Thursday 3 December 2015

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI LEO#HAPA KAZI TU#

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam  Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ULE “moto” aliouwasha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Kassim Majaliwa kwenye bandari ya Dar es Salaam wiki iliyopita, na kukolezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wa kumsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw.  Rished Bade, umeendelea kusambaa kwenye eneo lote la bandari na viunga vyake baada ya leo tena Bw. Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta makontena mengine 2431yenye bidhaa  hayajulikani yaliko.
Baada ya kugundua hilo tena kwa ushahidi wa nyaraka, Waziri Mkuu ambaye wiki iliyopita aliahidi kuwa "Tunataka ku-deal na wajanja wajanja wa TRA." ameagiza kabla ya jua kuzama leo hii Desemba 3, 2015, awe amepata majibu ya kina na timilifu juu ya “uhuni” huo uliofanywa na watumishi wa umma pale bandarini. Waziri Mkuu pia alifanya ziara kama hiyo pale stesheni kuu ya reli iliyo chini ya Kampuni ya Reli Tanzania TRL



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scaner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015  kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo  Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali.(Picha na Ofisi ya Waziri )




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu,  Kassim Majliwa  akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es salaam kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea steheni ya reli ya Dar es salaam Desemba 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hii ndiyo bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa takriban wiki mbili sasa, imekuwa gumzo kwa wakazi wa jiji na nchi jirani baada ya Utawala wa serikali ya awamu ya tano kuanzisha "fagio" la chuma.
 Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandarini na shirika la http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=308888&d=1449148891 
reli Tanzania(TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini. Katika maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.
Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.

Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger