Wednesday 30 September 2020
Vijana Kagera Watakiwa Kutosubiri Ajira kutoka Serikalini.
Vijana katika halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera wameaswa kutosubiri ajira kutoka serikalini bali wajikite katika kujiajili haswa katika kilimo,uvuvi na ufugaji ili kuweza kujikwamua na umasikini.
Hayo yamesemwa na bwana Agape Ishabakaki wakati akizungumza na mpekuzi blog ambaye pia ni mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la FUAP TANZANIA linalojiusisha na masuala ya kusaidia wakulima na wafugaji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya watu haswa vijana ili kujenga utamaduni wa kujiajili uku wakiwa wamesubiri ajira kutoka serikalini.
Bwana Agape amesema kuwa shirika hilo kwa sasa limetua mkoani Kagera hususani katika wilaya ya Missenyi na litazungukia kata mbalimbali ili kutoa elimu kwa vijana juu ya faida za kujiajili na kutoa elimu kwa vijana hao kujikita katika kilimo kwa manufaa yao ya badae .
Katika hatua nyingne bwana Agape amesema kuwa zaidi ya miti elfu kumi ya matunda itazalishwa na shirika hilo na zoezi hilo litaanza tarehe mbili mwezi wa kumi katika kata ya Bugorola ili kuwapa fursa vijana pamoja na wananchi wa Missenyi kuwa na elimu juu ya utunzaji mazingira pamoja na kuwa na utamaduni wa kupanada miti katika maeneo yaliyowazunguka.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo bwana Josephat Joseph John amesema kuwa kwa sasa hivi shirika ilo lina mradi unaoitwa AGRI EXPERIENCE ambapo mradi huo utawawezesha vijana wengi kujifunza na kujua namna ya kufuga kuku wa kisasa pamoja na kufahamu ujuzi mbalimbali wa biashara ya mayai ya kisasa, ufugaji wa nyuki nk.
Bwana Josephat amesema kuwa vijana watumie shirika hilo vizuri kwa kuwa elimu itatolewa bila malipo yoyote na ku ongeza kuwa kabla yakuondoka mkoani hapa vijana wawe wameisha pata maarifa na ujuzi wa kujiajili wenyewe kupitia kilimo na ufugaji wa kisasa uku akitaja kauli mbiu yao kuwa ni “Kijana wa kagera kulima kwa tija kwa maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla 2020-2025”.
Serikali Kusimamisha Mishahara Ya Maafisa Utumishi Watakaosababisha Watumishi Kutolipwa Mishahara
Maafisa Utumishi watakaozembea na kusababisha Watumishi wa Umma nchini kutolipwa mishahara yao kwa wakati, watasimamishiwa mishahara na Serikali mpaka watakapohakikisha watumishi hao wamelipwa mishahara yao.
Hayo yamesemwa jana na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya Mfumo Mpya wa Kitanzania wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara kwa kundi la pili la Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala 140 kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Kigoma na Tabora yanayofanyika jijini Dodoma katika Ukumbi wa VETA.
DKt. Michael amesema, kuna tatizo katika baadhi ya Taasisi za Umma kwani wapo Maafisa Utumishi wanajifanya miungu watu wakati wajibu wao ni kumtengenezea mazingira mazuri ya kikazi mtumishi ili ajisikie yuko sehemu salama na aweze kutekeleza ipasavyo jukumu la kuwahudumia wananchi.
“Msiwafanye watumishi mnaowasimamia kuona sehemu ya kazi kama jehanamu, hivyo mbadilike kwani Serikali haitomvumilia yeyote atakaye kinzana na azma yake ya kuboresha huduma kwa wananchi”, Dkt. Michael alisisitiza.
Ameongeza kuwa, ni lazima Maafisa Utumishi wabadilike kwa kuwajengea mazingira Watumishi wa Umma kuipenda Serikali yao kwasababu inawajali na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Dkt. Michael amefafanua kuwa, Serikali inamhakikishia mtumishi usalama wa ajira yake tofauti na sekta binafsi, hivyo hakuna Afisa Utumishi atakayevumiliwa pindi akisababisha Serikali kulaumiwa na Watumishi wa Umma au Wananchi.
Naye, Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi, Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw. Boniface B. Chatila kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, ameahidi kuwa, wakirejea katika maeneo yao ya kazi watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuondoa kero ya Watumishi wa Umma kufuata huduma Ofisi ya Rais Utumishi Dodoma, huduma ambazo wanastahili kupewa katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, Bw. Chatila amemhakikishia Dkt. Michael kuwa, ujuzi watakaoupata kupitia mafunzo ya Mfumo Mpya wa Kitanzania wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara watautumia ipasavyo kuongeza ufanisi kiutendaji ili kuboresha utoaji huduma kwa umma.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, ACP Ibrahim Mahumi amesema, suala la mtumishi kukosa mshahara hivi sasa linachukuliwa kama ni kosa kubwa hivyo Afisa Utumishi atakayebainika atasimamishiwa mshahara ikiwa ni hatua ya awali na atachukuliwa hatua za kinidhamu ikizingatiwa kuwa, mfumo mpya utaonesha uzembe wa afisa huyo.
Mfumo Mpya wa Kitanzania wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara utaanza kutumika rasmi Mwezi Novemba, 2020 mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya makundi yote ya Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala ambao ndio wenye jukumu la kuutumia mfumo huo kiutendaji.
Sumaye aishukia CHADEMA, asema hawawezi kuongoza nchi
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema vyama vya Upinzani nchini haviwezi kuongoza nchi kwa sababu hawana sera.
Ameyasema hayo Leo septemba 30,2020 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini katika mkutano wa Mgombea Mwenza Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kunadi Sera za Chama cha Mapinduzi katika viwanja Vya Haydom.
Sumaye amesema Chama alichotoka CHADEMA, ni Chama cha Uwana harakati na hakina sera zozote za kuwasaidia wananchi.
'CHADEMA wanafikiri kuwa nchi ya Tanzania bado ipo mikononi mwa Wakoloni, wanapiga kelele utafikiri bado tunatawaliwa' alisema Sumaye
'Nilienda kule lakini baada ya kugundua hawana chochote nikaamua kurejea nyumbani' alisisitiza Sumaye
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Simon Lulu amesema Chama hicho kinajiandaa kwa ushindi wa kishindo kwa sababu kimefanya maendeleo kwa wananchi.
Amemweleza Mgombea Mwenza kiti cha Urais Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28 mwaka huu, Upinzani mkoani hapo hawataambulia hata kiti cha Udiwani.
Wahamiaji Haramu 32 Wakamatwa Wilayani Pangani
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa wahamiaji hao Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora alisema kwamba wahamiaji hao walikamatwa Septemba 27 mwaka huu usiku.
Alisema ukamatwa huo waliofanya baada ya kupata taarifa kutoka wananchi wa Kijiji cha Buyuni kupitia Mwenyekiti wa Kijiji hicho Diwani Akida ambaye aliwaeleza uwepo wa mazingira yasiyoridhisha kwenye eneo lake hasa eneo la bahari baada ya boti moja kukwama.
Alisema baada ya kupata taarifa hiyo wao kama wahifadhi wana jukumu la kulinda maliasili na kuangalia usalama kwenye miji yote inayowazunguka waliandaa kikosi kazi cha kwanza waliokwenda eneo la tukio na walipofika waliwakuta wahamiaji hao eneo la bahari karibu na hifadhi hiyo katika kijiji cha Buyuni.
Alisema baadae hapo waliamua kutuma kikosi cha pili na ndipo walipofika na kufanikiwa kukaweka chini ya ulinzi wahamiaji 28 ambao ni raia wa Ethiopia lakini alfarji wakapata taarifa nyingine ya uwepo wa wahamiaji wengine wanne ambao ni raia wa Somalia na wakatuma kikosi na kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi.
“Kati yao wapo wahamiaji 32 raia wa Ethiopia 28 na raia wa Somalia wanne akiwemo mwanamke mmoja kwa hiyo baada ya kufanikisha tukio hilo tumewafikisha na kuwakabidhi kwenye mamlaka ya Polisi kwa ajili ya hatua zaidi”Alisema
Awali akizungumza kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda aliwapongeza askari wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa kazi nzuri kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Polisi wilaya ya Pangani.
Hata hivyo amesema kwamba hivi sasa wametangaza vita mpya kwa mawakala wanaojishuhulisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu mkoani Tanga kwamba hawatasalimika watasakwa popote iwe ni nchi kavu, majini na kisha kufikishwa mahakamani.
Tundu Lissu adai bado hajapokea wito wa malalamiko
Lissu ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 30, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, na na kusisitiza kuwa kwa sababu hana wito wowote yeye ataendelea na ratiba zake za kampeni kama ilivyo kwenye ratiba.
Jana Septemba 29, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Wilson Mahera alitoa taarifa ya kuthibitisha kumuandikia barua ya wito Tundu Lissu, kufuatia tuhuma mbalimbali anazodaiwa kuzitoa kati ya Septemba 25 na 26 mjini Musoma
Armenia yakataa upatanishi wa Urusi katika mzozo na Azerbaijan Huku Mapigano Yakizidi Kupamba Moto
Waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan amesema haitakuwa sahihi kufanya mazungumzo ya amani na Azerbaijan chini ya upatanishi wa Urusi, wakati mapigano ya kuwania udhibiti wa jimbo yakiwa yanaendelea.
"Sio sahihi kabisa kuzungumzia kuhusu mkutano kati ya Armenia, Azerbaijan na Urusi katika wakati wa uhasama mkubwa," amesema Pashinyan wakati akizungumza na shirika la habari la Urusi Interfax.
Ameongeza kuwa hali endelevu na mazingira yanahitajika kwa ajili ya mazungumzo hayo.
Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti Jumatano kuwa waziri mkuu Pashinya amesema Armenia haifikirii kuweka walinzi wa amani katika jimbo la Nagorno-Karabakh.
Kwa miaka kadgaa, vikosi vya Armenia na Azabajani vimekuwa vikizozania jimbo hilo la Karabakh, ambalo liliamua kutaka kujitenga na Azabajani baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieeti katika miaka ya 1990.
Mzozo huo wa muda mrefu uliibuka tena Jumapili huku pande hizo mbili zikirushiana silaha nzito za moto na kulaumiana kwa kuzuka kwa vurugu.
Karibu watu 100 wamethibitishwa kufa katika mapigano hayo ya hivi karibuni na pande zote mbili zinadai kuwa zimesababisha hasara kubwa kwa vikosi vya wapinzani.
DW
Benki ya Maendeleo ya Afrika yaipa Tanzania bilioni 15
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imetoa zaidi ya shilingi bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya kutoa huduma kwa jamii katika Wilaya ya Buhigwe, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini na Kibondo mkoani Kigoma.
Hayo yamesemwa na na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya mtandao wa barabara ya Afrika Mashariki (EARNP) inayojenga mkoani humo.
Choma amesema kuwa AfDB imetoa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 256.2 kwa ajili ya kujenga barabara ya kujenga barabara ya kutoka Kabingo-Kasulu hadi Manyovu yenye urefu wa 260km. Ujenzi wa barabara hiyo ni moja ya utekelezaji wa miradi ya EARNP ambao unaiunganisha Tanzana na Burundi.
Kutokana na fedha zilizotolewa na benki hiyo miradi mbalimbali itatekelezwa katika wilaya hizo ikiwa ni pamoja na vituo vya mabasi, shule za msingi na sekondari, ujenzi wa masoko na ukarabati wa mabomba ya kusambaza maji, ujenzi wa vituo ya afya na hospitali za wilaya pamoja na barabara za mtaa.
Hospitali Ya Wilaya Karagwe Yakamilika Kwa 98%
Hayo yamesemwa jana (Jumanne, Septemba 29, 2020) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kayanga, katika mikutano uliofanyika kwenye uwanja wa Changarawe, wilayani Karagwe, mkoani Kagera wakati .
Akielezea ujenzi wa vituo vya afya kwenye wilaya hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. milioni 900 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya vituo cha afya ambapo kati ya hizo, sh. milioni 500 zimetumika wa majengo ya kituo cha afya cha Kayanga ambapo kituo hicho kimekamilika na kinatoa huduma.
“Shilingi milioni 400 zimetumika kwa ujenzi wa majengo ya kituo cha afya cha Nyakayanja na ujenzi umekamilika. Pia shilingi bilioni 2.5 zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi huku fedha za dawa kwa mwezi zilikuwa ni wastani wa shilingi milioni 53,” alisema.
Akielezea uboreshaji wa miundombinu kwenye wilaya hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alisema uk. 74-76 wa Ilani ya uchaguzi ya CCM, unaelezea mpango wa Serikali kuanza ujenzi mpya (km 6,006.04) na ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Mugakorongo - Kigarama - Murongo yenye urefu wa km 105.
“Ilani yetu imeenda mbele zaidi na kuelezea mpango wa kukamilisha/kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina (km 7,542.75) barabara za mikoa kadhaa ikiwemo barabara ya Murushaka – Murongo yenye km 125.”
Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe, Bw. Innocent Bashungwa, mgombea udiwani wa kata ya Kayanga, na wagombea wa CCM wa kata za wilaya hiyo.
Alisema sh. bilioni 1.4 zimetolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya kufungua barabara mpya, matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi, muda maalum na makalvati. Alisema kati ya hizo, sh. milioni 585 zimetolewa kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofi na baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa kazi ni ukarabati katika barabara ya Nyakagoyagoye-Karongo ambao uligharimu sh. milioni 31.
Akielezea ukarabati uliofanywa, alisema sh. milioni 19 zimetumika katika barabara ya Kanyabuleza-Runyaga; sh. milioni 14 zimetumika na katika barabara ya Mato-Karehe; sh. milioni 23 zimetumika katika barabara ya Kihanga - Rwabitembe – Mshabaiguru, sh. milioni 16 zimetumika katika barabara ya Nyakahanga – Kamahungu, sh. milioni 16 zimetumika katika barabara ya Kishoju – Bujuruga na sh. milioni 23 zimetumika katika barabara ya Igurwa-Kibona-Nyakahita.
Alizitaja barabara nyingine zilizofanyiwa ukarabati kuwa ni Katoju-Ihembe – Bisheshe iliyogharimu sh. milioni 98, barabara ya Kanyabuleza Jct-Makabulini iliyotumia sh. milioni 69, barabara ya KDVTC FADECO iliyotumia sh. milioni 73, barabara ya AMRI – CLASIC iliyogharimu sh. milioni 38 na barabara ya Rukore – Chanika iliyotumia sh. milioni 115.
Alisema TARURA ilifanya matengenezo ya madaraja na makalvati katika barabara za Katoju- Rugu - Ruhita (sh. milioni 17), Igurwa-Nyakashozi-Rwentuhe (sh. milioni13), Rukore - Chanika (sh. milioni 12), Rubale - Kibogoizi (sh. milioni 6) na barabara ya Kasheshe - Rubare (sh. milioni 7).
“Shilingi milioni 124 zimetumika kwa ajili ya matengenezo maalum katika barabara za Kajunguti - Rubare - Misha (km. 9), Nyabiyonza-Kafunjo (km. 6), Kibaoni Nyabiyonza Sec - Kakuraijo (km. 3.15), Nyakakika - Kandegesho (km.5), Lukole - Kigarama, Lukoyoyo – Kantabire -Nyakasimbi na Ahamulama – Busecha,” alisema.
Vijiji 73 Kati Ya 77 Misenyi Vyapatiwa Umeme
VIJIJI 77 kati ya vijiji 73 vya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera vimepelekewa huduma ya umeme na vijiji 4 bado havina umeme.
Hayo yamesemwa jana (Jumanne, Septemba 29, 2020) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kassambya, katika mikutano uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, wilayani Missenyi, mkoani Kagera.
Amevitaja vijiji ambavyo havina umeme na vipo kwenye mpango wa kupelekewa umeme kuwa ni vijiji vya Buchurago, Katano, Kakunyu na Bugango.
Akizungmzia sekta ya mifugo ambayo imetajwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 hadi 2025 kuanzia ukurasa 47-52, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeisimamia vizuri sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wanapata manufaa.
“Shilingi milioni 23 zimetumika kukarabati machinjio ya Bunazi hapa Misenyi, pia tumerahisisha uuzaji wa mazao ya mifugo kwa kufuta tozo kero 114 katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na kuimarisha masoko ya mazao ya mifugo kwa kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo,” alisema.
Alisema Serikali imepanga kuanzisha vituo vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika mikoa 18 ambayo haina vituo, kuimarisha huduma za tiba za mifugo kwa kuhakikisha kila wilaya ina maabara, kliniki na daktari wa mifugo.
Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Nkenge, Dkt. Florent Kyombo na wagombea udiwani 13 wa CCM wa kata za wilaya hiyo. Mgombea udiwani wa kata ya Kassambya, Bw. Yusuph Jumbe na wenzake sita, wamepita bila kupingwa.
Kuhusu barabara, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 3.57 zilitolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara za wilaya hiyo zikiwemo barabara za Bukwali-Kashenye-Bushango, Ngorogoro-Kyabugombe, Mabuye –Itara na Ruzinga - Mugongo.
Alizitaja barabara nyingine kuwa ni za Gera – Ishozi – Ishunju, Nyankele – Kilimilire, Mabale–Mwemage-Kyaka, Nyankele-Nyamilembe–Kenyana na Kituntu–Bwengabo. Alisema mwaka 2020/2021, sh. milioni 711.6 zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara kwa muda maalum.
(mwisho)
GGML, RAFIKI SURGICAL MISSION WATOA GARI LA WAGONJWA KWA ZAHANATI BUKOLI – GEITA
Wellness & Customer Service Manager at CVPeople Tanzania
CVPeople Tanzania | Full time Wellness & Customer Service Manager Dar es Salaam , Tanzania Job Description Our client is looking for Wellness & Customer Service Manager, the ideal candidate will supervise day-to-day operations in the customer service medical department Responsibilities: Respond to customer service issues in a timely manner. Create effective customer service procedures, […]
The post Wellness & Customer Service Manager at CVPeople Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.
Systems & Database Adminstrator at CVPeople Tanzania
CVPeople Tanzania Systems & Database Adminstrator Dar es Salaam , Tanzania Job Description The ideal candidate will be responsible in structuring, monitoring and adminstration of the network environment (LAN, WAN) including any new installations, upgrades, .Maintenance of Cisco, Alcatel and 3COM equipment utilized on the LAN and WAN networks. Configuration, monitoring and management of servers […]
The post Systems & Database Adminstrator at CVPeople Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.
Head of Finance at CVPeople Tanzania
CVPeople Tanzania | Full time Head of Finance Dar es Salaam , Tanzania Job Description Monitor expenditure and revenue in the organisation to ensure these are aligned with the Business Unit/ company’s operational plan. Partake in Financial Planning process [budgeting, modelling, forecasting and reporting] Oversee and ensure the efficient management of Accounts Payable, Accounts Receivable, […]
The post Head of Finance at CVPeople Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.
Security Technician at CVPeople Tanzania
CVPeople Tanzania Security Technician Dar es salaam , Tanzania Job Description Install, maintain, or repair security systems, alarm devices, and related equipment, following blueprints of electrical layouts and building plans Mount and fasten control panels, door and window contacts, sensors, and video cameras, and attach electrical and telephone wiring in order to connect components Test […]
The post Security Technician at CVPeople Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.
Deputy Principal (Academic) at SJUIT
St. JOSEPH UNIVERSITY IN TANZANIA VACANCY ANNOUNCEMENT We have been retained by our client, who is a leading college of HEALTH AND ALLIED SCIENCES in Dar-es- Salaam. We invite applications from suitable qualified and experienced Tanzanians to apply for the following vacant positions available in Dares Salaam. The college offers various NACTE approved Diploma […]
The post Deputy Principal (Academic) at SJUIT appeared first on Udahiliportal.com.
Principal at SJUIT
St. JOSEPH UNIVERSITY IN TANZANIA VACANCY ANNOUNCEMENT We have been retained by our client, who is a leading college of HEALTH AND ALLIED SCIENCES in Dar-es- Salaam. We invite applications from suitable qualified and experienced Tanzanians to apply for the following vacant positions available in Dares Salaam. The college offers various NACTE approved Diploma Programmes. […]
The post Principal at SJUIT appeared first on Udahiliportal.com.