Saturday, 13 July 2024

KATAMBI AENDELEA NA ZIARA KUELEZEA MIRADI YA MAENDELEO ALIYOITEKELEZA KWA WANANCHI

...

 





Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu,ameeleza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi jimboni kwake.

Amebainisha hayo leo Julai 12,2024 kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Kata Nne, ambazo ni Mwawaza, Masekelo,Ndala pamoja na Kambarage.
Amesema mwaka 2020 kwenye uchaguzi mkuu,wananchi walimpatia ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ili akawatumikie na kuwaletea maendeleo,na hadi sasa ametekeleza ahadi zake kwa asilimia 99.5,huku akimshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,kwa kumpatia fedha na kutekeleza miradi mingi kwa wananchi.

"Mwaka 2020 kwenye uchaguzi mkuu wananchi mlinipatia ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, na kazi yangu ni moja tu kuwatumikia na kuwaletea maendeleo," amesema Katambi.
"Maendeleo yetu ni faida yetu, ili tupate maendeleo lazima tuwe wa moja,na nimetekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 99.5"ameongeza Katambi.

Nao viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakiongozwa na Mwenyekiti Anorld Makombe, wamempongeza Mbunge Katambi kwa kazi kubwa ambayo anaifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi na kuitendea haki ilani ya uchaguzi ya CCM.
Nao Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga,kwa nyakati tofauti wakizungumza kwenye mkutano huo wakiongozwa na Meya Elias Masumbuko,wamesema miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa kwa wananchi, kwa kushirikiana na Mbunge chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Wametaja miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa ikiwamo sekta ya elimu,afya,kilimo,mifugo,maji, nishati,miundombinu ya barabara,ujenzi wa uwanja wa ndege,masoko,stendi ya mabasi na jengo la utawala manispaa ya Shinyanga.
Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko,amempongeza Katambi kwa uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwamo ya ujenzi wa masoko,na hata kusababisha ukusanyaji mapato kuongezeka kutoka bilioni 2 hadi bilioni 6.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe akizungumza kwenye mkutano huo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye mkutano huo
Katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga akizungumza kwenye mkutano huo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger