Tuesday 2 April 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 3, 2024



\
Share:

SERIKALI KUENDELEA KUWALEA WAZALISHAJI,WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI WA NDANI



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na wa Makatibu Wakuu unaojumuisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu wakiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bw. Rashid Mchatta walipotembelea Kiwanda cha Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industry Limited kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani Machi 30,2024 kujionea shughuli za uzalishaji na kutatua changamoto.

 ............... 

Serikali itaendelea kuwalea wazalishaji wawekezaji na wazalishaji wa ndani ya nchi ili waweze kukuza mitaji yao na kuchangia katika maendeleo ya ya Taifa kwa ujumla. 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, wakati wa ziara yake kwenye Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industry Limited kilichopo Kibaha mkoani Pwani tarehe 30 Machi 2024. 

Akiongoza ujumbe wa Makatibu Wakuu wakiwemo Dkt. Natu Mwamba (Wizara ya Fedha), Dkt. John Jingu (Wizara ya Afya), na Bw. Rashid Mchatta (Katibu Tawala Mkoa wa Pwani), Dkt. Abdallah alieleza kuwa lengo la ziara hiyo lilikuwa kujionea shughuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto zinazokikabili Kiwanda hicho na kutafuta suluhisho. 

Dkt Abdallah pia alibainisha kuwa Ziara hii inaashiria dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha sekta ya viwanda nchini kwa kuwaunga mkono wawekezaji wa ndani na kuwawezesha kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Dkt. Abdallah akiwa na ujumbe huo alikipongeza Kiwanda hicho kwa utendaji kazi mzuri na kuahidi ushirikiano kutoka kwa wizara husika katika kutatua changamoto zilizopo ili kuwezesha kiwanda hicho kufanya kazi kwa ufanisi Vilevile. 

Alibainisha kuwa Kiwanda hicho kinachotoa ajira za moja kwa moja 200 na zisizo za moja kwa moja 300 ni moja ya Kiwanda cha kimkakati kinacholzalisha dawa za maji tiba (Fluid Therapy) mbalimbali Nchini ili kupunguza utegemezi wa kuagiza dawa hizo nje ya nchi. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Dkt Muganyizi Kairuki akitoa taarifa kwa ujumbe huo amesema Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha chupa za maji tiba milioni 50 kwa mwaka ambapo asilimia 60 huuzwa nchini wakati asilimia 40 huuzwa Nchi za nje zikiwemo Rwanda, Comorro, Malawi, Zambia, Namibia, Congo, Mozambique na Yemen


 Vilevile ametaja baadhi ya Dawa zilizosajiliwa kuzalishwa kiwandani hapo kuwa ni pamoja na "Sodium Chloride (0.9%w/v), Compound Ringer Lactate, Dextrose (5%w/v) &Sodium Chloride(0.9%w/v), Dextrose (5%w/v ) na Dextrose(10%w/v). Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na wa Makatibu Wakuu unaojumuisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu wakiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bw. Rashid Mchatta walipotembelea Kiwanda cha Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industry Limited kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani Machi 30,2024 kujionea shughuli za uzalishaji na kutatua changamoto.
Share:

MWALIMU NA MWANAFUNZI WAUAWA MBEYA


Watu wawili jinsi ya kike wakazi wa Kiwanja Kata ya Mbugani Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wameuawa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka miwili kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali nyumbani kwao.

Waliouawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani na Mkazi wa Kiwanja kata ya Kiwanja Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya na mwingine ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye.

Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni Machi 31,2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake.

Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya baada ya kutoonekana bidhaa hizo ziliachwa nje.

Akizungumza na EATV Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiwanja mahali alipokuwa akiishi mwalimu huyo Gideon Peter Kinyamagiha amesema walifika nyumbani kwa marehemu na walipoingia ndani walikuta sururu ikiwa na damu na marehemu wawili na mtoto wa kiume wa mwalimu huyo akiwa amejuriwa uongozi ulitoa

Kinyamagoha anasema baadaye walitoa taarifa Polisi ambao nao walifika na kufanya uchunguzi wa awali kisha kuchukua miili na kwenda kuihifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi ambapo majeruhi amekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.

Tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamtafuta mtu/watu waliohusika katika tukio hilo la mauaji ya aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani Heriety Lupembe (37) na Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Isenyela Ivon Tatizo (15) wote wakazi wa Kijiji cha Kiwanja Wilaya ya Chunya
SACP Benjamin Kuzaga


Kwa Mujibu wa taarifa ya jeshi la Polisi SACP Benjamin Kuzaga inaeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 31, 2024 majira ya saa 2:30 usiku wakati marehemu akiwa nyumbani kwake sebuleni na watoto wawili Ivon Tatizo na Haris Barnaba Mtweve (06) Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Mchepua wa kiingeleza ya Ken Gold aliyejeruhiwa kwa kupigwa kitu butu kichwani.

Kamanda Kuzaga Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, mtu huyo aliwavamia marehemu na kuanza kuwashambulia na baada ya kufanya hivyo alifunga milango kwa nje na kuondoka na funguo. 

Chanzo cha tukio hili bado kinachunguzwa.

Majeruhi mtoto Haris Mtweve anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi wa tukio hili ikiwa ni Pamoja na msako dhidi ya mtu au watu waliohusika. 

Aidha, linatoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa za mtu au watu waliohusika katika tukio hili kutoa taarifa ili wakamatwe.

CHANZO - EATV
Share:

Monday 1 April 2024

MAANDALIZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2024 YAKAMILIKA


 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Tabia Mwita akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru leo Aprili 1, 2024, Mkoani Kilimanjaro. Katikati ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kushoto) akieleza jambo Viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Watendaji kutoka ofisi yake na Kamati mara baada ya kukagua hatua za maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Mkoani Kilimanjaro.
Sehemu ya vijana wa Halaiki wakiwa katika mazoezi kwenye uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), kuelekea uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Kilimanjaro.

Na; Mwandishi Wetu – Kilimanjaro

Serikali imesema kuwa shughuli za maandalizi kuelekea kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 zakamilika.

Amesema hayo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Tabia Mwita, leo tarehe 1 Aprili, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa mwenge huo.

Aidha, WAZIRI Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru 2024 Kitaifa zitakazofanyika katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), tarehe 2 Aprili, 2024, Mkoani Kilimanjaro.

Amesema baada ya uzinduzi mwenge huo utakabidhiwa kwa vijana sita kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuukimbiza katika mikoa 31 yenye jumla ya halmashauri 195 za Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa siku 195.

Kwa upande wengine, Mhe. Tabia Mwita amesema kwa kipindi chote cha kuukimbiza Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kuhamasisha amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa pamoja na kuwahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni “Kutunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.
Share:

MPENZI WANGU ANAVUTA SIGARA HADI NASHINDWA KUMBUSU!


Jina langu naitwa Jesca kutokea Arusha, Tanzania, wakati naanza mahusiano na mpenzi wangu nilimkuta ni mtu anayekunywa sana pombe na kuvuta sigara, ndio ulikuwa mtindo wake wa maisha kila siku.

Binafsi sipendi kabisa harufu ya sigara, kwa kuwa nilimpenda nilifumbia macho lile tatizo nikiamini kwamba kadri muda unavyokwenda naweza kumbadilisha.

Nilimudu pale mwanzoni ila siku zilivyosogea ikawa ni kero kubwa kwangu, wakati mwingine nilikua nashindwa hata kumbusu, kwa kifupi nilikuwa sifurahii kabisa penzi langu ingawa sikutaka kumuonyesha.

Nakumbuka tena harufu ile ya sigara ilikua inanishinda kabisa asubuhi, kinywa cha mtu anayevuta sigara kinakuwa na harufu ya utofauti kama hupendi harufu ya sigara lazima ikukere.

Kwa kua na yeye hakua tayari kuacha, nilishindwa kuendelea naye nikamwambia tu kwamba tuishie pale, nikachukua vitu vyangu na kurudi kwa wazazi wangu. 

Nikiwa nyumbani kwetu kuna ndugu yangu alikuja na kumueleza changamoto hiyo, naye aliniambia kuna mtu anaweza tusaidia hadi mpenzi wangu kuacha kutumia pombe na sigara tena ndani ya muda mfupi.

Alichukua simu yake kunipatia namba ya Kiwanga Doctors ambayo ni +254 769404965  kisha tutawasiliana na Kiwanga Doctors.

Kiwanga Doctors alitueleza kitu tunachoweza kufanya ili kushinda hali hiyo na kutupatia tiba, nilirudi kwa mpenzi wangu na ndani ya muda mfupi mpenzi wangu aliacha kuvuta sigara kabisa na kuachana na pombe. Shukrani sana kwa  Kiwanga Doctors.

Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.

Mwisho.

 


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 1, 2024

 






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger