Wednesday, 5 June 2024

SHUWASA YAENDESHA WARSHA KWA MADIWANI, YAANIKA HATUA ZILIZOFIKIWA UJENZI MRADI MKUBWA WA MAJI SHINYANGA

...

Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Ndugu. Said Kitinga akizungumza wakati akifungua warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imeendesha warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kueleza utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA na hatua zilizofikiwa kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa eneo linalohudumiwa na SHUWASA.

Warsha hiyo imefanyika leo Jumatano Juni 5,2024 katika Ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga
kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Wakili Julius Mtatiro.

Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga amesema mradi huo mkubwa unaenda kumaliza tatizo la maji Shinyanga huku akiishukuru serikali kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maji ili kutatua changamoto za wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola ameeleza kuwa kupitia mradi huo ambao tayari utekelezaji wake unaendelea wanaenda kumaliza tatizo la huduma ya maji katika maeneo yote ya Shinyanga.

Mhandisi Katopola ameeleza kuwa hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa sasa ni nzuri katika maeneo yote wanayoyahudumia na kwamba SHUWASA imeendelea kupanua mtandao wa maji safi, kuongeza mapato yatokanayo na mauzo ya maji, kuongeza idadi ya wateja, kupunguza upotevu wa maji na inaendelea na ujenzi na utekelezaji wa miradi ya maji.

Ameeleza kuwa, SHUWASA inajihusisha na utoaji wa huduma ya maji safi na usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Miji midogo ya Tinde, Didia na Iselamagazi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mhandisi Katopola amesema mnamo tarehe 20.06.2022, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ilisaini Mkataba wa fedha na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (French Development Agency - AFD) kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wenye thamani ya EURO milioni 76 (Euro 75 ni mkopo wa riba nafuu toka Shirika la Maendeleo la Ufaransa na Euro milioni 1 zinatolewa na Serikali ya Tanzania).

Nao washiriki wa warsha hiyo, mbali na kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya maji ili kumtua mama ndoo kichwani huku wakishauri mradi huo utakelezwe kwa wakati ili kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa Shinyanga.

Aidha wameshauri wananchi waendelee kushirikishwa kuhusu hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na utoaji elimu kwa jamii.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Ndugu. Said Kitinga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Wakili Julius Mtatiro leo Jumatano Juni 5,2024 katika Ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakati akifungua warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa lengo la kueleza utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA na hatua zilizofikiwa kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa eneo linalohudumiwa na SHUWASA. PICHA na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akizungumza kwa niaba na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro leo Jumatano Juni 5,2024 wakati akifungua warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA

Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza wakati wa warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger