnyamazisha Lissu zinaonesha kuwa CHADEMA si chama cha uhuru wa maoni wala ushirikiano wa kweli. Ni chama ambacho hata viongozi wake wanawekewa vizuizi ndani ya safu zao. Wakati CHADEMA wakijigamba kuwa wanapigania demokrasia, viongozi wake wenyewe wanawekewa mipaka. Aidha, serikali ya Rais Samia imeendelea kukuza uhuru wa mijadala, ikizingatia falsafa ya 4R’s ambayo imepanua nafasi ya demokrasia nchini Tanzania.

Uchaguzi Wazi kwa Maendeleo ya Tanzania

Wakati serikali inayoongozwa na CCM ikitimiza ahadi zake kwa wananchi, Watanzania wanaweza kuona kupitia ahadi zisizo na msingi na matarajio yasiyotimizwa ya upinzani. Wakati CHADEMA wakiendelea na vita vya ndani, Rais Samia anajikita katika matokeo halisi – kuboresha maisha ya wananchi, kuimarisha uchumi, na kuunganisha taifa. Tofauti hii inaonesha wazi ni chama kipi kwa kweli kina maslahi ya wananchi moyoni.

Watanzania wanahitaji utulivu, maendeleo, na serikali inayojua inakoelekea. Mgogoro wa uongozi ndani ya CHADEMA unaonesha kuwa upinzani hauko tayari kuleta mambo hayo. Mvutano huu wa ndani unakumbusha kuwa ni CCM pekee inayokuwa na dira, nidhamu, na umoja wa kulipeleka taifa mbele.

Hitimisho

Mgogoro wa uongozi ndani ya CHADEMA, ukiambatana na tuhuma za Freeman Mbowe za kumhujumu Makamu wake Tundu Lissu, umeonesha chama kilichoparaganyika na upungufu mkubwa wa uongozi. Vita hivi vya madaraka vinaonesha kuwa vipaumbele vya viongozi wa CHADEMA ni matamanio binafsi badala ya utumishi kwa umma, hali inayowaacha Watanzania wakijiuliza vipi chama chenye mgawanyiko kama huu kinaweza kuongoza nchi.

Wakati CHADEMA wakikosa umoja, Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wanaendelea kutoa utulivu, umoja, na maendeleo ambayo Watanzania wanayahitaji. Wakati CHADEMA wanapigania madaraka, CCM inapigania mustakabali wa Tanzania. Uchaguzi ni wazi: ni CCM pekee inayokuwa na dira, umoja, na kujituma vinavyohitajika kuisogeza Tanzania katika njia ya amani, ustawi, na maendeleo.
Share:

TAKUKURU YAONGEZA UFANISI KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO KATIKA JIJI LA TANGA

 


Na Oscar Assenga,TANGA


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Tanga katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024 umefanikisha kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato yanayotokana na ada za leseni za biashara.

Hatua hiyo inatokana na ufuatiliaji wa uzingatiaji wa uchukuaji wa leseni za biashara katika sehemu za Biashara mbalimbali katika Halmashauri ya Jiji la Tanga ambapo pia wameongeza ufanisi pia katika ushuru wa nyumba za kulala wageni pamoja na ushuru wa huduma katika Jiji la Tanga.

Hayo yalibainishwa leo na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Ramadhani Ndwatah (Pichani )wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Takukuru kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2024.

Alisema kwamba taasisi hiyo kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga walifanya kazi ya kufika kwenye maeneo ya Maduka,Zahanati, Hospitali,Hotel, Vituo vya Mafuta,Bar,Kumbi za Starehe,Shule,Viwandani na Masoko katika kata zote za Halmashauri ya Jiji hilo.

“Tulifanya ufuatiliaji wa ulipaji wa ushuru wa huduma ,ushuru wa nyumba za kulala wageni (Hotel Levy) pamoja na ukaguzi Leseni za Biashara na tulichobaini ni kwamba asilimia 64.35 ya wafanyabiashara hawakuwa na leseni za biashara na zaidi ya asilimia 90 ya wafanyabiashara hawakuwa wamelipa ushuru wa huduma (Service Levy) pamoja na ushuru wa nyumba za kulala wageni (Hotel Levy).

Akizungumzia hatua walizochukua alisema ni kufanya uelimishaji kwa wadau hao juu ya matakwa ya kisheria juu ya ulipaji wa tozo hizo na madhara yake kwao na kwa Halmashauri na Serikali kwa ujumla iwapo tozo hizo hazitalipwa.

Aidha alisema matokeo na mwitikio wa wadau katika utekelezaji wa hatua hizo ni kwamba katika kipindi cha Julai –Septemba mwaka huu Halmashauri ya Jiji la Tanga iliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 1,938,185,915.22 sawa na wastani wa asilimia 32.6 ya lengo la mwaka katika vyanzo vya ushuru wa huduma (Service Levy),Ushuru wa Nyumba za Kulala wageni (Hotel Levy).

Alisema pia walikusanya katika ada za leseni za Biashara (Business Licence Free) ukilinganishwa na kiasi cha Sh.Bilioni 1,246,611,579.43 sawa na wastani wa asilimia 22.6 ya lengo la mwaka kilichokusanywa katika kipindi cha April hadi June mwaka 2024 katika vyanzo hivyo.

Hata hivyo alisema katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2024 Takukuru mkoa huo imetekeleza jukumu la uzuiaji wa Rushwa,Elimu kwa Umma na Uchunguzi wa Mashtaka mbalimbali.

Share:

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AFANIKISHA MAFUNZO YA UCHAGUZI KWA MABALOZI 227 WA CCM BUKOBA MJINI

 



Mabalozi 227 wa Chama Cha Mapinduzi; CCM, Bukoba Mjini wamenufaika na mafunzo yaliyotolewa katika semina iliyoandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira kuhusu Sheria za Uchaguzi na Vyama Vya Siasa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ushiriki wa Wanawake katika Siasa

Aidha, wakati wa semina hiyo, Cde Issa Haji Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Oganaizesheni aliongea moja kwa moja na mabalozi hao kupitia simu ya Mbunge Lugangira na kujibu hoja zao na kupokea Salaam za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mabalozi wa CCM wa Bukoba Mjini.
Lugangira akitumia simu yake kuwasiliana na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.

Semina hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Shirika la Omuka Hub na FES Tanzania, ilihudhuriwa pia na Shaban Mdoe, Katibu wa CCM Bukoba Mjini na Hadija Mkelenga, Katibu wa UWT Bukoba Mjini ambao pia walitoa mada.


Sehemu ya mabalozi hao.

Mbunge Neema Lugangira akishiriki kutoa mafunzo hayo.
Share:

BONDIA EMMANUEL SHIJA AJIANDAA KWA PAMBANO LA KIHISTORIA DHIDI YA MUSKOTALY BALINT


Bondia Emmanuel Shija (wa pili kushoto)
Emmanuel Shija, bondia maarufu kutoka Tanzania, anajiandaa kwa pambano la kihistoria dhidi ya Muskotaly Balint kutoka Hungary kwa ajili ya taji la dunia la K-1 Rules World Kickboxing Federation (WKF). Pambano hili la Super Middleweight (78.1 kg – 172 lbs) litafanyika Desemba 21, 2024, katika mji wa Dunaujvaros, Hungary, na linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


ALC Group, kampuni inayomiliki na kusambaza bidhaa za vilainishi kama Flying Horse Lubricants na Toboa, imemsaidia Emmanuel Shija kwa kumdhamini katika maandalizi ya pambano hili la kimataifa. Kwa msaada wa ALC Group, Shija anapata vifaa bora na mazingira ya kisasa ya mazoezi, ambayo yatamuwezesha kujiandaa kwa kiwango cha juu kabla ya pambano lake la Desemba.

Pambano hili ni muhimu sana kwa Shija na kwa Tanzania kwa ujumla. Ushindi wa Shija utaleta heshima kubwa kwa taifa letu na kuonyesha uwezo wa wanamichezo wa Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa. Shija amekuwa na mafanikio makubwa katika mashindano ya kimataifa, na sasa anapigania taji la dunia – hatua ambayo itamuweka kwenye historia ya kickboxing duniani.

Kwa msaada wa ALC Group, na bidhaa zake za Flying Horse na Toboa, Emmanuel Shija anapata vifaa na mazingira bora ya mazoezi ambayo yatamuwezesha kujiandaa kwa kiwango cha juu. Pambano hili lina nafasi ya kuwa hatua muhimu ya kuonyesha uwezo wa wanamichezo wa Tanzania duniani, na mashabiki wa Tanzania wanatarajia kuona bondia wao akifanya vyema na kuleta mafanikio makubwa.

Kwa ujumla, ni fursa ya kipekee kwa Emmanuel Shija na michezo ya Tanzania kuonesha uwezo wake kwenye jukwaa la kimataifa, na ALC Group inajivunia kuwa sehemu ya mafanikio haya


Share:

Friday, 8 November 2024

WAANDISHI WA HABARI REDIO ZA MWANZA, KAGERA, GEITA NA MARA WAPATIWA MAFUNZO YA M - MAMA

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.  Jesca Lebba akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa semina ya waandishi wa habari wa radio Kanda ya ziwa

Na Mbuke Shilagi Mwanza.

Waandishi wa Habari wa Radio Kanda ya Ziwa wamepatiwa semina ya mfumo wa M-mama ambapo wametakiwa kuelimisha jamii kuhusu mfumo wa M-mama na matumizi sahihi ya namba 115 pindi mama mjamzito, aliyejifungua ndani ya siku 42 pamoja na mtoto mchanga ndani ya siku 28 atakapoona dalili za hatari katika mwili wake atoe taarifa mapema kupitia namba hiyo.

Akizungumza mapema leo Novemba 8, 2024 mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba jijini Mwanza uliohudhuriwa na waandishi wa habari wa Radio kutoka Kagera, Geita,  Mwanza na Mara pamoja na wadau wa Afya amesema kuwa kupitia mfumo wa M-mama tangu umezinduliwa tayari rufaa elfu 98 zimepokelewa ambapo akina mama walikuwa elfu 78 na watoto wachanga elfu 19 wamenufaika kupitia mfumo huo.

"Kama tunavyojua kuwa M-mama ni huduma ya usafiri wa dharura wa kumfikia mama mjamzito, mama aliyejifungua ndani ya siku 42 pamoja na mtoto mchanga ndani ya siku 28 pindi wanapopatwa na dalili za hatari ndani ya jamii au hata katika vituo vya afya ikiwa lengo ni kuondoa au kupunguza kabisa vifo vya mama na mtoto", amesema Dkt.  Jesca.

Aidha amesema kuwa katika mfumo wa M-mama walengwa ni mama mjawazito, mama aliyejifungua mpaka siku 42, mtoto mchanga mpaka siku 28, pamoja na jamii kwa ujumla ikiwa lengo kuu ni kuokoa maisha ya mama na mtoto pamoja na kumuwaishia huduma za kiafya mlengwa huyo.
 
"Serikali ililiona hilo na kuleta mfumo huu wa M-mama ili kusaidia au kuepusha sababu ya pili ya miundombinu na usafiri ili basi kumuwezesha mlengwa kufika kwa wakati katika kituo cha afya na kupatiwa matibabu",

"Naomba tuendelee kuelimisha jamii kupitia mfumo huu kutumika ipasavyo na ninaomba nisisitize mfumo huu kutumika vizuri na wamama wajawazito waache kutumia dawa za kienyeji badala yake wahi katika kituo cha afya na hapo utaokoa mtoto aliye tumboni na maisha yako pia", amesema Dkt. Jesca.













Share:

WALENGWA WA TASAF SHINYANGA WAPONGEZA MRADI WA BARABARA YA TANESCO - SANJO, WAPATA FAIDA ZA KIUCHUMI NA HUDUMA BORA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Walengwa wa Mpango Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wameeleza kupata manufaa makubwa kutokana na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mashema (Mtaa wa TANESCO) katika kata ya Chamaguha.

Mradi huu, uliofadhiliwa na TASAF kupitia ajira za muda mfupi, umeweza kufungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mtaa huo kwa kuwapa malipo kwa kazi walizofanya, huku baadhi yao wakijiongezea mapato kupitia shughuli za kilimo na biashara.

Barabara hii yenye urefu wa kilomita 2 inayoanzia Mtaa wa TANESCO na kuunganisha mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha imesaidia kupunguza usumbufu wa usafiri ambao awali ulilazimu wakazi kutafuta njia ndefu.

Katika mahojiano na waandishi wa habari Novemba 8, 2024, walengwa wa TASAF wamesema, ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2 umewezesha wakazi wa mtaa wa TANESCO na Sanjo kuepuka umbali mrefu wa kupita maeneo mengine, jambo ambalo lilikuwa linawaathiri hasa kwa upande wa usafiri.
Martha Daniel Chacha, mmoja wa wakazi wa mtaa huo, amesema kuwa kabla ya mradi, eneo hilo lilikuwa na majaruba, lakini sasa ni rahisi kufika kwenye huduma muhimu kama zahanati ya Chamaguha hivyo imewezesha wakazi kuepuka vikwazo vya usafiri.

Aidha walengwa wameeleza furaha yao kwa kupata malipo mazuri ya kazi walizofanya na wameomba miradi mingine kama hiyo iendelee ili kuboresha hali ya maisha yao zaidi.
Tabu Buganga Malaba 

"Ufuatiliaji wa mradi ulikuwa mzuri, tulilipwa kwa wakati. Tunashukuru TASAF kwa kuturahisishia maisha yetu, tunaomba mradi mwingine uje ili tuendelee kunufaika," amesema Tabu Buganga Malaba na Gigwa Masingija, miongoni wa walengwa.

Fundi Msimamizi wa Ujenzi wa Mradi huo, Paul Ramadhani, pia amepongeza usimamizi mzuri wa mradi, na kusema kwamba ufanisi ulioonekana unatoa picha nzuri kwa miradi ya baadaye.

Mwenyekiti Mstaafu wa Mtaa huo Suleiman Mzee, ameiomba serikali iendelee kutekeleza miradi mingine ya barabara kwani mahitaji bado yapo.
Octavina Kiwone

Kwa upande wake, Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Octavina Kiwone, amesema kuwa barabara hiyo imejenga daraja la kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa Chamaguha na kuunganisha jamii na huduma muhimu.

Afisa Mtendaji wa Mtaa wa TANESCO, Bundala Shija, amefafanua kuwa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mashema, wenye urefu wa mita 2,000, ulianza kutekelezwa tarehe 7 Desemba 2022 na kukamilika kwa asilimia 100 tarehe 12 Mei 2023.

Mradi huu uligharimu jumla ya shilingi 13,860,500/- kwa ajili ya kuanzisha mradi, kulipa walengwa, na kununua vifaa vya ujenzi.

Akizungumza kuhusu utekelezaji wa mradi, Shija amesema, “Mradi huu wa barabara ni sehemu ya ajira za muda zilizofadhiliwa na TASAF, ambapo utekelezaji ulisimamiwa na Kamati ya Usimamizi ya Jamii kwa kushirikiana na mtoa huduma au fundi ngazi ya jamii, kwa niaba ya serikali ya mtaa. Walengwa 114 walishiriki katika ujenzi, ingawa baadhi yao hawakujitokeza."
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa TANESCO, Bundala Shija

Ameongeza kuwa kutokana na ubora wa kazi iliyoonyeshwa, TARURA ilichukua hatua ya kuiboresha barabara zaidi kwa kuweka moramu na kalvati, hivyo kuhakikisha barabara inapitika muda wote, hata katika hali mbaya ya hewa.

Shija pia ameomba TARURA kuendelea kuboresha barabara zingine katika eneo hilo na maeneo mengine, ili kuendelea kuboresha miundombinu na maisha ya wananchi.

“Tunaiomba TARURA iendelee kutufikishia maendeleo kwa kuboresha barabara nyingine zinazohitaji msaada. Hii itasaidia sana katika kukuza uchumi wa eneo letu,” amesema Shija.

Kwa jumla, mradi huu umeonyesha jinsi miradi ya miundombinu inayofadhiliwa na TASAF inavyoweza kuwa chachu ya maendeleo, hasa kwa walengwa wa Mpango Kunusuru Kaya Maskini, na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Octavina Kiwone akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Octavina Kiwone akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Octavina Kiwone akionesha miti iliyopandwa na Walengwa wa TASAF pembezoni mwa barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha.
Martha Daniel Chacha akielezea faida wanazopata kupitia barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha
Waandishi wa habari, maafisa kutoka TASAF wakitembelea barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Waandishi wa habari, maafisa kutoka TASAF wakitembelea barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Waandishi wa habari, maafisa kutoka TASAF wakitembelea barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Waandishi wa habari, maafisa kutoka TASAF wakitembelea barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Waandishi wa habari, maafisa kutoka TASAF wakitembelea barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Waandishi wa habari, maafisa kutoka TASAF wakitembelea barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Waandishi wa habari, maafisa kutoka TASAF wakitembelea barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Waandishi wa habari, maafisa kutoka TASAF wakitembelea barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa TANESCO, Bundala Shija akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha
Mwenyekiti Mstaafu wa Mtaa wa TANESCO kata ya Chamagusa Suleiman Mzee akiomba serikali iwapatie miradi mingine ya barabara
Fundi Msimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha, Paul Ramadhani akielezea namna walivyojenga barabara hiyo kwa ufanisi mkubwa
Gigwa Masingija akielezea namna alivyoshiriki ujenzi wa barabara ya Mashema inayounganisha Mtaa wa TANESCO na Sanjo katika kata ya Chamaguha
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger