Monday 28 September 2020
Mgombea ubunge jimbo la Wanging'ombe-Njombe (Chadema) aahidi kuinua sekta ya kilimo
Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mgombea Ubunge jimbo la Wanging’ombe mkoni Njombe Dkt Dismas Luhwago (CHADEMA) amesema kama wananchi wakimpa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo kwa miaka mitano atahakikisha sekta ya kilimo inakuwa na tija katika kukuza uchumi wa jimbo hilo kwa kuanzisha mikopo ya pembejeo na kusimamia kilimo cha mazao ya biashara yenye bei kubwa katika masoko ya kimataifa likiwemo zao la parachichi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Gonelamafuta kata ya kidugala ambapo amesema kuwa taarifa za kiutafiti zinaonyesha kuwa wilaya hiyo inafursa ya kuzalisha mazao ya biashara kama korosho,makademia na vanilla ambayo yana soko kubwa Katika masoko ya kimataifa na bado hayajaanza kuzalishwa.
“Tutaazisha mkakati wa kulima mazao ya biashara sio ya chakula,ya chakula mtalima kwa ajili ya chakula lakini tutakuwa na mazao ya biashara na parachichi namba moja” Alisema Luhwago
Amesema kuwa atasimamia serikali kuwasaidia wakulima kupata pembejeo za kilimo kwa haraka kwa kupata mkopo kutoka bank ya kilimo.
“Serikali imeanzisha benki ya wakulima lakini kwa bahati mbaya wananchi wengi wa Wanging’ombe mlio wengi hamna sifa ya kukopesheka kwasababubu hamna sifa ya kukopesheka kwasababu hamna dhamana,mashamba yenu hayajapimwa,viwanja vyenu havijapimwa.Inamaana hamna hati tukishirikiana na serikali nitahakikisha tunapima maeneo yenu mpate hata hati za kimila,mimi nimewahi kopa hadi miioni ishirini kwa kutumia hati za kimila”aliongeza Luhwago
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally Kakurwa azindua awamu ya tatu ya Kampeni za CCM
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally Kakurwa amezindua awamu ya tatu ya Kampeni za CCM Kutokea Kongwa Mkoani Dodoma Kwenye Mkutano Mkubwa wa Mgombea Mwenza wa CCM Mama Samia Suluhu Hassani. Chama Cha Mapinduzi kimeingia Awamu ya 3 Kati ya 6 za Kuwasha Mitambo yake ya Kampeni za Kumnadi Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli, Wabunge na Madiwani wote nchi nzima.
Bashiru atoa Onyo kwa Wanaokusanya kadi za Wapiga kura kuwarubuni.
Na John Walter- Manyara
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ametoa onyo kali kwa wale wote wanaopita kukusanya shadada za kupigia kura kwa visingizio vya kutoa mikopo kwa wananchi.
Ametoa onyo hilo Septemba 27, 2020 akiwa kata ya Engusero wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara akiwa ameongozana na Mgombea Mwenza wa CCM wa Urais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan baada ya uzinduzi wa Kampeni awamu ya tatu kati ya sita, uliofanyika wilayani Kongwa mkoa wa Dodoma.
"Tusilaghaiwe, shahada yetu ya kupiga kura, ina kazi ya kupiga kura tusidanganywe kwamba shahada hiyo unaweza ukapata mikopo, ukiona mtu anakwambia hivyo mtafute mwenyekiti wa Kitongoji akamatwe na achukuliwe hatua za sheria."
Katibu Mkuu ameongeza kuwa, "Ukiona mtu anakuhamasisha kufanya fujo, usimkubalie kwasababu nchi hii ni nchi huru na ni kisiwa cha amani."
Awali, katika uzinduzi huo, Wilayani Kongwa Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuzipongeza kamati za siasa za ngazi zote pamoja na wenyeviti wa mashina kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kuhakikisha ushindi mkubwa unapatikana.
Uzinduzi huo ni wa awamu ya tatu kati ya sita ambapo awamu ya nne itafanyika Zanzibar.
Wawili mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya kada wa CCM Njombe
Na Amiri Kilagalila,Njombe
Watu wawili wanashikiliwa na vyombo vya dola mkoani Njombe kwa tuhuma za mauaji ya kada wa Chama cha Mapinduzi na mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Iringa Emmanuel Mlelwa aliyeuawa na kutambuliwa siku 6 baada ya kifo chake.
Akizungumza katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wilayani Ludewa,mkoani Njombe.Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya.amesema watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji hayo huku wakiendelea na upelelzi wa awali.
Aidha amewata wananchi kuwa wavumilivu kwa sasa kwa kuwa vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na mauaji hayo
“Sasa hivi tupo katika kampeni kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu,lakini kampeni haiwezi ikatumika kuvunja amani.Kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,tutawasaka wahusika kwa nguvu zote kuhakikisha wametiwa mbaroni”alisema Marwa Rubirya mkuu wa mkoa wa Njombe
Vile vile aliema “Maendeleo mnayoayaona katika nchi yetu yanaonekana kwasababu tuko katika mazingira ya amani,niwaombe wakati serikali tunapoendelea kushughulika na jambo hili niwaombe wananchi tuendelee kuonyesha ukomavu kuhimili jambo hili” aliongeza Marwa Rubirya
Amewathibitishia wananchi kuto kuachwa yeyote atakayebainika kuhusika na mauaji hayo “Niwathibitishie kuwa hakuna aliyehusika na uhalifu huu,ambaye hata chukuliwa sheria kwa mujibu wa sheria za nchi yetu”
Nao chama cha Mpainduzi CCM mkoa wa Njombe kupitia kwa mwenyekiti wake Jassel Mwamwala kimewataka vijana kuendelea kuwa watulivu kwa kuwa serikali inaendelea kulifanyia kazi swala hilo.
“Na ninny vija tunaomba tulieni acheni mihemko serikali yetu inafanya kazi na hakika tutapata jibu”alisema Mwamwala
Kijana huyo ameuawa kikatili wiki lililopita na watu wasiojulikana na mwili wake kutambuliwa baada ya siku sita ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mji wa Njombe kibena
Marehemu Emmanuel Mlelwa alihudumu kama mwenyekiti wa wanafunzi wa CCM wa vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Njombe kabla hajahamia mkoa wa Iringa ambako nako alikuwa akihudumu kwa cheo hicho akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumain kabla mauti hayajamkuta wakati akiwa likizo.
Mama Samia aeleza Makubwa yaliyofanywa na yatakayofanywa na Ccm Mkoa wa Manyara
Na John Walter- Manyara
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema chama Cha mapinduzi kwa uongozi makini waliouonyesha kuwaongoza wananchi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kinastahili kuendelea kuongoza.
Samia ameyasema hayo wakati akizindua awamu ya tatu ya Kampeni za CCM kitaifa septemba 27,2020 katika wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara.
Samia amesema kwenye Miundo Mbinu Mkoa wa Manyara katika ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2020-2025, wamepanga Kukamilisha na Kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina Katika barabara za Kongwa Ranch - Kiteto - Simanjiro - KIA (km 483); Babati -Orkesumet - Kibaya (km 225); Mbulu - Magugu (Mbuyu wa Mjerumani) (km 63;) Babati (Dareda) – Dongobesh (km 60).
Aidha katika ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhusu Wafanyabiashara Wadogo, imeeleza kuwa yametengwa maeneo rasmi kwa ajili ya wajasiriamali wakiwemo mama lishe na wauza mbogamboga kufanyia biashara katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Manyara.
Kuhusu Kilimo Samia amesema Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kufanya Ukarabati na ujenzi wa bwawa la Dongobesh (Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu) ambao umekamilika.
Akizungumzia Nishati, amesema ilani hiyo ambayo awamu inayomalizika imefanya mengi itaendelea kuhakikisha wananchi wote wanapatiwa umeme kwenye nyumba zao bila kujali aina ya nyumba wanayoishi.
Amesema serikali ya Ccm imetekeleza Mpango Kabambe wa Kupeleka Umeme Vijijini (REA I, REA II na REA III) ambapo jumla ya vijiji 8,587 kati ya vijiji 12,319 vya Tanzania Bara vimefikiwa na umeme ambayo ni sawa na asilimia 70; pamoja na Kupunguza gharama za kuunganisha umeme vijijini ambapo gharama za kuunganisha umeme vijijini zimepungua kutoka wastani wa shilingi 454,000 hadi shilingi 27,000; huku kasi ya usambazaji wa umeme vijijini ikiongezeka.
Akizungumza kuhusu Afya Mgombea Mwenza huyo wa Urais amesema CCM inatambua kuwa huduma za afya ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo ya nchi ambapo katika Mkoa wa Manyara ukarabati unefanyika katika vyumba vya upasuaji, wodi za kulaza wagonjwa, jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na wodi za wazazi na watoto na kuwekewa vifaa vya kisasa vya upasuaji na maabara.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Kiteto Edward Ole Lekaita amewaomba wananchi wa Kiteto wampe kura za ndio yeye, Madiwani wa ccm pamoja na Rais ili kuwawakilisha bungeni.
Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo katika ziara mkoani Manyara kwa ajili ya Kampeni kunadi Sera za Chama cha Mapinduzi na Wagombea nafasi za Udiwani, Ubunge na Rais kupitia Chama hicho.
Sunday 27 September 2020
Tundu Lissu atakiwa kufika mbele ya kamati ya maadili ya NEC
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.
Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.
Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.
YANGA SC WAICHAPA MTIBWA SUGAR 1 - 0
Viongozi Wa Dini Wa Kamati Ya Amani Wakemea Madhabahu Kutumika Kisiasa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum ambaye amesema kuwa, baadhi ya viongozi wa dini wameanza tabia ya kuwanadi wagombea katika nyumba za ibada jambo ambalo halitakiwi kufanyika na kupelekea kuvunja amani ya nchi.
Amesema, kitendo hicho kinachofanywa na baadhi ya viongozi wa dini kinaweza kupelekea kuvuruga amani iliyopo na kupelekea kuweka matabaka.
Sheikh Salum amesema, kazi kubwa ya viongozi wa dini ni kuhubiri amani na si kusimama katika nyumba za ibada na kuaza kufanya kampeni kwani si jukwaa sahihi.
“Sisi kwa umoja wetu viongozi wa dini wote wa kamati za amani na kwa ujumla wake hatupendezwi na tabia iliyoanza kujitokeza kwa sasa ya kuona maaskofu, mashekhe, Mapadri maimamu wanasimama katika nyumba za ibada kufanya kampeni na kumnadi Mgombea yoyote kufanya hivi ni kuatarisha amani ya nchi yetu”amesema Sheikh Salumu
Amesisitiza kuwa, nyumba za ibada zikianza kufanya kampeni zitakuwa zimepola nafasi za wanasiasa na majukwaa yao.
Amesema, watanzania wanapaswa kuachwa waende katika majukwaa ya siasa wakasikilize sera za wagombea ili waweze kuchagua ni nani anawatosha na kuwataka viongozi wa dini kutokutumiwa na wanasiasa
Korea Kaskazini yaonya kuhusu shughuli za kijeshi la Korea Kusini kwenye eneo lake- KNCA
Kulingana na shirika la habari la habari la Korea Kaskazini, KNCA hii leo mamlaka za nchini humo zilikuwa zinazingatia namna ya kuukabidhi mwili huo kwa Korea Kusini iwapo utapatikana.
Ripoti ya KNCA ililiita tukio hilo kuwa ni baya na ambalo halikutakiwa kutokea ingawa ilionya kwamba shughuli za kijeshi za Korea Kusini karibu na eneo kulikotokea tukio hilo zilikuwa zimevuka na kuingia kwenye eneo la maji ya Korea Kaskazini na kutaka kusimamishwa kwa shughuli hizo ili kuepusha hali ya wasiwasi.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Korea Kusini alipoulizwa alisema hawezi kuzungumzia tuhuma hizo za Korea Kaskazini kwa sasa.
DW
SGR ni mradi utawanufaisha watanzania wote
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dar es Salaam
Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaotekelezwa na Serikali nchini utawanufaisha watanzania wote moja kwa moja ikiwa ni ajira kwa upande wa reli yenyewe, kilimo, ama biashara hatua inayosaidia kuinua kipato na uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Kwa hatua ya awali mradi unamanufaa makubwa na umetoa ajira kwa Watanzania asilimia 51 na wageni asilimia 49 tofauti na hapo awali ambapo ilipangwa wataalamu wa ndani wawe asilimia 20 na wataalamu wan je ya nchi wawe asilimia 80.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Kipande cha Morogoro Mkakutupora Singida Mhandisi Mteshi Tito kwa wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati wa siku ya pili ya ziara yao ya kutembe mradi huo na kuongeza hatua hiyo ya uwiano huo wa ajira imefikiwa baada ya Watanzania kuonesha uwezo mkubwa wa uelewa kwenye masuala ya reli.
Aidha, mradi huo unaendelea kutoa ajira kwa watanzania katika maeneo yao ambapo unapita ikizingatiwa ni mradi mkubwa unaopitia mikoa mingi inapopita reli kuanzia Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Kigoma ambapo unatarajiwa kufika.
Fauka ya hayo mradi pia unatarajiwa kuwa kutoa fursa nyingi za kiuchumi ambapo utasaidia kusafirisha mizigo kwenda nchi jirani zisizo na bandari ikiwemo Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasiaya Kongo na Uganda hatua itakayosaidia kuchochea kukua kwa uchumi wa nchi.
Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Jamila Mbaruku amewapongeza wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa na moyo wa uzalendo wa kuthamini na kuchukua hatua ya kujionea mradi unaotekelezwa na Serikali kwa fedha za ndani.
“Naamini mtakuwa mabalozi na wajumbe wazuri kwa kuwatangazia Watanzania juu ya mradi wetu huu wa reli ya SGR kwa kuwa ninyi ndiyo wizara yenye kuisemea Serikali, mmeuthamini, mmethubutu na mmeweza kutembelea eneo lote inapopita reli yetu kutoka kituo cha Ihumwa Dodoma hadi kituo kikuu eneo la Posta jijini Dar es Salaam” alisema Jamila.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Zahara Nguga amesema kuwa kuna dhana potofu inayoenezwa na watu kuwa mradi huo utawanufaisha wafanyakazi peke yao, la hasha, mradi huo utawanufaisha pia wafanyabiashara na wakulima kutoka maeneo mbalimbali inapopita reli hiyo.
“Hata wakulima, mtu anaweze kuwekeza Kilosa akatoka Dar es salaam saa 11 asubuhi na saa 1 yupo Kilosa akisimamia mifugo, mashamba na mazao yake na jioni anarudi Dar es Salaam kuimarisha maisha yake ya ndoa. Huu ni mradi unawanufaisha watanzania wote” alisisitiza Mkurugenzi Msaidizi huyo.
Wakitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo, Mkuu wa Idara ya Sera na Mipango Petro Lyatuu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Leah Kihimbi wamesema kuwa waliazimia kutembelea mradi huo kwa kuzingatia wizara yao ndiyo yenye dhamana ya habari na mradi huo hauna budi kutangazwa na vyombo vya habari ili kuwaelimisha na kuwapa uelewa wananchi juu ya miradi inayotekelezwa na nchi yao.
Lengo la ziara yao la kuufahamu mradi huo limefikiwa kwa kuwa wamejionea malighafi zinazotumika kuutekeleza zinatoka hapa nchini ikiwemo saruji na nondo zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania na baada ya kukamilika utakuwa na manufaa mengi ikiwemo matumizi mazuri ya muda wa kusafiri ambapo muda wa kusafiri kutoka Dodoma hadi Dar es salaam utakuwa ni saa tatu na Morogoro hadi Dar es Salaam itakuwa ni dakika 90 sawa na saa 1:30.
Aidha, wameongeza kuwa wamepanda treni inayotumia umeme inayotumiwa na wahandisi kutekeleza majukumu yao na kusema ukiwa ndani ya treni hiyo unaweza kuendelea kufanya kazi za ofisini bila kuwa na mtikisiko wowote na kuongeza kuwa mradi umekuja umejali maisha ya watu kwa maana watautumia na Shirika la Reli limejali vitu vya asili vya kuitamaduni ikiwemo mito na miti ambayo wameitunza vizuri.
Saturday 26 September 2020
BWALO GYMNASTIC CENTRE YAENDESHA SHINDANO LA MBIO ZA MARATHON SHINYANGA
Miongoni mwa wadau wa michezo walioshiriki mbio hizo za Marathon ya Kwanza iliyoandaliwa na Bwalo Gymnastic Centre Shinyanga- BGC kwa kushirikiana na Mlezi wa BGC ACP Debora Magilimba ni askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga.
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akiwa na washiriki wa mbio za Marathon leo Shinyanga
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akiwa na washiriki wa mbio za Marathon leo Shinyanga
Washiriki wa mbio za Marathon wakipiga picha ya kumbukumbu.
Washiriki wa Mbio za Marathon wakikimbia
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akikabidhi zawadi kwa washiriki wa mbio za Marathon leo Shinyanga