Sunday, 7 July 2024

LIGI YA BUTONDO KISHAPU SHAGY CUP YAHITIMISHWA KWA KISHINDO! BODABODA FC YALAMBA MIL. 1.5

...

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo na mdhamini wa ligi ButondoKishapu Shagi Cup

Na Sumai Salum - Kishapu

Timu ya Bodaboda Fc ya Kishapu mkoani Shinyanga imeibuka na  ubingwa wa mshindi wa kwanza kwa bao la goli 1 kwa "Nunge" (0) dhidi ya Fama FC ya Igaga katika Ligi ya Butondo Kishapu Shagy cup na kuondoka na kitita cha Tsh. 1,500,000/=.
 
Akizungumza Julai 6,2024 katika Viwanja vya shule ya Msingi Lubaga palipochezwa ligi hiyo wakati akifunga mashindano hayo Mbunge wa jimbo la Kishapu na mfadhili wa ligi iliyoanza Mei,15,2024 huku timu 16 zikishiriki  Mhe. Boniphace Butondo amesema kuwa mchezo umekuwa mzuri hakukuwa na taarifa zozote za matukio ya kutisha hivyo na hatoishia hapo bali michezo itaendelea.

"Pongezi kwenu mshindi wa kwanza (Bodaboda fc Kishapu),mshindi wa pili Fama FC pamoja na mshindi wa tatu Ngundangali FC kiukweli mmekuwa waungwana kwa kipindi hiki chote cha mashindano haya na hata leo ninapoyafunga nikiwa mgeni rasmi napenda kutamka kuwa hatutaishia hapa bali tujiandae hivi karibuni tena tutaanza kule Masanga ligi nyingine na nitafadhili kama kawaida jezi kwa timu zote kumi na sita (16) na mipira na timu zote zilizoshiriki ligi hii zitashiriki na Masanga pia tuwe tayari ndugu zangu", amesema Mhe. Butondo.

Aidha amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa kijiji cha Lubaga pamoja na serikali kwa kuwa na utayari wa kuipokea ligi hiyo na kuwa wavumilivu katika kipindi chote huku akitoa wito kwa viongozi wa timu zote kuhakikisha usajili wa wachezaji unaibua vipaji vya vijana wa ndani ya Kishapu kwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Joseph Mkude amezipongeza timu zote zilizoshiriki na kusema kuwa umewaweka pamoja vijana licha ya kuwa wanatoka maendmwo tofautitofauti ya Kishapu na nje.

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Kishapu na mwenyeji wa mashindano hayo Mhe. Joel Ndettoson amemshukuru Mbunge Butondo kwa mchango mkubwa wa kuwaleta vijana pamoja na kuwapongeza timu zote huku akiongeza kuwa si rahisi kombe kuvuka Daraja (kutoka nje ya watoto wa mjini kata ya Kishapu)

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga  Cde. Benard Werema ameendelea kuwashukuru vijana wote waliomwamini na kumuombea kuchaguliwa nafasi hiyo adhimu ya kuwatumikia wananchi na amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

Aidha zawadi mbalimbali za fedha taslimu zimetolewa kwa Golikipa Bora,Kocha bora,Msemaji Bora wa mashabiki,Timu yenye nidhamu pamoja na Mashabiki bora.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo na mdhamini wa ligi ButondoKishapu Shagi Cup akizungumza katika Viwanja vya shule ya Msingi Lubaga ligi hiyo ilipokuwa ikichezwa na timu kuni na sita (16)  akidhamini  kwa kutoa jezi na mipira kwa timu zote - Picha zote na Sumai Salum
Diwani wa kata ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson akizungumza kwenye kilele cha ligi ya Butondo Kishapu Shagy cup iliyofungwa na Mbunge wa jimbo hilo Mhe Boniphace Butondo ambae pia ni mdhamini wa ligi hiyo huku ushindi ukibakia kata ya Kishapu kwa Bodaboda FC.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Mkude akiwasalimia wananchi na kutoa pongezi kwa timu zote zilizoshiriki katika ligi ya Butondo Kishapu Shagy cup katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga Wilayani humo huku Bodaboda Fc ikiondoka na kitita cha 1,500,000 na kombe kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fama FC ya Igaga.
Mbunge wa jimbo la Kishapu  Mhe. Boniphace Butondo (kulia) na Mhe.Mkuu wa  Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakiteta jambo katika ufungaji ligi ya Butondo Kishapu Shagy cup huku bodaboda FC kuibuka na ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Fama FC  katika Viwanja vya shule ya msingi Lubaga wilayani humo
Kiungo Madia Madoshi aliyeiletea ushindi  Bodaboda Fc wa goli 1-0 dhidi ya Fama FC Ligi ya Butondo Shagi cup iliyomalizika  Julai 6,2024 katika Viwanja vya shule ya Msingi Lubaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga na kufungwa na mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo na kuondoka na kitita la 1,500,000 na kombe.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM mkoa wa Shinyanga Bw. Benard Werema akizungumza kwenye ufungaji ligi ya Butondo Kishapu Shagy Cup  katika uwanja wa mpira wa shule ta Msingi Lubaga huku bodaboda FC Kishapu ikiibuka mshindi wa kwanza katika  ligi hiyo.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger