Saturday, 31 May 2025

Video Mpya : LUTEMA - SHIKOME

 

Share:

GESI YA KUPIKIA NI SAFI NA SALAMA,TUITUMIE-EWURA


Mkaguzi wa Bidhaa za Petroli EWURA, Mhandisi Mbarouk Shaame akiwasilisha mada kuhusu matumizi sahihi na salama kwa Mama Lishe, Waendesha Bodaboda, Wajasirianali na Wasambazji wa Gesi ya kupikia mkoani Iringa
..

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kutoa hamasa kwa wadau mbalimbali mkoani Iringa kutumia gesi ya kupikia (LPG) ambayo ni nishati safi, ya uhakika na inayotunza afya na mazingira.

Mkaguzi wa bidhaa za Petroli EWURA Mhandisi Mbarouk Shaame, akitoa mada kwa mama lishe, waendesha bodaboda, wauzaji na wasambazaji wa LPG mkoani Iringa.

Pia alisisitiza kuwa EWURA huhakikisha vigezo vya usalama wakati wa uagizaji, uhifadhi, usambazaji na usafirishaji wa gesi ya kupikia vinazingatiwa ili nishati hiyo isilete madhara kwa watu, mali na mazingira.

Mhandisi Shaame alieleza kuwa, EWURA husimamia mlolongo mzima wa biashara ya gesi ya kupikia (LPG)nchini kwa kushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo NEMC, TBS na Wakala wa Vipimo ili kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na upatikanaji wa nishati hiyo huku ikichagiza utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia.

Akihitimisha semina hiyo, Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, Mhandisi Hawa Shani Lweno, alitoa mwito kwa watanzania kuchangamkia fursa ya biashara ya kusambaza gesi ya kupikia(LPG) ili kusogeza huduma hususani katika maeneo ya pembezoni, ambapo alisiitiza kuwa EWURA hutoa leseni na vibali kwa njia rahisi na rafiki kupitia mfumo wa kieletroni wa LOIS.


Mkaguzi wa Bidhaa za Petroli EWURA, Mhandisi Mbarouk Shaame akiwasilisha mada kuhusu matumizi sahihi na salama kwa Mama Lishe, Waendesha Bodaboda, Wajasirianali na Wasambazji wa Gesi ya kupikia mkoani Iringa


Mkaguzi wa Bidhaa za Petroli EWURA, Mhandisi Mbarouk Shaame akiwasilisha mada kuhusu matumizi sahihi na salama kwa Mama Lishe, Waendesha Bodaboda, Wajasirianali na Wasambazji wa Gesi ya kupikia mkoani Iringa


Mkaguzi wa Bidhaa za Petroli EWURA, Mhandisi Mbarouk Shaame akiwasilisha mada kuhusu matumizi sahihi na salama kwa Mama Lishe, Waendesha Bodaboda, Wajasirianali na Wasambazji wa Gesi ya kupikia mkoani Iringa.


Afisa Habari Jeshi la Zimamoto mkoani Iringa,Zmm 0145 Fc Adolf Kameya,akitoa elimu ya kukabiliana na moto wa gesi ya kupikia kwa mama lishe, dereva bodaboda, wajasiriamali na wasambazaji wa bidhaa hiyo wakati wa semina ya EWURA kwa wadau hao.

Afisa Habari Jeshi la Zimamoto mkoani Iringa,Zmm 0145 Fc Adolf Kameya,akitoa elimu ya kukabiliana na moto wa gesi ya kupikia kwa mama lishe, dereva bodaboda, wajasiriamali na wasambazaji wa bidhaa hiyo wakati wa semina ya EWURA kwa wadau hao.
Share:

WARATIBU WA MTAKUWWA WATAKIWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MPANGO HUO KIKAMILIFU ILI KUTOKOMEZA UKATILI


Na WMJJWM - Dodoma

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju ametoa wito kwa Waratibu wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kuhakikisha wanaimarisha uratibu na utekelezaji wa mpango huo katika ngazi za mikoa na halmashauri.

Akizungumza katika kikao kazi cha waratibu wa MTAKUWWA kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara kilicholenga kuwapatia Mafunzo kuhusu uratibu na utekelezaji wa Mpango Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya St. Gasper jijini Dodoma kinalichoanza  Mei 28 hadi 31 , 2025, Mpanju amesema kikao hicho ni muhimu katika kujenga uelewa kuhusu uratibu wa MTAKUWWA II (2024/25 – 2028/29).

Wakili Mpanju amesema Waratibu wa MTAKUWWA ni kiungo muhimu katika kuhakikisha afua za mpango huo zinatekelezwa kikamilifu na ni lazima wasimame imara, washirikiane na maafisa wa mikoa, halmashauri na wadau wote ili kuandaa na kusimamia mipango mikakati ya utekelezaji wake.

Aidha, amesisitiza kuwa Mpango huo unalenga kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake, watoto na jamii kwa ujumla huku akisisitiza kila mkoa kuhakikisha unaandaa mpango mkakati wake wa utekelezaji wa MTAKUWWA.

Pia amesisitiza utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango huo huku akiwasihi kusimamia na kushauri katika utengaji wa Bajeti kwaajili ya utekelezaji wa Mpango huo katika maneno yao.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamiii Patrick Golwike amewataka Waratibu hao kwenda kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo hayo kwa  kusimamia vizuri utekelezaji wa mpango huo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa weledi ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto 

Katika kikao hicho washiriki ambao ni waratibu wa MTAKUWWA kutoka mikoa yote 26 walieleza kuwa kikao hicho kimewajengea uelewa wa kina kuhusu wajibu wao na namna bora ya kuendesha shughuli za uratibu na kueleza kuwa kupitia majadiliano ya pamoja na miongozo waliyopewa sasa wana uwezo wa kuratibu kwa ufanisi afua za kupambana na ukatili katika jamii.

Aidha, wameeleza kuwa maagizo yaliyotolewa na Serikali kupitia Wizara yamepokelewa kwa uzito mkubwa na kwa pamoja wameahidi kwenda kuyatekeleza kwa vitendo mara watakaporejea katika maeneo yao ya kazi.

Share:

Friday, 30 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 31,2025

Magazeti





 








Kaka yangu aliondoka nyumbani miaka 17 iliyopita akisema anaenda kutafuta maisha na atarajea kipindi
Share:

WAANDISHI WA HABARI 8 WAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UMAHIRI KATIKA UANDISHI WA HABARI ZA TAKWIMU ZANZIBAR


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAREHE: 28 MEI 2025

WAANDISHI WA HABARI 8 WAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UMAHIRI KATIKA UANDISHI WA HABARI ZA TAKWIMU ZANZIBAR

·      Redio jamii Pemba zaibuka kidedea kwa kuendeleza misingi ya usawa wa kijinsia, wakifuatiwa na gazeti la Zanzibar Leo

·      Asya Hassan wa Zanzibar Leo aibuka mshindi wa Jumla

·      Waandishi chipukizi nao wang’ara.

Jumla ya waandishi wa habari wanane (8) na vyombo vya habari vitatu (3) wameibuka kidedea katika tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari za Takwimu za wanawake na uongozi zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS) pamoja na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO).

Miongoni mwa vipengele vilivyoshindaniwa ni kipengele cha radio, kipengele cha magazeti, kipengele cha mitandao ya kijamii, kipengele cha waandishi wa habari vijana (YMF) na kipengele cha vyombo vya habari vyenye kuendeleza na kukuza usawa wa kijinsia.

Kati ya washindi hao wanane, watano miongoni mwao walitoka katika kipengele cha waandishi wa Habari vijana ambao walitambuliwa kwa kuzawadiwa vyeti pamoja na iPad kwa kila mmoja. Washindi hao ni:

  1. Salum Ameir Salum
  2. Zurima Ramadhan
  3. Nihifadhi Abdulla Issa
  4. Fatma Hamad Faki
  5. Maryam Nassor Suleiman

Vilevile, Asya Hassan Bakar kutoka gazeti la Zanzibar Leo aliibuka kuwa mshindi wa jumla na mshindi katika kipengele cha gazeti, alizawadiwa cheki ya shilingi Milioni moja na Laki tano, cheti pamoja na trofi, mwengine ni Huwaida Nassor Moh’d kutoka Assalam Fm Radio ambae amekua mshindi wa kwanza katika kipengele cha Redio nae alizawadiwa cheki ya Shilingi milioni moja, cheti pamoja na trofi na mshindi wa kwanza katika kipengele cha mitandao ya kijamii ni Salum Ameir Salum alipokea cheki ya Shilingi milioni moja, cheti pamoja na trofi

Kwa upande wa Vyombo vya Habari jumla ya vyombo vitatu vya habari vilitambuliwa kwa juhudi zao katika kuendeleza na kukuza usawa wa kijinsia kwenye kazi zao za kila siku, vyombo hivyo vilizawadiwa cheki ya Shilingi milioni mbili (2,000,000) kwa kila kimoja pamoja na vyeti vya shukran. Vyombo vya habari vilivyoibuka washindi ni:

  • Redio Jamii Micheweni.
  • Redio Jamii Mkoani.
  • Shirika la Magazeti ya Serikali.

Waandaaji wa Tuzo hii wanatoa wito kwa waandishi wa habari wa na vyombo vya Habari kuendelea kuandika habari zinazohusu takwimu za wanawake na uongozi, kusimamia na kukuza usawa wa kijinsia, kuelezea mazuri yanayofanywa na wanawake na vikwazo mbalimbali vinavyowazuia wanawake wasifikie nafasi za uongozi.

Jumla ya kazi 235 kutoka vyombo vya habari vya aina zote vikiwemo magazeti, redio, televisheni pamoja mitandao ya kijamii, ziliwasilishwa kwa ajili ya kushindanishwa, ambapo jumla ya kazi 120 zilikabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi na hatimae kupatikana washindi hao.

Tuzo hizi ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Kuwawezesha Wanawake kushika nafasi za uongozi (SWIL), ambayo inatekelezwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiyay a Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) na Jumuiyay a Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), kwa ushirikiano na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.

Imetolewa na:

TAMWA ZNZ, JUWAUZA, ZAFELA & PEGAO.

 

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

PRESS RELEASE

Date: 28th May 2025

8 JOURNALISTS EMERGE WINNERS IN THE DATA JOURNALISM AWARDS.

·      Community radio in Pemba lead in promoting gender equality, followed by Zanzibar Leo newspaper

·      Asya Hassan of Zanzibar Leo crowned overall winner

·      Emerging young journalists also shine

A total of eight (8) journalists and three (3) media outlets have emerged winners in the Data Journalism Awards focusing on women and leadership. The awards were organized by the Tanzania Media Women’s Association – Zanzibar (TAMWA ZNZ) in collaboration with the Office of the Chief Government Statistician (OCGS), the Association of Women with Disabilities Zanzibar (JUWAUZA), the Zanzibar Female Lawyers Association (ZAFELA), and the Pemba Environment, Gender and Advocacy Organization (PEGAO).

Award categories included radio, newspaper, social media, young media fellows (YMF), and media institutions promoting gender equality.

Out of the eight winners, five were recognized under the young media fellows’ category and were awarded certificates and an iPad each. These winners are:

1. Salum Ameir Salum

2. Zurima Ramadhan

3. Nihifadhi Abdulla Issa

4. Fatma Hamad Faki

5. Maryam Nassor Suleiman

Asya Hassan Bakar from Zanzibar Leo Newspaper emerged as both the overall winner and the winner in the newspaper category. She received a cheque for TZS 1.5 million, a certificate, and a trophy.

Another winner, Huwaida Nassor Moh’d from Assalam FM Radio, won in the radio category and received a cheque of TZS 1 million, a certificate, and a trophy.

In the social media category, Salum Ameir Salum was awarded and received a cheque of TZS 1 million, a certificate, and a trophy.

Regarding media houses, three media houses were recognized for their continued efforts in promoting gender equality in their daily work. Each was awarded a cheque of TZS 2 million and a certificate of appreciation. The awarded media outlets are:

·       Micheweni Community Radio

·       Mkoani Community Radio

·       Corporation of Government Newspapers

The organizers call upon journalists and media outlets to continue producing stories that focus on women and leadership statistics, promoting and upholding gender equality, highlighting the achievements of women, and uncovering barriers that hinder women from accessing leadership positions.

A total of 235 entries from various media including newspapers, radio, television, and social media were submitted for the competition. Of these, 120 entries were forwarded to the panel of judges for review, which resulted in the final selection of winners.

These awards are part of the implementation of the Strengthening Women in Leadership (SWIL) program, which is jointly implemented by TAMWA ZNZ, JUWAUZA, PEGAO, and ZAFELA, in collaboration with the Royal Norwegian Embassy in Tanzania.

Issued by:

TAMWA ZNZ, JUWAUZA, ZAFELA & PEGAO.

 

Share:

TANZANIA NA JAPAN WATIA SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA MPANGO WA PAMOJA WA UWEKEZAJI BIASHARA YA KABONI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan zimetia saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara ya Kaboni utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya Kaboni nchini Tanzania.

Utiaji saini wa makubaliano hayo umefanyika Mei 28, 2025 Tokyo, Japan kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Serikali ya Japan ikiongozwa na Waziri wa Mazingira, Mhe. Asao Keiichiro (Kei).

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo, Waziri Masauni amesema Makubaliano ya Mashirikiano yaliyosainiwa yamekusudiwa kuimarisha uhusiano kati ya Japan na Tanzania kwa maendeleo endelevu na hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Amesema ushirikano huu utaongeza fursa ya kupanua soko la Biashara ya Kaboni kutoka kwa wawekezaji wa Japan watakaowekeza katika miradi ya biashara ya Kaboni itakayoibuliwa nchini.

Waziri Masauni ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anawataka wataalamu kutoka nchi hizi mbili kufanya kazi haraka,kwa bidii, na kwa pamoja kwa manufaa ya nchi zote mbili ili kuhakikisha kuwa makubaliano hayo yanaenda katika hatua ya utekelezaji.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa “Tuko tayari kufanya kazi kwa ukaribu na wenzetu wa Japan ili kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kwa faida ya nchi zote mbili. Tayari Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeimarisha uwezo wa kitaasisi na kisheria katika usimamizi wa Biashara ya Kaboni ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais iliandaa kanuni za mwaka 2022 za kuratibu biashara ya Kaboni”.

Aidha, Mhandisi Mhandisi alibainisha kuwa katika Mfumo wa Kitaasisi, Serikali imeanzisha Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira iliyofanyiwa marekebisho ya 2025.

Hafla ya utiaji saini ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja, na Watendaji kutoka Ofisi hiyo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger