Saturday, 13 December 2025

WAZIRI HOMERA AZINDUA HUDUMA YA VYETI VYA KUZALIWA KWA MASAA 48 AITAKA TEHAMA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA HAKI

Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Dkt Juma Zuberi Homera baada ya kutoka kuzindua huduma ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ndani ya masaa 48.matumizi jijini Dar es Salaam tarehe 12 disemba 2025

Na Mwandishi Wetu Malunde 1 Blog 

Katika kuimarisha utoaji wa haki na huduma kwa wananchi, Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Dkt. Juma Zuberi Homera, amezindua rasmi huduma ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ndani ya masaa 48. 

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Taasisi ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Dkt. Homera amesema mpango huo utarahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi na kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa wakati, hatua ambayo itachangia kuimarisha uchumi wa taifa.

Dkt. Homera amesema masuala kama ndoa, vifo na mirathi yote yanahitaji vyeti ili wananchi waweze kupata stahiki zao, hivyo mpango huo wa masaa 48 utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zilizokuwa zikijitokeza. 

Amebainisha kuwa utekelezaji wa mpango huu ni sehemu ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais, unaolenga kuhakikisha haki inapatikana kwa haraka na ufanisi kwa Watanzania wote.

Katika ziara hiyo, Waziri Homera pia ametembelea Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na Roscoe of Tanzania, ambako amezindua magari mapya matatu yaliyotolewa na serikali—mawili kwa ajili ya wakuu wa taasisi na moja kwa matumizi ya wananchi pamoja na watumishi. 

Aidha, amewataka viongozi kuhakikisha wanatoa matamko yenye msingi wa utafiti ili kuepusha hasara na migogoro ya kisheria inayoweza kujitokeza kutokana na kauli zisizo sahihi.

Akiwa katika Shule ya Sheria Tanzania, Dkt. Homera amewasisitiza watendaji kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu, kuacha masilahi binafsi na kuhakikisha taaluma ya sheria inasimamiwa kwa weledi. 

Pia amehimiza matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma, akisisitiza kuwa mifumo ya kielektroniki itasaidia kuharakisha upatikanaji wa haki na kuongeza ufanisi katika taasisi za kisheria nchini.























Share:

Friday, 12 December 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 13,2025


Magazeti




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 12,2025

Magazeti
 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger