Sunday, 5 January 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 6,2025

 

Magazeti ya leo
 
         
Share:

UUNGANISHAJI UMEME VIJIJINI WAFIKIA ASILIMIA 99.9



Na mwandishi wetu, Dar

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2024, vijiji vilivyounganishwa na umeme nchini vimefikia 12,301 kati ya vijiji 12,318 ambayo ni sawa na asilimia 99.9.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 5 Januari, 2025 na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mha. Jones Olotu wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya upatikanaji umeme vijijini kwa Wanahabari tulipotoka, tulipo na tunapokwenda kuelekea Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati jijini Dar es Salaam.

"Vijiji 17 vilivyobakia wakandarasi wanaendelea na ujenzi wa miundombinu na vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi januari mwaka 2025," amesema Mha. Olotu.

Ameongeza kuwa, Tanzania Bara ina jumla ya vitongoji 64,359 ambapo tayari vitongoji 33,657 sawa na asilimia 52.3 vimefikiwa na umeme na vitongoji 30,702 vilivobaki vipo kwenye mpango wa kupatiwa umeme kwa kipindi cha miaka mitano.

Vile vile, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imefanikiwa kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi maeneno ya vijijini kwa kuwatengenezea fursa za uwekezaji kwa kutumia huduma ya umeme.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati unaotarajiwa kufanyika januari 27 - 28 na kuhudhuriwa na watu wasiopungua 1,500 kutoka nchi mbalimbali.

Miongoni mwa washiriki ni Wakuu wa Nchi za Afrika, Mawaziri wa Nishati na Fedha, Mabalozi, Taasisi za Kimataifa, Makampuni yaliyowekeza kwenye sekta ya Nishati na watafiti.


Share:

WAZIRI WA MIPANGO NA UWEKEZAJI APONGEZA KIWANDA CHA MATI SUPER BRANDS LTD

 



Na Mwandishi Wetu,
Manyara


Waziri wa nchi Ofisi ya Rais ,Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amepengeza Wawekezaji wazawa wa kiwanda cha Mati Super brands limited kwa kulipa kodi stahiki za serikali na kutengeneza ajira kwa vijana hivyo kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Manyara na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha Mati Super Brands limited ,waziri kitila mkumbo amepongeza wawekezaji hao waliowekeza ambao wamelipa kodi ya kiasi cha shilingi bilioni 8 kwa mwaka 2024 na kuchangia maendeleo ya nchi.

“Rais Dr.Samia Suluhu Hassan anapambana kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na Mati Super Brands Limited imeajiri Watanzania 269 hilo ni jambo kubwa” Anaeleza Profesa Kitila Mkumbo ,Waziri wa nchi Ofisi ya Rais ,Mipango na Uwekezaji

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa kiwanda hicho kimekua na mchango katika jamii na kimekua kikilipa kodi stahiki za serikali ikiwemo kondi ya Ongezeko la thamani (VAT) ,ushuru wa uzalishaji wa bidhaa,kodi ya mapato (income tax Pamoja na kodi nyingine.

“Kwa kipindi cha miaka mitatu tumekua tukilipa kodi ambapo mwaka 2022 tumelipa kodi bilioni 7,2023 tumelipa bilioni 7.9 ,mwaka 2024 tumelipa kodi bilioni 8 na mwaka 2025 tunatarajia kulipa kodi zaidi ya bilioni 12” Anaeleza Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited ,David Mulokozi








Share:

KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI; UMEME NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA



Na Regina Ndumbaro Ruvuma 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia umeme na nishati jadidifu Dkt. Khatibu M. Kazungu, amesema kuwa umeme ni muhimu kwa uchumi, uhai, na maendeleo ya kisiasa na kijamii hivyo ni jukumu la Wizara kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya uhakika.

Ametoa kauli hiyo Januari 4 2025,
alipotembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Kidatu Mkoani morogoro, kinachozalisha megawati 204 za umeme Dkt. Kazungu amesisitiza  kuwa Wizara ya Nishati ina jukumu muhimu la kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa kutosha, jambo ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa. 

Ameongeza kuwa ni muhimu kusimamia miradi ya uzalishaji umeme ili kuwa na usambazaji wa nishati kwa ufanisi na kuhakikisha kwamba maendeleo ya uchumi na jamii yanaendelea. "Wizara ya Nishati inajukumu kubwa kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya uhakika kwa ajili ya kusukuma mbele shughuli mbalimbali za maendeleo", amesema Kazungu.

Katika ziara hiyo,  amebainisha kuwa kituo cha Kidatu kilianza kuzalisha umeme tangu mwaka 1975 na kwa sasa kinatimiza miaka 50 ya huduma ambapo ameonyesha changamoto za usafirishaji wa umeme kutoka bwawa la Mwalimu Nyerere kwenda Dodoma  changamoto hii inahitaji kutatuliwa haraka ili kuhakikisha usambazaji wa umeme unafanyika bila vikwazo.

Akiwa kwenye kituo hicho, Dkt. Kazungu amezungumzia mtambo namba mbili unaofanyiwa ukarabati ulioanza  mwezi  Mei mwaka 2024 na unatarajiwa kukamilika Januari 2025 huku akitoa maagizo ya kuhakikisha kuwa mkandarasi anasimamiwa kwa karibu ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na mtambo huo uweze kuungana na mitambo mingine ambayo itaongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme.

Dkt. Kazungu amefafanua kuwa ukarabati huo utasaidia kuzalisha umeme mwingi zaidi, ukilinganisha na umeme unaopatikana sasa, hii itasaidia kukidhi mahitaji ya umeme ambayo yanazidi kuongezeka kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na ongezeko la idadi ya watu amesisitiza kuwa usimamizi mzuri wa miradi ya nishati utawezesha maendeleo endelevu na kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Akizungumza Meneja wa mradi wa Kidatu HPP Mhandisi Manfred Lucas Mbyalu ameeleza huduma zingine zinazotolewa na kituo  hicho cha kufua umeme ni kinatoa huduma ya zahanati pamoja na elimu kwa wafanyakazi na wategemezi wao pamoja na wakazi wa vijiji jirani ili kuisaidia jamii kupata huduma bora za kijamii.

Kipekee ameeleza namna ambavyo TANESCO  itaendelea kuhakikisha kituo cha kufua umeme cha kidatu mitambo yake inakuwa katika hali nzuri na inapatikana muda wote (plant availability) ili kuhakikisha wanachangia umeme wa kutosha kwenye gridi ya Taifa kufanikisha adhma ya serikali ya awamu ya sita ya kukuza uchumi wa wa wananchi na nchi kwa ujumla.

Imeelezwa kuwa  ili kuendeleza maendeleo ya umeme nchini, ni muhimu kwa Serikali na wadau wa sekta ya nishati kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya umeme, Hii itasaidia kupunguza changamoto za upungufu wa umeme na kuongeza uzalishaji wa umeme kwa ufanisi, hivyo kuunga mkono juhudi za Serikali za kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.
Share:

Saturday, 4 January 2025

NILIVYOMFANYA EX WANGU AKANISAHAU MOJA KWA MOJA!

Kabla sijaajiriwa nilikuwa kwenye uhusiano na binti mmoja hivi na nilifanikiwa kumpa ujauzito na kwao baada ya kugundua ni mjamzito wakaamua kumleta nyumbani na nikakubali ujauzito nao wakaniachia binti nilee ule ujauzito mpaka atakapojifungua.

Nilifanikiwa kulea ujauzito kwenye hali ngumu sana mpaka akafanikiwa kujifungua salama, baada ya kujifungua nilifanikiwa kupata kazi kwenye moja ya kampuni kubwa ambazo zinalipa vizuri sana.

Hapo maisha yalibadilika na kuwa mazuri kabisa ila mkataba ulivyoisha kule kwenye kazi yangu ndipo mwanamke huyo akaanza jeuri na kuwa na mahusiano na wanaume wengine wengi wa nje na mwishowe akaamua kuondoka na mwanangu.

Kusema kweli ulipita muda mrefu sana tangu aondoke ila mwaka 2020 akaja akanitafuta na kuniletea mwanangu. Lakini baada ya muda akaanza tena usumbufu wa kutaka kuwa kwenye uhusiano na mimi tena ilihali mimi nimekwishaoa.

Usumbufu wake ukaleta madhara mpaka kwenye ndoa yangu ambako huyo mwanamke niliyemuoa ndiye anayenitunzia mwanangu hivi sasa.

Sasa nikawa sijui nitumie njia gani ili kumfanya awe mbali na mimi, baadaye nilienda kwa mganga aitwaye Dr Bokko akanifanyia dawa za kumfanya awe mbali na mimi na sasa ni mwaka wa nne hajawahi kunitafuta. Mpigie Dr Bokko +255618536050.

Mwisho.


Share:

Friday, 3 January 2025

WATENDAJI UBORESHAJI WATAKIWA KUHAMASISHA WANACHI KUJIANDIKISHA

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu)  Dkt. Rose Likangaga akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mjumbe wa Tume, Dkt. Zakia Mohamed Abubakar. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu)  Dkt. Rose Likangaga akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mjumbe wa Tume, Dkt. Zakia Mohamed Abubakar. 

Mwenyekiti wa Mafunzo, Bw. Khalid Khalif akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo. 
Na Mwandishi wetu, Songea
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura mkoani Ruvuma wametakiwa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao baadae mwaka huu.
 
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu)  Dkt. Rose Likangaga wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa watendaji hao mkoani Ruvuma.
 
“Mnahimizwa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao,” ilisema sehemu ya hotuba hiyo.
 
Dkt Likangaga akisoma hotuba hiyo alisema ni matarajio ya Tume kuwa, mara baada ya zoezi hili lililopo mbele yao kukamilika watu watakaokuwa wamepatiwa kadi watakuwa ni Wapiga Kura Halali.
 
Aidha alisema, jukumu la uhamasishaji linawahusu moja kwa moja wao watendaji kwa kushirikiana na wadau wengine katika maeneo yao kupitia nyenzo walizonazo.
 
“Ninasisitiza kwamba, mabango na vipeperushi mtakavyopewa na Tume mvisambaze mapema katika kata zote zilizopo katika halmashauri zenu. Kazi yenu kubwa ni kusimamia na kuendesha shughuli zote za uboreshaji katika halmashauri zenu,”ilisisitiza hotuba hiyo.
 
 Watendaji hao wameatakiwa kuisoma kwa umakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Sheria za Uchaguzi, Kanuni za Uboreshaji, Maelekezo na Miongozo yote inayotolewa na Tume ili kazi yao ifanyike kwa uadilifu na haki.
 
Pia wametakiwa kuwasiliana na Tume kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala yote yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu yao pindi wanapokutana na changamoto zozote.
 
“Tume imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na hivyo nanyi mna wajibu wa kuhakikisha kuwa mnatekeleza kikamilifu majukumu yote mliyokasimiwa,” ilisema sehemu ya hotuba hiyo.
 
Pia Tume imewataka watendaji hao kuwa makini katika kila eneo la usambazaji na utunzaji wa vifaa na muda sahihi wa ufunguaji na ufungaji wa vituo vya kuandikishia wapiga kura.
 
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unataraji kuanza Januari 12 hadi 18, 2025 katika mikoa ya Songwe, Njombe, Rukwa na Ruvuma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Mbinga, Mbinga Mji, Wilaya ya Songea na Manispaa ya Songea ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
 
Mafunzo hayo yaliwahusisha Maafisa Waandikishaji,Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi, Maafisa TEHAMA wa Halmashauri.


Washiriki wakisikiliza hotuba ya kufunga mafunzo hayo. 
Mafunzo yakiendelea 

mmoja wa wakufunzi akitoa maelekezo wakati wa mafunzo kwa vitendo. 

Washiriki wakifanya mafunzo kwa vitendo. 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger