Saturday 4 November 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 3,2023

                            
Share:

ZAMBIA YATUA TANZANIA KUJIFUNZA MBINU ZA KUPAMBANA NA UJANGILI NA BIASHARA HARAMU YA NYARA NA MAZAO YA MISITU

Na John Bera - Manyara

Timu  ya  Maafisa Wandamizi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Zambia vinavyohusika na uzuiaji ujangili wamefika nchini kwa lengo la  kujifunza namna Tanzania ilivyofanikiwa katika mapambano dhidi ujangili. 

Timu hiyo iko nchini kwa siku tano kuanzia Oktoba 29 hadi 4 Novemba  2023.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Hifadhi ya Ziwa Manyara, Kamishna wa uzuiaji ujangili nchini Zambia, Brigedia Jenerali, Herman Kamwita ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Zambia  alisema wamekuja kuona  namna Tanzania ilivyofanikiwa kuendesha operesheni za kupambana na ujangili na utekelezaji wa Mkakati wa kupambana na ujangili.


Alisema Kamisheni ya kudumu ya Tanzania na Zambia ya Ulinzi na Usalama ilipendekeza Mamlaka ya nchi hizo mbili kuwa na utaratibu wa kubadilisha uzoefu katika kulinda rasilimali za wanyamapori na misitu.

Alisema wameweza kupitishwa katika mbinu mbalimbali  ambazo Tanzania inatumia katika kupambana na ujangili na kuwa wamepanga kwenda kuzitumia wakirudi nchini kwao.


Aliongeza kuwa, "Pia tumepata fursa ya kwenda Hifadhi ya Ziwa Manyara na tumeona wanyama mbalimbali na hii imedhihirisha namna wenzetu walivyopiga hatua kwenye uhifadhi na niwahakikishie kuwa tutakwenda kutumia mbinu hizi ili kuimarisha sekta ya utalii nchini kwetu.’’ 


Awali, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Uzuiaji Ujangili na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi Taifa  Bw. Kiza Yusuph Baraga alisema wamepokea ugeni kutoka Zambia na kuwa kupitia ziara hiyo pande hizo mbili zimebadilishana uzoefu.

"Pia imekuwa ni nia ya nchi yetu kuendelea kutangaza utalii hasa kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza Utalii kupitia filamu ya The Royal Tour. "

Alisema ugeni huo pia umepata fursa ya kujionea vivutio vya utalii baada ya kutembelea Hifadhi ya Ziwa Manyara na kushuhudia shughuli mbalimbali za utalii ambazo zinafanywa kwa teknolojia ya hali ya juu.

"Wamefurahi sana na wametuahidi kuwa sehemu ya kutangaza utalii wetu nchini Zambia. Nitoe wito kwa watalii mbalimbali husani wa ndani ya nchi na nje ya nchi kuja kutembelea vivutio vyenye wanyama wengi."

Naye Kamshina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini, Betrida Lyimo alishukuru wizara kupeleka ugeni huo katika Ikolojia ya Tarangire Manyara na kuwa wameweza kubadilishana mambo mengi.

Kwa upande wake Wakili Mwandamizi Ofisi ya Mashtaka Makao Makuu ambaye pia ni Mratibu wa upelelezi, uendeshaji wa kesi za makosa ya rushwa, udanganyifu na utakatishaji fedha sehemu ya makosa ya mazingira na maliasili wa Kikosi cha Taifa ya Kupambana na Ujangili Theophil Daniel Mutakyawa alisema kupokea ugeni huo na kubadilisha uzoefu ni mwanzo wa kushirikiana katika kupambana na ujangili kwa kubadilishana taarifa.

Alisema makosa ya ujangili ni makosa yanayovuka mipaka yanayohitaji nguvu ya pamoja ya nje ya nchi, kikanda katika kupambana uhalifu huo mkubwa.

"Tumezungumza na kuelewana kuwa sasa wanaporudi nchini kwao na sisi kubaki huu utakuwa mwanzo wa kuendelea kupeana uzoefu, kupeana taarifa ili tuweze kupambana na uhalifu mkubwa."


Share:

DC NGARA  : MAADILI NI NGUZO MUHIMU KATIKA JAMII


Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi akifungua mafunzo ya maadili kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Ruleje Wilayani Ngara tarehe 02 Novemba,2023

Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya ziwa -Mwanza Bw Godson Kweka akitoa neno la utangulizi katika mafunzo ya maadili kwa viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Ngara.Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Ruleje Wilayani Ngara tarehe 02 Novemba,2023


Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya maadili kwa watumishi na viongozi wa halmashauri ya Ngara. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Kanisa katoliki Ruleje wilayani Ngara tarehe 02 Novemba,2023.




Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya maadili kwa viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Kanisa katoliki Ruleje wilayani Ngara tarehe 02 Novemba 2023.



......

Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi amesema kuwa Maadili ni nguzo muhimu katika kufanikisha mipango ya maendeleo ya nchi yoyote duniani.

Kanali Kahabi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya Maadili kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa- Mwanza yalifanyika tarehe 02 Novemba,2023 katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Rulenge Wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Katika hotuba yake Kanali Mathias alisema kuwa, "Maadili kwa kiongozi na mtumishi wa umma yana umuhimu mkubwa sana katika utawala na maendeleo ya nchi kwani Kiongozi ama mtumishi wa umma anapokuwa na maadili katika utendaji kazi wake, atahakikisha anafanya kazi kwa uaminifu mkubwa na kusimamia vyema rasilimali za nchi ili ziweze kuwanufaisha wananchi na kuieletea serikali maendeleo."

Kwa mujibu wa Kanali Mathias, kiongozi ama mtumishi wa umma anapokua na maadili anakua na ujasiri wa kusimamia Sheria, Kanuni, na Taratibu za nchi. “Huwezi kuwa na ujasiri wa kusimamia sheria inayokataza mienendo ama tabia isiyofaa kama wewe mwenyewe mwenendo wako sio mzuri lazima nafsi ikusute” alisema.

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ya Ngara, alitumia fursa hiyo kuwaonya watumishi wenye mienendo isiyofaa kuacha mara moja tabia hizo. “Kuna viongozi na watumishi wenzangu kutoka Ofisi nyeti kabisa mmekua mkianzisha migongano ambayo haina tija unakuta mtumishi hamuheshimu mkuu wake wa kazi huo ni utomvu wa nidhamu sio sahihi kabisa muache mara moja,” alisema

Kanali Mathias alionya tabia ya baadhi ya watumishi kutumia lugha chafu kwa Viongozi. “Tunawaona baadhi yenu kwenye mitandao ya kijamii mnaanzisha mijadala ya hovyo isiyokuwa na tija kuwasema na kutumia lugha chafu dhidi ya Viongozi, muache mara moja huko ni kukosa maadili” alisema.

katika hatua nyingine, Kanali Mathias alitoa rai kwa washiriki hao kuhakikisha kuwa wanaishi yote yanayoelekezwa katika mafunzo hayo. “Ndugu washiriki tunajifahamu sisi tulioko hapa Ngara tunaguswa vipi na mafunzo haya? Jamani tubadilike leo tuna mafunzo haya yakatubadilishe kama hatutaki kubadilika sisi wenyewe basi sheria zitatubadilisha kwa lazima,” alisema

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa Bw, Godson Kweka alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili imefanya mafunzo hayo katika wilaya ya Ngara kutokana na changamoto mbalimbali za kimaadili zinazoikabili Wilaya hiyo.

Bw. Kweka alieleza kuwa kumekua na tabia ya baadhi ya watumishi na viongozi katika Halmashauri hiyo kutoa siri za serikali kinyume na taratibu. “Wapo baadhi ya waheshimiwa mkiwa kwenye vikao vya maamuzi hata kabla kikao hakijaisha taarifa tayari ziko kwenye mitandao ya kijamii jambo hili ni kinyume na taratibu na ni kosa kisheria,” alisema.

Bw. Kweka alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya madiwani wenye tabia ya kuwakataa watumishi katika Halmashauri bila kuwa na sababu yoyote ya msingi. “Unakuta serikali inaleta watumishi ambao ni wataalamu katika nyanja mbalimbali katika Halmashauri lakini Mhe. Diwani unasimama na kusema hatumtaki mtumishi huyu hafai , sote tunafahamu kuwa ipo sheria ya utumishi wa umma ambayo ina taratibu na hatua za kumchukulia mtumishi aliyefanya makosa kwa hiyo kama kuna jambo taratibu za kuwasilisha suala hilo kwenye mamlaka husika zifuatwe.“

Aidha, Bw. Kweka alikemea vikali tabia ya baadhi ya waheshimiwa Madiwani kuingilia shughuli za kiutendaji. “Kumekua na tabia ya baadhi ya waheshimiwa madiwani kwenda kwenye vituo vya kazi anakwenda shuleni ama zahanati anachukua daftari la mahudhurio anachora mstari na kuulizia mtumishi huyu yuko wapi jamani huko ni kuingilia utendaji wa Viongozi waliopo watumishi hao wana wasimamizi wao kwa hiyo kila kiongozi afanye kwa mamlaka ya nafasi yake,” alisema.

Mada mbalimbali ziliwasilishwa katika mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na mada kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na mada kuhusu mgongano wa Maslahi na uwajibikaji wa pamoja.
Share:

Friday 3 November 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 4,2023









Share:

WASHINDI SHINDANO LA BE ROAD SAFE KWA NJIA YA SANAA WATUNUKIWA TUZO, RC DAR AIPONGEZA PUMA ENERGY TANZANIA

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Amend wametoa tuzo kwa wanafunzi ambao wameibuka washindi wa michoro ya usalama barabarani kupitia  kampeni ya Be Road Safe kwa njia ya sanaa.

Katika utoaji wa tuzo huo umefanyika katika Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ambaye aliwakilishwa ba Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo .

Kampeni hiyo inalenga kuleta mageuzi ya usalama wa watoto na vijana barabarani nchini Tanzania huku ikielezwa wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Kubugumo,  Kufaru,  Msewe, Kibasila na Mtambani wameshiriki katika kampeni hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo shindano la kuchora.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila,  wakati wa utoaji tuzo hizo kwa washindi,  Mkuu wa Wilaya Halima Bulembo amesema wanaipongeza kampuni ya Puma Energy Tanzania pamoja na Ammend kwa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watoto walioko shule za msingi.

Asema mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto walioko katika shule za msingi yatasaidia kupunguza ajali za barabarani hususan katika maeneo ambayo mafunzo hayo yametolewa huku akishauri elimu hiyo yatolewe nchi nzima kuongeza uelewa.

Amesisitiza Serikali inaamini kwa kufanya hivyo kitaokolewa kizazi cha sasa na kijqacho kwa kuwa elimu ya matumizi bora ya barabara inaendelea kusambaa.

Amesema kuwa kupitia mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto hususan walioko katika shule za msingi Puma imefanya jambo kubwa katika kuepusha ajali za barabarani ambazo zimekuwa sikiisababishia nchi hasara kubwa kwa kupoteza nguvu kazi na mali.

"Mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yaliyotolewa na Puma Energy Tanzania kwa kushirikiana na Ammend katika shule tano ni vyema yakatolewa pia katika shule nyingi zaidi kuwajengea uwelewa watoto wangi wa Dar es Salaam na hata nje ya mkoa huo.

"Serikali ya mkoa (Dar es Salaam) tunaamini kuwa kwa kufanya hivi tunaokoa kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa elimu ya matumizi bora na sahihi ya barabarani inaendelea kusambaa," amesema Bulembo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah, amesema mafunzo yaliyotolewa kwa wanafunzi hao ni utekelezaji wa mpango wa 'Be road safe Africa) unaotekelezwa na Ammend katika nchi tano za Afrika ambazo ni Zambia, Zimbabwe, Tanzania, Botswana na Ghana.

Amesema kuwanzishwa kwa mpango huo kunatokana na takwimu mbaya za ajali za barabarani ambazo zinasababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

"Nchini Tanzania pekee Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani kimetoa takwimu zinazoonyesha kutokea kwa vifo 1,545 na majeruhi 2,278 kwa mwaka 20222 kutokana na ajali 1,720 za barabarani.

Fatma akizungumzia kampeni hiyo ya 'Be Road Safe' amesema kuwa ni jukwaa muhimu shirikishi linalokuza jamii salama kwa watoto.

 "Kupitia mashindano hayo ya kuchora tumeongeza ubunifu na uelewa thabiti wa kanuni za usalama barabarani miongoni mwa wanafunzi na kuongeza ufahamu kwa jamii ya Watanzania.

Amesema tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 2013 'Be Road Safe' umekuwa mwanga wa matumaini na kwamba ni msingi wa kimkakati wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) wa kampuni hiyo chini ya mpango mkuu wa 'Be Puma Safe' ambao pia unajumuisha uwezeshaji wa wananchi hususan vijana.

Hafla hiyo iliyofanyika Shule ya Msingi Kibugumo ilihidhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Michael Deleli, Mkurugenzi wa Shirika la Ammend Simon Kalolo, walimu na wanafunzi kutoka shule zilizoshiriki mafunzo na shindano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo(wa tatu kulia) akimkabidhi kikombe mwanafunzi wa darasa sita katika Shule ya Msingi Kibugumo Feisali Msiakwe baada ya kuibuka mshindi wa mchoro wa usalama barabarani na kuifanya shule yake kuwa kinara katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Amend.Wengine katika picha hiyo ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Fatma Abdallah( wa kwanza kushoto), Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kibugumo Salvatory Lasway ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo( wa kwanza kulia).

Mwanafunzi wa darasa sita katika Shule ya Msingi Kibugumo Feisali Msiakwe akinyanyua juu kikombe cha ushindi baada ya mchoro wake wa kuelimisha kuhusu usalama barabarani kushinda katika shindano la michoro ya usalama barabarani kwa Mkoa wa Dar es Salaam.Feisali amepata kitita cha Sh.500, 000 na shule yake baada ya kuibuka mshindi wa mchoro wa usalama barabarani na kuifanya shule yake imepata Sh.milioni tano ambazo zimetolewa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kupitia Mkurugenzi wake Fatma Abdallah(wa kwanza kushoto waliosimama.)
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo(wa tatu kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Abdallah( wa kwanza kushoto) wakiwa wameshika mfano wa hundi ya Sh.milioni tano iliyotolewa kwa Shule ya Msingi Kibugumo baada ya mwanafunzi wake Feisali Msiakwe ( wa nne kushoto) kuibuka mshindi wa mashindano ya mchoro wa usalama barabarani katika mkoa wa Dar es Salaam.Mashindano hayo yameandaliwa na Puma kwa kushirikiana na Shirika la Amend Tanzania.Wengine katika picha hiyo ni walimu na wadau wa usalama barabarani.












Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger