Sunday, 30 May 2021

CHAVITA KOROGWE YAENDESHA WARSHA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA

...

CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) wilayani Korogwe mkoani Tanga kimeendelea kutoa elimu kwa watoa huduma za Afya wilayani  ili itumike kwa watu wenye ulemavu viziwi kuweza kupata huduma bora  za Afya  pindi wanapofuatilia upatikanaji wa huduma katika  vituo vya afya.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civil Society (Fcs), yanalenga kuwahakikisha watu wenye ulemavu wanatambuliwa wanapata takwimu au taarifa ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati ya huduma za afya ipasavyo ili kuodokana na dhana ya unyanyapaa

Akiongea wakati wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa CHAVITA wilaya ya Korogwe Happyness Kuboja alisema kuna wakati wanfuatilia huduma hizo wanapata vikwazo kutoka kwa wahudumu wa Afya kwa kutozingatia miongozo inayotolewa na serikali juu ya kuwapatia kipaumbele Watu wenye ulemavu. matokeo yake tunakosa huduma ama kupata huduma tofauti na ugonjwa wenyewe wanapofika katika vituo vya kutolea huduma za afya kiasi cha kushindwa kupata matibabu.

“Tumekuwa tukipata kero nyingi sana tunapokwenda kupata huduma za afya kutokana na wahudumu kutokuelewa miongozo mbali mbali inayowahusu linalotupelekea wakati mwingine kukosa huduma na kuishia kurudi nyumbani huku tatizo likiwa linabaki bila kupatiwa ufumbuzi alisema Kuboja.

“Lengo kubwa lamafunzo haya ni kuwaelimisha wahudumu wa afya jinsi ya kupanganga mikakati ya uboreshaji wa huduma kuwapokea na kuwahudumia wenye ulemavu wa kusikia na wengineo  wakati wanapofika kupata huduma” aliongeza.

Kuboja aliiomba serikali kutenga bajeti ambayo ni endelevu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa wahudumu katika taasisi zote ili kuweza kuwajenga kimawasiliano na kuondoa dhana potofu inayopelekea wenye ulemavu kuonekana ni watu wasiofaa kwenye jamii.

Naye Katibu wa chama hicho ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa mafunzo hayo Mr Ally Nassoro alisema mafunzo hayo ya siku tatu ni maalun kwa wahudumu wa afya pekee lakini pia wataendelea kuyatoa kwa wahudumu wengine ili kuweza kujenga wigo mpana wa upatikanaji wa huduma  kati ya watu wenye ulemavu 

Nassoro alifafanua kwamba kwa kufanya mafunzo hayo wataweza kuondoa hali ya unyanyapaa kwa wenye ulemavu wanapokwenda kutibiwa hospitali na vituo vya Afya.

“Tunajaribu kuwaelimisha wahudumu kufuata miongizo na Sera ya Taifa ya huduma za afya alisema.

Pia aliwataka wale wote wanaopata mafunzo hayo kutumia vyema katika hospitali na vituoni kuwapatia huduma bora watu wenye ulemavu.

Aidha washiriki wa mafunzo hayo walipendekeza Kupatiwa mafunzo ya mawasiliano ya Lugha ya Alama ili kuweza kuwasilisha na viziwi pindi wanapofika maeneo ya huduma hii itakuwa rahisi kwao kuwahudumia ipasavyo.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger