Friday 29 March 2019

KUTANA NA MWANAMKE ANAYEFANYA MAPENZI NA MIZIMU..ADAI ANASIKIA RAHA KULIKO KUFANYA NA BINADAMU WA KAWAIDA

Anaitwa Amethyst Realm Mwanamke Kutoka Uingereza, Amewahi lalamika katika Kipindi cha Televisheni cha 'This Morning' cha ITV ya Uingereza kwamba Amefanya Mapenzi na zaidi ya Mizimu 20.

Anasema Kisanga Kiliamza Mwaka 2005 Akiwa na Miaka 15 Ambapo yeye Pamoja na Familia yake Walipohamia Katika Nyumba Mpya na Baada ya Siku chache akaanza Kuhisi Mtu Anamshikashika Usiku Huku Hamuoni na Kupelekea kufanya nae Mapenzi, na Hali hiyo iliendelea Kumtokea Kwa Miaka Mingi.

Anasema Ilianza kama Nguvu fulani hivi Inampapasa, Baadae Akawa anaona Kabisa Anahemewa Mihemo Maeneo ya Shingoni na Anashikwashikwa Sehemu za Mwili wake Usiku bila Kumuona anaemshika na Baadae Wanafanya Mapenzi.

Hali hii anasema Ilimtokea Kwa Miaka Mingi hadi Siku Moja Alipomtembelea Mpenzi wake, na Mpenzi Wake Alipokua Anarudi Nyumbani Usiku Alikuta Kivuli Kinakimbia Kupitia Dirishani na Akahisi Alikua na Mwanaume Ndani na Hapo ndipo ilikua mwisho wa Mzimu huo Kuja.

Amethyst Anasema Alimwambia Mpenzi wake Asihangaike Kumfatilia Kwasabu Asingempata kwakua hakua Mtu wa Kawaida bali Ulikua ni Mzimu, Baada ya Kuambiwa Hvyo Jamaa Akapaki Mabegi Akasepa!!. .
.
Amethyst anasema Alikua Anahisi kabisa Ladha ya Penzi huku Anaemfanya Haonekani na Alikua Amefanya Mapenzi Mara nyingi sana na Mizimu zaidi 20 tofauti na Hadi Anaiambia ITV Mwaka 2017 Anasema Alikua Anaujauzito Alioupata Kwa njia hiyo na Chaajabu ni Kwamba Alionyesha Kuridhia Kuendelea na Mahusiano yake na Mizimu!. .
.
"Ni Kweli Hauwezi (Mzimu) Kuninunulia Maua au Kunitoa Kwenda Sehemu Kufurahi lakini Furaha Ninayoipata Kwake Ni Special, Naota Ndoto nzuri na Najihisi Furaha" - Amethyst .
.
"Wakati wa Tendo Nahisi Miguso na Raha ya Ajabu Huku Anaenifanya Simuoni na Kuna Muda Hua Nashangaa Nageuzwa Kabisa Kufanyishwa Mapenzi Styles Tofautitofauti" - Amethyst .
.
"Nimewahi Sikia Mara nyingi juu ya Jambo hili la Mwanamke Kulala na Viumbe Wasioonekana Usiku na Sasa Ninahisi nina Ujauzito wa Viumbe hao" Alisema Amethyst. .
.
"Sio Pekeangu tuu Nilie Katika Mahusiano na Mzimu, Nasikia Habari Nyingi kama Hizi Watu huenda Sehemu Fulani Kukutana na Wapenzi wao ambao ni Mizimu" - Amethyst

Hali hii ya Kushiriki Mapenzi na Mzimu inaitwa 'Spectrophilia'. #Love
Share:

Ofisi Ya Makamu Wa Rais Yapongezwa Na Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Viwanda, Biashara Na Mazingira

Na Lulu Mussa
Serikali imesema itaendelea na juhudi za kushawishi wadau wa maendeleo na Jumuiya za Kimataifa ili kupata fedha za kusimamia uratibu wa shughuli za mazingira na kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi nchini. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameyasema hayo hii leo Jijini Dodoma wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji  wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Amesema Tanzania ni Mwanachama kwenye Mifuko na Mikataba mbalimbali duniani hivyo kuna fursa za kunufaika na fedha zitolewazo na mifuko hiyo akitoa mfano wa Green Climate Fund. 

Aidha Waziri Makamba ameainisha mafanikio yaliyopatikana katika Ofisi yake kwa kipindi cha mwaka 2018/2019, kuwa ni pamoja na kufanya Mapitio ya Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 1997 na Mkakati wa Utekelezaji wake,  kuandaa rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mazingira wa mwaka 2019 - 2023, na Maandalizi ya Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Viumbe Vamizi (Invasive Alien Species).  

Pia, katika kipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha rasimu ya mwisho ya Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchini baada ya kupata maoni ya wadau kabla ya kuwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004. 

Waziri Makamba amesema katika kuhakikisha usimamizi na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira unazingatiwa jumla ya miradi 1,254 ya maendeleo imefanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na Ukaguzi wa Mazingira na katika kuharakisha uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira linatoa Kibali cha Awali cha Mazingira (Provisional Environmental Clearance) ili kuwawezesha wawekezaji kuendelea na maandalizi ya awali ya mradi wakati mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira unaendelea.  

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Sadick amepongeza uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa jitihada za kuhifadhi mazingira nchini. " Kamati inatambua jitihada za Ofisi yenu katika kuhifadhi mazingira, sisi tunawaunga mkono" alisisitiza Mhe. Sadick.


Share:

Kauli ya Bunge Baada ya Mahakama Kuu Kutupilia Mbali Kesi ya Joshua Nassari




Share:

WAZIRI WA FEDHA DKT. MPANGO AAGIZA KUTOTUMIA FUNGU LA LISHE KWA MATUMIZI MENGINE


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Binti wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ambaye ni Mwanaharakati  wa masuala ya lishe, wanawake na watoto Duniani, jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao, Dkt. Mpango, alimweleza Princess Sarah Zeid kwamba Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya masuala ya lishe, utapiamlo na udumavu wa watoto licha ya nchi kuwa na chakula cha kutosha.

Dkt. Mpango alisema kuwa iwapo eneo la lishe halitasimamiwa kikamilifu Taifa litazalisha watoto wenye udumavu wa ubongo na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na utendaji hafifu wakiwa katika shughuli mbalimbali.

Alisema ipo mikoa ambayo inazalisha mazao mengi  kama Mbeya na Njombe lakini ina kiwango kikubwa cha watoto wenye utapiamlo, na kutoa wito kwa kila mtanzania kuhakikisha anaangalia ni chakula gani kinahitajika kwa ajili ya lishe ya watoto na wakinamama wajawazito ili kupunguza udumavu na vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.

Aidha amempongeza Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, kwa kampeni yake anayoifanya duniani kote kupambana na vifo vya wakinamama wajawazito na watoto kwa kuwa mchango wa wanawake ni mkubwa katika jamii ikiwemo uzalishaji mali.

Alisema idadi ya wanawake nchini Tanzania ni asilimia 51 ya idadi ya watu wote wanaokadiriwa kufikia milioni 55 ambapo mchango wako katika sekta mbalimbali za uchumi umekuwa mkubwa hivyo jitihada za kuwalinda zinahitajika.

Alimweleza Binti Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid kwamba kwa kutambua umuhimu wa lishe serikali imelivalia njuga suala la lishe kwa kutenga bajeti kila mwaka katika kila wizara na kwamba fedha hizo zimewekewa wigo zisitumike kwa matumizi mengine.

"Nimeziagiza Wizara, Mikoa na Halmashauri zote nchini kutumia fungu lililotengwa kwa ajili ya lishe  kwa matumizi yaliyopangwa  ili kuhakikisha watanzania wanaimarika kiafya na kushiriki kikamilifu katika Shughuli za Maendeleo" Alisema Dkt. Mpango.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Mkutano kati yake na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid na

Kwa upande wake Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ambaye aliambatana na Mwakilishi wa Shirika  la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) nchini Tanzania, Bw. Michael Dunford, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake katika kupambana na utapiamlo unaosababishwa na ukosefu wa lishe.

Amewataka watanzania kuhakikisha suala la Lishe linapewa kipaumbele  na kila mmoja kwa manufaa ya Taifa na Dunia kwa ujumla na kwamba atahamasisha jumuiya ya kimataifa kuchangia jitihada za Serikali za kupambana na tatizo la lishe, na vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa-WFP nchini Tanzania Bw. Michael Dunford, amesema kuwa shirika lake linatambua mchango mkubwa wa Serikali katika kupambana na masuala ya lishe duni na shirika lake litaendelea kushirikiana na nayo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

Mwisho


Share:

WAZIRI MKUU : UTOAJI WA ELIMU BORA NI KIPAUMBELE CHA NCHI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo na kufikia malengo ya Milenia 2025, Elimu kwa wote (EFA) na Mkakati wa Kupambana na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA). 


Amesema ili kuweza kufanikisha malengo hayo wanahitaji sekta hiyo kuwa bora, imara, inayokidhi mahitaji ya jamii kwa kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kukabiliana na matatizo ya kijamii, kitaifa na kimataifa.


Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 29, 2019) wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Parokia ya Ikwiriri, mkoani Pwani. Ameipongeza Parokia hiyo kwa kubuni mradi wa ujenzi wa shule.


Amesema sekta ya elimu ni wakala wa mabadiliko katika jamii kiuchumi, kiteknolojia na kiutamaduni katika kuleta maendeleo ya nchi na wadau muhimu wa sekta hiyo ni pamoja na Serikali, washirika wa maendeleo, mashirika ya kiraia na ya kidini, sekta binafsi na jamii kwa ujumla. 


Waziri Mkuu amesema kuwa wadau wote hao wamekuwa wakichangia kwa njia mbalimbali katika kuboresha utendaji wa sekta hiyo na kusababisha Serikali kupata mafanikio makubwa sana katika upatikanaji wa huduma za Jamii zikiwemo za elimu, afya na maji.

”Hivi sasa kila Kijiji nchini kina shule ya msingi na ongezeko limefikia idadi ya shule 17,659 zikiwemo zilizo chini ya Kanisa katoliki 204. Pia tumeweza kujenga shule za sekondari katika kila kata ambapo ongezeko limefikia shule za sekondari 4,883 nchi nzima zikiwemo zilizo chini ya kanisa katoliki 266”.

Waziri Mkuu amesema idadi hiyo ya shule imesaidia kutoa fursa kwa wanafunzi wengi kupata elimu nchini katika ngazi mbalimbali.  ”Hivi sasa kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015/2010 tunatekeleza mpango wa elimu bila ada kwa kutoa sh. Bilioni 24.4 kila mwezi”.

Amesema lengo la Serikali la kutoa kiasi hicho cha fedha kila mwezi ni kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata fursa bila vikwazo na  Wilaya ya Rufiji nayo inanufaika, ambapo imetengewa kiasi cha milioni 394.5 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Lengo la Serikali kutoa Elimumsingi Bila Ada ni kuleta ujumuishi kwa kuhakikisha watoto wote hususan wale ambao wanatoka katika familia zisizo na uwezo wanapata haki ya msingi ya kupata elimu.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuongezeka kwa ufaulu wa darasa la saba kumeleta changamoto ya uwepo wa miundombinu ya shule za sekondari hususan kwa kidato cha kwanza ambayo ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa sera ya Elimumsingi Bila Ada.

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengoalitumia fursa hiyo kuishikuru Serikalikwa kurejesha hali ya usalama na utulivu katika eneo la Rufiji na Kibiti.

Kardinali Pengoalisema kurejea kwa hali ya utulivu na usalama katika maeneo hayo kumemuondolea mzigo wa kiutendaji uliokuwa ukimuumiza kwa kuwa mapadri aliokuwa akiwapangia katika parokia za huko walikuwa wakisema ‘tumekosa nini’.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

HIKI NDIYO KIJIJI CHA AJABU ZAIDI DUNIANI...HAKINA KABURI HATA MOJA,KUZAA MARUFUKU!!


Kijiji cha Mafi Dove kilichopo kusini mwa nchi ya Ghana, chenye wakazi takribani 5000, lakini hakuna kati yao aliyezaliwa kijijini hapo kutokana na mila inayokataza kuzaliwa watoto.

Kama ilivyo kwa vijiji vingi kuwa na tamaduni zao, kijiji cha Mafi Dove kimekuwa na mila hii ambayo imegeuka kuwa mwiba kwa wanawake, kwani wanapokuwa wajawazito na kutaka kujifungua, hulazimika kuondoka kijijini hapo na kwenda kijiji cha jirani, ili aweze kujifungua mtoto wake na kisha kurudi.
Mwananchi wa kijiji cha Mafi Dove asimulia.

“Wakati mababu zetu walipokuja katika ardhi hii, sauti kutoka mbinguni ilisikika ikiwaambia hapa ni mahali patakatifu, hivyo ukitaka kuishi ni lazima ufuate masharti, sheria ya hapa ni hakuna mtu anayeruhusiwa kuzalia hapa”, alisikika moja wa wakazi wa kijiji hicho alipohojiwa na BBC.

Hiyo ni moja tu ya mila za ajabu zinazopatikana kijijini hapo, kwani zipo mila zingine ambazo pia wakazi wake wanazitekeleza mpaka sasa, ikiwepo kutofuga mnyama yeyote au hata ndege wa kufuga, na pia hawaruhusiwi kuchinja mnyama yeyote.

Lingine la kushangaza zaidi katika kijiji hicho ni kwamba hakina kaburi hata moja, kwani pia hawaruhusiwi kuzika wafu, hivyo mtu akifa hulazimika kwenda nje ya kijiji ili kuzika ndugu yake.

Mpaka sasa mila hizo zinaendelea kutekelezwa, huku baadhi ya wanawake wakilalamika kupata shida kubwa hususan juu ya mila ya kutojifungua kijijini hapo, kwani hulazimika kutembea umbali mrefu kwenda kijiji kingine kujifungua.
Share:

BINADAMU ALIYEPONZWA NA 'KULA SANA MISOSI' AKAJIKUTA ANA KILO 980

KEITH Martin raia wa Uingereza ni moja kati ya watu ambao wameweka historia ya kuwa na uzito usio wa kawaida na unene uliopitiliza.

Martini akiwa na miaka 42 alikuwa na kilo zisizopungua 980 na hakuweza kujigeuza alipolala alihudumiwa na watu wa fani tofauti tofauti zaidi ya 7 wakiwemo manesi na watu waliomsaidia usafi.

Akizungumza na jarida la North Sky huko nyumbani kwake Kaskazini mwa Uingereza Martin alieleza kuwa, "Najilaumu mwenyewe, siwezi kumlaumu yeyote ni kosa langu nilikuwa nakula mwenyewe, hakuna aliyeniwekea bunduki kichwani nilifanya mwenyewe" alieleza Martin.

Vyanzo vinaeleza kuwa Martin alifiwa na mama yake akiwa na miaka 16 tu baada ya hapo akaanza kula vyakula vya mafuta na sukari (junk food) kwa lengo la kujifariji hali iliyompelekea kuwa na uzito na unene uliopitiliza.

Hata hivyo Martin alifariki dunia mwaka 2014 akiwa na miaka 44 huku chanzo cha kifo chake kikielezwa kilitokana na tatizo la pumu.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
Share:

HUYU NDIYO MGUNDUZI WA VIDONDA VYA TUMBO...ALIMEZA BAKTERIA KUWEZA KUTAFUTA DAWA

Daktari Barry Marshall ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Nobel aliyoipata kutokana na kugundua chanzo cha vidonda vya tumbo kwa kufanya majaribio katika mwili wake.

Wataalamu wengi wa Afya miaka ya nyuma waliamini kuwa bacteria hawezi kuishi ndani ya tumbo la mwanadamu kutokana na joto pia tindikali na asidi iliyopo humo. Hivyo basi iliaminika kuwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo unatokana na mawazo au kutokula kwa muda mrefu.

Dkt. Barry akiwa na miaka 32 aligundua kuwa vidonda vya tumbo husambazwa na bacteria anayeitwa Helicobacter pylori na alipojaribu kuwashirikisha wataalamu wengine alipingwa na hakuna aliyeamini kuwa bacteria huyo anaweza kuishi katika tumbo la binadamu kutokana na mazingira ya tindikali.

Barry Hakukata tamaa aliendelea na majaribio ili kuweza kugundua dawa ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo na alipokwama ni jinsi ya kufanya majaribio, kwani taratibu hazikumruhusu kujaribu nadharia zake za bacteria anayepelekea vidonda vya tumbo. 

Daktari huyo alifanya maamuzi magumu ya kuwameza vimelea hao wajulikanao kama Helicobacter pylori, chini ya uangalizi wa rafiki yake aitwaye Robin Warren na baada ya wiki kadhaa alikuwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Hii iliwahadaha walimwengu wa wataalamu wa afya, na alipojaribu kutumia dawa alizoziandaa mwanzo hazikufanya kazi. Akiwa mgonjwa sana hatimaye aligundua antibayotiki inayotibu vidonda vya tumbo. 

Ilipofika mwaka 2007 alitunukiwa tuzo ya ya Nobel kwa ujasiri huo uliohatarisha maisha yake.
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

Share:

WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2018 WATANGAZIWA FURSA YA KUBADILISHA TAHSUSI(COMBINATION)

Serikali imetoa fursa kwa wanafunzi waliofaulu kidato cha nne mwaka 2018 na wanaotegemea kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo kwa mwaka 2019 kubadilisha Tahsusi(Combination).

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo Serikali ya Awamu ya Tano inawapa wahitimu hao fursa ya kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (Combination) na kozi mbalimbali walizozichagua kwenye fomu ya “F4-Selform.

Amesema Fursa hii itawawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeo ya Kidato cha Nne 2018 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania, NECTA.

“Kwa mara ya kwanza Wanafunzi watakuwa na uwezo wa kubadili machaguo au kuchagua kutoka Kidato cha Tano kwenda Chuo au Chuo kwenda Kidato cha Tano kwa kadiri ya mahitaji yake na jinsi alivyofaulu mitihani yake” alisema Jafo na kuongeza;

"Unajua wanafunzi hujaza Fomu za F4-Selform kabla ya kufanya mitihani sasa matokeo huweza kuja tofauti na vile alivyojaza lakini mwanafunzi huyo amefaulu hivyo ni wakati sasa kwa kubadilisha machaguo kwa kadiri ya ufaulu wake na anavyopendelea mwenyewe "

Aidha Waziri aliongeza kuwa : "Ofisi yangu imetoa fursa hii kwa wahitimu kubadili machaguo yao ili kutoa mwanya zaidi kwa mwanafunzi kusoma fani au Tahasusi itakayomwandaa kuwa na mtaalam fulani katika maisha yake ya baadaye kwa namna ambayo anatamani yeye mwenyewe au kwa kushauriwa na wazazi au walezi wake; Hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya wanafunzi hawakujaza kwa uhakika Tahasusi au Kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao."

Aliongeza kuwa zoezi la awali la kuingiza taarifa zilizo kwenye “Selform” za wanafunzi kwenye kanzidata ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI, kama zilivyojazwa wakiwa shuleni kabla ya kuhitimu limekamilika na sasa wanafunzi wataweza kufanya mabadiliko kwa njia ya mtandao, (online) na baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hii ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia kidato cha Tano na Kozi za Vyuo.

Waziri Jafo aliwakumbusha wahitimu wote  kuwa, endapo wanapenda kurekebisha machaguo ya Tahasusi na Kozi au kuhama kutoka Chuo kwenda Kidato cha Tano kulingana na ufaulu wao katika masomo wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa Selform unaopatikana katika anuani ya www.selform.tamisemi.go.tz na   maelekezo ya jinsi ya kufanya mabadiliko watayapata kwenye video ya mafunzo  inayopatikana kwenye tovuti ya TAMISEMI www.tamisemi.go.tz

Pia alifafanua kuwa Ili mhitimu aweze kuingia kwenye mfumo itabidi kutumia namba ya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2018, jina lake la mwisho, mwaka wa kuzaliwa na alama ya ufaulu aliyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa. 

Zoezi hili la kubadilisha Tahasusi litafanyika kuanzia tarehe 01/04/2019 hadi tarehe 15/04/2019.


Share:

Aliyekuwa mkurugenzi Takukuru apandishwa mahakamani na Kusomewa Mashitaka 8

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Kulthum Mansoor amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na makosa nane ikiwemo la utakatishaji fedha wa shilingi bilioni 1.4.

Kulthum amepandishwa kizimbani leo Ijumaa Machi 29, 2019 akitokea kituo cha polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam ambako alikuwa mahabusu toka jana Alhamisi alipokamatwa kwa tuhuma hizo.

Mshtakiwa amekosa dhamana kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpatia. 

Jana, Rais Magufuli akizungumza Ikulu mara baada ya kumuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mlowola alisema kuna mkurugenzi mmoja wa makao makuu Takukuru aliwauzia viwanja hewa wafanyakazi wenzake, lakini anashangaa hajapelekwa mahakamani hadi sasa.

“Wala sijapata taarifa kwamba hizo fedha amezirudisha kwa wafanyakazi aliowadhulumu. Wafanyakazi wanaumia, wanalalamika pembeni.

“Amewadanganya kwamba ana viwanja Bagamoyo, lakini mpaka leo hawajapewa,” alisema Rais Magufuli.

Alisema kashfa hiyo iliibuliwa tangu Balozi Mlowola alipokuwa mkurugenzi wa taasisi hiyo, lakini hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

“Suala hili lilianza tangu wakati wa Balozi Valentino, nikamuuliza huyu mbona harudishi fedha au hapelekwi mahakamani, akawa na kigugumizi, sasa na wewe usiwe na kigugumizi kwa sababu nafasi za ubalozi zimeisha.

 “Ndiyo maana huwa najiuliza hawa Takukuru huwa ni kwa ajili ya watu wengine, wao ‘hawaji-takukuru’ humo humo ndani?” alihoji. 


Share:

ATEMBEZEWA KICHAPO CHA MBWA KOKO AKIIBA SUTI YA MAREHEMU MOCHWARI

 Kizazaa cha aina yake kimeshuhudiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kakamega nchini  Kenya baada ya mwanaume mmoja kufumaniwa na kupewa kichapo cha mbwa msikitini kwa tuhuma ya kuiba nguo za marehemu. 

Tukio hilo limetokea Alhamisi, Machi 29,2019 ambapo Mwanamume aitwaye Bastanik Wande kutoka kijiji cha Indangalasia alifumaniwa na ndugu wa marehemu akiiba nguo za marehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini humo.
 
Inaelezwa kuwa mshukiwa huyo ambaye ni jamaa wa karibu wa marehemu huenda alishirikiana na watu wasiojulikana kupanga njama ya kumuua ndunguye kwa njia tatanishi. 

Inadaiwa familia ilifanya tambiko ili kuwatesa wauaji na katika kujikinga kutokana na nuksi za aina yoyote ambazo huenda zikamwandama, hivyo Wande aliamua kuiba suti ya marehemu. 

Aidha familia ya marehemu ilikuwa imechukua hatua ya kumtenga mshukiwa katika mipango ya mazishi na walimwonya dhidi ya kugusa kitu chochote cha marehemu. 

"Tunashangaa kama anadai hakuhusika na kifo hicho basi mbona alikuwa akichukua nguo zake? Tulimwonya dhidi ya kuchukua mali yoyote ya marehemu na tumejitolea kusimamamia gharama zote za mazishi bila usaidizi wake, " alisema mmoja wa watu wa familia hiyo.

 Lakini Wande aliyakana madai hayo na kutaka mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na serikali kuingililia kati na kumnasua kutoka kwa mtego huo.

 "Watu wamenivamia na kuniumiza, nilikuwa nimeenda mochwari kumtoa ndugu yangu na nimeshtuka kuwaona watu wamenizingira na wakaanza kunipiga na kuniumiza, naiomba serikali kuingililia kati na kunisaidia kwani nahisi watu hao wana nia mbaya kwa sababu wametishia kuzichoma nyumba pamoja na mali zote za marehemu." Wande alisema huku akiwa na maumivu mengi. 

Haijabainika kisa hicho kiliishia wapi ila vurugu hilo liliendelea kwa muda kabla ya kila mtu kwenda zake na kuuacha mwili wa marehemu.

 Hadi habari hii ikiandikwa, hamna ripoti kamili kutoka kwa familia ya marehemu kuhusu mipango baada ya kisa hicho kilichowashtua wengi katika hospitali hiyo. 
Chanzo -  Tuko
Share:

Breaking News: Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Maombi ya Joshua Nassari Kupinga Kuvuliwa Ubunge

Mahakama Kuu kanda ya Dodoma imetupilia mbali maombi ya Joshua Nassari ya kupinga kitendo cha Spika wa Bunge kumvua ubunge wa Arumeru Mashariki kutokana na utoro bungeni

Akisoma maamuzi hayo leo Ijumaa Machi 29, 2019 Jaji wa Mahakama Kuu Dodoma, Latifa Mansour   ametumia kifungu cha 5 (4) kuwa Nassari alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa Katibu wa bunge wala si kama alivyofanya.

Kifungu kingine kilichombana Nassari  ni cha kanuni ya 146 (2) kwamba alijifukuzisha mwenyewe kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bunge bila taarifa.


Share:

Picha : SAFARI YA MWISHO YA MWANDISHI WA DW CHARLES OLE NGEREZA JIJINI ARUSHA

 Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoani Arusha Cloud Gwandu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha- APC) Charles Ole Ngereza.
 Mweka hazina wa Klabu ya  waandishi wa habari Mkoani Arusha Pamela Mollel akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya mwenyekiti wa (APC)
 Mratibu wa APC Arusha Seif Mangwangwi akilia kwa huzuni mara baada ya mwili wa Charles Ngereza ulipowasili waliopo pembeni yake ni baadhi ya waandishi wa habari wakiwa msibani. 
 Baadhi ya Viongozi wa kanisa la Sent-James Anglican PASTOR, MICHAEL GILAISI  QAWOGA  UIJILISTI NA UMISSION wakiongoza ibada nyumbani ya maziko ya aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Idhaa ya Kiswahili DW  Charles Ole Ngereza.
Watoto wa marehemu Charles Ngereza, Faith na Fransis wakiwa kanisani.
 Mary Mwita Mke wa marehemu Charles Ngereza akiwa kanisani ibada ikiwa inaendelea.
 Mke wa Marehemu Charles Ngereza Mary Mwita akiwa ibadani katika kanisa la Anglikana Sent. James Arusha
Mjane Mary Mwita akielekea Jeneza kuuaga mwili wa mume wake kwa mara ya mwisho
 Waandishi wa habari wakiwa msibani katika viwanja vya shule ya sekondari Baraa Jijini Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari Jijini Arusha wakielea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa katika kata ya baraa ambapo shughuli ya  za Ibada na taratibu zingine zinafanyika. 




Na Vero Ignatus, Arusha
'Kwaheri Charles Ngereza  Kiongozi wetu' Haya ni maneno ya Wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Arusha wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao  kwa mara ya mwisho.

Marehemu Charles Ngereza hadi anafariki  alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa  Arusha ambapo aliwahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali ikiwemo Radio Five ya Jijini Arusha,Itv &Radio one hadi mauti inamkuta alikuwa mwakilishi wa Idhaa ya Kiswahili ya DW Ujerumani.

Ameshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2005 hadi umauti ulipomkuta, Katika uhai wake Charles Ngereza amekuwa  akifanya kazi kwa uadilifu na siku zote amekuwa mtu wa kushauri zaidi badala ya kuhoji, alisema Claude Gwandu mwenyekiti wa APC.

Akiwa mmoja wa wanaounda kamati ya utendaji  ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Ngereza amekuwa kiunganishi kikubwa kati ya waandishi wa habari wa ndani na nje na kwa hapa tutamkumbuka zaidi katika kutoa ushauri na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Siku zote Ngereza amekuwa akiamini katika diplomasia, hata pale mambo yanapokwama amekuwa msaada mkubwa kuhakikisha suluhisho inapatikana na katika kamati zetu pale ndani ya APC amekuwa akishirikishwa kwenye kamati  mbalimbali ikiwemo ile kamati ya  nidhamu na maadili pale mambo yanapoonekana hayaendi sawa.

"Sisi kama wanahabari wa Mkoa wa Arusha tunasema tumempoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya habari na kwa msemo wa sasa hivi tunaweza kusema tumepoteza ‘jembe’ na hakika pengo lake halitazibika japo mambo ya Mungu ni mengi tutaendelea kumuomba yeye ili aweze kupatikana mfano wa Ngereza",alisema mweka hazina wa APC Pamela Mollel. 

"Ngereza alikuwa ni zaidi ya rafiki kwa kuwa alikuwa akishiriki hata kwa mambo ya kijamii ndani ya APC tumekuwa na miradi ya kijamii ikiwemo kupanda miti katika shule za kata, Ngereza amekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi hizi ili kuona jamii na yenyewe inafaidika na uwepo wa Chama wa waandishi wa habari mkoa wa Arusha.

Wapendwa kwa ufupi nipende tu kusema yapo mambo mengi sana ambayo Ndugu yetu, kaka yetu Charles Ngereza ameyafanya lakini wacha tuishie hapa kwa ufupi sababu hata kama tukisema tuendelee kuyasema hapa hatutaweza kuyamaliza,kikubwa sisi kama wanahabari Mkoa wa Arusha, wafanyakazi wenzake tunaahidi tutaendelea kuyaenzi yale yote aliyoyaacha ili kuendeleza umoja na ushirikiano aliokuwa akiusisitiza.

Tunaamini Charles amefariki mwili lakini roho yake bado ipo mioyoni mwetu, kwa kuwa hata wakati anaugua anapambania afya yake kila siku tulimsihi na kumpatia faraja na hakika aliamini katika Mungu.

Tuliamini alipokwenda India kupata matibabu atarejea akiwa mzima na  kuendelea katika mapambano yetu ya kila siku lakini alirejea akiwa ameendelea kudhoofu",alisema Mustafa Leu Katibu wa Apc

Akiongoza ibada ya mazishi mchungaji wa kanisa la Anglikana ametoa angalizo kwa ndugu jamaa na marafiki kuwa makini katika kipindi hicho cha majonzi na kuwataka wasijesababisha msiba mwingine baada ya huo kwa maneno yasiyo ya hekima watakayoyatoa kwa mjane na watoto walioachwa.

"Mara nyingi msiba unapotokea ndipo watu wengi hijitokeza haswa ndugu na kuanza kuzungumza hovyo bila hekima kaa kimya ,wacheni kuzungumza hovyo, wapendwa msimpe shetani nafasi kwenye misiba ya watu"

Akitoa salamu za rambirambi mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Lengai Ole Sabaya amesema kuwa marehemu alikuwa mpatanishi alikuwa hapendi kuona ugomvi unatokea. 

Kama wanahabari ndugu jamaa na marafiki zake niwape pole  tamaa tuliamini kila jambo linaletwa kwa mapenzi ya Mungu, tulikaa na kushauriana namna nyingine ambapo mwenzetu ataweza kupata tiba lakini wakati tukiwa kwenye mikakati hiyo Charles alizidiwa na kukimbizwa hospitali na baadae alifariki dunia.

 Inatia uchungu sana lakini hamna namna, tunasema yote ni Mapenzi ya Mungu. Nenda Charles tuko nyuma yako.
Share:

Mwanasheria Wilaya Ya Makete Awaonya Wananchi Wanaojihusisha na UCHAWI Kwa Kizingio Kwamba Hakuna Sheria

Na Amiri Kilagalila
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe Godfrey Gogadi amewataka wananchi wilayani humo kuachana na vitendo vya kishirikina ili watumishi wa serikali wakiwemo waalimu waweze kufanya kazi zao.

Gogadi amesema ipo sheria ya uchawi hapa nchini na endapo itathibitika kwa mtu yeyote atachukuliwa hatua za kisheria na kuwaasa wananchi kuachana na vitendo hivyo ambavyo havina faida.

Vitendo vya kishirikina Vimekuwa vikiendelea katika baadhi ya vijiji  wilayani makete na kusababisha watumishi wakiwemo waalimu mara kwa mara kujikuta wakilala nje ya nyumba zao huku wengine wakiwakuta nyoka katika nyumba zao.

Katika Mkutano wa mkuu wa wilaya hiyo VERONICA KESSY na wananchi wa vijiji vya Mbalatse na Lupombwe,mwanasheria huyo ameamua kuwakumbusha wananchi uwepo wa sheria dhidi ya vitendo vya ushirikina pindi mtu yeyote atakapobainika.

“Ndugu zangu tunasheria yetu ya uchawi ambayo inakataza matendo haya na yale ni kosa la kijinai kwa hiyo msije mkafikiri kwamba kwenye uchawi hakuna sheria kama itathibitika pasipo shaka kuna mtu anajihusisha na haya maswala taratibu za kisheria zitachukuliwa, kwa hiyo ndugu zangu tubadilike kwa kuwa uchawi hauna faida na kama unafaida kwanini tusingefanya maji yafike huku”alisema Gogadi

Mkuu wa wilaya hiyo Mh Veronica Kessy amesema inashangaza mpaka sasa wananchi kuendelea kukumbatia vitendo hivyo ambavyo vinatia aibu wilaya ya Makete ndani na nje ya wilaya hiyo

“Mnanisikitisha na kudhihirisha kwamba kimaendeleo bado mkoa nyuma,kwa ustaarabu tu wenye michezo hii muiache kwasababu mnafahamika na wenzenu wanawafahamu na majina yenu tunayo na yule mama mmekataa kumrudisha sijui mlishamla nyama,watu wanakazana kuleta maendeleo lakini wengine wanaimani za kipepo tutapataje maendeleo”alisema VERONICA KESSY

Aidha amewaomba viongozi wa dini kukemea vitendo hivyo kwa kuwa moja ya kazi ya madhehebu ya dini ni kurekebisha mienendo ya waumini .

“Niombe sana madhehebu ya dini kila mtu anajua mungu yupo lakini wengine wanavibuli sasa wachungaji ndio kazi yenu tunawaomba sana maana hili linatuchafua Tanzania nzima ni Makete tunatia aibu”

Mmoja wa mwananchi aliyekuwepo kwenye mkutano huo amewaomba wananchi wenzake wanaofanya vitendo vya kishirikina kuviacha kwa kuwa havina faida yeyote huku akielezea machungu aliyonayo ya kumzika wifi yake aliyefariki dunia kwa kukatwa mapanga kwa madai ya kujiusisha na vitendo vya kishirikina.

“Kweli mimi naomba swala la uchawi kama kuna mtu yupo hapa naomba mviache kabisa, mimi hapa nilitoka juzi kisasapu msibani wifi yangu wamemkata na mapanga wanahisi alikuwa ni mchawi”alisema Mwananchi


Share:

Waitara: Viongozi Jenganeni Mahusiano Mazuri Na Waandishi Wa Habari Kwani Ni Nguzo Muhimu Kwa Maendeleo Ya Taifa

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amewataka viongozi kutoka ngazi mbalimbali  kujenga Mahusiano Mazuri na waandishi wa habari kwani ndio nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
 
Waitara amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau wa elimu   katika kikao  cha Maandalizi ya Mashindano ya Umoja wa Michezo  shule za Sekondari ,Tanzania [UMISETA] unaodhaminiwa na Coca cola.
 
Mhe.Waitara amesema waandishi wa habari wanatakiwa kupewa kipaumbele katika mambo  ya  Msingi ya Serikali vivyo hivyo katika mashindano hayo ya UMISETA ni vyema vyombo vya habari vikatumika kuibua vipaji vya wachezaji mbalimbali na serikali za mitaa  kuwawezesha wanahabari katika kutekeleza majukumu yao kwani ni nguzo muhimu.
 
“Sio kwamba mpaka aje Mkurugenzi,Waziri  No.hata wewe unaweza ,mwanafunzi kafanya vizuri tangaza hiyo,shule za kata zinatoa matokeo mazuri tangaza hiyo.Kuna Ofisi zingine zina pwaya  ni mzigo  akimwona mwanahabari hata  ushirikiano hatoi yeye yupoyupo tu.
 
"Hivyo katika Mashindano haya tumieni vyombo vya habari,kupitia blogs,redio,magazeti ,vyombo vya habari vyote kuhamasisha michezo.”
 
Aidha waitara ameagiza Maafisa elimu wilaya ni mikoa kufuatilia somo la michezo kufundishwa kwa nadharia na vitendo,viwanja vya michezo kufufuliwa,kusimamia makusanyo ya fedha za michezo  na nyimbo za uzalendo ikiwa ni pamoja na wimbo wa Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki kuimbwa hasa kwenye mashindano hayo.
 
“Unakuta mtu mzima na ofisi yake ukimwambia imba anasingizia ana kikohozi ,tatizo  sio kikohozi bali haujui huo wimbo.hivyo tuhamasishe nyimbo za uzalendo kwa Taifa Letu.”
 
Katika kuboresha na Kutunza Mazingira Mhe.Waitara ameagiza kila mwalimu apande mti  mmoja wake shuleni na kila mwanafunzi miti miwili nyumbani na shuleni.
 
Mkurugenzi Idara ya Elimu Tanzania,Julius Nestory amesema watashirikiana na wadau mbalimbali katika kukuza vipaji vya wanafunzi shuleni huku akipongoza Copa  Coca Cola kwa  kudhamini Mashindano ya UMISETA.
 
Kwa Upande wake ,Mkurugenzi wa Mambo ya Umma na Mawasilino ,Coca Cola  Haji Mzee Ally amezitaja mikoa atakayoanza katika kuzindua Mashindano ya UMISETA 2019 ni Tabora,Manyara na Ruvuma huku akisema kuwa kutakuwa na mkakati kabambe wa kuzipa zawadi shule zitakazokusanya  takataka  za plastiki  za kampuni yoyote katika kuhakikisha utunzaji wa Mazingira .
 
Mwenyeji wa Mashindano UMISETA 2019 ni Mkoa wa Mtwara na yanatarajia kuanza mwezi ujao.


Share:

MNEC SALIM ASAS ACHANGIA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYERERE


Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akiongea na wanafunzi na wazazi wa shule ya sekondari ya Nyerere wakati wa maafari ya kidato cha sita akimwakirisha mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi. 
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akimkabidhi mkuu wa shule ya sekondari ya Nyerere fedha alipewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha
Mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa ajili ya kuasidia ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule hiyo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi,wazazi mbalimbali pamoja wanafunzi wa kidato cha sita. 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
MJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas amechangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyerere iliyopo katika kata ya migoli mkoani Iringa

Akimwakilisaha MNEC Salim Asas wakati wa mahali ya kidato cha sita katika shule hiyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu na tayari ameona jitihada zinazoendelea hivyo kiasi cha shilingi milioni mbili alipewa na MNEC basi zitasaidia katika ujenzi huo.

“Nimepewa pesa hizi na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas nije niwaletee kwa niaba yake hivyo nimezifikisha salama na nyie mzitumieni katika kumalizia ujenzi wa nyumba hizo za walimu ili walimu waishi vizuri” alisema Baraza

Baraza alisema, mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas anayependa kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali ndio maana katika shule hiyo amechangia zaidi ya mara moja kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu katika shule hiyo.

“Mmesema hapa wenyewe kuwa mara kadha amekuwa akiwasaidia kuchangia maendeleo katika shule hii na leo kanituma niwaletee hizi pesa kwa ajili ya mchango wake kwenye shule hii kwa lengo la kuboresha taaluma kwa wanafunzi wa hapa”, alisema Baraza

Aidha Baraza aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wasoma sana na kufaulu mitihani iliyopo mbele yao na kurudisha fadhila kwa walimu na wazazi wao waliowalea na kuwafundisha hadi hapo walipofika.

“Hakuna kitu kizuri kwa mwanafunzi kufaulu mtihani na kusonga mbele hiyo maana walimu wanawafundisha mkiwa shuleni lakini mkiwa nyumani wazazi wenu wanatumia gharama kubwa kuwa somesha huku wakitegemea kupata matokeo chanya ya mtihani wenu wa mwisho”, alisema Baraza 

Baraza aliongeza kwa kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kusimamia kikamilifu malengo waliyojiwekea ili kuifikia ndoto ambayo wamekuwa nayo kwa miaka mingi ya kupata au kufika maisha bora ambayo kila mwanadamu anatamani kuyafikia.

Lakini Baraza aliwapongeza walimu na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kwa kupata matokeo mazuri kila mwaka na kusaidia kukuza taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo na kuwaandaa vijana ambao watakuaja kulisaidia taifa hapo baadae.

Awali akisoma taarifa ya shule hiyo mkuu wa shule Laurent Manga alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya umaliziaji wa nyumba ya walimu inayojengwa kwa nguvu za wazazi,wanafunzi na serikali.

“Mgeni rasmi sis hapa tunaupungufu wa bati mia moja na ishirini,saruji mifuko mia tatu,mbao mia moja themenini na tisa pamoja na misumari kilo hamsini,hivyo ndio vinakwamisha umaliaji wa nyumba hiyo ya walimu” alisema Manga

Manga alisema, uongozi wa shule uliweka malengo yake ya kuborsha makazi ya walimu kwa kuanza kujenga nyumba tano ambazo mpaka sasa nyumba tatu zenye uwezo wa kuhifadhi walimu sita zimekamilika na nyingine moja mafundi wapo kazini na ya mwisho ikiwa hatua ya renta.

Hata hivyo Manga alimalizia kwa kutoa shukrani kwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa mchango wake wa kimaendeleo ambao amekuwa akiufanya katika shule hiyo na mahali pengine.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger