Friday 29 March 2019

Tazama Hapa Sifa 10 za Simu Mpya ya Infinix ZERO 6 Inayotumia Teknolojia ya Artificial intelligent


AI, TEKNOLOJIA MPYA KATIKA SIMU NCHINI.
Baada ya uzinduzi rasmi wa Infinix ZERO 6 nchini Tanzania, simu  yenye teknolojia ya Artificial intelligent, wengi wamekuwa wakihoji kuhusiana na ufanyaji kazi wa teknolojia hiyo, hivyo basi leo ningependa kuwajuza namna teknolojia ya AI kwenye kamera za Infinix ZERO 6 inavyofanya kazi.


Pamoja na sifa zingine nzuri za infinix ZERO 6, sifa kuu zaidi  ya Infinix ZERO 6 ni kamera , Infinix Zero 6 imewekwa nguvu nyingi sana upande wa kamera ambapo kamera za nyuma ni MP 12+MP 24 zenye kupiga picha/picha jongefu na mng’ao  wa hali ya juu sana, na kamera ya mbele ni MP 20.

Na katika kuongeza ubora wa kamera ya Infinix ZERO 6, ndipo teknolojia ya AI inapofanya kazi sambamba na kamera. Teknolojia ya AI inaiwezesha ZERO 6 kupiga picha zenye muonekano halisi ya mazingira husika mfano kama ni bahari au ua basi utapata picha zenye rangi halisi ya vitu hivyo.

Vile vile kioo cha mbele kimewekewa ulinzi kioo cha Gorilla inchi 6.2. Uwezo wake wa betri ni 3650mAh pamoja na XCharge kwa ajili ya teknolojia ya kuchaji haraka

Mbali na kamera, imekuwa ni kama tamaduni kwa Infinix kuzalisha simu zenye muoneka wa kuvutia na safari hii tunawapa asilimia 100% kwani wamehama kabisa kutoka material ya plastic na metal hadi kwenye alminium na class.

Infinix imezingatia swala la rangi, Infinix Zero 6 imekuja na rangi tatu tofauti Milan Black, Sapphire Cyan na champagne gold, simu hii inatikana nchi nzima .


sifa za zero 6.

Infinix ZERO 6 Specifications:
Network: 4G/3G/2G
OS Version: AndroidTM 8.1
Display: 6.18 INCH FHD+
Processor: Qualcomm SDM 636
Dimensions: 156.8*75.9*7.95mm 
ROM + RAM: 64GB + 6GB
Battery: 3650mAh
Front camera: 12MP AF+24MP AF WITH QUAD FLASHLIGHT
Back camera: 20MP 4IN1 WITH FLASHLIGHT




Share:

Kigogo wa TAKUKURU anayedaiwa kuwadhulumu wenzake viwanja, Kulthum Mansoor amekamatwa

Mkurugenzi wa Mipango TAKUKURU Kulthum Mansoor, ambaye jana Machi 28, 2019, alitajwa na Rais Magufuli kwa tuhuma za kuwadhulumu viwanja, baadhi ya wafanyakazi wenzake wa TAKUKURU amekamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Oysterbay.

Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo,  Kulthum alikamatwa jana Alhamisi Machi 28, 2019 na kupelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam ambapo leo Ijumaa March 29 atafikishwa mahakamani

Jana, Rais Magufuli akizungumza Ikulu mara baada ya kumuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mlowola alisema kuna mkurugenzi mmoja wa makao makuu Takukuru aliwauzia viwanja hewa wafanyakazi wenzake, lakini anashangaa hajapelekwa mahakamani hadi sasa.

“Wala sijapata taarifa kwamba hizo fedha amezirudisha kwa wafanyakazi aliowadhulumu. Wafanyakazi wanaumia, wanalalamika pembeni.

“Amewadanganya kwamba ana viwanja Bagamoyo, lakini mpaka leo hawajapewa,” alisema Rais Magufuli.

Alisema kashfa hiyo iliibuliwa tangu Balozi Mlowola alipokuwa mkurugenzi wa taasisi hiyo, lakini hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

“Suala hili lilianza tangu wakati wa Balozi Valentino, nikamuuliza huyu mbona harudishi fedha au hapelekwi mahakamani, akawa na kigugumizi, sasa na wewe usiwe na kigugumizi kwa sababu nafasi za ubalozi zimeisha.

 “Ndiyo maana huwa najiuliza hawa Takukuru huwa ni kwa ajili ya watu wengine, wao ‘hawaji-takukuru’ humo humo ndani?” alihoji.


Share:

Tangazo La Mafunzo Ya Kilimo Nchini Israel

UTANGULIZI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatangaza mafunzo katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini Israel. 

Mafunzo hayo ni ya miezi 11 kuanzia mwezi Septemba, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mafunzo hayo yatahusisha pia vitendo (field attachment) kwenye mashamba makubwa ya mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum.

SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI
      i. Awe ni raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 20-35 pamoja na cheti cha            kuzaliwa na Kitambulisho cha Uraia. 
 ii.Awe amehitimu mafunzo ya Kilimo katika ngazi ya shahada ya Chuo Kikuu,                         Stashahada au Astashahada ya Vyuo vya kilimo vinavyotambulika nchini.
iii.Awe na afya njema. 
iv.Awe na ujuzi wa kuandika na kuongea lugha ya Kiingereza.  
 v. Awe na uwezo wa kufanya kazi na watu wa tamaduni mbalimbali. 
vi.Awe tayari kurejea nchini baada ya mafunzo yake.        
                                                       
UTARATIBU WA KUFANYA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yakiwa yameambatishwa na nakala za nyaraka zifuatazo:

     i. Cheti cha kuzaliwa na uraia. 
   ii. Vyeti vya kitaaluma.
 iii.Hati ya Kusafiria au uthibitisho wa maombi ya pasipoti.
  iv.Cheti cha kuthibitisha afya kutoka hospitali inayotambulika.
    v. Barua ya kuonesha sababu za kushiriki mafunzo hayo  (Motivation letter) kwa lugha           ya Kiingereza.
  vi. Wasifu (Curriculum Vitae).
 vii. Picha mbili ndogo (Passport size).
viii. Majina na anwani za wadhamini watatu wanaoishi nchini akiwemo mwalimu wa                 Chuo ulichohitimu.

Maombi yote yatumwe kupitia anwani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Jengo la LAPF
Ghorofa ya 6,
Barabara ya Makole,
S.L.P   2933,
DODOMA.

Au kwa baruapepe; mafunzo.israel@nje.go.tz

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili, 2019

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.


Share:

Urusi yasema jeshi lake litaendelea kuwepo Venezuela

Urusi imesema wanajeshi wake wataendelea kubakia Venezuela kwa muda wote watakaohitajika kubakia na kuyapinga madai ya rais wa Marekani Donald Trump ya kuitaka iondoe wanajeshi wake katika nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro.

Hatua ya Urusi ya kupeleka wanajeshi pamoja na vifaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa nia ya kumuimarisha rais Nicolas Maduro imezusha wasiwasi mkubwa kimataifa kuhusu mgogoro wa Venezuela ambako utawala wa rais Trump unatia msukumo wa kufanyika mabadiliko ya kiutawala.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesisitiza leo kwamba wanajeshi wake waliko Venezuela hawasababishi kitisho cha aina yoyote kwa mtu yoyote.Maria Zakharova msemaji wa wizara hiyo amesema jeshi la Urusi nchini Venezuela linahusika katika utekelezaji wa makubaliano ya shughuli za kijeshi na ushirikiano wa kiufundi na wataendelea kuwepo huko kwa kipindi watakachohitajika kuwepo.. 

Credit:DW


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 29




Share:

Thursday 28 March 2019

Picha : MADIWANI WA MIKOA MITANO WAFANYA ZIARA AGAPE NA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA KISHAPU

Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao kutoka Mikoa ya Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga na Kigoma wametembelea Shirika la Agape AIDS Control Programme na vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga. 

Lengo la ziara hiyo ya siku mbili iliyoanza Machi 27 na kumalizika Machi 28,2019 ni kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vituo vya Taarifa na Maarifa wilayani Kishapu na Washirika wake likiwemo Shirika la Agape. 

Mwezeshaji wa ziara hiyo,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao alisema katika siku ya kwanza ya ziara,walitembelea kituo cha Taarifa na Maarifa cha kata ya Ukenyenge,kukagua vyumba vya usiri kwa wanafunzi wa kike na vyoo katika shule za msingi Kanawa na Bulimba,zahanati ya Negezi na Gender Club katika shule ya sekondari Ukenyenge. 

“Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa hiyo mitano walijifunza namna vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu jinsi vinavyoshirikiana na jamii na viongozi wa serikali kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii”,alieleza Amani ambaye pia ni Meneja Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi unaotekelezwa na Agape wilayani Kishapu. 

“Washiriki wa ziara hii pia wametembelea shirika la Agape lenye makao yake Makuu katika Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga linalojihusisha na masuala ya ulinzi wa mtoto,utoaji msaada wa kisheria,kutokomeza mimba na ndoa za utotoni,ukatili wa kijinsia,malezi na makuzi bora ya mtoto”,aliongeza Amani. 

Aidha alisema wakiwa katika shirika la Agape,Washiriki wa ziara hiyo pia waliwatembelea wanafunzi wahanga wa mimba na ndoa za utotoni wanaosoma katika shule ya Agape Knowledge Open School inayomilikiwa na Agape iliyopo katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Miongoni wa madiwani hao akiwemo Pessa Pessa kutoka kata ya Bwakira Chini halmashauri ya wilaya ya Morogoro waliishukuru TGNP Mtandao kwa kuwazesha kufika mkoani Shinyanga kujionea mambo mazuri yanayofanywa na Vituo vya Taarifa na Maarifa na shirika la Agape katika kupiga vita matukio ya ukatili wa kijinsia. 

“Kwa kweli bila TGNP Mtandao tusingeweza kuyafahamu mambo mema yanayofanywa na wenzetu katika kuhakikisha watoto wanalindwa lakini pia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia”,aliongeza Festo Mwalyego ambaye ni diwani wa kata ya Tembela halmashauri ya wilaya ya Mbeya. 

Naye Stimar Heda John (kata ya Ijombe halmashauri ya wilaya ya Mbeya),aliwaomba viongozi wa serikali kutembelea shirika la Agape kwani linafanya kazi kubwa kuwasaidia watoto wanaokumbana na vitendo vya ukatili hivyo serikali ione namna ya kuwaongezea nguvu ili kusaidia Watanzania wengi zaidi. 

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao kutoka Mikoa ya Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga (Kishapu) na Kigoma wakiwasili katika Ofisi za Shirika la Agape AIDS Control Programme katika kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga leo Machi 28,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Agape,Lucy Maganga akiwakaribisha Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga (Kishapu) na Kigoma. 
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Agape,Lucy Maganga akikaribisha madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa.
Mwezeshaji wa ziara ya Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika la Agape katika kulinda watoto na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Mwezeshaji wa ziara ya Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao akielezea historia ya Shirika la Agape.
Diwani wa kata ya Ukenyenge wilaya ya Kishapu,Josephina Malima akizungumza wakati wa ziara hiyo na kueleza namna wanavyoshirikiana na vituo vya taarifa na maarifa,serikali na wadau mbalimbali likiwemo shirika la Agape na TGNP Mtandao katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Diwani wa kata ya Tembela halmashauri ya wilaya ya Mbeya,Festo Mwalyego akielezea jinsi Imani za kishirikina zinavyochangia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika jamii na kuitaka jamii kuepukana na imani hizo. 
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Fredina Said akielezea shughuli wanazofanya wilayani Kishapu kupiga vita ukatili wa kijinsia. 
Diwani wa Kata ya Ijombe halmashauri ya wilaya ya Mbeya,Stimar Heda John akipongeza kazi zinazofanywa na shirika la Agape katika kulinda haki za watoto.
Meneja Fedha wa Shirika la Agape Nkwimba Ng'homano Lugisi (wa pili kushoto) akieleza namna wanavyowahifadhi kwa muda mabinti waliofanyiwa vitendo vya ukatili katika chumba maalum kilichopo katika ofisi za shirika la Agape.
Nje ya chumba cha kuhifadhi mabinti waliofanyiwa vitendo vya ukatili . Kushoto ni Mwezeshaji wa ziara ya Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao akielezea jambo kwa Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa.
Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa wakiondoka katika ofisi za shirika la Agape.
Hapa ni katika shule ya Agape Knowledge Open School ambapo mabinti wahanga wa mimba na ndoa za utotoni wanapewa elimu ya kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.Kulia ni Peter Amani akitambulisha Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Mbeya,Morogoro,Kigoma,Mara na Shinyanga waliotembelea shule hiyo.
Peter Amani akielezea namna mabinti wanavyosoma katika shule hiyo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo,Kalunga Zacharia akielezea changamoto zilizopo katika shule hiyo kuwa ni uhaba wa madarasa,mabweni,vitabu na madawati.
Diwani wa kata ya Bwakira Chini halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Pessa Pessa akilishukuru na kulipongeza shirika la Agape kuwapatia elimu watoto hao ambao ni wahanga wa mimba na ndoa za utotoni na kuahidi kushirikiana nao katika kuendelea kuwapatia msaada zaidi ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Songwa wilayani Kishapu Rahel Madundo akiwasisitiza watoto hao kusoma kwa bidii.
Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Mbeya,Morogoro,Kigoma,Mara na Shinyanga wakiongozwa na wanafunzi kutembelea shule hiyo.
Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Mbeya,Morogoro,Kigoma,Mara na Shinyanga,viongozi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya Madiwani na viongozi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.
Wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa na viongozi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malundev- Malunde1 blog
Share:

BANCABC YATOA MSAADA WA MABATI 200 KWA WILAYA YA KILINDI

Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu
(Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo.
Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia). 
Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia). 
Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo, mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati yaliyotolewa na BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo.
Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa
mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo.
Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo baada ya kukabidhi msaada
wa mabati 200. Wengine katika picha ni Asmah Abubakar na Raphael Kalinga wa BancAbc.
***

BancABC kupitia Huduma ya Mkopo Rahisi imejidhatiti kuhakikisha inainua na kuendeleza mazingira ya elimu katika wilaya ambazo benki hiyo inafanya shughuli zake kupitia miradi yake ya kusaidia jamii inayowazunguka. 

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw. Emmanuel Nzutu alisema wanaunga mkono juhudi za serikali kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

"Hivyo leo sisi kama Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Sauda Salum Mtondoo.” 

Alisema BancABC inaamini katika umuhimu wa Elimu bora ndani ya jamii zetu hapa Tanzania ,hivyo inaunga mkono Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli,alisema na kuongeza kuwa katika miradi mbali mbali ya elimu inayofanywa na benki hiyo lengo lake kuu ni kusaidia kuinua kiwango cha elimu na kuifikia kila jamii hasa maeneo ya vijijini.

"BankABC inatoa huduma ya Mkopo ambao ni mahususi kwa wafanyakazi wa serikali, Easy loans ambapo inakupa nafasi ya kulipa Mkopo kwa muda wa miaka sita na vile vile una uwezo wa kuweza kuongeza Mkopo hata kabla ya kumaliza kulipa ule wa awali.

Uzuri wa mkopo huu tofauti na mikopo mingine ni kwamba, mwenye kuomba Mkopo anaweza kuchagua ni mradi gani wa kuwekeza fedha zake kwa mfano kulipa karo ya shule, kununua gari, kufanya marekebisho ya nyumba, kulipa kodi ya nyumba au kumalizia ujenzi,Vile vile tunaweza kununua Mkopo wako wa awali ukabaki na Mkopo mpya",alisema Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw. Emmanuel Nzutu. 

Alisema Mkopo huo utakuwa na bima ya maisha pale ambapo mwenye Mkopo anapofariki, familia yake itapewa fedha taslimu Tzs 500, 000 kwa ajili ya kugharamia mazishi. 

"Tunatoa wito kwa wateja wetu na wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na Bancabc na kuchangamkia Mkopo huu kwani sisi tunakuweka karibu na ndoto zako",aliongeza Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw. Emmanuel Nzutu.

Naye mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo,wakati akipokea msaada huo aliishukuru benki hiyo kwa msaada walioutoa wa kuchangia suala la elimu katika Wilaya yake,aidha pia DC Mtondoo ameikaribisha benki hiyo kutoa huduma zao mbalimbali kwa Wananchi.

"BancABC tunawashukuru mno kwa msaada wenu mlioutoa,lakin pia tunawakaribisha msogeze pia huduma zenu kwa Wananchi wilayani hapa,ili Wananchi wanedelee kunufaika na huduma zenu mnazozitoa",alisema DC Mtondoo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger