Thursday 14 September 2023

DC DODOMA ATAKA MAOFISA TARAFA,WATENDAJI WA KATA,WENYEVITI WA MITAA JIJI LA DODOMA KUSIMAMIA KWA UFANISI ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri,akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili ya kujenga uwezo kuhusu mfumo wa Anwani za Makazi kwa Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma.


Mratibu wa Anwani za Makazi Kitaifa kutoka Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Jampyon Mbugi,akitoa maelezo kuhusu Mafunzo ya kujenga uwezo wa Mfumo wa Anwani za Makazi Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili ya kujenga uwezo kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma.


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili ya kujenga uwezo kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amewataka Maofisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuwa anuani za makazi ni hitaji la msingi kwasasa kutokana na kukua kwa teknolojia nchini.

Shekimweri ameyasema hayo leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kujenga uwezo Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi.

“Kwa sasa hivi ni rahisi kuita gari la kukodi (Uber) ukaonesha eneo unapokwenda na huduma hiyo ikakufikia, hivyo unaweza kuita huduma ukiwa nyumbani kwako,”amesema Bw.Shekimweri

Amesema kuwa taarifa zinaonesha kwamba uwepo mfumo wa anwani za makazi nchini tayari umeleta mafanikio makubwa katika utendaji kazi wa serikali ikiwamo ufuatiliaji wa kodi za serikali.

“Zoezi hili ni lazima likatekelezwe kutokana na Jiji linakua kwa kasi, makazi yanaongezeka, mitaa inaongezeka hakuna namna zaidi ya kuziingiza taarifa hizi kwenye mifumo yetu, zoezi hili ili lifanyike kwa mafanikio ni lazima liwe shirikishi hasa madiwani hivyo kwenye mpango kazi muone umuhimu wa kuwashirikisha,”amesema

Hata hivyo ametoa wito kupitia vikao vya kisheria ikiwamo Mabaraza ya madiwani kupewa muda wa kuwasilisha elimu ya suala hilo na wajibu wao wa kuhamasisha wananchi kujisajili na mfumo wa anwani za makazi.

Kwa upande wake Mratibu wa Anwani za Makazi Kitaifa kutoka Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Jampyon Mbugi, amesema hadi sasa Jiji la Dodoma limekusanya taarifa na kutoa anuani za makazi 245,000 kati ya hizo 163,000 ni za majengo na 81,277 ni viwanja vitupu.

“Wananchi 299,330 ndio waliosajiliwa kwenye mfumo wa anwani za makazi, idadi hii haiakisi uhalisia wa takwimu za idadi watu waliopo ndani ya Jiji la Dodoma inayokadiriwa kuwa zaidi ya 765,000,”alisema.

Aidha amesema kuwa zaidi ya wananchi 465,849 hawajasajiliwa kwenye mfumo huo na hivyo serikali imeamua kuongeza msukumo wa suala hilo hususan kwa kutumia Wenyeviti, Watendaji wa Kata na Mitaa.

''Dhamira ya Wizara ni kuhakikisha Dodoma inakuwa ya mfano na kuwa chachu kwa halmashauri zingine kuja kujifunza namna ya kufanikisha utekelezaji wa mfumo huo.''amesma Mhandisi Mbugi
Share:

MPYA:TANGAZO KUTOKA NECTA KWA WANAFUNZI ACSEE 2024

Share:

WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA IDARA YA MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama.(kulia) akimsikiliza Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw.George Lugome wakati akielezea kuhusu kazi ya mtambo wa kukata karatasi mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama.(kulia) akimsikiliza Mpiga Chapa Msaidizi Mkuu Bw.Ophin Malley mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akiwa pamoja na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw.George Lugome akichukua maelezo kuhusu Mashine ya kuprint maandishi kutoka kwenye kompyuta kwenda kwenye bati (CTP) mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akioneshwa nyaraka iliyochapwa na moja ya mashine katika kiwanda mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akitazama nyaraka za Serikali zilizochapwa na moja ya mashine katika kiwanda mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akitazama nyaraka za Serikali zilizochapwa na moja ya mashine katika kiwanda mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akimsikiliza Fundi wa Mashine za utengenezaji wa mihuri Bw.Mohammed Ally mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mpiga Chapa Msaidizi Bw.Mosses Sampa akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama gazeti la Serikali la Kwanza kuchapishwa mwaka 1961 mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama akitazama baadhi ya vitabu katika maktaba ya Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama (kulia) akizungumza na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw.George Lugome kwenye maktaba ya Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama (kulia) akimsikiliza Mpiga Chapa Msaidizi Bw.Pater Kikuli mara baada ya kufanya ziara kutembelea Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali leo Septemba 14,2023 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA MAPYA AJIRA ZA AFYA-SEPTEMBA 2023

Share:

TBS YAWATAKA WAZALISHAJI WA MABATI KUZALISHA MABATI YENYE VIWANGO


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania limewataka wazalishaji wa Mabati nchini kuzalisha mabati kwa mujibu wa viwango ili kuepuka usumbufu na gharama zisizo za lazima.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Septemba 13,2023 Jijini Dar es Salaam, Afisa Viwango Bw.Anold Mato amesema bati zinazofaa kwaajili ya kuezekea nyumba ni geji isiyozidi 30.

Amesema bati nyingine zimetengenezwa kwa ajili ya shughuli nyingine kama kutengenezea uzio wakati wa utekelezaji wa miradi, lakini si kwa kuezekea nyumba.

"Mzalishaji wa mabati yenye geji 32 ambayo kwa kawaida ni kwaajili ya uzio, mzalishaji anatakiwa kuweka taarifa ambayo inaonesha kuwa mabati hayo ni kwaajili ya kutengenezea uzio na si kuezekea nyumba". Amesema

Aidha amesema kuwa bidhaa ya mabati imewekwa viwango maalumu vya ubora vinavyostahili kutumika na wazalishaji ambapo bati hutengenezwa kwa chuma na kupakwa madini ya zinki au aluminium zinki ili yawe na uwezo wa kuhimili kutu.

"Viwango vya mabati ni vya lazima na inapotengenezwa inapaswa kuwa na alama ya mzalishaji, kiwango cha madini ya zinki kilichopakwa na geji. Yote haya yaandikwe kwenye bati husika sokoni ili mnunuzi aone na ajue". Ameeleza.

Pamoja na hayo amesema kuwa watumiaji wa mabati inafaa wapate uelewa wa matumizi ya mabati ambapo itasaidia kuepuka hasara zisizo za lazima.


Share:

DKT. JINGU AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HOSPITALI YA LIGULA - MTWARA



Na. WAF, Mtwara

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu Septemba 13, 2023 ametembelea Hopsitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula na kukagua miradi ya jengo jipya la upasuaji, jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD), Jengo jipya la Wagonjwa wa dharura (EMD) pamoja na Jengo la wazazi (martenity) ambayo ipo katika hatua za mwisho za ukamilikaji.

Dkt.Jingu amesema kuwa lengo la Kufanya Ukaguzi Wa Miradi mbali mbali ya uboreshaji wa Huduma za Afya inayoendelea ni kuangalia ubora wa miradi hiyo kuendanda na thamani ya fedha iliyowekezwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili wananchi waweze kupata Huduma bora za afya.

Aidha Dkt. Jingu amepata wasaa wa kuzungumza na Watumishi wa Afya katika Hospitali hiyo na kuweza kusikiliza na kutatua baadhi ya changamoto wanazopitia watumishi hao.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara-Ligula, Dkt. Lobikieki Kissambu amemshukuru Dkt. Jingu kwa kuweza kutembelea Hospitali hiyo kwani ni faraja kwa uongozi na Watumishi kwa ujumla kutembelewa na wasimamizi kutoka ngazi ya juu.
Share:

Wednesday 13 September 2023

KARATA 21 TU ZINAKUPA USHINDI KWENYE BLACKJACK1 YA MERIDIANBET!!



PTR Blackjack 1 ni mchezo mpya wa karata kutoka kampuni ya Playtech. Mchezo huu wa kasino ya mtandaoni ya Meridianbet unachezwa na pakiti nane za kadi na unafuata sheria za Ulaya za kawaida. Blackjack ni mchezo wa kadi wa kuvutia na unaopendwa sana na wachezaji wa aina zote, mara nyingine unaweza kuwaona watu wakicheza blackjack katika sinema.

Mchezo wa kadi wa PTR Blackjack 1 unachezwa kutoka studio ya moja kwa moja na kuna meza nyingi za kuchagua, kila moja ikiwa na kiwango cha chini cha dau tofauti, na kila meza inaweza kuchukua wachezaji saba. Chagua meza yako na anza kucheza.

Hebu tuangalie jinsi ya kubashiri na kushinda katika mchezo wa kasino ya mtandaoni ya Meridianbet wa PTR Blackjack 1. Ikiwa raundi ya mchezo tayari imeanza wakati unajiunga na meza, subiri raundi inayofuata kuweka dau zako.

Kuweka dau, chagua chipi na weka kwenye eneo la ubashiri. Unaweza kuweka mara nyingi zaidi kwenye maeneo tofauti ya ubashiri kwa wakati mmoja.

Kipima muda kwenye dirisha la mchezo kinakuonyesha muda uliobaki wa kuweka dau zako. Baada ya kengele, ubashiri hautaruhusiwa tena, na raundi ya mchezo itaanza.

Mafanikio huweza kulipwa kwa ubashiri unaoshinda mwishoni mwa kila raundi ya mchezo. Ili kucheza raundi nyingine ya mchezo wa PTR Blackjack 1, weka tena dau zako au tumia kitufe cha "Rebet."

Kuanza, chagua moja kati ya thamani sita za chips kwenye kibodi cha chini na bonyeza eneo wazi la ubashiri kuweka dau.

Mchezo wa kadi wa PTR Blackjack 1 unatoka kwa mtoa huduma wa Playtech!

Kawaida, ubashiri kwenye blackjack hufanywa kwa kubofya duara mbele ya eneo la ubashiri. Kwanza, unapaswa kuweka ubashiri wako wa msingi, kisha unaweza kuweka ubashiri wa hiari wa upande.

Baada ya ubashiri wa msingi kuwekwa na kuthibitishwa, ikiwa chaguo la ubashiri wa mara nyingi linasaidiwa na raundi bado iko wazi, ubashiri wa ziada unakubaliwa.

Baada ya raundi ya ubashiri, tumia Hit, Stand, Double, Split, na Insurance ikiwa kadi ya kwanza ya muuzaji ni Ace. Ikiwa hutafanya hoja, utasimama moja kwa moja.

Ikiwa unachagua kudouble, kiasi kinacholingana na ubashiri wako wa msingi kinachukuliwa kutoka kwa akaunti yako na ubashiri wako wa msingi unadoubled.

Lengo la mchezo wa blackjack ni kufikia jumla ya kadi kubwa kuliko muuzaji bila kuzidi 21. Mkono bora ni blackjack, ambapo jumla ya thamani ya kadi mbili zilizogawanywa ni 21. Mchezo unachezwa na pakiti nane za kadi, na muuzaji daima anasimama kwa 17.

Hapa kuna muhtasari mfupi wa sheria za mchezo wa kasino ya mtandaoni. Mchezo unachezwa na muuzaji ambapo anaruhusu hadi wachezaji 7 kwenye meza ya blackjack. Unachezwa na pakiti 8 za kadi za kawaida za 52. Thamani za kadi kwenye blackjack ni kama ifuatavyo:

Kadi za 2 hadi 10 zina thamani ya alama zilizoonyeshwa kwao, na kadi za picha kama vile Jack, Queen, na King zina thamani ya 10. Aces wanaweza kuwa na thamani ya 1 au 11, kulingana na ni ipi inayofaa mkono wako.

Baada ya muda wa kuweka ubashiri kumalizika, muuzaji atagawa kadi moja kwa kila mchezaji kwa uso uliopo.

Kugawanywa kuanza na mchezaji wa kwanza kushoto mwa muuzaji, kisha inaendelea kwa mzunguko wa saa na kumalizika kwa muuzaji.

Kisha muuzaji atagawa kadi nyingine kwa kila mchezaji na kuweka kadi ya pili ya muuzaji chini.

Ikiwa thamani ya mkono wako wa awali wa kadi mbili ni sahihi 21, umeshinda blackjack. Ikiwa muuzaji ana Ace kama kadi ya kwanza iliyofunikwa, utapewa nafasi ya kununua bima kujilinda dhidi ya hatari ya muuzaji kupata blackjack.

Wachezaji wanaweza kuchagua kuchukua kadi ya ziada, inayojulikana kama Hit, au wanaweza kubaki na kadi zao za awali, inayojulikana kama Stand.

Mchezo wa PTR Blackjack 1 una chaguo la Bet Behind, maana unaweza kujiunga na hatua wakati wowote, wakati interface ya mtumiaji wa juu na muuzaji mwenye fadhili atakuongoza kupitia kila sehemu ya mchezo huu kwa urahisi wa kushangaza.

PTR Blackjack 1 ni mchezo wa kasino ya mtandaoni wa kadi uliopo katika studio ya Playtech, ambapo wameboresha kila sehemu ya mchezo ili kuufanya uwe wa kusisimua zaidi, na kipengele cha Bet Behind.

Cheza PTR Blackjack 1 kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na furahia mchezo huu wa karata.

 

NB: Kasino Mtandaoni ya Meridianbet inakuja na bonasi Baab Kubwa, kupitia mchezo wa Aviator unakupa beti za bure 200 kila siku zikitoka bila mpangilio. Kusanya Beti za Bure.


Share:

DAWA ILIYOMPONYA BABU YETU UGONJWA WA PRESHA!

 


Jina langu ni Alex, siwezi kusahau jinsi ambayo tulizunguka huko na kule na Babu yetu katika Hospitali mbali mbali kutafuta msaada wa kitiba kwa Babu ambaye alikuwa anaugua ugonjwa wa Presha au Msukumo wa Dawa (BP).

Wazazi wetu tayari walikuwa wametangulia mbele za haki, hivyo sisi wajukuu zake ndio hasa tulikuwa na jukumu zima la kumtunza kwa hali na mali kwani hakuna mwingine ambaye angeweza kufanya hivyo zaidi yetu katika familia ile.

Kaka yangu mkubwa ndio aliyekuja na suluhisho la ugonjwa wa Babu baada ya kuzunguka sana, suluhisho lenyewe ni pale alipopata namba za African Doctors  (+254769404965), mtaalamu wa tiba asili kupitia tovuti yake, www.african-doctors.com ambayo hutembelewa na idadi kubwa ya watu kila siku wanaotaka huduma zake.

Nakumbuka siku hiyo kaka alinitumbia namba hiyo WhatsApp na pamoja na link ya tovuti hiyo ili niweze kusoma na kujiridhisha kama tunaweza kutumia huduma za mtu huyo. Baada ya kusoma kuhusu huduma zake, tulishaurina kuwa tumtafute mtu huyu mara moja kwani inaonekana tiba zake ni za uhakika.

Basi tukaamua kuwasiliana na African Doctors  na kumueleza hali halisi ya Babu yetu na jinsi ambavyo tumehaingaika sehemu mbalimbali kutafuta tiba na kumuomba atufanyie dawa mara moja.

Tunashukuru kwa ukaribu wake waliotuonyesha siku ya kwanza hadi Babu yetu anakuja kupona kabisa, African Doctors  alitutumia dawa hizo za asilia na Babu akaanza kutumia. Haikuchukua kipindi kirefu Babu alianza kusema kuwa anajisikia vizuri sana, na hali yake ya kiafya iliendelea kutengamaa kadiri siku zilivyozidi kusonga.

Kwa sasa Babu ni mzima wa afya anaendelea na shughuli zake za kila siku za uzalishaji mali, kikubwa zaidi kila siku anatusifu wajukuu zake kwa kumpambania huku akisema katika miaka yake 67 hapa duniani hajawahi kutokea mtu aliyeugusa moyo wake kama African Doctors.

Kumbuka African Doctors ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Pia anatibu magonjwa kama kaswende, kisonono, kifua kikuu, presha, kifafa, upungufu wa nguvu za kiume, kuvimba miguu, kaswende, vile vile anawezesha wanawake kubaba ujautizo, wanaume kutungisha mimba n.k.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.



Share:

UTUNZAJI KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA SERIKALI NDIO MSINGI MKUU WA TAIFA - MAHIMBALI


Na Mwandishi wetu -Dodoma 

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali amesisitiza kuwa utunzaji wa kumbukumbu na Nyaraka za Serikali ndio msingi mkuu wa Taifa katika uendeshaji wa shughuli zote za Taasisi.


Amesema hayo leo septemba 13, 2023, wakati akifungua mafunzo ya maadili katika utumishi wa Umma kwa watumishi wa Taasisi ya Uhamasishaji wa Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali Madini , Mafuta na Gesi asilia (TEITI), yanayofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.


Amesema kuwa, ana matumaini kila mtumishi wa taasisi hiyo atapata uelewa kuhusu Kanuni na maadili ya Utumishi wa Umma yatakayo mpelekea kujua haki na wajibu wake wakati akitekeleza majukumu yake sehemu ya kazi.



“Ndugu Washiriki, kumbukumbu na Nyaraka za Serikali ndio msingi mkuu wa Taifa letu katika uendeshaji wa shughuli zote za Taasisi. Uzalishaji, utumiaji, utunzaji na uteketekezaji sahihi wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali ni jambo la msingi na la kuzingatiwa na watumishi wote.


Ni muhimu kufuata na kuzingatia miiko ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka pamoja na kuzingatia usiri na utengano sambamba katika matumizi yake” amesema Mahimbali.



“Ili Utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika. Watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo katika Utumishi wa Umma" ameongeza Mahimbali.


Katika hatua nyingine, Mahimbali amewaahidi watumishi wa TEITI kuwa Wizara itawaboreshea maslahi ili kufanya kazi katika mazingira bora na yenye hadhi ya utumishi ya umma.


Pia, akitoa salaam kutoka kwa Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, Mahimbali amesema kuwa waziri anawasihi kuzingatia mafunzo hayo kwa kila mada itakayo tolewa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili kuongeza ufanisi katika utendajikazi wa kila siku.



Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI, Mariam Mgaya amesema kuwa uwepo wa taasisi hiyo unasaidia wananchi kujua uwazi na uwajibikaji sambamba na kuziba mianya ya rushwa kwasababu wananchi wanakuwa na taarifa za kutosha kuhusu shughuli za uendeshaji na usimamizi wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia.


Akizungumzia juu ya majukumu ya taasisi hiyo Mariam amefafanua kuwa TEITI inajukumu la kuweka mahusiano mazuri baina ya Serikali, Kampuni na Wananchi katika sekta zote za rasilimali madini ,mafuta na Gesi asilia.

Share:

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI AITAKA TRC KUONGEZA KASI KATIKA KUSIMAMIA MIRADI INAYOENDELEA ILI IKAMILIKE KWA WAKATI NA KWA THAMANI HALISI YA FEDHA

Ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ya kutembelea Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Kwa ajili ya kujitambulisha, kujifunza na kujionea miradi inayoendelea chini ya Usimamizi wa Shirika Hilo na kukagua Stesheni ya treni ya kisasa ya SGR ya Tanzanite Jijini Dar es salaam

Na Mwandishi wetu Dar es Salaama 

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe David Kihenzile ameutaka uongozi wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) kuongeza kasi katika kusimamia miradi inayoendelea ili ikamilike kwa wakati na kwa thamani halisi ya fedha.


Mhe kahenzile ameyasema hayo wakati wa ziara ya kujitambulisha, kujifunza , kuongea na Menejimenti ya Shirika na kujionea miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na shirika la reli Tanzania kwenye ofisi za shirika hilo zilizopo stesheni Jijini Dar es salaam tarehe 13 Septemba,2023.


“Naupongeza uongozi wa Shirika kwa usimamizi makini wa miradi inayoendelea ya uboreshwaji wa reli ya kati na ujenzi wa Reli ya kisasa(SGR) ,ununuzi wa mabehewa na vichwa vya treni, Miradi hii kwa sasa ni jicho la nchi yetu hivyo natoa rai kwenu muongeze kasi ya usimamizi ili ikamilike kwa wakati na thamani halisi ya fedha kwani tunaitegemea sana ili kuinua uchumi wa wananchi, sekta zingine, kuongeza mapato ya shirika na hatimaye muweze kujitegemea na kujiendesha”amesisitiza Mhe Kihenzile



Mhe Kihenzile amemshukuru Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kwa nafasi ya Naibu Waziri Uchukuzi ili amsaidie Waziri Prof Makame Mbarawa na kuahidi ushirikiano wa karibu wa Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zake zote ili kuongeza kasi ya utendaji na hatimaye kuongeza tija kwa Taifa.


Akitoa salamu za Shirika Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bi. Amina Lumuli amesema shirika hilo liliundwa mwaka 2017 baada ya kuvunjika kwa RAHCO na TRL na kurithi majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na mashirika hayo ikiwemo kuanzisha,kusimamia,kuendeleza miundombinu ya Reli, kutoa huduma,kufanya ukarabati,kuingia mikataba na kuimarisha vitendea kazi kulingana na sheria ya reli namba kumi ya Mwaka 2017.



Bi Amina amesema mtandao wa reli Nchini umegawanyika katika kanda tatu ikiwemo reli ya kati(DSM-KGM), reli ya kaskazini(TAN-MOS-ARU), na reli ya kusini(Mtwara-Mbamba bay), huku kukiwa na aina mbili za reli ya kawaida(MGR) yenye urefu wa km 2,707 na reli mpya ya kisasa(SGR) ambapo km 4,752 zinatarajiwa kujengwa.


Kuhusu Miradi inayoendelea Bi Amina amesema Shirika lilipata mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 300 kutoka Benki ya Dunia mwezi machi,2014 kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha mradi wa usafirishaji wa reli kutoka tani 135 km ekseli hadi tani 18.5, uboreshaji madaraja na ununuzi wa mabehewa 44 ya mizigo ambavyo vimeshakamilika



Kwa upande wa Reli ya Mwendokasi(SGR) Bi Amina amesema ujenzi wa reli kutoka DSM hadi Mwanza wenye jumla ya km 1,596 unaohusisha km 1,219 njia kuu na km 377 za mapishano umefikia katika hatua mbalimbali za utekelezwaji zilizogawanywa kwa vipande vitano kwa awamu ya kwanza ambavyo ni Dsm-Moro(km300) asilimia 98.52, Moro-Makutupora(km422) asilimia 94.99, Makutupora-Tabora(km368) asilimia 10.92, Tabora-Isaka(km 165) asilimia 4.63 na Isaka-Mwanza (km 341) asilimia 37.22.


“Ujenzi wa reli ya kisasa unaendelea vizuri awamu ya kwanza na kwa awamu ya pili ya kipande cha Tabora-kigoma(km 506) usanifu unaendelea ambapo mpaka sasa jumla ya Dola za kimarekani Bil 3.75 sawa na Zaidi ya shilingi tril 23 zimeshatumika na tayari jumla ya vichwa vya treni vya umeme 17 na seti 10 za EMU ukarabati unaendelea Nchini korea,mabehewa ya mizigo 1,430 yameagizwa na tayari mabehewa ya abiria 59 yalishawasili” amesisitiza Bi Amina


Mnamo tarehe 30 Agosti,2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko madogo ya baraza la mawazili na makatibu wakuu yaliyopelekea kuanzishwa kwa Wizara mpya ya Uchukuzi na kuteuliwa Prof Makame mbarawa kuwa Waziri, Mhe David Kihenzile Naibu Waziri, Prof Godius Kahyarara katibu mkuu na Dkt Ally Possi Naibu katibu Mkuu.



Share:

KAMPUNI YA NYUMBAFASTA IMEKUJA NA SULUHISHO LA KIDIGITALI KWA WAPANGAJI NA WENYE NYUMBA

Kampuni ya Nyumbafasta inaleta suluhisho la kidijitali kwa wapangaji na wenye nyumba nchini Tanzania. Suluhisho hili litawawezesha wapangaji kupata nyumba za kupanga bila malipo ya kodi ya mwezi mmoja na kuwasiliana moja kwa moja na wenye nyumba kwa gharama ndogo, kuanzia shilingi elfu moja tu.

Zaidi ya hayo, Nyumbafasta inawasaidia wanunuzi na wauzaji wa nyumba na viwanja kwa kutoa huduma ya uhakiki wa mali kupitia mfumo maalum. Mfumo huu umetengenezwa na vijana wa Kitanzania na unapatikana mtandaoni kote nchini kupitia tovuti yetu - www.nyumbafasta.co.tz.


Kupitia Nyumbafasta, wapangaji wanaweza kupata nyumba bora kwa bei nafuu na kusaidiwa kuokoa muda wa kutafuta nyumba, huku ikipunguza migogoro isiyo ya lazima wakati wa kununua nyumba au viwanja.


Tunawaalika wamiliki wa nyumba za kupangisha nchini kote kujisajili kwenye tovuti yetu bila malipo yoyote kupitia www.nyumbafasta.co.tz au kutumia huduma bora na yenye uweledi isiyo na gharama kupitia kitengo chetu cha huduma kwa wateja.


Tunawakaribisha kutumia Nyumbafasta kwa huduma ya upangaji bila malipo ya kodi ya mwezi mmoja na ununuzi wa nyumba na viwanja vilivyo hakikiwa ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Pamoja na hayo tumechukua hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wetu na jamii na kuendeleza huduma bora kwa wateja wetu.Tunayo furaha kumkaribisha Barbara Hassan katika jukumu hili muhimu la kuwa mwakilishi wetu mpya na balozi wa kampuni yetu. Hii yote ni

katika kuhakikisha tunabaki kuwa kinara katika sekta ya uuzaji na upangaji wa nyumba na viwanja. Tunayo furaha kubwa kutangaza uteuzi huu wa Balozi Mpya katika timu yetu,

Barbara Hassan - tukiamini katika uchapaji wake kazi. Barbara amepata sifa kubwa katika sekta ya utangazaji kutokana na uzoefu wake mkubwa na uwezo wa kushirikiana na wadau mbalimbali katika jamii.

Tunaamini Barbara atachangia maarifa na utaalamu wake kuhakikisha tunabaki kuwa chaguo la kwanza na bora kwa wateja wetu na kuendeleza miradi yetu ya upatikanaji wa Nyumba na Viwanja kwa haraka.


Ameonesha dhamira ya dhati katika kuendeleza sekta ya Nyumba za kupanga, Nyumba za kuuza na Viwanja kwa kutoa huduma bora kwa wateja. Tunatarajia kufanya kazi kwa karibu naye ili kuleta mafanikio makubwa kwa kampuni yetu.


Kampuni yetu - Nyumbafasta - inajitolea kuendelea kuwa wabunifu na kutoa huduma za hali ya juu katika sekta hii. Uteuzi wa Balozi Mpya ni hatua muhimu katika kufanikisha malengo haya yanatimia.

Tunasema Makato yasio ya lazima Sio Shida Zetu

Kwa maelezo zaidi au kwa mahojiano, tafadhali wasiliana na: Robinson Marley 0652493300.


Share:

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIHISTORIA MTWARA, LINDI



Na Mwandishi Wetu, Mtwara

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi kuanzia tarehe 15-20 Septemba, 2023. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, katika ziara hiyo ya mikoa ya kusini, Rais Samia atazindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kama ilivyo desturi ya uongozi wake wa kuwajali wananchi wa chini, Rais Samia pia atasikiliza kero na matatizo ya wananchi kwenye maeneo yote atakayotembelea.

Pamoja na mambo mengine, Rais Samia atazindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini wakati wa ziara yake ya mkoa wa Mtwara.

Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mikindani Mkoa wa Mtwara ulianza mwaka 2021.

Hospitali hiyo kubwa na ya kisasa itahudumia mamilioni ya wakazi wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Ujenzi wa hospitali hiyo unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 15.8.

Tangu alipoingia madarakani mwezi Machi 2021, Rais Samia amefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya ambao haujawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru miaka 62 iliyopita.

Katika ziara yake ya mikoa ya kusini, Rais pia atazindua Chujio la Maji Mangamba na atakagua ujenzi wa uwanja wa ndege, pamoja na kuzindua barabara za mkoa wa Mtwara.

Mikoa ya Lindi na Mtwara inatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa Tanzania na ni maarufu kwa kilimo cha korosho, shughuli za uvuvi na rasilimali ya gesi asilia.

Serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwenye bandari ya Mtwara, huku jitihada zikiendelea kukamilisha uwekezaji wa kampuni binafsi za kimataifa wa Dola za Marekani takribani bilioni 40 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 100) kwenye mradi mkubwa wa kuchakata gesi asilia (LNG) mkoani Lindi.
Share:

USIKU WA WADAU WA HABARI NA VYOMBO VYA HABARI KANDA YA ZIWA KUFANYIKA SEPTEMBA 29


Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (Mwanza Press Club - MPC) imeandaa Usiku wa marafiki na wadau wa vyombo vya habari Kanda ya Ziwa, unaotaraji kufanyika Septemba 29, 2023.

Lengo kuu ni kuwapa nafasi wadau wa vyombo vya habari kueleza utekelezaji wa mipango yao kwa mwaka 2023 mbele ya vyombo vya habari.

Pia malengo madogo ni, kuwapa nafasi wadau wa habari kutangaza huduma na bidhaa wanazozalisha/ kutoa, kuwapa nafasi wananchi kuzijua taasisi za umma na binafsi na kazi wanazozifanya na pia kujenga mahusiano ya kiutendaji baina ya serikali, taasisi za kiserikali, AZAKI na mashirika binafsi na vyombo vya habari.


Faida za kushiriki ni wadau watapata nafasi ya kushiriki wiki ya wadau wa habari kabla ya usiku wa wadau wa habari, ambapo waandishi wa habari watatembelea taasisi zitakazoshiriki, logo za wadau zitachapishwa kwenye tshirt na mabango yote, kila mdau atapata nafasi ya kunadi taasisi yake.

Mratibu MPC
6.8.2023
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger