Saturday 30 March 2019

MWANAMKE 'ALIYEFARIKI' MWEZI DISEMBA AJIFUNGUA MTOTO

Mtoto akiwa kwenye mashine ya kumpatia joto

Mwanamke mmoja mwenye miaka 26 amejifungua mtoto wa kiume siku ya Alhamisi licha ya kutangazwa kuwa ni mfu toka Disemba.

Mwanamichezo wa kimataifa, bi Catarina Sequeira alipatwa na shambulio kali la pumu akiwa nyumbani kwake.

Bi Sequeira amezikwa Ijumaa, siku moja baada ya mtoto kutolewa tumboni mwake.

Mtoto huyo aliyepewa jina la Salvador, amezaliwa baada ya kukua kwa wiki 32 tumboni mwa mama yake kwa wiki 32, na sasa yupo chini ya uangalizi kwenye hospitali ya watoto.

Hii ni mara ya pili nchini Ureno kwa mtoto kuzaliwa kutoka kwa mama ambaye ni 'mfu wa ubongo'.

Sequeira ambaye alikuwa mwanariadha wa mbio za mitumbwi amekuwa akisumbuliwa na pumu toka utoto wake.

Aliwahi kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa wakati wa uhai wake.

Shambulio lililochukua uhai wake lilimpata akiwa na mimba ya wiki 19, hali iliyomfanya kupoteza fahamu. Siku chache akiwa chumba cha wagonjwa mahututi hali ilizidi kuwa mbaya na akatangazwa kuwa 'mfu wa ubongo' Disemba 26. Madaktari wakamuwekea mashine ya kusaidia kupumua ili mtoto tumboni aweze kuishi. Mashine hiyo iliwekwa kwa siku 56.
Sheria ya kutoa viungo yaamua 'kesi' hii

Madaktari wanasema malengo yalikuwa ni kusubiri mpaka Ijumaa ambapo ujauzito huo ungefikisha wiki 32, lakini mfumo wa hewa wa mama huyo uliharibika ghafla na kulazimisha upasuaji ufanyike Alhamisi ili mtoto atolewe.

Wiki 32 ndiyo kipindi ambacho madaktari wanansema mtoto anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuishi.
Mkuu wa kitengo cha maadili cha hospitali hiyo, Filipe Almeida, ameelezea kuwa maamuzi ya kumuacha mtoto aendelee kukuwa kwenye tumbo la mama yake yalifikiwa kwa pamoja na familia ya mama huyo, kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kipinga kwa maandishi sheria ya kutoa viungo vyake baaa ya kufariki.

"Kuwa mtoaji wa viungo si tu kuwa na nafasi ya kutoa ini au mapafu, lakini pia inahusu kuwa na uwezo wa kujitoa ili mtoto wako aishi," Almeida ameuambia mtandao wa Observador.

Baba wa mtoto huyo alitaka azaliwe, kama ilivyokuwa kwa familia nzima ya marehemu.

Hata hivyo mama wa Sequeira, bi Maria de Fátima Branco, ameiambia televisheni moja ya Ureno kuwa alimuaga binti yake Disemba 26, na uamuzi wa kumuacha mtoto huyo azaliwe umefikiwa baada ya baba yake, Bruno, amekuwa akitaka kuwa baba kwa muda sasa.

Mtoto huyo amezaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.7kg na anatazamiwa kubaki hospitali kwa walau wiki tatu zijazo.

Mwaka 2016, mtoto mwengine ajulikanaye kama, Lourenço, alizaliwa jijini Lisbon baada ya kukaa kwa wiki 15 baada ya mama yake kufariki.
Chanzo - BBC
Share:

JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKAMATA WAGANGA WA JADI 19 WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI




Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limedai kuwakamata waganga wa Jadi 19 ambao wamekuwa wakipiga ramli chonganishi na kusababisha kuendelea kuwepo kwa matukio ya mauaji ya wananchi ambayo yamekuwa yakitokana na imani potofu za kishirikina.


Hayo yamebainishwa leo Machi 30,2019 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema katika misako mbalimbali ambayo inaendelea kufanyika na jeshi hilo ili kukabiliana na uhalifu pamoja na kupunguza mauaji yatokanayo na imani potofu za kishirikina, wamefanikiwa kuwakamata waganga hao 19 pamoja na watuhumiwa wengine 16 wakiwa na vitu vya wizi na madawa ya kulevya.

“Waganga hawa wa jadi tumewakamata pia wakiwa na nyara za serikali ambazo hutumia kupigia ramli chonganishi ambayo ni mikia ya nyumbu, ngozi ya kenge, ngozi ya simba, kucha za simba, mayai ya mbuni, kichwa cha kenge, jino la ggiri, pamoja na bundi mmoja ambaye tukimtoa hapa atakimbia,”amesema Kamanda Abwao.

“Pia katika msako mwingine tumefanikiwa kukamata watuhumiwa saba (7) wakiwa na mali za wizi ambazo ni pikipiki 2, mashine 3 za kunyolea saluni za kike, Tv 5, Radio Sabwoofer  5, Deki 5, King’amuzi kimoja, komputa moja, Friji moja, baiskeli 3, pamoja na watuhumiwa wengine tisa (9) wanawake wakiwa na madawa ya kulevya aina ya bangi uzito wa kilogramu 35 na heroine gramu 195,”ameongeza.

Aidha Kamanda amesema watuhumiwa wote hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi za Kisheria, ili liwe fundisho kwa watu wengine ambao hawataki kuzitii sheria za nchi.

Pia ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga, kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa dhidi ya waharifu, wakiwamo na wanganga wa jadi ambao wamekuwa wakitoa tiba kwa kupiga Ramli Chonganishi, ili mkoa ubaki kuwa salama kwa kudumisha amani na utulivu.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga (ACP) Richard Abwao akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa juu ya misako ambayo wanaendelea kuifanya ya kukamata wahalifu, wauza madawa ya kulevya pamoja na waganga wa Jadi ambao wamekuwa wakitoa tiba kwa kupiga ramli chonganishi na kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia kutokana na imani za kishirikina.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga (ACP),Richard Abwao akionyesha nyara za serikali ambazo zimekuwa zikitumiwa na Waganga wa Jadi kinyume na Sheria na kutoa tiba kwa kupiga ramli chonganishi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao akionyesha dhana ambayo hutumiwa na waganga wa Jadi kutibia wateja wao na kupiga ramli Chonganishi inayo sababisha mauaji ya kishirikina kwa watu wasio na hatia wakiwamo wazee.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao, akionyesha madawa ya kulevya aina ya Bangi Kilogramu 35 ambayo wameyakamata kutoka kwa wanawake 9 waliokuwa wakifanya biashara hiyo zikiwamo na Heroine Gramu 195.

Nyara za serikali pamoja na dhana ambazo hutumiwa na Waganga wa Jadi kupigia ramli chonganishi.

Nyara za serikali pamoja na dhana ambazo hutumiwa na Waganga wa Jadi kupigia ramli chonganishi.

Afisa wa jeshi la polisi akionesha nyara za Serikali pamoja na dhana ambazo hutumiwa na Waganga wa Jadi kupigia Ramli Chonganishi.

Nyara za Serikali pamoja na dhana ambazo hutumiwa na Waganga wa Jadi kupigia ramli chonganishi.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakichukua matukio ya wahalifu waliokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo wakiwamo na Waganga wa Jadi ambao hutoa tiba kwa kupiga ramli chonganishi inayosababisha mauaji ya kishirikina kwa watu wasio kuwa na hatia.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiendelea na uchukuaji wa matukio.

Vitu vingine vya wizi vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi.

TV pamoja na Pikipiki ya wizi ambayo imekamatwa na Jeshi la Polisi SANLG yenye namba za usajili MC 187 BEM.

Vitu vingine kama unavyoona vikiwa vimekamatwa katika msako huo wa Jeshi la Polisi ndani ya siku nne kwa mkoa mzima ambapo zoezi hilo ni endelevu ili kuhakikisha mkoa unabaki kuwa salama.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga (ACP) Richard Abwao, akitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo, kuacha Tabia ya kupenda kwenda kutibiwa kwa Waganga wa Jadi, bali waende kwenye huduma za kiafya kupatiwa matibabu sahihi na siyo kwenda kupigiwa Ramli Chonganishi.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

Live | Magufuli Akiwatunuku Kamisheni Maofisa Wapya JWTZ

Live | Magufuli Akiwatunuku Kamisheni Maofisa Wapya JWTZ


Share:

Mbowe Kuongoza Kamati Kuu ya CHADEMA Leo

Kamati Kuu ya chama kikuu  cha upinzani nchini (Chadema) leo inakutana ili kupokea taarifa na kujadili mwenendo wa hali ya siasa nchini.
 
Taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya chama hicho imeeleza kuwa, kikao hicho ni cha siku moja na kilichofanywa kwa mujibu wa Katiba ya Chadema toleo la mwaka 2016.

Kikao hicho kitaongozwa na Mbowe, ikiwa ni baada ya kukosa vikao kadhaa kutokana na kuwekwa rumande katika Gereza la Segerea tangu Novemba mwaka jana mpaka alipopata dhamana tarehe 7 Machi 2019.

Kazi zinazotarajiwa kufanywa na kamati hiyo ni pamoja na kupokea taarifa na kujadili mwenendo wa kisiasa nchini, na kisha kuchukua mwelekeo baada ya mjadala wa taarifa hiyo.




Share:

JINSI KAZI ZINAVYOUA NA WATU NA HAWAJALI

Jeffrey Pfeffer anaposema kuwa ''kazi zinawaua watu na hakuna anayejali,'' hasemi kwa njia ya mafumbo.

Anasema kwa hakika kabisa kutokana na utafiti alioufanya kwa miongo kadhaa, nchini Marekani na duniani kwa ujumla.

Profesa Pfeffer kutoka shule ya biashara ya Chuo cha Stanford na mwandishi na mwandishi msaidizi wa vitabu 15 kuhusu muundo wa kampuni na masuala ya uongozaji rasilimali watu, ametoa hoja katika kitabu chake cha hivi karibuni kiitwacho , ''Kufa kwa ajili ya Mshahara'' Jinsi mifumo ya kazi inavyoathiri na hata kusababisha kukatisha maisha ya watu.

Katika kitabu hicho anazungumzia tuko la Kenji Hamada, mwenye miaka 42 aliyekufa kwa mshtuko wa moyo akiwa kwenye dawati lake kazini jijini Tokyo.Nilifanya kazi saa 72 kwa wiki na ilikua inanichukua saa mbili kufika kazini.

Kabla ya kifo chake, alifanya kazi siku 40 mfululizo bila kupumzika na mjane wake anasema Kenji alikuwa na msongo mkubwa

Huu ni moja kati ya mifano iliyokuwa kwenye chapisho lake, ambapo mwandishi anaeleza madhara ya mfumo wa kazi ambao wakati mwingine ''si ya kibinaadamu'' kutokana na majukumu makubwa ya kazi.

Kwa mujibu wa ushahidi uliowekwa na Pfeffer,nchini Marekani, asilimia 61 ya wafanyakazi wanaona kuwa msongo umewafanya waumwe na asilimia 7 wanasema walilazwa kutokana na sababu zinazohusiana na kazi.

Makadirio yake ni kwamba msongo una uhusiano na vifo vya wafanyakazi 120,000 wa Marekani.Wafanyakazi hupoteza maisha kutokana na majukumu mengi ya kazi

Kwa mtazamo wa kiuchumi, msongo umewagharimu waajiri zaidi ya dola za Marekani 300,000 kwa mwaka nchini Marekani.

Katika kitabu chako umeeleza kuwa kuna mfumo wa ufanyaji kazi unaowaua watu.Ni ushahidi gani ulionao kuhusu hili na ni kwa jinsi gani mfumo wa kisasa wa ufanyaji kazi unawaathiri waajiriwa?

Kuna ushahidi wa madhara ya kiafya.Saa nyingi za kufanya kazi,kupunguzwa kazi, kukosa bima ya afya, masuala ya kiuchumi, migogoro kwenye familia na maradhi.

Kazi sasa imekua si ya kibinaadamu.Kwa upande mwingine, makampuni yameacha kuwajibika kwa ajili ya wafanyakazi wao.

Lakini changamoto za kiuchumi zimeongezeka, hofu ya kukosa ajira pia inaongezeka.

Katika Benki za uwekezaji, kwa mfano, kuna namna ya ufanyaji kazi, unakwenda nyumbani kwako kuoga na kurejea ofisini.

Katika mfumo huo, waajiriwa wengi huingia katika uraibu wa madawa, kwa sababu wanaishia kutumia Cocaine na madawa mengine ili wawe macho.

Mfanyakazi wa kiwanda, rubani wa ndege, mwendesha lori, wana idadi ya saa za kufanya kazi.

Lakini kuna kazi nyingine hakuna saa maalumu za kazi.

Nchini Marekani, sababu ya tano ya vifo ni sehemu ya kazi.

Lakini nani anawajibika kwa vifo hivi?

Waajiri na serikali zinawajibika kwa kutochukua hatua yoyote kuhusu suala hili.

Ni kazi kubwa tunapaswa kufanya kitu kwa ajili ya kukomesha hili.Lakini hatutaweza kufanya chochote kama mtu mmojammoja.

Kama unataka kutatua tatizo yapaswa kuwa katika utaratibu ambao utatoka kwa mtindo wa sheria.

Mazingira mabaya ya kazi husababisha maradhi kama vile sukari na shinikizo la damu.

Lakini tukizungumzia gharama,makampuni yanaweza kuleta hoja kuwa kufanya mabadiliko katika mfumo wa kazi kutaathiri kipato cha kampuni.

Hii si kweli, anasema Profesa Pfeffer.''Tunajua kuwa watu walio katika msongo wa mawazo wako katika nafasi kubwa ya kuacha kazi''.Tunajua kuwa wafanyakazi wasio sawa kisaikolojia hawawezi kuizalishia kampuni inavyopaswa''.

Alitolea mfano kuwa inafahamika kuwa Marekani na Uingereza zaidi ya 50% ya siku za kazi hupotea kwa sababu ya wafanyakazi kutokuwepo kutokana na msongo wa kazi.

Hivyo kuna athari kubwa kwa mfanyakazi mgonjwa anayekwenda kazini na asifanye kazi kama anavyotakiwa.Hali hii huigharimu kampuni.Wafanyakazi wanapaswa kuzijali afya zao

Wafanyakazi wanapaswa kujijali

Kwa upande wa wafanyakazi, Profesa ameandika kuwa watu wajijali.Lakini ameulizwa swali kuwa itakuwaje ikiwa muajiriwa akadai kuboreshewa mazingira ya kazi na kuna uwezekano akaishia kufukuzwa?

Je mazingira ya kazi yatabadilishwaje?

Profesa anasema, kwanza waajiriwa wanapaswa kujali afya zao.

Ikiwa unakwenda kazini, mahali ambapo huwezi kuoanisha maisha ya kazi yako na familia, unapaswa kuacha kazi hiyo.

Jambo jingine ni kwamba watu wanapaswa kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa.
Chanzo - BBC
Share:

RADI YABOMOA NYUMBA NA KUUA MTU RUKWA

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 30




Share:

Friday 29 March 2019

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatoa tahadhari ya mvua nchini

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya siku tano ya kunyesha mvua kubwa inayoweza kusababisha athari ikiwemo mafuriko.

 Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, mvua hizo zinatarajiwa kuanza kunyesha leo Ijumaa Machi 29 hadi Aprili 2, 2019 na kwamba zinaweza kuleta athari kwenye makazi ya watu.

Mvua hiyo inatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

Pia zinaweza kuleta shida katika usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii. Mamlaka hiyo imesema kuanzia leo hadi Machi 31, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na Morogoro.

Imeeleza kuwa Aprili Mosi hadi Aprili 2, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

TMA imeshauri Menejimenti ya Maafa na watoa huduma za dharura pamoja na wadau wengine kuchukua hatua za kuweka mipango stahiki kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.


Share:

KUTANA NA MWANAMKE ANAYEFANYA MAPENZI NA MIZIMU..ADAI ANASIKIA RAHA KULIKO KUFANYA NA BINADAMU WA KAWAIDA

Anaitwa Amethyst Realm Mwanamke Kutoka Uingereza, Amewahi lalamika katika Kipindi cha Televisheni cha 'This Morning' cha ITV ya Uingereza kwamba Amefanya Mapenzi na zaidi ya Mizimu 20.

Anasema Kisanga Kiliamza Mwaka 2005 Akiwa na Miaka 15 Ambapo yeye Pamoja na Familia yake Walipohamia Katika Nyumba Mpya na Baada ya Siku chache akaanza Kuhisi Mtu Anamshikashika Usiku Huku Hamuoni na Kupelekea kufanya nae Mapenzi, na Hali hiyo iliendelea Kumtokea Kwa Miaka Mingi.

Anasema Ilianza kama Nguvu fulani hivi Inampapasa, Baadae Akawa anaona Kabisa Anahemewa Mihemo Maeneo ya Shingoni na Anashikwashikwa Sehemu za Mwili wake Usiku bila Kumuona anaemshika na Baadae Wanafanya Mapenzi.

Hali hii anasema Ilimtokea Kwa Miaka Mingi hadi Siku Moja Alipomtembelea Mpenzi wake, na Mpenzi Wake Alipokua Anarudi Nyumbani Usiku Alikuta Kivuli Kinakimbia Kupitia Dirishani na Akahisi Alikua na Mwanaume Ndani na Hapo ndipo ilikua mwisho wa Mzimu huo Kuja.

Amethyst Anasema Alimwambia Mpenzi wake Asihangaike Kumfatilia Kwasabu Asingempata kwakua hakua Mtu wa Kawaida bali Ulikua ni Mzimu, Baada ya Kuambiwa Hvyo Jamaa Akapaki Mabegi Akasepa!!. .
.
Amethyst anasema Alikua Anahisi kabisa Ladha ya Penzi huku Anaemfanya Haonekani na Alikua Amefanya Mapenzi Mara nyingi sana na Mizimu zaidi 20 tofauti na Hadi Anaiambia ITV Mwaka 2017 Anasema Alikua Anaujauzito Alioupata Kwa njia hiyo na Chaajabu ni Kwamba Alionyesha Kuridhia Kuendelea na Mahusiano yake na Mizimu!. .
.
"Ni Kweli Hauwezi (Mzimu) Kuninunulia Maua au Kunitoa Kwenda Sehemu Kufurahi lakini Furaha Ninayoipata Kwake Ni Special, Naota Ndoto nzuri na Najihisi Furaha" - Amethyst .
.
"Wakati wa Tendo Nahisi Miguso na Raha ya Ajabu Huku Anaenifanya Simuoni na Kuna Muda Hua Nashangaa Nageuzwa Kabisa Kufanyishwa Mapenzi Styles Tofautitofauti" - Amethyst .
.
"Nimewahi Sikia Mara nyingi juu ya Jambo hili la Mwanamke Kulala na Viumbe Wasioonekana Usiku na Sasa Ninahisi nina Ujauzito wa Viumbe hao" Alisema Amethyst. .
.
"Sio Pekeangu tuu Nilie Katika Mahusiano na Mzimu, Nasikia Habari Nyingi kama Hizi Watu huenda Sehemu Fulani Kukutana na Wapenzi wao ambao ni Mizimu" - Amethyst

Hali hii ya Kushiriki Mapenzi na Mzimu inaitwa 'Spectrophilia'. #Love
Share:

Ofisi Ya Makamu Wa Rais Yapongezwa Na Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Viwanda, Biashara Na Mazingira

Na Lulu Mussa
Serikali imesema itaendelea na juhudi za kushawishi wadau wa maendeleo na Jumuiya za Kimataifa ili kupata fedha za kusimamia uratibu wa shughuli za mazingira na kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi nchini. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameyasema hayo hii leo Jijini Dodoma wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji  wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Amesema Tanzania ni Mwanachama kwenye Mifuko na Mikataba mbalimbali duniani hivyo kuna fursa za kunufaika na fedha zitolewazo na mifuko hiyo akitoa mfano wa Green Climate Fund. 

Aidha Waziri Makamba ameainisha mafanikio yaliyopatikana katika Ofisi yake kwa kipindi cha mwaka 2018/2019, kuwa ni pamoja na kufanya Mapitio ya Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 1997 na Mkakati wa Utekelezaji wake,  kuandaa rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mazingira wa mwaka 2019 - 2023, na Maandalizi ya Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Viumbe Vamizi (Invasive Alien Species).  

Pia, katika kipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha rasimu ya mwisho ya Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchini baada ya kupata maoni ya wadau kabla ya kuwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004. 

Waziri Makamba amesema katika kuhakikisha usimamizi na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira unazingatiwa jumla ya miradi 1,254 ya maendeleo imefanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na Ukaguzi wa Mazingira na katika kuharakisha uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira linatoa Kibali cha Awali cha Mazingira (Provisional Environmental Clearance) ili kuwawezesha wawekezaji kuendelea na maandalizi ya awali ya mradi wakati mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira unaendelea.  

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Sadick amepongeza uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa jitihada za kuhifadhi mazingira nchini. " Kamati inatambua jitihada za Ofisi yenu katika kuhifadhi mazingira, sisi tunawaunga mkono" alisisitiza Mhe. Sadick.


Share:

Kauli ya Bunge Baada ya Mahakama Kuu Kutupilia Mbali Kesi ya Joshua Nassari




Share:

WAZIRI WA FEDHA DKT. MPANGO AAGIZA KUTOTUMIA FUNGU LA LISHE KWA MATUMIZI MENGINE


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Binti wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ambaye ni Mwanaharakati  wa masuala ya lishe, wanawake na watoto Duniani, jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao, Dkt. Mpango, alimweleza Princess Sarah Zeid kwamba Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya masuala ya lishe, utapiamlo na udumavu wa watoto licha ya nchi kuwa na chakula cha kutosha.

Dkt. Mpango alisema kuwa iwapo eneo la lishe halitasimamiwa kikamilifu Taifa litazalisha watoto wenye udumavu wa ubongo na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na utendaji hafifu wakiwa katika shughuli mbalimbali.

Alisema ipo mikoa ambayo inazalisha mazao mengi  kama Mbeya na Njombe lakini ina kiwango kikubwa cha watoto wenye utapiamlo, na kutoa wito kwa kila mtanzania kuhakikisha anaangalia ni chakula gani kinahitajika kwa ajili ya lishe ya watoto na wakinamama wajawazito ili kupunguza udumavu na vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.

Aidha amempongeza Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, kwa kampeni yake anayoifanya duniani kote kupambana na vifo vya wakinamama wajawazito na watoto kwa kuwa mchango wa wanawake ni mkubwa katika jamii ikiwemo uzalishaji mali.

Alisema idadi ya wanawake nchini Tanzania ni asilimia 51 ya idadi ya watu wote wanaokadiriwa kufikia milioni 55 ambapo mchango wako katika sekta mbalimbali za uchumi umekuwa mkubwa hivyo jitihada za kuwalinda zinahitajika.

Alimweleza Binti Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid kwamba kwa kutambua umuhimu wa lishe serikali imelivalia njuga suala la lishe kwa kutenga bajeti kila mwaka katika kila wizara na kwamba fedha hizo zimewekewa wigo zisitumike kwa matumizi mengine.

"Nimeziagiza Wizara, Mikoa na Halmashauri zote nchini kutumia fungu lililotengwa kwa ajili ya lishe  kwa matumizi yaliyopangwa  ili kuhakikisha watanzania wanaimarika kiafya na kushiriki kikamilifu katika Shughuli za Maendeleo" Alisema Dkt. Mpango.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Mkutano kati yake na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid na

Kwa upande wake Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ambaye aliambatana na Mwakilishi wa Shirika  la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) nchini Tanzania, Bw. Michael Dunford, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake katika kupambana na utapiamlo unaosababishwa na ukosefu wa lishe.

Amewataka watanzania kuhakikisha suala la Lishe linapewa kipaumbele  na kila mmoja kwa manufaa ya Taifa na Dunia kwa ujumla na kwamba atahamasisha jumuiya ya kimataifa kuchangia jitihada za Serikali za kupambana na tatizo la lishe, na vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa-WFP nchini Tanzania Bw. Michael Dunford, amesema kuwa shirika lake linatambua mchango mkubwa wa Serikali katika kupambana na masuala ya lishe duni na shirika lake litaendelea kushirikiana na nayo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

Mwisho


Share:

WAZIRI MKUU : UTOAJI WA ELIMU BORA NI KIPAUMBELE CHA NCHI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo na kufikia malengo ya Milenia 2025, Elimu kwa wote (EFA) na Mkakati wa Kupambana na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA). 


Amesema ili kuweza kufanikisha malengo hayo wanahitaji sekta hiyo kuwa bora, imara, inayokidhi mahitaji ya jamii kwa kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kukabiliana na matatizo ya kijamii, kitaifa na kimataifa.


Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 29, 2019) wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Parokia ya Ikwiriri, mkoani Pwani. Ameipongeza Parokia hiyo kwa kubuni mradi wa ujenzi wa shule.


Amesema sekta ya elimu ni wakala wa mabadiliko katika jamii kiuchumi, kiteknolojia na kiutamaduni katika kuleta maendeleo ya nchi na wadau muhimu wa sekta hiyo ni pamoja na Serikali, washirika wa maendeleo, mashirika ya kiraia na ya kidini, sekta binafsi na jamii kwa ujumla. 


Waziri Mkuu amesema kuwa wadau wote hao wamekuwa wakichangia kwa njia mbalimbali katika kuboresha utendaji wa sekta hiyo na kusababisha Serikali kupata mafanikio makubwa sana katika upatikanaji wa huduma za Jamii zikiwemo za elimu, afya na maji.

”Hivi sasa kila Kijiji nchini kina shule ya msingi na ongezeko limefikia idadi ya shule 17,659 zikiwemo zilizo chini ya Kanisa katoliki 204. Pia tumeweza kujenga shule za sekondari katika kila kata ambapo ongezeko limefikia shule za sekondari 4,883 nchi nzima zikiwemo zilizo chini ya kanisa katoliki 266”.

Waziri Mkuu amesema idadi hiyo ya shule imesaidia kutoa fursa kwa wanafunzi wengi kupata elimu nchini katika ngazi mbalimbali.  ”Hivi sasa kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015/2010 tunatekeleza mpango wa elimu bila ada kwa kutoa sh. Bilioni 24.4 kila mwezi”.

Amesema lengo la Serikali la kutoa kiasi hicho cha fedha kila mwezi ni kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata fursa bila vikwazo na  Wilaya ya Rufiji nayo inanufaika, ambapo imetengewa kiasi cha milioni 394.5 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Lengo la Serikali kutoa Elimumsingi Bila Ada ni kuleta ujumuishi kwa kuhakikisha watoto wote hususan wale ambao wanatoka katika familia zisizo na uwezo wanapata haki ya msingi ya kupata elimu.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuongezeka kwa ufaulu wa darasa la saba kumeleta changamoto ya uwepo wa miundombinu ya shule za sekondari hususan kwa kidato cha kwanza ambayo ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa sera ya Elimumsingi Bila Ada.

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengoalitumia fursa hiyo kuishikuru Serikalikwa kurejesha hali ya usalama na utulivu katika eneo la Rufiji na Kibiti.

Kardinali Pengoalisema kurejea kwa hali ya utulivu na usalama katika maeneo hayo kumemuondolea mzigo wa kiutendaji uliokuwa ukimuumiza kwa kuwa mapadri aliokuwa akiwapangia katika parokia za huko walikuwa wakisema ‘tumekosa nini’.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger